STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, November 10, 2013

Al Ahly wazidi kulisogeza taji la Afrika


NI miujiza tu ndiyo itakayoweza kuizuia Al Ahly kutetea taji lao la ubingwa wa Afrika baada ya Ahmed Abdul Zaher kuiongezea bao la pili hivi punde na kuifanya Orlando Pirates kutakiwa kurudisha mabao hayo na kupata jingine la ziada iwapo wanataka kuivua taji Wamisri hao waliotawala sehemu kubwa ya pambano hilo linalochezwa mjini Cairo.
Zaher alifunga bao hilo dakika ya 78 na kuifanya Al Ahly kujiweka tayari kunyakua taji la nane la ubingwa huo na kuzidi kuweka rekodi kwa ngazi za klabu barani Afrika.

No comments:

Post a Comment