STRIKA

USILIKOSE

Sunday, May 19, 2013
Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa atiwa mbaroni kisa...!
Warembo Miss Tabata 2013 kutembelea Mbuga ya Mikumi
![]() |
Miss Tabata wakiwa kwenye pozi ya picha ya pamoja |
WAREMBO watakaoshiriki kinyang'anyiro cha shindano la Miss Tabata
2013 watatembelea mbuga ya wanyama ya
Mikumi wikiendi ijayo.
Mratibu wa shindano hilo
Godfrey Kalinga mapema leo kuwa, lengo la ziara hiyo ni kukuza utalii wa ndani.
Alisema kuwa warembo hao pia watapata fursa ya kujua vivutio vilivyomo kwenye
mbuga hiyo iliyoko mkoani Morogoro.
“Hii siyo mara yetu ya kwanza
kuwapeleka warembo wetu mbugani. Tumekuwa tukifanya kila mwaka,” alisema
Kalinga.
Kapinga alisema kuwa
ziara hiyo imedhaminiwa na CXC Africa.
Shindano la kumsaka Miss
Tabata litafanyika Mei 31 katika ukumbi
wa Da’ West Park, Tabata.
Wadhamini wa shindano
hilo ni Nipashe, Redds, Dodoma Wine, Nipashe, Vayle Springs, Multichoice, Fredito
Entertainment, CXC Africa, Brake Point na Saluti5.
Warembo watakaoshiriki
kwenye shindano hilo linaloandaliwa na Bob Entertainment na Keen Arts ni
Madgalena Bhoke (21), Kabula Juma Kibogoti (20), Upendo Dickson Lema (22), Hidaya David Mwenda (22), Aneth Ndumbalo (19), Dorice Mollel (22), Eunice Nkoha (19),
Kazunde Musa Kitereja (19), Rehema Kihinja (20), Pasilida Mandali (21), Brath Chambia (23),
Joaniter Kabunga (21), Recho Mushi (20),Caroline Sadiki (20) na Suzan Daniel (18).
Warembo watano watachaguliwa
kushiriki mashindano ya Miss Ilala na baadaye Miss Tanzania.
Anayeshikilia taji la
Miss Tabata kwa sasa ni Noela Michael ambaye pia ni Miss Ilala.
Simba na Yanga zaingiza Mil, 500, zenyewe zazoa Mil. 250
Simba na Yanga zilipoumana jana uwanja wa Taifa |
PAMBANO la watani wa jadi Simba na Yanga la Ligi Kuu ya Vodacom lililochezwa jana (Mei 18 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa mabingwa wapya Yanga kushinda mabao 2-0 limeingiza sh. 500,390,000.
Mechi hiyo namba 180 ambayo ilikuwa kati ya saba la kuhitimisha ligi hiyo msimu wa 2012/2013 ilishuhudiwa na watazamaji 57,406 waliokata tiketi kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 30,000.
Kila klabu imepata mgawo wa sh. 123,970,927.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 76,330,677.97.
Kiingilio cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo waliokata tiketi hizo walikuwa 19,039 na kuingiza sh. 95,195,000 wakati kile cha sh. 7,000 kiliingiza watazamaji 17,647 na kupatikana sh. 123,515,000.
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 63,036,064.81, tiketi sh. 3,818,890, gharama za mechi sh. 37,821,638.88, Kamati ya Ligi sh. 37,821,638.88, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 18,910,819.44 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 14,708,415.12.
Golden Bush Veterani yaendeleza ubabe Dar
![]() |
Wakali wa soka la maveterani Dar, Golden Bush |
Timu hiyo ilipata ushindi katika michezo ya Bonanza iliyofanyika kwenye viwanja wa Staki Shari, Ukonga ambapo wakali hao waliwacharaza wapinzani wao hao.
Mabao ya Di Natale na 'kisiki' wa zamani wa Moro Utd na Yanga, Yahya Issa yalitosha kuizamisha Ukonga Veterani na kuwafanya Golden Bush kurejea maskani mwao wakichekaaa kwa ushindi huo.
Msemaji wa klabu hiyo, Onesmo Waziri 'Ticotico' alisema licha ya ushindi huo bado hakufurahishwa kwa vile walipania kutoa kipigo zaidi ya hicho.
Ticotico alisema wamekuwa na mazoea ya kuzigonga timu pinzani mabao kuanzia manne hiyo ushindi wa 2-0 wanaona kama hawakutenda haki kwa Ukonga.
Saturday, May 18, 2013
Wanawake Mbeya wamcharukia Mchumba wa Dk Slaa kwa kumkashifu Mama Salma Kikwete
UMOJA
wa wanawake wa chama cha Mapinduzi Mkoani Mbeya(UWT) umemshukia
Bi.Josephine Mushumbusi ambaye ni mchumba Katibu Mkuu wa chama cha
Demokrasia na maendeleo CHADEMA kufuatia kauli za udhalilishaji dhidiya Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
Hatua hiyo inatokana na kauli za kiudhalilishaji zilizotolewa mwishoni mwa wiki na mchumba huyo wa Katibu Mkuu wa Chadema kuwa mama Kikwete ameshindwa kumshauri Rais ambaye ni mume wake kuiongoza nchi vizuri.
Demokrasia na maendeleo CHADEMA kufuatia kauli za udhalilishaji dhidiya Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
Hatua hiyo inatokana na kauli za kiudhalilishaji zilizotolewa mwishoni mwa wiki na mchumba huyo wa Katibu Mkuu wa Chadema kuwa mama Kikwete ameshindwa kumshauri Rais ambaye ni mume wake kuiongoza nchi vizuri.
Kauli
hiyo imetolewa jana na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Mkoa wa Mbeya
Bi.Priscilla Mbwaga wakati akitoa Tamko kwa waandishi wa habari juu
ya Matusi ya wazi yaliyotolewa na Bi.Mushumbusi kwa Mke wa Rais katika
mikutano ya hadhara iliyofanyika Wilayani Mbozi Kata ya Vwawa Mkoani hapa.
Bi.Mbwaga alisema kuwa katika mikutano yake ya Hadhara Bi.Mushumbusi alidai kuwa mama Salma Kikwete ameshindwa kumshauri mume wake kuingoza nchi na kuacha Twiga wakiwa wanakunjwa na kuondoka na kwamba yeye akiwa Ikulu hataacha kumshauri mume wake Dkt.Slaa katika masuala ya kuingoza Nchi
Hata hivyo Mwenyekiti huyo alisema kama umoja huo wanalaani vikali lugha chafu na za kichochezi zinazopandikizwa chuki miongoni mwa jamii ya watanzania .
Alisema kuwa kama umoja wa wanawake wanalaani matusi hayo na kwamba umoja huo ulifuatilia mikutano hiyo na kugundua kuwa ilikuwa imetawaliwa na matusi badala ya kutoa sera kwa wananchi kuwa wanataka kufanya nini.
“Sisi kama umoja wa wanawake Mkoa tunaeleza umma ambao una imani na kuwa katika utamaduni na maadili yao hawapendi na wala hawajazoea kusikia matusi katika jamii yao hivyo wakiangalie vizuri na kwa makini Chadema kuwa cha hicho kina watu wa maadili gani , mahali pote siku zote na miaka yote ni matusi,kuongea uongo, uzushi na kashfa wasimamapo majukwaani “alisema Mwenyekiti huyo.
Aidha Bi.Mbwaga alisema kuwa wanawake wa mkoa wa Mbeya wanadhani kuwa kauli ambazo zimetolewa na Mushumbusi ni ni za kuwadhalilisha wanawake wote wa Tanzania kwani Mama Salma ni Kiongozi wa juu pamoja
na Mushumbusi .
“Tunamshangaa sana Mushumnbusi anaposimama majukwaani na kutoa kashfa nzito za namna hii ni kama nani kwa wanawake wa Tanzania 'alihoji Mwenyekiti huyo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi Mkoani hapa (CCM),Bw.Amani Kajuna alisema kauli aliyotoa Dkt.slaa kuwa Rais Kikwete ana Udini ni ulaghai mkubwa ambao anaufanya kwa wananchi na kuendelea kuiweka nchi katika mazingira magumu .
“Kama vijana tunatambua kuwa Rais Kikwete ni kiongozi wa watanzania, na kwamba hana sifa ya Udini hii ajenda inaanzishwa kisiasa ili kujipatia umaarufu wa bure wa kudhani kuwa ndiyo njia ya kuwapeleka ikulu mwaka 2015 jambo ambalo halitawezekana ,maana watanzania hawataweza kukubali" alisema Mwenyekiti huyo.
Hata hivyo Bw.Kajuna aliendelea kusema kuwa Dkt. Slaa amekuwa akimtuhumu Rais Kikwete kuwa ni FREEMASON , “hebu tumuulize huyu mtu amekutana lini na Rais kwenye iman hiyo” na kwamba katika uongozi wake watanzania wameona miradi mikubwa ya maendeleo ya nchi yetu kwa ukuaji wa wa pato la Taifa.
Bi.Mbwaga alisema kuwa katika mikutano yake ya Hadhara Bi.Mushumbusi alidai kuwa mama Salma Kikwete ameshindwa kumshauri mume wake kuingoza nchi na kuacha Twiga wakiwa wanakunjwa na kuondoka na kwamba yeye akiwa Ikulu hataacha kumshauri mume wake Dkt.Slaa katika masuala ya kuingoza Nchi
Hata hivyo Mwenyekiti huyo alisema kama umoja huo wanalaani vikali lugha chafu na za kichochezi zinazopandikizwa chuki miongoni mwa jamii ya watanzania .
Alisema kuwa kama umoja wa wanawake wanalaani matusi hayo na kwamba umoja huo ulifuatilia mikutano hiyo na kugundua kuwa ilikuwa imetawaliwa na matusi badala ya kutoa sera kwa wananchi kuwa wanataka kufanya nini.
“Sisi kama umoja wa wanawake Mkoa tunaeleza umma ambao una imani na kuwa katika utamaduni na maadili yao hawapendi na wala hawajazoea kusikia matusi katika jamii yao hivyo wakiangalie vizuri na kwa makini Chadema kuwa cha hicho kina watu wa maadili gani , mahali pote siku zote na miaka yote ni matusi,kuongea uongo, uzushi na kashfa wasimamapo majukwaani “alisema Mwenyekiti huyo.
Aidha Bi.Mbwaga alisema kuwa wanawake wa mkoa wa Mbeya wanadhani kuwa kauli ambazo zimetolewa na Mushumbusi ni ni za kuwadhalilisha wanawake wote wa Tanzania kwani Mama Salma ni Kiongozi wa juu pamoja
na Mushumbusi .
“Tunamshangaa sana Mushumnbusi anaposimama majukwaani na kutoa kashfa nzito za namna hii ni kama nani kwa wanawake wa Tanzania 'alihoji Mwenyekiti huyo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi Mkoani hapa (CCM),Bw.Amani Kajuna alisema kauli aliyotoa Dkt.slaa kuwa Rais Kikwete ana Udini ni ulaghai mkubwa ambao anaufanya kwa wananchi na kuendelea kuiweka nchi katika mazingira magumu .
“Kama vijana tunatambua kuwa Rais Kikwete ni kiongozi wa watanzania, na kwamba hana sifa ya Udini hii ajenda inaanzishwa kisiasa ili kujipatia umaarufu wa bure wa kudhani kuwa ndiyo njia ya kuwapeleka ikulu mwaka 2015 jambo ambalo halitawezekana ,maana watanzania hawataweza kukubali" alisema Mwenyekiti huyo.
Hata hivyo Bw.Kajuna aliendelea kusema kuwa Dkt. Slaa amekuwa akimtuhumu Rais Kikwete kuwa ni FREEMASON , “hebu tumuulize huyu mtu amekutana lini na Rais kwenye iman hiyo” na kwamba katika uongozi wake watanzania wameona miradi mikubwa ya maendeleo ya nchi yetu kwa ukuaji wa wa pato la Taifa.
CHANZO:MPEKUZI HURU
Hivi Ndivyo Yanga walivyoitambia Simba Taifa
Beki
wa Simba, Musa Mudde (kushoto) akichuana na mshambuliaji wa Yanga,
Didier Kavumbagu katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara
uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo.
Beki wa Simba, Shamte Ramadhani akimtoka mshambuliji wa Yanga, Simon Msuva
Nahodha
wa Yanga, Nidir Haroub 'Canavaro' akiwa amenyanyua kombe la Ubingwa wa
Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara pamoja na wachezaji wenzake.
Shabiki wa Yanga akipelekwa kupewa huduma ya kwanza baada ya kuzimia wakati mchezo ukiendelea.
Kikosi cha Simba.
Makocha wa yanga wakipanga mikakati ya Ushindi.
Timu zikiingia uwanjani.
Timu zikisalimiana.
Kocha wa Simba, Patrick Liewig
Kocha wa Yanga, Ernst Brandts
Beki wa Simba, Shomari Kapombe akimtoka mshambuliji wa Yanga, Simon Msuva
Msanii Juma Nature akitumbuiza wakati wa mchezo huo.
Mshambuliaji wa Simba, Felix Sunzu akitafuta mbinu za kuwatoka mabeki wa Yanga.
Mashabiki wa Yanga.
Raha ya ushindi.
Kocha wa Yanga, Ernst Brandts akiwa amebebwa na wachezaji wake.
Kiduku
KARIBU JANGWANI NGASA
Mashabiki wa Yanga wakiwa wamembeba mshambuliaji
wa Simba, Mrisho Ngasa mara baada ya mpira kumalizika, ikiwa ni ishara ya
kumkaribisha katika klabu yao.
Mashabiki wa yanga.
Wachezaji wa timu ya Yanga wakishangilia ubingwa
wa Ligi Kuu ya Vodacom baada ya kuifunga Simba 2-0 katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam
Kipa wa Simba, Juma Kaseja akijaribu bila
mafanikio kuokoa mpira wa kichwa uliopigwa na mshambuliaji wa Yanga, Didier
Kavumbagu katika mchezo wa kufunga pazia la Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika
kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
KARIBU NYUMBANI
Mashabiki
wa Yanga wakiwa wamembeba mshambuliaji wa Simba, Mrisho Ngasa mara
baada ya mpira kumalizika, ikiwa ni ishara ya kumkaribisha katika klabu
yao.
Refa
wa mechi ya Simba na Yanga, Nartin Saanya akiwa chini baada ya kugongwa
kwa bahati mbaya na mchezaji wa Yanga, Didir Kavumbagu.
Refa, Martin Saanya akipata matibabu.
PICHA ZOTE NA FRANCIS DANDE WA HABARI MSETO
Majina ya wanavyuo walionaswa wakijiuza haya hapa
Wanafunzi wa kike wa chuo kikuu cha Dar es salaam [UDSM],Chuo cha elimu ya biashara [CBE]na chuo cha mamlaka ya Elimu na ufundi stadi [VETA],Dar es salaam ,wamefikishwa katika mahakama ya jiji samora wakidaiwa kufanya biashara ya kuuza mili yao.
Washitakiwa hao waliokamatwa katika eneo la kona Baa Ambiance Sinza wilayani kinondoni ambao ni miongoni mwa wanawake 35 wanaodaiwa kufanya biashara hiyo na wote walifikishwa mahakamani hapo.
Kesi hiyo ilikuwa chini ya hakimu Willian Mtaki ambapo muendesha mashitaka,bwana John Kijumbe,alisema wasichana hao walikamatwa katika mazingira tofautitofauti.
Wanafunzi hao ni Yasinta Kilimo mwenye miaka 21 CBE mkazi wa upanga,Morin Masatu miaka 19 UDSM,mkazi wa kinondoni na mwanafunzi wa VETA aliyefahamika kwa jina moja la Khadija.
“Nilikwenda pale baa kuchukua simu yangu ambayo ilipotea hivyo waliniita nikaichukue ndipo askari wa jiji wakanikamata,”Alisema Khadija akijitetea.
Kwa mujibu wa bw. Kijumbe washitakiwa hao wamekosa dhamana baada ya kushindwa kutimiza masharti ya kila mmoja kuwa na wadhamini wawili au kulipa faini ya kulipa sh. 200,000.
Kesi hiyo inatarajiwa kusikilizwa tena mei 28 mwaka huu,ambapo washitakiwa wote walipelekwa Segerea.
Wakati huohuo, jeshi la Polisi mkoa wa kinondoni , limewakamata watuhumiwa 716 waliokuwa wakijihusisha na biashara ya kuuza miili kati yao wanaume 38 na wanawake 678.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi mkoa wa kipolisi Kinondoni Charles Kenyela, alisema watu hao walikamatwa kwenye msako uliodumu kwa miezi sita kwenye maeneo mbalimbali ya Kinondoni.
Maeneo hayo ni baa, kumbi za starehe, madanguro, sehemu za wazi katika ufukwe wa Bahari ya Hindi, na makaburini ambapo kati ya wanaume waliokamatwa wengine ni mashoga pamoja na wateja wa machagudoa.
“Msako huo ulifanyika Maisha Club, Coco Beach, Barabara ya Tunisia , Travertine Hotel, Tandale Uwanja wa Fisi, Ambiance Club, Shekilango pamoja na Mwinanyamala” Alisema
Kamanda Kenyela aliongeza kuwa , jeshi hilo pia limewakamata raia 12 kutoka nchini Ethiopia walioingia nchini bila kibali kati ya Mei 2 na 6, mwaka huu katika eneo la Kimara Mwisho na Tegeta Kibaoni.
Alisema kukamatwa kwao kulitokana na taarifa walizozipata kutoka kwa raia wema waliowaona maeneo.
Credit:Mpekuzi Huru
Mbunge Chadema aanguka ghafla Bungeni
![]() |
Mhe. Taratibu Abama |
MBUNGE wa Viti Maalum, pichani Mwanamrisho
Taratibu Abama (Chadema), ameanguka
bungeni, baada ya kujisikia vibaya.
Mbunge huyo alianza kujisikia vibaya,
hali iliyomfanya kuketi katika viti vilivyo karibu na zahanati ya Bunge.
Kwa mujibu wa watu walioshuhudia
walisema mbunge huyo alipata huduma ya kwanza katika zahanati hiyo kwa zaidi ya
saa mbili kabla ya kupelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Dodoma.Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya
hospitali hiyo, zinasema mbunge huyo alilazwa wodi namba 18.
Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya
Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Dk. Zainab Chaula, alithibitisha kupokelewa kwa mbunge
huyo.
“Ni kweli yupo hapa na hali yake inaendelea vizuri sasa ,”alisema.
Bondia Jonas Segu ang'ara Thailand
Jonas Segu akimuadabisha mpinzani wake |
Segu akimkong'ota m,pinzani wake |
TANZANIA imetengeneza historia mpya kwenye
ngumi za kulipwa nchini Thailand baada ya mabondia wake kuwa wanapigwa kila
mara wanapokwenda kuiwakilisha nchi na bara la Afrika. Safari hii JEMBE,
kijana mtanashati anayeinukia kwenye masumbwi Jonas Segu kutoka katika
ukumbi wa mazoezi wa Respect Gym Boxing Club ya Mabibo Loyola chini ya
kocha Christopher Mzazi ameonyesha kipaji kikubwa cha kusukuma msumbwi
alipoushangaza umati wa maelfu ya wananchi wa Thailand pamoja na nchi za
ukanda wa Indo-China.
Segu alikuwa anachuana na bingwa wa IBF
katika mara la Asia Pacific Patomsuk Pathompothong kutoka Thailand
katika uzito wa Light Welter ambaye ni bondia namba 7 duniani
katika viwango vya IBF. Mpambano wao ulifanyika katika jiji lenye mahekalu ya
dhahabu la Bangkok na kurushwa na television katika nchi zote za ukanda
wa Indo-China za Laos, Myanmar, Cambodia, Vietnam na Thailand
yenyewe.
Mpambamo wa Segu na Pathompothong
ulianza kwa bondia wa kitanzania kuchomoka kama upinde kwenye kona yake na
kumshambulia Pathompothong kwa makonde mazito ya kumshikisha adabu.
Segu alitupa makonde ya mchanganyiko na kumzidi Pathompothong
kutokana na uzito na umakini wa ngumi zake. Kwa kipindi chote cha raundi ya
kwanza ilimbidi Pathompothong ajilinde na kukimbia akizunguka ndani ya
ulingo ili kudhoofisha masumbwi ya Segu aliyekuwa anayachanganya kama
mashine ya kukomboa mpunga ambao unalimwa kwa wingi nchini Thailand!
Jonas Segu alikuwa chini ya uangalizi makini wa bondia maarufu mstaafu George
“Lister” Sabuni ambaye aliweza kumpa maelekezo ya nini cha kufanya kwenye
mpambano huo wa mwaka. Katika raundi ya 2, 3 na 4 Segu aliuonyesha umati
wa mashabiki wa Thailand kuwa yeye kweli ni bingwa mtarajiwa na hakwenda
Thailand kula wali wao ila kuiwakilisha nchi yake ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania. Segu alimhenyesha Pathompothong vilivyo kwa kumchakaza kwa
makondde mfululizo hususan akiutumia mkono wake hatari wa kulia ambao
ulionekana dhahiri kuwa unaleta madhara makubwa kwa Pathompothong.
Ilididi timu ya wataalam wa Pathompothong
kutafakari namna ya kumdhibiti kijana huyo wa Kitanzania ambaye kweli
alionekana kuwa alienda Thailand kuuchukua mkanda wa IBF Pan Pacific na
sio kufuata ulaji!
Raudi ta 5 Pathompothong
aliingia ulingoni akiwa mtu tofauti kabisa akirusha msumbwi mfululizo na
kutembea ulingoni kama siafu huku akimvuta Segu kenye kamba ili
amkandamizie masumbwi yake. Kijana huyo nadhifu wa kitanzania (mwenye sura
nzuri ya kuvutia na ambaye wasichana wengi wa Thailand walishinda karibu na
hoteli aliyoshukia ili kuweza kuongea naye) alitumia wakati huo kumwonyesha
Pathompothong kuwa yeye hababaishwi na masumbwi yake kwani amefanya
mazoezi ya kutosha. Segu alibadilishana masumbi na Pathompothong vilivyo
na kuufanya umati wa mashabiki waliojazana kwenye ukumbi huo kumshangilia kama
vile yeye ndiye bondia wao wakiimba Tanzania, Tanzania, Tanzania!
Katika raundi ya 6 mabondia wote
waliingia ulingoni kama vifaru na kubadilishana masumbwi ya mchanganyiko
(combinations) wakitafuta kudhibiti harakati za mpinzani mwenza. Ni katika
kubadilishana huku kwa masumbwi ambako Segu aliumizwa mkono na Mthailand Pathompothong.
Inawezekana kuwa ni katika juhudi za kumzuia ili asiendelee kurusha masubwi ya
nguvu na kudhoofisha nguvu zake.
Kuumia mkono kwa Segu ilikuwa
dhahiri kwani mwanzoni mwa raundi ya saba wakati Pathompothong alipokuwa
anamiliki ulingo dhidi ya kijana huyo mtanashati wa kitanzania.
Katikati ya raundi ya saba Segu aliona kuwa hawezi kuutumia mkono wake
vizuri na kumwashiria refarii wa mpambano kuwa anaacha!
Segu aliacha pambano hilo katika raundi
ya saba wakati mashabiki wengi katika ukumbi huo wakiwa wanaimba Tanzania,
Tanzania, Tanzania kwa jinsi alivyokuwa anapeperusha vyema bendera ya “Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania”
Yanga yazima ngebe za Simba, Toto, Polisi zaungana na Lyon kushuka daraja
![]() |
Kipa Ally Mustafa 'Barthez' alkidaka penati ya Simba |
Didier akishangilia bao lake dhidi ya Simba leo |
LICHA ya kutimia ahadi ya kuibuka na ushindi mbele ya watani zao, Mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Yanga imeshindwa kulipa kisasi kwa Simba.
Yana iliyonyukwa mabao 5-0 msimu uliopita na kujitapa kwamba leo ni lazima ingelipa kisasi imeishia kushinda mabao 2-0 na kunogesha ubingwa wao.
Mabao ya kila kipindi yaliyofungwa na nyota wa kimataifa wa Yanga, Didier Kavumbagu na Hamis Kiiza 'Diego' yalitosha kuzamisha jahazi la Msimbazi ambao walipoteza pia penati waliopata.
Kavumbagu aliiandikia Yanga bao la kwanza dakika ya nne kwa kuunganisha mpira wa kona uliopigwa na Haruna Niyonzima kabla yha Simba kupata penati baada ya Ngassa kluchezwa rafu na Mussa Mudde kushindwa kuukwamisha kwa kumlenga kipa Ally Mustafa 'Barthez'.
Bao la pili lilitupiwa kimiani katika dakika ya 63 na Kiiza baada ya kuunganisha krosi iliyomkana na mpira wa kurushwa wa Mbuyi Twite na mabeki wa Simba kuzembea kuruka na Kiiza kufungwa kwa kichwa na kuiandikia Yanga bao lililokata ngebe za kocha msaidizi wa Simba, Jamhuri Kihwelu 'Julio' aliyedai wangeifunga Yanga iwe isiwe kwa ubora wa kikosi chao.
Julio akizungumzia mechi hiyo alisema wanakubali kipigo, lakini wamefurahi kwa kushindwa kulipa kisasi cha mabao 5-0.\
Pamoja na kushindwa kulipa kisasi, lakini Yanga imeendeleza rekodi yake ya kutopoteza mechi yoyote katika duru la pili na ndani ya mwaka 2013.
Katika tukio lililosisimua mashabiki waliokuwa uwanjani ki kitendo cha mwamuzi, Martin Saanya kuanguka wakati akienda kuwaamulia Kavumbangu na Nassoro Masoud 'Chollo' na kufanya pambano hilo kusimama kwa muda ili atibiwe na jingine ni lile la Ngassa kuvishwa jezi ya Yanga na kushangiliwa kwa kubebwa na wanachama wa Yanga walioimba karibu nyumbani.'
Katika mechi nyingine, Toto African na Polisi Moro licha ya kushinda mechi zao za nyumbani dhidi ya Ruvu Shooting na Coastal Union, zimejikuta zikishuka daraja zikiungwana na African Lyon.
Toto iliifunga Ruvu mabao 2-0 kwenye uwanja wa CCM Kirumba na Polisi kuinyoa Coastal 2-0 kwenye uwanja wa Jamhuri Morogoro kwa mabao ya Kenneth Masumbuko na Ally Shomari.
Timu hizo zimeshuka daraja kwa vile Mgambo JKT ikiwa uwanja wa Mkwakwani ikipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Lyon na kuvikisha pointi 28 ambazo zimeshindwa kufikiwa na Toto na Polisi ambazo zimemaliza na poinbti 25 tu.Nao Mtibwa Sugar imejikuta ikiloa mbele ya JKT Ruvu kwenye uwanja wa Chamazi, huku JKT Oljoro ilikubali kipogo cha bao 1-0 toka kwa Azam kwa bao la Seif Abdallah, na Kagera Sugar kuizamisha Prisons Mbeya kwa bao 1-0 kupitia kwa Paul Ngway alifunga dakika ya 87 katika lililofanyika uwanja wa Sokoine Mbeya na kumaliza kwenye nafasi ya nne nyumba ya Simba.
Msimamo baada ya kumalizika kwa msimu wa 2012-2013:
P W D L F A D Pts
Young Africans 26 18 6 2 47 14 33 60
Azam 26 16 6 4 46 20 26 54
Simba 26 12 9 5 39 26 13 45
Kagera Sugar 26 12 8 6 28 20 8 44
Mtibwa Sugar 26 10 9 7 29 25 4 39
Coastal Union 26 8 11 7 25 24 1 35
Ruvu Shooting 26 8 7 11 23 28 -5 31
JKT Oljoro FC 26 7 8 11 22 29 -7 29
Tanzania Prisons 26 7 8 11 16 23 -7 29
Ruvu Stars 26 8 5 13 22 39 -17 29
JKT Mgambo 26 8 4 14 17 27 -10 28
Toto Africans 26 5 10 11 24 33 -9 25
Polisi Morogoro 26 5 10 11 15 23 -8 25
African Lyon 26 5 4 17 16 39 -23 19
Ugaidi? Watano wanaswa na vifaa vya milipuko Dar
![]() |
Kamanda Kova |
WAKATI hofu ya ugaidi iliyotanda Jijini Arusha hivi karibuni haijatulia, Jeshi la polisi nchini linawashikilia watuhumiwa watano, akiwamo mwanamke mmoja baada ya kuwanasa na vifaa vya milipuko mbalimbali ya hatari eneo la Kunduchi Mtongani jijini Dar es Salaam.
Watuhumiwa hao ni Juma Khalifani (24), Ruben Patrick (26), Happy Charles (28), Sadick Self (32) na Iddi Shaban (40) wote ni wakazi wa Kunduchi Mtongani.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini, Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Sulemain Kova, alisema kupitia oparesheni yao walifanikiwa kuwakamata wahalifu hao ambao walikuwa na milipuko hatari kinyume cha sheria.
Alisema kuwa watuhumiwa hao hawana uhalali wa umiliki wa vifaa hivyo hali ambayo iliwapa shaka zaidi juu ya suala hilo.
Kamanda alisema watuhumiwa hao baada ya kukamatwa walifanikiwa kuwakuta na nyaya 62 za milipuko zikiwa zimefungwa betri, vifaa vya kusababisha milipuko zikiwa nane (Supreme Plain detonator), nyaya ndefu mizunguko minne, mabomba 20 ya urefu wa sentimenta 30 ambazo zilijazwa mbolea ya urea na tambi rola moja.
Kova alisema vifaa hivyo ni hatari vikiunganishwa vinaweza kuhatarisha maisha ya watu pamoja na mali zao.
Pia alisema milipuko hiyo hutumika kupasulia miamba na kwamba jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi zaidi ili kujua madhumuni halisi ya watuhumiwa hao katika kumiliki vifaa saidizi na milipuko hatari.
Hata hivyo, alisema katika tukio hilo walifanikiwa kukamata dawa za kulevya aina ya bhangi gunia moja.
Kamanda Kova alisema wanashikilia gari aina ya Noah iliyosajiliwa kwa namba T.772 BYC pamoja na bajaji ya miguu mitatu yenye namba T959 BTE ambazo zimekamatwa zikiwa nyumbani kwa mtuhumiwa Sadick Seif ambaye alishindwa kuthibitisha uhalali wa kumilki vyombo hivyo vya usafiri.
Alisema baada ya upelelezi kukamilika watuhumiwa hao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani.
Aidha Kamanda Kova amewataka watu ambao wanatumia milipuko hiyo kujisalimisha kwa haraka lasivyo watachukuliwa hatua kali kwa mujibu wa sheria za usalama za nchi.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, alisema kuwa wamejipanga vyema katika suala la oparesheni ili kuwakamata wahalifu wote.
Alisema katika mkoa wake kuna matapeli wa aina mbalimbali na kwamba hivi karibuni kuna watuhumiwa walimtapeli raia wa kichina kumuuzia kiwanja ambacho tayari kilishatolewa hati ya uhalali kwa mtu mwingine.
Kenyela alisema katika tukio hilo wanamshikilia wakili mmoja wa kujitegemea kuhusika katika utapeli huo na kwamba atafikishwa mahakamani hivi karibuni.
Alisema tatizo jingine ni kuwepo kwa raia wa kigeni kuingia nchini bila kuwa na kibali hali ambayo inasababishia kuhatarisha usalama na kwamba tayari wameshachukuliwa hatua.
Pia aliwataka wananchi kutoa taarifa dhidi ya watu wahalifu ili waweze kuchukuliwa hatua
CHANZO:
NIPASHE
Cheka amcheka Mwakyembe, kisa...!
Bondia Francis Cheka akiwa na mataji aliyonyakua katika ngumi |
![]() |
Bondia Benson Mwakyembe |
Akizungumza na MICHARAZO, Cheka alisema si kweli kuwa amewapiga mabondia wa Dar Es Salaam tu katika maisha yake kwani Karama Nyilawila anatokea Mbeya na Mada Maugo ambaye pia amewahi kupata kipigo kutoka kwake ni wa mkoa wa Mara.
Cheka alikuwa akizungumzia madai ya Mwakyembe ya wiki iliyopita kuwa bondia huyo wa Morogoro amekuwa akikwepa kukutana naye huku akijitapa kuwapiga wachezaji wa Dar Es Salaam tu.
Cheka alisema pia tangu 2008 amewapiga mabondia wa nje ya nchi katika ardhi ya Tanzania bila kupoteza pambano.
"Nyilawila sio wa Dar, maskani yake ni Mbeya, Maugo anatoka Mara, labda Kaseba, Rashid Matumla, Hassani Matumla na Mtambo wa Gongo (Maneno Osward) ndio wa Dar," alisema.
"Ila mimi sikuwa napigana na bondia kimikoa... hii sio michuano ya ridhaa ni ngumi za kulipwa yeyote anayekuja hutambuliwa bondia wa uzito husika na sio eneo analotoka.
"Lazima wanipe heshima yangu kama mabondia bora Tanzania kwa sasa, kama hawamheshimu bingwa wao wanataka wampe nani heshima hiyo?
"Waangalie nimetetea taji la IBF Afrika mara ngapi na kushinda, wapigane wenyewe kwa wenyewe waache nihangaike anga la kimataifa nililete heshima kama alivyofanya Snake Man (Rashid Matumla)," alisema.
Leo ndiyo leo, Simba au Yanga leo Taifa?
![]() |
Wekundu wa Msimbazi watawapa nijni mashabiki wao kwa Yanga leo? |
![]() |
Vijana wa Jangwani wataweza kulipa kisasi kwa Simba leo Taifa? |
Tambo za timu hizo kutoka kwa viongozi, makocha na wachezaji mbali na mashabiki na wanachama wao kwa karibu wiki mbili mfululizo, wengi wanataka kuziona zinahitimishwa vipi baada ya dakika 90 za mtanange huo ambao utachezeshwa na mwamuzi, Martin Saanya.
Yanga ambao wameshatwaa taji la Ligi Kuu msimu huu wakiwanyang'anya watani zao hao wameapa kutoa kipigo kwa Wekundu wa Msimbazi ili kunogesha sherehe zao za ubingwa, wakati Simba wakipania kuwavurugia sherehe hizo.
Viongozi na makocha wa pande zote mbili wameelea matumaini yao kwa pambano hilo la leo wakiamini kwamba vikosi vyao vitaibuka na ushindi na kuzima ngebe za wapinzani wao.
Yanga wenyewe watashuka dimbani wakitokea visiwa vya Pemba wakati watani zao wanatokea Unguja walipokuwa wameenda kuweka kambi kujiandaa na mechi hiyo ambayo inasubiriwa kwa hamu na mashabiki wakikumbushia pambano kama hilo la msimu uliopita kuwa na matokeo ya aina yake.
Jangwani waliokuwa kwenye mgogoro mkubwa kati ya wanachama na viongozi wao waliaibishwa kwa kunyukwa mabao 5-0 na Simba na kunyang'anywa taji lao huku wakiongezewa idadi ya deni la vipigo baada ya kushindwa kulipa kisasi cha mabao 6-0 walichopewa tangu mwaka 1977.
Safari hii Yanga wapo vyema wana amani na utulivu na wameshanyakua taji la ubingwa mapema, tofauti na wapinzani wao ambao ni hivi karibuni hali imerejea kuwa shwari klabuni kwao.
Simba iliyo chini ya kocha Patrick Liewig kutoka Ufaransa inapewa nafasi kubwa ya kuizima Yanga inayonolewa na Mholanzi, Ernie Brandts kutokana na rekodi nzuri iliyowekwa na kikosi chake cha vijana waliopewa jukumu baada ya 'mafaza' kudengua na kuenguliwa kikosi cha Mfaransa huyo.
Hata hivyo Yanga wanapewa turufu zaidi kwa uimara wa kikosi chao na reklodi yao ya kutopoteza mechi yoyote katika duru zima la pili na mwaka mzima wa 2013 mpaka sasa, huku safu yake ya mbele ikiwa kama wembe na safu yao ya ulinzi kuwa kama zege kwa kutopitika kirahisi.
Lakini kwa soka la Simba na Yanga lenye kila aina ya mbinu lolote linaweza kutokea na pengine burudani wanayoisubiria mashabiki wa timu hizo na soka kwa ujumla kushindwa kuipata kwa nama timu zilivyokamiana.
Timu zote zina wachezaji wazuri wenye vipaji na uwezo mkubwa wa kufanya lolote muda wowote na katika eneo lolote la uwanja, hivyo mashabiki wanapaswa kusubiri kuona kipi kitakachotokea baada ya filimbi ya mwisho ya mwamuzi Saanya toka Morogoro na wasaidizi wake.
Katika pambano la raundi ya kwanza timu hizo zilitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1 na Simba itaingia uwanjani leo ikiwa na kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu kiungo wao nyota na aliyekuwa mfungaji wa moja ya mabao yaliyoizamisha Yanga Mei 6 mwaka jana , Patrick Mutesa Mafisango alipofariki kwa ajali ya gari Mei 17, 2012 ambapo inaelezwa wachezaji watavaa vitambaa vyeusi kama ishara ya kumkumbuka.
Pia mashabiki maalum wameandaliwa kwa mechi ya leo wakiwa na jezi namba 30 aliyokuwa akiivaa mchezaji huyo kama ishara ya kumuenzi mkali huyo kutoa DRC, ingawa alikuwa pia na uraia wa Rwanda.
Mbali na pambano hilo la Taifa pia leo kuna mechi nyingine sita katika viwanja vingine zitakazofungia msimu huu, huku masikio na macho ya mashabiki yakielekezwa kwenye mechi inazozihususisha timu zinazopigana kuepuka kushuka daraja inazozihusisha timu za Polisi Morogoro, Toto Africana na Mgambo JKT.
Toto wenyewe watakuwa uwanja wa nyumbani CCM Kirumba kuwakaribisha Ruvu Shooting, kama itakavyokuwa kwa Polisi Morogoro watakaokuwa Jamhuri, Morogoro kuumana na Coastal Union ya Tanga kadhalika Mgambo JKT watakuwa uwanja wa Mkwakwani kuumana na African Lyon iliyoshuka daraja.
Matokeo yoyote ya viwanja hivyo vitatu vitatoa picha halisi ya timu zipi mbili za kuungana na Lyon kucheza Ligi Daraja la Kwanza msimu ujao na kuzipisha rasmi Ashanti United, Mbeya City na Rhino Rangers zilizopanda daraja.
Mechi nyingine za leo za kuhitimishia msimu ni JKT Oljoro watakaowakaribisha washindi wa pili wa ligi hiyo, Azam kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha, JKT Ruvu wataumana na Mtibwa Sugar uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam na Prisons Mbeya itaialika Kagera Sugar katika uwanja wa Sokoine Mbeya.
Je, ni Simba au Yanga itakayocheza leo Taifa ama ni Toto, Polisi na Mgambo itakayoungana na Lyon? Tusubiri.
Real Madrid wamaliza msimu kwa aibu Hispania
![]() |
Wachezaji wa Atletico Madrid wakitanua na taji lao la Mfalme |
![]() |
Ronaldo alipomuumiza Gabi na kuzodolewa akitolewa uwanjani |
WALIOKUWA mabingwa wa Hispania, Real Madrid wamemaliza vibaya msimu wa 2012-2013 baada ya kubanjuliwa mabao 2-1 na wapinzani wao, Atletico Madrid katika Fainali ya Kombe la Mfalme, huku nyota wao Cristiano Ronaldo na kocha Jose Mourinho walilimwa kadi nyekundu kwa nyakati tofauti.
Atletico waliokuwa kwenye uwanja wa ugenini wa wapinzani wao, Santiago Bernabeu walipata ushindi huo na kunyakua taji hilo katika muda wa nyongeza kwa mabao ya Diego Costa aliyefunga dakika ya 35 na lile la jioni la jioni la dakika ya 99 kupitia Joao Miranda lilitosha kuikata ngebe za Real waliotangulia kupata bao.
Bao hilo liliwekwa kimiani na Ronaldo dakika ya 14 tu ya mchezo huo kabla ya kujikuta akiishia kutolewa nje na mwamuzi kwa kumpiga mchezaji wa Atletico, gabi kama ilivyokuwa kwa kocha wake ambaye ni mreno mwenzie, Mourinho maarufu kama 'the Only One' a.k.a Special One.
Kipigo hicho kimeifanya Real Madrid kumaliza msimu huu bila taji lolote kutokana nna ubingwa waliokuwa wanaushikili wa Ligi ya Hispania kunyakuliwa na watani zao Barcelona pia kuondolewa kwenye nusu fainali za Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Redd's Miss Bagamoyo 2013 kufanyika Mei 24
![]() |
Rose Lucas, Mshindi wa shindano la Redd's Miss Bagamoyo 2012 |
Mratibu wa shindano hilo ambaye pia ni Mkurugenzi wa kampuni ya Asilia Decoration, Awetu Salim aliiambia MICHARAZO alisema kambi ya mazoezi kwa warembo hao inaendelea mjini humo na kwamba maandalizi kwa ujumla yamekamilika na anatarajiwa fainali za mwaka huu kuwa za aina yake.
Anasema hii inatokana na warembo waliojitokeza safari hii ambao alidai ni vimwana haswa wenye sifa na vigezo vyote na kuwataka mashabiki wa fani hiyo kujitokeza kwa wingi kuhudhuria.
Awetu aliongeza kuwa katika kusindikiza shindano hilo siku hiyo ukumbi kutakuwa na burudani mbalimbali za muziki na ngoma asilia toka kwa wasanii na makundi tofauti akiwamo mwanadada Aisha Ramadhani a.k.a Isha Mashauzi na bendi yake ya Mashauzi classic, muziki wa kizazi kipya kutoka kwa Chuo cha Sanaa(tasuba), ngoma ya kabila la wakwere wenyeji wa Bagamoyo na nyinginezo.
MSAM kuwaaga wenzao kwa harambee ya ujenzi wa msikiti
![]() |
Jengo la Chuo cha Kumbukumbu ya Mwl Nyerere linavyoonekana kwa mbali |
NA MWANDISHI WETU
UMOJA wa Wanafunzi wa Kiislam Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu
Nyerere (MSAM) kilichopo Kigamboni Jijini
Dar es Salaam unaomba wadau mbalimbali
kujitokeza katika mahafali ya kuwaaga wanafunzi wa kiislam wanaomaliza chuo ambayo
yataambatana na harambee ya uchangiaji
wa fedha za ujenzi wa msikiti chuoni hapo.
Ombi hilo limetolewa na Katibu Mkuu wa MSAM Abdullatif
Jafari wakati akizungumza na mwandishi wa habari hivi karibuni Jijini Dar es
Salaam.
Jafari alisema chuo kimewapa
ruhusa ya kutafuta mdhamini wa ujenzi wa msikiti kwa kipindi kirefu ila
hadi sasa hawajapata mafanikio kwani baadhi ya wahisani wamekuwa wakiaahidi
bila mafanikio pamoja na ukweli kwamba MSAM imekuwa ikiteleza maagizo yao kila
wanapohitaji.
Alisema matarajio yao ni kuhakikisha kuwa wanapata kiasi cha
shilingi milioni mia moja za kuanzia ujenzi hivyo basi wanaaomba watu wenye nia
nzuri kwa vijana wa kiislam wanaoishi maeneo ya chuo waweze kufanikisha zoezi
hilo mapema.
Katibu huyo alisema wanafunzi wamekuwa wakichanga mara kwa
mara ila juhudi zao zimekwama hivyo wanaomba mtu, taasisi yoyote yenye uweze kuwasaidia
ujenzi wa msikiti huo ili waweze kumuabudu mungu kwa amani na kwa wakati.
’’Jumamosi ijayo tunawaaga wenzetu wanaomaliza hivyo basi
tunataka kutumia fursa hiyo kuweza kuchangisha fedha za ujunzi wa msikiti
nadhani nao watakuwa wameacha alama Fulani katika haarakati hizi’’, alisema.
Jafari alisema iwapo tutapata ushirikiano kutoka kwa wadau
mabalimbali nchini tunaamini kuwa upo uwezekano mkubwa wa kufanikisha zoezi
hilo mapema na dhana ya kufikiria mtu mmoja tutaondokana nayo.
Alisema ni vema jamii ikatambua kuwa kufanikisha ujenzi huo
itakuwa imechangia msaada mkubwa katika kujenga imani na maadili ya vijana
ambao wanasoma katika chuo hicho cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni.
Aidha Katibu huyo alitoa rai kwa wale wote wenye nia ya
kuchangia ujenzi huo wa msikiti na hawataweza kufika wanaweza kutoa michango
yaao kwa njia za M Pesa 0766656730, Tigo Pesa 0713774828 au akaunti namba ya
jumuiya Muslim Students Association of Mwalimu Nyerere (MSAM) 3300825636 Kenya Commercial
Bank Samora Avenue.
Subscribe to:
Posts (Atom)