STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, November 10, 2013

Mwanamke anaswa kwa wizi wa kichanga, ajitetea alitaka kulinda ndoa yake isiyo na mtoto kwa muda mrefu

MWANAMKE mmoja wa Kijiji cha Kashishi, Halima Mbuja anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kuiba mtoto mchanga.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Nzega, Tabora zilizothibitishwa na Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Peter Ouma zinasema kuwa mwanamke huyo alimuiba mtoto huyo Novemba 3 na kunaswa naye Novemba 9.
Taarifa hizo zinasema kuwa mtoto huyo aliibwa kutoka kwa mama yake aitwaye Tatu Mmbasha mara waliporuhusiwa kutoka hospitali ya wilaya ya Nzega baada ya kuzaliwa baada ya Halima kujifanya msamaria mwema na kumsaidia.
Inadaiwa baada ya kumpokea mtoto huyo, mwanamke huyo alitoweka naye na kumuacha katika hali ngumu mama mzazi wa kichanga hicho ambapo baada ya Polisi kupata taarifa ilishirikiana na wasamaria wema kumtafuta mtoto huyo na kumkuta katika kijiji cha Kashishi akiwa hai mwenye afya tele.
Kamanda wa Polisi alisema mtuhumiwa huyo alikiri kuiba mtoto huyo kwa nia ya kutaka kulinda ndoa yake ambayo ina miaka mingi, bila ya kuwa na mtoto na kwamba taratibu za kumfikisha mahakamani kwa kosa alililofanya zinafanyika.

No comments:

Post a Comment