STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, January 14, 2014

HIZI NDIZO POROJO NYINGINE ZA MWISHO WA DUNIA


WAKATI binadamu wakiendelea na mipango yao ya kuifanya dunia kuwa sehemu salama ya kuishi kimazingira, kiulinzi na usalama, utabiri mpya wa kutisha unaonesha kuwa mwaka 2032 ndiyo mwisho wa sayari hii ya tatu katika mfumo wa jua. Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali katika mitandao ya internet, sayari iitwayo Nibiru, ambayo kisayansi inafahamika kama Planet X ipo njiani kuigonga dunia na hivyo kusababisha majanga mbalimbali kutokea.
ITAONEKANA ANGANI KAMA MWEZI
Kwa mujibu wa mitandao hiyo ya kisayansi, sayari hiyo ambayo inaisogelea dunia kwa kasi kubwa, itaonekana kubwa na angavu wakati wa usiku angani na kuwa katika umbo la mwezi na hivyo kufanya miezi ionekane miwili.
DALILI KWAMBA IPO JIRANI
Taarifa zaidi za kisayansi zinasema kuwa, kadiri sayari hiyo inavyozidi kusogea, dunia itaanza kutikisika na kusababisha matetemeko ya ardhi kuongezeka sehemu mbalimbali. Mbali na dunia kutikisika na matetemeko, milipuko ya volcano nayo itatokea huku idadi kubwa ya milipuko hiyo mipya ikiongezeka, vimbunga vikubwa kama Tsunami vitaibuka na mwishowe dunia itapigwa na bomu la miamba midogo na vimondo kutokea angani.
DUNIA ITAKUMBWA NA GIZA NENE
Wakati volcano zote duniani zitakapoanza kulipuka na zingine mpya kujitokeza, dunia itafunikwa na giza nene  na matope kwa wakati wote wa usiku na mchana huku watu wakitakiwa kusoma katika Biblia Joel 2: 1-2 na Zephaniah 1:14-17.
NI TUKIO LA AINA YAKE KARNE YA 21
Nibiru inatajwa kama kitu kinachoisogelea dunia kinachoaminiwa kusababisha madhara makubwa ambapo kama hakitaigonga dunia, kitasababisha mtikisiko usio wa kawaida kitakapopishana nayo. Baadhi ya wanasayansi wanaamini kuwa kitendo hicho kitatokea mapema katika karne ya 21 (tuliyonayo sasa). WANASAYANSI WAPINGANA
Baadhi ya wanasayansi wanapinga kwa maelezo kwamba hakuna ushahidi wowote wa kitafiti unaoonesha wazi kwa mabingwa wa anga za juu waliobobea wa masuala ya nyota.
MWANAMKE ALIWAHI KUOTA NDOTO
Kwa mara ya kwanza jambo hilo lilitokea mwaka 1995, wakati mwanamama Nancy Lieder muasisi wa mtandao wa ZetaTalk, aliwahi kudai kuoteshwa ndoto kwamba, Mei 2003 kuna kitu kitaingilia mfumo wa jua (solar system) na kusababisha dunia kutoboka tundu litakalosambaratisha sehemu kubwa ya kizazi cha binadamu. Lieder aliifafanua kuwa, kitu hicho kitakuwa na ukubwa wa mara nne ya dunia.
BAADA YA NDOTO
Baada ya mwanamama Lieder, mtu wa kwanza kuizungumzia Nibiru alikuwa Mark Hazlewood, mwanachama wa zamani wa mtandao wa ZetaTalk ambaye mwaka 2001 alichapisha kitabu kilichoitwa Blindsided na kusema kuwa mwisho wa dunia ungekuwa mwaka 2003 baada ya kuwasili kwa sayari ya kumi (Nibiru). Katika mfumo wa sasa, baadhi ya wanasayansi wanasema sayari ziko 12, wakizitaja kwa namba 1. Jua 2. Mercury 3. Venus 4. Dunia 5. Luna (mwezi) 6. Mars 7. Jupiter 8. Saturn 9. Uranus 10. Neptune 11. Pluto 12. Nibiru.
IMANI NYINGINE YASEMA MWISHO WA DUNIA NI FEBRUARI 22, 2014
Hata hivyo, utabiri mpya uliotolewa na watu wa jamii ya Vikings jijini New York, Marekani umesema mwisho wa dunia ni Februari 22, mwaka huu. Mitandao mbalimbali pamoja na gazeti maarufu la Daily Mail la Uingereza lilielezea utabiri huo uliofanywa na jamii hiyo ukidai kuwa mwisho wa dunia utatokana na Mungu Odin kupigana na kuuawa na shetani Wolf Fenrir, hivyo kuiachia dunia anayoishikilia. Wamesema baada ya kuiachia dunia itafurika maji ambayo yatakuwa na sumu, hivyo viumbe wote watateketea. WATUMISHI WA MUNGU TANZANIA
Baadhi ya watumishi wa Mungu nchini wamekuwa wakisimamia andiko la kwenye Biblia linalosema kuwa, hakuna mwanadamu anayeijua siku wala tarehe ya mwisho wa dunia na ni siri ya Muumba. Makanisa mengi nchini Tanzania yana sera tofauti lakini yanaongozwa na Biblia moja. Makanisa hayo ni Romani Katoliki, Lutheran (KKKT), Anglikana na makanisa ya kiroho kama Full Gospel& Bible Fellowship la Zakaria Kakobe.
FREEMASON WABARIKI
Jamii ya Freemason tayari imebariki mwisho wa dunia kwamba umefika na dunia inatarajie tukio kubwa la pamoja. Mitandao ya jamii hiyo inataja kama hizi ni nyakati za mavuno kwa maana kwamba, upande wa Mungu na shetani kushindania watu huku waendao upotevuni  wakiwa wengi.
MFUMO WA DUNIA TANGU KUUMBWA
Kwa mujibu wa kitabu kinachoitwa Panorama ya Biblia, ulimwengu tangu kuumbwa kwake umekuwa na matukio makubwa kila baada ya miaka 2000 (inaweza isitimie au ikapita kidogo). Tangu kuumbwa kwa Adamu na Eva mpaka gharika inadaiwa ni miaka 2000. Gharika hadi dunia kubadili mfumo wa mawasiliano (Mnara wa Babeli) ni miaka 2000. Kuzaliwa kwa Yesu hadi saa ni miaka 2000 ambapo katika karne hii, dunia huenda ikaingia katika tukio kubwa sana ambalo halijawahi kutokea.
GPL

Ethiopia yashindwa kuhimili vishindo vya Libya CHAN 2014

Ethiopia
Libya
WAWAKILISHI wa ukanda wa Afrika Mashariki na Ethiopia jana ilianza vibaya michuano ya CHAN-2014 baada ya kufungwa mabao 2-0 na Libya katika pambano la kundi C lililochezwa kwenye uwanja wa Free State, Bloemfontein.
Ethiopia wanakamata nafasi ya pili katika ubora wa viwango vya soka kwa nchi za CECAFA nyuma ya Uganda ambayo juzi ilianza kwa kuipa kipigo Burkina Faso walishindwa kuhimili vishindo vya waarabu na kujikuta wakifungwa bao la mapema katika dakika ya nne tu ya kuanza kwa pambano hilo.
Bao hilo liliwekwa kimiani na Elmutasem Abushnaf na kudumu hadi wakati wa mapumziko na kwenye kipindi cha pili Ethiopia waliwabana Libya na kuonyesha dalili za kurejesha bao hilo kabla ya kujikuta wakiruhusu tena bao la pili katika dakika ya 83 lililofungwa na Abdulsalam Omar akimalizia kazi nzuri ya Motasem Sabbou.
Michuano hiyo inatarajiwa kuendelea tena leo kwa michezo ya kundi D ambapo DR Congo itaavana na Mauritania kabla ya majirani Burundi kuvaana na Gabon katika mechi nyingine na kesho kuanza mechi za raundi ya pili kwa timu za kundi A kuonyeshana kazi.

Hatimaye Ronaldo azika 'mzimu' wa Messi Ballon d’Or

Ronaldo akiwa na tuzo yake
Ronaldo akilia kwa furaha
Incomparable: Legendary striker Pele won an honourary prize at the Gala in Zurich
Gwiji Pele alipea tuzo katia usiku huo mjini Zurich
Emotional: The Brazilian couldn't keep back the tears
Emotional: The Brazilian couldn't keep back the tears
Mfalme wa soka: Gwiji wa Brazil, Pele alishindwa kujizuia kutoa machozi alipokuwa jukwaani
Out at the top: Retied Jupp Heynckes was named Coach of the Year after winning the Champions League
Retied Jupp Heynckes ameshinda tuzo kocha bora wa mwaka wa dunia baada ya kuiwezesha Bayern Muich kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya
Stunner: Zlatan Ibrahimovic won the Puskas prize for the best goal of the year for his goal against England
Mkali: Zlatan Ibrahimovic ameshinda tuzo ya Bao Bora la mwaka, maarufu kama Puskas 
Unreal: His overhead kick was during Sweden's 4-2 friendly win over England in November 2012
Bao lake tik tak Sweden ikiifunga 4-2 England Novemba mwaka 2012 ndilo bao bora la mwaka
Recognised: German keeper Nadine Angerer won the women's Player of the Year award
Kipa wa Ujerumani, Nadine Angerer ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa kike wa mwaka wa Dunia
Duo: Ronaldo and Angerer pose side-by-side after being named the best players in the world
Wawili: Ronaldo na Angerer baada ya kutajwa wanasoka bora wa dunia 
Shot stopper: Angerer in goal for the German national team during a friendly against Japan
Prize: She was part of the Germany team that won the women's European Championships last year
Taji: Angerer alikuwemo kwenye kikosi cha Ujerumani kilichoshinda Kombe la ubingwa wa Ulaya kwa wanawake
***
NYOTA wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo hatimaye ameufunika 'mzimu' wa Lionel Messi baada ya usiku wa jana kutangazwa kuwa Mwanasoka Bora wa Dunia.
Ronaldo ametwaa tuzo ya Ballon D’or kwa kumpiku Lionel Messi ambaye ni mpinzani wake mkubwa.
Mara baada ya kukabidhiwa, huku akionyesha kweli Ronaldo alipania kuibeba tuzo hiyo safari hii, alijikuta akimwaga chozi mbele ya gwiji la soka duniani, Pele.
Ronaldo mara ya mwisho aliibeba tuzo hiyo mwaka 2008 wakati akiitumikia Manchester United aliyoiwezesha kubeba ubingwa wa Ulaya na Dunia, kabla ya baadaye kuhamia Real Madrid.
Tokea tuzo hizo zilipoanza kuendeshwa na Fifa, hakuna mchezaji aliyewahi kushinda zaidi ya Messi ambaye alizitwaa mara nne mfululizo.
Lakini jana kwa mara ya kwanza, Ronaldo kama alivyokuwa akipewa nafasi hiyo kweli ameshinda na kumbwaga Messi. Huku Frank Ribbery akishika nafasi ya tatu.

Arsenal mbele kwa mbele yarejesha kileleni ikilipa kisasi kwa Villa

Kitu!
Werawera mwanawaneee!
VIJANA wa Arsene Wenger wamezidi kuonyesha dhamira yao ya kunyakua taji la Ligi kuu ya England baada ya usiku wa jana kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo baada ya kuitambia Aston Villa ikiwa kwao kwa kuicharaza mabao 2-1.
Ushindi huo umeifanya Arsenal kuchupa toka nafasi ya tatu iliyokuwepo baada ya Chelsea na Manchester City kuiporomosha na kupokezana kwa muda uongozi wa ligi hiyo mwishoni mwa wiki kwa kufikisha poiinti 48, moja zaidi ya City yenye 47 na mbili zaidi ya Chelsea iliyokusanya pointi 46.
Mabao yaliyoihakikishia Arsenal kurejea kileleni yalifungwa na Jack Wilshere alifunga dakika ya 34 na Olivier Giroud akaongeza la la pili dakika ya 35 na kluifanya vijana hao wa London ya Kaskazini kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa mabao 2-0.
Kipindi cha pili kilikuwa cha wenyeji kuweza kujipatia bao pekee la kufutia machozi lililofungwa na nyota wao  Cristian Benteke katika dakika ya 76 na kuifanya Arsenal kuvuna pointi tatu na pia kulipa kisasi cha kunyukwa na Villa katika mechi yao ya duru la kwanza kabla ya vijana hao wa Wenger kuzinduka.

Monday, January 13, 2014

Ghana waanza vyema CHAN wainyuka Congo kimoja

CHAN 2014 : Group C Ghana and Congo collide
GHANA imeanza vyema michuano ya CHAN inayofanyika nchini Afrika Kusini baada ya jioni hii kuilaza Jamhuri ya Kongo kwa bao 1-0 katika pambano lililochezwa kwenye uwanja wa Free State.
Bao pekee lililoihakikishia 'vigogo' hao kukusanya pointi tatu muhimu, lilitupiwa kambani na Theophilus Anobaah katika dakika ya 34 ya pambano hilo.
Muda mfupi ujao kundi hilo la C litashuhudia pambano jingine kali kati ya DR Congoi itakayoumana na Ethiopia kwenye uwanja huo huo katika mfululizo wa michuano hiyo.

Simba yashindwa kutamba kwa Waganda taji hilooo!


FUPA lililowashinda watetezi wa Kombe la Mapinduzi, Azam jioni ya leo umewashinda pia Simba, baada ya 'Mnyama' kuchezea kichapo cha bao 1-0 toka kwa vijana wa KCC ya Uganda ambao wamenyakua taji hilo na kuondoka nalo ikiwa ni kwa mara ya kwanza kwa timu ya nje ya Tanzania kutwaa kombe hilo.
Simba ambayo ilikuwa ikipewa nafasi kubwa ya kuficha aibu ya Tanzania kushuhusia timu zake zote zikikongotwa na wageni, ilishindwa kuhimili vishindo vya Waganda licha ya kucheza jihad hasa dakika za lala salama.
Bao pekee lililowanyong'onyesha Simba na watanzania kwa ujumla lilitumbukiwa na Herman Wasswa katika kipindi cha kwanza.
Kwa ushindi huo KCC imekuwa klabu ya kwanza nje ya Tanzania kunyakua taji hilo tangu lilipoanzishwa mwaka 2006, ikiwa haijapoteza mchezo wowote tangu kuanza kwa michuano hiyo Januari Mosi.
Timu hizo zote zilikuwa kundi B mpaka kufika fainali zilikuwa hazijapoteza mechi zao na katika mechi baina yao zilishindwa kutambiana kwa kutoka suluhu.
Michuano hiyo ilishirikisha timu 12 nne kutoka nje na nyingine za Tanzania Bara na Zanzibar. klabu za nje ni URA na KCC za Uganda, Tusker na AFC Leopards za Kenya.
Kutwaa kwa taji hilo KCC imefuata nyayo za dada zao wa netiboli waliotwaa ubingwa wa mchezo huo kwa kuifunga Tanzania katika fainali siku mbili zilizopita.
Simba iliifunga URA ya Uganda katika mechi ya nusu fainali na KCC ikailamba Azam kwa mabao 3-2 na kuitemesha taji ililotwaa mwaka jana kwa kuichapa Tusker ya Kenya.