BAADA ya kukosa penalti katika mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya mahasimu wao, Real Madrid, beki wa Atletico Madrid Juanfran Torres amewaomba radhi mashabiki wa klabu hiyo.Beki huyo wa kulia aliyefunga penati ya ushindi katika hatua ya 16 Bora dhidi ya PSV Eindhoven ndiye aliyekuwa mchezaji pekee wa Atletico aliyekosa penalti kwenye Uwanja wa San Siro, Milan Italia wakati wa mikwaju ya penalti na kusaidia kuipa Real Madrid taji la 11 baada ya Cristiano Ronaldo kufunga ya mwisho.
Real Madrid ilishinda kwa penalti 5-3 baada ya kumaliza dakika 120 timu zote zikifungana bao 1-1, huku Antonie Griezmann akipoteza penalti ambao ingeweza kuisawazishia Atletico katika kipindi cha kwanza.
Juanfran walitia simanzi akiwashinda wachezaji wenzakwa kwa huzuni kubwa iliyowapata baada ya matokeo hayo na beki huyo amewaomba radhi mashabiki wao kwa kile kilichotokea.
Leo Jumatatu Juanfran ameaandika barua maalum kwa mashabiki wa Atletico Madrid ili kuwaomba radhi kwa kilichotokea. Barua hiyo imetupiwa pia katika akaunti ya klabu hiyo ya Instagram.
Waraka huo unasomeka hivi;
![]() |
| Wakara huo wa Juanfran |
Hello Atleticos,
Nimeomba klabu kuwafikishia barua juu ya kila kitu ninachojisikia
Kamwe sitasahau moyo wa dhati mlioonesha kwangu wakati nilipokuja kwenu kuomba msamaha. Nikiona machozi yangu yakitiririka mbele ya maelfu ya mashabiki wa Atletico waliofika uwanjani na kunisaidia kuendana na uhalisia wa huzuni kubwa iliyokuwa imejaa kwenye nafsi yangu. Vile vile bila ya kusahau sapoti niliyopata kutoka kwa wachezaji wenzangu, kocha na watu wote wanaounda familia hii ya Atletico.
Pia ningependa kuwashukuru kwa imani kubwa ambayo mara zote mmekuwa mkionesha kwetu na zaidi ya yote ni kutufanya sisi kujiona watu wa tofauti wengine na wenye nafsi ya kipeke kutokana na uwepo wetu hapa Atletico.
Miaka miwili iliyopita, niliwaambia kwamba tungerejea tena fainali na tumefanya hivyo, sasa, nawaambia kwamba, Gabi, nahodha wetu hivi karibuni au baadaye atanyanyua Kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya na kusherehekea sote kwa pamoja.
Nawapenda sana na tusonge mbele Wana-Atletico.


RAIS wa wa Jamhuri
STRAIKA Mbwana Samatta amweka rekodi ya kuwa Mtanzania wa kwanza kuiwezesha timu yake kucheza michuano ya Ligi Ndogo ya Ulaya (UEFA Europa League) baada ya kuisaidia Genk ya Ubelgiji kufuzu hatua hiyo kwa kuilaza Charleroi.

NAHODHA wa Chelsea John Terry amemuunga mkono Jose Mourinho kufanikiwa kwenye
Klabu yake mpya Manchester United huku akimueleza kuwa Meneja huyo ndie
bora kupita yeyote aliewahi kucheza chini yake. 

MSHAMBULIAJI wa KImataifa wa Sweden, Zlatan Ibrahimovic amekuwa akihusishwa na kutaka kutua Manchester United ili kuungana na Kocha wake wa zamani, Jose Mourinho, lakini wakala wake wamesema klabu atakayojiunga nayo itashangaza wengi.
KLABU YA Tottenham Hotspur imetangaza kuwa itacheza mechi zake za Ligi ya Mabingwa Ulaya mwakani kwenye Uwanja wa Wembley.
WAKALA wa beki kisiki wa Barcelona, Dani Alves amekanusha taarifa kuwa mteja wake amesaini mkataba wa awali na Juventus, japo amekiri kuwa mabingwa hao wa Italia na klabu nyingine zinamwinda mchezaji huyo.
Benitez Akisaini Mkataba huo wa kumweka Newcastle United Miaka 3
Wakati wa Mkutano na Waandishi wa habari juu ya kuongeza Miaka 3 kuifundisha Klabu hiyo ya Newcastle United
Kwenye Mkutano na Waandishi huko St. James Park





HEBU msikieni CR7. Straika nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amesema kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya itakuwa na thamani kubwa zaidi kuliko mataji mawili yaliyonyakuliwa na wapinzani wao, Barcelona msimu huu.
