STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, April 27, 2014

Ronaldo atuma salamu kwa Bayern Munich

Cristiano Ronaldo scores to put Real Madrid ahead against Osasuna
Ronadl alivyokuwa akiitesa Osasuna usiku wa jana
CRISTIANO Ronaldo ametuma salamu kwa mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Bayern Munich baada ya usiku wa jana kutupia kambani mabao mawili wakati Real Madrid ilipoizamisha timu ya Osasuna kwa mabao 4-0 katika Ligi Kuu ya Hispania.
Ronaldo ambaye amerejea tena dimbani toka kwenye majeraha, aliiongoza Madrid kupata ushindi huo mnono uliowasogeza karibu na mahasimu wao wa jiji la Madrid Atletico Madrid wanaongoza msimamo wa ligi hito katika uwanja wa Santiago Bernabeu.
Real Madrid keshokutwa itakuwa ugenini nchini Ujerumani kuumana na Bayern Munich katika pambano la marudiano la nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa baada ya wiki hii kupata ushindi wa bao 1-0 nyumbani, huku Ronaldo na Gareth Bale wakiwa hawapo fiti kama mechi yao ya jana dhidi ya Osasuna.
Mkali huyo alifunga bao la kwanza dakika ya sita kwa kazi nzuri ya Angel di Maria, bao lililodumu hadi kipindi cha kwanza kumalizika kabla ya kuongeza la pili katika dakika ya 52 akimalizia kazi ya Isco.
Bao la tatu lilifungwa na Sergio Ramos katika dakika ya 60 kwa kazi murua ya di Maria na Daniel Carvajal alimalizia udhia dakika saba kabla ya kumalizika kwa mchezo huo kwa kazi muru ya Isco na kuifanya Madrid kufikisha pointi 82, tatu nyuma ya Atletico inayocheza leo.
Katika mechi nyingine za ligi hiyo Elche ikiwa nyumbani ililazimishwa sare ya 1-1 na Levante siku ya Ijumaa wakati jana Granada ilipokea kipigo cha mabao 3-0 toka kwa wageni wao Rayo Vallecano, wakati Getafe ilishinda nyumbani bao 1 - 0 dhidi ya  Málaga.
Nayo timu ya Real Betis ikiwa uwanja wao wa nyumbani ilitandikwa bao 1-0 na Real Sociedad wakati leo ligi hiyo imeendelea leo kwa Espanyol ikiwa nyumbani kulazwa mabao 2-1 na Almería na baadaye   Valencia itaumana na vinara, Atletico Madrid, Athletic Club itaumana na Sevilla na Villarreal itaialika Barcelona kabla ya kesho Celta Vigo kupepetana na Real Valladolid.

No comments:

Post a Comment