STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, April 27, 2014

Chelsea yaizima Liverpool Anfield

Demba Ba akiiandikia Chelsea bao dakika ya 45 ya mchezo wao wa leo
Mimi ndiyo Only Special bwana!! Mourhino akijipiga kifua kuonyesha umahiri wake kwa kuzima Liverpool kwao kwa maba 2-0
Liverpool wakiwa hawamini kama wamelala nyumbani
 CHELSEA chini ya kocha wake, Jose Mourinho ikiwa ugenini kwenye uwanja wa Anfield imefanikiwa kuisimamisha Liverpool baada ya kuizamisha Liverpool kwa mabao 2-0 katika Ligi Kuu ya England.
Liverpool ambayo ilikuwa ikitarajiwa kujiandikishia rekodi ya kuelekea kunyakua taji la kwanza la Ligi Kuu baada ya miaka 24, ilishindwa kuamini kama imelala nyumbani kwao kwa vijana wa Mourinho.
Mabao ya 'jioni' katika kila kipindi kupitia kwa Demba Ba na Willian yalitosha kuipa ushindi huo Chelsea na kuwasogelea wapinzani wao kwenye mbio za kuelekea kwenye ubingwa wa ligi hiyo.
Demba Ba alifunga bao la uongozi dakika chache kabla ya timu kwenda mapumziko kabla ya Torres kuvunja mtego wa kuotea na kumpa pasi murua Willian aliyezamisha bao sekundu chache kabla ya mchezo huo kumalizika.
Chelsea iliyotumia muda mrefu 'kupaki basi' na kuinyima fursa Liverpool kuipenya ngome ya vijana hao wa The Blues ambap hawakutarajiwa kupata ushindi huo katika mechi yao leo.
Hii ni kwa sababu Mourinho alishatangaza mapema angekichezesha kikosi cha pili ili kuweka nguvu kwa mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa hatua ya nusu fainali dhidi ya Atletico Madrid watakaowafuiata Stanford Bridge siku ya Jumanne.
Kwa ushindi huo, Chelsea imeweza kupunguza pengo la pointi na kufikisha mbili nyuma ya wapinzani wao wanaoongoza msimamo wa ligi hiyo wakiwa na pointi 80 wakati ligi imesaliwa na raundi mbili kabla ligi haijamalizika mwezi ujao.
Dakika chache zijazo Manchester City waliopo nafasi ya pili watakuwa ugenini kuvaana na Crystal Palace katika mfululizo wa ligi hiyo wakiwa na pointi 74 kutokana na mechi 34.

No comments:

Post a Comment