MSHAMBULIAJI nyota wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) na timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Mbwana Samata, amesema mechi ya Jumapili dhidi ya Msumbiji (Mambas) itakuwa na ushindani kwa pande zote mbili lakini amewataka Watanzania wasiwe na wasiwasi.
Samata na mshambuliaji mwenzake wa TP Mazembe, Thomas Ulimwengu, waliwasili jijini Dar es Salaam jana asubuhi wakitokea Tunisia ambako klabu yao imeweka kambi kujiandaa na mechi za Ligi ya Klabu Bingwa Afrika.
Akizungumza na gazeti hili juzi usiku kabla ya kupanda ndege kuja nchini, Samatta, alisema kuwa anaamini Taifa Stars ina nafasi nzuri ya kushinda mechi hiyo licha ya kwamba itakuwa ni ngumu na ni lazima wacheze kwa kujihadhari.
Samata alisema watahakikisha wanapata matokeo mazuri Jumapili na kujiweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele.
"Kwa upande wangu nimetoka katika maandalizi ya Ligi ya Klabu Bingwa, niko fiti kulipigania taifa langu, Inshaallah Allah atatia wepesi," alisema mshambuliaji huyo wa zamani wa Simba na African Lyon (zamani Mbagala Market).
Jana mchana Samatta aliliambia gazeti hili wamefika nchini salama lakini wataungana na wachezaji wenzao wa Stars Ijumaa baada ya kurejea wakitokea Mbeya.
“Ndiyo tumeshafika Dar, niko pamoja na Tom," alisema mshambuliaji huyo anayependwa na mashabiki wa TP Mazembe.
Aliongeza kuwa wanaahidi watapambana na akawataka Watanzania wajitokeze kwa wingi Jumapili kuishangilia timu hiyo.
Kabla ya kwenda Mbeya, Stars iliweka kambi ya wiki mbili jijini Gaborobe, Botswana kwa ajili ya kujiandaa na mechi hiyo ya Jumapili kabla ya kurudiana Agosti 3 mwaka huu mjini Maputo.
Nyota mwingine wa Stars kiungo, Mwinyi Kazimoto, anatarajiwa kuwasili leo mchana akitokea Qatar kujiunga na timu hiyo.
NIPASHE
STRIKA
USILIKOSE
Thursday, July 17, 2014
STEVE NYERERE AHIMIZA JAMII KUSAIDIA WALEMAVU
| Steve Nyerere alipokuwa akiwasilia shule ya Sinza Maalum |
Steve Nyerere alitoa wito huo juzi wakati wa sherehe ya siku ya kuzaliwa kwa mtoto wa Kajala Masanja aitwaye Paula iliyofanyika katika Shule Maalum Sinza inayofundisha watoto wenye ulemavu wa akili, ambako alisema pamoja na umuhimu wa kuwasaidia yatima, lakini pia makundi mengine ya watoto kama walemavu wa akili yanapaswa kuangaliwa kwa jicho la ziada.
"Unajua jamii na hata sisi wasanii tumezoea kila tukitaka kutoa misaada tunakimbilia kwenye vituo vya kulelea yatima, lakini kumbe wapo watoto wengine wahitaji kama watoto hawa ambao wameonyesha furaha na uwezo wa hali ya juu wa utambuzi tofauti na hali zao," alisema.
Nyota huyo wa kuigiza sauti za watu mashuhuri, aliwapongeza walimu wa shule hiyo ya Sinza Maalum kwa kazi kubwa na ngumu waliyonayo katika kuwatunza na kuwalea wanafunzi hao ambao walimtambua kwa haraka Steve Nyerere walipoulizwa kama kuna mtu yeyote katika msafara uliotembelea shuleni hapo na kumtaja yeye kwa kwenda kumshika mkono na kuamsha vicheko.
BADO KIDOGO UMSIKIE THEA KWENYE INJILI
MUIGIZAJI nyota nchini, Ndimbangwe Misayo 'Thea' amesema yupo hatua ya mwisho kabla ya kuibukia studio kurekodi wimbo wake wa kwanza wa muziki wa Injili, fani anayopanga kujitosa jumla kwa lengo la kumtumia bwana.
Akizungumza na MICHARAZO, Thea alisema kuwa mpango wake wa kuhamia kwenye muziki wa Injili unaendelea kwa kuanza kutunga nyimbo kabla ya kuingia studio kwa ajili ya kurekodi ili mashabiki wa miondoko hiyo washuhudie kipaji kingine alichonacho.
"Nipo kwenye maandalizi ya kuanza kuimba nyimbo za Injili, kuna kazi nimeanza kuziandika na muda ukifika nitaingia studio na kuanza kutoa kazi moja baada ya nyingine, mashabiki wa muziki huo wavute subira," alisema.
Thea ambaye aling'ara kwenye michezo ya kuigiza ya kwenye luninga akiwa na kundi la Kaole Sanaa kabla ya kuhamia kwenye filamu alisema kiu yake ni kumtumikia Mungu kama alivyokuwa akiutumikia ulimwengu na hatanii katika hilo. Alisema uimbaji ni fani aliyokuwa nayo tangu udogoni kwa kuimba kanisani na kwenye kwaya ya kanisa lake kabla ya kuzamia kwenye filamu.
Akizungumza na MICHARAZO, Thea alisema kuwa mpango wake wa kuhamia kwenye muziki wa Injili unaendelea kwa kuanza kutunga nyimbo kabla ya kuingia studio kwa ajili ya kurekodi ili mashabiki wa miondoko hiyo washuhudie kipaji kingine alichonacho.
"Nipo kwenye maandalizi ya kuanza kuimba nyimbo za Injili, kuna kazi nimeanza kuziandika na muda ukifika nitaingia studio na kuanza kutoa kazi moja baada ya nyingine, mashabiki wa muziki huo wavute subira," alisema.
Thea ambaye aling'ara kwenye michezo ya kuigiza ya kwenye luninga akiwa na kundi la Kaole Sanaa kabla ya kuhamia kwenye filamu alisema kiu yake ni kumtumikia Mungu kama alivyokuwa akiutumikia ulimwengu na hatanii katika hilo. Alisema uimbaji ni fani aliyokuwa nayo tangu udogoni kwa kuimba kanisani na kwenye kwaya ya kanisa lake kabla ya kuzamia kwenye filamu.
KAJALA: SASA NIMEZALIWA UPYA BONGO MOVIE
NYOTA wa filamu nchini, Kajala Masanja amesema filamu yake mpya anayojiandaa kuingiza sokoni iitwayo 'Laana' inakuja kuthibitisha kuwa kwa sasa amezaliwa upya na yupo kikazi zaidi kuwapa burudani.
Kajala ambaye alinusurika kwenda jela katika kesi iliyokuwa ikimkabili kabla ya kusaidiwa na Wema Sepetu kwa kumlipia faini ya Sh. milioni 13, alisema filamu hiyo mpya itatoka hivi karibuni kwani tayari ameishaikabidhi kwa wasambazaji.
Akizungumza na MICHARAZO, Kajala anayemiliki kampuni ya Kay Entertainment alisema baada ya misukosuko aliyokumbana nayo kwa sasa ametuliza akili kwa ajili ya kufanya kazi akianza na filamu ya 'Laana' ambayo amewashirikisha wasanii nyota nchini.
Kajala aliwataja baadhi ya wasanii walioicheza filamu hiyo ni Ahmed Salim 'Gabo', Philemon Lutwazi 'Uncle D', Mama Kawele, Mama Sonia, yeye (Kajala) na wakali wengine.
"Kwa sasa nipo kikazi zaidi na naanza hesabu na 'Laana' iliyotengenezwa na kampuni yangu ya Kay Entertainment chini ya muongozaji Leah Richard 'Lamata' na bada ya hapo natarajia kutoa 'Pishi' wakati 'Heart Attack' niliyoiandaa kabla ya misukosuko ikisubiri kwanza," alisema Kajala.
Msanii huyo alisema anaamini kazi hizo zitathibitisha kuwa anachokisema hatanii, bali ni kweli amezaliwa upya chini ya kampuni yake.
MATOKEO KIDATO CHA SITA YATOKA EBU YACHUNGILIE HAPA
NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA
ACSEE 2014 EXAMINATION RESULTS ENQUIRIES
Tuesday, July 15, 2014
'Shujaa' waa Ujerumani haamini kama wametwaa ndoo
| KIkosi cha Ujerumani na kocha wao wakishangilia ubingwa |
![]() |
| Mario Gotze akiwa na famnilia yake akishangilia ubingwa |
Kiungo huyo wa Bayern Munich alianzia benchi katika mechi hiyo hiyo, lakini aliingizwa mwishoni mwa kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Miroslav Klose.
Gotze hakumuangusha kocha Joachim Low na akafunga goli katika dakika ya 113 kufuatia krosi ya Andre Schurrle na kuwapa Ujerumani ubingwa wa nne wa Kombe la Dunia.
"Ni hisia za aina yake, sijui nizielezee vipi. Nilipiga shuti tu na sikujua nini kitatokea. Ni ngumu kuamini," alisema nyota huyo mwenye umri wa miaka 21.
"Kwetu sisi,ndoto imekua kweli. Najivunia timu na nina furaha ya kupindukia kwa kila kilichotokea Brazil.
"Kila mchezaji katika timu yetu anastahili kutajwa hapa na tunajivunia kutwaa kombe hili."
Gotze amecheza mechi sita za Kombe la Dunia 2014 na amefunga magoli mawili.
MAYWEATHER KURUDIANA NA MAIDANA SEPTEMBA.
BINGWA wa masumbwi wa
uzito wa welter ambaye hajapigwa mpaka sasa, Floyd Mayweather
anatarajiwa kucheza pambano la marudiano na Marcos Maidana wa
Argentina.
Mayweather mwenye umri wa miaka 37 raia wa Marekani
anatarajiwa kutetea mikanda yake ya ubingwa inayotambuliwa na Baraza la
Ngumi Duniani-WBC na Chama cha Ngumi Duniani-WBA dhidi ya maidana
aliyemdunda katika pambano lililofanyika Mei 3 mwaka huu.
Wawili hao
wanatarajiwa kupambana tena jijini Las Vegas, Septemba mwaka
huu.
Akihojiwa Mayweather ametamba kuwa ana uhakika wa kushinda pambano
hilo pamoja na kukiri kuwa utakuwa mpambano na mgumu.
Katika pambano
lililofanyika Mei, jaji wa kwanza alitoa alama 114-114, wakati majaji
wawili waliobakia walitoa alama 116-112 na 117-111 ambapo alama zote za
juu zilikwenda kwa Mayweather.
Mayweather anakaribia kufikisha rekodi ya
kucheza mapambano 49 bila kupigwa iliyowekwa na bingwa wa zamani wa
uzito wa juu Rocky Marciano, ambapo mpaka sasa ameshashinda mapambano 46
bila kupigwa.
Mnigeria, Wema, Sir Nature kupamba Usiku wa Matumaini
![]() |
| Wema Sepetu |
Kawaida ya tamasha hilo hufanyika Julai 7, lakini kutokana na mwaka huu tarehe hiyo kuangukia kwenye mfungo wa mwezi wa Ramadhani, waandaaji wake wameamua kupeleka hadi Nanenane kwa heshima ya waumini wa Kiislam.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo, Abdallah Mrisho alisema kuwa 'Usiku wa Matumaini' safari hii umeboreshwa kwa upande wa burudani ambapo Mnigeria Yami Alade anatarajia kutua kutumbuiza.
Mrisho alisema kwa upande wa wasanii wa nyumbani 'ujazo'umeongezwa kwa kuwakusanya wakali watupu kuanzia waigizaji, wasanii wa muziki wa kizazi kipya hadi wanamiochezo.
Wasanii wanaoatarajiwa kupanda jukwaani siku hiyo ni pamoja na Ali Kiba, Roma Mkatoliki, Madee, Juma Nature na wengineo kibao akiwamo Wema Sepetu atakayeimba na kucheza nyimbo za 'baby' wake, Diamond Platnumz.
"Upande wa masumbwi kutakuwa na pambano kati ya Mada Maugo na Thiomas Mashali, huku Khaleed Chokoraa aliyehamia kwenye ngumi atazipiga siku hiyo na Saim Memba, " alisema Mrisho kutoka kampuni ya Global Publishers ambao ndiyo waandaaji wa tamasha hilo la kila mwaka.
Aliongeza kuwa, Naibu Waziri wa Fedha na Mbunge, Mwingulu Nchemba atapanda ulingoni kuzipiga na Dk Hamis Kigwangala, huku wana Bongo Movie JB atazipiga na Cloud 112 na Irene Uwoya atappetana na Jackyline Wiolper.
"Pia kutakuwa na pambano la soka la Bongo Movie dhidi ya wapinzani wao Bongofleva na mechi ya wabunge wa Simba na Yanga ambao safari hii watakuwa na nyota wapya, Yanga wana Ridhiwani Kikwete na Simba wanaye Godfrey Mgimwa," alisema Mrisho.
Mwaka jana pambano la wabunge lilianzishwa na Rais Jakaya Kikwete kabla ya kupokewa na mwamuzi wa zamani wa kimataifa nchini, Othman Kazi 'Collina'.
KAJALA ampa UJUMBE mzito MWANAE akisherehekea miaka 12 ya kuzaliwa kwake
| Paula |
| Kajala na mwanae Kajala |
Katika kuikumbuka siku hiyo muhimu kwa mwanae, Kajala kupitia ukursa wake wa INSTAGRAM ameandika ujumbe maalu kwa mtoto wake kueleza magumu yao yote waliopitia tangu siku ya kwanza Paula alipokuja duniani kwa kuzaliwa mpaka sasa...Kiukweli Kajala amefunguka mengi sana.....
Fainali za Usomaji wa Qur'an Julai 25
FAINALI za kumtafuta bingwa wa kuhifadhi Q'uran kwa njia ya kughani (Tajuweed) mwaka huu zitafanyika kwenye Msikiti wa Manyema jijini Dar es Salaam, Ijumaa ya mwisho ya mfungo mtukufu wa Ramadhani Julai 25 mwezi huu.
Aidha, siku hiyo itakuwa ni sawa na funga ya 27 ya mwezi huu mtukufu wa Ramadhani, hivyo waumini wa dini ya Kiislamu watakuwa ndani ya maombi maalum maarufu kama “Lailatul Qadir” ambayo huyatumia kuomba msamaha na kufutiwa madhambi maradufu na Mwenyezi Mungu.
Hayo yalisemwa na Katibu wa Taasisi ya Kuhifadhi na Usomaji wa Kuran ya Sheikh Yahya Hussein (Sheikh Yahya Hussein Tahfidh Q’uran and Tajweed Foundation), Maalim Hassan Yahya katika taarifa aliyotuma kwenye vyombo vya habari mwishoni mwa wiki.
Maalim alisema fainali hizo zitawakutanisha washindi wote wa michuano ya kusoma Koran watakaokuwa wameshinda kwenye michuano ya taasisi mbalimbali inayoendelea hivi sasa Afrika Mashariki na Kati.
“Tutakuwa na washindanaji walioshinda kutoka nchi zote za Afrika Mashariki na Kati ambazo ni Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, Congo DRC, Sudan Kusini na Tanzania,”alisema Maalim
Aidha alisema kuwa kutakuwa na majaji kutoka nchi hizo na wengine kutoka Saudi Arabia na Iran.
Alisema kuwa ni washindi watatu wa mwanzo watapata nafasi ya kwenda Hijjah kwa gharama za taasisi yake pia watazawadiwa vyeti na fedha taslimu.
Aidha, siku hiyo itakuwa ni sawa na funga ya 27 ya mwezi huu mtukufu wa Ramadhani, hivyo waumini wa dini ya Kiislamu watakuwa ndani ya maombi maalum maarufu kama “Lailatul Qadir” ambayo huyatumia kuomba msamaha na kufutiwa madhambi maradufu na Mwenyezi Mungu.
Hayo yalisemwa na Katibu wa Taasisi ya Kuhifadhi na Usomaji wa Kuran ya Sheikh Yahya Hussein (Sheikh Yahya Hussein Tahfidh Q’uran and Tajweed Foundation), Maalim Hassan Yahya katika taarifa aliyotuma kwenye vyombo vya habari mwishoni mwa wiki.
Maalim alisema fainali hizo zitawakutanisha washindi wote wa michuano ya kusoma Koran watakaokuwa wameshinda kwenye michuano ya taasisi mbalimbali inayoendelea hivi sasa Afrika Mashariki na Kati.
“Tutakuwa na washindanaji walioshinda kutoka nchi zote za Afrika Mashariki na Kati ambazo ni Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, Congo DRC, Sudan Kusini na Tanzania,”alisema Maalim
Aidha alisema kuwa kutakuwa na majaji kutoka nchi hizo na wengine kutoka Saudi Arabia na Iran.
Alisema kuwa ni washindi watatu wa mwanzo watapata nafasi ya kwenda Hijjah kwa gharama za taasisi yake pia watazawadiwa vyeti na fedha taslimu.
Brazili yamtimua 'Big Phil' ni baada ya aibu aliyowapa nyumbani
![]() |
| Scolari katika picha tofauti kabla ya kutimuliwa kocha wa Brazil |
Kikosi cha kocha Scolari cha Brazil kilikuwa kikipewa nafasi ya kutwaa ubingwa wa michuano hiyo lakini kilikumbana na kipigo cha aibu cha magoli 7-1 katika nusu fainali dhidi ya waliokuja kuwa mabingwa Ujerumani. Katika kukamilisha mwisho wao mbaya, walikumbana na kipigo kingine cha 3-0 dhidi ya Uholanzi katika mechi ya kusaka mshindi wa tatu.
Scolari, ambaye aliiongoza Brazil kutwaa taji lao la tano na la mwisho la Kombe la Dunia 2002, alisema baada ya mechi hiyo kwamba atawasilisha ripoti kwa mabosi wake katika Shirikisho la Soka la Brazil (CBF) na ni wakati huo tu hatima yake itaamuliwa.
Lakini gazeti la O Globo liliripoti jana kwamba Scolari alitimuliwa Jumapili usiku. Gazeti hilo lilisema taarifa rasmi ingetoka baadaye jana.
Hapakuwa na uthibitisho kutoka CBF, wala mshauri wa habari wa Scolari.
Scolari aliichukua timu hiyo Novemba 2012 na amepoteza mechi tano tu kati ya 29 alizokuwa madarakani. Aliiongoza Brazil kutwaa Kombe la Mabingwa wa Mabara mwaka jana kwa ushindi wa kukumbukwa wa 3-0 dhidi ya mabingwa wa dunia wa wakati huo Hispania katika mechi ya fainali.
Alikuwa ni mtu anayependwa sana Brazil kwa ucheshi wake na pia kwa wachezaji ambao humchukulia kama baba yao.
Alikuwa na sapoti ya taifa kuelekea kwenye Kombe la Dunia na kulikuwa na upinzani mdogo kwa kikosi alichoteua, jambo ambalo ni nadra sana nchini Brazil, kunakofahamika kama "taifa la makocha milioni 200."
Kama kuondoka kwake kutathibitishwa, makocha wanaopewa nafasi ya mapema kama warithi wake watakuwa ni Tite, kocha ambaye aliiongoza Corinthians kutwaa Kombe la Ligi ya Klabu Bingwa Amerika Kusini (Copa Libertadores) na Kombe la Dunia la Klabu 2012, na Muricy Ramalho, ambaye ni kocha wa sasa wa klabu ya Sao Paulo.
Subscribe to:
Posts (Atom)






