STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, March 18, 2014

Ruvu Stars waachia tatu, wajipanga kurekodi video

Roggert Hegga enzi akiwa Twnaga Pepeta
BENDI mpya wa muziki wa dansi ya Ruvu Stars, imekamilisha kurekodi nyimbo zao tatu mpya na tayari wameanza kuzisambaza kwenye vituo vya redio kwa ajili ya kuchezwa hewani.
Mmoja wa viongozi na muimbaji wa bendi hiyo yenye maskani yake Mlandizi, Pwani Rogert Hegga 'Catapillar', alisema wamemaliza kurekodi nyimbo hizo katikati ya wiki iliyopita na tayari baadhi ya vituoi zimeanza kuzirushwa hewani wakijiandaa kurekodi video zake.
Hegga alizitaja nyimbo zilizorekodiwa ambazo ndizo zinazoitambulisha bendi hiyo kwa mashabiki wa muziki wakiwa wanataka kurejesha enzi za bendi za majeshi kutamba nchini ni pamoja na 'Network Love' utunzi wa  Mhina Panduka 'Baba Danny' a.k.a Toto Tundu, 'Jua Kali' wa Kuziwa Kalala na 'Spirit' ambao ni utunzi wake (Hegga).
"Tumeshakamilisha kurekodi nyimbo zetu za utambulisho na tumeshasambaza na baadhi ya vituo zimeanza kuzicheza," alisema Hegga.
Mtunzi na muimbaji huyo wa zamani wa bendi kadhaa maarufu nchini ikiwamo ya African Stars, Mchinga Sound, G8 Wana Timbatimba na Extra Bongo, alisema vibao hivyo ni mwanzo wa maandalizi ya kupakua albamu yao na kuwataka mashabiki wasubiri kupata uhondo zaidi.
"Mashabiki wajiandae tu kupata burudani, nyimbo hizi zitaleta mapinduzi makubwa katika muziki wa dansi kwani zimeenda shule na studio tuliyorekodia ni bab'kubwa," alisema.
Baadhi ya wanamuziki wanaounda bendi hiyo inayomilikiwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ni Khadija Mnoga 'Kimobitel', Hamis Amigolas, Hegga, Victor Mkambi, Mhina Panduka na wengine waliotoka bendi kadhaa za jijini Dar es Salaam.

Rooney alizwa na mwaka wa shetani Man Utd

WAKATI Kocha wa Manchester United, David Moyes akikata tamaa kwa timu yake kumaliza nne bora katika Ligi Kuu England msimu huu, mshambuliaji wa timu hiyo, Wayne Rooney amesema kipigo cha mabao 3-0 walichokipata nyumbani dhidi ya Liverpool ndicho kibaya zaidi kwenye kipindi chake cha soka.
Steven Gerrard alifunga mara mbili kwa njia ya penalti kabla ya Luis Suarez kutupia la tatu huku Nemanja Vidic akitolewa nje kwa kadi nyekundu.
"Ulikuwa wakati mgumu. Ni moja kati ya siku mbaya zaidi kutokea kwangu katika maisha yangu kisoka. Liverpool inastahili pongezi kwa kucheza vizuri," Rooney aliiambia MUTV.

Jennifer Mgendi ana Shelina na Bonny Mwaitege, Bahati Bukuku

BAADA ya kitambo kirefu tangu alipoachia filamu yake ya mwisho ya 'Chai Moto' muimbaji mahiri wa muziki wa Injili nchini, Jennfer Mgendi anatarajiwa kuibuka na kazi mpya iitwayo 'Shelina'.
Akizungumza na MICHARAZO, Mgendi alisema filamu hiyo itakayozungumzia changamoto wanazopata watoto wa kike na jinsi imani ya Mungu inavyoweza kuleta ufumbuzi wa changamoto hizo itawashirikisha wasanii mbalimbali wa filamu na muziki wa Injili nchini.
Mgendi, ambaye anaendelea kutamba kwa sasa na albamu yake mpya ya 'Hongera Yesu' alisema miongoni mwa wasanii watakayoicheza filamu hiyo inayotarajiwa kuzinduliwa rasmi Juni mwaka huu ni pamoja na Bahati Bukuku, Bonny Mwaitege, Bibi Esther, Christina Matai na wengineo.
"Nipo katiuka hatua ya mwisho kabla ya kuanza kushuti ila itafahamika kwa jina la 'Shelina' na itawashirikisha wasanii kadhaa nyota wa filamu na muziki wa Injili nchini, akiwamo Bahati Bukuku, Boniface Mwaitege," alisema.
Kabla ya filamu hiyo, Mgendi alishatoa filamu za 'Joto la Roho', 'Pigo la Faraja', 'Teke la Mama' na 'Chai Moto' inayoendelea kutamba kwa sasa sokoni

#6 waula maboresho Taifa Stars

JOPO la wang’amua vipaji limetangaza majina ya wachezaji 36 waliopataikana katika mchakato wa maboresho ya timu mpya ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ulioshirikisha mechi za mikoa yote ya Bara na Visiwani.
Kaimu Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Salum Madadi amesema jopo hilo liling’amua vipaji 143 katika mchakato, lakini waliochukuliwa kwa sasa ni hao 36 tu.
Amewataja wachezaji waliochaguliwa katika mchakato huo kwa upande wa makipa ni Abdulaziz Khatib Haji (Mjini Magharibi), Abubakar Abbas Ibrahim (Tanga), Benedicto Tinoko Mlekwa (Mara) na Mtindi Kheri Ali (Kaskazini Unguja).
Hawa sasa basi; Kikosi cha mwisho cha Taifa Stars kilichocheza mchezo wa kirafiki nchini Namibia Machi 5, mwaka huu. Sasa zinakuja sura mpya kabisa kuunda timu hiyo.
Kwa upande wa mabeki wa pembeni waliochaguliwa katika mchakato huo ambao upo chini ya udhamini wa Kilimanjaro Premium Lager ni Edward Peter Mayunga (Kaskazini Pemba), Hussein Moshi (Tabora), Omari Kindamba (Temeke) na Shiraz Abdallah (Ilala).
Mabeki wa kati ni Abbas Ali Haji (Kaskazini Unguja), Ancy Abdon (Kagera), Emma Namwamba (Temeke), Hussein Juma Akilimali (Njombe), Joram Nasson (Iringa), Kayombo Silvanus Henrico (Ilala), Miraji Maka (Mwanza),  Ramadhan Ame Ramadhan (Kusini Unguja) na Said Juma Ali (Mjini Magharibi).
Viungo wapo Abubakar Mohamed Ally (Kusini Unguja), Hashim Ramadhan Magoma (Shinyanga), Juma Said Jega (Lindi), Mtenje Alban Juma (Tanga), Ryna Mgonyike (Temeke) na Yusuf Mpilipili (Temeke).
Washambuliaji ni Abdallah Kagumbwa (Temeke), Abrahman Othman Ally (Mjini Magharibi), Athanas Fabian Bayagala (Mbeya), Athanas Mdamu (Mwanza), Ayubu Hashim Lipati (Ilala), Chunga Said (Manyara), Mbwana Mshindo Mussa (Tanga), Michael David Mlekwa (Lindi), Mohamed Seif Said (Kusini Pemba), Omar Athuman Nyenje (Mtwara), Paul Michael Bundala (Ilala), Ramadhan Kapalamoto (Kinondoni) na Roman Nyapunda (Temeke).
Amesema wastani wa umri wa wachezaji hao ambao watafanyiwa vipimo vya afya Machi 19 na 20 mwaka huu kabla ya kuingia kambini Machi 21 mwaka huu, huko Tukuyu mkoani Mbeya ni miaka 21.
Timu hiyo itakuwa chini ya Madadi akisaidiwa na makocha Hafidh Badru, Salum Mayanga na Patrick Mwangata. Aprili 13 mwaka huu utafanyika mchujo ili kupata wachezaji wa mwisho watakaoungana na wale wa Taifa Stars watakaoingia kambini Aprili 22 mwaka huu.
Taifa Stars inatarajiwa kucheza mechi ya kirafiki mapema mwezi Mei mwaka huu ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mechi za mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika (AFCON) zitakazofanyika mwakani nchini Morocco.

Monday, March 17, 2014

Si Uchawi! Kiatu chako kinaweza kukujulisha umri wako!!


EBU jaribu mwenyewe uone kisha nicheki kwenye micharazomitupu@yahoo.com au wakuzataboy@yahoo.com
1: Andika namba ya kiatu chako.

2: Zidisha kwa5.

3: Jumlisha 50

4: Zidisha kwa 20 ...

5: Jumlisha 1013 

6: Toa mwaka uliozaliwa....

7: Namba ya kwanza ni size ya kiatu, na namba mbili za mwisho ni miaka yako.

Waliopenya maboresho Taifa Stars kutajwa leo

Rais wa TFF, Jamal Malinzi
MCHAKATO wa ung’amuzi wa vipaji kwa ajili ya maboresho ya timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars, ulioshirikisha wang’amuzi wa vipaji zaidi ya 40 umekamilika jana na majina ya nyota hao yataanikwa kesho Jumatatu.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura, wachezaji hao watafanyiwa vipimo vya afya kabla ya kuingia kambini Tukuyu, Mbeya na watakaoingia kambini ni wale watakaokuwa wamefaulu vipimo.
Wang’amuzi wa vipaji waliokuwa Lushoto ni Abdul Mingange, Ayoub Nyenzi, Boniface Pawasa, Charles Mkwassa, Dan Korosso, Dk. Mshindo Msolla, Edward Hiza, Elly Mzozo, Hafidh Badru, Hamimu Mawazo, John Simkoko, Jonas Tiboroha, Juma Mgunda na Juma Mwambusi.
Kanali mstaafu Idd Kipingu, Kenny Mwaisabula, Kidao Wilfred, Madaraka Bendera, Madaraka Selemani, Mbarouk Nyenga, Mohamed Ally, Mussa Kissoky, Nicholas Mihayo, Pelegrinius Rutayuga, Peter Mhina, Salum Mayanga, Salvatory Edward, Salum Madadi, Sebastian Nkoma, Sekilojo Chambua, Selemani Jabir na Shabani Ramadhan.
Wengine ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho hilo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi, Kidao Wilfred na Ayoub Nyenzi ambaye mbali ya kuwa  mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho hilo, pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Vijana.
Yumo pia Kaimu Mkurugenzi wa Ufundi, Salum Madadi na Mshauri wa Rais (Ufundi), Pelegrinius Rutayuga.
Mkakati huo umebuniwa na TFF kwa lengo la kupata nyota wa kujumuishwa katika kikosi cha sasa cha Stars inayokabliwa na kampeni ya kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa Afrika (AFCON), zitakazochezwa mwakani nchini Morocco.

Tusiruhusu ushoga nchini ni kama kumbeep Mungu-Sheikh aonya


http://bloggerimports.files.wordpress.com/2008/12/img_2954-raisidd.jpg?w=640
Sheikh Mohammed Muhenga
SERIKALI imeombwa kufuata nyayo za serikali ya Uganda chini ya Rais Yoweri Museveni kwa kuktaa kuruhusu ushoga.
Serikali imeombwa kufuata nyayo za serikali ya Uganda chini ya Rais Yoweri Museveni kwa kukataa kuruhusu ushoga licha ya kuziudhi nchi za magharibi zinazokingia kifua vitendo hivyo.
Ombi hilo limetolewa na Imamu wa Msikiti wa Mwembechai, Sheikh Mohammed Muhenga, alipokuwa akiwahutubia waumini kabla ya swala ya Ijumaa iliyoswaliwa msikiti hapo, jijini Dar es Salaam.
Imamu Muhenga alisema kitendo cha Watanzania kunyamazia na kukumbatia matendo maovu yanayomchukiza Mungu vinaweza kuzua balaa kwa taifa.
"Tushirikiane kukemea maovu, tusinyamazie matendo yanayomchukiza Mungu kwani hakuna anayeweza kuhimili ghadhabu za Mungu akiamua kutuadhibu,"alisema .
Sheikh huyo alisema vitendo vya ulevi, biashara ya watu kujiuza, ujambazi na matendo mengine kwa kisingizio cha kukabiliana na hali ngumu ya maisha vinapaswa kuepukwa kwa nguvu zote.
"Huku ni sawa na kumbeep Mungu, je akiamua kutupigia tupo tayari kuhimili ghadhabu yake, tukemee maovu na kukemea kwani Mtume Muhammad (Sallallah Aley Wasalam) anasema miongoni mwa dalili 10 za kiama ni umma wake kugeuza pombe kuwa chai, watu kurejea enzi za Kaum Lut," alisema.
Sheikh alisema matendo vya ushoga na maovu mengine ni kuvuka mipaka kwa wanadamu ya uumbaji na humchukiza Mungu, hivyo ni wajibu wa kila mtu kukemea na kuyakataa matendo hayo.
Hivi karibuni Uganda ilipitisha sheria kali dhidi ya vitendo vya ushoga na kukera nchi ya Marekani na washirika kwake ambao wameruhusu vitendo hivyo katika nchi zao licha ya kwenda kinyume na mafundisho ya kidini.

Maafa! Nane wafa mgodini wakichimba dhahabu

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEheVO-yFu1eXU8rBz8T2or-Ju6EDw0WANzohJuqwB-gznjg64LLdt457Xp3Hknvz8ecoigpuV9P6NtgqOga42ZkUv0ap58cBWwGAEyWC2RU0eLeNz3Itb98lPeBA-njALSgerp4-BhmQsOR/s1600/Geita+gold+mine+1.jpg
Picha haihusiani na habari, ila wanaoonekana ni Vijana wakiwa machimboni
WATU wanane wamefariki dunia na moja kunusurika katika machimbo  madogo ya dhahabu yaliyopo vijiji cha Kalole na Nyangalaya kata ya Lunguya  wilayani Kahama, Shinyanga baada ya kuangukiwa na vifusi.
Ofisa Mtendaji wa kijiji cha Kalole, Furaha Mashamba, alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 5:00 usiku wakati wachimbaji hao wakiendelea kuchimba dhahabu.
Alisema katika matukio hayo, watu saba walikufa katika machimbo ya kijiji cha Kalole na mmoja   machimbo ya Nyangalata.
Mashamba alisema kuwa baada ya tukio hilo, wakazi wa kijiji hicho walipewa taarifa na kwenda eneo la tukio kujaribu kuwaokoa, lakini ilishindikana.
Hata hivyo, kwa mujibu wa mtendaji huyo, mmoja wa wachimbaji aliokolewa akiwa hai.
Aliwataja waliofariki ambao ni wakazi wa kijiji cha Kalole kuwa ni Mwadogo Kibasi Kiaka (26), Juma Malingaya (30), Charles Iheyolo (21), Roma Masolwa (26), Juma John (33), Paul James (24), Ngaleba Kacheyekele (24) na Daudi John wa kijiji cha Nyangalata Alimtaja aliyenusurika kuwa ni Michael Pius (43) mkazi wa Morogoro.
Ofisa Mtendaji huyo alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mashimo hayo kutokuwa na usalama wa kutosha na maji kuingia kutokana na mvua za masika zinazoendelea kunyesha wilayani Kahama.
Kwa upande wake, Ofisa Madini wilayani Kahama, Amir Chande, alisema kuwa machimbo ya kijiji cha Kalole yalishafungwa muda mrefu, lakini wachimbaji wamekuwa wakiyavamia kuendelea na uchimbaji kinyemela.
Chande alitoa agizo kwa wachimbaji ambao bado wapo eneo hilo kusitisha kazi hiyo haraka hadi hapo serikali itakapotoa maelekezo mengine.
“Mnaoendelea kuchimba mpo hapa kimakosa na kwa sababu hakuna mwenye leseni hapa ya uchimbaji wa madini, ni makosa kufanya kazi hii ya uchimbaji na kuanzia sasa machimbo  tunayafunga kwa usalama wenu,” alisema Chande.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Evarist Mangala, alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kueleza kuwa miili ya wachimbaji hao imetambuliwa na kuchukuliwa na ndugu zao kwa mazishi.
CHANZO: NIPASHE

PSG haishikiki Ufaransa, Zlatan nouma!



Cruising: Ibrahimovic scored twice in the first-half to restore PSG's eight point lead at the top of the table
Oyooooooo! Zlatan akishangilia bao
PSG inaelekea kutetea taji lake la ubingwa wa Ligue 1 nchini Ufaransa baada ya usiku wa jana kupata ushindi wa mabao 2-0 nyumbani dhidi ya St Etienne.
Mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic 'Acadabladabla' ndiye aliyefunga mabao hayo na kuipa PSG ushindi wa saba mfululizo kwenye mashindano yote.
Wapinzani wao wa karibu, Monaco nao jana waliendelea kupata ushindi na kuwafukuza wapinzani wao kwa kuizabua Lyon kwa mabao 3-2.
PSG inayotetea taji la ligi hiyo inaendelea kuongoza msimamo kwa tofauti ya pointi nane ikiwa na pointi 70 huku Monaco wakiwafuata kwa mbali wakiwa na 62.

Hii ilitokea Kitonga baada ajali ya malori mawili


Baadhi ya abiria wa kutoka sehemu mabalimbali wakisubiri lori lililoziba barabara kuondolewa baada ya kupata ajali ya kugongana na lori jingine kwenye mlima Kitongo. Ajali hiyo imesababisha magari mengi kuweka kambi kwa muda wa zaidi ya saa nne.

Lori likiwa limetumbukia kwenye korongo mlimani kitonga

Lori la mafuta lililopo upande wa kulia na lori la mizigo lililopo upande wa kulia yaligongana na kuziba barabara kwenye mlima kitonga na kusababisa magari mengine kukwama kwa zaidi ya saa manne



Jana tulilazimika kufanya utalii ndani ya mlima kitonga baada ya kukwama kwa zaidi ya masaa manne

Sunday, March 16, 2014

Yametimia! CCM yaibuka kidedea Jimbo la Kalenga, Chadema hoi


Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kalenga kwa tiketi ya chama cha CCM,Ndugu Godfrey Mgimwa akiwa amebebwa juu na wafuasi wa chama hicho usiku huu,kwenye Ofisi za CCM mkoa,huku wakisubiri matokeo rasmi kutangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi muda wowote kuanzia sasa.
TOSA no.1
CCM 98 ,Chadema 20, CHAUSTA 0
Ipamba no2. CCM 104, Chadema 10,CHAUSTA 0
Isakulilo CCM 83,Chadema 8,CHAUSTA 0


Kilindi A CCM 69 ,Chadema 23, CHAUSTA 0
Ofisi ya Kijiji(Kilindi) CCM 117, Chadema 53, CHAUSTA0
Zahanati CCM 117,Chadema 67, CHAUSTA 1
Ifunda
Kivalali A CCM 99 Chadema 19 CHAUSTA 0
Kivalali B CCM 109 Chadema 14, CHAUSTA 1
Muwimbi CCM164, Chadema 22 CHAUSTA 0


Mahanzi CCM 130 Chadema 46 CHAUSTA 0
Ikungwe A CCM 131 Chadema 23 CHAUSTA 0
Ikungwe B CCM 216 Chadema 13 CHAUSTA 0
Magunga CCM 184 ,Chadema 4 CHAUSTA1
Wasa CCM 149,Chadema 15 CHAUSTA 0
Usengelidete CCM 260,Chadema 46,CHAUSTA O

KAMANDA WA UVCC MKOA WA IRINGA SALIM ASAS AKICHEZA KWA SHANGWE VIWANJA VYA CCM MKOA KUSHEREKEA USHINDO WA CCM KALENGA

Arsenal yaibutua Spurs yaendelea kuibana Liver

Arsenal's Tomas Rosicky after scoring against Tottenham
Kitu! Arsenal ikijipatia bao pekee lililowarejesha kwenye nafasi ya tatu


BAO la dakika ya pili lililofungwa na Romas Rosicky liliiwezesha Arsenal kuibuka na ushindi muhimu ugenini dhidi ya Tottenham Hotspur na kuendelea kufufua matumaini ya kumaliza ukame wa mataji iliyonayo kwa muda mrefu.
Tottenham ambayo imetoka kuchezea kichapo cha aibu cha mabao 3-1 katikati ya wiki kwenye Ligi ya Europa dhidi ya Benfica, licha ya kucharuka kusaka bao la kusawazisha walijikuta wakimaliza dakika 45 za kwanza wakiwa nyuma.
Hata pamoja na kufanya mabadiliko ya wachezaji, Spurs ilishindwa kulipa kisasi kwa wapinzani wao waliowafunga pia katika mechi ya mkono wa kwanza walipowafuata Emirates na kujikuta wakiendelea kusalia kwenye nafasi ya tano wakiwa na pointi 53, huku Arsenal ikichupa hadi nafasi ya tatu nyuma ya Liverpool ilitoka kuitoa nishai Manchester Utd ikiwa kwao.
Timu hizo mbili zina pointi 62 ila zinatofautiana mabao ya kufungwa na kufungwa nyuma ya Chelsea wanaoongoza wakiwa na pointi 66, Manchester City walikuwa wakishika nafasi ya pili mpaka mchana wa leo imerejea kwenye nafasi yake ya nne ikiwa na pointi 60.

CCM yaelekea kunyakua kiti cha Kalenga



TUPO Live Kutoka Kalenga Kunakofanyika Uchaguzi wa Mbunge wa Jimbo hilo hii leo.
Matokeo ya AWALI nikama Ifuatavyo 
KATA YA IFUNDA Ambapo Chadema ilikuwa hai kiasi chake Matokeo niliyopokea haya hapa.
CCM kura 451,CHADEMA 261 NA CHAUSTA 2 JIMBO LA KALENGA LINA KATA 13,JUMLA YA KATA 11 ZOTE CCM WAMESHINDA BADO KATA 2 TU,MATOKEO HAYA NI LIVE KUTOKA KALENGA HAPA
MCHANGANUO MBALI MBALI WA MATOKEO
 Kata ya nzi kituo cha tanroad 
CCM 142, CDM 26, CHAUSTA  1.KITUO CHA OFISINI A  CCM 116  CDM 2, OFISINI B  CCM 112, CDM 34, CHAUSTA 1. KITUO CHA NZI SHULE  CCM 137, CDM 37, CHAUSTA3
DJ SEK

Rais JK aipa Simba Mil 30, Rage hagombei Mei 4

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEillaEEFMRuqEODNSQRGBkBteyU-tWto8t7FPCWBeEN2r1d-xO2jNixNWM-VkoRqBJeiw4CrRDXErKqSwhUIuFSAyqmjeODBu4YTaIGEn7lwje6TcZZxFdbtuNMG6uFDg0o8fLktGlHx04/s1600/IMG_7676.jpg

RAIS Jakaya Kikwete ameipa klabu ya Simba Sh. Milioni 30 ili washughulikie hati ya kiwanja chao kilichopo maeneo ya Bunju B, Dar es Salaam. Akizungumza kwenye Mkutano maalum wa marekebisho ya Katiba ya klabu hiyo uliofanyika asubuhi ya leo Bwalo la Maofisa wa Polisi, Oysterbay mjini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage alisema pamoja na mchango huo, Rais JK aliwatakia heri katika mkutano huo huku akimkabidhi hundi ya fedha hizo kwa ajili ya upatikanaji wa  hati hiyo.  
“Tunamshukuru Rais kwa msaada wake ameonyesha yeye ni mwanamichezo wa timu zote hivyo huu ni ushindi wa Simba na sio wa Rage,”alisema
Alisema kuwa Jumamosi ijayo atapitisha greda kwa ajili ya kusafisha Uwanja huo ili wachezaji waanze mazoezi kwenye Uwanja wao.
Rage alisema kuwa fedha hizo watazitumia vizuri ikiwa sambamba na kupunguza deni la wizara ya Ardhi wanaowadaiwa Sh41 Milioni kati ya Sh92 walizokuwa wanadaiwa.
Simba iliuziwa Kitalu 226 namba 1. Bunju mwaka 2006, uongozi wa Simba ulilipa Sh 50 Milioni Desemba 29, 2011.
Katika hatua hiyo hiyo, Simba imefanya marekebisho kwenye ibara ya 26(5 )sifa za wagombea ambapo kipengele hicho awali kilikuwa kinasomeka “Asiwe aliyewahi kutiwa hatiani kwa kosa la jinai kwa kuhukumiwa kifungo.
Kipengele hicho sasa kinasomeka “Asiwe ametiwa hatiani kwa kifungo cha zaidi ya miezi sita bila mbadala wa adhabu. Na endapo ametiwa hatihani kwa kifungo cha zaidi ya miezi sita, awe amemaliza muda wa miaka 5, tangu kuisha kwa kifungo husika bila kitiwa hatiana kwa jingine lolote la jinai.
Wanachama hao hao wamegoma kukipitisha ibara ya 26 (9) Mgombea awe ametimiza angalau miaka mitatu ya uanachama. Ambapo sasa kinasomeka angalau awe na mwaka mmoja wa wanachama.
Pia ibara ya 25 (8) (iii) wajumbe watano wa kamati ya utendaji. Mwenyekiti aruhusiwe kuteuwa wajumbe wengine watano wa kamati ya utendaji ambao anaweza kubadilisha kwa kadri anavyoona inafaa.wajumbe hawa wa kuteuliwa wanatakiwa kuwa na sifa zilizile wanazotakiwa kuwa nazo wajumbe wa kuchaguliwa na wanachama.
Aidha Rage amesisitiza kuwa hana mpango wa kugombea uongozi kwenye uchaguzi mkuu ujao wa klabu hiyo utakaofanyika Mei 4.

Liverpool yawachinja Mashetani Wekundu Old Trafford

Steven Gerrard
KOCHA David Moyes ameendelea kuvunja rekodi za Manchester Utd baada ya Liverpool kupata penati mbili kwenye uwanja wa Old Trafford na kuifumua Mashetani Wekundu kwa mabao 3-0 katika mfululizo wa Ligi Kuu ya England na kuchupa hadi nafasi ya pili.
Penati hizo za vipindi viwili vimeifanya Manchester Utd kubaki kwenye nafasi ya 7 ikiwa na pointi 48 na Liverpool kufikisha pointi 62 na kuiengua Manchester City yenye pointi 60.
Mikkwaju miwili ya penati ya dakika ya 34 ya kipindi na jingine la dakika ya 46 kupitia nahodha Steve Gerrard na bao jingine la dakika ya 84 la Luiz Suarez lilitosha kumnyamazisha Moyes na vijana wake nyumbani kwa mara nyingine.
Penati ya kwanza ilitokana na Raphael da Silva kuunawa mpira  kabla ya Phil Jones alimvamia na kumuangusha Joe Allen wa Liverpool na kumsukuma na penati hiyo kumwamisha dakika moja baada ya kuanza kwa kipindi cha pili.
Liverpool ilipata penati nyingine ya tatu na Gerrard lakini mkwaju wake ukagonga mwamba na kurejea uwanjani kabla ya Luiz kuja kumalizia shuti la Daniel Sturridge baada ya kuzamisha bao la tatu lililoipa Liverpool ushindi mnono kuelekea kwenye mbio za ubingwa wa England.
Dakika chache baadaye  Arsenal itakuwa uwanja wa White Hartlane kuumana na mahasimu wao wa London Kaskazini, Tottenham Hotspur.