Mchezaji Idd Suleimana Tanzania akichanja mbuga mbele ya wachezaji wa Kenya U20 |
Ngorongoro imepata ushindi huo baada ya kushindwa kutambiana na vijana wenzo katika mechi iliyochezwa kwenye uwanja wa Taifa ikiwa ni siku moja tangu kaka zao kunyukwa 3-0 na Burundi katika mechi ya kimataifa ya kirafiki kuadhimisha sherehe za Muungano.
Katika mechi hiyo Tanzania ilipata penati kupitia kwa Kevin Friday, Mohammed Hussein, Mange Chagula na Iddi Suleiman, huku Mudathir Yahya alikosa yake.
Wakenya walipata penati zao kupitia Geofrey Shiveka, Timonah Wanyonyi na Victor Ndinya, huku Evans Makari na Harison Nzivo walipoteza.
Kwa kufuzu huko Tanzania sasa inatarajiwa kuvaana na Nigeria katika hatua inayofuata katika kuwania kucheza fainali hizo zitakazofanyika nchini Senegal.
No comments:
Post a Comment