Al Ahly ya Misri |
Bao la ugenini walilopata Al Ahly dhidi ya wenyeji wao liliisaidia kuivusha hatua hiyo baada ya matokeo ya jumla kuwa mabao 2-2, baada ya mchezo wao wa kwanza kupata ushindi wa bao 1-0.
Al Ahly waliyoiondosha Yanga kwenye raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa ya Afrika kabla ya kutolewa na Al Ahly Bengazhi na kutupwa kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Katika mechi nyingine Sewe Sport ya Ivory Coast iliifunga Bayelsa United ya Nigeria kwa bao 1-0 na kufuzu hatua ya makundi kwa jumla ya mabao 3-0 baada ya wiki iliyopita kushinda mabao 2-0.
Kinyang'anyiro cha michuano hiyo kinaendelea tena leo kwa michezo itakayozikutanisha Nkana Red Devils ya Zambia itakayokuwa ugenini dhidi ya Bizertin ya Tunisia, ambapo mechi yao ya awali iliisha kwa suluhu ya kutofungana.
Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini ambayo ilikung'utwa mabao 2-1 nyumbani na ASEC Memosa itakuwa Ivory Coast kujaribu kubadilisha matokeo dhidi ya wapinzani wao hao, nayo Coton Sport ikiwa na hazina ya ushindi wa mabao 2-1 iliyopata nyumbani dhidi ya Petro de Luanda itakuwa nchini Angola kuangalia wanatokaje ugenini.
Nazo timu za Léopards de Dolisié ya Jamhuri ya Kongo na Medeama ya Ghana zitapepetana Accra Ghana, huku wenyeji wakiwa nyuma kwa mabao 2-0, huku Etoile du Sahel ya Tunisia itakuwa nyumbani kuikaribisha Horoya ya Guinea walioshindwa kutambiana wiki iliyopita.
Mechi nyingine ya mwisho itazikutanisha timu za Real Bamako na 'ndugu' zao, Djoliba katika pambano lililozikutanisha timu za nchi moja ya Mali.
Katika mechi ya kwanza Real ilipata ushindi wa mabao 2-1 nyumbani na hivyo leo ikiwa ugenini itakuwa na kazi ya kulinda nafasi yake na kutinga hatua ya makundi ambayo kwa kawaida ina mamilioni ya fedha kutoka Shirikisho la Soka Afrika (CAF).
No comments:
Post a Comment