STRIKA

USILIKOSE

Friday, August 3, 2012
Mobby Mpambala ala shavu Pilipili
MKALI wa filamu za mapigano nchini, Mobby Mpambala amelamba dume katika kampuni ya
Pilipili Entertainment baada ya kupewa shavu la kutengeneza filamu mpya iitwayo 'The Same Plan'.
Akizungumza na MICHARAZO, Mpambala aliyedai sehemu kubwa ya mafanikio yake kimaisha na kisanii yamechangiwa na mkewe, Jasmine, alisema kampuni ya Pilipili imempa nafasi hiyo baada ya kukutana nao katikati ya wiki iliyopita ili kufanya nao kazi.
Mpambala, alisema katika mzungumzo yao na kampuni hiyo waliafikiana kufyatua kazi ya
utambulisho na kudai tayari yu mbioni kuandaa filamu iitwayo 'The Same Plan', aliyodai itawashirikisha wakali kadhaa wa fani hiyo nchini ambao hata hivyo hakuweza kuwataja majina.
"Namshukuru Mungu, neema zinazidi kunifungukia baada ya Pilipili Entertaiment kunipa shavu la kufanya nao kazi na natarajia kutoa filamu ya kwanza iitwayo 'The Same Plan'," alisema.
Aliongeza tenda hiyo mpya imekuja wakati akijiandaa kutoa kazi mbili kwa mpigo zilizokamilika kupitia kampuni yake ya Wazagi za 'Fuvu' na Anti Virus'.
Mpambala, alisema hawezi kujivunia mafanikio yote aliyonayo bila kumshukuru mkewe Jasmine, ambaye alitoka nae mbali kabla hata hajapata umaarufu kama alionao, licha ya kukiri alishakuwa na mwanamke mwingine aliyezaa nae watoto watatu na kuachana nae na pia kuoa mke mpya, Zolla.
"Hakuna siri siri ya mafanikio yangu ukiondoa baraka za Mungu na za wazazi, pia mke wangu ni sehemu ya haya yote, ndio maana nimefika hapa hata kupata tenda kama ya Pilipili," alisema.
Mwisho
Klabu ya Azam yafafanua sakata la Ngassa
TAARIFA hii imetolewa na Meneja wa klabu ya Azam, Patrick Kahemela
Klabu ya Azam FC inapenda kutoa taarifa ya ufafanuzi juu ya sakata la mchezaji Mrisho Ngasa ambalo linaonekana kupotoshwa
1. Azam FC ilitangaza kuwa biashara ya mchezaji Mrisho Ngasa ingefungwa siku ya Jumatano 1/08/2012 saa saba mchana na ilivitaka vilabu vyenye interest na mchezaji huyo kufika makao makuu ya Azam FC ofisi ndogo zilizopo kwenye kiwanda cha unga cha Azam-Mzizima zikiwa na pesa taslimu. Bei ya mauzo iliyopangwa ilikuwa ni Dola 50,000. Lakini katika mawasiliano ya email kwa makatibu wakuu wa Simba na Yanga, Azam FC iliweka bayana kuwa ilikuwa tayari kushusha bei ya mauzo na ingemuuza Ngasa kwa timu ambayo dau lake lingekuwa kubwa zaidi ya mwenzake.
Kwa maana hiyo biashara ya mchezaji mrisho ngasa ilifanyika kwa uwazi. Lengo la Azam FC lilikuwa ni kutoa haki kwa kila klabu yenye uwezo wa kifedha kuweza kupata huduma ya Ngasa.
Pia tunaomba ifahamike bayana kuwa mchezaji Mrisho Ngasa alipewa taarifa kuwa anauzwa na aliombwa asaidie kushawishi klabu anayoitaka ifike kwetu na ofa yake. Ngasa alitamka bayana kuwa yupo tayari kwenda klabu yoyote ambayo Azam FC itaona imekidhi mahitaji yake kwa masharti kuwa maslahi yake ya kimkataba kati yake na Azam FC yazingatiwe.
2. Hadi kufikia siku ya Jumatano 01/08/2012 saa saba mchana. Ni klabu ya Simba pekee iliyojibu kwa maandishi na kuonesha nia ya kumchukua Ngasa. Yanga wao hawakuwahi kujibu email, ingawa kwa majibu ya simu Mjumbe wao wa Kamati ya usajili Bw Sefu Magari alitangaza kuwa Ngasa hana thamani ya zaidi ya milioni 20. Na Yanga haikuwa tayari kuboresha ofa yake.
3. Muda wa kufungwa kwa biashara ya kumuuza Ngasa ulipofika, ni simba pekee kupitia kwa makamu Mwenyekiti wake Bw Geofrey Ngange na Mhasibu wake ndiyo waliofika wakiwa na pesa taslimu shilingi milioni 25. Yanga hawakuonekana na hawakutaka kupokea hata simu walizokuwa wakipigiwa kuulizwa kama wana interest.
4. Kikao cha dharura cha Azam FC kilikaa na kuamua kuwa biashara ya kumuuza Ngasa ilishindikana kutokana na kutokupatikana kwa mnunuzi mwenye dola 50,000. Kwa maana hiyo Azam FC iliamua kumpeleka Ngasa kwa mkopo kwenye klabu iliyofika na kuonesha nia ya kumhitaji (Simba)
5. Simba walipewa sharti la kuhakikisha wanamlipa Ngasa mshahara wake kamili (TZsh 2,000,000) pamoja na stahiki zake nyingine zote za kimkataba
6. Sababu za kumpeleka Ngasa kwa mkopo ni kumuepusha na adhabu ambayo klabu ya Azam FC ingetoa kwa Ngasa kama angebaki.
7. Azam FC inapenda kuweka wazi kuwa haijamlazimisha Ngasa kwenda Simba kama inavyopotoshwa. Kama Ngasa anataka kuvunja mkataba wake au kama Yanga bado wanamhitaji basi waje na dola 50,000 na Azam FC itawauzia kwani licha ya kwamba amepelekwa kwa mkopo simba lakini Ngasa bado ni mali ya Azam FC
8. Tunaomba kuweka msimamo wetu kuwa hatupo tayari kumlipa Ngasa na kuvunja mkataba wake na hatuna sababu ya kufanya hivyo. Kama Ngasa hataki kwenda tunakompeleka Azam FC inamruhusu kubakia klabuni na kutumikia adhabu.
9. Lakini Ngasa na washauri wake waelewe kuwa akiamua kubaki Azam FC atakaa nje ya uwanja kwa muda wote uliosalia kwenye mkataba wake, kwani Azam FC haipotayari kumvisha jezi mchezaji anayefanya vitendo vya utovu wa nidhamu.
10. Kwa kuwa Sakata hili limeanza kuhusishwa na sakata la Mchezaji ramadhani Chombo. Naomba nitoe ufafanuzi kama ifuatavyo. Redondo alipewa option tatu za kuchagua baada ya kufanya vitendo vya utovu wa nidhamu timu ilipokuwa safarini Mwanza.
a. Kupelekwa kwa mkopo Moro United?
b. Kupatikana kwa mnunuzi mwenye shilingi milioni 40
c. Kukubali adhabu ya kufungiwa kwa miezi mitatu na kulipwa nusu mshahara wahati akitumikia adhabu.
Redondo alithibitisha kuipenda Azam FC kwa kukataa kuuzwa au kupelekwa kwa mkopo. Alikubali kutumikia adhabu yake na ilipoisha alirudi na kuomba msamaha na sasa ni mmoja kati ya wachezaji wenye nidhamu ya hali ya juu sana. Azam FC inajivunia kuwa na mchezaji kama Redondo na bila kupepesa macho wala kung’ata maneno. Azam FC inamchukulia Redondo kama mtu spesho na mwenye mapenzi ya dhati na klabu yake na inamtaka aendelee kuwa na moyo huo.
Thursday, August 2, 2012
Baada ya kuiapa Yanga taji la Kagame, Saintfiet 'aibukia' Harambee Stars
MAKOCHA wa timu mbalimbali barani Afrika na waliowahi kufundisha soka barani humu, wametuma maombi ya kupata kazi ya kuifundisha timu ya taifa ya Kenya - Harambee Stars.
Kwa mujibu wa kituo cha Supersport, ukiachana na makocha Otto Pfister, Adel Amrouche, Giuseppe Dossena, Ratomir Dujovic, Goran Stevanovic na Milovan Rojavic, kocha mkuu wa klabu ya Yanga kutoka Ubelgiji Tom Saintfeit nae ametuma maombi ya kutaka kuinoa Harambee Stars.
Tom Saintfiet ambaye bado hajatimiza hata mwezi mmoja tangu aje kujiunga na Yanga anapambana kocha wa zamani Ghana ambaye aliongoza Black Stars katika michuano ya African Cup of Nations 2012 na akatimuliwa baada ya timu kuondolewa kwenye michuano hatua ya nusu fainali.
Japokuwa makocha ni wengi waliotuma maombi lakini Otto Pfitster anaonekana kuwa na nafasi kubwa kutokana na CV yake, akiwa tayari ameshazifundisha timu za Burkina Faso, DR Congo, Cameroon na Ghana. Pia tayari ameshachukua kombe la dunia la vijana chini ya miaka 17 na kikosi cha Ghana.
Siku ya leo ndio shirikisho la soka la Kenya (FKF) kupitia kamati kuu watawatangaza makocha waliongia kwenye kinyang'anyiro cha mwisho katika kueleka kumteua kocha mkuu wa Harambee Stars.
CHANZO:SHAFII DAUDA BLOGSPOT
Kocha wa Atletico ya Burundi kumrithi Stewart Azam?
KUSITISHWA mkataba kwa kocha wa Azam FC Stewart Hall kunamuweka kocha wa Atletico ya Burundi
katika nafasi nzuri ya kuifundisha timu hiyo.
Baadhi ya vyombo vya habari nchini vimemkariri Stewart akikiri kusitishiwa mkataba wake huku akiweka bayana anafurahia kutimiza malengo makuu matatu katika klabu hiyo ikiwemo ujenzi wa Complex ya Chamazi, kuinua soka la vijana na kuiweka Azam katika chati ya juu katika soka la Tanzania.
Uongozi wa Azam nao umekiri kuachana na kocha huyo ukidai kuwa walipofikishwa na kocha huyo kunahitaji mtu mwingine wa kuwaendeleza na kuzipuuza taarifa kwamba walimtimua Stewart kwa sababu ya kumpanga Ngassa katika mechi yao na Yanga kinyume na agizo lao.
Hata hivyo uomgozi huo umesema kuwa wakati wakiendelea kumsaka kocha mpya timu itakuwa chini ya kocha wa vijana , Vivek Nagul na Kally Ongalla, ingawa taarifa ambazo bado hazijadhibitishwa ni kwamba Azam inamneyemelea kocha wa Atletico, Kaze Cedri aliyeufutia uongozi huo.
Habari zilidai kuwa viongozi wa Azam walionyeshwa kuvutiwa na kocha huyo baada ya timu yake kuonyesha kandanda la kuvutia kwenye michuano hiyo.
Ni siku ambayo ilicheza kandanda la kuvutia kwenye michuano ya Kagame Cup na kuichapa Yanga mabao 2-0, kabla ya kuoka sare na APR huku pia ikisakata kabumbu la uhakika.
Aidha inaelezwa kuwa kutua kwa Cedri Azam itaisaidia klabu hiyo kupunguza gharama kubwa walizokuwa wakimlipa kocha huyo Muingereza ambaye aliwahi kuinoa timu ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes kabla ya kunyakuliwa na Azam.
Habari za ndani katika klabu hiyo zinasema kuwa Stewart alikuwa akipokea 'mkwanja' mnene kuliko hata unaodaiwa kulipwa kocha wa timu ya taifa, Taifa Stars na kutokea sakata la Ngassa limekuwa nafuu kwa uongozi huo kumpa mkono wa kwaheri.
Juhudi zinafanywa na MICHARAZO kupata uthibitisho wa Cedri kutakiwa Azam na tukifanikiwa mtazipata kupitia hapa hapa.
Mwanahawa Chipolopolo atua T Moto
ALIYEKUWA muimbaji nyota wa kundi la King's Modern Taarab 'Wana Kijoka Kazima Taa', Mwanahawa Ally 'Chipolopolo' amelihama kundi hilo na kutua T-Moto Modern Taarab.
Akizungumza na MICHARAZO
, Chipolopolo alisema ametua T-Moto wiki iliyopita baada ya kuvutiwa na masilahi aliyoahidiwa na kundi hilo na kwa sasa anajifua nao kwa ajili ya maonyesho ya sikukuu ya Eid el Fitri ambapo ndipo atakapotambulishwa rasmi.
Chipolopolo, alisema ameondoka King's kundi lililomtangaza vema kwa baraka zote bila ya ugomvi wala chuki kwa lengo la kusaka ujuzi na kusaka masilahi.
"Yaani ni wiki tu iliyopita ndio nimetua hapa T-Moto nikitokea King's kwa nia ya kuongeza ujuzi na kutafuta masilahi zaidi, ila sijaondoka katika kundi langu la awali kwa chuki au ugonvi," alisema.
Muimbaji huyo ambaye ni mtoto wa mpuliza saksafone wa zamani wa bendi za Urafiki Jazz, Bima Lee, Shikamoo Jazz na Msondo Ngoma, Ally Rashid 'Mwana Zanzibar' alisema anaamini kuwepo kwake T-Moto kutamsaidia kumpaisha zaidi kutokana na aina ya wasanii atakaokuwa nao.
Alisema pamoja na kuondoka, King's, lakini hatalisahau kundi hilo kwa kusaidia kumnyanyua baada ya kusota katika makundi ya awali aliyoyapitia katika safari yake kimuziki.
"Nimeondoka King's lakini silisahau asilan kwa namna lilivyonisaidia kufika hapa nilipo hata T-Moto wakakiona kipaji changu," alisema.
Mwisho
Kim Poulsen awaita Bahanunzi, Chuji kikosi cha Stars
MFUMANIA nyavu aliyefunika kwenye michauno ya Kombe la Kagame, Said Bahanunzi wa Yanga na viungo 'watukutu' Athuman Idd Chuji na Ramadhani Chombo 'Redondo' ni kati ya wachezaji 21 waliotangazwa kuitwa katika kikosi cha timu ya taifa Taifa Stars.
Kocha mkuu wa timu hiyo Kim Poulsen amekitangaza kikosi hicho jana kwa ajili ya kujiandaa na pambano la kirafiki la kimataifa linalotarajiwa kuchezwa katikati ya mwezi huu nje ya nchi.
Poulsen alisema kikosi hicho kinatarajiwa kuingia kambini wiki ijayo tayari kujiwinda na mechi hiyo ya kirafiki ambayo hata hivyo mpaka sasa haifahamiki itakuwa dhidi ya nchi gani.
Kocha huyo alisema amewaita wachezaji hao watatu na wengine kutokana na kuonyesha uwezo mzuri wakati wa michuano ya Kagame, ambapo bahanunzi aliibuka mfungaji bora huku Chuji na Redondo waking'ara katika nafasi ya kiungo mwanzo mwisho.
Kim alisema ameomba mechi hiyo ya kirafiki ambayo iko kwenye kalenda ya FIFA ichezwe ugenini kwa lengo la kuwapa uzoefu wachezaji wake.
Wachezaji waliotajwa na kocha huyo ni pamoja na makipa watatu, Nahodha Juma Kaseja (Simba), Deogratias Munishi 'Dida'na Mwadini Ally (wote Azam).
Mabeki ni nahodha msaidizi, Aggrey Morris na Erasto Nyoni (Azam), Kelvin Yondani (Yanga) na Shomari Kapombe (Simba).
Viungo walioteuliwa katika timu hiyo ni Chuji na Frank Domayo (Yanga), Haruna Moshi 'Boban', Ramadhani Singano 'Messi' na Mwinyi Kazimito (Simba), Mrisho Ngassa,Redondo na Salum Abubakar 'Sure Boy' (Azam) na Shabani Nditi kutoka Mtibwa Sugar.
Wengine ni washambuliaji John Bocco (Azam), Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu(TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo), Bahanunzi na Simon Msuva.
Kocha huyo alisema ameshindwa kuwaita Amri Maftah wa Simba na Nurdin Bakari wa Yanga kwa sasa kutokana na kwamba wachezaji hao bado ni majeruhi.
Simba wamalizana na Azam kuhusu Ngassa, mwenyewe adai haendi kokote kwa vile hajashirikishwa
MABINGWA wa soka wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Simba wametangaza kumsajili mshambuliaji nyota wa Azam na timu ya Taifa (Taifa Stars), Mrisho Ngassa kwa mkataba wa mkopo wa mwaka mmoja.
Hata hivyo Ngassa mwenyewe amesisitiza kuwa hajashirikishwa katika 'dili' hilo na kudai kama uongozi wa Azam haumtaki katika klabu yao imvunjie mkataba na kumlipa chake kuliko kumpeleka kwenye klabu ambayo hajawahi kuitoa kuichezea.
Uongozi wa Simba na Azam jana ulinukuliwa kwamba umefanikisha mpango wa Ngassa kutua Msimbazi baada ya kuwazidi kete Yanga waliokuwa tayari kulipa Sh Milioni 20, milioni tano pungufu na zile walizotoa Simba.
Awali, uongozi wa Azam ulishatangaza kuwa uko tayari kumuuza winga huyo kwa klabu yoyote itakayotoa dau la dola 50,000 (sawa na zaidi ya Sh. milioni 80), jambo ambalo limeonekana kuwa gumu kabla ya Simba kumpata mchezaji huyo kwa ofa ya mkopo ya Sh. milioni 25.
Ngassa ambaye alitakiwa sana na kocha wa Simba, Milovan Circkovic, anatarajiwa kuichangamsha safu ya ushambuliaji ya timu yake mpya katika ligi kuu ya Bara na pia katika michuano itakayoanza mapema mwakani ya Ligi ya Klabu Bingwa Afrika.
Akizungumza jana jijini Dar, Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geofrey Nyange 'Kaburu' alisema kuwa wamemsajili Ngassa kwa mkopo na tayari wamefikia makubaliano na Azam, hivyo mchezaji huyo ataichezea timu yao katika msimu ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara ambayo inatarajiwa kuanza Septemba Mosi.
Kaburu alisema kuwa wamemsajili mshambuliaji huyo kutokana na maelezo ambayo walipewa na Cirkovic ili kuziba nafasi ya Emmanuel Okwi ambaye sasa anaelekeza nguvu zake katika kusaka timu atakayoichezea soka la kulipwa barani Ulaya.
"Usajili wa Ngassa umeshakamilika, ni mali yetu kwa muda wa mwaka mmoja baada ya kukamilisha usajili wake wa kuichezea Simba kwa mkopo," alisema Kaburu.
Naye Meneja wa Azam, Patrick Kahemele, alinukuliwa akisema wameamua kumpeleka Ngassa Simba kutokana na maelezo ya Cirkovic kumuhitaji ambapo wanaamini ataendeleza kipaji chake na kuendelea kuisaidia Taifa Stars.
Kahemele alisema kuwa Azam ilifikia maamuzi ya kumuuza mshambuliaji huyo baada ya kuonyesha hadharani mapenzi aliyonayo na mabingwa wa Kombe la Kagame, Yanga, lakini alidai Yanga imekwama kumpata kwa vile iligoma kuongeza dau katika fedha ilizotaka kutoa.
Azam ilitangaza kwamba iko tayari kumuuza Ngassa kwa gharama ya Dola za Marekani 50,000 baada ya nyoya huyo kuonyesha mapenzi yake kwa Yanga kwa kuvaa na kuibusu nembo ya klabu hiyo wakati akishangilia goli aliloifungia Azam katika mechi yao ya nusu fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati dhidi ya AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Ngassa aliyeihama Yanga mwaka juzi aliisaidia Azam kumaliza kwenye nafasi ya pili katika msimu wa ligi uliopita ambapo mwakani itashiriki kwa mara ya kwanza mashindano ya Kombe la Shirikisho yanayoandaliwa na Shirikisho la Soka la Afrika (CAF).
Akizungumza na MICHARAZO, Ngassa alisema hana taarifa za kupelekwa Simba na kudai kwa tararibu anazopfahamu alipaswa kushirikishwa katika mazungumzo ya klabu hizo mbili kabla ya kufikiwa maamuzi.
"Kama ni kweli wamefanya hivyo hawajanitendea haki, nilipaswa kushirikishwa na kama klabu ya Azma hainitaki basi inilipe changu nijue wapi pa kwenda na sio kunipeleka sehemu kama mzigo usio na maamuzi," alisema Ngassa mtoto wa kiungo wa zamani wa Pamba na Simba, Khalfan Ngassa.
Ngassa alisema yeye anauheshimu mkataba wake na Azam ambao umesaliwa muda wa mwaka mmoja, lakini ni vigumu kwake kukubali kirahisi kupelekwa Simba, ingawa hakuweka bayana atachukua hatua gani katika sakata hilo ambalo kwa kiasi fulani linataka kufanana na lile la wachezaji Mohammed Banka aliyekuwa Simba na Ramadhani Chombo wa 'Redondo' wa Azam ambao walitolewa kwa mkopo na klabu zao kwa klabu za Villa Squad na Moro United lakini wakagoma kwa vile hawakushirikishwa katika uhamisho huo.
Wednesday, August 1, 2012
Bondia Mbongo kuwania taji la IBF Afrika
BONDIA Ramadhani Shauri wa Tanzania anatarajiwa kupanda ulingoni siku ya Idd Pili kuzipiga na Mganda Sunday Kizito katika pambano la kimnataifa la kuwania ubingwa wa IBF-Afrika.
Pambano hilo limepangwa klufanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee na litaratibiwa na Promota Lucas Rutainurwa.
Rais wa Shirikisho la Ngumi za Kulipwa nchini, TPBC ambaye pia ni Rais wa IBF Afrika/USBA, Onesmo Ngowi, aliiambia NIPASHE jana kuwa maandalizi ya pambano hilo yameanza na litasindikizwa na michezo kadhaa ya utangulizi.
Ngowi, alisema pambano hilo la Shauri na Kizito litakuwa ni la uzito wa Feather (kilo 58) kuwataja mabondia hao wana rekodi zinasisimua hivyo kutabiri pambano la aina yake siku husika.
Rais huyo alisema Shauri anayetoka kambi ya kocha Christopher Mzazi ana rekodi ya mapambano 12 akishinda 11 na kupoteza moja, huku mpinzani wake akiwa na rkodi ya kucheza pia michezo12 akishinda saba ba kupoteza 9.
Ngowi alisema siku ya pambano hilo Mtanzania mwingine Nassib Ramadhan atavaana na Mkenya, Twalibu Mubiru kuwania ubingwa wa IBF Afrika Mashariki na Kati.
Naye promota wa pambano hilo lililopewa jina la 'The Rumble of the City' alisema ameamua kuwekeza katika Utalii wa Michezo ili kusaidia ajira kwa vijana sambamba na kukuza uchumi wa Tanzania.
Rutainurwa alisema kuwa ana ratiba ya mapambano ya ubingwa wa Afrika kila baada ya miezi miwili mwaka huu na mwaka kesho ambayo itaipa Tanzania nafasi ya kunyanyua mataji na kuwawezesha vijana kujiajiri.
Promota huyo aliyaomba makampuni na wadhamini mbalimbali kujitokeza kufanikisha michezo hiyo inayosimamiwa na kampuni yake ya Kitwe General Traders.
Mwisho
Ngassa adaiwa kumfukisha kazi Azam kocha Stewart Hall
WINGA nyota wa timu ya Azam, Mrisho Ngassa anatajwa kuwa ndiye chanzo cha 'kutimuliwa' kwa aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Stewart John Hall.
Azam imedaiwa kumsitishia mkataba kocha huyo kutoka Uingereza ikiwa ni siku chache tu tangu aiwezeshe timu hiyo kucheza fainali za Kombe la Kagame, michuano iliyoishiriki kwa mara ya kwanza katika historia yao.
Hata hivyo uongozi wa Azam umekuwa wagumu kuweka bayana ukweli juu ya taarifa hizo za kumtimua Stewart na sababu zilizowafanya waachane nae kutokana na baadhi ya viongozi wake kutupiana mpira kila walipokuwa wakitafutwa kuthibitisha ukweli.
Afisa Habari wa klabu hiyo, Jafer Idd alisema asingeweza kusema lolote na kulitaka MICHARAZO iliwasiliane na Katibu Mkuu, Idrisa Nassor 'Father' ambaye naye alikwepa kijanja kuthibitisha suala hilo akidai angelitumia namba la mtu wa kulizungumzia hilo.
"Aisee juu ya ukweli au la, ngoja nikutumie namba ya mtu ambaye atakuambia kila kitu," Nassor aliiahidi MICHARAZOP licha ya kutotekeleza ahadi hiyo.
Hata hivyo habari zilizopatikana jana jijini zinasema kuwa, Stewart ni kweli ametemwa na Azam na sababu kuu ikiwa ni kitendo chake cha kukaidi agizo la uongozi huo juu ya kumtomchezesha winga Mrisho Ngassa.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari ni kwamba uongozi wa Azam ulimtaka kocha huyo asijaribu kumuingiza uwanjani Ngassa katika mechi yao ya fainali dhidi ya Yanga kwa kukerwa na kitendo cha winga huyo kuibusu jezi ya Yanga mara baada ya pambano la nusu fainali dhidi ya As Vita ya Kongo.
Inadaiwa, uongozi ulihisi winga huyo asingeitendea haki Azam kwa mapenzi makubwa aliyonayo kwa klabu yake ya zamani ya Yanga ambayo imetajwa kuchuana na Simba ili kumrejesha kikosini kwa msimu ujao.
UNAMKUMBUKA MWANA ZANZIBAR?
MPULIZA Saksafone wa zamani wa bendi ya Msondo Ngoma, Ally Rashid 'Mwana Zanzibar' yu hoi nyumbani kwake Keko Machungwa jijini Dar
kutokana na kupatwa na maradhi ya Kiharusi. Mmoja wa watoto wake, Mwanahawa Ally 'Chipolopolo' alisema baba yake alipatwa na maradhi hayo wakati akienda katika mazoezi ya bendi hiyo na kwa sasa hawezi kuzungumza wala kutembea.
Kinachomliza Mwanahawa ni kitendo cha baba yake kutelekezwa na uongozi wa bendi hiyo.
MICHARAZO ilijaribu uusaka uongozi wa bendi hiyo, lakini baadhi ya viongozi simu zao zilikuwa hazipatikani na nyingine zikilia bila kupokelewa bila kufahamika sababu yake.
Kocha Michelsen aita 22 Copa Coca Cola
Kocha wa timu za Taifa za vijana za Tanzania, Jakob Michelsen ameita wachezaji 22 kwa ajili ya michuano ya kimataifa ya Coca-Cola itakayofanyika baadaye mwaka huu nchini Afrika Kusini.
Baadaye watachujwa na kubaki 16 ambao ndiyo watakaokwenda kwenye michuano ya Afrika Kusini. Wachezaji waliochaguliwa wametokana na michuano ya Copa Coca-Cola iliyofanyika jijini Dar es Salaam na mkoani Pwani kuanzia Juni 24- Julai 2 mwaka huu.
Wachezaji walioitwa ni Abdulrahman Mandawanga (Dodoma), Abraham Mohamed (Mjini Magharibi), Ayoub Alfan (Dodoma), Bakari Masoud (Tanga), Daniel Justin (Dodoma), Denis Dionis (Ilala), Edward Songo (Ruvuma), Fikiri Bakari (Tanga), Hassan Kabunda (Temeke), Joseph Chidyalo (Dodoma), Mutalemwa Katunzi (Morogoro) na Mwarami Maundu (Lindi).
Wengine ni Nankoveka Mohamed (Ilala), Nelson Peter (Morogoro), Omari Saleh (Singida), Rajab Rajab (Mwanza), Said Said (Kagera), Shiza Kichuya (Morogoro), Shukuru Msuvi (Temeke), Tanganyika Suleiman (Kigoma), Tumaini Baraka (Kilimanjaro) na William John (Ruvuma).
Pia Michelsen ameongeza wachezaji saba kwenye kikosi cha Serengeti Boys ambacho Septemba mwaka huu kitacheza na Kenya kuwania tiketi ya fainali za vijana wenye umri chini ya miaka 17 za Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Morocco.
Wachezaji walioongezwa kwenye kikosi hicho ambao pia wametoka kwenye Copa Coca-Cola ni Abdallah Baker (Mjini Magharibi), Abdallah Kheri (Mjini Magharibi), Calvin Manyika (Rukwa), Dickson Ambunda (Mwanza), Hassan Mganga (Morogoro), Miza Abdallah (Kinondoni) na Mzamiru Said (Morogoro).
TFF yaridhia Ligi Kuu Tanzania kuendeshwa na kampuni
KWA mara ya kwanza Ligi Kuu Bara itaandika historia msimu ujao, ambapo sasa itasimamiwa na kuendeshwa na kampuni, 'Tanzania Premium League' (TPL). Hatua ya kupitisha mabadiliko hayo, ilifikiwa katika kikao cha siku mbili cha Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Akizungumza jana, mwenyekiti wa kamati ya kuendesha mchakato wa kampuni, Wallace Karia alisema TFF imepitisha kampuni kuwa chombo huru cha kuendesha ligi hiyo itakayoanza rasmi Septemba Mosi mwaka huu.
"Tulichokuwa tunatofautiana na TFF juu ya ligi kuendeshwa na chombo huru, lakini sasa kamati ya utendaji imetoa baraka," alisema Karia."Kuna mambo madogo ya kufanyiwa mabadiliko, hata hivyo hali hiyo siyo kikwazo cha ligi kusimamiwa na chombo huru," aliongeza Kiria.
Karia alisema baadhi ya maeneo ya kufanyiwa marekebisho ni suala la muundo wa kisheria wa uendeshaji ligi na kasoro ndogo walizozibaini awali.
Kimuundo kutakuwa na Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa TPL, kiongozi wa juu wa klabu iliyoshinda Ligi Kuu msimu uliotangulia.
Pia kutakuwa na Makamu Wenyeviti wa Bodi watatu, ambao ni viongozi wa juu wa timu mbili zilizoshika nafasi ya pili na tatu na Makamu wa pili wa Rais wa TFF anayewakilisha klabu.
"Pia bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya Ligi Kuu inahusisha wenyeviti au wakurugenzi au kiongozi wa juu wa klabu zote 14 (16) zinazocheza Ligi Kuu, ambapo kila klabu itatoa mjumbe mmoja na TFF pia itakuwa na hisa kwenye kampuni.
Wajumbe wengine wa bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya ligi ambao hawatapiga kura ni mjumbe mmoja kutoka Chama cha Wanasoka wa Kulipwa, Chama cha Waamuzi (FRAT), Chama cha Makocha (TAFCA0 na Wadhamini wa Ligi Kuu.
"Kutakuwa na kamati huru ya nidhamu na rufaa ambayo itateuliwa na Bodi ya wakurugenzi ya TPL kila mwaka. Maamuzi ya kamati hii yatapaswa kutekelezwa na klabu zote zinazoshiriki Ligi Kuu lakini yanaweza kupigwa kwenye Kamati ya Nidhamu na Rufaa ya TFF," aliongeza Kiria.
Uhusiano kati ya TPL na TFF utaruhusu Makamu wa pili wa Rais TFF kuwa makamu wenyeviti wa bodi ya wakurugenzi wa TPL.
Aidha, uchaguzi wa makamu wa rais wa TFF utafanywa na Bodi ya Wakurugenzi wa TPL au UTAFOC na kiongozi huyo atapaswa kuwa ama kiongozi wa juu wa klabu ya Ligi Kuu au Ligi Daraja la Kwanza au mmoja wa wanahisa wa Klabu inayoshiriki Ligi Kuu au Daraja la Kwanza.
Kuhusiana na mapato ya milango ambayo kwa sasa TFF inachukua asilimia 10, TPL itapaswa kutoa asilimia ya hisa za TFF kutoka pato lake na klabu zitapaswa kutoa asilimia tano (5%) pato la milangoni.
Kuhusu kumiliki hisa za kampuni, klabu zote zinazocheza Ligi Kuu zitakuwa na hisa sawa kwenye kampuni, ambazo zitapatikana kutokana na klabu kuwa mwananchama, na iwapo iwapo itashuka daraja, hisa zake zitahamia kwa klabu iliyopanda daraja.
Wakati huohuo, klabu zote 14 zinazoshiriki Ligi Kuu zinatarajia kufanya kikao leo kwenye ukumbi wa JB Delmont, ambapo moja ya ajenda ni kujadili kwa kina suala la kampuni hiyo.Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Yanga, Mwesigwa Celestine alikiri kuwapo kwa mkutano huo leo.
Msemaji wa Shirikisho la soka nchini, TFF, Boniface Wambura hakukataa wala kukubali taarifa hizo zaidi ya kusema wakati kikao cha Kamati ya Utendaji kinakutana, yeye hakuwepo ofisini.
Source: Mwananchi
Monday, July 30, 2012
More 120,000 US Dollars from UAE Embassy for iftar and Zakatul fitr in Tanzania
The Embassy of the United Arab Emirates(UAE)in the country through Sheikh Khalifa bin Zayed Al Hahyan, Sharjah Charity Internation and Red Cresent organizations will use more $120,000 to provide Itfal and Zakatul Fitr to seven regions of the country during this holly months of Ramadan.
Speaking in Dar es Salaam on behalf of UEA ambassador in the country H.E Ambassador Mallalla Mubarak Al Ameir and his second secretary, Mohammed Obaid Salem AlZaabi,the embassy accountant Abdallah Ahmedina said the money will benefit seven regions of the country, he named the regions as Dar es Salaam, Iringa, Kilimanjaro, Arusha, Pwani, Dodoma and Morogoro .
Ahmedina was speaking this when he donated Iftal at Al Makbool Mosque in Msasani, Dar es Salaam.
He explained that his embassy gave the money to the mentioned regions and that the remaining money will be given to, widows, orphans , disabled and other less privileged people during Zakatul Fitr cerebrations.
Ahmedina said this is not the first time for his embassy to provide Iftal and Zakatul Fitr and promised that his embassy is committed to continue providing Iftal and Zakatul Fitr to all Muslims in the country during the period of Ramadan .
"Its our tradition to give people Iftal and also zakatufitr,and this year we will use $122,000 for that purpose , this money has come from organizations which are Sheikh Khalifa ($80,000), Red Cresent ($36,000)and Sharjah Charity (6,000),"he said
On his speech , Al Makbool mosque clergy, Sheikh Mussa Abdallah,thanked the embassy for the donation which he said will help fasting Muslims during this holly months of Ramadan.
"There are some muslims who are fasting but do not have food for iftal , we thanked the Embassy of United Arab Emirates (UAE)and the other three organizations for the donation which we strong believe will help many Muslims” he said
UAE's Embassy gave iftar to Moslims in Dar
Al Rahman Mosque Sheikh, Abdullah Salim Bahssany has asked companies , organizations and individuals to provide free Iftal to Muslims during fast breaking time in this months of Ramadan.
The sheikh said there are some Muslims who are lacking iftal and its good to help them with food, he was speaking this on Saturday in Dar es Salaam when the Embassy of the United Arab Emirate (UEA)in the country through Khalifa Bin Zaayid Al Nahyaan group gave iftal to Muslims during fast breaking at his mosque.
The embassy and the group will provide the food to members of Al Rahman Mosque and other surrounding areas the whole months of Ramadan.
He thanked the Embassy and the group for the iftal and he asked other people to emulate the gesture shown by the embassy and the group .
“Am asking all Muslims in Kinondoni District who are observing the holly months of Ramadan but are not sure of getting the iftal to come here for the food and also prayers , we are very happy and thank the Embassy of United Arab Emirates(UAE) is giving us the iftal, am asking others to emirate this welcome gesture” he said
Some members of the mosque thanked the embassy for the iftal saying it will ease some of the problems which they face to get the iftal at selling points.
“This is good as it helps us to get the iftal within the mosque premises , buying this at some selling points is very tiresome as there are queues and also some people may lack money to buy Iftal ” said one member of the church who identified himself as Mustafa Ali .
Kipemba sasa vitani na Waanchari, Warenchoka
MUIGIZAJ
MUIGIZAJI mkongwe nchini, Issa Kipemba anajipanga kufyatua filamu mpya inaozungumzia uhasama wa makabila mawili makuu ya mkoani Mara ya Warenchoka na Waanchari.
Nyota huyo wiki iliyopita alikuwa mkoani humo kuonana na 'machifu' wa koo hizo ili kujua chanzo vita vyao na pia kupata baraka za kuicheza filamu hiyo.
Akizungumza na NIPASHE juzi siku moja baada ya kurejea toka safarini, Kipemba aliyewahi kutamba na Kaole Sanaa, alisema safari yake ilikuwa na mafanikio tofauti na alivyofikiri.
Kipemba alisema amejifunza mengi katika safari yake hiyo na kwa sasa anajipanga ili kufyatua filamu hiyo itakayokuja baada ya kazi yake ya 'Injinia' kuingiza sokoni.
Alisema hajajua filamu hiyo itawashirikisha wasanii wapi kutokana na ukweli inahitaji umakini wa hali ya juu kama alivyofanya katika kazi yake ambayo inakaribia kutoka hewani ya 'Injinia'.
"Unajua sitaki kulipua kazi, nataka kuonyesha mfano kwa wadau wengine wa filamu, kwamba kazi hii si ya kulipuliwa kwa nia ya kujipatia fedha tu," alisema.
Machejo wa ITV ana Ngekewa
MSANII nyota wa maigizo aliyepo kundi la Jakaya Theatre linaloonyesha michezo yake kupitia kutuo cha ITV, Halid Chihame maarufu kama 'Alex Machejo' au 'Mzee wa Rivasi', amefyatua wimbo mpya uitwao 'Ngekewa' ikiwa ni maandalizi yake ya kupakua albamu kamili.
Akizungumza na MICHARAZO, Machejo, alisema wimbo huo ameurekodia katika studio za Kili Records chini ya mtayarishaji wake mahiri, C9 na tayari ameshakisambaza kwenye vituo vya redio na kuanza kuchezwa hewani.
Machejo alisema kibao hicho amekiimba peke yake na kipo katika miondoko aliyoipa jina la 'Flava Champlin', huku akiwa tayari ameshakamilisha nyimbo nyingine tano kwa ajili ya kuzirekodi kuwapa burudani mashabiki wake.
"Kaka nimeanza kusambaza kibao changu kipya kiitwacho 'Ngekewa' wakati huo huo nikiwa na nyimbo nyimbo tano zilizokamilika ambazo natarajia kuzifyatua wakati wowote kuanza wiki ijayo," alisema.
Alizitaja nyimbo hizo nyingine zitakazofuatia baada ya 'Ngekewa' ni 'Wa Kwalu', 'Mtoto kwa Mama Hakui', 'Tanzania', 'Nasubiri' na Kimanzichana'.
Msanii huyo aliyetamba na michezo kama 'Kovu la Siri', 'Kivuli', 'Utelezi', 'Riziki' na 'Bakora', alisema mipango yake ni kufyatua albamu kamili hapo baadae, ingawa alisema itategemeana na maamuzi ya menejimenti inayomsimamia kazi zake.
Simba, Yanga zatishia Super8
USHIRIKI wa Simba na Yanga katika michuano mipya inayotarajiwa kujumuisha timu nane za Tanzania Bara na Visiwaniinayokwenda kwa jina la "BancABC Super 8" uko katika hatikati kutokana na timu hizo kutoiweka ligi hiyo kwenye kalenda zao, imefahamika.
Ligi hiyo inayofanana na Ligi ya Muungano inatarajiwa kufanyika kuanzia Agosti 4 hadi 18 mwaka huu chini ya udhamini wa benki ABC na itajumuisha timu nane.
Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage, alisema jana kwamba ligi hiyo ni nzuri kwa lengo la kuiandaa timu lakini klabu yake itakuwa radhi kushiriki endapo mgawanyo wa mapato ya mlangoni utabadilishwa na kuwa zaidi ya yale yanayopatikana kwenye mechi za Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
Rage alisema kwamba klabu zimechoka kunyonywa na hivyo Simba itakuwa tayari kushiriki endapo klabu zitapata mgao wa zaidi ya asilimia 60 ya mapato ya mlangoni.
"Ni lazima kwanza tukae na kukubaliana tunapata nini sisi klabu, wakati wa kuona klabu zinanyonywa umepita na sasa kila mkataba ambao TFF watakuwa wameingia wanatakiwa kutushirikisha vilabu ili tujue maslahi yetu," alisema Rage.
Katibu Mkuu wa Yanga, Mwesigwa Selestine aliliambia gazeti hili jana kwamba klabu yake inaona ligi hiyo imeingiliana na programu zao za maandalizi ya msimu ujao wa ligi kuu hivyo maamuzi ya kushiriki au kutoshiriki yatajulikana baada ya kufanyika kwa kikao cha pamoja na benchi la ufundi la timu hiyo.
Mwesigwa alisema kwamba mara baada ya kocha mpya, Tom Saintfiet kutua, alipewa ratiba ya michuano iliyopo na hivyo kocha huyo aliandaa programu yake ambayo itaanza kutekelezwa hivi karibuni baada ya mapumziko ya wachezaji kumalizika.
"Uwezekano wa timu yetu kushiriki ni mdogo, haikuwa kwenye programu na hivyo inabidi uongozi na benchi la ufundi tujadiliane na kufanya maamuzi yatakayoisaidia timu," alisema katibu huyo.
Shirikisho la Soka Nchini (TFF) lilitangaza kusaini mkataba wa miaka mitatu na benki ABC ambayo itadhamini ligi hiyo mpya yenye lengo la kuziandaa klabu kwa ajili ya msimu mpya wa ligi.
CHANZO:NIPASHE
Azam yakana kuchunguza kipigo cha Yanga
WAKATI taarifa zilizagaa jana kwamba Azam imewasimamisha wachezaji wake wawili Mrisho Ngassa na Salum Aboubakar 'Sure Boy' kwa tuhuma za kucheza chini ya kiwango dhidi ya Yanga katika fainali ya Kombe la Kagame waliyolala 2-0 Jumamosi na kwamba nyota wengine watatu Aggrey Morris, Said Morad na kipa Deogratius Munishi 'Dida' wanachunguzwa, uongozi wa klabu hiyo ya Chamazi umesema walifungwa kihalali na hakuna mchezaji wa wanayemtuhumu kwa chochote.
Afisa Habari wa Azam FC, Jaffer Idd alisema Yanga walitumia makosa machache yaliyofanywa na mabeki wa Azam na kupachika mabao yaliyowapa ushindi wana Jangwani hao.
"Timu yetu ilicheza vizuri kwenye mechi ya fainali lakini Yanga ilituzidi ujanja na kutumia vizuri nafasi chache walizopata," alisema Jaffer.
Alisema hawawezi kumlaumu mchezaji yeyote kwa kipigo hicho kwa sababu wachezaji walioifikisha fainali timu hiyo ndio waliocheza mechi hiyo ya fainali na akawasifu wachezaji wa timu hiyo kwa ushujaa wa kuifikisha Azam fainali licha ya kwamba ilikuwa ikishiriki michuano hiyo kwa mara ya kwanza.
Jaffer alisema uongozi wa Azam umeridhika na matokeo hayo na kwamba sasa wanaelekeza nguvu zao katika maandalizi ya Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho Afrika.
Akizungumza na gazeti hili jana, Ngassa alisema kuwa timu yake juzi haikuwa na bahati ya kutwaa ubingwa huo lakini wanamshukuru Mungu kwa kufika fainali.
Ngassa alisema kwa dakika chache alizopewa kucheza, zikiwemo za mechi ya fainali alijituma na kuisaidia timu yake.
"Sidhani kama kuna aliyecheza chini ya kiwango, tumejituma na tumefika mbali licha ya kutochukua ubingwa," alisema Ngassa na kuongeza kwamba hajasimamishwa na uongozi wa timu yake kama ambavyo ilikuwa inazungumzwa jana.
Ilidaiwa pia kwamba uongozi wa Azam haukufurahishwa na kitendo cha Ngassa kwenda upande wa mashabiki wa Yanga na kushangilia baada ya kufunga goli kwenye mechi ya nusu fainali ya Kombe la Kagame dhidi ya Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Wachezaji wa Azam wamepewa mapumziko ya siku mbili ambapo kesho wataanza mazoezi ya kujiandaa na msimu ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
Kidunda adundwa Olimpiki
BONDIA pekee wa Tanzania katika mashindano ya Olimpiki, Seleman Kidunda jana alipigwa kwa pointi 20-7 na bondia Vasilli Beraus toka Jamhuri ya Moldova.
Batungi: Mkali wa Kikapu achekeleaye ajira jeshini
LICHA ya mchezo wa kikapu kumpatia rafiki wengi na kufahamika ndani na nje ya nchi, nyota wa klabu ya ABC, Gilbert Batungi 'B10' amesema kitu kikubwa anachojivunia kupitia mchezo huo ni elimu na ajira aliyopata jeshini.
Batungi, aliyeingia kwenye kikapu kwa ushawishi wa kaka yake aitwaye Jerome, alisema ajira hiyo aliipata mwaka 2006 kutokana na umahiri wake dimbani.
Alisema anaifurahia ajira hiyo kwa vile hakuwahi kuiota kuja kuipata maishani mwake.
Batungi, anayemudu nafasi ya kati, alisema pia kikapu kilimwezesha kupata nafasi ya kusoma Shule ya Sekondari Jitegemee baada ya kung'ara katika UMISSETA mwaka 2000 iliyofanyikwa jijini Mwanza.
Alisema wakati akishiriki michuano hiyo alikuwa mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Binza, kwa jinsi alivyong'ara aliuvutia uongozi wa Jitegemee iliyomchukua akiwa kidato cha pili na kusoma hadi alipohitimu kidato cha nne.
Alisema kutua kwake Jitegemee kulimwezesha kuonwa na kuitwa timu ya mkoa wa Dar tangu mwaka 2001 na ile ya taifa 2005 na kuzichezea mpaka sasa bila kutarajia.
Juu ya pambano gumu alilowahi kukutana nalo, Batungi apendae kula ugali kwa dagaa na mboga za majani na kunywa juisi ya embe, alitaja mchezo wa mwaka 2005 kati ya Tanzania na Kenya wa kuwania ubingwa wa Afrika Mashariki.
"Naikumbuka mechi hii kwa vile ilikuwa mara yangu ya kwanza kuichezea timu ya taifa, pia licha ya ugumu wake niliisaidia Tanzania kuilaza Kenya kwa mara ya kwanza."
Alisema mchezo huo uliochezwa Nairobi na kuisha kwa Tanzania kuiduwaza Kenya kwa vikapu 61-60.
"Hakika mafanikio niliyopata katika mechi hiyo hasa kuaminiwa na makocha na kutiwa moyo na wachezaji wenzangu, ni jambo linalonifanya nisiisahau," alisema.
Batungi, aliyekuwa mmoja wa wawaniaji wa Tuzo za TASWA za 2012 kama Mchezaji Bora wa Kikapu kwa mara ya pili mfululizo, alisema safari yake ya michezo kwa kiasi kikubwa imechangiwa na makundi matatu ya watu asiowasahau milele.
Alitaja kundi la kwanza ni wazazi wake waliomuunga mkono kwa kumtia moyo tangu utotoni, pili makocha wote waliomfundisha katika timu tofauti, na wachezaji wenzake waliomtia nguvu kwa kukitambua kipaji chake katika mchezo huo.
"Nitakuwa mchoyo wa fadhila kama sintowashukuru watu hawa kwa hapa nilipofika," alisema.
Batungi, aliyetwaa ubingwa wa Majiji akiwa na timu ya mkoa wa Dar 'The Dream Team', ubingwa wa Taifa wa Kikapu (NBL) na ule wa Muungano akiwa na klabu ABC ni mnazi mkubwa wa soka mchezo alioupenda kabla ya kaka yake kumbadilisha.
Ni shabiki mkubwa wa klabu za Chelsea na Simba akivutiwa na kiungo Mwinyi Kazimoto na Didier Drogba.
B10
Mkali huyo alitoboa siri ya jina lake la utani la 'B10', akisema ni kifupi cha ubini wake na jezi namba 10 anayopenda kuivaa tangu alipoibukia katika kikapu mwaka 1998.
"Naipenda mno jezi namba 10, nimekuwa nikiivaa tangu naanza kucheza kikapu na ndio maana wengi huniita B10, ikimaanisha Batungi Namba 10," alisema
Batungi, anayechizishwa na rangi nyekundu na nyeupe akimzimia nyota wa kikapu nchini Abdallah Ramadhani 'Dullah', alisema ndoto zake ni kuiona Tanzania ikitamba kimataifa na kuwasaidia vijana chipukizi kuja kuvaa 'viatu' vyao mara wakistaafu.
Nyota huyo anayependa kucheza Pooltable, alisema mchezo wa kikapu umedidimia kwa kukosekana viongozi makini na wenye uchungu na mchezo huo.
Alisema wengi wa viongozi wa sasa ni wababaishaji wanaojali masilahi yao na ndio waliochangia hata wadhamini kuukimbia mchezo huo na kutoa rai kwa wadau wenzake kubadilika kwa kuwachagua watu makini.
"Tusipozinduka na kuchagua watu wenye mapenzi na uchungu na kikapu, tutarajie mchezo huo kudidimia zaidi," alisema. Alidai kama angekutana na Rais au Waziri wa Michezo, angeomba serikali isaidie michezo yote badala ya kuangalia soka tu, pia angeiomba ishinikize makampuni kuwekeza kwenye michezo kwa kusaidia udhamini.
"Pia ningeiomba serikali iwekeze nguvu katika michezo ya vijana ili kusaidia taifa kuwa na nyota wa baadae kwa michezo yote ili itambe kimataifa," alisema.
Batungi, ambaye hajaoa ila ana mtoto mmoja, alisema hakuna ujinga anaoujutia kama tabia aliyokuwa nayo enzi akiibuka katika kikapu ya kutega mazoezi magumu kwa kusingizia ugonjwa alipokuwa akisoma Jitegemee.
Alisema kitu kinachomhuzunisha ni kifo cha nyota wa Netiboli, Grace Daudi 'Sister' na kudai kitu kimngine anachokifanya nje ya ajira yake jeshini ni biashara ya kuuza nguo.
ALIPOTOKA
Gilbert Paul Batungi, alizaliwa Januari 5, 1983 mkoani Shinyanga akiwa wa sita kati ya watoto saba wa familia yao.
Alisoma Shule ya Msingi Binza ya Maswa-Shinyanga na kuendelea na masomo ya Serkondari Shule ya Binza na baadae Jitegemee.
Kimichezo alianza kucheza soka na kutamba katika timu ya shule kabla ya kaka yake kumshawishi kucheza kikapu ambapo aliianza kuucheza rasmi mwaka 1998 katika klabu ya Black Wizard ya Shinyanga.
Baada ya kung'ara katika UMISSETA mwaka 2000 iliyofanyika Mwanza na kuonwa na Jitegemee alihamia jijini Dar na kupata fursa ya kuzichezea timu za Mgulani JKT, Chang'ombe Boys na Vijana.
Mwaka 2004 akiwa ameshamaliza masomo yake ya Sekondari, aliitwa JKT Mgulani kama mchezaji wa kiraia na miaka miwili baadae akapata fursa ya kuwa miongoni mwa walioajiriwa jeshini na kuhamia timu ya ABC anayoichezea mpaka sasa.
Batungi, anayetamani kuwa na watoto wawili pale atakapooa, aliwakumbusha wachezaji wenzake kujibidiisha kufanya mazoezi na kuwa makini na ugonjwa wa Ukimwi aliodaai unapoteza nguvu kazi kubwa ya taaifa.
Alisema rai hiyo ya kujikinga Ukimwi sio kwa wachezaji tu bali jamii kwa ujumla kwa kuitaka kuepuka ngono zembe, wawe waaminifu na kutumia kinga, huku akisisitiza kinga sahihi ni kufanya ibada na kufanya mazoezi ili kupunguza mihemko.
Aliwasihi wachezaji wenzake kujituma uwanjani na kuwa na nidhamu ili kusaidia kushawishi wadhamini kuwasaidia.
Mwisho
Ubalozi wa UAE kutumia zaidi ya Dola 1200,000 kufuturisha mikoa saba nchini
UBALOZI wa Nchi za Falme za Kiarabu (UAE) nchini, kupitia taasisi za Sheikh Khalifa bin Zayed Al Hahyan, Sharjah Charity Internation na Red Cresent, unatarajia kutumia zaidi ya dola 120,000 za Marekani, kuifadhili mikoa saba nchini kwa ajili ya futari na Zakatul Fitr kipindi chote cha mfungo wa mwezi wa Ramadhani.
Akizungumza kwa niaba ya Balozi wa UAE nchini Tanzania, Mallalla Mubarak Al Ameir na msaidizi wake, Mohammed Obaid Salem AlZaabi, baada ya kugawa futari katika msikiti wa Al Makbool, Msasani Dar es Salaam juzi, Mhasibu wa ubalozi huo, Abdallah Ahmedina, alisema baadhi ya msikiti ya mikoa hiyo ndiyo itakayonufaika.
Ahmedina, aliitaja mikoa ambayo waumini wake tangu kuanza kwa mfungo wa mwezi wa ramadhani wamekuwa wakifuturishwa na watakuja kupewa Zaka kwa ajili ya Eid El Fitri ni Dar es Salaam, Iringa, Kilimanjaro, Arusha, Pwani, Dodoma na Morogoro.
Mhasibu huyo alichangua kuwa kiasi cha dola 80,000 zinatoka asasi ya Khalifa, dola 36,000 kutoka Red Cresent na dola 6,000 zinatoka Sharjah na kusema utaratibu huo wa kusaidia waumini wa misikiti ya mikoa hiyo umeanza tangu ubalozi wao uwe nchini na utaendelea kwa lengo la kuwasaidia waumini kutekeleza ibada yao ya funga bila ya hofu ya kukosa futari au kuisherehea Eid.
Alifafanua, kati ya fedha hizo zilizotolewa na asasi hizo tatu zinatumika kwa futari na zilizosalia ni kwa ajili ya kugawa Zakatul fitr ambayo huwalenga waumini wajane, yatima, walemavu, maskini na fukara ili kuisherekea sikukuu kwa furaha na amani.
"Miaka yote huwa tunatoa futari na kugawa zakatufitr, mwaka huu tutatumia kama dola 122,000 za Marekani zinazotolewa na asasi zilizopo chini ya ubalozi wetu za Sheikh Khalifa, Red Cresent na Sharjah Charity," alisema.
Akitoa shukrani kwa niaba ya waumini wake, Imamu wa msikiti wa Al Makbool, Sheikh Mussa Abdallah, aliushukuru ubalozi huo kwa kile walichosema umewasaidia kutimiza moja ya nguzo za dini yao.
"Waumini wengine hawana uwezo wa kupata futari kama hii, tunashukuru ubalozi na asasi zote zilizochangia msaada huu na Inshallah, Mwenyenzi Mungu awazidishie," alisema Imamu Abdallah.
Alisema baadhi ya watu waliokuwa hawafungi kwa kutokuwa na hakika ya kupata futari kwa sasa hawana sababu tena kwa vile wamepata uhakika wa kupitia ufadhili huo wa ubalozi wa UAE.
Sunday, July 29, 2012
Mapembe: Fundi 'mvunja mbavu' aliyejitosa kwenye muziki
TANGU utotoni, aliwavutia watoto na wanafunzi wenzake kwa kipaji cha kuchekesha, ila hakujitambua au kuota kama kipaji hicho kingemtoa kimaisha.
Ndio maana mara alipohitimu darasa la saba katika Shule ya Kiwalala, Lindi alijitosa kwenye ufundi uashi na baada umakenika katika miji tofauti.
Hata hivyo alivyotua Dar na kufanya kazi ya udereva wa daladala ndipo alipobaini alikuwa amechelewa mno, baada ya msanii Khalfan Ahmed 'Kelvin' kukitambua kipaji chake na kumshawishi kuingia kwenye sanaa.
Wengi wanamfahamu kama 'Mapembe' ila majina yake kamili ni Ismail Makomba mmoja wa wachekeshaji mahiri nchini.
Mapembe alisema wazo la Kelvin alilipuuza kwa kudhani angepoteza muda bure, lakini alipong'ang'aniwa aliamua kujiunga na kundi la msanii huyo la Simple Production na kuanza kuonyesha makeke.
Mkali huyo aliyevutiwa kisanii na Abdallah Mkumbira 'Muhogo Mchungu' alicheza kazi yake ya kwanza mwaka 2003 iitwayo 'Sheria' kisha kufuatiwa na 'Lugha Gongana', 'Talaka ya Mdundiko', 'Msela Nondo' na 'Ngoma Droo' na nyingine.
Alijitoa kwa ruksa Simple Production na kuanzisha kampuni binafsi ya Karena Production iliyozalisha filamu tano za Trafiki, Mdimu, Mbagala, Kiduku, Mpambano na sasa akijiandaa kuingiza sokoni 'Posa' akiwa pia ni muajiriwa wa kampuni ya Al Riyamy.
Mapembe ambaye pia ni mwanaharakati anajishughulisha pia na muziki akiwa ameshatoa nyimbo kadhaa na kwa sasa yupo studio kukamilisha kibao kiitwacho 'Gesi ya Kusini'.
Nyimbo zake nyingine zinazotamba hewani kwa sasa zikiwa katika miondoko ya Zouk ni Mwalimu, Nandenga, Usalama wa Raia, Muungano na Ubaya wa Mafisadi.
Mapembe anayemshukuru Kelvin na kampuni ya Al Riyamy kumfikisha alipo, anajipanga kurudi 'darasani' Chuo cha Taifa cha Sanaa Bagamoyo ,TaSUBA, ili kuongeza maarifa.
Mume huyo wa mtu na baba wa mtoto mmoja aitwae Makomba, alisema sanaa Bongo imepiga hatua kubwa, isipokuwa tatizo la wizi unaofanywa na watu wachache.
Aliiomba serikali iwasaidie wasanii kunufaika na kazi zao kwa kuweka sheria kali za kuthibiti maharamia hao, huku akiwataka wasanii wenzake kupendana na kushirikiana.
Pia aliwakumbusha wasanii wenzake wasijikite kutoa kazi zao katika nyanja za mapenzi na kusahau mambo mengine ikiwemo masuala ya kisiasa na kijamii, kama anavyofanya yeye kupitia muziki aliojitosa hivi karibuni.
Mapembe alizaliwa Januari, 1972 Kiwalala, Lindi akiwa ni mtoto wa pili kati ya watatu wa familia yao, alisoma Shule ya Msingi Kiwalala kabla ya kujishughulisha na kazi za ufundi uashi, magari na udereva na baadae kuingiza kwenye uigizaji.
Mobby Mpambala: Asiyeamini kama filamu zimempa nyumba, gari na kampuni
ALIPOSHAWISHIWA na nyota wa filamu nchini, Single Mtambalike 'Rich', aingie katika fani ya uigizaji, Mobby Mpambala, hakutilia maanani wazo hilo kutokana na imani aliyokuwa nayo juu ya sanaa ya Tanzania kwamba hailipi.
Hata hivyo baada ya ushawishi wa muda mrefu na kuamua kujitosa rasmi mwaka 2000, msanii huyo amejikuta 'akiisujudia' fani hiyo kwa jinsi ilivyomwezesha kiuchumi na kimaisha tofauti na alivyofikiria mwanzoni.
Mkali huyo wa filamu za mapigano na zile za kutisha, alisema kipindi kifupi cha kuweko kwake kwenye sanaa hiyo imemwezesha kujenga nyumba katika kiwanja alichokuwa nacho eneo la Gongolamboto, kununua gari na kumudu kuanzisha kampuni binafsi ya kuzalisha filamu ya 'Wizaga Entertainment'.
Pia, msanii huyo anamiliki kundi la sanaa la Mtazamo Family linalojihusisha na sanaa za ngoma, maigizo na sarakasi huku akiendesha kiwanda kidogo cha kutengeneza masofa na samani nyingine za majumbani eneo la Amana-Ilala.
"Sio siri kabla ya kuingia kwenye sanaa niliidharau fani hii kutokana na hali ya mambo ilivyokuwa miaka ya nyuma ambapo wasanii hawakuwa na chochote cha kujivunia, lakini leo nakiri sanaa Bongo inalipa kutokana na mafanikio makubwa niliyoyapata katika kipindi kifupi," alisema.
Mpambala alisema alikutana na Rich mwaka 1996 na kumtaka ajiunge kwenye sanaa baada ya kugundua kipaji chake na umahiri wake wa michezo ya Kungfu na utunisha misuli, ila alimpuuza kwa vile aliringia ujuzi wake wa ufundi seremala.
Alisema hata hivyo shinikizo la Rich pamoja na ndugu na jamaa zake waliotambua kipaji alichonacho, ndipo mwaka 2000 alipojitosa kwa kushiriki filamu ya 'Kidole Tumbo' iliyozuiwa na serikali kutoka.
Mpambala alisema Rich 'alimbeba' kwa kumshirikisha katika kazi zake kadhaa kama 'Swahiba', iliyomtambulisha kwa mara ya kwanza yeye na Rose Ndauka, 'Mahabuba' na 'Heshima ya Penzi'.
Alisema kazi hizo zilimfungulia neema kwa kushirikishwa kazi nyingine kadhaa zinazofikia 30 kwa sasa, akizitaja baadhi kuwa ni; 'Kamanda', 'Jozani', 'Signature', 'Secretary', '007', 'Time to Fight, 'Zuadiswa', 'Before Death', 'Hii ni Tatu', 'Criminal', 'Jamal' na 'The Chase' aliyoitaja kama filamu bomba kwake.
AMRI PURI
Mpambala, alisema licha ya kwamba hakuwahi kuota kuwa msanii, lakini alimzimia mno nyota wa zamani wa filamu za Kihindi, Amri Puri 'Mzee Ashanti', ambaye kwa sasa ni marehemu.
Alisema alivutiwa na Amri Puri, kwa aina yake ya uigizaji kama mbabe na jitu katili, kitu alichodai amekuwa akimuiga katika baadhi ya picha alizocheza kama njia ya kumuenzi mkali huyo wa Bollywood.
Mpambala anayezishabikia Simba na Manchester United, akipenda kula ugali kwa dagaa na kunywa soda ya Pepsi, alisema hakuna kitu cha furaha kwake kama siku alipomuoa mkewe wa kwanza aitwae, Jasmine mwaka 2004 na ndoa nyake ya pili dhidi ya Zola mwaka 2011.
"Kwa kweli siku nilipofunga ndoa na wake zangu hawa ndio tukio la furaha kwangu, na ninahuzunishwa na kifo cha baba yangu mlezi, Abdul Ally Kibena aliyefariki mwaka 1999," alisema.
Mpambala, anayechizishwa na rangi ya bluu, alisema kingine kinachompa furaha ni kufanikiwa kufyatua kazi zake binafsi tano za filamu kupitia kampuni yake ya Wizaga.
Alizitaja kazi hizo kuwa ni 'I Wonder', My Brother', 'Criminal' aliyoshirikiana na 'Carlos', 'Fuvu' na 'Anti Virus' anazotarajia kuziingiza sokoni hivi karibuni.
SKENDO
Mpambala anayemzimia 'swahiba' wake Haji Adam 'Baba Haji', alisema kati ya vitu vinavyomkera ni tabia ya baadhi ya wasanii chipukizi kupenda kujihusisha na skendo kwa nia ya kutafuta umaarufu.
Alisema vitendo vinavyofanywa na wasanii hao wasiojitambua vinaidhalilisha fani yao pamoja na kuzichafua familia za wasanii hao, licha ya wenyewe kuonekana kutojali.
Mkali huyo mwenye watoto sita, alisema ifike wakati wasanii watambue umaarufu hupatikana kupitia umahiri wa kazi zao na sio kujidhalilisha ovyo magazetini.
Mpambala anayependa kutumia muda wake wa ziada kufanya mazoezi na kuendesha kazi za useremala katika kiwanda chake na kundi lake la sanaa lililotoa ajira kwa vijana 30, alisema kama angekutana na Rais au Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, angeomba sanaa isaidiwe.
"Ningewaomba wasaidie iundwe kwa sheria kali ya kuthibiti wizi wa kazi za wasanii sambamba na kuwepo kwa mipango mizuri ya kutambuliwa kwetu kama ilivyo kwa watu wa kada nyingine wanaothaminiwa na kuenziwa nchini."
ALIPOTOKA
Mobbi Nassor Saleh Mpambala 'Mobby Mpambala', alizaliwa Novemba 28, 1965 katika wilaya ya Igunga,Tabora akiwa mtoto wa tatu kati ya nane wa familia yao.
Alisoma elimu yake ya Msingi katika Shule ya Makurumla, jijini Dar kabla ya kurejea Tabora kumfuata mama yake aliyekuwa ametangana na baba yake na kujishughulisha na biashara ndogo ndogo huku akijiendeleza kwenye michezo ya sarakasi na kungfu aliyoicheza tangu utotoni.
Mpambala anayewashukuru wazazi wake, Rich na mkewe wa kwanza Jasmine kwa namna walivyomsaidia kufika mahali alipo, amejaliwa kuwa na watoto sita watatu akiwapata katika ndoa yake ya kwanza nao ni Edo, 27, Mariam22 na Saleh,20.
Watoto wake wengine ni Goodluck, 18, anayesoma Sekondari jijini Arusha, Zuwena, 13 aliyepo darasa la sita katika Shule ya Msingi Mapinduzi-Kigogo jijini Dar na Munira, 5 anayesoma chekechea.
TPBO yasitisha mapambano kisa....!
ORGANAIZESHENI ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBO), imesitisha kwa muda mapambano yao yote ya ngumi ili kupisha mfungo wa Mwezi wa Ramadhani.
Rais wa TPBO, Yasin Abdallah 'Ustaadh' alisema wamechukua uamuzi huo ili kuwapa nafasi mabondia na mashabiki wa ngumi kujikita kwenye ibada hiyo ya funga ambayo ni moja ya nguzo tano na muhimu kwa maisha ya waumini wa dini ya Kiislam.
Ustaadh, alisema kusitishwa kwa michezo hiyo haina maana kwamba TPBO haifanyi kazi, kisha akafafanua kuwa ofisi zao zinaendelea kufanya kazi kama kawaida isipokuwa haitaruhusu pambano lolote katika kipindi hiki cha mfungo.
"TPBO, tumesimamisha mapambano yote ya ngumi ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani ili kuungana na waislam katika utekelezaji wa ibada yao ya funga, ingawa ofisi zetu zilizopo Temeke Mwembeyanga zinaendelea kufanya kazi ikiratibu mapambano yatakayofanyika baada ya mfungo huo," alisema Ustaadh Yasin.
Aidha, alisema TPBO inawatakia mfungo mwema mabondia na wadau wa ngumi wenye imani na dini ya Kiislam ili waweze kufunga na kumaliza bila matatizo.
Mwisho
YANGA KAMA KAWA KAMA DAWA YABEBA TENA KOMBE LA KAGAME
KLABU ya soka ya Yanga jana ilitwaa kwa staili ya aina yake ubingwa wake wa pili mfululizo na wa tano jumla wa Kombe la Kagame, la klabu bingwa ya soka ya Afrika Mashariki na Kati, kwa kuifunga Azam mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Taifa.
Ushindi huo si tu uliiwezesha kwa namna nyingi kulipa kisasi cha kudhalilishwa kwa mabao 3-1 na Azam kulikoandamana na kupigana uwanjani na kufungiwa wachezaji wake katika mchezo wa ligi kuu ya Bara Mei, bali pia ulikuwa wa kikatili.
Bao la kwanza la Yanga lilifungwa na Hamisi Kiiza katika dakika ya 44 likiwa la tano kwa mchezaji huyo katika michuano ya mwaka huu, baada ya kunasa pasi ya nyuma ya beki wa pembeni wa Azam Ibrahim Shikanda.
Lakini goli ambalo lilinogesha ushindi huo, na ambalo litakuwa liliikata maini vibaya Azam ni la mshambuliaji mpya hatari Said Bahanuzi la dakika ya mwisho ya majeruhi.
Zikiwa zimeongezwa dakika tatu za majeruhi, mpira mrefu uliopigwa toka nyuma na beki Kelvin Yondani katika dakika ya 93 ulimkuta Bahanuzi akikabiliana na Said Morad.
Akitumia ubavu aliojaaliwa na Mola, pande la mtu Bahanuzi alimzungusha Morad kabla ya kumtoka na kuachia shuti kali lililotinga kwenye nyavu za juu za goli na kumfanya mfungaji-mwenza aliyeongoza kwenye Kombe la Kagame kwa pamoja na Kiiza.
Tedy Etekiama wa Vita ya JK Kongo pia alifunga mabao sita lakini CECAFA, shirikisho la soka la ukanda huo, liliwatunuku wauaji hao wa Yanga kutokana na kuipa timu yao ubingwa.
Tofauti na mechi zilizotangulia, Azam ambayo ilifika fainali ya Kombe la Kagame kwa mara ya kwanza ikishiriki mara ya kwanza jana ilijenga mashambulizi yake taratibu kutokana na mpira wake wa pasi fupi fupi za kasi kuikauka.
Kocha wa Yanga Tom Sentfiet aliwashukuru wachezaji wake kwa kumudu kucheza kwa "mbinu tulizopanga" na kwamba kufungwa kwao katika mechi ya kwanza kuliisadia kurekebisha makosa yaliyoipa ushindi wa mechi zote tano zilizofuata.
Yanga ilikuwa pia bingwa wa Kombe la Kagame katika miaka ya 1975, 1993 na 1999 na mbali na kukata tiketi ya michuano hiyo tena mwakani imebakiza kikombe kimoja kufikia rekodi ya Simba ambayo ndiye bingwa pekee mara sita.
Pia iwapo kama mwakani itafanikiwa kutetea taji hilo itakuwa timu ya pili baada ya AFC Leopard ya Kenya iliyowahi kufanya hivyo mfululizo wakati ikitamba katika soka la Afrika.
Katika vurugu za ushindi wa Azam Mei, wachezaji sita wa Yanga walitozwa faini zinazofikia jumla ya sh. milioni nane ambazo sasa zinaweza kulipwa kutoka katika zawadi ya sh. milioni 45 ya bingwa wa Kombe la Kagame.
Azam inapata sh. milioni 30 wakati Vita imezawadiwa sh. milioni 15 kwa kushika nafasi ya tatu baada ya kuifunga APR ya Rwanda 2-0 mapema jana.
Timu zilikuwa:
YANGA: 'Barthez', Oscar Joshua, Stephano Mwasika, 'Cannavaro', Kelvin Yondani, Haruna Niyonzima, 'Chuji', Rashid Gumbo (Juma Seif dk.74), Hamisi Kiiza, Said Bahanuzi', David Luhende.
AZAM: 'Dida', Ibrahim Shikanda (Samir Haji dk.68), Erasto Nyoni, Said Morad, Aggrey Moris, Jabir Aziz, Kipre Tchetche (Mrisho Ngasa dk.68), Salum Abubakar, John Bocco, Ibrahim Mwaipopo, 'Redondo'.
Subscribe to:
Posts (Atom)