STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, November 10, 2013

Ni Al Ahly au Orlando Pirates Ligi ya Mabingwa Afrikawa bingwa mpya Afrika

http://news.bbcimg.co.uk/media/images/70056000/jpg/_70056514_ahly_pirates.jpg

WAKATI macho na masikio ya mashabiki wa soka yakielekezwa katika pambano la kukata na shoka baina ya Arsenal itakayokuwa ugenini Old Trafford kuwakabili wenyeji wao Manchester United, Afrika leo kuna kipute cha Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Al Ahly ya Misri na Orlando Pirates ya Afrika Kusini.
Pambano hilo la marudiano baina ya timu hizo linatarajiwa kufanyika saa 1 jioni mjini Cairo, huku mabingwa watetezi, Al Ahly ikipewa nafasi kubwa ya kutetea tena taji hilo baada ya kupata sare ya 1-1 katika mechi ya kwanza iliyochezwa mjini Johannesburg, Afrika Kusini.
Mechi hiyo ambayo itachezwa kwenye uwanja wa Osman Ahmed Osman (Arab Contractors) inatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na presha kubwa walionao mabingwa wa zamani wa ligi hiyo, Orlando ambapo kocha wake Roger De Sa, ametamba anataka kuwapa raha mashabiki wake kwa kutwaa taji hilo.
Hata hivyo kikosi hicho kinapaswa kuwa makini katika pambano hilo iwapo inataka kutwaa taji mikononi mwa Al Ahly ambayoi itashuka dimba ikiwategemea nyota wake kama Mohammed Aboutrika, Wael Gomaa, Ahmed Abdul Zaher na Waleed Soliman ambao watakuwa uwanja wa nyumbani.
Sare ya aina yoyote katika pambano hilo la leo litaiwezesha wenyeji kunyakua taji kwa mara nane na kuzidi kuweka rekodi katika michuano hiyo.
Orlando Pirates iliyoanzishwa 1937 inataka kunyakua taji hilo kwa mara ya pili baada ya kufanya hivyo kwa mara ya kwanza mwaka 1995 walipoikandika ASEC Memosas kwa jumla ya mabao 3-2.

No comments:

Post a Comment