STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, November 10, 2013

Inasikitisha! Walimu wafa ajalini


AJALI za barabarani zimeendelea kuchukua roho na watanzania wenzetu baada ya walimu wakuu watatu wa Shule tofauti za Tarafa za Magole, wilayani Kilosa kufariki katika ajali mbaya.
Taarifa kutoka Morogoro zinasema kuwa walimu hao watatu ambao majina yao yametajwa kuwa ni Mwl Margareth Kimbo, Mwl Agrey Kikwesha na Mwl Lanford Mhando waliaga dunia baada ya gari walilokuwa wakisafiria nalo lililobeba walimu wengine kupasuka tairi na kupinduka.
kutoka shule mbalimbali za Tarafa ya Magole wilayani Kilosa, wamefariki dunia baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupata ajali.
Walimu wengine 17 waliokuwa katika gari hilo wamejeruhiwa baadhi hali zao zikielezwa kuwa mbaya na wamelazwa hospitalini.

Walioshuhudia wandai ajali hiyo ilitokea katika kijiji cha Mvumi, Rudewa eneo la Kisangata mkoani Morogoro wakati walimu hao walipokuwa wakiitikia wito wa ghafla toka kwa Mkuu wa Wilaya hiyo.
Inaelezwa kuwa walimu na waratibu zaidi ya 17 walikuwa katika gari hilo aina ya Toyota Hiace kabla ya tairi ya nyuma kupasuka na gari kuringika mara nne na kupelekea maafa hayo na majeruhi hao.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro Faustine Shilogile alithibitisha kuhusiana na ajali hiyo aliyodai gari hilo lilipasuka tairi kabla ya kuanguka likibiringika mara kadhaa na kusababisha vifo vya walimu hao wakuu na wengine kujeruhiwa vibaya.

No comments:

Post a Comment