STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, November 10, 2013

Wanawake wa3 wacharangwa mapanga, wachomwa moto kwa tuhuma za uchawi

Picha hii haihusiani na habari
WANAWAKE watatu wa Kijiji cha Nyamikoma, wilayani Busega mkoa wa Simiyu wameuwawa kikatili wakishambuliwa kwa silaha za jadi kisha kuchomwa moto kwa kutuhumiwa wanajihusisha na vitendo vya kishirikina.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka mkoani humo na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Simiyu, Salum Msangi ni kwamba wanawake hao ambao majina yao hayakupatikana mara moja wana umri kati ya miaka 30-70.
Inaelezwa kuwa kwa muda mrefu wanawake hao na mwenzao mmoja aliyenusurika na kifo walikuwa wakituhumiwa kuwafanyia wenzao ulozi na kuufanya uongozi wa kijiji hicho kuitisha mkutano ili kuwajadili.
Inaelezwa katika mkutano huo ulioitishwa na Mwenyekiti wa Kijiji uliwaamuru wanawake hao wanne kuhama kijiji hicho na wakati wakiwa katika harakati za kuhama ndipo wakavamiwa na baadhi ya wanakijiji na kuanza kuwashambulia.
Wanawake hao walishambuliwa kwa silaha kama mapanga, mawe, magogo, nondo kabla ya kuchomwa moto kama nyama ya kubanika na kupoteza uhai wao, huku pia nyumba zao zikibomolewa na watu hao waliofanya unyama huo.
Taarifa kutoka kijijini hapo zinasema kuwa kabla ya wanakijiji hao kufanya unyama huo wanadai waliwahi kumnasa mmoja wa wanawake hao aliyekuwa na umri wa miaka ya 30 akifanya ulozi katika nyumba ya wanakijiji mwenzake na kumbana kuwataja wenzake wanaoshirikiana katika vitendo hivyo.
Miongoni mwa majina 15 yaliyotajwa watatu pamoja na yeye mwenyewe ni wa kijiji hicho na ndipo ukalazimishwa kuitishwa mkutano ili kuwatimua kijijini hapo kabla ya watu wenye hasira kuwafanyia ukatili huo wa kutisha.
Kamanda wa Polisi wa Simiyu, Salum Msangi, alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema wanawashikilia watu 19 kuhusiana na mauaji hayo na wengine wakiendelea kusakwa huku wakiwaonya wananchi kuacha kutumia sheria mikononi na kuendesha ukatili kama huo.
Kamanda huyo alisema wananchi wanapaswa kuepuka imani potofu juu ya ushirikiana na kudai voitendo hivyo vimezidi kukithiri katika eneo lake na kudai Polisi inarudia kuwataka kuacha imani hizo.

No comments:

Post a Comment