STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, November 10, 2013

Sunderland yaiduwaza Manchester City

Phil Bardsley scored
Kipa wa Manchester City Mannone akiwa haamini kama mpira unatinga wavuni kuipa ushindi Sunderland

KLABU ya Sunderland imeendelea kujitutumua katika Ligi Kuu ya England baada ya jioni hii kupata ushindi wake wa pili katika ligi hiyo kwa kuikwanyua Manchester City kwa bao 1-0.
Bao la dakika ya 21 kupitia kwa Phil Bardsley aliyemalizia kazi nzuri ya Wes Brown, lilitosha kuwafanya vijana wa Gustavo Poyet kuibuka na ushindi huo nyumbani japo haujawatoa kwenye nafasi ya pili toka mkiani licha ya kufikisha pointi 7.
Manchester City waliokuwa wapo kamili licha ya kufanya mabadiliko katika kipindi cha pili ili kutaka kurejesha bao hilo ilijikuta ikishindwa kufurukuta kwa vijana wa Poyet ambao walicheza 'ng'adu ng'adu' ili kulinda bao lao na mpaka filimbi ya mwisho ya mwamuzi Michael Dean, wenyeji waliibuka kidedea.
Kipindi hicho ambacho kimetokea muda mchache baada ya Tottenham Hotspur nao kulala kwa bao 1-0 toka kwa Newcastle United imeendelea kusalia na pointi zake 19 ikishika nafasi ya saba na kuna hatari ya kuporomoka iwapo pambano linaloendelea sasa kati ya Manchester United dhidi ya Arsenal litaisha kwa Mashetani Wekundu kushinda.

No comments:

Post a Comment