STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, June 23, 2013

Miaka 13 ya Kikosi ilikuwa noumaa, Kalapina afunika, Chid ndani ya nyumba


 Chid Benz akikonga nyoyo za mashabiki wake wakati wa shoo ya Kikosi cha Mizinga kutimiza miaka 13 iliyofanyika katika ukumbi wa New Msasani jijini Dar es salaam. (Picha zote na Habari Mseto Blog).
 Chid Benz
 Fukuda akichana mistari
 Katibu wa CUF, Julius Mtatiro ambaye alikuwa mgeni rasmi  akizungumza wakati wa shoo maalumkundi la muziki wa Hip Hop la Kikosi cha Mizinga kutimiza miaka 13.
Baadhi ya watu waliotoa mchango mkuwa kwa wasanii wa Kikosi cha Mizinga walipewa vyeti, hapa mwandishi Joseph Zablon akionesha cheti chake baada ya kukabidhiwa ba mgeni rasmi. 
 Mwakilishi wa Clouds Radio akipokea cheti.
   
 Kala Pina 'Nabii Koko' akitumbuiza
 
 Afande Sele akipagawisha  mashabiki.


Friday, June 21, 2013

Japhet Kaseba, Mada Maugo kumaliza ubishi Septemba 7

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgu0krDXi4TPIp2ayBWZQ0W7CMehUiojc_Tx_djN0BQ1pI4T3tDZbyezuWm2US0FUya9KGDcXYXpPr8gwdU6E4ZU5xJIBui92XNQKNTNY8uM2N_uaDKTFQdnMRR2UoFlKSqqkQwTZr3JfzE/s1600/7.JPG
Mada Maugo (kushoto) akichuana na Kaseba katika pambano lao la kwanza April 16, 2011
MABONDIA machachari wa ngumi za kulipwa wenye upinzani mkubwa nchini, Japhet Kaseba 'Champion' na Mada Maugo 'King maugo Jr' wanatarajiwa kuvaana Septemba 7 mwaka huu katika pambano la kumaliza ubishi baina yao litakalofanyika jijini Dar es Salaam.
Wanamasumbwi hao walipambana mara ya mwisho April 16, 2011 na Maugo kuibuka kidedea kwa TKO  ya raundi ya saba baada ya wapambe wa Kaseba kuingia ulingoni na kumvua bondia wao glovu ikiwa bado raundi moja kabla ya pambano hilo kumalizika.
Akizungumza na MICHARAZO hivi punde, Kaseba alisema pambano hilo litakuwa la kuwania taji lililo wazi la WBF kwenye ukumbi kati ya Diamond Jubilee au PTA na litasimamiwa na Shirikisho la Ngumi za Kulipwa Tanzania (PST).
Kaseba alisema anaamini pambano hilo ndilo litakalomaliza ubishi kati yake na Maugo baada ya kutoridhishwa na ushindi aliopewa walipoumana mara ya mwisho.
Bondia huyo aliyetoka kumnyuka Mmalawi, Rasco Simwanza kwa KO ametamba kuibuka na ushindi mbele ya Maugo ambaye kwa sasa yupo katika maandalizi ya kwenda Russia kuzipiga na mwenyeji wake Movsur Yusupov Julai 27 kwa sababu amebaini ili kumaliza ubishi ni lazima ashinde kwa KO kitu alichoanza kutumia sasa katika mapambano yake.
"Nimebaini ukimpiga mtu kwa KO hakuna malalamiko tofauti na kumaliza pambano na kushinda kwa pointi, hivuo Maugo ajiandae kukumbana na KO ya hatari kwa vile kiu yangu ni kutwaa ubingwa wa dunia kama nilivyofanya kwenye Kick Boxing," alisema Kaseba.
Maugo mwenyewe hakupatikana kueleza tambo hizo za mpinzani wake, ingawa imefahamika kuwa tayari kila kitu juu ya pambano hilo ikiwemo kusainishwa kwa mikataba kumeshafanyika.

Mbunge wa NCCR-Mageuzi ashambuliwa, wawili washikiliwa na Polisi

Mbunge wa Kasulu Mjini (NCCR), Moses Machali akiwa amelazwa wodini.
Akisiendelea kupata nafuu baada kushambuliwa.

Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma,David Misime akizungumza na waandishi wa habari mjini humo jana kuhusu tukio la  Mbunge wa Kasulu Mjini (NCCR) Moses Machali kuvamiwa na vibaka eneo la Area E juzi usiku. 
 

Na. Jeshi la Polisi Dodoma.
DODOMA IJUMAA JUNI 21, 2013.  Jeshi la Polisi Mkoa Dodoma linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kumvamia na kumshambulia Mheshimiwa MOSES S/O MACHALI, miaka 31, Muha, Mbunge wa Kasulu Mjini kupitia NCCR – Mageuzi wakati anaelekea nyumbani kwake
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Bw. David. A. Misime  alisema Tukio hilo limetokea tarehe 20/06/2013 majira ya 19.00 hrs  katika eneo la Area ‘E’ katika Manispaa ya Dodoma
alikutana na vijana wanne (4) walikouwa amesimama katikati ya barabara akapiga honi lakini hawakupisha. Aliamua kuwauliza “Jamani mnasimama katikati ya barabara si nitawagonga?” Nao wakamjibu: “Wewe si unajifanya mtto wa Mbunge, tutakupiga sasa”. Alisisitiza Kamanda Misime
Kamanda Misime alisema Mheshimiwa alipojaribu kupita vijana hao walipiga gari lake. kitu ambacho kilimfanya  ashuke ili atazame kama gari hilo limepata uharibifu.wowote, ndipo vijana hao wakaanza kumshambulia kwa ngumi na mateke huku naye akijitahidi kujihami.
Hata hivyo Bw.Misime alisema,  walitokea vijana wawili (2) na kumsaidia. Mheshimiwa mbunge ambapo kijana mmoja kati ya waliokuwa wanamshambulia Mheshimiwa Machali ‘alimng’ata’ mgongoni kijana aliyekuwa anamsaidia Mheshimiwa Mbunge.
Bw. Misime alisema Watuhumiwa baada ya kuona wamezidiwa nguvu walitimua mbio. Ambapo pia Mheshimiwa Machali aligundua kuwa simu yake ya mkononi wameondoka nayo vijana hao.
Kamanda David. A. Misime alisema jeshi la Polisi mkoani Dodoma lilifanya  Msako mkali ulifanyika  usiku wa manane ambapo watuhumiwa wawili (2) walikamatwa ambao aliwataja kuwa ni JEREMIA  LAWRENT MKUDE@ JERRY, Miaka 18, Mkaguru Mkazi wa Chaduru, Manispaa ya Dodoma. aliyekutwa akiwa na jeraha usoni alilopata wakati anapambana na Mheshimiwa Mbunge na vijana waliokuwa wanamsaidia.
Kamanda huyo wa Polisi Mkoa wa Dododoma alimtaja mtuhumiwa mwingine anayeshikiliwa na jeshi la polisi kuwa  ni CHARLES  CHIKUMBILI, Miaka 22, Mkulima, Mkazi wa Swaswa, katika Manispaa ya Dodoma.
Kamishna Msaidizi  wa Jeshi la Polisi, Bw. David Misime alisema   askari walipowafanyia upekuzi wa mwili watuhumiwa usiku huo wa manane wamekutwa na misokoto miwili (2) ya bhangi.
MWISHO:
CONTACT:
POLISI MKOA WA DODOMA
DAWATI LA HABARI, ELIMU NA MAHUSIANO,
Phone:  0715 006523, Luppy Kung’alo – Mrakibu msaidizi wa Polisi (ASP)

Wanasoka Bora wa Mwaka SPUTANZA kufahamika kesho

CHAMA cha Wanasoka Tanzania (Sputanza), kesho kinatarajia kuwapatia tuzo wanasoka bora wa mwaka maarufu kama Sputanza Football Players Award katika hafla itakayofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubillee, jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa chama hicho, Abeid Kasabalala alisema tuzo hizo zitatolewa kwa mwanasoka bora wa mwaka, mwanasoka bora chipukizi, kocha bora wa msimu na kipa bora.

Alisema tuzo hizo zinazodhaminiwa na Kampuni ya Kishen Enterprises Ltd zitakuwa zikitolewa kila mwaka kuwaongezea wachezaji ari uwanjani wakati wa mashindano mbalimbali ya ndani na nje ya nchi.

“Makocha na viongozi kutoka mikoa mbalimbali wanatarajia kuwasili kesho (leo) ambao kwa kushirikiana na Kamati ya Utendaji ya Sputanza, watafanya uteuzi wa washindi kwa kutumia vigezo vilivyopo,” alisema Kasabalala.

Aliongeza kuwa katika tuzo hizo, pia watatoa vyeti vya kuwakumbuka na kuwapongeza wachezaji wa zamani waliochezea timu ya taifa miaka ya nyuma ambapo alisema kiingilio kitakuwa sh 10,000 na sh 50,000.

Golden Bush kupimana ubavu wenyewe mbele ya wakala wa kimataifa

Baadhi ya wachezaji wa timu ya Golden Bush Veterani
TIMU za soka za Golden Bush Fc inayoshiriki Ligi Daraja la Nne wilaya ya Kinondoni na Golden Bush Veterani asubuhi ya kesho zinatarajiwa kumenyana katika pambano la kirafiki huku wakishuhudiwa na wakala wa soka kutoka Msumbiji, Ashraf ambaye atakuwa na kazi ya kuangalia vijana wa kuondoka nao.
Kwa mujibu wa msemaji na mlezi wa timu hizo Onesmo Waziri 'Ticotico' pambano hilo litachezwa saa 1:30 asubuhi kwenye uwanja wa Kinesi maarufu kama St James Park, huku wakala huyo aliyekuwa kusaka wachezaji wa kwenda kucheza soka la kulipwa nchini kwao atakuwa na akishuhudia pambano hilo.
Ticotico alisema tayari mmoja wa wachezaji wa kikosi cha vijana wanaoongoza kwenye msimamo wa kundi lao katika ligi wanayoshiriki wakiwa na pointi 12 kwa michezo minne bila kupoteza wala kutoa sare mechi yoyote, lakini alikuwa akipenda kuwaangalia vijana vizuri kabla ya kuondoka na vijana watakaomkuna kisoka.
"Kesho uwanja wa Kinesi (st James park) utakuwa moto ambapo timu hizo mbili zitaumana kuanzia saa moja na robo asubuhi. Game hii itakuwa kipimo tosha kwa wazee ambao watakuwa wanafanya maandilizi ya mwisho kabla ya bonanza la Pugu siku ya jumapili week hii ambapo Golden Bush tumepata mwaliko maalum na Mbunge wa Ukonga Mama Mwaiposa," alisema.
Ticotico alisema pambano hilo litachezeshwa na mwamuzi Fred Mazuni badala ya waamuzi waliozoeleka katika mechi za timu hizo, Madaraka Seleman 'Mzee wa Kiminyio' au Ally Mayay.
Katika mechi mbili baina ya timu hizo Wazee walinyanyaswa kwa vipigo mfululizo, jambo ambalo ndilo limefanya abadilishwe  mwamuzi kwa hisia kwamba Babu Mada na Mayay wamekuwa wakiibeba timu ya vijana ambao ni viongozi na makocha wao.

Uhuru Seleman athibitishia kutua Coastal Union


KIUNGO mchezeshaji wa aliyekuwa akiichezea Azam kwa mkopo kutoka Simba, Uhuru Seleman ametua Coastal Union ya Tanga pia kwa mkopo kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Uhuru aliithibitishia MICHARAZO kwamba ametua Coastal kwa ajili ya ligi ijayo na kwamba anajifua vilivyo ili kuwapa raha mashabiki wa klabu hiyo aliyowahi kuichezea msimu wa 2007-2008 na kufikia kuzigombanisha Simba na Coastal wakimgombea kila mmoja alipodai ni mchezaji wake.
Kiungo huyo ambaye amewahi pia kutamba na Mtibwa Sugar, alisema amefurahi kutua Coastal kwa kuamini atapata nafasi nzuri ya kuonyesha kipaji chake baada ya kushindwa kupata fursa hiyo ndani ya Simba na hata Azam walipomchukua msimu uliopita.
"Ni kweli nimetua Coastal kwa mkopo na najiandaa kuichezea kwa msimu ujao, nimefurahi kwa sababu naamini nitarejesha makali yangu," alisema Uhuru.
Uongozi wa Coastal kupitia Mkurugenzi wake wa Ufundi, Nassor Binslum amethibitisha suala la kumnyakua kiungo huyo akidai wamezungumza na Simba ili wamchukue kwa mkopo na watasaidiana nao kulipa mshahara wa mchezaji huyo wakati akiichezea timu yao ambayo ilimaliza msimu wa ligi iliyopita katika nafasi ya 6.
Mabingwa hao wa zamani wa kandanda nchini mbali na kumnyakua Uhuru pia imewanasa wachezaji wengine wapya katika kukiimarisha kikosi chao baadhi yao ni beki Juma Nyosso na Haruna Moshi (wote Simba), Kenneth Masumbuko toka Polisi-Moro, Marcus Ndeheli na Said Lubawa (JKT Oljoro) na Abdallah Ally kutoka visiwani Zanzibar.

Juma Seif Kijiko atua Ruvu Shooting, wa5 watupiwa virago

Juma Seif Kijiko aliyesajiliwa Ruvu Shooting Stars
KIUNGO wa zamani wa Yanga aliyekuwa akiichezea African Lyon katika Ligi Kuu iliyoisha hivi karibuni, Juma Seif Dion 'Kijiko' ametua Ruvu Shooting kwa mkataba wa miaka miwili.
Kwa mujibu wa Msemaji wa Ruvu Shooting, Masau Bwire, Kijiko alisaini mkataba huo jana tayari kuichezea timu yao kwa msimu ujao.
Bwire alisema Kijiko anakuwa mchezaji wa tano kusajiliwa na timu yao baada ya kuwanyakua Cosmas Ader kutoka Azam, Elias Maguli (Prisons-Mbeya), Juma Nade (Kagera Sugar) na Jerome Lembeli toka Ashanti United.
Aidha Bwire alisema klabu yao imewatema kikosini wachezaji watano kwa sababu mbalimbali ikiwemo kushuka viwango na kuwataja kuwa ni Paul Ndauka,  Charles Nobert, Gido Chawala, Frank Mabande na Liberatus  Manyasi.
"Tumemsajili kiungo wa zamani wa Yanga, Juma Kijiko aliyeichezea Lyon msimu uliopita na pia tumewaacha wachezaji wetu watano kwa sababu mbalimbali na kikosi chertu kitaanza kujifua kwa msimu ujao kuanzia Juni 24," alisema Bwire.
Bwire aliwataka wachezaji wote wa timu hiyo kuhudhuria mazoezi hayo yatakayokuwa chini ya kocha wao Charles Boniface Mkwasa.

Nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Mkoa kutimkia wikiendi hii


Na Boniface Wambura
TIMU nne zimefuzu kucheza hatua ya nne (nusu fainali) ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) baada ya kushinda mechi zao za hatua ya tatu ya michuano hiyo itakayotoa washindi watatu watakaocheza Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu ujao.

Katika hatua hiyo Polisi Jamii ya Mara itaikaribisha Kimondo SC ya Mbeya kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma wakati Stand United FC ya Shinyanga itakuwa mgeni wa Friends Rangers ya Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Azam Chamazi.

Mechi za kwanza zitachezwa Juni 23 mwaka huu wakati zile za marudiano zitafanyika kwenye viwanja vya Sokoine jijini Mbeya na Kambarage mjini Shinyanga, Juni 30 mwaka huu.

Kwenye hatua ya tatu ya RCL, Friends Rangers iliing’oa Kariakoo ya Lindi kwa jumla ya mabao 2-0, Stand United FC ikaitoa Machava FC ya Kilimanjaro kwa mabao 2-1, Kimondo SC ikaishinda Njombe Mji mabao 6-5 wakati Polisi Jamii iliitambia Katavi Warriors kwa mabao 7-6.

Hatua ya mwisho ya ligi hiyo itachezwa Julai 3 mwaka huu kwa mechi za kwanza wakati zile za marudiano zitakuwa Julai 7 mwaka huu.

Kim Poulsen amtema Pazi, amuita Luhende Stars

Kocha wa Taifa Stars, Kimm Poulsen
Na Boniface Wambura
BEKI wa Yanga, David Luhende ameongezwa kwenye kikosi cha Taifa Stars kwa ajili ya mechi dhidi ya Uganda (The Cranes) kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ligi za Ndani (CHAN) zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini.

Kocha Kim Poulsen amesema kutokana na uamuzi huo wa kumuongeza beki huyo wa kushoto amemuondoa mchezaji mmoja kwenye kikosi chake. Mchezaji huyo ni mshambuliaji Zahoro Pazi wa JKT Ruvu.

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager sasa itaingia kambini kwenye hoteli ya Tansoma jijini Dar es Salaam, Julai 3 mwaka huu badala ya Julai 4 mwaka huu kama ilivyokuwa imepangwa awali.

Mechi ya Uganda itachezwa Julai 13 mwaka huu, saa 9 kamili alasiri kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati ile ya marudiano itachezwa wiki mbili baadaye jijini Kampala, Uganda.

Wachezaji wanaotakiwa kambini ni Aggrey Morris (Azam), Aishi Manula (Azam), Ally Mustafa (Yanga), Amri Kiemba (Simba), Athuman Idd (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Haruni Chanongo (Simba), John Bocco (Azam), Juma Kaseja (Simba), Juma Liuzio (Mtibwa Sugar) na Kelvin Yondani (Yanga).

Wengine ni Khamis Mcha (Azam), Mrisho Ngasa (Simba), Mudathiri Yahya (Azam), Mwadini Ali (Azam), Mwinyi Kazimoto (Simba), Nadir Haroub (Yanga), Salum Abubakar (Azam), Shomari Kapombe (Simba), Simon Msuva (Yanga) na Vincent Barnabas (Mtibwa Sugar).

Chid Benz kushiriki miaka 13 ya Kikosi leo New Msasani Club

 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgsRmvXwbSJaHszeaIBlQllQfjJ7Zmu0z3OF6Tw9tQQzPJDPSzOZCFLwHxcHfXfoKxRPCsvzqnvRsKNHB5kzFNa0y595Ct7WWWKOJBuzZNNjd1eyOTfa00aYb4X-axVtADtpB7ybdvnw5M/s400/KIKOSI.jpg
WAKATI maadhimisho ya miaka 13 ya Kikosi cha Mizinga inatarajiwa kufanyika leo kwenye ukumbi wa New Msasani Club, kiongozi wa kundi hilo, Karama Masoud 'Kalapina' amefichua kumaliza 'bifu' lake na Chid Benz na kumtangaza kwamba ni miongoni mwa wasanii watakaonegesha onyesho hilo kabambe.
Aidha Kalapina amesema kuwa makundi na msanii yeyote ambaye angependa kujitokeza kushiriki katika show yao hata kama siyo kwa kupanda jukwaani anawakaribisha kwa nia ya kufanikisha maadhimisho hayo na pia kutangaza Amani na Upendo Tanzania.
Akizungumza mapema asubuhi hii, Kalapina alisema Chid Benz naye atakuwepo katika show yao, licha ya kwamba mapema mwezi uliiopita walitibuana baada ya Benz kuvamia shoo ya Kikosi na kulazimika kutimuliwa jukwaani kitemi na kuibua hisia kwamba 'vita' ya wawili hao imeanza.
Hata hivyo, Kalapina alisema kwa sasa kikosi wamekuwa na hivuo wamezika tofauti zao za zamani na kuamua kufanya kazi baada ya kutumia muda mwingi kufanya harakati za kuisimamisha hop hop Bongo ambapo ilikuwa ikipata vikwazo vingi kiasi cha kutotangazika licha ya msaada mkubwa kwa jamii.
"Tumeshakuwa, mambo ya ubabe na kila lililokuwa likiwaudhi watu kwa sasa bhaaas, ndiyo maana Chid mdogo weangu nimemualika na pia naruhusu makundi yote yanayotuunga mkono na wasanii wengine waje ukumbini kutuopa sapoti kwa nia ya kutangaza amani na upendo kupitia tamasha hili la leo," alisema.
Kikosi cha Mizinga kitafanya onyesho hili likisindikizwa na wasanii kibao nyota nchini akiwemo 'Dume la Simba' Afande Sele, Manzese Crew, gangwe Mob, Mansu-Lee, Stereo, Nikki Mbishi, Young Killer na wengine huku kukiwa na maonyesho mbalimbali yenye utamaduni wa hip hop kama uchoraji kudance n.k.

Kocha Patrick Liewig aipa Simba siku 4

http://in2eastafrica.net/wp-content/uploads/2012/12/Patrick-Liewig.jpg
Kocha wa zamani wa Simba, Patrick Liewig
ALIYEKUWA kocha mkuu wa klabu ya Simba, Patrick Liewig, ameipa klabu hiyo siku nne kuhakikisha kuwa wanamlipa madai yake kabla hajamtaka mwanasheria wake kuwashtaki ifikapo Jumatatu.
Liewig aliyechukua mikoba ya kuifundisha Simba baada ya Mserbia Milovan Cirkovic, aliliambia gazeti hili kuwa anadai kiasi cha dola za Marekani 26,000 (Sh. milioni 42).
Akizungumza na NIPASHE jana, Liewig, alisema kwamba amemueleza Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Hanspoppe Zacharia, kuwa anahitaji kupewa haki yake hiyo ili arejee kwao na hapendi kuona anabaki nchini wakati hana kazi.
Liewig alisema kuwa anashangazwa kuona Simba wakishindwa kumpa taarifa za kusitishwa kwa mkataba wake kwa maandishi na kumuacha arejee nchini.
"Nilianza kusikia kwamba Simba hainihitaji mapema, hata waandishi walipenda kuniuliza hatma yangu kila mara Simba ilipokuwa inapoteza mechi... kumbe walitaka niamke na kujua kuwa nafasi yangu ndani ya klabu ni ndogo," alisema kocha huyo.
Aliongeza kuwa hivi sasa anasubiri kukutana na Hanspoppe ili ajue malipo yake yatakavyokuwa na haamini hata kidogo kuwa klabu hiyo itatekeleza madai yake baada ya kuondoka nchini.
"Napenda haki zangu nizipate sasa ili tumalizane kwa amani. Si tabia njema kufikisha malalamiko CAF (Shirikisho la Soka la Afrika) au FIFA (Shirikisho la Soka la Kimataifa)," aliongeza kocha huyo.
Simba iliamua kuachana na Liewig baada ya timu yake kushindwa kutetea ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara na mwishowe kumrejesha kocha na mchezaji wao wa zamani, Abdallah Kibaden 'King'.
Hata hivyo, ni uongozi wa Simba ndiyo uliokuwa ukiunga mkono uamuzi wa kutowachezesha baadhi ya nyota wao wenye majina makubwa kama Haruna Moshi 'Boban' na Juma Nyosso na kuwachezesha zaidi yosso wao kuelekea mwishoni mwa msimu na mwishowe kujikuta wakipoteza ubingwa mapema.
Liewig anaidai Simba fedha za mshahara wake wa mwezi Aprili na Mei mwaka huu ambao ni dola za Marekani 14,000 (Sh. milioni 14) na kingine kilichobakia kinatokana na makubaliano ya kuvunja mkataba wao uliopaswa kumalizika mwishoni mwa mwezi huu.
Hanspoppe alikiri kuwa Simba inadaiwa na kocha huyo na kueleza kwamba klabu inasaka fedha kutoka kwa wadau wake ili kuhakikisha wanalipa madeni yote kabla ya kuanza kwa msimu mpya .
Mapema mwaka hii mmoja wa wanachama wa Simba, Rahma Al Kharoos, aliokoa jahazi kwa kumlipa Milovan madai yake baada ya kutimuliwa kama ilivyo sasa kwa Liewig.

Chanzo:NIPASHE

Mabondia wa Tanzania wafungwa Mauritius kwa dawa za kulevya



Mabondia waliohukumiwa

Mabondia wanne wa Tanzania wafungwa miaka 15 jela nchini Mauritius kwa makosa ya kuingiza dawa za kulevya aina ya heroin.

Mabondia hao ni Case Ramadhani Fills, Nathanael Elia Charles, Ally Rajabu Msengwa na Petro Charles Mtagwa.

Wakati kesi hiyo ilipoanza kusikilizwa, wote walikiri makosa ya kuingiza mihadarati hiyo nchini Mauritius wakati walipokwenda kushiriki mashindano ya ndondi barani Afrika mwaka 2008.
Wakiwa mbele ya Jaji, waliiambia mahakama kuwa walilazimika kuingia katika biashara hiyo haramu kutokana na hali zao za maisha kuwa maskini.
"Tunaomba radhi kwa taifa la Mauritius", waliiambia mahakama.
"Tu watu maskini na tunategemewa na familia, watoto na wazee wetu wanaotugemea."
"Kwa dawa hizi tungepata kiasi cha Pauni £4,000". walisema
Jaji Benjamin Marie Joseph alisema katika kutoa adhabu hiyo yote hayo ameyafikiria, kwani walitoa ushirikiano mzuri wakati wote wa uchunguzi wa kesi hiyo, kulikowezesha hata wafanyabiashara hiyo, raia wa Mauritius kukamatwa.
Wamekuwa mahabusu kwa siku 1,722, sawa na miaka miatano, hivyo watatumikia miaka kumi iliyobakia jela. Pia watatakiwa kulipa faini ya pauni £1,600 na gharama nyingine za uendeshaji wa kesi hiyo.
Kwa mujibu wa mwandishi wa habari wa BBC nchini Mauritius Yasine Mohabuth in Mauritius, Jaji aliwashutumu kwa kuukosea umma wa Mauritius kwa kuingiza dawa hizo za kulevya aina ya heroin.
Mabondia hao waliwasili Mauritius tarehe 10 Juni 2008 na kuweza kupita uwanja wa ndege bila kunaswa hadi walipokamatwa katika hoteli waliyofikia ya Quatre Bornes.
Kwa pamoja walimeza gram 4639.04 za heroin zikiwa katika vifuko 358 vijulikavyo kama pipi.

BBC

Thursday, June 20, 2013

Waraka namba 2 wa Zola D kwa Watanzania

Zola D katika pozi
BARUA MAALUM KUTOKA KWA DAVID MICHAEL MLOPE,aka ZOLA D KWENDA KWA WATANZANIA WOTE WALIOSHIRIKI KATIKA MSIBA WA MANGWEAR.pamoJa na LANGA KILEO.

DAVID MICHAEL MLOPE BOX 70098 DAR ES LAAM TANZANIA.
PHONE +255715296889.
barua no 2.

naendelea pale nilipoishia kwenye barua ya mwanzo namba 1 ...... habari zenu ndugu zangu watanzania hope wote ni wazima na mnaendelea na mishe za maisha mimi mzima siJambo Japo nina stress nyingi sana mpaka nimepungua kg 3,kutokana na mawazo na kuto kulala tokea msiba wa arbert mangwear pia tumepata pigo Jingine la mdogo wetu langa kileo,siJui niseme nini kwa Jinsi inavyo niuma ila nina mwachia Mungu maana ndio kazi yake pia pole sana wazazi wa langa kileo baba na mama pamoJa na familia yote kwa uJumla pia asante sana watanzania wote walioJitokeza kwenye safari ya kumsindikiza ndugu yetu msanii mwenzetu langa kileo leo nataka kugusia sana upande wa maisha yetu na dini kama binadamu tunaopita tu kwenye hii dunia maana kila mtu atakufa vitabu vya dini vimeandika.Ndugu zangu wapendwa watanzania dunia imekwisha ndugu zangu tuanze kufanya ibada na kutenda yaliyo mema coz free masons wanawatumia ndugu zetu kwenye big brother na seemu mbali mbali kuwaonyesha wakiwa watupu uchi na kuwadanganya kwa pesa,na sasa wameingia africa mashariki kwa kishindo sana hawa free masons Juzi tu nimepigiwa simu na watu kampuni Jina siri yangu wanataka nikacheze video ya ngono na mwanamke kwa kitita cha milion 70 nikawaeleza siwezi kufanya uchafu kama huo,na leo tena wamenipigia wakisema watanipa milion 100 bado nimekataa Je unaelewa kwa nini nimekataa? free masons wanataka viJana shupavu na wenye akili na vipaJi ili waweze kuwatumia kuitangaza dini yao na wanaweza kukupa maisha ya Juu kwa gharama yoyote ile, Mungu atuepushe nao na Mungu atulindie watoto wetu inshallah wasiingie kwenye dini ya kishetani,wahi kuwapeleka madrasa watoto mapema waitambue dini mapema na kuwapeleka kwenye mafunzo ya dini kwenye makanisa tuliyoyazoea tokea kitambo na tuachane na makanisa mapya yanayoanzishwa kila kukicha na wachungaJi wao wanaJiita miungu watu,ndugu zangu naelewa watu wanaweza kuniona kama nilie changanyikiwa hapana ila nimeamua kupoteza muda wangu kukaa chini na kuandika machache ninayoyaona kwa upeo wangu na vipaJi alivyonipa Mungu kuelimisha na kuburudisha,siwezi kukaa kimya pale ninapo tizama taifa langu lina teketea kwa maovu,na tunapelekeshwa kishetani na dini feki na makampuni ya kigeni katika nchi yetu tuna acha utamaduni wetu na tunaingia kwenye utamaduni wa watu wa kishetani kwa upeo wetu mdogo na umasikini tumetekwa na pesa na starehe kiasi kama sisi wasanii ukitizama storia ya msanii mwanzo kabla aJawa super star alikuwa ni mtu wa kufanya ibada ila sasa amekuwa super star awezi tena kufanya ibada wala kutoa dhaka au kuwasaidia wazazi wake kisa yeye ni star na yupo bussy Je swali huyu star msanii ni kioo cha Jamii au amegeuka kuwa moto wa Jamii? kila kukicha kwenye magazeti utaskia story za sifa mbaya na picha chafu za wasanii sehemu flani wakifanya ngono na mambo mengine ya kumchafua Mungu wetu,ndugu zangu wasanii naomba tubadilike na tuwe mfano ili tuweze kuliongoza taifa letu salama na tuwafundishe wadogo zetu waige mfano mzuri wa tabia zetu nJema na sio uchafu wetu,ndugu zangu watanzania mimi sitaki kuwachosha maana nina MAMBO MENGI SANA YA KUANDIKA ILA NAONA KWA LEO NISHIE HAPA,NACHUKUA NAFASI HII KUAMBIA NAWAPENDA SANA WATANZANIA WENZANGU PIA NAWAPENDA VIONGOZI WANGU WA TANZANIA PIA NAIPENDA NCHI YANGU YA TANZANIA NIPO TAYARI KUFA KUITETEA NCHI YANGU NA WANACHI WANGU NAWATAKIA MAISHA MEMA NA FAMILIA ZENU NI MIMI MTIIFU WENU KATIKA UjENZI WA TAIFA LETU TUKUFU, DAVID MICHAEL MLOPE AKA ZOLA D.ITAENDELEA!!!!!

Zola D awashukuru Watz msiba wa Ngwair, Langa, lakini...!


Mwili wa Ngwair ukiingizwa kaburini, ambapo Zola D (mwenye miwani) naye alikuwa mmoja wa walioshiriki mazishi hayo mjini Morogoro.

BARUA MAALUM KUTOKA KWA DAVID MICHAEL MLOPE,ZOLA D KWENDA KWA WATANZANIA WOTE WALIOSHIRIKI KATIKA MSIBA WA MANGWEAR...

DAVID MICHAEL MLOPE BOX 70098 DAR ES LAAM TANZANIA.
PHONE +255715296889.

habari za leo watanzania wote ,nachukua nafasi hii kwa niaba ya wasanii wa kundi la chemba sqward east zoo,kuwashukuru watanzania wote walioshiriki katika msiba wa ndugu yetu mpendwa mangwear hakika nimeona upendo wenu kwa kumzika ndugu yetu Arbert k mangwear kwa upendo wenu mkubwa sana,mimi binafsi sina cha kuwalipa ila nina imani kubwa sana Mungu atawalipa,na sio kwa mangwear tu naomba mzidi kushilikiana na sisi wasanii wenu hata siku nikifa mimi au msanii mwingine naomba mtuzike KWA UPENDO msituache maana sie sote ni binadamu tunapita tu hapa kwenye hii dunia kila mtu atakufa muhimu ni kupendana na kushirikiana kwa upendo,pia kama tunagombana hapa duniani ni bora tupatane kabla ya kifo kutukumba siku yetu ya kufa hakuna anaetambua itakuwa lini, maana Mungu alisema ukisamehe na yeye atakusamehe siku yako ya kihama,kuna mambo mengi nimejifunza kwenye hii dunia,kwamba tujitahidi kufanya yaliyo mema kutengeneza njia bora siku tukifa,napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru sana wana kamati wote waliojitolea tokea mwanzo kuandaa safari kutoka south africa mpaka tanzania asante sana BRO P FUNK MAjANI , BONGO RECORDS kwa upendo wako na mchango wako kwetu sie wadogo zako Mungu ATAKULIPA ZAIDI NA ZAIDI ,ASANTE SANA RADIO CLOUDS FM KWA KUSHIRIKI KWA UPENDO WENU MKUBWA ,na wafanyakazi wake wote walioshiriki kwa upendo katika kukamilisha safari ya mpendwa wetu MANGWEAR,asante sana BRO ADAMU jUMA VISUAL LAB NIMEONA KAZI KUBWA ULIYOIFANYA MUNGU AKUBARIKI SANA ENDELEA KUWA NA MOYO HUO HUO , ASANTE SANA, BRO MIRAD AYO,BRO MAjIZO,BRO TC TIMOTH CHERULA,ADAMU MCHOMVU,RADIO TIMES FM,RADIO EAST AFRICA NA EAST AFRICA TV,ITV,CHANEL TEN BRO RIZ 1 KIKWETE,BRO SUGU,SIST j DEE,Dj CHOKA, PUSH NA WENGINE WENGI,AMBAO NIMEWASAHAU MAjINA YENU ASANTENI SANA SANA WOTE WALIOTOA MAGARI YAO KWENDA MOROGORO KUZIKA,PIA ASANTE SANA WANAKAMATI WA MOROGORO,ASANTE SANA VIONGOZI WA POLICE DAR ES SALAAM NA VIONGOZI WA POLICE MOROGORO KWA KUIMALISHA ULINZI KATIKA MSAFARA WA MANGWEAR KUANZIA DAR MPAKA MOROGORO NINA MAMBO MENGI SANA YA KUANDIKA ILA NAONA KWA LEO NISHIE HAPA,NACHUKUA NAFASI HII KUAMBIA NAWAPENDA SANA WATANZANIA WENZANGU PIA NAWAPENDA VIONGOZI WANGU WA TANZANIA PIA NAIPENDA NCHI YANGU YA TANZANIA NIPO TAYARI KUFA KUITETEA NCHI YANGU NA WANACHI WANGU NAWATAKIA MAISHA MEMA NA FAMILIA ZENU NI MIMI MTIIFU WENU KATIKA UjENZI WA TAIFA LETU TUKUFU, DAVID MICHAEL MLOPE AKA ZOLA D.ITAENDELEA!!!!!

Barabara ya Kimara King'ongo yafungwa mwezi mzima kisa....!




HIVI ndivyo wakazi wa Kimara King'ongo Kata ya Kimara na Samanga wanavyohenyeka majira ya asubuhi kwa kutembea kwa miguu kupandisha kilima sumbufu cha Peter's School ambacho kinatengenezwa kwa kuwekewa zege ili kuruhusu magari kupita bila usumbufu .
Matengenezo ya barabara hiyo yanayoendelea kwa sasa yamefanya njia hiyo ifungwe kwa mwezi mzima tangu Juni 1-30, ili ikiachiwa wakazi wa eneo hilo wafurahie huduma ya usafiri baada ya sasa kila siku asubuhi magari ushusha abiria darajani badala ya kuzunguka njia ya kutokea Stop Over au Kimara Temboni.

Hatimaye mhanga wa bomu la Arusha azikwa

HATIMAYE aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA (BAWACHA) Kata ya Sokoni I, Judith William Moshi, aliyefariki kwa mlipuko wa bomu kwenye viwanja vya Soweto jijini Arusha siku ya Jumamosi (Juni 15, 2013) wakati wa ufungwaji wa kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani umezikwa leo jijini humo.
Chini baadhi ya picha za msafara wa mazishi wa mwanadada huyo ambaye alikuwa miongoni mwa watu watatu waliokufa katika mlipuko huo ambao al manusura ungewakumba viongozi wa kuu wa chama hicho akiwamo Mwenyekiti wao, Freeman Mbowe (Mbunge).

Hapa ni Sugu akiwa na Peter Msigwa wakiongoza msafara.
Viongozi  wa chadema watua Arusha kwa ajili ya kutoa heshima zao za mwisho kwa wale waliofariki katika mkutano wa Chadema wakati wa mripuko wa bomu. Huku wakishirikiana na wananchi wa Arusha, John Mnyika ataongoza shughuli hizo.
Hili ndilo jeneza lililolobeba mwili wa marehemu ukipelekwa sokon 1


 

Mbowe, Lema wajisalimisha Polisi

Mwenyekiti wa CHADEMA  Fremaan Mbowe pamoja na mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema leo wamejisalimisha Polisi  baada ya jeshi hilo kutangaza linawasaka baada ya vurugu ziliztokea jana mjini Arusha.
Akiongea na waandishi wa habari,  Fremaan Mbowe alisema kuwa wao wamejisalimisha kama polisi walivyosema wanawatafuta na walipofika waliandika maelezo ambapo alisema kuwa polisi waliwaita kwa mambo mawili, moja likiwa ni kwa kuwahoji kwanini walifanya mkutano usio wa halali ambapo alisema kuwa;
"Jambo la kufanya mkutano pasipo kuwa halali sio kweli kwani polisi walituruhusu tukafanye mkutano katika sehemu hile lakini kinachotushangaza tumefanya wamekuja kutupiga mabomu na kusema sio wa halali na kuhusiana na ushahidi msimamo wangu upo pale pale tunao ushahidi wa kutosha na tunamjua aliyerusha bomu Jumamosi, lakini hatutautaoa hadi  Rais atakapounda Tume Huru ya majaji ili wafuatilie suala hili. Hao ndiyo tutawaonyesha ushahidi huo, lakini siyo Polisi hatuwezi kuwapa," alisema Mbowe.
Afande Chagonja akiongea na waandishi wa habari
Kwa upande wa Polisi kupitia Kamishna wa Mafunzo na Operesheni za Kijeshi,  Paul Chagonja akiongea na wanahabari alisema waliwahoji wabunge hao na kuwaomba ushahidi waliokuwa nao kama wanavyodai, lakini waheshimiwa hao hawakutoa ushirikiano.
"Mbowe alisema kuwa ana ushahidi na hata katika vyombo vya habari ametangaza lakini nashangaa tulivyomuuliza hapa amesema kuwa hana ushahidi wowote na wala hajawahi kutamka hivyo sasa sisi kwa kuwa kasema hivyo nitakaa na makachero wangu na tutaangalia jinsi ya kufanya"alisema Chagonja
Aidha alisema kuwa alimuliza mbunge wa Arusha mjini kwanini awali alikuja kuwasifia Polisi baadae akawageuka ilihali alishasema katu hawezi kusema uongo na kuwajibu kuwa, yeye anafuata mwenyekiti wake anachosema.

Polisi waua raia kwa risasi Mbeya, RPC afafanua kilichotokea




 Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya  Diwani Athuman
---

MAUAJI YA MTU MMOJA KUFUATIA VURUGU YA WANANCHI WA KIJIJI CHA LUMBILA WILAYA YA MBOZI KUWASHAMBULIA ASKARI WALIOKUWA WANAFANYA OPERESHENI.
--
MNAMO TAREHE 19.06.2013 MAJIRA YA SAA 13:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA LUMBILA KATA YA RUANDA WILAYA YA MBOZI MKOA WA MBEYA. RAJABU S/O WILSON MWASHITETE, MIAKA 25, MNYIHA, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA LUMBILA ALIUAWA KWA KUPIGWA RISASI NA ASKARI POLISI WALIOKUWA KATIKA MSAKO DHIDI YA WAHALIFU/WAPORAJI KATIKA ENEO LA MLIMA SENJELE.

CHANZO NI BAADA YA ASKARI POLISI WAKIWA KATIKA OPERESHENI ENEO HILO KUZINGIRWA NA KUNDI LA WANANCHI ZAIDI YA 150 WA KIJIJI HICHO WAKIWA NA SILAHA ZA JADI MAPANGA, MARUNGU, SHOKA NA MAWE WAKIWAZUIA ASKARI HAO KUKAMATA WAHALIFU NA KUANZA KUFANYA VURUGU BAADA YA KUWA WAMEKAMATA MALI INAYODHANIWA KUWA YA WIZI AMBAYO NI MAFUTA  AINA YA DIESEL MADUMU ZAIDI YA 100.

HATA HIVYO KUFUATANA NA VURUGU ZILIZOJITOKEZA WALIFANIKIWA KUCHUKUA MADUMU MACHACHE AMBAYO NI MADUMU MATATU YENYE UJAZO WA LITA 60, MADUMU MAWILI YENYE UJAZO WA LITA 20 NA 
MADUMU NANE LITA 30 HIVYO UVAMIZI HUO WA WANANCHI NDIO ULIOWAFANYA ASKARI POLISI WASHINDWE KUCHUKUA VIELELEZO VYOTE.


MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA MBOZI.  AIDHA KATIKA TUKIO HILI CHARLES  S/O JOSE  MWAWALO,MIAKA 27,MNYIHA,MKULIMA MKAZI WA KIJIJI CHA LUMBILA ALIJERUHIWA KWA KUPATA MICHUBUKO TUMBONI AMBAPO UCHUNGUZI UNAFANYWA KUBAINI NI KITU GANI KILICHOMJERUHI.

PIA WANANCHI WALIFUNGA BARABARA KUU YA MBEYA/TUNDUMA KWA KUWEKA MAWE NA MAGOGO NA KUSABABISHA MSONGAMANO MKUBWA WA MAGARI BARABARANI. 

HALI ILIKUWA SHWARI BAADA YA KAMANDA WA POLISI KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI KUFIKA ENEO LA TUKIO NA KUZUNGUMZA NA WANANCHI PAMOJA NA VIONGOZI WA ENEO HILO KISHA KUFUNGUA BARABARA .

ASKARI POLISI WANNE WALIJERUHIWA KATIKA TUKIO HILO KATI YAO WATATU WALIPATIWA MATIBABU NA KURUHUSIWA NA ASKARI MMOJA  AMELAZWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA KWA MATIBABU ZAIDI . 

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA BADALA YAKE KUWA NA UTAMADUNI WA KUTATUA KERO/MALALAMIKO YAO KWA NJIA YA MAZUNGUMZO KWA KUYAWASILISHA KATIKA MAMLAKA HUSIKA. AIDHA ANAWATAARIFU WALE WOTE WALIOWAHI KUIBIWA/KUPORWA MALI MBALIMBALI YAKIWEMO MAFUTA WAJITOKEZE POLISI KWA AJILI YA HATUA ZINAZOSTAHILI.


Signed By,
                          
[DIWANI ATHUMANI  

[DIWANI ATHUMANI   - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

NMB, Wabunge walivyoonyeshana kazi Dodoma

KATIKA kuendeleza na kuimarisha uhusiano mzuri baina ya Benki ya NMB na Watunga Sheria wa Bunge la Jamhuri, mwishoni mwa wiki timu hizo zilionyeshana kazi kwa kuumana katiuka pambano lililoandaliwa na Benki hiyo ambao uilihudhuriwa na mashabiki lukuki wa timu hizo wea mjini Dodoma.
 Hiki ndicho kikosi kamili cha timu ya benki ya NMB kilichong’ara katika mechi na timu ya Wabunge kwenye Uwanja wa Jamhuri.
 Kikosi kamili cha timu ya Wabunge.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mh. George Mkuchika ambae alikua ndiye mgeni rasmi akikagua kikosi cha timu ya NMB  kabla ya mpambano huo.
 Naibu waziri wa habari Vijana,Utamaduni na Michezo Mh.Amos Makalla (Jezi ya njano na Bluu) akipigwa chenga na  Afisa mkuu wa fedha NMB  Waziri  Waziri katika mtanange huo uliokuwa wa kukata na shoka.
 Mbunge wa Kinondoni Mh. Iddi Azan ambae ndiye mlinda mlango wa timu ya wabunge  (Jezi ya rangi ya chungwa) akiongoza wachezaji wenzake kufurahia goli moja walilolipata na kuwapa ushindi dhidi ya timu ya NMB
Mashabiki wa timu zote mbili wakifuatilia mtanange huo ambao uliisha kwa Wabunge kuibuka kidedea dhidi ya NMB.

Prof Lipumba mgeni rasmi miaka `13 ya Kikosi cha Mizinga

http://sphotos-a.ak.fbcdn.net/hphotos-ak-ash3/p480x480/712_467874856634160_1616825647_n.jpg
Kiongozi wa Kikosi cha Mizinga, Karama Masoud 'Kalapina'
 MWENYEKITI wa Chama cha CUF, Prof Ibrahim Lipumba anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika onyesho la maadhimisho la miaka 13 ya Kikosi cha Mizinga zinazotarajiwa kufanyika kesho kwenye ukumbi wa Msasani Club, jijini Dar es Salaam.
Kiongozi wa Kikosi, Karama Masoud 'Kalapina' aliiambia MICHARAZO kwamba, Prof Lipumba ndiye atakayekuwa mgeni rasmi baada ya mipango ya awali kumualika Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Idd Azan kushindikana kumpaka kwa kuwaomba udhuru.
Kalapina alisema maandalizi ya onyesho hilo ambalo mashabiki watalazimika kulipa Buku 5 tu mlangoni, yamekamilika ikiwemo kuongezeka kwa idadi ya wasanii na makundi yatakayowasindikiza katika onyesho hilo ambalo litaambatana na maonyesho mbalimbali yenye asili ya utamaduni wa Hip hop.
"Maandalizi ya onyesho la Kikosi cha Mizinga yamekamilika ikiwemo kutarajiwa Mwenyekiti wa Kitaifa wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba kuwa mgeni rasmi baada ya kumkosa Mhe. Idd Azan, pia burudani zimeongeza zaidi katika kunogesha miaka hiyo 13," alisema Kalapina. 
Mkali huyo ambaye pia ni mwanaharakati na mwanasiasa alisema baadhi ya wasanii watakaoshiriki kupigwa mizinga 21 ya Kikosi kesho ni Afande Sele, Young Killer, Manzese Crew, Stereo, Kala Jeremiah, LWP, Mansu-Lee, Gangwe Mob  wakiwa na Inspekta Harun na wengine wakiwamo Kikosi cha Mizinga chenyewe.
Shughuli nyingine zitakazoambatana na onyesho hilo ni maonyesho ya uchoraji na kupaka rangi, mitindi ya nguo na mavazi, kucheza break dance na utoaji wa tuzo kwa watu na asasi zilizosaidia Kikosi cha Mizinga kufika hapo ilipo ikiwa inatimiza miaka hiyo 13 tangu kuzaliwa kwake.