HABARI zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa Katibu wa Taasisi na Jumuiya za Kiislam Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda amehamishwa toka hospitali ya Muhimbili alipokuwa amelazwa kupelekea gereza la Segerea.
Habari hizo zinasema askari Polisi wamefika hospitalini hapo na kuondoka na Sheikh Ponda ambaye jana alisomewa mashtaka akiwa kitandani.
Tunafuatilia kujua ukweli wa jambo hili sambamba na kujua kilichosababisha Sheikh huyo kukimbizwa huko wakati akiendelea kupata matibabu ya jehara alilolipata kwa kilichoelezwa kupigwa risasi na Polisi mjini Morogoro mwishoni mwa wiki wakai wa shamrashamra za sikukuu ya Eid el Fitry.
STRIKA
USILIKOSE
Thursday, August 15, 2013
LIGI DARAJA LA KWANZA KUANZA SEPT 14
Na Boniface Wambura
MICHUANO
ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) inayoshirikisha timu 24 zilizogawanywa
katika makundi matatu msimu huu (2013/2014) itaanza kutimua vumbi
Septemba 14 mwaka huu.
Kila
timu itakayoongoza kundi lake katika ligi itakayochezwa kwa mikondo
miwili (nyumbani na ugenini) ndiyo itakayopanda daraja kucheza Ligi Kuu
ya Vodacom (VPL) msimu wa 2014/2015.
Mechi
za ufunguzi kwa kundi A zitakuwa kati ya Tessema vs Green Warriors
(Uwanja wa Karume, Dar es Salaam) wakati Septemba 15 mwaka huu ni
Transit Camp vs Polisi Dar (Uwanja wa Mabatini, Pwani), Ndanda vs
Friends Rangers (Uwanja wa Nangwanda, Mtwara) wakati Villa Squad vs
African Lyon itachezwa Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
Kundi
B ni Burkina Faso vs Polisi Moro (Uwanja wa Jamhuri, Morogoro), Mkamba
Rangers vs Lipuli (Uwanja wa CCM Mkamba, Morogoro), Majimaji vs Mlale
JKT (Uwanja wa Majimaji, Songea) wakati Septemba 15 mwaka huu Kimondo SC
vs Kurugenzi (Uwanja wa Sokoine, Mbeya).
Mechi
za ufunguzi kundi C ni Polisi Mara vs Polisi Dodoma (Uwanja wa Karume,
Musoma), Kanembwa JKT vs Polisi Tabora (Uwanja wa Lake Tanganyika,
Kigoma), Stand United vs Mwadui (Uwanja wa Kambarage, Shinyanga), na
Pamba vs Toto Africans (Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza).
Mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo utamalizika Oktoba 26 mwaka huu wakati wa pili utamalizika Machi 22 mwakani.
Wednesday, August 14, 2013
Serikali yaingilia kati mzozo wa Yanga na Azam Media
Kwa mujibu wa chanzo cha habari cha mtandao huu, klabu ya Yanga ni kama imeibuka kidedea kwenye madai yake ya kupinga utaratibu mzima wa mkataba huo baina ya kamati ya ligi na Azam Media.
Hii inakuja baada maamuzi ya mkutano huo kuamuru kwamba vipengele vya mkataba huo kupitiwa upya na klabu ya Yanga na Kamati ya Ligi na vile ambavyo vitaonekana kuwa na matatizo virekebishwe.
Pia imeamuliwa kwamba Yanga SC itakaa kikao na Azam Media kuzungumzia mambo mbalimbali ambayo Yanga imeonekana kuwa na shaka nayo kuhusu Azam pamoja na maslahi ya Yanga kupitia dili hilo la ununuaji wa haki za matangazo ya TV ya mechi za ligi uliofanywa na Azam Media.
Shafii Dauda
Ni Mauaji Kila Kona Mbeya
Dunia Imeisha! 'Babu' mbaroni kwa kubaka 'vijukuu'
MBAKAJI
ERASTO MWAKYOMO (50) ANAYETUHUMIWA KWA UBAKAJI AKIWA KATIKA OFISI YA
MWENYEKITI WA MTAA WA MAPELELE KABLA YA KUCHUKULIWA NA MWENYEKITI WA
DAWATI LA WATOTO NA UKATILI WA KIJINSIA MARY GUMBO.
WATOTO WALIOKUWA WAKIBAKWA WAKITOA MAELEZO JINSI WALIVYOKUWA WAKITENDEWA
MWENYEKITI WA MTAA WA MAPELELE CHRISTOPHER MWAKIBETE AKIANDIKA BARUA KWA WAZAZI NA MTUHUMIWA KUPELEKWA POLISI
BAADHI YA WAZAZI NA NDUGU WA WATOTO WAKIWA NYUMBANI KWA MWENYEKITI WA MTAA.
***************
Ezekiel Kamanga
ERASTO MWAKYOMA mwenye umri wa miaka hamsini mkazi wa mtaa wa Mapelele Kata ya ILEMI jijini Mbeya anahojiwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kuwadhalilisha watoto wawili wa kike wote wakazi wa Mapelele.
Wazazi wa watoto hao baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa
watoto hao ambao mmoja ana umri wa miaka minne na mwingine mitano walitoa
taarifa kwa Balozi wa mtaa Bwana CASIAN MWEZIMPYA ambapo baada ya kutafakari
kwa kina aliamua kulipeleka suala hilo kwa Mwenyekiti wa Mtaa.
Mwenyekiti wa mtaa Bwana CHRISTOPHER MWAKIBETE Aliamua
kuwaita wazazi na mtuhumiwa kuwahoji yaliyotukia ambapo nao watoto walipewa
nafasi ya kueleza ambao walieza kuwa ERASTO Alikuwa akiwashika sehemu za siri
na kuwapaka mafuta kabla ya kufanya nao mapenzi.
Baada ya kusikiliza kwa makini MWAKIBETE aliamuru kuwa suala
hilo ni la kisheria na kitaalamu hivyo hawezi kuchukua hatua zozote bali suala
hilo analazimika kulipeleka Polisi ambapo Mwenyekiti wa Dawati la watoto na
jinsia MARY GUMBO Alimchukua mtuhumiwa hadi kituo cha Polisi kati.
Baada ya mahojiano ya awali GUMBO aliwachuchukua watoto hadi
Hospitali ya Rufaa kwa uchunguzi na mtuhumiwa kubaki kituo cha kati kwa
mahojiano zaidi,hata hivyo uchunguzi umebaini kuwa baadhi ya watoto mtaani hapo
wamekuwa wakitendewa vitendo vya ukatili lakini vimekuwa vikifumbiwa macho na
baadhi ya wazazi wakihisi ni aibu kwa watoto wao.
Na Mbeya yetu Blog
BREAKING NEWS!! UZEMBE WA TANESCO WASABABISHA KIFO CHA BINTI WA MIAKA 26 JIONI HII MBALIZI MBEYA
HAPA NDIPO MAREHEMU ALIPOGUSA NA KUKUTWA NA MAUTI
NYAYA
ZA UMEME AMBAZO ZIMENING'INIA MITA MOJA KUTOKA USAWA WA ARDHI
ZIMESABABISHA KIFO CHA NEEMA B. KIPENYA (26) ALIPOTELEZA NA KUKAMATA
NYAYA HIZO KISHA KUFARIKI PAPO HAPO.
KATI
YA NGUZO HADI NGUZO NI UMBALI WA ZAIDI YA MITA 75 MAHALI AMBAPO
PALIPASWA KUWA NA NGUZO TATU LAKINI IKAWEKWA NGUZO MOJA , HALI MTEJA WA
ENEO HILO ALIKUWA AMELIPIA NGOZO TATU ZAIDI YA MIAKA MIWILI ILIYOPITA .
HAPA NDIPO ALIPO TELEZA MAREHEMU NEEMA NA KUANGUKIA NGUZO HIZO
ASKARI AKIPATA MAELEZO KUTOKA KWA MASHUHUDA
MWENYEKITI
WA KIJIJI CHA MSHIKAMANO BWANA KISMAN MWANGOMALE AMBAYE NDIYE MTEJA WA
KWANZA KULIPIA TANESCO NGUZO TATU NA KUFUNGWA NGUZO MOJA , NA AMETOA
TAARIFA MARA KADHAA TANESCO NA HATA KUANDIKA BARUA KWA NIABA YA KIJIJI
LAKINI HAKUNA UTEKELEZAJI ULIOFANYIKA HADI MADHARA YAMETOKEA NDIPO
TANESCO WAMEFIKA.
MMOJA
KATI YA WATUMISHI WA TANESCO AMBAYE ALIFIKA ENEO LA TUKIO NA KUKATA
UMEME USILETE MADHARA ENEO HILO , HATA HIVYO ALINUSURIKA KUPIGWA NA
WANANCHI WENYE HASIRA KALI AMBAO WALIKERWA NA TUKIO HILO.
MWENYEKITI
WA KIJIJI CHA MSHIKAMANO WA KWANZA KUSHOTO NA WATUMISHI WA TANESCO
WAKIANGALIA NGUZO ZILIZO ELEMEWA NA UZITO WA NYAYA HIZO NA KUSABABISHA
NGUZO KUSHINDWA KUHIMILI UZITO WA NYAYA HIZO.
WAOMBOLEZAJI WAKILIA KWA UCHUNGU KWANI MUDA MFUPI ULIOPITA WALIKUWA NA MAREHEMU NYUMBANI HAPO.
MOJA KATI YA NDUGU AMBAYE ALIZIRAI KATIKA ENEO LA TUKIO
MWILI
WA MAREHEMU UKIWA KATIKA CHUMBA CHA MAITI HOSPITALI YA IFISI ILIYOKO
WILAYA YA MBEYA UKISUBIRI UCHUNGUZI ZAIDI WA KITABIBU.
PICHA NA EZEKIEL KAMANGA
SHEIKH PONDA ASOMEWA MASHITAKA AKIWA HOSPITALI
Katibu Mkuu wa Jumuiya na
Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda amesomewa mashitaka
ya uchochezi na Mwanasheria wa serikali, akiwa wodini MOI anapoendelea
kupata matibabu. Sheikh Ponda arijeruhiwa Jumamosi iliyopita akiwa
katika mhadhara wa Kiislamu huko mkoani Morogoro. Baada ya kujeruhiwa
Ponda alilazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili kabla ya kuhamishiwa
katika Taasisi ya Mifupa (MOI) aliposomewa mashitaka. Kesi yake
itaendelea pindi atakapopata nafuu.UCHAGUZI TFF SASA KUFANYIKA OKTOBA 18, USAJILI KUPITIWA IJUMAA
Na Boniface Wambura
KAMATI
ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imetoa
tangazo la uchaguzi wa Kamati ya mpya ya Utendaji ambao utafanyika
Oktoba 20 mwaka huu. Pia Kamati hiyo imetoa tangazo za uchaguzi wa Bodi
ya Ligi Kuu ya Tanzania (TPL Board) ambao utafanyika Oktoba 18 mwaka
huu.
Akitangaza
mchakato huo wa uchaguzi leo (Agosti 14 mwaka huu) jijini Dar es
Salaam, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Hamidu Mbwezeleni amesema nafasi
zitakazogombewa kwa upande wa TFF ni Rais, Makamu wa Rais na wajumbe 13
wa Kamati ya Utendaji wakiwakilisha kanda mbalimbali.
Fomu
kwa wagombea zitatolewa kuanzia Agosti 16 mwaka huu kuanzia saa 3
asubuhi hadi saa 10 kamili jioni kwenye ofizi za TFF. Mwisho wa kuchukua
na kurudisha fomu ni Agosti 20 mwaka huu. Fomu kwa nafasi ya Rais ni
sh. 500,000, Makamu wa Rais ni sh. 300,000 wakati wajumbe ni sh.
200,000.
Mbwezeleni
amesema kwa wale ambao walilipia fomu katika mchakato uliofutwa na
wanakusudia kugombea nafasi zilezile walizolipia, hawatalipia tena ada
ya fomu husika bali watatakiwa kuambatanisha risiti za malipo wakati wa
kurudisha fomu za maombi hayo ili kuthibitisha malipo yao.
Kwa
upande wa uchaguzi wa TPL Board, fomu zitaanza kutolewa Agosti 16 hadi
20 mwaka huu, na nafasi zinazogombewa ni Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti
ambapo ada ni sh. 200,000 wakati wajumbe wa Bodi ada ni sh. 100,000.
KAMATI YA SHERIA SASA KUPITIA USAJILI IJUMAA
Kamati
ya Sheria na Hadhi za Wachezaji iliyokuwa ikutane jana (Agosti 13 mwaka
huu) na leo (Agosti 14 mwaka huu) kupitia usajili wa wachezaji kwa
klabu za Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza sasa itakutana keshokutwa
(Agosti 16 mwaka huu) saa 4 asubuhi.
Mwenyekiti
wa Kamati hiyo Alex Mgongolwa amepanga tarehe hiyo mpya baada ya kikao
cha jana kushindwa kupata akidi. Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji
ina wajumbe saba, na ili kikao kiweze kufanyika ni lazima wapatikane
wajumbe kuanzia wanne.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Tuesday, August 13, 2013
Rais Kikwete akutana na vijana wachoraji walioacha kutumia dawa kulevya
Kijana
Jimmy Changchuu alieachana na matumizi ya dawa za kulevya akimkabidhi
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete picha aliyochora yeye na kijana mwenzake
wakati vijana hao walimpomtembelea Rais Ikulu jijini Dar es Salaam
leo.Vijana hao wanalelewa katika kituo cha Pilli Missanah Foundation
kilichopo Kigamboni Jijini Dar es Salaam.
Vijana
walioachana na Matumizi ya dawa za kulevya kutoka katika kituo cha
Pilli Missanah Foundation kilichopo Kigamboni jijini Dar es Salaam
wakiwa katika picha ya pamoja na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu
jijini Dar es Salaam leo.Kulia pembeni ya Rais ni Mwanzilish Kituo hicho
Bi.Pilli Missanah na watatu kushoto ni mfadhili mkuu wa kituo hicho
Bwana Zacharia Hans Poppe. Picha na Freddy Maro
Picha ya pamoja.
Kumekucha Redd's Miss Ilala 2013, kivumbi kufanyika Ijumaa hii
Warembo
wanaotarajia kushiriki Redd's Miss Ilala, wakiwa wamepozi wakati wa
mazoezi kwenye Mgahawa wa Billicanas, Dar es Salaam, tayari kwa
mashindano yatakayofanyika Ijumaa kwenye Ukumbi wa Golden Jubilee
jijini.
Warembo
wanaotarajia kushiriki Redd's Miss Ilala, wakiwa wamepozi wakati wa
mazoezi kwenye Mgahawa wa Billicanas, Dar es Salaam, tayari kwa
mashindano yatakayofanyika Ijumaa kwenye Ukumbi wa Golden Jubilee jijini
Warembo wakiwa katika moja ya miondoko wakati wamazoezi
Mwalimu wa warembo hao, Akhsas Peter akiwapanga vizuri kabla ya kupigwa picha na wandishi wa habari.
Warembo wakipita Mtaa wa Makunganya katikati ya Jiji la Dar es Salaam, wakitokea mazoezini katika Mgahawa wa Billicanas.
Mwandishi
Mwandamizi wa Habari za Michezo wa gazeti la Jambo Leo, Asha Kigundula
(kulia), akitoa maelezo kuhusu kazi za kila siku za waandishi wa habari
kwa warembo wa wanaotarajia kushiriki mashindano ya Redd,s Miss Ilala
walipotembelea chumba cha habari cha Jambo Leo
Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Jambo Concepts Tanzania Limited (JCTL),
Juma Pinto (aliyekaa kulia), akizungumza na warembo hao waliomtembelea
ofisini kwake, Dar es Salaam. Aliyekaa katikati ni Mratibu wa mashindano
hayo, Juma Mabakila. JCPL ni wachapishaji wa magazeti ya Jambo Leo,
Staa Spoti, Dar Metro na jarida la Jambo Brand Tanzania.
Mchakato wa Uchaguzi Mkuu TFF kuweka hadharani kesho
MCHAKATO wa uchaguzi wa kamati mpya ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) unatarajiwa kutangazwa kesho (Agosti 13 mwaka huu).
Mwenyekiti
wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Hamidu Mbwezeleni atakutana na Waaandishi
wa Habari kwenye ofisi za TFF saa 6 kamili mchana ambapo mbali ya
mchakato utakavyokuwa anatarajia kutangaza tarehe mpya ya uchaguzi huo
ambao awali ulitarajiwa kufanyika Septemba 29 mwaka huu.
Kamati
ya Uchaguzi ya TFF ilikutana Jumapili (Agosti 11 mwaka huu) na
inatarajia kuwa na kikao kingine leo (Agosti 12 mwaka huu) ambapo pamoja
na mambo mengine itazungumzia maandalizi ya uchaguzi huo.
Mbali
ya Mbwezeleni, wajumbe wengine wa Kamati hiyo ni Moses Karuwa (Makamu
Mwenyekiti), Mohamed Sinani, Chabanga Dyamwale na Kitwana Manara.
MAGORI, LINA WAINGIA KAMATI ZA CAF
Watanzania
Crescentius Magori na Lina Kessy wameteuliwa kuwa wajumbe kwenye kamati
ndogondogo (standing committees) mpya za Shirikisho la Mpira wa Miguu
Afrika (CAF) zilizotangazwa juzi na Katibu Mkuu wa shirikisho hilo
Hicham El Amrani.
Magori
na Lina ambao ni wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF watakuwa kwenye
kamati hizo kwa kipindi cha miaka miwili (2013-2015). Magori ameteuliwa
kuwa mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Mashindano ya Mpira wa Miguu wa
Ufukweni (Beach Soccer) wakati Lina ameingia kwenye Kamati ya Maandalizi
ya Mpira wa Miguu kwa Wanawake.
Makamu
wa Rais wa TFF, Athuman Nyamlani ameteuliwa tena kuwemo kwenye Bodi ya
Rufani ya CAF yenye wajumbe 12 kwa kipindi kingine cha miaka miwili.
Nyamlani alikuwepo kwenye bodi iliyopita, na itaendelea kuwa chini ya
uenyekiti wa Prosper Abega kutoka Cameroon.
Rais
wa TFF, Leodegar Tenga ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya
CAF yuko kwenye kamati tano za Shirikisho hilo. Kamati hizo ni Kamati ya
Fedha ambayo ni Makamu Mwenyekiti na Kamati ya Maandalizi ya Fainali za
Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN).
Kamati
nyingine ni Kamati ya Masoko na Televisheni ambayo ni Mwenyekiti,
Kamati ya Ufundi na Maendeleo, na Kamati ya Ushauri na Vyama Wanachama
wa CAF.
KAMATI YA SHERIA KUPITIA USAJILI
Kamati
ya Sheria na Hadhi za Wachezaji chini ya Mwenyekiti wake Alex Mgongolwa
inakutana leo jioni (Agosti 13 mwaka huu) na kesho (Agosti 14 mwaka
huu) kupitia na kufanyia uamuzi usajili wa wachezaji wenye matatizo.
Hatua
ya kwanza ya usajili imeshamalizika wakati hatua ya pili ya usajili
inaanza kesho (Agosti 14 mwaka huu) ikihusisha wachezaji ambao watakuwa
hawajasajiliwa katika Ligi Kuu ya Vodacom msimu huu na wale kutoka nje
ya Tanzania.
Hivyo,
dirisha la uhamisho kwa wachezaji wa kimataifa litafungwa baada ya
hatua ya pili ya usajili kumalizika Agosti 29 mwaka huu.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
CHADEMA yalaani tukio la kupigwa risasi kwa Sheikh Ponda
CHAMA cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA) kimeungana na vyama na asasi nyingine kulaani vikali tukio la kupigwa kwa risasi na Polisi kwa Katibu wa Jumuiya ya Kiislam Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda.
CHADEMA imelaani tukio hilo katika tamko lake iliyolitoa leo kupitia Mjumbe wake wa Kamati Kuu, Prof Abdallah Safari.
Kagera Sugar yamaliza ziara Uganda kwa kipigo
BAADA ya jana kuinyuka Bunawaya ya Uganda katika mechi zake za kirafiki za kimataifa za kujiandaa na Ligi Kuu Tanzania Bar, timu ya Kagera Sugar jioni ya leo imemaliza mechi zake nchini humo kwa kucharazwa bao 1-0 na Watoza Ushuru wa URA.
Kagera itakayofungua dimba la ligi kuu Agosti 24 dhidi ya Mbeya City, jana iliitafuna Bunawaya kwa bao 1-0 ikiwa ni mechi yao ya pili baada ya ile ya awali kulazimishwa 0-0, leo ilishindwa kuendeleza ubabe kwa URA ambao waliifunga Simba na kutoka sare ya 2-2 na Yanga kabla ya kulala kwa Coastal Union ilipokuwa nchini Tanzania mwezi uliopita.
Hata hivyo kocha msaidizi wa Kagera, Mrage Kabange amesema wanashukuru mechi hizo zimewasaidia kujiweka vyema na kuwaandaa vizuri wachezaji wao kabla ya kuanza kipute cha ligi msimu mpya.
Msimu uliopita Kagara Sugar ikiwa chini ya kocha King Abdallah Kibadeni, ilimaliza ligi ikiwa nafasi ya nne, ikitanguliwa na vigogo, Yanga, Azam na Simba zilizokuwa kwenye Tatu Bora.
Ashanti wawafuata mabingwa wa Kagame Bunjumbura
KIKOSI cha timu ya Ashanti inaatarajiwa kuondoka mjini Kigoma kesho kuelekea Burundi kwa ajili ya mechi mbili za kirafiki za kimataifa dhidi ya wenyeji wao, ili kujiandaa na pambano lao la fungua dimba kati yao na Yanga.
Ashanti iliyorejea Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu baada ya awali kushuka mwaka 2007 itapepetana na Yanga Agosti 24 katika moja ya mechi za fungua dimba, mchezo utakaochezwa katika uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Timu huyo ilikimbilia Kigoma kuweka kambi na kesho itaavuka mpaka kuelekea katika mji wa Makamba kuumana na timu ya Daraja la Kwanza nchini Burundi iitwayo Makamba.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Kigoma ni kwamba mechi hiyo itachezwa keshokutwa mjini humo kabla ya Ashanti United kusogea mbele hadi Bunjmbura mwishoni mwa wiki na kuvaana na Mabingwa wa Kombe la Kagame 2013, Vital'O.
Kocha wa timu hiyo Mbaraka Hassain anaamini mechi hizo zitawasaidia kuwaweka vyema kabla ya kuwavaa Yanga ambao Jumamosi itajitupa uwanja wa Taifa kupapatana na Azam katika pambano la Ngao ya Hisani litakalochezwa uwanja wa Taifa.
Azama waliokuwa Afrika Kusini kwa ajili ya kambi yao ya mazoezi na kucheza mechi nne za kirafiki na kushinda moja na kupoteza tatu, imetua leo mchana na tayari imejichimbia katika kambi yao iliyopo Chamazi, nje ya jijini tayari kuwasubiri Yanga Jumamosi.
Haya ndiyo majina ya wanaodaiwa wauza Unga na Bangi nchini
Majina ya
watanzania 255 wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya yamejulikana
na JAMHURI imeamua kuyachapisha...
Uchunguzi
uliofanywa umebaini kuwa kwenye orodha hiyo wapo watu maarufu na baadhi
wamekuwa wakitoa misaada ,huku wengine wakijifanya ni wazee wa kanisa na kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii....
Uchunguzi
wetu usio na chembe ya shaka unaonesha
kuwa orodha hii ya watu watakaoandikwa hapo chini kwa sasa wapo chini ya uangalizi
wa mahakama na polisi..
"Ni
kweli kuna watu tumewapeleka mahakamani, huko wamewekwa chini ya uangalizi na
wanatakiwa kuripoti kwa muda wanaopangiwa.Tunafanya hivyo baada ya
uchunguzi wetu kubaini kwa ni kweli
wanahusika na biashara hii haramu."Alisema Nzowa
Nzowa
aligoma kuyataja majina hayo, lakini uchunguzi uliofanywa na JAMHURI kutoka ndani ya jeshi la polisi na mahakama
umefanikiwa kuyapata majina
hayo...
Katika
orodha hii, yumo mchungaji aliwekwa chini ya uangalizi , na baada ya kumaliza
muda huo, siku tatu baadaye alikamatwa na
dawa nchini Brazil.Pia yumo Sheikh anayetoa misaada mbalimbali,lakini
baada ya kukamatwa na dawa kilo 211, eneo la Kunduchi Dar es salaam, kwa
sasa amekimbilia Afrika kusini....
DAWA
ZINAVYOINGIZWA NCHINI:
Hadi sasa kiwango
kikubwa cha dawa za kulevya kinaingizwa nchini kwa njia ya meli katika bahari
ya Hindi.
Baada ya
meli kuwasili Tanzania, wasafirishaji hutumia boti ndogo ziendazo kasi kuchukua
dawa hizo.Maeneo yanayotumiwa zaidi kuingiza dawa ni Bagamoyo, Zanzibar, Tanga
na Mtwara....
Jijini Dar,
boti hizo hutia nanga katika eneo
la Bagamoyo ambako pia ndiko kwenye njia
kuu ya uingizaji wa bidhaa za magendo zisizolipiwa kodi...
Biashara hiyo
haramu huwahusisha baadhi
ya polisi ambao
mara kadhaa wamekuwa
wakiwapa ulinzi wahalifu
hao.
Viwanja vya
ndege vinavyotumiwa kuingiza
madawa ya kulevya
ni Julius Nyerere ( DAR ) na
Abeid Amani Karume ( ZANZIBAR)
Taarifa toka
kitengo cha kuzuia
dawa za kulevya
zinasema kuwa wasafirisha
wanaotumia ndege wamekuwa
wakibuni mbinu mbali
mbali zikiwemo za
kutumia manukato kwa
ajili ya kuwapumbaza mbwa wenye
mafunzo ya kubaini
madawa ya kulevya....
Habari
zaidi zinasema kuwa
kitengo kimepata vifaa
maalumu vya kubaini
kama ndani ya
mizigo kuna madawa
ya kulevya. Vifaa hivyo
ni mfano wa
sindano ambayo huchomwa
kwenye mizigo na
kuipitisha kwenye ngozi
ya mwili.
Kama kuna
dawa, ikigusishwa kwenye ngozi unga hupukutika
na kama mzigo
hauna dawa za
kulevya basi hakuna
kitakachotokea....
Tayari vifaa
hivyo vimeanza kutumika
katika uwanja wa
kimataifa wa Julius Nyerere.
Lisake gazeti la Jamhuri utaiona orodha nzima ya majina hayo 250.
Source: Gazeti la Jamhuri.
Monday, August 12, 2013
Sheikh Ponda chini ya Ulinzi mkali wa Polisi, MOI
Kiongozi wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania Sheikh Ponda Issa
Ponda akiwa amelazwa kwenye chumba maalumu katika taasisi ya mifupa
Muhimbili (MOI), muda mfupi baada ya kufikishwa hospitalini hapojana.
Picha na Venance Nestory.
KATIBU wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu
Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda yupo chini ya ulinzi huku akitibiwa
majeraha katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Sheikh Ponda alisafirishwa usiku wa manane kutoka
Morogoro baada ya juzi kupigwa na kitu kinachodaiwa kuwa ni mtutu wa
bomu saa 12:25 jioni alipokuwa akisind
ikizwa na wafuasi wake kwenda katika Msikiti wa Mungu Mmoja Dini Moja mara baada ya kumaliza kutoa mhadhara katika kongamano mjini hapo.
ikizwa na wafuasi wake kwenda katika Msikiti wa Mungu Mmoja Dini Moja mara baada ya kumaliza kutoa mhadhara katika kongamano mjini hapo.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa Kongamano hilo, Sheikh Idd Mussa Msema, alidai kuwa Sheikh Ponda alipigwa risasi tatu begani.
Taarifa kutoka ndani ya familia ya Ponda zilisema
kwamba baada ya kupata taarifa za kupigwa risasi, baadhi ya masheikh
walifunga safari kwenda Morogoro na kumrejesha Dar es Salaam usiku
huo huo. Kabla ya kurudishwa Dar es Salaam, imeelezwa kuwa Sheikh Ponda
alipelekwa katika Zahanati ya Islamic Foundation.
Mmoja wa wanafamilia alidokeza kwamba Sheikh Ponda
alifichwa na alikuwa chini ya ulinzi mkali wa wafuasi wake na hakuna
aliyeruhusiwa kumsogelea.
Muhimbili
Hata hivyo, habari zilizopatikana baadaye jana
zilisema kuwa alifikishwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya
kupatiwa matibabu.
Sheikh Ponda alifikishwa Muhimbili jana saa 7:18
mchana na alipelekwa kwenye chumba cha wagonjwa wa dharura na baadaye
alitolewa na kupelekwa kwenye chumba cha x-ray kwa ajili ya vipimo.
Baadaye alipelekwa chumba cha upasuaji.
Eneo kubwa la hospitali hiyo lilikuwa na idadi
kubwa ya askari na mmoja wa askari waliokuwa doria hospitalini hapo
alisema walitawanywa kwenye hospitali mbalimbali za Dar es Salaam baada
ya kupata taarifa kuwa angeletwa kwa matibabu.
“Nakuambia tuko hapa tangu saa kumi na moja
asubuhi, tumetawanywa hospitali mbalimbali baada ya kupata taarifa kuwa
analetwa Dar. Bahati nzuri kaletwa hapa Muhimbili... tunasubiri apate
matibabu na tutamtia mbaroni,” alisema askari huyo.
Taarifa ya polisi
Msemaji wa Polisi, Advera Senso alisema jana
katika taarifa yake kuwa Sheikh Ponda yuko Hospitali ya Muhimbili
akitibiwa baada ya kupata majeraha yaliyotokana na purukushani na polisi
wakati wafuasi wake walipokuwa wanataka kumtorosha.
MWANANCHI.
Njemba yafia gesti ikifanya mapenzi na demu wake
MFANYABIASHARA wa sokoni Kariakoo jijini Dar ambaye pia ni mkazi wa Kigogo Flesh, Hamad Kiponda (46), amefia nyumba ya kulala wageni akiwa na mpenzi wake Latifa Saidi (25).
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi alisema tukio hilo lilitokea juzi saa saba mchana katika nyumba hiyo iitwayo Sansiro iliyoko Kiwalani kwa Gude.
Alisema kuwa kutokana na tukio hilo, Latifa alitoa taarifa polisi kwamba mpenzi wake aliishiwa na nguvu ghafla na kuanza kutokwa povu mdomoni wakati wakifanya mapenzi.
Minangi alieleza kuwa mtoa taarifa huyo aliomba msaada kwa wahudumu wa gesti hiyo, lakini Kiponda alifariki papo hapo kabla ya kupelekwa hospitali.
Chanzo cha kifo chake bado hakijafahamika, wakati mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa uchunguzi zaidi huku Latifa akishikiliwa kwa kuhojiwa.
Wakati huo huo, moto umezuka ghafla katika nyumba ya Matiku Nestori (43) mkazi wa Tuamoyo Kigamboni, yenye vyumba sita na kuteketeza vyumba vinne pamoja na mali zote zilizokuwemo ndani ambazo bado thamani yake haijajulikana.
Kwa mujibu wa Kamanda Minangi tukio hilo lilitokea juzi saa nane mchana na chanzo cha moto huo inasadikiwa ni hitilafu ya umeme iliyosababisha moto kuanzia kwenye nguzo.
Tanzania One
Papii Catalogue sasa aamua kuwatetea wanawake
| Catalogue akizungumza kueleza |
Catalogue aliutaja wimbo huo ni 'Mwanamke Hapigwi' ambao una mashairi unaohimiza wanaume kuacha kutumia ubabe kwa wanawake kama kuwapiga, kuwanyanyasa na kuwaona hawana maana kwa sababu wanawake wanahitaji kutunzwa na kubembelezwa na kama kupigwa basi hupigwa kwa upande wa khanga.
Rapa na muimbaji huyo alisema wimbo huo ameutunga maalum katika kuwapigania wanawake katika zama hizi za matukio ya unyanyasaji dhidi yao hasa majumbani na katika mapenzi.
Catalogue alisema wanaume wamekuwa na desturi ya kuwapiga na kuwanyanyasa wanawake na wapenzi wao na ikitokea wanawake hao wakachoka na kuamua kuwakimbia kwa wanaume wengine wanaojua kuibembeleza wanaume wa awali huona kama wameonewa na kuanzisha songombingo.
"Huu ni wimbo maalum kwa ajili ya kutetea wanawake ni utatambulishwa sambamba na rapu mpya iitwayo 'Utaishije mjini bila ya kazi'," alisema.
Katika hatua nyingine dansa kiongozi wa bendi hiyo, Hassain Mussa 'Super Nyamwela' ametamba kuwa ujio wa wanenguaji wawili wapya kutoka Kongo, Jolie Kindu 'Mrisho Ngassa' na Grace Kamba 'John Bocco' kutazidi kuipaisha bendi yao huku akiwapiga vijembe wapinzani wao kuwa wataishia 'kukopi na kupesti'.
Nyamwela alisema ukali walionao madansa hao wa kike utaiweka kileleni Extra Bongo na kuthibitisha kuwa wao siku zote ni wa kwanza katika safu ya unenguaji kwa sababu wapo chini ya mwalimu asiyechuja (yaani yeye Nyamwela).
Kocha Liver amuwakia Suarez, amtaka aombe radhi
| Kocha wa Liverpool |
KOCHA wa Liverpool, Brendan Rodgers amemweleza mshambuliaji Luis Suarez kwamba ni lazima aombe radhi kwa kutaka kulazimisha kuihama klabu hiyo.
Suarez (26) amekuwa akifanya mazoezi peke yake baada ya kutaka kulazimisha kuhama Anfield katika kipindi hiki cha usajili.
"Kwanza anapaswa kuomba radhi kwa wachezaji wenzake na klabu," alisema Rodgers alipoulizwa kwamba nini kinachofuata anachopaswa kufanya mshambuliaji huyo.
Ofa mbili za Arsenal zikimekataliwa na Liverpool kwa ajili ya mshambuliaji huyo wa Uruguay.
"Nimemuona kwa muda. Najua huyu si Luis Suarez tunayemfahamu na ni kazi yangu kuwalinda mashabiki na wachezaji kwa sababu wanastahili zaidi ya hilo," aliongeza Rodgers.
Kocha huyo wa Liverpool alikuwa akizungumza baada ya timu yake kula kipigo, bila ya Suarez, cha goli 1-0 dhidi ya Celtic katika mechi yao ya mwisho ya ya kirafiki ya kujiandaa na msimu juzi.
"Amekuwa kwa siku kadhaa akifanya mazoezi peke yake," alisema Rodgers, ambaye atamkosa Suarez wiki hii kwa vile anasafiri na timu yake ya taifa ya Uruguay kwenda kucheza mechi ya kirafiki nchini Japan wiki hii.
"Atakaporejea kutoka katika mechi ya kimataifa tunamuangalia kuanzia hapo."
Pigo la karibuni zaidi katika matumaini ya Suarez' ya kuondoka Anfield lilikuja siku moja tu baada ya Rodgers kumtaka akubali kwamba hatauzwa, pale mmiliki wa Liverpool, John Henry aliposema kwamba nyota huyo hatauzwa kwa pesa yoyote kwa klabu yoyote hata nje ya Uingereza.
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger, ameendelea kusema kwamba bado wanamhitaji mchezaji huyo huku ripoti zikisema kwamba klabu hiyo ya London inapanga kumfanya Suarez kuwa ndiye mchezaji anayelipwa pesa nyingi zaidi klabuni hapo kwa kumpa mshahara wa paundi 160,000 kwa wiki endapo atajiunga nao.
(Sunday Mirror)
Subscribe to:
Posts (Atom)









