STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, July 2, 2013

Hivi ndivyo Rais Obama alivyopokelewa Tanzania

RAIS OBAMA akiteremka kwenye Air Force One na mtoto wake pembeni mara baada ya kuwasili katika ardhi ya Tanzania wakati akitokea afrika ya Kusini jana mchana kwa ziara ya kikazi nchini.Barack Obama akipokewa na Wananchi wa  Tanzanian huku wanaband wakitumbuiza nyimbo mbalimbali kwenye uwanja wa Mwl.Julius Kambarage jijini Dar es Salaam jana mchana akitoka Africa kusini.


Rais Obama akipita kwenye kapeti jekundu huku akiwa na furaha na kucheza nyimbo za wabongo kwenye uwanja wa jijini Dar es salaam wa Mwl. Julius Kambarage mchana wa jana.

Karibu  Tanzania....karibu!!!

Ilikuwa ni patashika kwa wacheza ngoma hapa!!! Obama mpaka akaachia Tabasamu

Rais Obama akicheza nyimbo za hapa kwetu Bongo huku akiwa na furaha kwa mapokezi baada ya kukanyaga ardhi ya Tanzania jana.U.S. President Barack Obama participates in an official arrival ceremony at Julius Nyerere Airport in Dar es Salaam, Tanzania, July 1, 2013. REUTERS-Jason ReedU.S. President Barack Obama walks with Tanzanian President Jakaya Kikwete during an official arrival ceremony at Julius Nyerere Airport in Dar es Salaam July 1, 2013. REUTERS-Jason ReedObama na JK.U.S. President Barack Obama and first lady Michelle Obama receive flowers, as their daughter Sasha (2nd R) watches, during an official arrival ceremony at Julius Nyerere Airport in Dar es Salaam, Tanzania, July 1, 2013. REUTERS-Jason ReedKaribu Baba ! Karibu Tanzania!

Rais na First Lady Obama wakisalimia wananchi wa Tanzanian baada ya kupokewa na Rais Jakaya Kikwete na First Lady Salma
Ni furaha hapa baada ya Rais Obama kutua Bongo, hapa anaonekana na mwenyeji wake rais Jakaya Kikwete wakipokewa kwa ngoma Ni mimi jamani ...tupo pamoja !. Karibu jamani ....jaribu mzee!!! Tunakupenda!! Mapokezi haya!!! angalia mavazi!!  Rais Barack Obama wa Marekani (kushoto) akizungumza katika mkutano na Waandishi wa habari wa Tanzania na Kimataifa Ikulu Jijini Dar es Salaam jioni YA JANA ambapo mbali na kuzungumzia mstakabali wa ziara yake nchini Tanzania na Afrika pia amezungumzia masulala mbalimbali ya Kimataifa ukiwepo mgogoro na Vurugu zinazoendelea nchini Misri na Congo DRC.

Monday, July 1, 2013

Simba kutambulisha nyota wake wapya mkoani


Na Elizabeth John
KLABU ya Simba ya jijini Dar es Salaam, imesema mara baada ya kuondoka kwa Rais wa Marekani, Barrack Obama nchini, itafanya ziara katika mikoa ya Katavi, Tabora na Rukwa kwa kucheza mechi za kirafiki kwa ajili ya kujiandaa na Ligi Kuu Bara.

Mbali na kwenda katika mikoa hiyo, pia ipo katika mchakato wa kupiga kambi katika moja ya nchi jirani kwa ajili ya maandalizi zaidi ya ligi hiyo.


Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa klabu hiyo, Ismail Aden Rage alisema wamepata mwaliko kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Rajab Rutengwe akiomba timu hiyo iende mkoani kwake.


“Tumepokea mwaliko kutoka kwa rafiki yangu Shehe Rajab ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi  akituomba tukamtembelee na kikosi changu chote, na sisi tupo tayari hatuna tatizo katika hilo,”.

“Kikubwa tunachosubili kama unavyojua hivi sasa nchi ina ugeni mkubwa wa Rais Obama, hivyo kila mtu yupo katika pilikapilika hizo lakini baada ya kuondoka tutasema tarehe rasmi ya kuondoka,”.


Alisema wakiwa huko wanatarajia Waziri Mkuu, Mizengo Pinda atakuwa mgeni rasmi katika mechi watakazocheza ambapo pia waziri huyo ameiomba timu yake ifike mpaka Jimboni kwake Mpanda Magharibi, Rukwa.


Alisema wakiwa katika mikoa hiyo pia watakwenda Tabora kucheza mechi ya kirafiki na baada ya kumaliza ziara hizo watarejea jijini Dar es Salaam.


Aliongeza kuwa wapo katika mipango ya kuhakikisha timu yake inaweka kambi moja ya nchi jirani ambapo ana uhakika baada ya kufanya hivyo, kikosi chake kitakuwa tayari kwa ligi kuu ya msimu ujao.


Wakati Simba ikijinadi hivyo, watani wao Yanga, wanatarajia kuondoka Ijumaa kwenda Kanda ya Ziwa kwa ajili ya kulitembeza kombe lao la ligi kuu pamoja na kucheza mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya KCC ya Uganda.


Mbali na hayo, pia itaingiza wanachama wapya pamoja na kuuza vifaa mbalimbali walivyonavyo.

Baada ya Obama leo, George Bush, mkewe nao kutua kesho Tanzania

RAIS mstaafu wa Marekani, George W. Bush na mkewe, Laura wanatarajiwa kesho kuwa nchini kuhutubia kongamano linalojadili wajibu wa wake wa marais katika kuinua wanawake duniani.

Kuwasili kwa Bush, ni mwendelezo wa wiki hii Jiji la Dar es Salaam kuwa katika pilikapilika za kupokea ugeni wa watu maarufu. Kongamano hilo limeandaliwa na Taasisi ya George Bush na litafanyika kesho na keshokutwa.

Taarifa iliyotolewa na taasisi hiyo kwa vyombo vya habari , inasema kongamano hilo litahudhuriwa na wake mbalimbali wa marais akiwemo mke wa Rais wa Marekani, Michelle Obama.

Pia Mwanzilishi wa Taasisi ya Wanawake ya Cherie, Cherie Blair atahudhuria. Wake wa marais wa Afrika watakaohudhuria ni Mama Salma Kikwete, Chantal Campaore wa Burkina Faso, Roman Tesfaye wa Ethiopia, Maria da Luz Dai Guebuza (Msumbiji), Penehupifo Pohamba (Namibia), Sia Nyama Koroma (Sierra Leone), Janet Museveni (Uganda) na Christine Kaseba wa Zambia.

Kongamano hilo litajikita zaidi katika kujadili masuala ya kuwekeza kwa wake, kuimarisha Afrika lakini pia wajibu wa wake wa marais katika kuhamasisha wanawake katika maeneo ya elimu, afya na kuwakwamua kiuchumi.
 
Ujio wa rais huyo mstaafu wa Marekani utakuja ikiwa ni saa kadhaa tangu mrithi wake, Barack Obama kutua Tanzania kwa ziara ya siku mbili ambapo anatarajiwa kuondoka kesho baada ya kumaliza shughuli mbalimbali alizopangiwa.

MAUAJI YA KUTISHA KWA VICHANGA MKOANI MBEYA, INATISHA!

Kichanga kikiwa kinaelea kwenye mto mita chache toka eneo la Mabatini

Wakazi wa Mbeya wakishuhudia unyama aliofanyiwa kichanga hicho
Askari Polisi aklikiopoa kitoto hicho toka mtoni
ASKARI WA JESHI LA POLISI AKIWA ANAKIWEKA KICHANGA HICHO NDANI MFUKO BAADA YA KUKITOA KUTOKA MTONI
Watoto nao wakishangaa kichanga hicho kilipokuwa kikiopolewa mtoni.
Huyu ndiye aliyebainika kukitupa kichanga chooni eneo la Stereo, Maanga, mjini Mbeya
Mwenyekiti wa mtaa wa Maanga, Mary Mwansankinga akiwa haamini alichokiona machoni mwake.
Asakri wa Jeshi la Zimamoto na Ukokozi wakihangaika kutaka kukiokoa kichanga kilichotuipwa chooni.
Baadhi ya mashuhuda wa tukio la mtaa wa Maanga
Hatimaye askari wanafanikiwa kukiopoa kichanga hicho cha kiume kutoka chooni.
 BAADHI YA WAKAZI WAKISHANGAA BAADA YA KITOTO KUOPOLEWA
 ASKARI WA ZIMAMOTO BAADA YA KUOSHA KICHANGA HICHO AMBACHO  KILIZALIWA KATIKA UMRI WAKE
 WANANCHI WAKILIA KWA UCHUNGU BAADA YA KUSHUHUDIA KICHANGA HICHO BAADA YA KUOPOLEWA 
 JESHI LA POLISI PAMOJA NA ASKARI WA ZIMA MOTO WAKIONDOKA ENEO LA TUKIO
HII NI NYUMBA AMBAMO MTOTO ALITUPWA CHOONI , WATU WANAJIULIZA WENGINE WANAANDAMANA KWENYE NYUMBA  ZA MAOMBI NA WAGANGA KUTAFUTA WATOTO WENGINE WANAWATUPA BILA YA KUWA NA HURUMA WALA HOFU YA MUNGU. 

PICHA NA MBEYA YETU

Mke wa Obama akutana na Mama Kikwete WAMA


Mke wa Rais wa Markani mama Michelle Barack Obama akiwasili katika ofisi za Wanawake na Maendeleo WAMA  jioni hii wakati alipotembelea katika ofisi hiyo na kuwa na mazungumzo na mwenyeji wake Mwenyekiti wa  WAMA Mama Salma Kikwete katika makao makuu ya taaisis hiyo leo...


Rais Barack Obama na Mke wake Michelle Obama wako  katika ziara ya siku mbili ya kikazi nchini Tanzania wakiongozana  na watoto wao jioni hii ....


Rais Barack Obama atakuwa na mazungumzo na mwenyeji wake Rais Jakaya Kikwete na pia watazungumza na waandishi wa habari Ikulu kabla ya kuendelea na kazi zingine.
2 

Mama Mchelle Obama akielekea katika lango kuu la ofisi za WAMA jioni hii.3 Mama Michelle Obama akilakiwa na mwenyeji wake mama Salma Kikwete wakati alipowasili katika ofisi hizo kwa mazungumzo mafupi.

Rais Obama atua salama ardhi ya Tanzania atapa mapokezi ya aina yake

Rais Barack Obama akiburudishwa na ngoma asilia za Tanzania

clip_image001
Add caption
Rais Barack Obama wa Nchini Marekani na Mkewe Michelle Obama wakiwa sambamba na watoto wao, wakiwasili mchana huu kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam mchana huu kwa ziara ya siku mbili hapa nchini.clip_image001[6]Ndege ya Raisi wa Marekani Ikiwa Kwenye Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere, mchana huu.clip_image001[8]Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mgeni wake wa Marekani, Barack Obama aliewasili nchini Mchana huu kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.clip_image001[10]Rais Barack Obama akikagua Gwaride maalum aliloandaliwa akiongozwa na Mkuu wa majeshi ya Ulinzi, Jenelari Davies Mwamunyange.  
RAIS wa Marekani ametua nchini salama na msafara wake ikiwamo familia yake na kupokewa na mapokezi ya aina yake na watanzania wakiongozwa na Rais Jakate Mrisho Kikwete na viongozi wengine waandamizi.
Rais wa Marekani Barack Obama, amewasili katika ardhi ya Tanzania muda mchache uliopita katia kuhitimisha ziara yake barani Afrika.
Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete na familia yake pamoja na maafisa wake wa serikali na wacheza ngoma za kitamaduni walimkaribisha Obama na familia yake mjini Dar es Salaam mara aliopowasilia majira ya saa nane mchana.
Mara baada ya ukaguzi wa gwaride na mambo mengine msafara wa Rais huyo anayetokea Afrika Kusini aliambatana na mwenyeji wake kwa ajili ya kuelekea Ikulu ya Tanzania kuendelea na ratiba zake ambapo inaelezwa anatarajiwa kufanyiwa dhifa maalum jioni hii katika makazi ya rais, Ikulu.

Idadi ya wahanga waliolipukiwa mafuta Uganda yaongezeka

http://a57.foxnews.com/global.fncstatic.com/static/managed/img/fn2/feeds/AFP/660/371/photo_1372613034592-1-HD.jpg?ve=1
Muokoaji katika tukio hilo la Uganda akitumia mti kutoa baadhi ya milii ya wahanga wa tukio hilo (Picha:AFP)
IDADI ya watu waliofariki katika ajali ya mlipuko wa moto uliotokana na ajali ya gari la mafuta kuanguka nchini Uganda imeongezeka ikielezwa kuwa sasa imefikia watu 33 badala ya 29 waliotangazwa awali.
Taarifa kutoka nchini humo zinasema baadhi ya majeruhi waliokuwa wamelazwa hospitalini kutokana na kuunguzwa sehemu kubwa ya miili yao wamefariki na kufanya idadi hiyo kuongezeka na kuna hofu idadi ikazidi kutopkana na ukweli wahanga wengi wapo katika hali mbaya licha ya madaktari kupigana kuwaokoa.
Hata hivyo Kamanda wa Polisi nchini, Andrew Kaweesa alinukuliwa na AFP kuwa mpaka jana walikuwa na takwimu inaoonyesha watu 31 kufariki kutokana na tukio hio na majeruhi wengine 10 wakiwa katika hali mbaya.
Tukio hilo lililotokea mji mkuu wa nchini hiyo, Kampala na iliyohusisha gari ndogo na lori hilo kabla ya kupinduka na watu kukimbilia eneo la tukio kuzoa mafuta na kutokea mlipuko ulioochoma baadhi ya miili kushindwa kutambulika kwa urahisi limetajwa ni tukio kubwa na baya tangu Desemba 2001 ambapo watu 90 walipoteza maisha katika ajali kama hiyo.
Katika ajali hiyo ya juzi, madereva wa bodaboda kadhaa nao walipoteza maisha yao wakati wakikimbilia kuzoa petrol iliyokuwa imebebwa kwenye lori hilo na kamanda Kaweesa alithibitisha pikipiki karibu 20 nazo ziliteketea kwa moto katika ajali hiyo.

Yametimia Tanzania! Obama kutua nchini mchana wa leo

http://www.thecitizen.co.tz/image/view/-/1868882/highRes/520959/-/maxw/600/-/qjnwx1/-/Obama+Drop+Clip.jpg
Itakuwa hivi mara baada ya Rais Obama kutua nchini kama alivyompokea Rais Kikwete alipozuru  Marekani
HAYAWI Hayawi sasa yamekuwa! Rais wa Marekani, Barack Obama anatarajia kuweka historia ya aina yake atakapotua nchini mchana wa leo katika ziara yake ya siku mbili.
Wiki kadhaa wakazi wa Dar walikuwa wakishuhudia pilikapilika za aina yake ikiwemo 'operesheni safisha jiji' yote ikiwa ni maandalizi ya ugeni huo mzito ambao umezua mjadala miongoni mwa watanzania bila mtu akihisi yake kichwani.
Ndege ya Air Force One itakayombeba  Obama na msafara wake itakanyaga ardhi ya Tanzania saa 8.40 mchana kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ambako atapokelewa na mwenyeji wake, Rais Jakaya Kikwete.
 Obama ambaye anafuatana na mkewe Michelle na binti zake, Malia na Sasha, anatua Tanzania ikiwa ni sehemu yake ya mwisho ya ziara yake barani Afrika.
Anawasili Tanzania akitokea Afrika Kusini ambako alikwenda Ijumaa baada ya ziara yake ya Senegal.
 
Historia imetimia
Imepita miaka 50, tangu Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere alipotembelea Marekani, Julai 13, 1963 na kukutana rais wa nchi hiyo wakati huo, John F Kennedy na ziara hiyo inaaminika kuanzisha urafiki wa viongozi hao ambao umedumu hadi sasa. 
Ujio wa Rais Obama una maana na faida kubwa kwa Tanzania katika maeneo ukiangalia kihistoria, kisiasa, kidiplomasia na kiuchumi pia.
Ziara ya  Obama ni heshima kubwa kwa Tanzania na itaingia katika vitabu vya kihistoria kwani ana rekodi ya kuwa mtu mweusi wa kwanza kuchaguliwa kuongoza taifa la Marekani. 
Kuchaguliwa kwake (Obama), ambaye baba yake mzazi alikuwa na asili ya Kenya kuliashiria nuru mpya kwa siasa za Marekani kwani watu weusi wa taifa hilo kwa miaka mingi walikuwa wakipigania haki za kufaidika na fursa za kiuchumi na kisiasa katika taifa la Marekani.
Tanzania, kwa miaka mingi ilikuwa inaunga mkono harakati za watu weusi na ndiyo maana iliikuwa karibu na viongozi wa harakati za kupigania haki za watu weusi.
Mwalimu Julius Nyerere alikuwa karibu na Martin Luther King na mkewe Correta , ambao waliongoza harakati za mtu mweusi kujikomboa.Pia, viongozi wengine wa harakati hizo za mtu mweusi kutambuliwa kule Marekani, Jesse Jackson, Andrew Young na Malcolm X waliitembelea Tanzania mara nyingi.    
Obama alipochaguliwa kushika nafasi hiyo mwaka 2008 alifurahiwa na wapenda amani kote duniani na hasa Waafrika kwani walimhesabu kuwa ni sehemu yao.
Kuja kwake leo ni heshima kubwa kwani Tanzania inakuwa nchi ya nne  Afrika kutembelewa na Obama baada ya Ghana mwaka 2009 na ziara yake ya hivi karibuni ya nchi za Senegal na Afrika Kusini.
Ukizingatia kuwa  Obama  ana miaka mitatu na nusu kabla ya kumaliza kipindi chake cha pili cha uongozi wake huenda ziara hii ndiyo ikawa ya mwisho kwake barani Afrika akiwa na wadhifa wa rais.

CUF yajipanga kuchukua hatua dhidi ya Jeshi, Polisi

 
http://zanzibardaima.files.wordpress.com/2013/01/lipumba1.jpg?w=640
Mwenyekiti wa CUF, Prof Ibrahim Lipumba

CHAMA cha Wananchi (CUF) kimesema kinawasilisha na mawakili wake na asasi za haki za binadamu kujua hatua za kisheria kuchukua dhidi ya  askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa madai ya kutekwa na kuteswa Naibu Mkurugenzi wa CUF Taifa, Shaweji Mketo, na viongozi wengine wa chama hicho Mkoa wa Mtwara.
Mpango huo ulitangazwa jana jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wake wa Taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba wakati akiongea na waandishi wa habari.

Prof. Lipumba alisema pia chama hicho kinawasiliana na mawakili hao kujua hatua za kisheria za kuch
ukua dhidi ya Jeshi la Polisi kwa madai ya kuwabambikia kesi viongozi hao  ambao kimedai walikamatwa na kupigwa na askari wa JWTZ katika kambi yao ya Naliendele.
Alisema pia wanawasiliana na asasi za kiraia zinazoshughulikia haki za binadamu na haki za wanawake kumsaidia kisaikolojia mwanamke anayedaiwa kubakwa na askari wa JWTZ mkoani humo na kufikishwa mahakamani.

Lipumba aliwataja viongozi wengine wa CUF waliodaiwa kutekwa na kuteswa kambini Juni 28, mwaka huu kuwa ni Salum Mohamed ambaye ni Mwenyekiti wa CUF Mtwara Mjini,Ismail Jamal Mwenyekiti wa CUF Mtwara vijijini.

Wengine ni Mwenyekiti wa Vijana Mtwara mjini, Ismail Njalu, Katibu wa CUF Mtwara mjini, Said Kulaga na Kashindye Kalungwana ambaye ni dereva wa jeshi hilo makao makuu.

Alidai viongozi hao baada ya kutekwa na askari wa JWTZ walivuliwa nguo zote na kulazwa kifudifudi, kumwagiwa maji ya baridi na kupakwa chumvi kisha kuanza kupigwa usiku kucha kwa kutumia mikanda ya jeshi, ngumi, mateke na fimbo maalum za ngozi za wanyama na miti maalum.

Alisema viongozi hao wakiwa njia kurejea Mtwara Mjini wakitokea Msimbati magari mawili ya jeshi yaliziba barabara baada ya kuliona gari la CUF  na wanajeshi walianza kuwashusha na kuwapiga kisha kuwarusha kwenye karandinga lao.

Alisema baadaye walipelekwa katika kambi ya Naliendele kabla ya kuachiwa saa 5:00 usiku na kukabidhiwa kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara.

“Kwa bahati mbaya Mketo alipigwa sana katika ubavu wake wa kulia ambao amewahi kufanyiwa operesheni kubwa miezi kadhaa iliyopita,. 

Alipoona anapigwa sana eneo hilo akaona awaombe askari wampige maeneo mengine lakini eneo hilo wamhurumie, kusikia vile askari wale walimgeuza kwa nguvu na kuanza kumpiga mateke ya nguvu zaidi katika eneo lile hadi alipoteza fahamu,”alisema.
Alisema Mketo alipozinduka Juni 28, mwaka huu  alijikuta ana dripu na hakuelewa ni ya nini na baadaye wanajeshi waliitoa.

Profesa Lipumba alisema tukio la utesaji raia ndani ya kambi ya jeshi ikiliunganishwa na matukio mengine kama ya utesaji wa Dk.Stephen Ulimboka , kutekwa nyara kwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Absalom Kibanda, kulipuliwa bomu katika mkutano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kunadhihirisha hatua za awali za kusambaratika kwa dola.

Msemaji wa JWTZ, Kapambala Mgawe, alipoulizwa kuhusu tuhuma hizo zinazoelekezwa kwa askari wa jeshi lake,  alisema suala hilo linatiwa chumvi na wanasiasa kwasababu kiutaratibu anayetekwa ni adui hivyo raia wa Tanzania hawezi kutekwa na wanajeshi.

Mgawe alisema tuhuma zinazoelekezwa kwa wanajeshi zina lengo la kutaka kulichafua jeshi hilo ili lisifanye kazi yake kwasababu vipo vipengele vya kisheria vinavyoruhusu askari wa JWTZ kuliingilia kati kudumisha amani kunapotokea Jeshi la Polisi limezidiwa.

Alisema katika kipindi hiki ambacho kuna vurugu nyingi zinajitokeza katika nchini jeshi litakapokuwa linachukua hatua ya kudhibiti yatesemwa mengi ikiwamo askari kuhusishwa na vitendo vya ubakaji.

CHANZO: NIPASHE

Watanzania 60 wakamatwa ziara ya Obama


http://graphics8.nytimes.com/images/2012/11/07/timestopics/Barack-Obama/Barack-Obama-sfSpan.jpg
Rais Obama na familia yake wakiwapungia mikono wananchi
 WAKATI Rais wa Marekani Barack Obama na msafara wake wa watu 600 ukitarajiwa kutua mchana huu nchini Tanzania, Watanzania 60 wanaishi nchini Afrika Kusini wamekamatwa  ikiwa ni maandalizi yaliyokuwa yakifanyika wakati rasi huyo aklipotua nchini humo juzi.ni.

Rais Obama aliwasili Afrika Kusini juzi kwa maandamano akitokea nchini Senegal.

Habari kutoka nchini humo zinasema watu hao 60 walikamatwa baada ya kudaiwa kuishi kinyume cha sheria Afrika Kusini. Baada ya Watanzania hao kutiwa mbaroni na vyombo vya usalama wamehifadhiwa hapa nchini kusubiri  hatua za kisheria zaidi.

Ofisa mmoja wa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere, Sadiki Msele amesema Watanzania hao walirejeshwa nchini jana na kwamba hivi sasa wanasubiri sheria kuchukua mkondo wake.

“Safisha safisha kama iliofanyika jijini Dar es Salaam, pia imefanyika Afrika Kusini na kuwaathiri wafanyabiashara na watu wengine,” amesema ofisa huyo.

Hivi sasa Rais Obama yupo njiani kutoka Afrika Kusini akiongoza na mkewe Michelle Obama na watoto wao wawili; Malia na Sasha kwa ajili ya kutua nchini Tanzania  leo kuanzia saa 8 mchana kwa ziara ya siku mbili ambapo moja ya maandalizi yaliyowaacha watu midomo wazi kudekiwa kwa barabara eneo la Ubungo.


Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga ameweka bayana barabnara zitakazofungwa kwa leo na kesho huku akiwataka wananchi wakae umbali wa mita 14 toka barabarani kutokana na hali ya usalama wakati wa ziara ya Obama kokote.
   

Gor Mahia, Bandari zashindwa kutambiana Kenya

Wachezaji wa Bandari, Gor Mahia wakiumana uwanjani (Picha Super Sport)
 MABINGWA wa zamani wa Kenya na Kombe la Washindi Afrika, Gor Mahia ya Kenya jana ilifanikiwa kukwea hadi nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu ya nchi hiyo baada ya kulazimishwa suluhu na Bandari Mombasa katika pambano kali lililochezwa kwenye uwanja wa City, jijini Nairobi.
Mahia kwa suluhu hiyo imeipumulia Bandari waliopo nafasi ya pili wakiwa na pointi 24 kwa tofauti ya pointi moja kwani vigogo hao wana pointi 23 na ikiwa na michezo miwili mkononi wakati ligi ikiwa raundi ya 15.
Katika pambano hilo lililokuwa likitangazwa na kituo cha redio cha Citizens ya Kenya, Gor Mahia itajilaumu kwa kukosa mabao mengi ya wazi mbele ya wageni wao ambao wanatenganishwa na vinara wa ligi hiyo ya Kenya Thika United kwa pointi mbili. Thika ambayo itashuka dimbani jioni ya leo kuumana na AFC Leopards ugenini inaongoza msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 26 ikicheza mechi 14.
Suluhu hiyo ya jana nyumbani ni ya pili kwa Gor Mahia kwani kabla ya pambano hilo na Bandari ililazimishwa sare kama hiyo na Thika United.

Brazil waiadhiri Hispania Kombe la Mabara

Job done: Brazil's players lift the trophy after a sensational performance against the world champions Spain
Brazil wakishangilia taji lao la ubingwa wa Mabara baada ya jana kuitafuna Hispania kwa mabao 3-0
Game over? Fred celebrates his second and Brazil's third
Fred akishangilia moja ya mabao yake mawili huku mfungaji mwingine Neymar akimfuata kwa nyuma kushoto
 WENYEJI wa Fainali za Kombe la Dunia za 2014 Brazil usiku wa kuamkia leo waliisurubu na kuishikisha adabu waatetezi wa taji hilo, Hispania kwa kuwalaza mabao 3-0 katika pambano la Fainali za Kombe la Mabara lililochezwa kwenye uwanja wa Maracana, mjini Rio de Janeiro.
Hispania ambao licha ya taji la dunia, pia inashikilia ubingwa wa nchi za Ulaya na jana ilikuwa ikiota kuongeza taji jingine la Mabara, lakini wakajikuta wakikumbana ana kipigo hicho toka kwa Brazili ambao wameanza kurejesha makali yao baada ya kuzorota miaka ya hivi karibuni na kufikwa na nchi za Ulaya.
Katika mchezo huo, mabingwa wa Dunia na Ulaya walipoteza mchezaji mmoja na pia wakashindwa kufunga Mabao ya Fred aliyefunga mawili na Neymar yalitosha kuizima Hispania iliyoing'oa Italia katika nusu fainali ya michuano hiyo ambayo katika mchezaji wa jana ilimpoteza Gerrard Pique na kukosa pia penanti iliyopoteza na Sergio Ramos.
Fred alifunga bao la kwanza dakika ya pili kabla ya Neymar akafunga bao la pili dakika moja kabla ya mapumziko na Fred anaongeza jingine dakika mbili baada ya kuanza kipindi cha pili na kuwafanya wenyeji kushangilia taji la tatu mfululizo la michuano hiyo.
Brazil imetwaa taji hilo kwa mara nne mara ya kwanza mwaka 1997 michuano ilipofanyika nchini Saud Arabia kabla ya kutwaa tena mwaka 2005 nchini Ujerumani, kisha kunyatua tena nchini Afrika Kusini katika fainali za mwaka 2009 na jana ikaongeza tena ikiwa nchi mwenyeji.
Katika mechi ya kusaka mshindi wa tatu wa michuano hiyo, Italia ilijifariji kwa kunyakua nafasi hiyo kwa kuilaza Uruguay kwa mikwaju ya penati baada ya kumaliza dakika 120 kwa kufungana mabao 2-2.
Katika hatua hiyo ya penati Italia walipata penati 3 dhidi ya mbili za Uruguay ambao walikuwa na kazi ya kurudisha mabao katika muda wa kawaida kupitia kwa Edinson Cavani.

APR, Vital'O katika fainali ya aina yake Darfur


http://upload.wikimedia.org/wikipedia/en/f/fe/Vital%27O_FC_logo.png


http://en.starafrica.com/football/files/2012/11/APR-logo.jpg


TIMU ya APR ya Rwanda leo inatarajia kukutana na majirani zao Vital'O ya Burundi katika mechi kali ya fainali ya mashindano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame) itakayofanyika kwenye Uwanja wa El Fasher ulioko Darfur Kaskazini nchini Sudan.
Timu hizo pinzani ambazo mwaka huu zilikutana katika michuano ya Ligi ya Klabu Bingwa Afrika na Vital'O kusonga mbele, zilikutana kwenye hatua ya makundi na kutoka sare ya goli 1-1 huku APR ikitangulia kupata bao na Warundi kusawazisha.
Wanyarwanda APR wamefika hatua hiyo baada ya kuwafunga wenyeji El Merreikh  El Fasher kwa penati 3-1 kufuatia sare ya 1-1 waliyomaliza katika dakika 120 huku Vital'O wakifuzu kwa hatua ya fainali leo baada ya  kuwafunga mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya Rwanda, Rayon Sports bao 1-0.
APR ambayo sasa iko chini ya kocha kutoka Ujerumani, Andreas Spier, inasaka ubingwa wa nne wa mashindano hayo. Mara ya mwisho walibeba taji la michuano hiyo inayofadhiliwa na rais wa nchi yao mwaka 2010 na wapinzani wao  Vital'0 hawajawahi kutwaa kombe hilo.
Bingwa wa leo atajinyakulia zawadi ya kwanza ya dola za Marekani 30,000 (Sh. milioni 48) huku mshindi wa pili akiwa na uhakika wa  kuondoka na dola za Marekani 20,000 (Sh. milioni 32).
Katika hatua nyingine, leo jioni kutakuwa pia na mechi ya kusaka mshindi wa tatu wa mashindano hayo ambapo wenyeji El Merreikh El Fasher watavaana na Rayon Sports kwenye uwanja huo huo wa El Fasher.
Yanga ya Tanzania Bara ndiyo inashikilia ubingwa wa mashindano hayo lakini ilishindwa kwenda kutetea taji lake mjini Darfur kufuatia amri ya serikali ya Tanzania kuzuia timu zake kwenda kwenye michuano hiyo kwa sababu za kisalama. Hata hivyo, serikali ilibaini baadaye kuwa hali ya Darfur ni shwari, lakini ruhusa yake haikuzisaidia timu za Tanzania za Yanga, Simba na Falcon ambazo nafasi zao zilishatwaliwa na timu nyingine.

Sunday, June 30, 2013

29 wafa kwa kuteketezwa kwa mlipuko wa lori la mafuta lililoanguka Uganda

Picha zote hazihusiani na ajali hiyo ya Uganda

WATU 29 wameripotiwa kufa nchini Uganda na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa vibaya na moto uliotokana na ajali ya lori la mafuta lililoanguka.
Habari kutoka Uganda zinasema ajali hiyo ya kusikitisha ilitokea katika barabara kuu ya jijini Kampala na kwamba zaidi ya pikipiki 20 nazo ziliungua kwenye tukio hilo ambalo limethibitishwa na jeshi la Polisi nchiini humo.
Inaelezwa kuwa mara lori hilo lilipoanguka wakazi wa jijini hilo walilivamia kwa nia ya kuzoa mafuta kabla ya kutokea mlipuko uliowaunguza watu hao ambao baadhi walikimbilia kwenye madimbwi ya maji ili kupoza machungu ya moto na kupotea uhai wao na kuopolewa kwenye maji.
Zaidi ya watui 2o wameripiwa kukimbizwa hospitalini wakiwa hoi kwa kujeruhiwa na moto huo ambapo unaelezwa ulianzishwa na mmoja wa wahanga hao wakati wakimbilia kwenye ajali hiyo bila kujua lori lilikuwa limerbeba petroli.

Wakati akitarajiwa kutua kesho, Obama aonywa mapema Tanzania


Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo yaNje na Ushirikiano wa Kimataifa, Edward Lowassa, amemtahadhalisha kujiepusha na kauli za kuunga mkono ushoga.
 

Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, ameliambia NIPASHE Jumapili ofisini kwake jijini hapa jana kuwa ushoga na hai za ndoa kwa watu wa jinsia moja vinaweza `kuiharibu’ ziara yake hapa nchini.

Mapema wiki hii, Rais Obama alikaririwa akizungumzia masuala hayo yanayotajwa kuwa ni moja ya haki za msingi za binadamu, alipokuwa Senegal, lakini akapingwa.
 

“Watanzania hawatalikubali na wataendelea kushikilia uhuru na heshima walizojengewa tangu awali, kwamba ushoga na ndoa za jinsia moja havikubaliki, alisema.

Akiwa Senegal, Rais Obama alitaka serikali za Afrika kutoa haki kwa mashoga kama inavyotoa kwa raia wengine.
 

"Ninachotegemea, I pray and hope (ninasali na kutegemea) kwamba kuhusu mashoga na ndoa za jinsia moja, Rais Obama hatarudia kauli aliyoitoa kule Senegal,” alisema.

Aliongeza, "ninasema hivi kwa sababu Tanzania hatuamini katika ushoga, na endapo utawalazimisha Watanzania, watakukatalia na kushikilia uhuru na heshima waliyojengewa toka awali."

AHIMIZA MAPOKEZI MAZURI
Hata hivyo, Lowassa aliwataka Watanzania kuiheshimu na kuitumiavema fursa ya kutembelewa na Rais Obama, hivyo wajitokeze kumlaki kwa wingi.
 

"Tutambue mataifa makubwa yanakimbilia maslahi ya karne inayofuata, kwa mfano Rais wa China, Xi Jiping siku moja baada ya kuapishwa kwake alikuja hapa nchini, " alisema.
 

Hivyo, alitoa wito kwa Watanzania kuhakikisha maslahi na fursa za kiuchumi zinakuwa za kwanza kulindwa, kwa kuwa ziara hiyo itafungua milango zaidi kwa wawekezaji kuja nchini.
 

Pia, Lowassa alisema ziara ya Rais Obama ni kielelezo cha amani na usalama uliopo, na kwamba itasaidia kuwavutia watalii na wadau wa sekta nyingine za maendeleo kuitembelea Tanzania.

KITUO CHA KIJESHI
Kuhusu hofu na tetesi kuwa ziara hiyo imelenga taifa hilo kuja hapa nchini kufungua kituo cha kujiimarisha kiulinzi, Lowassa alisema Watanzania wanapaswa kufahamu kuwa tayari nchi hiyo ina kituo cha kijeshi nchini Kenya.


"Tuangalie maslahi yetu tuachane na mitazamo hasi, kama ni kituo cha kijeshi tayari kipo Kenya, tujiulize kwa nini marais wa Marekani Bill Clinton na George Bush walivyofanyaziara zao hapa nchini hawakwenda Kenya," alisema.

WALINZI WA NDANI KUWEKWA KANDO
Kuhusu ziara hiyo kutumia ulinzi wa kimataifa huku majeshi ya Tanzania yakiwekwa kando kwa ushiriki wa moja kwa moja, Lowassa alisema Rais wa Marekani ana kiwango cha juu cha ulinzi unaosimamiwa na nchiyake pekee.
 

"Ni sahihi walinzi wetu kukaa pembeni, huyu ni kama Rais wa dunia, lakini hata majeshi yetu yanafanya kazi ya ulinzi lakini sio kwamba yatakaa nyuma tu," alisema.
 

SUMAYE: TUMKARIBISHE
Naye, Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye, alisema ziara ya Rais Obama haina ujumbe zaidi ya kuhimiza watu wajitokeze kumpokea.
 

Hata hivyo, Sumaye alikwepa kuzungumzia kwa undani hatua ya kuwafukuza wafanyabiashara kutoka kandoni mwa barabara, ili kupisha mapokezi ya Rais Obama.
 

“Ninachokielewa ni kuwa barabara ambazo wanapita viongozi kama Rais Obama zinatakiwa kuwa katikahali ya usalama na hivyo kutakiwa kuboreshwa,” alisema.

LIPUMBA: MAFANIKIO NI MADOGO KIUCHUMI
Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba, alisema mafanikio ya ziaraya Rais Obama yapo katika kujitangaza kimataifa kuliko kiuchumi.
 

Profesa Lipumba ambaye ni mchumi aliyebobea, alisema changamoto iliyopo ni kwamba bado biashara kati ya nchi mbili hizo siyo kubwa kama ilivyo kwa nchi kama China na Tanzania.
 

Alitolea mfano, mwaka 2012 bidhaa za hapa nchini zilizouzwa Marekani zilikuwa na thamani ya Dola milioni 66 ikilinganishwa na zile zilizouzwa China ambapo zilikuwa ni zaidi ya Dola milioni 500.
 

Alisema bidhaa zilizoagizwa kutoka Marekani zilikuwa na thamani ya Dola milioni 230 huku za kutoka China zikiwa na thamani ya zaidi ya Dola milioni 1,100.

"Utakubaliana nami kuwa mahusiano yetu na China ni makubwa kuliko Marekani licha ya nchi hii kutoa fursa kwetu ambazo hatujazitumia ipasavyo," alisema
 

Profesa Lipumba alisema Marekani kupitia mpango wake wa kusaidia Maendeleo ya Afrika (AGOA), ulitoa fursa kwa bidhaa za Afrika kuuzwa nchini humo bila ushuru, lakini Tanzania haikuitumia.

Pia alisema utawala wa George Bush, uliisaidia Tanzania kupitia Mfuko wa Changamoto za Milenia (Millenium Challenge Compact (MCC) kupewa Dola milioni 700 kwa ajili ya kusaidia miundombinu na ujenzi wa nyaya za umeme kutoka bandarini hadi Zanzibar.

"Pana uwezekano wa mpango wa pili wa MCC, Tanzania ikapata msaada wa kuimarisha miundombinu ya umeme, lakini pia kampuni za Marekani kuja kuwekeza hapa kwetu," alisema.
 

Alisema uwekezaji wa kampuni hizoutategemeana na wafanyabiashara wa hapa nchini pamoja na serikali kutumia fursa mbalimbali za nchi hiyo.
 

Katika hatua nyingine, Profesa Lipumba alisema ili nchi iweze kujikwamua na umasikini itatokana na jinsi itakavyotumia sera na juhudina siyo kutegemea msaada kutoka nje.
 

HOTELI ZIMEJAA
Wingi wa wageni wakiwamo watakaofika kwa ajili ya ziara ya Rais Obama, umesababisha hoteli nyingi za jijini Dar es Salaam `kujaa’.
 

Uchunguzi wa NIPASHE Jumapili ulibaini kwamba kwa zaidi ya wiki sasa, hoteli nyingi hazikupokea wageni kutokana na kile kilichoelezwa kuwa, nyingine zililipiwa ingawa vyumba havikutumika kwa wakati.
 

POLISI: WASIO NA KAZI WASIJE MJINI
Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga, amewataka wananchi ambao hawatakuwa na mambo muhimu ya kufanya katikati ya jiji, wasifike huko kupunguza msongamano wa watu na magari baada ya kuwasili kwa Rais Obama.
 

Alisema, baadhi ya barabara zitafungwa kwa muda kwa ajili ya viongozi kuzitumia, hivyo kusababisha msongamano.
 

Hekaheka zimetanda jijini Dar es Salaam, ikiwa ni zaidi ya saa 24 kabla ya kuwasili kwa Rais Barack Obama.
 

Rais Obama, atawasili nchini kesho akitokea Afrika Kusini, ambapo pamoja na mambo mengine, alizungumza katika mkutano wa ‘viongozi vijana wa Afrika’ na kujibu maswali kutoka nchi tofauti.
 

Mkutano huo ulifanyika jana jioni huko Soweto nchini Afrika Kusini, ambapo alipokewaa na kujibu maswali kutoka Kenya, Uganda, Nigeria na Afrika Kusini kwenyewe.
 

Jijini Dar es Salaam, shughuli kadhaazikiwamo za ulinzi na usalama, zinafanyika kwa kasi na umakini kuhakikisha ziara ya Rais Obama inafanyika pasipo bughudha. kujibu maswali kutoka Kenya, Uganda, Nigeria na Afrika Kusini kwenyewe.
 

Jijini Dar es Salaam, shughuli kadhaazikiwamo za ulinzi na usalama, zinafanyika kwa kasi na umakini kuhakikisha ziara ya Rais Obama inafanyika pasipo bughudha.
 

Hata hivyo, sehemu kubwa inayohusu masuala ya itifaki, ulinzi na usalama yanafanywa na taasisi za Marekani, kwa kuzishirikisha taasisi za ndani kwa kiwango kidogo.
 

“Hawa jamaa (Wamarekani) wanapoingia nchi yeyote wakiwa naRais wao, shughuli nyingi na uamuzi wanafanya wao, sisi wa ndani inakuwa kushirikishwa kwa kiasi kidogo,” kilieleza chanzo cha NIPASHE Jumapili kutoka moja ya taasisi zinahusika katika ziara hiyo.
 

Maeneo kadhaa ya jijini humo, yaliendelea kudhibitiwa kwa ulinzi mkali na doria za mara kwa mara, huku kandoni mwa baadhi ya barabara wakionekana askari wa Jeshi la Wananchi (JWTZ).
 

Mathalani, kandoni mwa barabara ya Morogoro, eneo la Ubungo, walionekana askari wa JWTZ maarufu kama MP.
 

Shughuli nyingine zimehusisha pia operesheni zinazofanywa na polisi kwa kusaidiana na mgambo wa jiji, kuhakikisha watu na bidhaa zilizopokandoni mwa barabara zitakazotumika kwa ziara ya Rais Obama, vinaondolewa.
 

Magari yaliyowabeba polisi wenye silaha za moto na mabomu ya machozi, yalionekana katika mitaa kadhaa jijini humu, wakihakikisha operesheni hiyo inafanyika pasipo kikwazo kutoka kwa wahusika.
 

Kila palipofanyika operesheni hiyo, baadhi ya askari walifanya doria zamu kwa zamu, kuhakikisha kuwa bidhaa na watu walioondolewa, hawarejei.
 

Hata hivyo, waathirika katika operesheni hiyo walieleza kutofurahia, huku wakihoji ni kwa nini serikali haikuwaandalia mazingira mbadala kabla ya utekelezaji wake. 
 
Walisema miongoni mwao, wamekopa mitaji kutoka kwenye taasisi za kifedha, hivyo kusimamisha biashara zao ili kupisha ujio wa Rais Obama, kutawaweka katika hali ngumu kiuchumi.
 

“Ikiwa ujio wa Rais Obama unatutesa wafanyabiashara kiasi hiki, ni vigumu kuhimili maisha yetu, kwa sababu hatujui hatma yetu baada ya yeye kuondoka,” alisema mfanyabiashara Zena Rashidi wa Kariakoo.
 

Hata hivyo, wamachinga walionekana jana katika kituo cha mabasi cha Mwenge walipofukuzwa, wakiwa wanaendelea na biashara zao.

Lakini walifanya hivyo kwa tahadhali ikiwamo kushika bidhaa chache mikononi, huku wakitumia 'janja' ya kupiga kelele za 'kumsifia' Rais Obama.
 

Walisikika miongoni mwao wakisema, 'praise to Obama' na wengine wakaitikia 'aaamen'. Walifanya hivyo zamu kwa zamu, lakini haikujulisha waliashiria nini.
 


BARABARA ZAPAMBWA
Aidha, barabara zote atakazopita Obama wakati wa ziara yake zimepambwa kwa bendera za Marekani na Tanzania; huku zikinakshiwa kwa picha yake ambayo imeandikwa 'President Barack Obama' karibu Tanzania.
 

Barabara hizo ni ile ya Nyerere kuanzia uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere, Ali Hassan Mwinyi, Mwai Kibaki na Bagamoyo.

NIPASHE Jumapili imeshuhudia pichana bendera hizo zikiwa zimewekwa kwenye mabango yote yaliyo barabarani kuanzia Ikulu hadi kwenye barabara hizo huku usafi wa jiji ukionekana kuimarika zaidi.
 

Jana gazeti hili lilishuhudia karibu barabara zote, vijana wanaofanyakazi ya kuweka bendera na picha ya Obama wakifanyakazi hiyo.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

Hatimaye Javu atua Jangwani

KLABU ya soka ya Yanga imemnasa mshambuliaji wa Mtibwa Sugar, Husssein Javu ambaye pia alikuwa akiwaniwa na Simba.

Habari kutoka Yanga zinasema kwamba, nyota huyo amesaini mkataba wa miaka miwili kwa ajili ya kuitumikia klabu hiyo katika michuano mbalimbali itakayoshiriki pamoja na Ligi kuu bara.
Aidha, mabingwa hao wa ligi kuu bara wamekana kumsajili mshambuliaji wa Kimataifa Mganda, Moses Oloya ambaye Simba nayo ilikuwa ikifanya mazungumzo naye