STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, April 27, 2014

Kocha mpya Stars aita wapya tisa yumo Javu, Maguli

Hussen Javu aliyeitwa Stars ya kuivaa Malawi
Elias 'Magoli' Maguli naye kaongezwa na kocha mpya wa Stars
kochaaaa
Kocha mpya wa Stars
 KOCHA Mkuu mpya wa Taifa Stars, Mart Nooij amewaongeza wachezaji tisa katika kikosi cha timu hiyo kinachojiandaa kwa mechi ya kirafiki na timu ya Malawi(The Flames) ambayo itakachezwa Mei 4 mwaka huu katika Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Stars iliyonyolewa mabao 3-0 jana na Burundi huku kocha huyo akishuhudia uwanjani, ambapo Rais wa TFF, Jamal Malinzi alimtambulisha na kueleza wamemsainisha mkataba wa miaka miwili kuinoa timu hiyo.
Wachezaji walioongezwa na kocha huyo ni Edward Manyama (JKT Ruvu), Elias Maguli (Ruvu Shooting), Hassan Dilunga (Yanga), Hussein Javu (Yanga), John Bocco (Azam), Kelvin Friday (Azam), Oscar Joshua (Yanga), Nadir Haroub (Yanga) na Shomari Kapombe (AC Cannes, Ufaransa).
Walioondolewa ni pamoja na beki Kelvin Yondani wa Yanga ambaye aliitwa awali na sababu za kuondolewa ni kushindwa kuripoti kambini.
Kikosi hicho cha Taifa Stars inategemewa kuingia kambini kesho Aprili 28 jijini Mbeya kujiandaa kwa mechi dhidi ya Malawi.
Wakati huo huo, Tanzania (Taifa Stars) imepangiwa kucheza na Zimbabwe katika raundi ya pili ya mechi za mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika (AFCON) zitakazofanyika mwakani nchini Morocco.
Kwa timu ya Taifa Stars itaanzia nyumbani ambapo mechi ya kwanza itachezwa kati ya Mei 16 na 18 wakati ile ya marudiano itachezwa Harare kati ya Mei 30 na Juni 1 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment