STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, July 30, 2013

Mabondia wa Tanzania huuza mechi zao Ulaya?

http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2011/11/Rashid-matumla.png
Rashid Matumla 'Snake Man'

Benson Mwakyembe
 

http://www.ibn-tv.com/wp-content/uploads/2012/02/Nyilawila.jpg
Karama Nyilawila aliyetwaa ubingwa wa WBF Ulaya

MABONDIA Mada Maugo na Benson Mwakyembe Jumamosi walipokea vipigo nchini Russia katika mapambano yao ya kimataifa, huku kukiwa na tuhuma kwamba mabondia wengi wa Kitanzania wanaoenda kupigana nje ya nchi 'huuza' mechi zao.
Maugo alipokea kichapo cha TKO ya raundi ya 5 katika pambano la raundi 8 dhidi ya bondia asiye na uzoefu Movsur Yusupov aliyecheza mapambano manne tu kulinganisha na Mtanzania huyo aliyepigana michezo 25.
Mtanzania mwingine, Mwakyembe alidundwa kwa KO ya raundi ya 7 ya pambano lake la raundi 8 dhidi ya bondia mwingine asiye na uzoefu Apti Ustarkhanov, ambaye hilo lilikuwa ni pambano lake la tatu na la pili kushinda tangu aingie kwenye ngumi za kulipwa.
Kina Maugo walipambana dhidi ya wenyeji wao katika mapambano ya uzito wa Super Middle ya raundi nane yaliyofanyika katika ukumbi wa Trade & Entertainment Centre 'Moskva', Kaspiysk chini ya wakala Mkenya Thomas Mutua.
Vipigo vya mabondia hao vimekuja wakati wadau wa ngumi za kulipwa wakihoji sababu zinazofanya mabondia wa Kitanzania kushindwa kutamba kila waendapo nje huku ripoti mbalimbali zikiwatuhumu mabondia wa majuu kuwatumia mabondia kutoka Afrika kupandisha chati zao katika viwango vya ubora kwa kuwanunua wawaachie washinde.
Ripoti za kuuzwa mechi au kuwapo kwa mchezo mchafu ziliwahi kutolewa na baadhi ya mabondia akiwamo Pascal Ndomba na Francis Cheka aliyepokea kichapo cha kushangaza mapema mwaka huu nchini Ujerumani.

Ndomba anayepigana uzito wa juu wa (Cruiserweight), alisema baadhi ya mawakala wa nje hutaka mabondia dhaifu wa kwenda kupigana na mabondia wao ili kupata ushindi kirahisi na kuboresha rekodi zao.
"Hili ndilo linalofanyika, bondia mkali mara chache sana kupelekwa nje na hata akienda basi atahujumiwa ili apoteze mchezo kwa manufaa ya mabondia wanaoenda kupigana nao," Ndomba alisema hivi karibuni.
Naye Cheka alitoa maelezo ya kufanyiwa 'hila' katika pambano lake dhidi ya Uensal Arik aliloongoza kwa raundi sita za mwanzo kabla ya kurushiwa kitaulo katika raundi ya saba na kupoteza mchezo kwa TKO.

Pascal Ndomba
"Sikupoteza pambano lile, ila mwenyeji alibebwa na mwamuzi aliyemaliza pambano kana kwamba nimesalimu amri, ni vigumu mabondia wa Tanzania kushinda nje," alisema Cheka mara alipotua nchini.
Cheka alisema kambi ya mpinzani wake walimfuata hadi hotelini alipofikia kuelekea pambano lao kumshawishi awaachie pambano hilo kwa ahadi ya pesa lakini alipokataa ndipo alipokuja kuhujumiwa ulingoni kwa mtu aliyekuwa upande wa kona yake kurusha taulo ulingoni ilhali alikuwa akiongoza kwa pointi.
Bondia huyo anayeaminika kuwa bora zaidi nchini kwa sasa katika uzito wake, alisema hakuambatana na kocha wake wakati akienda katika pambano hilo hivyo hata kwenye kona yake walikuwa wenyeji wake na ndiyo waliorusha taulo ulingoni.
Hata hivyo, wapo waliomtuhumu kwamba huenda Cheka alicheza 'dili' na wakala wa pambano hilo ili kutotibua rekodi ya mpinzani wake ambaye alikuwa amepoteza pambano moja tu ya 18 aliyokuwa amecheza.
NIPASHE ilizungumza na Marais wa Mashirikisho ya Ngumi za Kulipwa Tanzania, Emmanuel Mlundwa wa PST na Yasin Abdallah 'Ustaadh' wa TPBO kutaka kujua ukweli kuhusu tuhuma hizo, ambapo walikuwa na maoni tofauti .
Mlundwa alisema kinachowaponza mabondia wa Tanzania siyo hujuma wala nini ila maandalizi duni wanayofanya kabla ya mapambano yao pia kuwa na viwango duni kulinganisha na wapinzani wao wanaoenda kucheza nao.

"Ngumi za kulipwa ni biashara, mabondia wa ngumi hizo wanapotafutiwa mechi wanapaswa kujiandaa, lakini hilo halifanyiki na hivyo kwenda kulitia aibu taifa na kujiharibia soko wao wenyewe bila kujua," alisema Mlundwa.
Nyota huyo wa zamani wa kimataifa wa ngumi, alisema siyo kweli kama kuna rushwa zinazofanyika bali Watanzania wanaopewa nafasi kulingana na rekodi zao nchini huenda kupigana kichovu kwa kukosa maandalizi mazuri.
Ustaadh yeye alisema
Francis Cheka
linalowaangusha mabondia wa Tanzania nje ya nchi ni maisha wanayoishi kuwa kinyume na nidhamu ya ngumi za kulipwa na kwamba kutokuwa na mameneja ni tatizo jingine linalowakwaza.
"Mabondia wengi hawafanyi mazoezi mpaka wakati wa pambano, hapo unatarajia afanye vizuri? Pia hawaishi kwa kuzingatia miiko ya ngumi na hivyo wanapoenda nje ni rahisi kupigwa na kuhisiwa labda wanauza," anasema.

Alisema ni vyema mabondia wakafanya kazi chini ya mameneja kama ilivyokuwa kwa Rashid Matumla kwani itafanya ajikite kwenye mazoezi tu na mambo mengine kuwaachia meneja zao.
Ustaadh alisema majukumu wanayobeba mabondia ya kufanya kila kitu wakati mwingine huwafanya washindwe kujikita kwenye mazoezi na hivyo kujikuta muda wa pambano ukifika hawajajiandaa vizuri.
Rais huyo wa TPBO-Limited, alisema pia mabondia wengi hutoa visingizio kila wanapopigwa nje ya nchi bila kuangalia kama sheria za ngumi zinasemaje wanapokuwa kwenye ulingo na kutolea mfano pigano la Cheka na Arik.
"Cheka alipolalamika nilimuuliza vipi katika pambano lake na Arik, hakutupa ngumi yoyote katika raundi ya 7 na kupigwa makonde mfululizo na kunieleza mkono wa kulia ulimzingua, sheria zinasema bondia asipojibu mapigo kwa zaidi ya ngumi 10 alizorushiwa refa anaweza kuvunja pambano au wasaidizi wa bondia kuingilia kati kwa kurusha kitaulo na ndivyo ilivyotokea," alisema.
Mada Maugo

Monday, July 29, 2013

Ajali nyingine yachukua roho za watu

View of the bus that crashed on July 28, 2013 on the road between Monteforte Irpino and Baiano, southern Italy.
basi lililopata ajali nchini Italia (Picha:AFP)
WATU wapatao 38 wamepoteza maisha yao huku wengine wakikimbizwa hospitali kwa matibabu kutokana na ajali ya basi iliyotokea nchini Italia.
Waokoaji wa Kusini kwa nchini hiyo wamesema watu hao walikuwa katika basi hilo walilokuwa wakisafiria lililotumbukia ndani ya mtaro wenye urefu wa mita 30.
Baadhi ya abiria waliokimbizwa hospitalini kwa matibabu hali zao zinaelezwa kuwa mbaya kwa majeraha waliyoyapata katika ajali hiyo.
Inaelezwa kuwa basi hilo lilikuwa limebeba abiria waliokuwa wakirudi mjini Napoli kutoka jimbo la kusini la Campania. Haijabainika chanzo cha ajali hiyo iliyohusisha pia magari kadhaa na kwamba basi hilo lililokuwa limebeba abiria 50 wakiwamo watoto waliokuwa wanatoka Naples baada ya kufanya hija.
Basi hilo liligonga magari kadhaa kabla ya kuanguka ndani ya mtaro mjini Avellino.
Picha zilionyesha miili ya watu iliyokuwa imetapakaa kando ya barabara pamoja na magari yaliyokuwa yameharibiwa kwenye ajali hiyo.
Dereva wa basi hilo ni miongoni mwa wale waliofariki.
Waathiriwa kadhaa hata hivyo hawakuweza kutambulika , kwa mujibu wa msemaji wa polisi akisema kuwa wangali wanatoa miili katika magari yaliyoharibiwa. 
Ajali hiyo ya Italia imekuja siku chache baada ya watu wengine zaidi ya 70 kufa katika ajali mbaya ya Treni ya kwenda kasi iliyokea Kaskazini Magharib ya Hispania wiki iliyopita.
 
BBC

Serikali lawamani, kisa Mwigulu kufanya kazi zisizomhusu

Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk Slaa

 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi

MDHAHARO wa kujadili mstakabali wa amani ya taifa ulioandaliwa na Jumuiya ya Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDASA), umeibua mambo mazito ambapo washiriki wameinyooshea kidole serikali wakidai ndiye mchawi wa wananchi. 

Mdahalo huo ambao kauli mbiu yake ilikuwa ni Mustakabali wa Amani na Usalama wa Wananchi wa Taifa Letu kwa Miaka 50 Ijayo, ulifanyika jana katika Ukumbi wa Nkrumah wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kuwashirikisha wanazuoni, wanasiasa, viongozi wa vyombo mbalimbali vya ulinzi na serikali.

 Wachokoza mada walikuwa ni mhadhiri wa sheria wa chuo hicho, Dk. Onesmo Kyauke aliyegusia mfumo wa utendaji wa Jeshi la Polisi katika kusimamia amani ya nchi, Profesa Benadetha Kiliani, mtaalam wa sayansi ya siasa na utawala kwa umma na mwanahabari nguli na mhadhiri wa Shule Kuu ya Uandishi wa Habari, Dk. Ayoub Rioba.

 Katika mada yake, Dk. Kyauke aliliponda jeshi la polisi linavyokiuka sheria katika kutekeleza majukumu yake kiasi cha kuruhusu kuingiliwa na wanasiasa na kuelekezwa jambo la kufanya. 

Bila kuuma maneno, mhadhiri huyo alimtaja wazi wazi Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Tanzania Bara), Mwigulu Nchemba, akidai kwa sasa analiendesha jeshi hilo kwa kuingilia majukumu ya Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) na Mwendesha Mashataka Mkuu (DPP). 

Alisema kuwa mwanasiasa huyo ambaye ni mbunge wa Iramba Magharibi, amekuwa akiwatuhumu wanasiasa wa vyama vya upinzani kuwa ni magaidi na polisi wamekuwa wakiwakamata na kuwafungulia mashtaka hayohayo anayosema kada huyo bila hata kuwa na ushahidi. 

Dk. Kyauke alitolea mfano wa matukio ambayo Nchemba amekuwa akiyafanya kuwa ni pamoja na lile la kuonyesha ushiriki wa kupanga tukio la ugaidi la Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA), Wilfred Lwakatare. 

Tukio lingine alisema ni wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani jijini Arusha, ambapo kiongozi huyo aliwataka wananchi wa jiji hilo kutochagua madiwani wa CHADEMA kwa kuwa ni chama cha ugaidi kwa madai kwamba ndio waliohusika kummwagia tindikali kijana wa CCM kule Igunga. 

Kutokana na matamshi hayo, mhadhiri huyo alisema baadhi ya wanachama wa CHADEMA waliweza kukamatwa kama njia mojawapo ya kuisaidia polisi; jambo linalowafanya kama wasomi kujiuliza kuwa Mwigulu siku hizi kawa DCI au DDP? 

Kuhusu utendaji wa Jeshi la Polisi, alisema ndilo limekuwa chanzo kikubwa cha uvunjifu wa amani kwa kupoka haki ya Kikatiba ya wananchi kuandamana na kufanya mikutano huku akitolea mfano wa mauaji yaliyofanywa na jeshi hilo ya mwandishi wa habari, Daudi Mwangosi, kijijini Nyororo, mkoani Iringa, wakati wa kuzindua matawi ya CHADEMA. 

Katika mauaji hayo, alisema ushahidi wa wazi umeonyesha namna gani polisi walivyoshiriki na tume zote zilizoundwa zikamuelekezea kidole Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa na Msajili wa Vyama vya Siasa, lakini hakuna hatua zilizochukuliwa hadi leo zaidi ya polisi mwenye cheo kidogo akitolewa kafara huku mkubwa wake akiendelea kupandishwa cheo. 

Pia alisema kumekuwepo na upendeleo wa jeshi hilo kwa kutetea chama tawala ikiwemo enzi za IGP Omar Mahita kudai kuwashikilia wanachama wa Chama cha Wananchi (CUF) na majambia ingawa hadi leo wamekosa uthibitisho lakini kutokana na uongo huo wameshindwa kumchukulia hatua kiongozi huyo. 

Katika mapendekezo yake, Kyauke aliitaka polisi kubadili mfumo wake wa kufanya kazi, na kuhoji kwa nini Tanzania ni dhambi kuandamana huku akimtaka Waziri Mkuu kufuta kauli yake ya kutaka wananchi kupigwa tu na jeshi hilo wanapokaidi amri. 

Prof. Kilian kwa upande wake, alisema mpaka sasa bado kiini cha uvunjifu wa amani hakijagundulika na badala yake pande zote zimekuwa zikirushiana mpira ikiwemo serikali, wananchi na wanasiasa. 

Alizitaja sababu zinazochangia matukio hayo kuwa ni pamoja na hali ya upinzani kuja juu hivyo chama tawala kinajihami kutokana na mabadiliko hayo, kuongezeka kwa kiwango cha umaskini na mfumo wa kiliberali ambao umechangia matabaka na uhuru wa kutoa maoni tofauti na enzi za ujamaa. 

Naye Dk. Rioba alisema suala la amani sio la kuombewa kanisani au msikitini bali ni la kisayansi zaidi na kudai kwamba wanasiasa wamekuwa wakijidanganya pale wanapowahimiza watu kuliombea taifa liwe na amani. 

Pia Rioba alikanusha vyombo vya habari kuwa vimekuwa vikichangia kuharibu amani na badala yake alivifananisha vyombo hivyo na bunduki ambapo kama isipotumiwa kamwe haiwezi kuharibu amani. 

Akifafanua hili alisema vyombo vya habari vitaharibu amani endapo tu wanasiasa watavitumia na kuitaka jamii ielewe kwamba vyombo hivyo vina dhima kubwa kama mlinzi wa taifa na ndio maana wakati mwingine vinapendekezwa kuwa NGO’s ili viweze kufanya kazi kwa uhuru zaidi. 

Katibu Mkuu wa CHADEMA Dk. Willibrod Slaa alisema mchawi wa hayo yote ni serikali, huku akinukuu ripoti ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora iliyomtuhumu aliyekuwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Michael Kamuhanda, na Msajili wa Vyama vya Siasa. 

Akisema amani sio suala la kuhubiriwa au kujadiliwa bali ni matokeo ya utekelezaji wa haki mbalimbali. 

Slaa pia alilalamikia vitendo vya ukatili vilivyofanywa Mtwara na vyombo vya dola dhidi ya wananchi, huku akimnyooshea kidole Brigedia Elia Athanas aliyekuwa amemwakilisha Mkuu wa Majeshi. 

“Jeshi letu lilikuwa linaheshimika sana, lakini siku za hivi karibuni linaelekea kupoteza heshima yake kwa jamii, tukirejea mfano katika uchaguzi mkuu uliopita ambapo mnadhimu wa jeshi, Abdulrahman Shimbo, alivyotoa kauli yenye utata, jeshi linaingiaje kwenye siasa wakati suala la uchaguzi ni suala la kiraia?” alihoji. 

Hoja ya Dk. Slaa kuhusu utendaji wa jeshi la wananchi mkoani Mtwara ilipingwa kwa haraka na Brigedia Athanas akisema: “Naomba kuweka wazi kuwa jeshi letu liko Mtwara, lina adabu na vitendo ambavyo vimekuwa vikiripotiwa ni vya propaganda tu kama alivyosema Dk. Slaa. 

Licha ya kiongozi huyo kujitetea, mchangiaji aliyefuata, Julius Mtatiro ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Tanzania Bara), alithibitisha kuwa wanajeshi wanabaka na walitenda vitendo vya kikatili dhidi ya raia na viongozi wa chama hicho akiwemo mkurugenzi wao, Shaweji Mketo. 

Mwakilishi wa NCCR Mageuzi, Faustine Sungura, alisema chama hicho hakiko tayari kufanya maandamano bali kinapambana kwa nguvu ya hoja na kwamba wataendelea kutumia nguvu ya hoja. 

Akihitimisha kongamano hilo, Wazri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi, alisema kuwa kati ya mambo ambayo yanampa changamoto ni amani ya nchi hii. 

“Tulirithi nchi ikiwa na amani, hivyo tuna deni la kurithisha nchi hii ikiwa ya amani katika kizazi kijacho. 

Dk. Nchimbi alikemea suala la udini, akiwatahadharisha Watanzania kuwa wasiingie katika vurugu na wasikubali kugawanywa kwa sababu ya dini zao. 

“Tukiingia katika vurugu za dini hatutapona, Wakristo na Waislam wote tukatae kugawanywa kwa kutumia misingi ya udini kwa manufaa ya Tanzania ya sasa na kizazi kijacho. 

Waziri Nchimbi huku akimtambua Dk. Slaa, alisema wanasiasa wote wana wajibu wa kuwatumikia wananchi, “Suala la amani sio suala la Chama cha Mapinduzi peke yake, ni suala la wanasiasa wote wa chama tawala na wapinzani kutambua kuwa wao ni watumishi wa umma, na kuvumiliana kisiasa ndiko kunaleta amani.

Taifa Stars watua kinyonge kupitia KIA

Wachezaji wa Stars wamekiwa wamepozi kusubiri safari ya kuja Dar wakitokea Kilimanjaro walipotua
Kocha Kim Poulsen na tabasamu la uchungu
Makocha Stars
Mfungaji wa bao pekee la Stars dhidi ya Uganda, Amri Kiemba na wenzake katika pozi.

Ngassa akiwa mbele ya wenzake


Wakipanda gari toka uwanjani
We mbona hupigi debe? Kama wanataniana wachezaji wa Stars (picha kwa hisani na Michuzi Blog)
Mwili haujengwi kwa mawe au matofali bali msosi kama hivi!


King Majuto, Mboto watikisa tena, After Death ya Kanumba kesho


MCHEKESHAJI mkongwe nchini, Amri Athuman 'King Majuto' ameibuka tena na filamu iitwayo 'Tikisa' ambayo inaendelea kutikisa katika soko la filamu Tanzania.
Katika filamu hiyo iliyoandaliwa na Salma Jabu 'Nisha' na kuandikwa na kuongozwa na Leah Richard 'Lamata', King Majuto kama kawaida yake anavunja mbavu mwanzo mwisho akishirikiana na Haji Salum 'Mboto' na wakali wengine walioigiza pamoja.
Kwa mujibu wa Lamata, mbali na  Majuto na Mboto, filamu hiyo imewashirikisha pia Hemed Suleiman 'PHD', Chuchu Hans, Jacklyne Wolper na wengine.
"Ni bonge la filamu ambalo karibu waigizaji wote wametikisa kama lilivyo jina la filamu yenyewe, ni moja ya kazi nzuri nilizowahi kuziandika na kuziongoza baada ya kutoka na 'Poor Minds' na 'Pain Killer'," alisema Lamata.
Katika hatua nyingine Lamata alisema kuwa filamu maalum ya kumuenzi marehemu Steven Kanumba 'The Great Pioneer' itaachiwa rasmi mtaani kesho Jumanne na kuwataka mashabiki wa nyota huyo wa zamani aliyefariki mwaka mwaka kukaa mkao wa kula kuipata filamu hiyo.
Lamata alisema filamu hiyo iliyowashirikisha nyota lukuki waliowahi kuigiza kazi mbalimbali na Kanumba enzi za uhai wake, imetungwa na na kuandaliwa na Jacklyne Wolper Massawe na kuongozwa na yeye na kwamba baadhi ya washiriki hao ni watoto Patrick na Jennifer walioibuliwa na Kanumba kupitia filamu kama Uncle JJ, Thisi is It na nyingine.
Pia wapo akina Patcho Mwamba, Wolper mwenyewe, Ben Blanco, Stanley Msungu, Irene Paul, Shamsa Ford, Mwanaidi Suka 'Mainda', Salama Salimin 'Sandra' na wakali wengine huku mhusika mkuu akiwa ni Philemon Lutwazi 'Uncle D' ambaye ameshabihiana na marehemu Kanumba.
'Shangazi mtu' Wolper akiwa na Jennifa na Patrick

Golden Bush Fc yatinga 10 Bora ligi ya Kinondoni


Kikosi cha Golden Bush Fc wakiwa na  makocha wao (wa kwanza kushoto waliosimama)  ni Waziri Mahadh 'Mandieta' na wa nane toka kushoto waliosimama) ni Madaraka Seleman 'Mzee wa Kiminyio'
TIMU ya soka ya Golden Bush Fc ya Sinza imekuwa klabu ya kwanza kufuzu hatua ya 10 Bora ya Ligi ya TFF Wilaya ya Kinondoni kuwania kupanda Daraja la Tatu baada ya kuikwanyua Spallows ya Kijitonyama kwa mabao 2-0.
Katika pambano hilo lililochezwa jana kwenye uwanja wa Mwananyamala, jijini Dar Es Salaam Golden Bush inayonolewa na nyota wa zamani wa Tanzania Shija Katina, Madaraka Seleman na Waziri Mahadh, ilipata mabao yote kupitia Zola.
Ushindi huo umeifanya timu hiyo kufikisha jumla ya pointi 21 na kuongoza katika kundi lake na hivyo kufuzu moja kwa moja kwenye 10 Bora kusubiri timu nyingine zitakaoungana nazo kusaka nafasi tatu za kupanda daraja la tatu.
Katika mechi zake 8 ilizocheza timu hiyo mpya kabisa, imeshinda mechi saba na kupoteza moja dhidi ya Kijitonyama ambapo ilifungwa bao 1-0 na kutibua rekodi yao ya kushinda mechi mfululizo tangu kuanza kwa ligi hiyo.
Mlezi wa klabu hiyo, Onesmo Waziri 'Ticotico' amewapongeza vijana wake pamoja na benchi nzima la ufundi kwa kazi nzuri waliofanya na kuwataka wasibweteke kwa vile hatua waliyotinga ni ngumu zaidi hivyo wagang'amale ili kuweza kutimiza malengo yao ya kuja kucheza Ligi Kuu misimu michache ijayo.

Polisi Dar wachimba mkwara mzito kuelekea sikukuu ya Eid

http://www.ippmedia.com/media/picture/large/Kova1(3)(2)(3).jpg
Kamanda Kova
JESHI la Polisi Kanda Maalum Mkoa wa Dar es Salaam imewatahadharisha na kuwaonya wakazi wa jiji hilo kuhusiana na vitendo vya uhalifu wakati wa kuelekea sikukuu ya Idd el Fitri ikiwataka kuwafichua wahalifu wanaoishi nao kabla kuingia matatani wahalifu hao watakapokamatwa.
Aidha jeshi hilo limesema limejipanga vyema katika kukabiliana na vitendo vyovyote vya uhalifu kwa kupeana mbinu mpya na kuwataka wakazi wa jiji hilo la Dar es Salaam kutokuwa na hofu yoyote na kuwahimisha wafanyabiashara kufanya shughuli zao kwa amani na utulivu bila mchecheto.
Kamanda wa Polisi kanda hiyo, Suleiman Kova, alisema jeshi lao limejipanga vyema kukabiliana na vitendo vyote vya uhalifu kuelekea katika sikukuu na wakati wa sikukuu yenyewe, lakini akasema wanawategemea ushirikiano wa wananchi kwa kuwafichua wahalifu hao mahali walipo.
Kamanda Kova, alisema kwa vile wahalifu wanaishi katika nyumba za wakazi hao, ni wajibu wao kuwafichua wahalifu au watu wanaowatilia shaka ili Polisi lifanye kazi zake na ikitokea wahalifu hao wakaachwa hadi waje wakamatwe basi wahusika wa nyumba au eneo hilo wataingizwa matatani.
"Kama wananchi wanajua mahali walipo wahalifu au wanaishi nao na kushindwa kuwafichua siku tukiwatia mikononi watambue wenye nyumba hiyo nayo wataunganishwa pamoja na wahalifu hao, hivyo tunawatahadharisha na kuwaomba raia wema wasifumbie macho uhalifu," alisema Kova.
Aliongeza, Polisi wamejipanga kukabiliana na vitendo vyote vya uhalifu na hasa uvamizi wa kwenye maeneo ya biashara katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye sikukuu, lakini pia wanajitaji msaada na ushirikiano mkubwa toka kwa raia wema kudhibiti vitendo hivyo.
Kadhalika aliwatoa hofu wafanyabiashara na wateja wao kuwa wafanye shughuli zao kwa amani na utulivu kwa vile Polisi wamejipanga na kutawanya vijana wao kila mahali kuhakikisha jiji la Dar es Salaam na raia wake wanakuwa katika hali ya utulivu na salama.
Kamanda Kova alisema jeshi la Polisi linajisikia vibaya kuona raia wake wakiishi kwa wasiwasi mkubwa wa matendo ya uhalifu na hasa mtindo mpya wa kihalifu uliozuka hivi  karibuni wa kutumia pikipiki na kwamba wamehamasishana na kupeana mbinu mpya kukabili vitendo hivyo.
Kova aliyasema hayo mapema leo asubuhi wakati akihojiwa kwenye kipindi cha Kumepambazuka cha Radio One Stereo.

Sunday, July 28, 2013

Coastal Union yazidi kutisha, yainyuka Simba kidude

 
TIMU ya soka ya Coastal Union ya Tanga imeendelea kuvitisha vigogo vya soka nchini ikiwa ni mwezi mmoja kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu  wa 2013-2014 baada ya jioni hii kuikwanyua Simba kwa bao 1-0 katika mechi ya kirafiki.
Ushindi huo ni wa pili mfululizo kwa mabingwa hao wa zamani wa soka nchini baada ya katikati ya wiki kuutafuna mfupa uliovishinda vigogo hivyo kwa URA baada ya kuwalaza Waganda hao bao 1-0.
Kabla ya kipigo hicho URA iliilaza Simba mabao 2-1 na kukaribia kuiadhiri Yanga kabla ya mabingwa hao wa kandanda nchini kuchimoa dakika za lala salama na kuambulia sare ya mabao 2-2.
Pambano la leo lililochezwa kwenye uwanja wa Mkwakwani Tanga ilishuhudiwa hadi wakati wa mapumziko kukiwa hakuna mbabe yeyote baada ya timu zote kutoshanga nguvu ya kutofungana.,
Hata hivyo katika kipindi cha pili Coastal walionyesha ilivyopania msimu ujao kwa kuwakimbiza Simba na kujipatia bao pkee lililowekwa kimiani na mchezaji wao mpya toka Kenya,  Crispian Odula Odwenye aliyefunga katika dakika 54.
Hicho ni kipigo kingine kwa Simba katika mechi zake za karibu za kirafiki za kujipima nguvu na inamfanya kocha wake, King Abdallah Kibadeni kurekebisha mapema kikosi chake kabla ya ligi.
 

ZIARA YA RAIS JAKAYA KIKWETE WILAYANI KARAGWE KAGERA

  Rais Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi ujenzi wa barabara ya Kagoma-Lusahunga katika wilayani BiharamuloRais Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi ujenzi wa barabara ya Kagoma-Lusahunga katika wilayani Biharamulo Rais Kikwete akipiga picha ya kumbukumbu na wananchi wa Ngara baada ya kuzindua kivuko cha MV Ruvuvu katika mto Rusumo Jumamosi Julai 27, 2013Rais Kikwete akipiga picha ya kumbukumbu na wananchi wa Ngara baada ya kuzindua kivuko cha MV Ruvuvu katika mto Rusumo  Rais Kikwete akishiriki kupiga ngoma na kikundi cha utamaduni cha Ngara wakati wa uzinduzi wa kivuko cha MV Ruvuvu katika mto Rusumo wilayani NgaraRais Kikwete akishiriki kupiga ngoma na kikundi cha utamaduni cha Ngara wakati wa uzinduzi wa kivuko cha MV Ruvuvu katika mto Rusumo wilayani Ngara Rais Kikwete akisimikwa kuwa chifu wa Wahaya na kukakabidhiwa mgolole na silaha za jadi za Wahaya katika sherehe ya kuzindua wilaya mpya ya Kyerwa (1)Rais Kikwete akisimikwa kuwa chifu wa Wahaya na kukakabidhiwa mgolole na silaha za jadi za Wahaya katika sherehe ya kuzindua wilaya mpya ya Kyerwa Rais Kikwete akisimikwa kuwa chifu wa Wahaya na kukakabidhiwa mgolole na silaha za jadi za Wahaya katika sherehe ya kuzindua wilaya mpya ya Kyerwa (2)Rais Kikwete akisimikwa kuwa chifu wa Wahaya na kukakabidhiwa mgolole na silaha za jadi za Wahaya katika sherehe ya kuzindua wilaya mpya ya Kyerwa Umati uliojitokeza katika sherehe za uzinduzi wa wilaya mpya ya Kyerwa (2)Umati uliojitokeza katika sherehe za uzinduzi wa wilaya mpya ya Kyerwa Umati uliojitokeza katika sherehe za uzinduzi wa wilaya mpya ya Kyerwa (3)Umati uliojitokeza katika sherehe za uzinduzi wa wilaya mpya ya Kyerwa Umati uliojitokeza katika sherehe za uzinduzi wa wilaya mpya ya Kyerwa (4)Umati uliojitokeza katika sherehe za uzinduzi wa wilaya mpya ya Kyerwa Wananchi wakimshangilia Rais Kikwete aliposimama kwa muda kuwasslimia wilayani Karagwe akielekea Rusumo kuzindua kivuko cha Ruvuvu (1)Wananchi wakimshangilia Rais Kikwete aliposimama kwa muda kuwasslimia wilayani Karagwe akielekea Rusumo kuzindua kivuko cha Ruvuvu Wananchi wakimshangilia Rais Kikwete aliposimama kwa muda kuwasslimia wilayani Karagwe akielekea Rusumo kuzindua kivuko cha Ruvuvu (2)Wananchi wakimshangilia Rais Kikwete aliposimama kwa muda kuwasslimia wilayani Karagwe akielekea Rusumo kuzindua kivuko cha Ruvuvu Wananchi wakimshangilia Rais Kikwete baada ya kuzindua  kivuko cha MV Ruvuvu  Jumamosi Julai 27, 2013 (1)Wananchi wakimshangilia Rais Kikwete baada ya kuzindua kivuko cha MV Ruvuvu jana Jumamosi Wananchi wakimshangilia Rais Kikwete baada ya kuzindua  kivuko cha MV Ruvuvu  Jumamosi Julai 27, 2013 (2)Wananchi wakimshangilia Rais Kikwete baada ya kuzindua kivuko cha MV Ruvuvu  Kivuko cha zamani kilichokuwa kikitumiwa na wananchi wa Ngara kuvuka mto RusumoKivuko cha zamani kilichokuwa kikitumiwa na wananchi wa Ngara kuvuka mto Rusumo Kivuko kipya cha MV Ruvuvu katika mto Rusumo kilichozinduliwa na Rais Kikwete Jumamosi Julai 27, 2013Kivuko kipya cha MV Ruvuvu katika mto Rusumo kilichozinduliwa na Rais Kikwete Rais Kikwete akihutubia umati NgaraRais Kikwete akiongea na wananchi katika sherehe ya kuzindua mradi wa umeme vijijini katika kijiji cha Nyaishozi, Wilaya ya Karagwe Rais Jakaya Kikwete yuko mkoani Kagera kwa ziara ya kikazi ya siku nane(PICHA NA IKULU)

Nape Nnauye ayakana kuwatusi wazee


KATIBU Mwenezi na Itikadi wa CCM, Nape Nnauye ameamua  kuvunja  ukimya  na  kutoa  utetezi  wake  kuhusu  kauli  yake chafu  iliyochapishwa  na moja ya magazeti maarufu nchini lililotuhumu kuwatusi  wazee  waliopendekeza  uwepo  wa  serikali  tatu kwa madai kwamba wanaodai serikali hizo wanakaribia kufa

Huu  ndiyo utetezi  wake:

"Nimestushwa sana na stori ya gazeti la Mtanzania inayodai kuninukuu kuwa nimesema wazee waliopendekeza serikali tatu wanasubiri kufa!

Kwakweli nimesikitishwa sana hata na jinsi maneno ndani yalivyopangiliwa kiasi kwamba inanipa tabu kuamini kama mhariri aliipitia hii stori ukiachilia mbali kama aliyetumwa kuja kuandika stori alikuwa ni "too junior".

Nawaheshimu sana wazee wangu hawa hata kama nikipishana nao kimawazo siwezi kufikia kutamka maneno makali kiasi hicho.

Nilichosema ni kuwa ukilinganisha vijana na wazee, vijana wana wajibu mkubwa wa kuamua kesho yao badala ya kudhani kuna mtu atawaamulia. Hivyo wana wajibu mkubwa kwani takwimu zinaonyesha asilimia 60% ya idadi ya watu nchini ni vijana! Sasa sijui kama kwa mwandishi na mhariri wake tafsiri ndio hiyo?!!!

Imenisikitisha  sana!

Nape Moses Nnauye
The CCM Secretary for Ideology & Publicity"

AT sasa aamua kupenda



AT katika poz



Na Elizabeth John
BAADA ya kutamba na ngoma yake ya ‘Kitumbua’, mkali wa muziki wa mduara nchini, Ally Ramadhan 'AT' anatarajia kuachia kazi mpya inayokwenda kwa jina la ‘Anapenda’.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, nyota huyo alisema kazi hiyo anatarajia kuisambaza katika vituo mbalimbali vya radio baada ya kukamilika.

“Nashukuru Mungu kupata nafasi nyingine tena ya kurudi katika kazi yangu baada ya kimya kisichojulikana," alisema.

Msanii huyo ambaye anajulikana kama mfalume wa muziki huo kwa sasa alifanya vizuri na vibao mbalimbali kikiwemo Kifuu Tundu, Bao la Kate na nyinginezo ambazo zilimpa umaarufu mkubwa katika tasnia ya muziki huo.

Pia mkali huyo yuko katika hatua za mwisho kukamilisha video ya kazi yake inayoitwa ‘Kitumbua’, ambayo muda wote itaanza kuonekana kupitia kwenye runinga runinga na akiamini utapata nafasi kubwa ya kuwakonga mashabiki wa tasnia hiyo.

Hivyo, aliwaomba mashabiki kumuunga mkono katika kazi zake zijazo ili kuhakikisha anafikia malengo aliyojiwekea katika tasnia hiyo ya muziki wa kizazi kipya nchini hususan wa ‘Mduara’ ambao anaendelea kufanya vizuri na kutishia waliopo kwenye burudani hiyo.

Maugo, Mwakyembe wachezea vichapo Russia

Mada maugo
Benson Mwakyembe
MABONDIA Mada Maugo na Benson Mwakyembe waliondoka nchini na tambo za kufanya kweli nchini Russia wamejikuta wakiambulia vipigo toka kwa wenyeji wao waliopambana nao jana nchini humo.
Maugo yeye alikumbana na kipigo cha TKO ya raundi ya tano toka kwa Movsur Yusupov katika pambano la uzito wa Super Middle la raundi nane.
Bondia huyo mwenye maneno mengi alisalimu amri mwenyewe katika pambano hilo lililoichezwa kwenye viwanja wa Trade & Entertainment Centre 'Moskva' Kaspiysk.

Naye Benson Mwakyembe alijikuta akichezea kichapo cha KO  ya raundi ya saba toka kwa Apti Ustarkhanov. Kama ilivyokuwa kwa pambano la Mtanzania mwenzake, Mwakyembe na mwenyeji wake walipigana katika uzito wa kilo 75 la raundi nane.
Mabondia hap walioondoka wakiapa kwenda kuwashikisha adabu wapinzani wao wanatarajiwa kurejea nchini kesho kutwa tayari na maandalizi ya mapambano yao mengine.
Maugo anatarajiwa kupanda ulingoni Agosti 30 dhidi ya Thomas Mashali katika moja ya mapambano yatakayosindikiza pigano kati ya Francis Cheka na Mmarekani Findley Derrick la kuwania ubingwa wa WBF litakalochezwa Diamond Jubilee.

Hatimaye Mbowe asalimisha ushahidi wa bomu la Arusha Polisi

HATIMAYE Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, jana amewasilisha kwa maandishi ushahidi wake makao makuu ya Jeshi la Polisi mjini Dar es Salaam. Maelezo ya Mbowe ambayo jana yaliwasilishwa, yamekuwa siri nzito, kwani yanatokana na msimamo wa CHADEMA kudai wana ushahidi na tukio la mauaji ya mlipuko wa bomu lililotokea Juni 15, mwaka huu mkoani Arusha. Wakili wa Mbowe, Peter Kibatala alilithibitishia MTANZANIA mjini Dar es Salaam jana, kuwa aliwasilisha saa 5 asubuhi ambapo alipokelewa na Mkuu wa Idara ya Operesheni za Upelelezi Tanzania (CID), Kamishna Advocate Nyombi.

Baada ya kuwasilisha maelezo hayo, Wakili Kibatala alikataa katakata kuzungumzia kilichomo ndani ya maandishi hayo, kwa madai kuwa ni siri yao na polisi.

“Nathibitisha bila shaka, nimewasilisha majibu kwa niaba ya Mbowe leo (jana), makao makuu ya polisi kama tulivyokubaliana, lakini yaliyoandikwa humo ni siri…siwezi kuzijadili tusubiri kutoka kwao,” alisema Kibatala.

Hatua ya kuwasilisha majibu hayo kimaandishi, ilifikiwa Jumatano wiki hii katika mahojiano baina ya Polisi na Mbowe.

Siku hiyo, Mbowe aligoma kuwasilisha ushahidi wake polisi kama alivyotakiwa kwenye barua aliyoandikiwa na jeshi hilo Julai 17, mwaka huu, kwa kile alichosema hadi Rais Jakaya Kikwete atakapounda tume ya kijaji kuchunguza tukio hilo.

Katika barua hiyo, Mbowe alitakiwa kufika bila kukosa akiwa na ushahidi wa mauaji ya mlipuko wa bomu hilo.

Hata hivyo, Mbowe aliripoti kuitikia wito wa barua hiyo, lakini aliendelea kushikilia msimamo wake wa kutowasilisha ushahidi huo kwa polisi.

Jeshi la Polisi, limekuwa katika mvutano na Mbowe likimtaka kuwasilisha ushahidi kuhusu mlipuko wa bomu hilo, katika Uwanja wa Soweto wakati wa mkutano wa kuhitimisha kampeni za uchaguzi mdogo wa madiwani katika kata nne na kuua watu wanne na kujeruhi wengine 70, katika uwanja huo ushahidi ambao alidai anao.

Endapo Mbowe atakutwa na hatia ya kutokuwa na ushahidi huo, atakumbwa na adhabu ya miaka mitatu jela au faini ya Sh 500,000.

Hii ni kwa mujibu wa Jeshi la Polisi katika barua yake kwa Mbowe, ikunukuu kifungu cha sheria ya kifungu cha 10(2) na (2A) cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai nchini, sura ya 20, kama ilivyorekebishwa mwaka 2002.

Aibu kwa Taifa! Watanzania wengine wanaswa na 'unga' ughaibuni

Baadhi ya Dawa za kulevya zikiwa zimenaswa
WIKI chache baada ya watanzania kadhaa akiwamo video Queen', Agnes Gerrard 'Masogange' na nduguye Mellisa Edward kunaswa Afrika Kusini na dawa za kulevya, watanzania wengine wawili wamekamatwa na dawa hizo huko Hongkong.
Taarifa zilizochapishwa na serikali ya nchi hiyo imesema watanzania hao ni kati ya abiria watatu walionaswa kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa nchi hiyo juzi wakiwa na 'unga' wenye thamani ya Dola za Kimarekani Milioni 3.34.
Taarifa hiyo imekuja siku chache tu baada ya mmoja wa wafungwa waliokamatwa nchini humo kwa kosa na kuingiza dawa hizo za kulevya kutuma waraka unaoeleza Tanzania ilivyochafuka ughaibuni kwa biashara hiyo kiasi kwamba Wabongo wanapekuliwa uchi wa nyama wafikapo uwanja wa ndege wa Hongkong.
Mfungwa huyo aliweka bayana namna biashara hiyo ilivyokithiri na kuhusisha vigogo wa serikali, wabunge na hata watu wenye thamani ya ulinzi na usalama wa raia.
Jisomee taarifa hiyo ya kukamatwa kwa watanzania hao ikiwa ni muendelezo wa raia wa Taifa hilo lililokuwa na sifa nzuri mbele ya macho ya dunia kunaswa wakiingiza dawa hizo katika mataifa mengine baadhi ikielezwa wamenyongwa CHINA na kuhukumiwa vifungo vya muda mrefu kama kilichowakuta mabondia wa Tanzania nchini Mauritius hivi karibuni.
Taarifa hiyo ya serikali ya Hongkong ilipachikwa katika tovuti yao juzi Julai 26, 2013.



Hong Kong Customs yesterday (July 25) detected three drug trafficking cases, with seizures totally valued at $4.78 million, in the department's escalated anti-narcotics efforts to combat drugs.

Customs officers at the Hong Kong International Airport (HKIA) intercepted a 26-year-old incoming male passenger arriving from Tanzania for clearance yesterday afternoon and seized 1.6 kilogrammes of heroin concealed in two false compartments of his hand carry briefcase. The drugs would fetch a value of about $1.28 million.

Later in the evening, Customs officers at the HKIA intercepted another 45-year-old man from Tanzania for clearance. On suspicion of concealment of drugs inside his body, the suspect was escorted to hospital where he discharged 204 grammes of heroin after staying for one day. The value of the drugs was about $0.16 million. The suspect is still in the hospital.

In the same evening, Customs officers intercepted a 28-year-old man at a carpark in Tai Kok Tsui. Approximately 2.03 kg of cocaine camouflaged as snacks were found inside a plastic bag carried by him.

Customs officers later escorted the suspect to a domestic flat nearby for a search and seized 1 kg of cocaine and 290 grammes of crack cocaine there. The total value of the seizure was about $3.34 million.

A Customs spokesperson said today (July 26) that all three suspects in the three cases were arrested for drug trafficking. The cases are still under investigation.

Under the Dangerous Drugs Ordinance, drug trafficking is a serious offence. The maximum penalty is life imprisonment and a fine of $5 million.

Ends/Friday, July 26, 2013
Issued at HKT 23:43

Mama amchoma mwanae mikono kisa kala samaki badala ya maharage

MTOTO Bryton Evarist (9) mkazi wa Temeke, Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, amejeruhiwa vibaya baada ya kuunguzwa mikono kwa kubanikwa kwenye jiko la mkaa na mama yake mzazi.

Mwanamke aliyefanya unyama huo ni  Asa Barnaba (24), ambapo inadaiwa baada ya tukio hilo alimfungia ndani kwa muda wa wiki mmoja na kumlazimisha kula na kuoga kwa kutumia mikono aliyomuunguza.

Tukio hilo linadaiwa kufanywa wiki tatu zilizopita majira ya usiku, baada ya mtoto huyo kudaiwa kula samaki wa kitoweo.

Akisimulia mkasa huo akiwa Hopitali ya Temeke, mtoto huyo ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tatu Shule ya Msingi Kibasila, alisema mama yake alichukua hatua hiyo baada ya kukasirishwa na kitendo hicho.

Alisema siku ya tukio, alirudi nyumbani mapema akitokea shuleni, alipofika nyumbani kwao alikuta chakula pamoja na mboga mbili aina ya maharage na samaki.

Bila ya kutambua kwamba samaki hao waliwekwa kwa ajili ya kitoweo cha usiku, aliamua kula na kuyaacha maharage.

"Mama aliporudi na kukuta nimekula samaki, aliniuliza kwa nini nimekula, lakini nilikataa kwa kuogopa kupigwa," alisema.

Hata hivyo, baada ya kubanwa sana, mtoto huyo aliamua kukubali kula ndipo mama yake alipochukua jiko la mkaa lenye moto na kumuweka mikono yake juu ya moto uliokuwa unawaka.
"Alichukua mikono yangu na kuniweka kwenye jiko, nilihisi maumivu makali sana," alisema.

SIRI YABAINIKA
Akiongea na NIPASHE Jumamosi, Afisa Ustawi wa Jamii wa Manispaa ya Temeke, Sharifa Ally, alisema mtoto huyo aligundulika kufanyiwa unyama huo baada ya wiki moja akiwa katika hali mbaya.
Alisema aligundulika baada ya kutoroka na kwenda kuomba msaada kwa wapita njia ili wamsaidie kumpeleka hospitali.

"Inashangaza sana kuona mama mzazi akiwa na moyo wa kikatili, muda wote alikuwa akienda kazini na kumuacha mtoto wake ndani akioza mikono," alisema Sharifa.

Sharifa, alisema hatua hiyo ilisaidia mtoto huyo kupelekwa kituo cha Polisi cha Chang'ombe na kisha kufikishwa Hospitali ya Temeke.

"Akiwa hospitalini, sisi Ustawi wa Jamii na Jeshi la Polisi tulisimamia kwa karibu matibabu yake pamoja kuangalia namna na kumfungulia kesi mhusika," alisema.

MAMA AKIRI
Mama wa mtoto huyo alipoulizwa sababu ya kufanya kitendo hicho, alisema aliamua kumchoma moto mtoto wake baada ya kuchoshwa na tabia yake ya wizi kwa muda mrefu.

"Huyu mtoto ana tabia ya wizi, mwanzo alikuwa akiniibia hela ndani, nilimuonya sana na wakati mwingine nilimpiga lakini hakusikia, ndipo alipokula mboga niliamua kumchoma moto ili asirudie," alisema Asa.

Hata hivyo, alisema anajutia kufanya tukio hilo na hakufikiria kwamba mtoto wake angepata majeraha kama aliyonayo kwa sasa.

Baba wa mtoto huyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Evarist akiongea kwa simu kutoka mkoani Kigoma, alisema bado hajapata taarifa ya tukio hilo na alionyesha kusikitishwa kwake.

"Aisee! sijapata kabisa taarifa ya jambo hilo, nasikitika sana," alisema na kukata simu.

Alipotafutwa Kamanda wa Mkoa wa Polisi wa Temeke, Engelbert Kiondo kwa njia ya simu, hakupatikana baada ya mtu aliyepokea kueleza yupo nje kikazi.
CHANZO: NIPASHE

Lion Boy amtwanga Mthailand kwa KO

Omari Kimweri
BONDIA Mtanzania Omari Kimweri  'Lion Boy' anayefanya shughuli zake nchini  Australia ameendelea kutamba katika nchi hiyo baada ya jana kumtwanga kwa  KO ya raundi ya kwanza bondia Ekkalak Saenchan wa Thailand   ikiwa ni mchezo wake wa 16 tangu aingie katika ngumi za kulipwa nchini humo 
Bondia huyo ambaye anaitangaza vyema nchi ya Tanzania Kimataifa ameahidi kuenderea kutoa vipigo kwa mabondia  mbalimbali  pindi wakutanapo ulingoni 
Bondia huyo aliyezaliwa Tanzania katika jiji la Dar es salaam mwaka1982 amekuwa gumzo nchini humo kwa kuonesha mchezo mzuri unaowavutia raia wengi wa Australia na kuweza kuwa bondia namba moja katika nchi hiyo huku katika Dunia akishikilia nafasi ya 52 katika mabondia 450 duniani wenye uzito wa light flyweight

Anasema lengo lake kubwa ni kuukamata ubingwa unaotambulika kimataifa Duniani wa WBA World light flyweight title unaoshikiliwa na bingwa namba moja Duniani ,Roman Gonzalez na IBF light flyweight title   unaoshikiliwa na  John Riel Casimero wa  Philippines ambao wanamuumiza kichwa.