STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, August 3, 2013

Kazimoto asaini mwaka Al Markhiya

Mwinyi Kazimoto
ALIYEKUWA kiungo wa Simba Mwinyi Kazimoto jana amesaini mkataba wa mwaka mmoja na nusu kwa ajili kuitumikia klabu ya Al Markhiya SC ya Doha, Qatar.
Habari za uhakika kutoka Qatar zinaeleza kwamba, Kazimoto amesaini mkataba baada ya kufaulu majaribio yake, sambamba na kukubaliana na uongozi ofa aliyopewa.
Imeelezwa kwamba, hatua ya Kazimoto kusaini mkataba huo imekuja baada ya uongozi wa timu hiyo kuongeza dau la kumnunua baada ya awali kugomea kwa madai kuwa halilingani na thamani waliyomnunulia.
Chanzo hicho kimeeleza kwamba, Al Markhiya iliwaangukia Simba kwa dau waliloafikiana kutokana na ukweli kwamba kwa sasa ipo katika hali mbaya ya kifedha na hasa ikizingatiwa kuwa wanahitaji kusajili wachezaji watakaoipandisdha tena daraja.
“Unajua timu imeshuka daraja hivi karibuni sasa wanajiimarisha kwa kusajili wachezaji wazuri na fedha waliyonayo haitoshelezi hivyo wameiomba Simba ipokee hicho walichonacho,”kilieleza chanzo hicho.
Juzi uongozi wa Simba kupitia kwa msemaji wake Ezekiel Kamwaga ulisema umeitupilia mbali ofa iliyotumwa na klabu hiyo kwa madai kuwa ni ya kipuuzi, huku ikidai pia Kazimoto ana maswali kwanza ya kujibu kwa Watanzania na mashabiki wa Simba kwa ujumla.
Simba pia ilidai inakusudia kuketi na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa ajili ya kumjadili nyota huyo kwa kitendo chake cha kutoroka nchini.

Kazimoto ambaye alisajiliwa na Simba mwaka juzi kutokea JKT Ruvu, alitoroka nchini akiwa na timu timu ya Taifa iliyokuwa ikijiandaa na mechi yake ya kufuzu fainali za Afrika zinazoshirikisha nyota wanaocheza ligi za ndani (CHAN) dhidi ya Uganda ‘The Cranes’.
 
Sports Lady

Mtanzania mwingine anaswa na 'Unga'' Zimbabwe


WIMBI la kukamatwa kwa watanzania nje ya nchi wakiwa na dawa za kulevya likiendelea kuzua mjadala nchini, Mwanamke mwingine wa Kitanzania anadaiwa kunaswa Zimbabwe akiwa na 'unga' unaokadiriwa kuwa na thamani yaDola za 45,000 akitokea India.
Mwanamke huyo aliyetajwa kwa jina la Jacklyne Mollel (34) anayeishi Afrika Kusini, inadaiwa alinaswa kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Harare Julai 27 akiwa na dawa hizo zenye uzito wa kilo 15 alipowasili na ndege ya Emirates akitokea India.
Taarifa zaidi zinasema mtanzania huyo ameshafikishwa mahakamani akikabiliwa na kesi hiyo ya kuingiza dawa hizo aina ya Ephedrine zikiwa na uzito wa Kilo 15 na kusomewa shtaka lake mbele ya Hakimu Mkazi Donald Ndirowei juzi jijini humo.

ISOME TAARIFA NZIMA ILIYORIPOTIWA NCHINI HUMO JUU YA MKASA HUO

A 34–year–old Tanzanian woman was last week arrested at the Harare International Airport after she was found in possession of an illicit drug with a street value of $45 000 upon arrival from India.
SENIOR REPORTER
Mollel Jackline Richard, who stays in South Africa, was not asked to plead when she appeared before Harare magistrate Donald Ndirowei yesterday.
She was remanded in custody to July 27.
Richard was allegedly found in possession of 15kg of ephedrine which stimulates the heart and nervous system. It is often found in herbal and diet pills.
The State alleged that Richard arrived at Harare International Airport aboard an Emirates flight from India.
The alleged drug pusher produced her passport at the immigration desk at the airport where an alert officer tipped CID Drugs detectives that Richard had a visa for India which is a known source for illicit drugs.
The court heard that Richard was taken for interviewing and during a search conducted on her by detectives they recovered 30 khaki envelopes containing a whitish substance which was wrapped with fabric sheets inside a maroon bag.
Tests were conducted on the substance and revealed that it was ephedrine. The drug was then taken for recording and weighing.

Friday, August 2, 2013

Nyota wa zamani wa Coastal Union afariki kwa ajali ya gari Morogoro



SOURCE: SALUTI5

Ronaldo kurudi OT kumpisha Bale Real Madrid?

Ronaldo akifurahia jambo
KLABU ya Real Madrid wapo tayari kumuuza Cristiano Ronaldo kwenda Manchester United mwezi huu baada ya nahodha huyo wa Ureno kukataa kuanza mazungumzo ya mkataba mpya.

Gazeti la Daily Star limedokeza kuwa, Mashetani Wekundu na Real Madrid wametumia siku 12 zilizopita kuzungumza juu ya ada ya uhamisho ya pauni mil. 80 na mabingwa wa EPL wamezidi kupata uhakika wa kumrudisha kipenzi chao Old Trafford. 

Rais wa Real, Florentino Perez mwanzoni alitaka kwamba uhakika kutoka kwa Ronaldo kama yupo tayari kusaini mkataba mpya na alishangazwa na mchezaji kuwa alikuwa tayari kurudi United. 

Hilo lilipelekea Madrid kufungua mazungumzo rasmi na United, wakitambua kwamba wanaweza wakamuuza kwa fedha kidogo ikiwa winga huyo atabakia kwamwaka mmoja zaidi ndani ya Bernabeu kwa kuwa atakuwa amebakisha mkataba wa mwaka mmoja tu.  

Lakini pia imeonekana wazi kwamba Madrid wanataka kumpata mbadala wa Ronaldo - Gareth Bale ambaye tayari wameshatoa ofa ya Pauni Mil. 85m kwa Spurs.
Mapema wiki hii aliyekuwa raisi wa Madrid - Ramon Calderon alikaririwa akisema kwamba Madrid wanajiandaa kumuuza Ronaldo na ndio maana wanafanya kila liwezekanalo kumsajili Gareth Bale kutoka Tottenham.

Ikumbukwe pia wakati akiwa bado kocha wa Man United Sir Alex Ferguson alikarriwa akisema kila kipo sawa kwa ajili ya usajili wa mchezaji mkubwa wakati wa dirisha kubwa la usajili litakapofunguliwa. 
Kadhalika wakati akihojiwa na BBC hivi karibuni aliyekuwa msaidizi wa Ferguson - Mike Phelan aliulizwa kama boss wake alikuwa akimzungumzia Ronaldo aliposema kuhusu usajili wa mchezaji mkubwa? Phelan alishindwa kukataa wala kukubali kuhusu suala hilo, akisema "no comment'. 

Rais JK akutana na kiongozi wa IYF ya Korea Kusini

RAISI Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na Kiongozi wa taasisi ya International Youth Foundation (IYF) ya Korea Kusini Mchungaji Ock Soo Park pamoja na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara na ujumbe wa IYF Ikulu jijini Dar es salaam
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akijadili chapisho la kitabu na Kiongozi wa taasisi ya International Youth Foundation (IYF) ya Korea Kusini Mchungaji Ock Soo Park aliyemtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo. Kushoto ni mkaliman
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na Kiongozi wa taasisi ya International Youth Foundation (IYF) ya Korea Kusini Ock Soo Park Ikulu jijini Dar esSalaam. (PICHA na IKULU)

102 kuiwakilisha JWTZ katika michezo ya EAC


 

WANAMICHEZO 102 kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) watashiriki katika michezo ya majeshi kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ambayo itafanyika Nairobi, Kenya kuanzia tarehe Jumatatu Agosti 5, 2013 hadi Agosti 17, 2013.

Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania alitarajiwa kukabidhi Bendera ya Taifa kwa wanamichezo hao mchana huu tukio ambalo lilitarajiwa kufanyika bwalo la askari katika kambi ya Twalipo Administration Unit (TAU) iliyopo mkabala na Chuo cha Uhasibu,       Dar es salaam.

Vyombo vya Habari vinakaribishwa kuchukua matukio katika hafla hiyo ya makabidhiano.

Kwa mawasiliano zaidi tel no_0715 270 236, 0754 270 236

Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
                            SLP 9203

Email:ulinzimagazine@yahoo.co.uk

Flaviana Matata azidi kupasua anga, atajwa katika list ya Forbes Africa Magazine Model

Flanianamatata

FORBES AFRICA Releases Forbes Africa's Magazine Model List for 2013. Angolan Model Maria Borges Tops The List

Announced a few days ago by FORBES AFRICA, a 21-year-old Angolan model Maria Borges makes the tops Forbes Africa's Magazine Model List for 2013 making her the hottest item of the moment in the catwalk. The magazine will hit stands on August 1st, so grab your copy for the list where other African models that came close to snatching the title for number 1 include Ajak Deng from Sudan, Grace Bol from Sudan, Candice Swanepoel of South Africa, Liya Kebede of Ethiopia, Katryn Kruger of South African and Miss Universe competitor Flaviana matata.
Maria-Borges-Forbes-Africa-Top-Model-BellaNaija-July2013-8-400x600
Maria Borgas

Mwanamke amuua mumewe kwa kisu, kisa....!

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma

JESHI la Polisi Mkoa wa Dodoma linamshikilia mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Jerida Jackson (33) mkazi wa Gulwe wilayani Mpwapwa kwa tuhuma na kumuua mume wake kwa kumchoma kisu kifuani .
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari Kamanda wa Polisi mkoani humo, David Misime alisema kuwa tukio hilo lilitokea Julai 31, mwaka huu saa nane usiku nyumbani kwao Godegode Mpwapwa.  
Misime alieleza kuwa mauaji hayo yalitokea baada ya marehemu kumgombeza mtoto wake ndipo kukatokea mtafaruku baina yao hali iliyosababisha mtuhumiwa kumchoma kisu. 
“Marehemu alimgombeza mtoto wake ndipo mtuhumiwa alihoji kwa nini anamgombeza mtoto baada ya kuhoji ndipo ukatokea mtafaruku baina yao na kumchoma mumewe kisu kifuani hadi kufikwa na mauti hayo,” alisema Misime.  
Aidha alimtaja marehemu kuwa ni Ramadhani Chiduo (41) ambapo Misime alitoa wito kwa wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi hali ambayo imekuwa ikisababisha madhara ikiwemo kifo na kuwataka kuwa na subira wakati inapotokea hali kama hiyo ya kutoelewana,

Hatimaye Owino awatuliza wanamsimbazi

BEKI wa kutumainiwa wa timu ya URA ya Uganda, Joseph Owino (kati waliokaa) akitia saini mkataba wa wa kuichezea Simba kwa miaka miwili.

MCHEZAJI wa nafasi ya beki wa kati aliyekuwa akiichezea URA, Joseph Owino hatimaye ametua Msimbazi baada ya jana kusaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Simba.

Owino alisaini mkataba huo jijini Dar es Salaam na kutuliza akili za wanamsimbazi ambao kikosi chao kilikuwa na tatizo la beki wa kati na kutua kwake ni kama amelimaliza tatizo hilo, ikizingatiwa kuwa alishawahi kukipiga katika timu hiyo.

Beki huyo alishaichezea Simba misimu miwili iliyopita kabla ya kuumia na kusajiliwa na Azam ambao walimgharamia matibabu kisha kumuacha na kurejea URA alikoendeleza 'libeneke' kiasi cha kuzifanya timu kadhaa kummezea mate ikiwamo Simba.

Kabla ya kutua nchini Owino alishawahi kuidokeza MICHARAZO kwamba alikuwa tayari kurejea Bongo kukipiga timu yoyote itakayomridhisha kimasilahi na hivyo kutua kwake Msimbazi kumetimiza madai yake hayo, japo awali kulikuwa na taarifa za sintofahamu.

Taarifa hizo zilidai kuwa huenda beki huyo mpole asingerejea Bongo kwa vile alikuwa amepata dili ya mamilioni ya fedha katika nchi za Arabuni na Ulaya ya Mashariki, lakini kutua kwake kumekata kilimilimi chote cha waliodai asingerejea tena Simba.

Simba inayoonyesha imedhamiria msimu huu, pia ilikuwa ikijiandaa kumsainisha beki mwingine wa kimataifa toka Burundi ili kuimarisha safu hiyo ya ulinzi baada ya awali kumnasa Issa Rashid 'Baba Ubaya' toka Mtibwa.

Twanga Pepeta kumtambulisha Ige Moyaba, wanenguaji wapya

http://thumbp4-ne1.thumb.mail.yahoo.com/tn?sid=2126005954&mid=AH7kimIAAAktUfuJcwAAAEaSIh8&midoffset=2_0_0_1_1265588&partid=2&f=1215&fid=Inbox&w=480&h=331
BENDI maarufu ya African Stars 'Twanga Pepeta' inatarajiwa kumtambulisha muimbaji wake wa zamani aliyekuwa ametimkia ughaibuni, Ige Moyaba katika onyesho maalum la shamrashamra za sikukuu ya Eid el Fitri litakalofanyika kwenye ukumbi wa Mango Garden siku ya Idd Pili.
Onyesho hilo ambalo pia litatumiwa na Twanga Pepeta kutambulisha waneguaji wake wapya limeandaliw ana kampuni ya Bob Entertainment na warembo watakaochuana kwenye kinyang'anyiro cha Redd's Miss Ilala 2013 nao watatambulishwa jukwaani siku hiyo.

Golden Bush Fc yawakumbuka yatima Sikukuu ya Eid el Fitry

 
Kikosi cha timu ya Golgen Bush Veterani katika picha ya pamoja walipokuwa mjini Morogoro kwa mechi zao za kirafiki

TIMU ya soka ya Golden Bush FC inayojumuisha timu ya veterani na ile ya vijana inayoshiriki Ligi Daraja la Nne Wilayani Kinondoni, siku ya Jumapili inatarajiwa kugawa msaada wa vyakula na vitu vingine kwa yatima wanaolelewa katika kituo cha New Orphans Family, kilichopo Kigogo jijini Dar es Salaam.
Zoezi hilo la ugawaji wa misaada hiyo kwa yatima hao utafanyika mara baada ya timu ya veterani kutoka kukipiga na timu ya Kijitinyama Veterani katika pambano la kurafiki litakalofanyika kwenye uwanja wa Kijitinyama.
Kwa mujibu wa taarifa ya Mlezi na Msemaji wa timu ya Golden Bush, Onesmo Waziri 'Ticotico' klabu yao imeamua kufanya jambo hili wakati wa kuelekea kwenye sherehe ya sikukuu ya Eid el Fitry kama njia ya kuwakumbuka na kuwafariji yatima ikiwa ni jukumu la kila mwana jamii.
Taarifa rasmi ya klabu hiyo kupitia Ticotico, inasomeka vizuri hapo chini isome mwenyewe;
Kwa niaba ya uongozi wa Golden Bush FC pamoja na wadau wote ambao tumekuwa nao katika timu yetu, tunaomba wapenzi wetu waungane na timu yetu siku jumapili ambapo Golden bush FC tutakuwa na shughuli nzito ya kutoa zawadi kwa baadhi ya wahitaji katika mojawapo ya vituo vya watoto yatima. Shughuli hiyo itarabiwa na baadhi ya viongozi wakishirikiana na wachezaji wetu ambapo kuanzia saa nne na nusu asubuhi siku ya jumapili ya tarehe 04/08/2013 kundi la wachezaji wote wataelekea maeneo ya Kigogo tayari kutoa zawadi kadhaa kwa kikundi cha New Orphans family.

Tumelazimika kufanya shughuli hii ya kijamii kwasababu timu yetu imejijengea jina kubwa kutokana na mafanikio makubwa katika soka yaani timu yetu ya vijana ambayo mpaka sasa ndiyo inayoongoza ligi daraja la nne Wilaya Kinondoni na timu yetu ya veterans inayoundwa na wachezaji mahili sana na waliocheza mpira wa miguu hadi kiwango cha timu ya taifa. Hivyo unaweza kuona kwamba pamoja na kutoa burudani ya uwanjani Golden bush FC tunalazimika kuungana na kundi hili maalum kuburudika kwa pamoja katika sherehe ya Eid.

Tumesukumwa na ubinadamu na wajibu wetu katika jamii, hivyo kwa pamoja tumechangishana na kupata kiasi flani kitakacho tuwezesha kununua walau zawadi kadhaa zitakazo saidia jamii hii ya wahitaji nao kusherehekea sikukuu kubwa ya Eid.

Nawatakieni kila la kheri katika mfungo huu wa Ramadhani.

Asanteni
Onesmo Waziri 'Ticotico' 
Msemaji wa Timu

Mtanzania kusimamia mechi ya CHAN

Na Boniface Wambura
SHIRIKISHO  la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limemteua Alfred Rwiza wa Tanzania kuwa kamishna wa mechi ya raundi ya pili ya michuano ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN).

Rwiza atakuwa kamishna katika mechi ya kwanza ya raundi hiyo itakayohusisha mshindi wa mechi kati ya Msumbiji na Namibia dhidi ya Angola itakayochezwa kati ya Agosti 9 na 11 mwaka huu. Mechi hiyo itachezeshwa na refa Noram Matemera kutoka Zimbabwe.

Matemera atasaidiwa na Wazimbabwe wenzake Tapfumaney Mutengwa atakayekuwa mwamuzi msaidizi namba moja, Ncube Salani ambaye ni mwamuzi msaidizi namba mbili wakati mwamuzi wa mezani (fourth official) ni Ruzive Ruzive.

TFF yatoa shushu ya usajili wa wachezaji

Na Boniface Wambura
SHIRIKISHO la Soka Tanzania, TFF imesogeza mbele tarehe ya mwisho ya usajili wa wachezaji nchini kwa msimu mpya kwa siku mbili zaidi tofauti na ivyokuwa imepangwa awali.

TFF ilitangaza awali kwamba mwisho wa usajili huo wa wachezaji ungekuwa Agosti 3 yaani kesho badala yake umetangaza kwamba utafungwa rasmi Jumatatu (Agosti 5). 

Uamuzi wa kusogeza mbele umetokana kuchelewa kupata disc ya usajili msimu huu ambayo ndiyo inayotumika kwa usajili wa elektroniki unaofanywa kwa wachezaji wa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom. Disc hiyo ambayo hutolewa na kampuni ya NAS Technology ya Tunisia tayari imeshawasili.

Kutokana na mabadiliko hayo, sasa kipindi cha pingamizi kitakuwa kati ya Agosti 6 na 12 mwaka huu wakati Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji itakutana Agosti 13 na 14 mwaka huu kupitia na kufanyia uamuzi usajili wa wachezaji wenye matatizo.

Hatua ya pili ya usajili itaanza tena Agosti 15 mwaka huu ikihusisha wachezaji ambao watakuwa hawajasajiliwa katika Ligi Kuu ya Vodacom msimu huu. Timu zitakazoruhusiwa kusajili ni zile ambazo zitakuwa hazijajaza nafasi zote za usajili. Dirisha dogo za usajili litafunguliwa kuanzia Novemba 15 mwaka huu hadi Desemba 15 mwaka huu.

Pia klabu za Ligi Kuu ya Vodacom zinapowasilisha usajili wao zinatakiwa kuambatanisha nyaraka zinazoonesha viwanja vyao vya mazoezi, nakala za bima kwa wachezaji pamoja na benchi la ufundi. Masuala hayo yameelezwa kwenye Kanuni za Ligi Kuu ya Vodacom

Sikinde kula Idd Dar, Bitchuka anatabasamu tamu

Hassani Bitchuka akiimba kando ya Adolph Mbinga

Baadjhi ya waimbaji wa Sikinde, Hassani Kunyata, Abdallah Hemba na Hassani Bitchuka
BENDI kongwe wa muziki wa dansi nchini, Mlimani Park 'Sikinde' imekamilisha mipango ya kuingia studio kurekodi nyimbo tano zilizosalia, huku ikitangaza ratiba yao ya sikukuu ya Eid el Fitri ambapo imesema Idd zote tatu watakuzila wakiwa jijini Dar es Salaam.
Aidha mwanamuziki wao mkongwe, Hassani rehani Bitchuka ameibuka na wimbo mpya uitwao 'Tabasamu Tamu' ambao unatarajiwa kutambulishwa rasmi katika maonyesho hayo ya sikukuu ya Idd.
Katibu wa bendi hiyo, Hamis Milambo aliiambia MICHARAZO kuwa wapo katika hatua ya mwisho kabla ya kuingia studio za Sound Crafters ili kurekodi nyimbo hizo kati ya sita za albamu mpya iitwayo 'Jinamizi la Talaka'.
Milambo alisema baadhi ya nyimbo hizo zilianza kupigwa kwenye maonyesho ya bendi hiyo kabla haijaingia mapumzikoni kupisha mfungo wa Ramadhani unaoelekea ukingoni.
"Tunafanya mipango ya kuingia studio hivi karibuni ili wakati wa Idd  albamu iwe imekamilika na ni nyimbo tano kati ya sita ndizo zitakazorekodiwa kwa vile 'Jinamizi la Talaka' yenyewe ilisharekodiwa na inaendelea kutamba hewani," alisema Milambo.
Alizitaja nyimbo hizo kuwa ni 'Nundu ya Ng'ombe' uliotungwa na mcharaza gitaa la solo wao, Ramadhani Mapesa 'Dolar Dolar', 'Za Mkwezi' wa Abdallah Hemba, 'Deni Nitalipa' na 'Kukatika kwa Dole Gumba' za nyota wao Hassain Rehani Bitchuka 'Stereo' na 'Kibogoyo' uliotungwa kwa ushirikiano wa wanamuziki wote wa Sikinde.
Juu ya ratiba yao ya sikukuu ya Eid, Milambo alisema safari hii wameamua kula sikukuu hiyo na mashabiki wao wa jijini Dar es Salaam.
Alisema Idd Mosi watakamua kwenye ukumbi wa TCC Chang'ombe kabla ya Idd Pili kufanya maonyesho yao katika ukumbi wa Pentagone Pub uliopo Mivinjeni Kurasini na kumalizia burudani yao itakayoenda sambamba na utambulisho wa wimbo wa Tabasamu Tamu uliotungwa na Bitchuka Magereza Ukonga.

Real Madrid yakaribia kuvunja rekodi ya Uhamisho wa Ronaldo kwa Bale



Cristiano Ronaldo
http://www.standard.co.uk/incoming/article8512730.ece/ALTERNATES/w620/Gareth-Bale-shoots.jpg
Gareth Bale, anayetajwa kuwa bado kidogo tu atue Real Madrid

Madrid, Hispania


KLABU ya Real Madrid inaamini kwamba, sasa ipo hatua za mwisho za kukamilisha uhamisho wa winga wa Tottenham, Gareth Bale baada ya kuanza kujiandaa kutoa pauni milioni 87 ambazo ni sawa na shilingi bilioni 209.3 za Tanzania.



Baada ya wiki nzima Spurs kusisitiza kwamba, Bale hauzwi, sasa Klabu hiyo ya White Hart Lane imenywea na tayari Real inajipanga kutoa dau hilo ambalo litaweka rekodi ya dunia kwa uhamisho wa wachezaji.



Sportsmail limeeleza kuwa linatambua wazi kuwa kikanuni, tayari Spurs imekubali dau hilo, lakini litamthibitisha mchezaji huyo kwa Real Madrid pale tu litakapopata mrithi wake.



Katika kujipanga upya, tayari Spurs inatarajia kukamilisha usajili wa Mshambuliaji wa Valencia, Roberto Soldado kwa dau la pauni milioni 26 (sh. bilioni 62.5 za Tanzania) ambapo pia Kocha Andre Villas-Boas anataka kumng'oa Alvaro Morata katika Uwanja wa Bernabeu ikiwa ni sehemu ya kumwachia Bale.



Morata, 20, anayecheza safu ya ushambuliaji, huku akiwa ameshakifungia mara mbili Kikosi cha Wakubwa cha Real, anatajwa kuwa mmoja wa wachezaji bora kwa siku zijazo.



Spurs inataka kuisisitiza Real Madrid kuwa Morata awe sehemu ya makubaliano ya wao kumwachia Bale.



Morata alikuwa kinara wa ufungaji kwenye michuano ya Ulaya ya wachezaji wenye umri chini ya miaka 21 (Euro U-21), ambayo ilifanyika Israel mwaka huu, baada ya kufunga jumla ya mabao manne na kuiwezesha Hispania kutwaa kombe.



Endapo Spurs itaridhia kumuuza Bale kwa pauni milioni 87, atakuwa amevunja rekodi ya dunia iliyowekwa na Cristiano Ronaldo, aliyetua Real Madrid kwa pauni milioni 80 akitokea Manchester United 2009.



Nyota anayefuata kwa kuuzwa ghali ni Zlatan Ibrahimovic, aliyetua Barcelona 2009, akitokea Inter Milan kwa pauni milioni 56.5. Kaka anafuata kwa pauni milioni 56 kutoka AC Milan kwenda Real Madrid (2009).


Edinson Cavani anashika nafasi ya nne kwa pauni milioni 55, akitokea Napoli kwenda PSG (2013), akifuatiwa na Radamel Falcao, pauni milioni 53, kutoka Atletico Madrid kwenda Monaco (2013).

Mieno, Umony waachwa msafara wa Azam Afrika Kusini

Mieno (kushoto) akiwa na Seif Abdallah Karihe. Mieno hatakuwepo kwenye msafara wa Azam kesho kwa vile ni majeruhi
Brian Umony ambaye hatakuwepo kwenye msafara wa Azam kesho

WACHEZAJI wa kimataifa kutoka Kenya,  Humphrey Mieno na Mganda Brian Omony wameondolewa kwenye msafara wa klabu ya Azam unaotarajiwa kuondoka kesho asubuhi kuelekea Afrika Kusini kwa ajili ya kambi ya mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya wa Ligi.
Meneja wa Azam, ambaye ndiye mkuu wa msafara wa timu  katika ziara hiyo Jemedari Said alisema Omony na Mieno wameachwa kwa sababu ya kuwa majeruhi na kwamba wachezaji 22 tu ndiyo watakaokuwa katika msafara wao utakaokuwa wa watu 33.
"Msafara wetu wa watu 33 utaondoka kesho saa 5:45 ukiwa na wachezaji 22 kati ya 24 waliosajiliwa msimu huu, Mkenya Humphrey Mieno na Mganda Brian Omony tunawaacha kwa vile ni majeruhi na wanaendelea na matitabu yao wakati wenzao wakienda kujifua," alisema.
Said alisema wengine watakaokuwa katika msafara huo ni benchi la ufundi lenye watu nane na waandishi wa habari watatu na kwamba wakiwa huku watacheza jumla ya mechi nne na timu za Ligi Kuu ya Afrika Kusini  kuanzia Jumatatu.
Azam ambayo itaitumia michezo hiyo minne pia kujiandaa na pambano lao la Ngao ya Hisani dhidi ya Yanga Agosti 17, itaanza kuvaana na Kaizer Chiefs Agosti 5 kabla ya kushuka tena dimbani Agosti 7  kuvaana na Mamelodi Sundowns.
Mchi nyingine itakayocheza timu hiyo itakayoiwakilisha Tanzania kwa mara ya pili kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika ni ile ya Agosti 9 itakapovaana na Orlando Pirates na kumalizia kambi yao ya muda nchini humo kwa kupepetana na Moroka Swallows Agosti 12.
Said, nyota wa zamani wa aliyewahi kutamba timu kadhaa ikiwamo Majimaji-Songea, alisema anaamini kambi hiyo itaisaidia timu yao kwa ajili ya maandalizi yao ya Ligi Kuu Tanzania Bara na pambano lao dhidi ya Yanga litakalochezwa kwenye uwanja wa Taifa.
Alisema mara watakaporejea nchini wataingia kambini moja kwa moja kwa ajili ya pambano hilo la Ngao ya Hisani na mechi yao ya fungua dimba ya Ligi Kuu kati yao na Mtibwa Sugar ambayo itachezwa Manungu Complex, nyumbani kwa wapinzani wao.

Mwanamuziki Pouline Zongo avunja ukimya


BAADA ya ukimya wa muda mrefu, mwimbaji nyota wa muziki wa kizazi kipya na  dansi, Pauline Zongo ameibuka upya na kibao kipya kinachokwenda kwa jina la Misukosuko ya mapenzi.

Pauline amerekodi kibao hicho na kundi jipya la muziki linalojulikana kwa jina la Ndege Watatu, linaloundwa na wanamuziki wengine wawili wa kike, Khadija Mnoga na Joan Matovolwa.

Akizungumza mjini Dar es Salaam wiki hii, Pauline alisema tayari kibao hicho kimeshaanza kurushwa kwenye vituo mbalimbali vya redio nchini na kupokewa vizuri na mashabiki.

Mwanadada huyo, aliyekuwa mmoja wa wasanii wanaounda kundi la East Coast amesema, wameamua kuunda kundi hilo kwa lengo la kuleta changamoto mpya katika muziki.

Pauline alisema aliamua kuwa kimya kwa muda mrefu kwa sababu ya kulea mtoto wake wa pili mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu. Mtoto wake wa kwanza ana umri wa miaka sita.

Alisema ukimya wake huo pia ulilenga kusoma mwelekeo wa muziki na pia kujipanga upya kabla ya kurudi ulingoni akiwa na vitu tofauti.

Mwanamama huyo, ambaye ni mwajiriwa wa bendi ya TOT Plus alisema, wameamua kuliita kundi lao kwa jina la Ndege Watatu kwa sababu sauti zao zinafanana na wanakijua wanachokifanya.

Pauline alisema uamuzi wake wa kujiunga na TOT Plus ulilenga kukuza kipaji chake cha muziki na pia kuwaonyesha mashabiki kwamba ana uwezo mkubwa katika fani hiyo.

"Kusema kweli, huwezi kuwa mwanamuziki kama hujui kupiga ala yoyote ya muziki,"alisema mwanamama huyo, ambaye ana uwezo wa kupiga gita, drums na kinanda.

Licha ya kundi lake la TOT kumruhusu kuwa mwanamuziki huru, Pauline alisema hawezi kutoa albamu kila mwaka kwa vile akifanya hivyo, hawezi kupata manufaa makubwa.

Alisema mwanamuziki anatakiwa kusonga mbele akiwa na mabadiliko badala ya kufanya kitu kile kile kila mwaka.

Mwanamama huyo alisema hakujifunza muziki kutoka kwa mtu yoyote. Anasema kuna siku alilala akaota ndoto anapiga gita, drums, kinanda na kuimba na alipozinduka usingizini, akaamua kutimiza ndoto yake hiyo.

Pauline anakiri kuwa, asili yake ni Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Anasema mama ni Mcongo na baba yake ni Mtanzania.

"Mimi nilizaliwa Congo. Wakati huo baba alikuwa akija Congo kibiashara ndipo akakutana na mama na kwetu tupo watoto wengi tu. Baadaye ikatokea kutokuelewana kati ya baba na mama, hivyo mimi na mdogo zangu tukaja Tanzania na baba na ndugu zangu wengine walibaki na mama Congo,"alisema.

Pauline anasema pia kuwa ni kweli kwamba anaye pacha wake wa kiume anayeitwa Paul Zongo, ambaye kwa sasa ni prodyuza wa muziki nchini Afrika Kusini. Alisema Paul ameshiriki kutengeneza nyimbo za kundi la Malaika la Afrika Kusini na wanamuziki wengine wa nchi hiyo.

Alipoulizwa iwapo ni kweli amezaa mtoto wake wa pili na mwigizaji filamu nyota wa Bongo, anayejulikana kwa jina la Mtunisi, alikiri kwamba ni kweli.

"Ndio ni kweli, lakini kwa sasa tumeshaachana, kila mtu ana maisha yake. Nina mchumba wangu, ambaye Mungu akitujalia, mwishoni mwa mwaka huu tutafunga pingu za maisha. Tumeshakaa kwenye uchumba kwa miaka miwili sasa.Mchumba wangu naye ni pacha kama mimi, tunapendana sana,"alisema.

Je, ni kitu kipi ambacho Pauline anakijutia katika maisha yake?

"Kiukweli sitaki kuficha, uhusiano nilioingia na baba mtoto wangu naujutia sana. Laiti ningesikiliza ushauri wa watu wengi, yasingenikuta yaliyonikuta,"alisema.

"Nilikuwa sisikilizi yote niliyokuwa naambiwa juu ya tabia za mwanaume huyo, lakini baada ya kuyaona, niliishia kujuta maana mapenzi yake yalinipotezea hata mwelekeo wa maisha yangu. Lakini kwa sasa nina nguvu mpya na nipo huru, nimejifunza siku nyingine sitafanya makosa,"alisisitiza.

Pauline alianzia muziki akiwa na kundi la East Coast lililokuwa na wasanii mahiri kama vile Crazy GK, Khamis Mwinjuma 'Mwana FA' na Ambwene Yesaya 'AY' kabla ya kuhamia TOT.

Akiwa East Coast, alijipatia umaarufu mkubwa aliposhiriki kuimba kibao cha Sister Sister akishirikiana na Crazy GK wakati akiwa TOT, aling'ara kupitia kibao cha Mnyonge Mnyongeni, alichokiimba kwa kushirikiana na Badi Bakule na Abdul Misambano.

East African Melody kula Idd Travertine

Baadhi ya waimbaji wa kundi hilo la EA Melody
BENDI Kongwe ya muziki wa Taarabu Nchini East African Melody imetangaza kutoa burudani wakati wa shamra shamra za sikukuu ya iddi  pili  katika  ukumbi wa Traventine Hotel akizungumzia onesho hilo  mwandaaji wa onesho hilo Habbas Husseni 'Chezntembaa'
Amesema ameamua kuchukua bendi hiyo itoe burudani ili ikonge nyoyo za mashabiki mbalimbali wa taarabu ambapo walikosa raha hizo wakati wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani
Katika Shamra shamra hizo za sikukuu ya iddi  watakuwa wakitambulisha nyimbo zao tatu mpya  ambazo ni Rabb nilinde ulioimwa na Mwanahawa Ally, Ukewenza sio dili,ulioimbwa na Mwanaidi Shabani na Stara ulioibwa na Sabaha Muchacho,
Ambapo siku hiyo wageni waalikwa ni Pr. Muhamed Elyas, Bi Shakirla ,Muhamed Issa Matona na wengine ambapo kiingilio 5000, ndani ya ukumbi wa Traventine Hotel iliyopo magomeni jijini Dar es salaam
Bendi hiyo imeakikisha kukonga nyoyo za mashabiki wao jukwaani kwa kuwa watakuwa wa kwanza kusikiliza nyimbo zao mpya wakiwa live jukwaani

Stephano Mwasyika atua Ruvu Shooting

http://in2eastafrica.net/wp-content/uploads/2012/03/Stephano-Mwasika.jpg
Stephano Mwasyika
 WAKATI dirisha la usajili likitarajiwa kufungwa rasmi leo, klabu ya soka ya Ruvu Shooting imekamilisha usajili wake kwa kuwanyakua nyota wa zamani wa Yanga na African Lyon na kukamilisha idadi ya wachezaji saba wapya iliyowanyakua kwa msimu ujao.
Afisa Habari wa timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara, Masau Bwire aliwataja wachezaji waliokamilisha usajili wao ni beki wa kushoto, Stephano Mwasyika aliyekuwa Yanga na kipa Abdul Juma Seif aliyekuwa akiidakia Lyon kabla ya kushuka daraja msimu uliopita.
Bwire alisema wachezaji hao wanaoungana na Juma Seif 'Kijiko' (Yanga), Cosmas Ader (Azam), Elias Maguli (Prisons-Mbeya), Juma Nade (Kagera Sugar) na Jerome Lembeli (Ashanti United) ambao walisajiliwa awali dirisha la usajili lilipofunguliwa mara baada ya kumalizika kwa ligi.
Wachezaji hao saba wapya wanachukua nafasi ya wachezaji watano waliotemwa katika kikosi hicho ambao ni Paul Ndauka,  Charles Nobert, Gido Chawala, Frank Mabande na Liberatus  Manyasi.
Bwire alisema wachezaji wote wa timu yao kwa sas wapo kambini pamoja na makocha wao kwa ajili ya kujiandaa na pambano lao la ufunguzi wa Ligi Kuu inayoanza Agosti 24 dhidi ya timu ya Prisons Mbeya.
Aliongeza kuwa katika kujiweka sawa kesho jioni kikosi chao kinatarajiwa kushuka dimba la Mabatini, Mlandizi Pwani kuvaana na Mabingwa wa soka mkoani humo, Kiluvya United katika pambano la kirafiki.
Bwire alisema mchezo huo ni muendelezo wa programu za benchi lao la ufundi chini ya kocha Charles Boniface kupima vijana wao kabla ya kuanza kwa ligi hiyo msimu wa 2013-2014.

Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu agawa misaada kwa yatima TMK

 Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu akiwakabidhi msaada wa vyakula watoto yatima wanaolelewa katika Kituo cha Dar Alqaama Tandika katika sherehe ya kutoa misaa kwa vikundi mbalimbali vya yatima, Dar es Salaam hivi karibuni.
                                        Akiwakabidhi watoto wa Kituo cha Hiyari Chang'ombe
                                              Upendo Maganga wakipata msaada huo
                                                                  Upendo Bokolani wakipata msaada huo
                                        Kituo cha WAVIBA KILAKALA wakipokea msaada
                                               Kituo cha Faraja kikipokea msaada huo
 Mwenye ulemavu wa viungo, Zamda akipokea msaada wa vyakula kutoka kwa Mtemvu
                                                  Aisha Shabani akipokea msaada huo
                                        Mwasiti Mtebwa akipata msaada
 Mama Mwandoro akipata msaada
                                                           Ashura Sadiki


Thursday, August 1, 2013

Picha za utupu zanaswa ukumbi wa Kanisa Dar



Kiongozi wa Kanisa la Greek Orthodox duniani, Papa Theodor’s II ameamuru kufungwa kwa ukumbi uliopo ndani ya eneo la kanisa hilo lililopo Kiwanja Namba 7509 katika Barabara ya Ali Hassan Mwinyi jijini Dar es Salaam kufuatia kuwepo kwa picha za utupu za wanawake ukutani..


Papa huyo alifikia uamuzi huo Februari 19, mwaka huu baada ya kutua nchini ambapo alifanya mazungumzo na Rais Jakaya Kikwete.
 Mbali na mazungumzo na JK, alipata nafasi ya kutembelea ukumbi huo ulio kwenye eneo la kanisa hilo ndipo ‘alikutana’ na picha za wanawake wa Kiafrika na Kizungu zikiwa zimetundikwa ukutani wakiwa kama walivyozaliwa.


Mbali na picha hizo za utupu, pia kulikuwa na picha ya mwanamitindo maarufu Bongo, Mariam Julius Odemba. Picha yake ilimwonesha akiwa amevaa nguo ya heshima na maandishi juu ya picha yakiwa yameandikwa; ‘Thanks British Legion for all your support. Miriam Odemba, 1st Oct 1999’.  

Imeelezwa kuwa baada ya kutua nchini, papa huyo alilala katika nyumba iliyo karibu na kanisa na klabu hiyo na usiku wakati akisali alishangaa kuwaona wanaume, tena wenye mwonekano mzuri wakiingia katika eneo hilo la kanisa akasitisha sala.

Kilichomshangaza zaidi ni kuwaona wanaume hao wakiwa na wasichana wabichi na baada ya kufika klabuni walikuwa wakipiga kelele huku muziki ukisikika kwa sauti ya juu.

 
 Kufuatia hali hiyo, aligundua kwamba watu hao walikuwa wakinywa pombe hadi usiku wa manane jambo ambalo ni kinyume na maadili ya imani hiyo.


“Kesho yake Papa Theodor’s aliamua kutembelea ndani ya klabu hiyo ndipo aliposhuhudia picha hizo chafu nyingi zikiwa zimetundikwa ukutani na chupa tupu za vinywaji vikali.

“Kuona hivyo papa alimuagiza kiongozi wa Bodi ya Wadhamini wa Kanisa, Dimitri Kimon akutane na mapadri wote mwezi wa nne (uliopita) na kujadili hilo nia ikiwa ni kurejesha usafi na kuondoa uchafu huo kanisani hapo.

“Katika mkutano huo waliamua kufunga na kuomba kisha kumtafuta wakili ili aweze kuwatoa waliokuwa wakiendesha ukumbi huo,” kilisema chanzo.

Chanzo kiliongeza kuwa, Julai 8, mwaka huu viongozi hao waliamua kufunga geti la kanisa hilo na kuimarisha ulinzi kwa kutumia kampuni ya ulinzi ili kuzuia wanachama wa klabu hiyo kuingia eneo hilo isipokuwa waumini.
 Kiongozi wa kanisa  hilo.

 Habari zinasema viongozi wa kanisa hilo waliwaambia waliokuwa wakiendesha ukumbi huo kwamba kiongozi wao mkuu hakupendezwa na picha chafu za ukutani na alihoji endapo dini nyingine zikigundua uchafu huo wataelewekaje kwa jamii?

Kuna madai kwamba wengi waliokuwa wakiingia kwenye ukumbi huo ni vigogo katika ngazi ya mawaziri na wabunge ambapo waandishi wetu walibahatika kuona jina la mbunge mmoja likiwa limeorodheshwa katika kitabu cha waliokuwa wakiingia.

Mwanachama mmoja wa klabu hiyo ambaye hakutaka jina lake kuandikwa  kwa madai kuwa si msemaji, alisema wanakusudia kufungua kesi mahakamani ili kupinga adhabu ya kufungwa ukumbi huo kwa kuwa wapo eneo hilo kwa muda mrefu.

“Sisi tupo katika eneo hili na tumefanya shughuli zetu siku zote hizo, tunashangaa leo kuona kanisa linatufungia geti. Ni lazima tutachukua hatua za kisheria,” alisema mwanachama huyo.

Mwandishi wetu alimpata wakili wa kanisa hilo ambaye pia ni Katibu Myeka, Edward Chuwa alipoulizwa kuhusu mgogoro huo alikiri kuwepo.

“Ni kweli kuna huo mgogoro kati ya kanisa na waendesha klabu hiyo lakini kwa kuwa mimi ni wakili naomba nisiseme chochote kwa sababu za kimaadili,” alisema Chuwa.

Naye wakili wa waendesha klabu hiyo, Evodi Mmanda alipopigiwa simu na kuulizwa kuhusu mgogoro huo naye alikiri kuwepo.

“Mgogoro huo naujua lakini kwa kuwa mimi ni wakili wao siwezi kusema chochote kutokana na maadili ya kazi yangu.” alisema Mmanda bila kusema ni lini kesi hiyo itasikilizwa. 

Credit : Uwazi  via  GPL

Azam kutimkia Bondeni kucheza mechi nne ratiiba kamili hii hapa!

Azam FC  inasafiri jumamosi hii kuelekea afrika ya kusini kwa maandalizi ya ligi kuu na itacheza michezo minne kama ifuatavyo
Tarehe 5 August, Azam Fc vs Kaizer Chiefs, 
Tarehe 7 August Azam Fc vs Mamelodi Sundows, 
Tarehe 9 August Azam Fc vs Orlando Pirates,
Tarehe 12 August Azam Fc vs Moroka Swalows
Kikosi cha Azam
KLABU ya soka ya Azam Fc, inatarajiwa kuondoka nchini keshokutwa kwenda Afriki Kusini kuweka kambi yao kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2013-2014.
Kwa mujibu wa taarifa za klabu hiyo timu hiyo ikiwa nchini humo itacheza mechi nne kabla ya kurejea nchini kuisubiri Yanga katika pambano la Ngao ya Hisani Agosti 17 na kisha kuifuata Mtibwa Manungu katika pambano la fungua dimba la Ligi Kuu.
Ratiba hiyo iliyotolewa na klabu hiyo inaonyesha itashuka dimbani Agosti 5 dhidi ya Kaizer Chiefs kabla ya siku moja baadaye kuwava Mamelodi Sundowns.
Baada ya siku moja yaani Agosti 9 Azam itaumana na Orlando Pirates na kumalizia ziara na kambi yao ya nchini humo kwa kuvaana na Moroka Swallows Agosti 12.

Maajabu ya Dunia! wanandoa waliozaliwa siku moja wafa siku moja wakiwa na miaka 94

WANANDOA katika jijini la California waliozaliwa siku moja na kuoana miaka 75 iliyopita wamefariki siku moja wakiwa na miaka 94.
 Couple Born on Same Day, Married 75 Years, Die One Day Apart

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Long Beach Press Telegram, Helen na Les Brown walifariki Julai 16 na 17 mwaka huu wote wakiwa na umri wa miaka 94.

Zach Henderson, Mmilikii wa Grosari moja ijulikanayo kwa jina la Ma N’Pa iliyopo Long Beach alinukuriwa wakisema kuwa alikuwa akiwaona wapendanao hao kila siku iitwayo kwa Mungu na kuuita uhusiano wao kuwa “ a Wonderful Blessing”.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Press –Telegram imesema kuwa wote walizaliwa siku moja yaani Desemba 31, 1918 na pia walianza kuwa pamoja mwaka 1937 katika masomo ya sekondari.

Imejulikana kwamba wanandoa hao walikuwa waamini wa Mashahidi wa Yehova (Jehova Witnesses) waliobarikiwa kuwa na mtoto wao Les Brown Jr.

Henderson anasema imani yao kwa Mwenyezi Mungu ndio iliyozidi kuimarisha ndoa yao hadi kufikia hapo.

Mtoto wao Les Brown Jr alinukuriwa akisema “Walikuwa pamoja kila siku kwa miaka 75, hakika upendo wao ulirandana” 

Post Telegram limeripoti kuwa Les Brown alikuwa akiumwa ugonjwa wa Parkison’s na mkewe Helen Brown alikuwa akisumbuliwa Kansa ya tumbo hadi mauti yao yalipowakuta

"She was completely cognitive," Henderson said, describing how he found Helen Brown a few days before she died. "It seems like she was waiting for Les to be comfortable and they were going to move on to something else with each other."

Ibada ya pamoja itafanyika siku ya Jumamosi mchana kwa ajili ya kuwakumbuka wanandoa hao huko Long Beach, California.

CHANZO: JAIZMELALEO/ABC NEWS/YAHOO NEWS