STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, November 10, 2013

Uchaguzi Mkuu wa TBF kufanyika Desemba 10


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Ndugu Wanahabari
Napenda kwa leo kuchukua fursa hii kutoa tangazo rasmi la tukio la uchaguzi mkuu wa viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF). Mwaka huu wa 2013 ndio ambao uongozi wa shirikisho unafikia ukomo wake, na kikatiba inabidi ufanyike uchaguzi kuwapata viongozi wapya watakaoendesha shughuli za shirikisho kwa miaka minne ijayo.
Hivyo basi, kwa niaba ya TBF natangaza rasmi kuwa uchaguzi mkuu wa viongozi wa shirikisho unatarajiwa kufanyika tarehe 10 Disemba 2013 huko mkoani Mbeya, ikiwa ni siku 30 kabla ya uchaguzi huo, ambapo kikanuni inapasa kutoa tangazo rasmi la uchaguzi. Uchaguzi huo utafanyika mara baada ya kumalizika kwa mashindano ya taifa cup ambayo mwaka huu yanafanyika mkoani Mbeya kuanzia tarehe 30 Novemba mpaka tarehe 8 Disemba 2013 huko jijini Mbeya.
Safu ya uongozi kikatiba wanaopaswa kuchaguliwa ni pamoja na:
 1. Rais
 2. Makamu wa Rais
 3. Katibu Mkuu
 4. Katibu Mkuu Msaidizi
 5. Mhazini
 6. Kamishna wa Mipango
 7. Kamishna wa Ufundi na Mashindano
 8. Kamishna wa Waalimu
 9. Kamishna wa Watoto na Mashule
 10. Kamishna wa Wanawake
 11. Kamishna wa Waamuzi
 12. Kamishna wa Tiba ya Wanamichezo
 13. Kamishna wa Walemavu
Taratibu zote za uchaguzi huu zitasimamiwa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) ambao ndio watakaokuwa wakitoa fomu za maombi ya wagombea.
Kwa niaba ya uongozi wa Shirikisho napenda kuchukua nafasi hii tena kuwaomba wadau, wapenzi wa michezo na wananchi wote kwa ujumla wenye sifa na wanaopenda kuongoza Shirikisho letu wajitokeze kwa wingi kuchukua fomu za maombi ya uongozi wa Shirikisho mara baada ya tangazo la Baraza la Michezo (BMT) la kuanza kuchukua fomu hizo kwa nafasi zote zilizo takazotangazwa. Shime wanamichezo katika kuleta mabadilko chanya katika mchezo wa mpira wa kikapu Tanzania.
Mussa Mziya
Rais
Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania(TBF

No comments:

Post a Comment