UMATI
mkubwa wa watu wamekusanyika mjini Vatican kushuhudia tukio la
kihistoria ambapo viongozi wawili wa zamani wa Kanisa Katoliki, Papa
John Paul II na Papa John XXIII wametangazwa watakatifu.
Ibada
iliyoendeshwa kwa pamoja kati ya Papa Francis na mtangulizi wake Papa
Benedict XVI imeangaliwa na karibu mahujaji milioni moja na wengine
mamilioni ya watu kupitia matangazo ya televisheni na redio.
Karibu ujumbe wa wageni 100 wamehudhuria sherehe hiyo, wakiwemo kutoka koo za kifalme na wakuu wa nchi na serikali.
Hii ni mara ya kwanza kwa papa wawili kutangazwa kwa wakati mmoja kuwa watakatifu.
Waandishi
wa habari wanasema hatua hii inachukuliwa kama njia ya kuziunganisha
kambi mbili za wapenda mageuzi na wasiotaka mabadiliko ya sheria katika
Kanisa Katoliki.
Chanzo BBC Swahili
No comments:
Post a Comment