KIKOSI cha Taifa Stars kinaingia
tena kambini Jumatano (Juni 11 mwaka huu) ikiwa ni sehemu ya maandalizi
ya mechi ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika dhidi ya Msumbiji
itakayochezwa Julai 20 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Stars inayodhaminiwa na
Kilimanjaro Premium Lager itakuwa na kambi ya siku tatu jijini Dar es
Salaam ikijumuisha wachezaji 28. Kwa mujibu wa programu ya Kocha Mart
Nooij, Stars itaingia tena kambini Juni 24 mwaka huu.
Wachezaji wanaotakiwa kuripoti
kambini ni Deogratias Munishi, Aishi Manula, Benedictor Tinoko, Kelvin
Yondani, Said Moradi, Nadir Haroub, Joram Nason, Shomari Kapombe, Oscar
Joshua, Edward Charles, Aggrey Morris na Pato Ngonyani.
Wengine ni Mwinyi Kazimoto,
Frank Domayo, Amri Kiemba, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Said Juma, Haruna
Chanongo, Himid Mao, Said Ndemla, John Bocco, Simon Msuva, Kelvin
Friday, Ramadhan Singano, Khamis Mcha, Mrisho Ngasa na Mwegane Yeya
No comments:
Post a Comment