STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, December 5, 2012

YANGA YAZINDUA KALENDA YAKE KWA MBWEMBWE



YANGA walitumia burudani ya muziki na wanenguaji kujaza watu kwenye makao makuu ya klabu yao jijini Dar es Salaam wakati wakizindua Kalenda yao ya mwaka 2013.
Mabingwa hao wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame) wameingia ubia wa mwaka mmoja na kampuni ya ‘Pecha Media & Health Promotion’ kutengeneza kalenda za klabu yao.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Nasib Limira alisema kuwa kampuni yake imeamua kutengeneza kalenda za Yanga ili kuisaidia klabu hiyo kukuza uchumi wake.
Alisema klabu hiyo inayojiandaa kwenda Uturuki kuweka kambi kwa ajili ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu huu, ina vyanzo vingi vya mapato, lakini inakosa fedha nyingi kutokana na kuwapo kwa ‘wajanja’ wanaotengenezaa bidhaa kwa jina la klabu hiyo na kuziuza kwa faida yao binafsi.
“Yanga ni klabu kubwa, lakini inakosa pesa nyingi kutokana na kuwapo kwa watu ambao wanajinufaisha kwa kutengeneza kalenda na bidhaa nyingine wakitumia jina la klabu hii. Tumeamua kuwasaidia kutengeneza kalenda hizi ikiwa ni sehemu ya mchango wetu katika kuwasaidia kuinua kipato chao,” alisema Limira.
Katibu Mkuu wa Yanga, Lawrence Mwalusako alisema kuwa kutengenewa kwa kalenda hizo ni mwanzo mzuri kuonesha kwamba wamedhamiria kuinua kipato cha klabu hiyo na kudhibiti mianya ya watu kutengeneza bidhaa kwa jina la klabu hiyo huku pesa za mauzo zikiishia kwenye mifuko yao bila klabu hiyo kunufaika chochote.
“Huu ni mwanzo tu, tunataka kuwadhihirishia wapenzi wa Yanga kwamba tuko makini na mali za klabu. Tumeanza na Kalenda, zitafuata bidhaa nyingine kama jezi maana watu wengui wamekuwa wakituhujumu katika hili,” alisema Mwalusako.
Alisema kalenda hizo zinauzwa kwa Sh. 5,000 na katika kila kalenda Yanga itapata Sh.1,500 na kwamba kampuni hiyo imeanza kwa kuitengeneza nakala 100,000.
Hiyo ni mara ya kwanza kwa Yanga, ambao wamemaliza mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo wakiwa katika nafasi ya kwanza, kutengeneza kalenda maalum za klabu yao tangu ianzishe mwaka 1935.

Afisa Habari KIFA afia ofisini



AFISA Habari wa chama cha soka Manispaa ya Kinondoni (KIFA), Seif Mairo 'Saddam', alifariki dunia jana baada ya kuanguka ghafla akiwa kwenye ofisi za chama hicho.
Taarifa za kifo chake ziliwasilishwa na Mweka Hazina wa KIFA, Harid Kamguna.
Kamguna alisema Mairo aligundulika kuwa tayari amefariki baada ya kufikishwa katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam.
Alisema Afisa habari huyo mwenye umri wa miaka 76 anatarajiwa kuzikwa leo mchana katika makaburi ya Ndugumbi jijini Dar es Salaam.
Alisema marehemu alianza kazi hiyo tangu mwaka juzi na alisifiwa kwa ushirikiano wake mzuri na vyombo vya habari.
Enzi za uhai wake Mairo, aliyekuwa akifahamika zaidi kama Saddam, mbali na kuucheza mpira katika timu mbalimbali pia amewahi kuziongoza klabu kadhaa pamoja na soka la kuendeleza vipaji vya watoto na vijana kupitia chama cha Kinondoni, KIDYOSA na ni mmoja wa waasisi wa chama cha yosso cha Dar, DAYOSA aliyowahi kuwa Katibu Msaidizi kwa kipindi kirefu kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu wa chama hicho.
Kamguna alisema marehemu ameacha mke na mtoto mmoja. Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi. Amen.

Chanzo:NIPASHE

Tanzania kubeba maombi AFCON 2017



Na Sanula Athanas
RAIS wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa), Leodegar Tenga amesema kuwa wamejipanga kutuma maombi ya kuandaa fainali za Mataifa ya Afrika mwaka 2017 huku akiipa nafasi kubwa Tanzania kuwa moja ya nchi zitakazoandaa.
Tenga, ambaye pia ni rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya shirikisho hilo jijjini Dar es Salaam jana.
"Kuna kitu ambacho tunakifanya kuhusu kuandaa michuano hiyo, kitakapokamilika tutawataarifu. Tanzania ina nafasi kubwa ya kuwa moja ya nchi zitakazoandaa michuano hiyo kutokana na miundombinu iliyopo na mapenzi ya soka miongoni mwa watu wake,” alisema Tenga bila kubainisha kitu kipi hasa wanakifanya.
Hata hivyo, taarifa kutoka Kenya zinaeleza Waziri wa Michezo na Vijana wa nchi hiyo, Ababu Namwamba alisema mwezi uliopita kuwa viongozi wa soka wa nchi za Uganda, Kenya na Tanzania walipanga kukutana Kampala, Uganda wakati wa michuano inayoendelea ya Kombe la Chalenji kuzungumza kutuma maombi ya kuandaa kwa pamoja AFCON 2017.
Waziri huyo alikaririwa na vyombo vya habari nchini humo akisema: “Tunasikitika kushindwa kutuma maombi ya kuandaa mashindano makubwa kutokana na miundombinu mibovu. Tunahitaji kuwekeza kwenye miundombinu ya michezo ili kuwa kwenye nafasi nzuri ya kuandaa mashindano makubwa,” alisema.
Kenya haijawahi kuandaa michuano mikubwa tangu iandae mashindano ya All African Games mwaka 1987. Tanzania yenye uwanja wa kisasa wa Taifa wa Dar es Salaa unaoweza kuchukua watu 60,000, ‘inazipiga fimbo’ nchi jirani za Kenya na Uganda.

UFAFANUZI WA WARAKA
Katika hatua nyingine, Tenga alisema sababu ya kuwaandikia wanachama wa TFF waraka wa kuwaomba wapitishe mabadiliko ya katiba ya shirikisho hilo badala ya kusubiri idhini hiyo kwenye Mkutano Mkuu wa Dharura, ni tatizo la ukosefu wa fedha.
Tenga alisema ni kweli kwamba walipaswa kuitishia mkutano wa dharura ili kupitisha mabadiliko hayo lakini TFF haina fedha ya kuitisha mkutano huo ambao hugharimu hadi Sh. milioni 110.
Alisema mabadiliko hayo ni maagizo ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) na kwamba wasipoyatekeleza, Tanzania haitaruhusiwa kushiriki michuano yoyote ya kimataifa kuanzia mwakani.
Nahodha huyo wa zamani wa timu ya taifa (Taifa Stars), alisema baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF wakiwamo wa mkoa wa Kagera wamepinga hatua hiyo huku Pwani wakihitaji ufafanuzi zaidi kabla ya kupitisha waraka huo.
“Tumetuma waraka kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF ili waturuhusu kufanya marekebisho ya katiba yetu. Tunatambua kwamba tulipaswa kuitisha Mkutano Mkuu wa Dharura ili wajumbe wakae na kupitisha, lakini hali yetu kiuchumi siyo nzuri,” alisema Tenga.
“Kwa miaka saba iliyopita tulikuwa tunatumia kati ya Sh. milioni 90 hadi 110 kuandaa kila Mkutano Mkuu wa TFF. Pesa iliyopo kwa sasa inatosha Mkutano Mkuu mmoja tu ambao ni wa Uchaguzi Mkuu.
“Endapo agizo hili la FIFA tungeliipata mapema, tungelizungumza katika mkutano uliopita, lakini tulipata taarifa Julai mwaka huu,” alisema.
Rais huiyo pia alizipongeza timu za taifa za Kilimanjaro Stars na Zanzibar Heroes kwa kuingia hatua ya nusu fainali katika michuano inayoendelea ya Kombe la Chalenji.

Chanzo: NIPASHE
   

SELCOM PAYPOINT YAANZA KUUZA VOCHA ZA ZUKU...!

Meneja wa matangazo na Masoko wa Kampuni ya SelCom wireless Paypoint Juma Mgori, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana wakati wa kutangaza rasmi Kampuni hiyo kuanza kuuza vocha za kulipia king’amuzi cha Zuku kupitia vituo mbalimbali vya Selcom Paypoint. Kushoto ni Meneja Mkuu wa Zuku Tanzania, Fadhil Mwasyeba.

Meneja wa matangazo na Masoko wa Kampuni ya SelCom wireless Paypoint Juma Mgori , akifafanua jambo kwa wanahabari (hawapo pichani) juu ya huduma wanazotoa ikiwa ni pamoja na ulipiaji wa bili mbalimbali kama za simu za makampuni yote, Luku, Startime, tiketi za treni za jijini Dar es Salaam, kulipia ada za mitihani (NECTA), kuangalia matokeo na sasa Zuku.

Meneja Mkuu wa Zuku Tanzania Fadhil Mwasyeba  akizunguma na waandishi wa habari wakati wa makubaliano ya mkataba wa kujiunga na SelCom kwa ajili ya Malipo ya Zuku.

Meneja Mkuu wa Zuku Tanzania Fadhil Mwasyeba kushoto akizunguma na waandishi wa habari wakati wa makubaliano ya mkataba wa kujiunga na SelCom kwa ajili ya Malipo ya Zuku, wengine ni  Meneja wa matangazo na Masoko wa Kampuni ya SelCom wireless Paypoint Juma Mgori   na Meneja wa Bidhaa na uboreshwaji wa viwango Julio Batilia .

Waandishi wa Habari Rehema Kilagwa wa NIPASHE (mbele kulia), Mwasiti wa The Guardian (wa pili kulia) na wengine wakifuatilia maelezo kutoka kwa kina Mgori wa SelCom na Fadhili wa Zuku (hawapo pichani) wakati wa mkutano wao na waandishi wa habari kuelezea namna wateja wanavyoweza kununua vocha za Zuku kupitia simu za mikononi jana Desemba 4, 2012.

Meneja Mkuu wa Zuku Tanzania Fadhil Mwasyeba (wa pili kushoto) akibadilishana hati ya makubaliano ya kulipia king'amuzi cha Zuku kwa njia ya mtandao na Meneja wa matangazo na Masoko wa Kampuni ya SelCom wireless Paypoint Juma Mgori,  makubariano hayo yamefanyika Dar es salaam jana kwa ajili ya kurahisisha hudumu hio. Wanaoshuhudia ni maofisa kutoka Selcom na Zuku.

UGANDA YAIFUATA KILI STARS NUSU FAINALI TUSKER CHALLENGE 

Chanzo BIN ZUBEIRY 

Wachezaji wa Uganda wakimpongeza Geoffrey Kizito (anayetazama kamera amekumbatiana na Kiiza), baada ya kufunga bao kwanza dakika ya nne dhidi ya Ethiopia katika Robo Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge kwenye Uwanja wa Mandela, Namboole mjini Kampala. Uganda ilishinda 2-0 bao lingine likifungwa na Robert Ssentongo dakika ya 60 na kwa ushindi huo, Uganda itamenyana na Tanzania Bara katika Nusu Fainali Alhamisi usiku, mchezo ambao utatanguliwa na Nusu Fainali nyingine kati ya Kenya na Zanzibar.
Ssentongo akisababisha

Kiiza mawindoni

Kipa Samson Asfaw Worku akiwa amedaka mpira, huku beki wake Girma Bekele Debele akimdhibiti Brian Umony kulia

Gotochi Panom Yietch akigombea mpira na Robert Ssentongo kulia

Robert Ssentongo anaondoka na mpira baada ya kumlamba chenga beki wa Ethiopia kulia

Hamisi Kiiza akimtoka Chala Deriba Debala wa Ethiopia

Kiiza, Walusimbi, Wasswa wakicheza na Ssentongo 

Kutoka kulia Hamisi Kiiza na Henry Kalungi wakimpongeza Robert Ssentongo kufunga bao la pili

Tuesday, December 4, 2012

Bwana Misosi avunja ukimya na mpya

Bwana Misosi katika pozi

STAA wa kitambo wa muziki wa Bongofleva, ambaye kwa sasa amejitosa kwenye fani ya filamu, Joseph Rushahu 'Bwana Misosi', amevunja ukimya kwa kuachia wimbo mpya uitwao 'Iweje'.
Wimbo huo umefyatuliwa na Bwana Misosi, baada ya kipindi kirefu cha ukimya tangu mwaka jana alipoachia nyimbo mbili za 'Pilato na Game' alioimba na Sir Juma Nature na Fid Q na ule wa 'Mungu Yupo Bize'alioimba na Said Chigunda 'Chegge'.
Akizungumza na MICHARAZO, Bwana Misosi, alisema wimbo huo mpya ameurekodia studio za HM Records zilizopo Kawe na anatarajiwa kuachia hivi karibuni sambamba na video yake aliyoanza kuishuti.
"Kaka nimekamilisha 'ngoma' mpya iitwayo 'Iweje' ambayo nimekamua mwenyewe bila kupigwa tafu na mtu na kwa sasa nakamilisha mipango ya video kabla ya kuachia kwa pamoja itakapokamilika video hiyo," alisema Bwana Misosi.
Msanii huyo alisema wimbo huo kama zilizotanguliwa zitakuwa za kufanyia show tu na wala hana mpango wa kutoa albamu kama alivyofanya mwaka 2004 na 2007.
"Sina mpango wa kutoa albamu, natoa singo tu kuwapa burudani mashabiki wangu sawia na kupata nafasi ya kugonga shoo," alisema.
Aliongeza wakati akiendelea na mchakato wa kupakua video ya wimbo huo wa 'Iweje', pia anaendelea na zoezi la upigaji picha wa filamu mpya ya pili anayotarajiwa kuibuka nayo.
Bwana Misosi , aliyeingia kwenye fani hiyo akiwa na filamu ya 'Mkoba' ambayo ipo njiani kuachiwa mtaani ikiwa imeshirikisha wakali kama Amanda na Mzee Majuto, alisema filamu hiyo mpya ya pili ipo hatua ya mwisho kabla ya kukamilika.

Zuku Tv yazindua huduma mpya ya malipo kwa wateja wao

Meneja wa kampuni ya Wananchi Satellite Ltd, Fadhil Mwasyeba (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa huduma za malipo kwa wateja wao uliofanyika leos asubuhi jiji Dar es Salaam baada ya kampuni hiyo kuingia mkataba na kampuni ya Selcom Wireless Ltd. Anayeonekana kati ni Meneja Uhusiano wa Selcom, Juma Tumaini Mgori.



KAMPUNI ya Wananchi Satellite Ltd inayomiliki televisheni ya kulipia ya Zuku kikishirikiana na kampuni ya Selcom Wireless Ltd zimeingia mkataba wa kuanza kutoa huduma rahisi ya malipo kwa wateja wa televisheni hiyo kwa nchi nzima.
Uzinduzi wa huduma hizo ulifanyika leo jijini Dar es Salaam baada ya viongozi wa pande hizo mbili kusaini mkataba huo mbele ya waandishi wa habari katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ukumbi wa Diamond, uliopo  Ubungo.
Meneja wa Wananchi Satellite kwa hapa nchini, Fadhili Mwasyeba alisema wameamua kurahisisha huduma ili kuwapa fursa wateja wao kufanya malipo kwa njia nyepesi na ya haraka tofauti na siku za nyuma.
"Tuna furaha juu ya ushirikiano huo mpya na utakaowajali wateja wetu wa Zuku. Ahadi yetu ni kutoa ufumbuzi rahisi kwa wateja wetu wafanyabiashara na wauzaji na ufumbuzi huui utatuwezesha kufika mbali zaidi ya matarajio ya vwateja wetu." alisema.
Aidha Mwasyeba aliongeza kuwa wakati wakiwarahisishia unafuu wa kulipa malipo ya kila mwezi kwa wateja wao, pia kampuni yao inaendelea na promosheni yao ya kuwazawadia wateja wao iitwayo Zuku Tunakuthamini-Pata Tv Bure'.
Alisema kinachotakiwa kwa wateja kuwaunganisha wateja watano kujiunga na Zuku na kulipia malipo na kisha kujishindia runinga kati ya inchi 22 na wale watakaofikisha idadi ya wateja 10 watanyakua rungina ya inchi 42 na walioungwanishwa nao wakiambulia 'offer' nyingine zinazotolewa na kampuni yao kupitia promosheni hiyo.
Naye Meneja Uhusiano wa Selcom, Juma Tumaini Mgori, alisema kuanza kutoa huduma hiyo kwa wateja wa zuku ni fursa ya kuwapa unafuu wateja wa televisheni hiyo popote walipo nchini kutokana na kampuni yao kuwa na vituo vya malipo zaidi ya 1500.
"Tunajitahidi kufanya kazi kwa ufanisi kwa malipo ya ushirikiano wa kipekee na zuku ili kuwafikia wateja kwa ukaribu zaidi," alisema na kuongeza;
Tuna furaha kufanya kazi na Zuku na tunaamini huu ni mwanzo tu wa ushirikiano wa kibiashara," alisema.
Televisheni ya Zuku inatoa uchaguziu mpana wa stesheni za burudani ikiwa ni pamoja na habari, michezo na sinema, majarida na muziki ikiwa imejumuisha chaneli za kimataifa kama BBC, MTV Base. Sentanta Sports, MGM Movies na nyinginezo ka gharama nafuu kwa ubora na kiwango cha hali ya juu.
Mameneja wa kampuni za Wananchi Satellite Ltd, Fadhil Mwasyeba (kushoto) na Juma Tumaini Mgori wa Selcom Wireless wakibadilishana mkataba waliosaini leo ili kutoa huduma rahisi na ya haraka ya malipo kwa wateja wa Zuku Tv. Uzinduzi huo uliofanyika leo asubuhi jijini Dar es Salaam.

PICHA ZA TIMU ZA TAIFA ZA TANZANIA BARA NA ZANZIBAR ZILIZOPOWEZA KUTINGA NUSU FAINALI ZA KLOMBE LA CHALENJI NCHINI UGANDA. (zote kwa hisani wa Bongostaz

Wachezaji wa Bara wakimpongeza Bocco baada ya kufunga bao la pili katika Robo Fainali ya kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge dhidi ya Rwanda. Bocco alishangilia huku akichechemea baada ya kufunfa bao hilo kutokana na kuumia, baada ya kugongwa na kipa wa Rwanda, Jean Claude Ndoli wakati anaenda kufunga. Bara ilishinda 2-0 na kutinga Nusu Fainali. 


Kaseja amedaka, huku Yondan akiwa tayari kumsaidia


Manahidha wakisalimiana kabla ya mechi, Juma Kaseja wa Bara kulia na Haruna Niyonzima wa Rwanda kushoto


Kikosi cha Rwanda leo


Kikosi cha Bara leo


Watanzania waliokuja kuisapoti timu hapa


Shomary Kapombe akimdhibiti Dadi Birori 


Athumani Iddi 'Chuji' akiruka juu kulia kuokoa


Amri Kiemba anamkokota mchezaji wa Rwanda


Kocha Milutin Sredojevic 'Micho'


John Bocco akiwashughulisha mabeki wa Rwanda


Refa anaonyesha kati, baada ya Kiemba anayekimbia nyuma yake kufunga bao la kwanza


Bao la Kiemba


Mwinyi Kazimoto kulia akimburuza mchezaji wa Rwanda


Ulinzi mkali langoni mwa Rwanda, lakini bado mbili zilipenya


Bocco anasababisha


Jean Claude Ndoli wa Rwanda aliyeruka hewani kudaka moja ya michomo ya hatari iliyoelekezwa langoni mwake