STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, November 10, 2013

Sevilla yaifumua Espanol kwao 3-1

http://www.soccersouls.com/wp-content/uploads/2013/01/1301799637-thumb02.jpg
Federico Fazio
ESPANYOL jioni hii imejikuta ikikumbana na kipigo cha paka mwizi kwa kunyukwa mabao 3-1 ikimaliza mechi yao ya nyumbani wakiwa pungufu baada ya mchezaji wake mmoja kuonyeshwa ya pili ya njano na kutolewa uwanjani na nyekundu katika mchezo uliomaliza hivi punde.
Kipigo hicho cha nyumbani Espanyol wamepewa na Sevilla ambao mpaka wakati wa mapumziko walikuwa mbele kwa mabao 2-1.
Bao la kwanza likitupiwa kambani na Federico Fazio dakika ya nne tu ya mchezo kabla ya Vitolo kuongeza la pili dakiia sita baadaye na wenyeji kupitia bao pekee kwenye dakika ya 24 kutia kwa Sergio Garcia.
Msumati wa mwisho katika jeneza la Espanyol ulipigiliwa katika dakika ya 59 na Carlos Bacca na dakika tano kabla ya mchezo kumalizika wenyeji walijikuta wakipata pengo baada ya kiungo wao Victor Sanchez kulimwa kadi nyekundu baada ya kuonyesha kadi mbili za njano ndani ya dakika tatu  ya kwanza kipewa dakika ya 82 na nyingine 85 na mwamuzi Miguel Ayza kumtoa nje.
Kwa ushindi huo Sevilla imefikisha pointi 16 ikichupa kutoka nafasi ya 14 hadi nafasi ya 10, huku wapinzani wao wakisaliwa na pointi zao 15 na kuporomoka hadi nafasi ya 12.
Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea jioni hii kwa mechi kadhaa ikiwemo ile ya mabingwa watetezi, Barcolona itakuwa ugenini kukabiliana na wenyeji wao Real Betis.

No comments:

Post a Comment