STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, November 10, 2013

Mashujaa wetu warejea nyumbani kuisubiri Afrika Kusini


WACHEZAJI wa timu ya Taifa ya Wanawake chini ya miaka 20, Tanzanite,
wakiwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es
Salaam, leo wakitokea nchini  Msumbiji ambako jana waliichabanga timu hiyo kwa mabao 5-1  katika mchezo wa marudiano wa raundi ya pili ya michuano ya
Kombe la kuwani tiketi ya kufuzu kucheza  kombe la Dunia.
   
Katika mechi ya awali iliyochezwa jijini Dar es Salaam, Tanzanite waliisasambua Msumbiji kwa mabao 10-0 na hivyo kusonga mbele katika michuano hiyo na sasa itakutana na Afrika Kusini iliyowang'oa Botswana. Mechi ya kwanza itachezwa uwanja wa ugenini kabla ya kurudiana nao jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment