STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, November 10, 2013

Mohammed Aboutrika aisogezea taji Al Ahly

Mohammed Aboutrika

MSHAMBULIAJI nyota wa Al Ahly, Mohammed Aboutrika ameifungia bao timu yake bao dakika chache zilizopita na kuiweka katika nafasi nzuri timu yake kutetea taji la Ligi ya mabingwa Afrika na kuzidi kuimarisha rekodi yao ya kutwaa taji hilo mara nyingi kuliko timu yoyote.
Mshambuliaji huyo mkongwe aliyenyakua tuzo mbalimbali ikiwemo ya Mchezaji Bora wa Afrika wa BBC-2008 na zile za Mchezaji anayecheza nyumbani Afrika, alifunga bao hilo dakika ya 54 akimalizia pasi murua ya Abdallah Al Said na kuiweka mbele timu yake kwa mabao ya jumla 2-1, ingawa pambano bado linaendelea. Ngoja tuone inakuwaje.

No comments:

Post a Comment