Thomas Mashali |
Karama Nyilawila |
Mwazoa ametoa ufafanuzi huo baada ya kuwepo kwa taarifa kwamba pambano hilo la kimataifa halitakuwepo kama ilivyopangwa na kwamba mashabiki wasisumbuke kwenda PTA kulishuhudia.
Akizungumza na MICHARAZO kwa njia ya simu toka jijini Tanga, Mwazoa alisema hafahamu wanaoeneza taarifa kwamba mchezo huo haupo ilihali alishalitangaza mapema na mabondia wanaendelea kujiandaa.
Hata hivyo alisema kwa namna hali ilivyo analazimika kukutana na mabondia hao wawili kuweza kuwekana sawa kabla ya kupanda ulingoni.
"Nilishatangaza mapema kwamba mabondia hao watapigana Mei Mosi, sasa taarifa kwamba pambano hilo halipo kwa kweli sijui uvumi unatokea wapi, hata hivyo nimewaita mabondia wote mjini hapa niweze kuzungumza nao," alisema Mwazoa.
Mwazoa alisema huenda wapinzani wake wanamfanyia hila pengine kwa kuona amekuwa kivutio kikubwa kwa mabondia kutokana na uhakika katika makubaliano na hata michezo anayoiandaa.
Mashali aliyemtwanga Japhet Kaseba hivi karibuni na kunyakua ubingwa wa UBO Afrika, atapambana na Nyilawila baada ya muda mrefu wa kila mmoja kumponda mwenzake kuwa hana ubavu wa kukabiliana naye kwenye ulingo.
Bondia huyo kwa sasa anauguza majeraha aliyoyapara kupoitia ajali aliyopata eneo la Kimara Suka wakati akiwa njiani kuelekea Tanga kuonana na promota huyo
Nyilawila aliwahi kuwa bingwa wa dunia wa uziato wa kati anayetambuliwa na WBF kabla ya kushindwa kwenyda kutetea taji lake hilo ili kuzipiga na Francis Cheka katika paambano la kirafiki mjini Morogoro na kudundwa.
No comments:
Post a Comment