STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, November 10, 2013

Tottenham yafa tena nyumbani EPL

Newcastle United's Tim Krul (third left) punches the ball clear from Tottenham Hotspur's Younes Kaboul
Hekaheka katika lango la Newcastle United
BAO pekee lililofungwa na Loic Remy wa Newcastle United katika dakika 13 lilitosha kuipa ushindi wa ugenini timu yake walipoifuata Tottenham Hotspur kwenye uwanja wake wa White Hart Lane katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyoisha hivi punde.
Mfungaji wa bao hilo alimalizia kazi nzuri ya Youn Gouffran na kuifanya wageni kuondoka na ushindi wa bao 1-0 na kiufikisha jumla ya pointi 17 ikilingana na Manchester United ambayo baadaye itashuka dimba la nyumbani kuikaribisha Arsenal katika pambani jingine la ligi hiyo.
Kipigo hicho cha pili nyumbani kwa Spurs imeifanya ishindwe kurejea katika Tatu Bora ya ligi hiyo baada ya awali kunyukwa mabao 3-0 na West Ham mwezi uliopita na kuwa mchezo wa tatu kupoteza msimu huu katika ligi hiyo inayozidi kushika kasi.

No comments:

Post a Comment