Na Boniface Wambura
USAILI wa waombaji uteuzi kwenye uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board) unaendelea na unatarajia kukamilika leo (Septemba 1 mwaka huu).
Kamati ya Uchaguzi ya TFF chini ya Mwenyekiti wake Hamidu Mbwezeleni ilianza usaili juzi (Agosti 30 mwaka huu) ambapo matokeo ya usaili yanatarajiwa kutangazwa keshokutwa (Septemba 3 mwaka huu).
Kati ya Septemba 4 na 6 mwaka huu, Kamati ya Uchaguzi kupitia Sekretarieti ya TFF itawasilisha kwenye Kamati ya Maadili ya TFF mashauri yote ya maadili ili kujadiliwa na kutolewa uamuzi na kamati hiyo.
Vilevile kati ya Septemba 4 na 6 mwaka huu ni kipindi cha kukata rufani kwenye Kamati ya Rufani ya Uchaguzi kwa masuala yasiyo ya maadili. Kwa watakaokata rufani wanatakiwa kuambatanisha na ada ya rufani kwa Katibu Mkuu wa TFF kabla ya saa 10 kamili jioni ya Septemba 6 mwaka huu.
STRIKA

USILIKOSE

Sunday, September 1, 2013
Kocha Kim amuongeza Jonas Mkude Stars
![]() |
Jonas Mkude |
Na Boniface Wambura
KIUNGO wa Simba, Jonas Mkude ameitwa kwenye kikosi cha Taifa Stars kinachojiandaa kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Gambia itakayochezwa Septemba 7 mwaka huu jijini Banjul.
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen amemuongeza mchezaji huyo ili kuimarisha sehemu ya kiungo. Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imeingia kambini tangu Agosti 29 mwaka huu kwenye hoteli ya Accomondia jijini Dar es Salaam.
Timu hiyo imefanya mazoezi leo asubuhi kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume wakati kesho Jumatatu (Septemba 2 mwaka huu) saa 10 jioni itafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ibrahim Kamwe 'Big Right' ajitoa TPBO-Limited, kisa....!
KATIBU mkuu wa Tanzania Professional Boxing Organisation (TPBO),
Ibrahim Kamwe ambaye anajulikana kwa jina la bigright amejitoa katika uongozi wa chama cha ngumi kama
kiongozi.
Bigright ambae ukiondoa mambo ya kichama mara nyingi amekuwa
akiwaongoza maofisa wa chama hicho katika shughuli mbalimbali na mapambano
mengi kama jaji mkuu ,mhifadhi rekodi za mabondia na mshauri katika shughuli
za kiufundi.
Akizungumza na MICHARAZO, Kamwe amesema ameamua kupumzika
shughuli za TPBO na kurudi kwenye ufundishaji wa vijana na kuendelea na kampuni
yake ndogo ya bigright promotion ambayo inajihusisha na utayarishaji wa
matamasha na uandaaji wa mapambano ya ngumi.
"Kwa kuwa naupenda mchezo wa
ngumi nimefanya shughuli hii kwa muda
mrefu kukiwa na utatautata wa hapa na pale na yote hii kwa ajili ya kuuendeleza mchezo
wa ngumi nchini lakini imekuwa ni ngumu kwangu kuendelea na wadhifa huo," alisema na kuongeza;
"Nawashukuru maofisa wenzangu wamekuwa wakinipa ushirikiano wa karibu. Ila kwa
sasa najitoa katika uongozi na nitajihusisha na ngumi kivingine ikiwemo
kuwaendeleza vijana na kuandaa mapambano madogomadogo ya kukuza vipaji," alisema.
Uzinduzi wa 'Foolish Age' wafana Dar, 'Anaconda' nouma!
Elizabeth Michael 'Lulu' akitoa
Shukrani kwaWadau wote waliojitokeza katika Usiku wake wa uzinduzi wa
Filamu yake Mpya iitwayo Foolish Age uliofanyika katika Ukumbi wa
Mlimani City Usiku wa Kuamkia jana
Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya
Proin Promotions Limited Geofrey Lukaza (Kushoto) akiwa na Waifu wake
Groly Lukaza (katikakati) pamoja na Pedeshee Mamaa Ng'onzi wakijiachia
Mbele ya Kamera ya Lukaza Blog usiku wa kuamkia jana katika uzinduzi wa
Filamu ya Lulu iitwayo Foolish Age katika Ukumbi wa Mlimani City chini
ya kampuni ya Proin Promotions Limited
Lady Jay Dee aka Anaconda akitoa
Burudani katika Uzinduzi wa Filamu mpya ya Lulu iitwayo Foolish Age
iliyotengenezwa na Kampuni ya Proin Promotions Limited, Lady Jay Dee
akiwa pamoja na Machozi Band walitoa Bururdani Safi Sana katika Uzinduzi
huo Uliofanywa na Kampuni ya Proin Promotions Limited katika Ukumbi wa
Mlimani City usiku wa Kuamkia jana
Msanii Barnaba akitoa burudani
katika uzinduzi wa Filamu mpya ya Lulu uliofanya na Kampuni ya Proin
Promotions Limited katika ukumbi wa Mlimani City Usiku wa Kuamkia jana
Katikati ni Mama Mzazi wa
Marehemu STEVEN KANUMBA akiongea kwa furaha huku akitoa machozi na
Msanii wa Filamu Tanzania Wema Abraham Sepetu(kushoto) na Rafiki yao
katika Uzinduzi wa Filamu ya Lulu ulioandaliwa na kufanywa na Kampuni ya
Proin Promotions Limited katika Ukumbi wa Mlimani City usiku wa Kuamkia
jana
Wema Sepetu (aliyepiga magoti)
akikumbatiana na Mama mzazi wa marehemu Steven KANUMBA wakati wa
Uzinduzi wa Filamu ya Mwanae Elizabeth Michael katika Ukumbi wa Mlimani
City, uzinduzi uliokwenda sambamba na burudani kutoka Kwa Wasanii
mbalimbali wa Muziki wa Bongo Fleva katika Ukumbi wa Mlimani City usiku
wa Kuamkia jana
Wadau wakisakata Mduara katika
uzinduzi huo wa filamu ya Lulu iitwayo Foolish Age uliofanyika katika
Ukumbi wa Mlimani City Usiku wa kuamkia leo, Uzinduzi huo wa Kufa mtu
uliofanywa na Kampuni ya Proin Promotions Limited ulifana kupita Kiasi
Baadhi ya Wadau Mbalimbali
waliojitokeza katika Uzinduzi huo uliofanyika katika Ukumbi wa Mlimani
City chini ya Kampuni ya Pron Promotions Limited.
Meza ya Viongozi wa Kampuni ya
Proin Promotions Limited Kuanzia Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni
ya Proin Promotions Limited Bw Geofrey Lukaza, akifuatiwa na Pedeshee
Mamaa Ng'onzi, Bwa Johnson Lukaza Mwenyekiti waa Makampuni ya Proin
Tanzania, Gadna G Habash na Lady Jay Dee aka Anaconda wakiwa makini
Kufuatilia Uzinduzi Mzima wa Filamu Mpya ya Lulu iitwayo Foolish Age
uliofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City chini ya Kampuni ya Proin
Promotions Limited.
Paul SekaBoy Mkurugenzi Wa
Sekaboyi Production akiwa na rafiki yake katika uzinduzi wa Filamu ya
Lulu iitwayo Foolish Age katika Ukumbi wa Mlimani City Usikuwa kuamkia
jana
Mmiliki wa Lukaza Blog Josephat
Lukaza akiwa katika Picha ya Pamoja na Mmoja wa Watembeleaji wakubwa
kabisa wa Lukaza Blog Maa Fetty katika Uzinduzi huo uliofanyika katika
ukumbi wa Mlimani City Usiku wa Kuamkia leo
Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya
Lady jay Dee akituzwa Mahela katika Uzinduzi wa Filamu Mpya ya LULU
iitwayo Foolish Age ndani ya ukumbi wa Mlimani City Usiku wa Kuamkia jana
Thamani ya SAkiba ya Wafanyakazi yafikia Bil. 178
Na Suleiman Msuya
THAMANI ya Mfuko wa Akiba ya Wafanyakazi Serikali
imekuwa kutoka bilioni 72.55 mwaka 2008/2009 hadi kufikia bilioni 178.3 mwezi
Juni mwaka 2013.08.30
Hayo yamebainishwa na Kaimu Mkurugenzi wa GEPF Festo
Fute wakati akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Alisema ongezeko hilo limechangiwa na kuongezeka kwa
wanachama pamoja na uwekezaji katika sekta mbalimbali kama amana za serikali, makampuni yaliyo orodheshwa
kwenye soko la mitaji (DSE), uwekezaji wa muda maalum kwenye mabenki ya
biashara, mikopo, hati fungani na majengo.
Fute alisema hadi kufikia mwaka huu GEPF imefanikiwa
kusajili wanachama 60, 030 ambapo kwa kipindi cha mwaka 2008/2009 walikuwa
wanachama 30,227 hiyo ikitokana na
jitihada zao za kuhakikisha kuwa watu wote wanafaidika na mfuko huo.
“Unajua katika mifuko hii ya hifadhi ya jamii moja
ya malengo yake ni kuhakikisha kuwa thamani ya mfumo inaongezeka jambo ambalo
tumeweza kulitekeleza kwani sasa mfumo una thamani ya shilingi bilioni 198.30,”
alisema.
Kaimu Mkurugenzi huyo alisema vitegauchumi wa mfuko
viliongezeka kutoka shilingi bilioni 64.94 mwaka 2009 hadi kufikia shilingi
179.68 mwaka 2013, ambapo na mapato yameongezeka kutoka shilingi bilioni 5.48 mwaka 2009 hadi
bilioni 18.25 mwaka 2013.
Alisema pamoja mafanikio hayo ya thamani ya mfuko
ila pia wamekuwa wakiwalipa wanachama wao mafao kwa wakati ambao kwa kipindi
cha mwaka 2012 hadi 2013 zaidi ya bilioni 5 zimelipwa kwa wanachama kama mafao.
Aidha akizungumzia kuhusu mpango wa hiari wa
kujiwekea akiba ya uzeeni (VSRS) alisema mfuko huo umekuwa na mafanikio makubwa
ambapo tangu mwaka 2009 hadi 2013 wameweza kusajili na wanachama 18,700 ambapo
jumla ya akiba za wanachama zilifikia kiasi cha shilingi bilioni 3.05.
Fute alisema katika mfuko huo wanachama
wamegawanyika katika makundi mbalimbali ambayo ni wafanyabiashara 7,480, kilimo
ufugaji 6,545, ujasiriamali 1,683 na waajiriwa 2,992.
Pia alisema pamoja na mafanikio ambayo wameyapata
pia mfumo huo unakabiliwa na changamoto mbalimbali kama kupitwa kwa sheria
inayoongoza mfuko na ufahamu mdogo wa watu kuhusu mfuko.
TAHLISO nao watoa mapendekezo yao Katiba Mpya
Na Suleiman Msuya
WAKATI jamii ya Kitanzania ikiwa imeelekeza mitazamo,
michango na mawazo juu ya aina ya Katiba ambayo wanaitaka Jumuiya ya Wanafunzi
wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO) wamependekeza kuwepo kwa haki ya
kupatiwa elimu bora, haki za wanaume pamoja na kuomba suala la muungano liwe la
wananchi wote kutoa maoni.
Hayo yamebainshwa na Mwenyekiti wa TAHLISO Amon
Chakushemeire wakati akizungumza na MICHARAZO, ambapo alisema mapendekezo hayo yametokana baraza wa
wanachama wa TAHLISO ambao walikutana Mkoani Mbeya kwa siku mbili ambapo waliweza
kujadili rasimu ya Katiba wakiwa sehemu ya baraza.
Mwenyekiti baada ya kuipitia kwa undani rasimu hiyo wajumbe
waligundua mambo makuu matatu ambayo ni haki ya kupatiwa elimu, haki za wanaume
na muundo wa muungano ndiyo yanahitaji kuwekwa kama mapendekezo baada ya kuona
watu wengi wamekuwa wakiyajadili mambo mengine na kuyaacha.
“Unajua watu wengi waliochangia rasimu ile
wameonekana kusauhau suala la haki ya kupatiwa elimu, haki za wanaume jambo
ambalo linaonekana kuwa linaweza kufanya yakasahaulika na kuendelea kuleta
athari kwa jamii,” alisema.
Alisema suala la elimu linahitaji kubainishwa kwenye
katiba moja kwa moja ili kuhakikisha kuwa jamii inapatiwa elimu kuanzia msingi
hadi mahali ambapo mfaidika ataweza kutumikia jamii.
Chakushemeire alisema suala la kuwepo kwa haki za
wanaume linaonekana kama halina tija ila ukweli ni kwamba jamii ya wanaume
imekuwa ikipata athari kubwa ila haina pahali pa kusemea.
Mwenyekiti huyo alisema suala la muundo wa muungano
ni vema likarejeshwa kwa wananchi ili waweze kufanya maamuzi wao wenyewe na
lisiwe ni suala la watu wachache.
Akizungumzia suala la TAHLISO kuhusishwa na
kuwapigia kampeni baadhi ya wagombea nafasi za Urais Katibu wa TAHLISO Donati
Salla alisema wao hawahusiki na mambo hayo na kuwataka wanachama wao kutotumia
nembo yao kufanya mambo yao binafsi.
Salla alisema wanaotajwa kuwa walikuwa viongozi wa
TAHLISO huko morogoro ni kweli kuwa ni wanachama TAHLISO ila hakutumwa na wao
na ni watu wenye maslahi yao binafsi jambo ambalo wanalipinga.
Aidha alitoa angalizo kwa baadhi ya watu ambao
wanajiita Taasisi ya Vijana Tanzania (TAVITA)
kuacha kuwashirikisha wanachama wa TAHLISO katika mikakkati yao ya kutumiwa na
watu wenye mipango ya kugombea Urais mwaka 2015.
Alisema kundi hilo linatarajiwa kukutana Septemba 7
mwaka huu nyumbani kwa Waziri Mkuu aliyejiuzulu wilayani Monduli.
Cheka, Mashali, King Class watoa vipigo kwa wapinzani wake
Bondia Chipaki Chipindi kushoto akionyeshana umwamba wa kutupiana makonde na Alphonce Mchumiatumbo katika mpambano wao Mchumiatumbo alishinda kwa TKO |
Bondia Deo Njiku akioneshana kazi na Alain Kamote wakati wa mpambano wao wa utangulizi Kamote alishinda kwa Point |
Bondia Mada Maugo akijikakamua kumpiga konde Thomasi Mashali wakati wa mpambano wao uliofanyika jana wa kugombania Ubingwa wa WBF-Afrika. Mashali alishinda kwa pointi mpambano huo. |
Thomasi Mashali kushoto na Maa Maugo wakioneshana umwamba |
Bondia Francis Cheka kushoto akioneshana umwamba na Phil Williams wa Marekani wakati wa kugombania ubingwa wa WBF uliofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee. Cheka alishinda kwa pointi. |
Bondia Francis Cheka kushoto akioneshana umwamba na Phil Williams wa Marekani wakati wa kugombania ubingwa wa WBF uliofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee. Cheka alishinda kwa pointi. |
Miss Utalii Tanzania 2013 kwenda Equatorial Guinea Sept 28
nchini
Tanzania tunashiriki kwa mara ya tano katika Miss Tourism
World, mara ya kwanza ikiwa ni mwaka 2005. Katika fainali zote tulizo shiriki
tumeshinda mataji ya Dunia , mataji hayo ni :
Miss Tuourism World 2005- Africa (Witness Manwingi –
Tanzania),
MISS TOURISM TANZANIA & MISS TOURISM WORLD 2005- AFRICA- Witness Manwingi |
Miss Tourism Tanzania & Miss Tourism World 2006 – SADC (Killy Janga Left),
Miss Tourism Tanzania & Miss Tourism World 2007 – Africa (Lillian Cyprian ),
Miss Tourism Tanzania & Miss Tourism World 2008- Internet (Lilly Kavishe 1ST Left)
Miss Tourism Tanzania ,the Miss Tourism World 2005- Africa witness Manwingi |
Miss Tourism Tanzania ,the Miss Tourism World 2005- Africa witness Manwingi (right) |
Miss Tourism Tanzania ,the Miss Tourism World 2005- Africa witness Manwingi |
Miss Tourism Model Of The World 2006 –Personality (
Witness Manwingi).
Miss Tourism Tanzania ,the Miss Tourism World 2005- Africa witness Manwingi |
Miss Tourism Tanzania ,the Miss Tourism World 2005- Africa witness Manwingi |
Miss Tourism Tanzania ,the Miss Tourism World 2005- Africa witness Manwingi |
Hadija saidi alishinda Taji la Miss Utalii Tanzania 2013,
baada ya kuwashinda washiriki wengine 24 kutoka mikoa yote ya Tanzania, katika
fainali zaTaifa zilizo fanyika Tanga Mei 19, 2013. Hajija Saidi Juma Mswaga, mwanafunzi
wa Diploma ya Mahusiano ya Umma na Matangazo katika Chuo cha DSJ.
![]() |
MISS TOURISM TANZANIA 2013 |
TOP 5 MISS TOURISM TANZANIA 2013 |
Anawaomba
watanzania kumpa ushirikiano wa hali na mali ikiwemo sala na Dua katika
kufanikisha maandalizi, safari na kutwaa taji hilo la Dunia.
“ Kwakuwa nakwenda kuwakilisha Taifa, anaye shiriki sio
Hadija tena bali ni Tanzania, najua jukumu kubwa la kuifanya Tanzania kushinda ,
najua pia kazi niliyo nayo ya kutangaza Utalii na Utamaduni wa Tanzania na kulinda heshima ya Miss Utalii Tanzania , ya kushinda kila mwaka
na siyo kushindwa , nikifuata nyayo za walionitangulia. Naomba Dua na sala zenu
Friday, August 30, 2013
David Mwantika amrithi Kelvin Yondani Taifa Stars, kocha Kim Poulsen amuita kikosini
Na Boniface Wambura
KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen ameongeza kwenye kikosi chake beki
wa Azam, David Mwantika kwa ajili ya mechi ya Kombe la Dunia dhidi ya Gambia
itakayochezwa Septemba 7 mwaka huu jijini Banjul.
Mwantika
ameitwa kwenye kikosi hicho kuziba nafasi ya beki Kelvin Yondani ambaye
ni majeruhi.
Mbali na Yondani Stars ina wachezaji majeruhi watatu ambao kocha Kim amewaondoa kwenye
kikosi hicho ni waweze kushughulikia matibabu yao.
Wachezaji hao ni Athuman Idd 'Chuji' ,
Shomari Kapombe na John Bocco 'Adebayor'.
Taifa
Stars imeingia kambini jana (Agosti 29 mwaka huu) na imeanza mazoezi
leo jioni kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume.
Timu hiyo
inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager pia itakuwa ikifanya mazoezi
kwenye Uwanja wa Taifa.
TFF, AZAM MEDIA ZASAINI MKATABA WA BIL. 5.5/-
Na Boniface Wambura
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na kampuni ya Azam Media leo (Agosti
30 mwaka huu) wamesaini mkataba wa haki za kipekee za televisheni
(exclusive rights) utakaoiwezesha Azam TV kuonesha mechi za Ligi Kuu ya
Vodacom (VPL).
Mkataba
huo wa miaka mitatu wenye thamani y ash. 5,560,800,000 umesainiwa
kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais, Athuman
Nyamlani amesaini kwa niaba ya TFF wakati aliyesaini kwa upande wa Azam
Media ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo Thys Torrington.
Ligi
Kuu ya Tanzania sasa itakuwa ikipatikana kupitia kisimbuzi (decorder)
cha Azam TV kitakachokuwa na chaneli zaidi ya 50. Mechi hizo
zinatarajiwa kuoneshwa moja kwa moja wakati wowote kuanzia mwezi ujao.
Makamu
wa Rais wa TFF, Nyamlani amesema udhamini huo wa televisheni ni fursa
pana kwa klabu kwani zitaweza kujitangaza zaidi huku wachezaji nao
wakipata soko zaidi za mpira wa miguu.
Gervinho achekelea kuhama Arsenal

MSHAMBULIAJI wa Ivory Coast, Gervinho (26) amebainisha kwamba alifurahi sana kuondoka Arsenal.
Nyota huyo amesema alikuwa na maisha magumu London Kaskazini na kwamba ilipotokea ofa ya kuondoka aliichangamkia haraka.
Gervinho alishuka kiwango na akashindwa kuonyesha makali yake Arsenal baada ya kujiunga na klabu hiyo kwa paundi milioni 10.8 akitokea Lille mwaka 2011.
Alikamilisha uhamisho wake wa kutua Roma mapema katika kipindi hiki cha usajili chini ya kocha wake wa zamani wa Ufaransa, Rudi Garcia na amesema atatisha chini ya kocha huyo.
Nyota huyo aliyesajiliwa kwa paundi milioni 8 alisema: "Ilikuwa ni faraja kubwa kwangu kuchezea Arsenal, lakini baada ya miaka miwili ya kupanda na kushuka ilikuwa ni wakati mwafaka wa mabadiliko.
"(Arsene) Wenger, nadhani ni kocha mkubwa. Ni mtu ambaye namheshimu sana na nina furaha kubwa kupata fursa ya kucheza katika timu yake. Nadhani washambuliaji wanahitaji kuaminiwa na kocha wao na kupewa muda mwingi wa kucheza. Nilitamani nami iwe hivyo. Lakini ukurasa huo umepita mambo yamebadilika. Naweka akiliyangu yote Roma.
"Roma ni timu kubwa yenye kocha mkubwa. Sikujiuliza kukubali ofa yao.
"Daima nina mahusiano mazuri na Garcia - amekuwa akinijengea kujiamiani daima, na alikuwa ndiye kocha wa kwanza kunichezesha kwenye wingi.
"Nataka kuonyesha naweza kuisaidia timu. Siko katika hali nzuri kimwili kwa sasa, lakini Garcia ananifahamu vyema, nina kazi ya kufanya ili niwe fiti tena."
(Talksport)
Diamond nouma, amzawadia Mzee Gurumo gari...wengine mpo...!
Msanii mkongwe wa muziki wa dansi, Muhidin Gurumo akijaribu
gari dogo alilokabidhiwa na mwanamuziki wa bongo fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond ‘
kutokana na kutambua mchango wake baada ya kustaafu kazi ya muziki.
Show.
Gari alilozawadiwa mzee Gurumo.
STAA wa nyimbo za 'Kesho', 'Nataka Kulewa', 'Mawazo' na vingine, Naseeb Abdul ameonyesha mfano kwa wadau wa muziki nchini baada ya kumzawadiwa gari mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansi aliyetangaza kustaafu, Muhidini Gurumo.
Diamond alimkabidhi Gurumo gari hilo kuonyesha kujali na kuthamini mchango wa mwanamuziki huyo, baada ya hivi karibuni kunukuliwa 'akilia' kwamba kwa miaka zaidi ya 50 ya kuwa mwanamuziki anastaafu akiwa hana hata baiskeli.
Alichokifanya Diamond ni jambo la kupongezwa na kuigwa na wadau wengine wa muziki kama alivyowahi kunukuliwa mwenyewe (Gurumo) kwamba angependa ale jasho na kupewa pongezi zake angali hai badala ya watu kumsubiri afe ndipo watu wajitokeze kumwagia sifa na kujifanya kumuenzi wakati akiwa hao walimtelekeza.
MICHARAZO inakupa pongezi Diamond na tunawaomba wengine wamsadie mkongwe huyo ambaye amestaafu siyo kwa sababu ya kuishiwa kimuziki, bali hali yake ya kiafya akisumbuliwa na maradhi na wenye kutaka kumchangia watume fedha kwa njia ya TiGO Pesa katika simu yake ya mkononi 0655-401383.
Thursday, August 29, 2013
Frank Ribery ndiye Mchezaji Bora Barani Ulaya awabwaga Messi na Ronaldo
![]() |
Frank Ribery ambaye kiimani ni Muislam akiomba dua kabla ya kuanza pambano la soka la timu yake ya Bayern Munich |
NYOTA wa Kifaransa anayeichezea klabu ya Bayern Munich, Frank Ribery amewagaragaza wakali wa Hispania, Lionel Messi wa Barcelona na Cristiano Ronaldo kwa kunyakua tuzo ya Mchezaji Bora wa Ulaya 2012-2013.
Mkali huyo aliyeisaidia Bayern Munich kunyakua taji la Ligi ya Mabingwa ya Ulaya na mengine mawili ya Ligi ya Ujerumani alitangazwa kunyakua tuzo hiyo leo barani humo.
Ribery amenyakua tuzo hiyo akimpokea Iniesta wa Barcelona aliyenyakua msimu uliopita akitanguliwa na Messi aliyetwaa mwaka 2010-2011.
Nafasi ya pili katika kimyang'anyiro hicho ilienda kwa Messim kisha Ronaldo aliyeshina nafasi ya tatu, ingawa hjakuweza kuhudhuria sherehe hizo zilizoenda sambamba na kutangazwa kwa makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu wa 2013-2014.
Rais Kikwete amteua Kamishna Mkuu Idara ya Uhamiaji
![]() |
Rais Jakaya Kikwete |
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
amemteua Ndugu Sylvester Ambokile Mwakinyule kuwa Kamishna Mkuu, Idara
ya Uhamiaji.
Taarifa
iliyotolewa leo, Alhamisi, 29 Agosti, 2013 mjini Dar es Salaam na
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Y. Sefue inasema kuwa uteuzi huo
umeanza jana, Agosti 28, mwaka huu, 2013.
Ndugu Mwakinyule anachukua nafasi ya Ndugu Magnus Ulungi ambaye atapangiwa kazi nyingine.
Ndugu Mwakinyule anachukua nafasi ya Ndugu Magnus Ulungi ambaye atapangiwa kazi nyingine.
Kabla
ya uteuzi wake, Ndugu Sylvester Ambokile Mwakinyule, alikuwa Naibu
Kamishna wa Uhamiaji na Mwambata wa Uhamiaji katika Ubalozi wa Tanzania,
London, Uingereza
Rais pia amemteua Dkt. Nyamajeje Calleb Weggoro kuwa Msaidizi wa Rais, Masuala ya Ushirikiano wa Kikanda.
Taarifa
iliyotolewa leo, Alhamisi, 29 Agosti, 2013 mjini Dar es Salaam na
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Y. Sefue inasema kuwa uteuzi huo
umeanza jana Agosti 28, mwaka huu, 2013.
Kabla
ya uteuzi huu, Dkt. Nyamajeje Calleb Weggoro alikuwa Mkurugenzi wa
Sekta za Uzalishaji (Productive Sectors) katika Sekretarieti ya Jumuiya
ya Afrika Mashariki (EAC).
Subscribe to:
Posts (Atom)