STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, November 10, 2013

Al Ahly Mabingwa wa Afrika kwa mara ya Nane

Al Ahly celebrate their record seventh African Champions League victory
Al Ahly walipokuwa wakishangilia taji lao la mwaka jana
KLABU ya Al Ahly ya Misri imeweka rekodi ya kutwaa taji la nane la Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya hivi punde kupata ushindi wa mabao 2-0 na kushinda kwa jumla ya mabao 3-1 dhidi ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini.
Mabao mawili kupitia kwa nyota wake, Mohammed Aboutrika katika dakika ya 54 na jingine la Ahmed Abdul Zaher la dakika ya 78 limetosha kuwapa Wamisri hao taji hilo na kuwaacha mbali wapinzani wao katika michuano hiyo Zamalek iliyotwaa taji hilo mara tano.
Pirates waliolazimishwa sare ya 1-1 nyumbani kwao katika pambano la kwanza la Fainali hizo za Afrika, hawakuonyesha kama walikuwa na nia ya kutwaa taji kwa mara ya pili kutokana na kufunikwa na wenyeji.
Kwsa ushindi huo Al Ahly licha ya kunyakua donge nono la ushindi wa kwanza, lakini imezidi kuboresha rekodi yao ya kunyakua taji hilo baada ya kufanya hivyo katika miaka ya 1982, 1987, 2001, 2005, 2006, 2008 na 2012 kabla ya leo tena kunyakua kwa mara ya nane.

No comments:

Post a Comment