STRIKA

USILIKOSE

Sunday, August 24, 2014
Neymar majanga Barcelona, La Liga yaanza kwa kishindo

Nyota huyo wa kimataifa wa Brazil, ndio kwanza alikuwa ameruhusiwa kucheza na madaktari wa timu hiyo baada ya kupona majeruhi ya mgongo aliyopata katika Kombe la Dunia lakini sasa anakabiliwa na majeruhi mengine.
Katika taarifa iliyotumwa katika mtandao wa klabu hiyo, imedai kuwa Neymar alikuwa akilalamika maumivu katika kifundo chake cha mguu wa kushoto na baada ya vipimo imegundulika kuwa ana matatizo ambayo yatachukua muda kidogo kupona.
Taarifa hiyo imeendelea kudai kuwa kurejea mazoezini kwa mchezaji huyo kutategemea kumalizika kwa maumivu hayo hivyo ni wazi hatakuwepo katika mchezo wa leo.
Neymar alicheza mechi 26 za La Liga msimu uliopita na kufunga mabao saba lakini msimu huu unaonekana tayari ameuanza vibaya kwa maumivu.
Kipute cha ligi hiyo ya Hispania kilianza usiku wa jana kwa kushuhudiwa Malaga wakitamba nyumbani kwa kuitandika Athletico Club bao 1-0, Sevilla ikilazimishwa sare ya 1-1 nyumbani na Valencia, huku Granada ikivuna ushindi nyumbani dhidi ya Deportivo la Coruna kwa kuilaza mabao 2-1 na Almeria na Espanyol wakitishana nguvu kwa kufungana bao 1-1.
Meya Silaa awatoa hofu wakazi wa Ilala

NA SULEIMAN MSUYA
WAKATI kukiwa na hali ya sintofahamu juu ya ubomoji wa mzumnguko wa uliopo katika makutano ya barabara ya Uhuru na Msimbazi Kariakoo Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam Meya wa Manispaa hiyo Jerry Slaa amesema ubomoaji huo unalenga kupisha ujenzi wa barabara ya mabasi yaendayo kasi.
Meya huyo alibainisha hilo wakati akizungumza na mwandishi wa habari hii jijini Dar es Salaam.
Alisema Mradi wa mabasi yaendao kasi unahusu barabara ya Morogoro, Kawawa na Msimbazi hivyo Manispaa inapaswa kuondoa ili kupisha ujenzi huo.
“Unajua Serikali ipo katika mkakati wa kuboresha miundombinu hivyo eneo lile la mzunguko wa Msimbazi linahusika hivyo tunapswa kuuondoa ili ujenzi uendelee”, alisema.
Slaa alisema pamoja na kuondoa mzunguko huo Manispaa inaendelea kutafuta eneo ambalo watauhamishia ili kuendelea kuonekana katika Manispaa hiyo na jiji kwa ujumla.
Meya huyo Manispaa ya Ilala aliwataka wananchi wa Ilala na maeneo mengine ya Dar es Salaam wasiwe na hofu juu ya kinachoondelea kwani ni katika harakati za kuboresha jiji.
Akizungumzia juu ya changamoto ambazo zinaikabili Manispaa ya Ilala alisema ni suala la kuondoa uchafu katika makazi ya watu ambapo kata 16 kati ya 26 za manispaa hiyo bado hazijapata mzabuni wa kukusanya taka.
Slaa alisema Manispaa ipo katika mkakati wa kuzisaidia Kata zilizobakia magari ya kubeba taka ambapo kwa kuanzia watatoa magari tisa kwa vikundi ambavyo vipo katika kata.
“Changamoto zipo nyingi ila hii ya taka inatuumiza vichwa sasa hivyo tumefikiria ili kuondoa taratibu za wananchi kuweka taka barabarani tumeamua kuvipatia vikundi katika Kata magari ili wafanye kazi hiyo ya kukusanya moja kwa moja wenyewe”, alisema.
Pia alisema manispaa hiyo inakabiliwa na changamoto ya bajeti inayotosha, watumishi wachache ambapo pia walio wengi wanaelimu ndogo ambayo haindani na kasi ya mahitaji ya jamii.
Alisema juhudi za manispaa hiyo ni kuhakikisha kuwa jamii inapata huduma zilizo na vigezo na kwa wakati ili wawe ni sehmu ya maendeo ya manspaa yao.
WAZIRI Wassira awafunda wajasiriamali

NA SULEIMAN MSUYA
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Sera na Mipango Stephen Wassira amesema wakati umefika kwa Watanzania kuondokana na mfumo wa kuuza malighafi katika masoko ya ndani na nje ya nchi ili waweze kupata faida kubwa ya mazao wanayozalisha.
Wassira alisema hayo wakati alipohudhuria Mkutano wa Bodi ya Magavana ya Proffensial Trade Association (PTA) uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Alisema kwa miaka mingi wakulima wa Tanzania wamekuwa wakiuza malighafi badala ya bidhaa iliyokamilika kutokana na malighafi hiyo halia ambayo inachangia wanyonywe na wanunuzi.
Waziri huyo wa Nchi Ofisi ya Rais Sera na Mipango alisema ili kuhakikisha kuwa wakulima wanapata mabadiliko kutokana na kilimo Serikali inaendelea kufanya juhudi za kuhakikisha kuwa viwanda vinakuwepo katika maeneo ya wakulima walipo.
“Kilimo ni moja ya sekta nzuri sana ila huwezi kuona manufaa yake iwapo wewe kila siku unauza malighafi kwa wenzako waliondelea jambo ambalo wanahakikisha kuwa linakwisha”’ alisema.
Wassira alisema Serikali inaendelea kutafuta wawekezaji ambao watakuja kuwekeza na kuwa kichochoe cha kukuza uchumi wa wakulima na jamii kwa ujumla.
Aidha alizungumzia mafanikio yaliyopatikana kupitia Benki ya PTA kwa Tanzania ambapo alisema kuwa imetoa msaada wa uboreshaji wa bandari ya Dar es Salaam, Uwanja wa ndege wa Mwalimu Julias Nyerere.
Waziri Wassira alisema serikali itaendelea kushirikiana na benki hiyo ya maendeleo ya PTA ili kuhakikisha kuwa inaendeleza sekta mbalimbali hasa kupitia mpango wa pili wa maendeleo ambao unatarajiwa kuaanza hivi karibuni.
Kwa upande wake Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda alisema juhudi zao ni kuhakikisha kuwa PTA inakuwa na ofisi zake hapa nchini ili kuhakikisha kuwa wanashiriki moja kwa moja kusaidia kutatua changamoto zilizopo hapa nchini.
Alitoa wito kwa PTA kusaidia Tanzania katika sekta ya miundombinu, kilimo, ujasiriamali na umeme akiamini kuwa maeneo hayo yakipata ufumbuzi ni wazi kuwa uchumi wanchi utakuwa kwa kasi.
Pinda alisema PTA ni moja ya mabenki ambayo hayana riba kubwa kwa mikopo yake inayotoa hivyo Tanzania itaendelea kushirikiana nayo ili kusaidia kutatua changamoto zinazoikabili jamii yake.
Waziri Mkuu alisema ni vyema wawekezaji wa ndani kutumia benki hiyo katika kuomba mikopo ambayo ina riba ndogo ili waweze kuwekeza ndani ya nchi yao.
Alisema kupitia benki hiyo ni wazi wajariamali wadogo na wakati watafaidika jambo ambalo litachochea ukuaji wa uchumi wa mtu mmoja mmoja na nchi kwa ujumla.
UDA kununua dalada zote Dar...Kivipi?

Na Suleiman Msuya
SHIRIKA la Usafirishaji Mkoa wa Dar es Salaam (UDA) kupitia bodi ya wakurugenzi limesema lipo tayari kuwalipa au kununua hisa za wasafirishaji watakao kuwa wapo tayari wakati wa mradi wa mabasi yaendayo kasi utakapoanza katika barabara ya Morogoro.
Hayo yamebainishwa na Mjumbe wa Kamati Maalumu ya Umoja wa Wamiliki wa mabasi ya usafiri Mkoa wa Dar esSalaam UWAMADA Therese Kitambi wakati akitoa taarifa kwa wajumbe kwenye mkotano uliofanyika kwenye ukumbi wa Kareemjee jijini Dar es Salaam.
Alisema katika mazungumzo ambayo wameyafanya walifikia muafaka kuwa UDA wapo tayari kununua mabasi ya wale wamiliki ambao watakuwa hawapo tayari kuwa na hisa katika kampuni hiyo na kwa wale ambao watakuwa tayari wataruhusiwa kununua hisa.
Kitambi alisema makubaliano hayo ni ya awamu ya kwanza ya mradi wa barabara ya Morogoro na hayahusi awamu zote za mradi huo wa mabasi yaendao kasi ambao utahusu takribani barabara zinazoingia mjini.
“Ndugu zangu wajumbe napenda kuwatarifu kuwa UDA wapo tayari kuungana na sisi kwa Yule ambaye atakuwa tayari ila kama hutaki anaweza kununua gari lako kulingana na thamani yake”, alisema
Alisema ni wazi kila mmoja anatambua kuwa Serikali imekataa kutulipa fidia sisi wamiliki wa magari hivyo basi ni vema watambue kuwa mpaka sasa kampuni hiyo ya UDA ndio imehitaji kushirikiana nao.
Kitambi alisema katika makubaliano hayo mmiliki wa mabasi ambaye amejiunga na UDA hawataruhusiwa kujiunga na kampuni nyingine ya usafiri jijini Dar es Salaam.
Aidha alisema kuhusiana na njia ambazo hazijahusika na mradi wa mabasi yaendao kasi aliasema wana UWAMADA wataendelea kutoa huduma hadi hapo mpango mwingine utakapoanza.
Mjumbe huyo alisema pamoja na makubaliano hayo pia UWAMADA utakuwa na wajumbe wawili ambao watakuwa wakurugenzi katika bodi ya UDA.
Kitambi aliwataka wana UWAMADA waendelee kushikamana ili kuhakikisha kuwa mafanikio yanapatikana na hakuna mtu ambaye ataonewa katika mchakato huo.
Nani kutwaa taji la KAGAME Leo?!
![]() |
APR |
![]() |
El Merreikh |
Taji la michuano hiyo kwa sasa lipo wazi baada ya waliokuwa watetezi, Vital'O ya Burundi kung'oka mapema kwenye michuano hiyo ambayo ilishuhudia wawakilishi wa Tanzania, Azma wakitolewa kwa mikwaju ya penati katika hatua ya Robo Fainali.
Timu hizo mbili zilifuzu hatua hiyo baada ya kushinda mechi zao za Nusu Fainali kwa mikwaju ya penati, APR wakiwatoa maafande na ndugu zao POlisi kwa mikwaju 4-3 baada ya kumaliza dakika 120 bila kufungana wakati Wasudan waliitoa KCCA ya Uganda kwa penalti 3-0 baada ya kumaliza dakika 120 wakitoka sare ya mabao 2-2.
Mechi hii ya leo inatarajia kuwa na upinzani mkubwa kutokana na ubora wa vikosi vya timu zote ambazo zinaundwa na vijana wadogo wenye vipaji, hali ambayo inakubwa ngumu kujua kama ni E;l Mereikha watakaotwaa taji lao la tatu la michuano hiyo au APR.Kabla ya mechi hiyo kutatanguliwa na mechi ya mshindi wa tatu kati ya Polisi na KCCA.
Di Maria njia nyeupe kutua Manchester United

Awali wote wawili walitajwa kwenye Kikosi cha Wachezaji 22 kwa ajili ya Mechi hiyo na Atletico Madrid kwa mujibu wa Jarida la Marca wakimnukuu Kocha wa Real Carlo Ancelotti.

Lakini walipofika huko Valdebebas, Kituo cha Mazoezi cha Real, Di Maria na Khedira walijulishwa kuwa hawamo kwenye Kikosi cha kwenda kwenye Mechi na Atletico na hilo liliwakera sana Wachezaji hao kwa mujibu wa Marca.
Wakati Di Maria akiamua kurudi Nyumbani kwake, Khedira aliamua, bila ya ruhusa ya kusafiri ya Real, kupanda Ndege kwenda kwao Germany, Mji wa Leipzig kumshuhudia Ndugu yake akicheza Mechi.

Hadi sasa haijajulikana wazi Wachezaji hao wanakwenda wapi mbali ya Kocha Ancelotti kutoboa kuwa wote wamekataa Mikataba mipya na Di Maria ameomba kuhama.
Hadi sasa Di Maria anahusishwa sana na kuhamia Manchester United na Leo zimeibuka ripoti kuwa Khedira yeye atakwenda Bayern Munich kuchukua nafasi ya Majeruhi wa muda mrefu Javi Martinez.Jarida la Marca, ambalo lipo karibu mno na Klabu ya Real Madrid, limethibitisha Wachezaji hao wawili watahama rasmi Wiki ijayo.

SITTI MTEMVU NDIYE MISS TEMEKE 2014

Redd's Miss Temeke 2014, Sitti Mtemvu akipunga mkono huku akiwa na
mshindi wa Pili, Salma Saleh (kushoto) na watatu, Neema Mollel, baada ya
kutangazwa kuwa washindi wa shindano hilo.
Warembo walioingia Tano bora wakipozi kusubiri hatua ya kupambana katika kujibu maswali.
Miss Ilala, wakifuatilia shindano la Redd's Miss Temeke, Viwanja vya TCC Club, Chang'ombe, Dar es Salaam
Washiriki wa Redd's Miss Temeke, wakionesha shoo, wakati wa shindano hilo.
Mshindi wa Pili wa Redd's Miss Temeke 2013, Narietha Boniface, akimvisha taji Redd's Miss Temeke 2014, Sitti Mtemvu baada ya kuibuka mshindi katika shindano hilo, TCC Chang'ombe
Warembo walioingia Tano bora wakipozi kusubiri hatua ya kupambana katika kujibu maswali.
Miss Ilala, wakifuatilia shindano la Redd's Miss Temeke, Viwanja vya TCC Club, Chang'ombe, Dar es Salaam
Washiriki wa Redd's Miss Temeke, wakionesha shoo, wakati wa shindano hilo.
Mshindi wa Pili wa Redd's Miss Temeke 2013, Narietha Boniface, akimvisha taji Redd's Miss Temeke 2014, Sitti Mtemvu baada ya kuibuka mshindi katika shindano hilo, TCC Chang'ombe
Arsenal chupuchupu ugenini, Chelsea, Swansea zazidi kupeta
![]() |
Diego Costa kazini |
![]() |
Arsenal wakishangilia mabao yao ya kusawazisha nyumbani kwa Everton |
Bao la dakika ya mwisho la Olivier Giroud liliiokoa Arsenal kulala ugenini kwa Everton na kutoka sare ya 2-2.
Vijana wa Arsene Wenger walitanguliwa kufungwa bao dakika ya 19 kupitia kwa Seamus Coleman kabla ya Steven Naismith kuwaongezea wenyeji bao la pili dakika ya 45 lililoonekana dhahiri ni la kuotea.
Hata hivyoi katika kipindi cha pili baadaya mabadiliko kadhaa yaliisaidia Arsenal kurejea na nguvu mpya na kurejea bao moja baada ya jingine dakika 10 za mwisho.
Baoa la kwanza la Ze Gunners lilifunmgwa na Aaron Ramsey katika dakika ya 83 kabla ya Giroud kuipa timu yake pointi moja kwa kusawzaisha bao dakika ya 90.
Katika mechi nyingine za ligi hiyo Chelsea waliendelea kukalia kiti cha uongozi baada ya mapema kupata ushindi wa mabao 2-0, huku West Ham ikizinduka ugenini na kupata ushindi mnono wa mabao 3-1 dhidi ya
Crystal Palace, huku Aston Villa ilibanwa nyumbani na Newcastle United kwa kutoka suluhu ya kutofungana.
Southampton iliendelea kuchechemea kwa kulazimishwa suluhu nyumbani na West Bromwich na Swansea inaendeleza ubabe baada ya wiki iliyopita kuitoa nishai Manchester United, iliifumua Banley kwa bao 1-0.
Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea leo kwa michezo mitatu, Hull City itakuwa nyumbani kupepetana na Stoke City, Tottenham Hotspur itaikaribisha QPR na Sunderland itaikaribisha Manchester United na kesho Manchester Citry itakuwa dimba la nyumbani kuumana na Liverpool.
TCRA yailima faini kituo cha Cloud's kisa....!

Wakielezea
uamuzi huo jijini Dar es Salaam, Kamati ya Maudhui ya mamlaka hiyo
ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Margaret Munyagi ilisema kuwa ukiukwaji
wa kanuni hizo ulifanywa kwa nyakati tofauti na vituo hivyo.
Alisema
kwa upande wa kituo cha redio cha Clouds, kupitia kipindi chake cha
‘Njia Panda’ kilichorushwa hewani Juni 15 mwaka huu kati ya saa 8.00
mchana na saa 10.00 jioni kilikuwa na mada iliyohusu safari ya kuzimu
ambapo maudhui yake yalijaa simulizi za kufikirika, za kishirikina na
kichawi.
Aidha
alisema kosa lingine kituo hicho hakikufuata kanuni za
Utangazaji(maudhui) za mwaka 2005 zinazowataka kuwasilisha ratiba ya
vipindi vyao kwa TCRA ili viidhinishwe na vilevile kuvichapisha katika
gazeti kabla ya kurushwa hewani ambapo kipindi cha Njia Panda
hakikuwasilishwa kwa ajili ya kuidhinishwa.
Wakati
huo huo, kituo cha televisheni cha Clouds kilirusha kipindi cha ‘Bibi
Bomba’ Mei 16 na Juni 6 mwaka huu kati ya saa 3.00 na saa 4.00 usiku
ambacho kilikiuka kanuni za Utangazaji (maudhui) za mwaka 2005.
Alisema
kipindi hicho kilidhalilisha mabibi hao walioshiriki pamoja na wanawake
kwa ujumla kutokana na maswali ya aibu waliyokuwa wakiulizwa na waamuzi
wa shindano hilo ambayo ni kinyume na kanuni hizo.
Aidha
alisema kituo hicho kinatozwa faini ya Sh milioni moja na kutakiwa
kuwasilisha TCRA mwongozo wa kuchuja na kusimamia maudhui yasiyofaa
kabla ya kutangazwa.
TCRA imesema kama Kanuni za Utangazaji zitaendelea kukiukwa hatua kali zaidi za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Friday, August 22, 2014
Mtibwa Sugar, Polisi Moro kupimana ubavu kesho Morogoro
![]() |
Polisi Moro |
![]() |
Mtibwa Sugar |
Mechi hiyo itafanyika katika uwanja wa Jamhuri uliopo mjini Morogoro kuanzia saa 10 kwa kiingilio cha sh 1,000.
kwa mujibu wa taarifa iliotolewa na Afisa habari wa Shirikisho la soka nchini TFF Boniface Wambura alisema tiketi za mechi hiyo zitaanza kuuzwa leo kupitia mtandao wa M-Pesa, CRDB Simbanking na maduka 30 ya Fahari Huduma yaliyopo katika wilaya zote za Mkoa wa Morogoro.
Alisema mashabiki 100 wa kwanza watakaoanza kuingia uwanjani wapata jezi za timu ya Mtibwa Sugar na Polisi Morogoro.
Aliongeza kusema kusema tayari mechi ya majaribio ya tiketi za elektroniki imeshafanyika katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya ambapo timu za Tanzania Prisons na Mbeya City zilichuana na kutoka sare.
Alisema mechi nyingine za majaribio ya tiketi za elektroniki zinatarajiwa kuchezwa Agosti 30 mwaka huu.
Alisema katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga kutakuwa na mechi kati ya Coastal Union na Mgambo Shooting wakati katika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba ni Kagera Sugar dhidi ya mabingwa wa Mkoa wa Kagera, Eleven Stars.
Wambura alisema Septemba 6 mwaka huu katika Uwanja wa Taifa kutakuwa na mechi kati ya Simba na Mtibwa Sugar.
Alisema mchezo wa ngao ya Jamii utakaozikutanisha timu ya Azam FC na Yanga afrika umepangwa kufanyika Septemba 13 katika Uwanja wa Taifa,uliopo jijini Dar es Salaam.
Mtibwa inatarajiwa kuanza ligi kwa kuikaribisha Yanga kwenye uwanja wa Jamhuri wakati Polisi Moro itakaribishwa tena katika ligi kwa kuumana na Azam kwenye uwanja wa Chamazi Septemba 20.
Wakati huo huo waamuzi wanaotarajia kuchezesha mechi za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu huu watafanya mtihani wa utimamu wa mwili (physical fitness test) mwezi ujao.
Mtihani huo utahusisha waamuzi wa daraja la kwanza (class one) wakiwemo wale wenye beji za Shirikisho la Kimataifa la soka duniani (FIFA).
Alisema mbali ya mtihani huo unaotarajiwa kufanyika kabla ya Septemba 10 mwaka huu, kutakuwa na semina ya makamishna ambao watasimamia mechi za VPL na FDL.
Alisema waamuzi wote wanatakiwa kutumia muda uliobaki kufanya maandalizi kwa ajili ya mtihani huo.
Majanga yaanza mapema Arsenal, Arteta kuikosa Everton kesho

MAJANGA yamezidi kuiandama Arsenal baada ya kiungo mkabaji wao, Mikel Arteta naye kuelekea chumba cha majeruhi kwa mechi mbili baada ya Jumanne kuumia kifundo cha mguu 'ankle' kwenye mechi ya kuwania kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Besiktas ya Uturuki.
Nahodha huyo wa Arsenal alitolewa nje katika dakika ya 50 kwenye Uwanja wa Olympic Ataturk baada ya kuumia wakati akiwania mpira dhidi ya mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Demba Ba.
Arsenal pia itamkosa Aaron Ramsey baada ya kutolewa nje kwa kadi mbili za njano katika kipindi cha pili kwenye mechi hiyo ya Uefa.
Arteta sasa ataikosa mechi ya Ligi Kuu England Jumamosi ugenini dhidi ya Everton pamoja na ile ya marudiano ya kuwania kufuzu hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Besiktas itakayopigwa Jumatano kwenye Uwanja wa Emirates.
Jana alitarajiwa kufanyiwa uchunguzi zaidi lakini ni wazi kabla ya hapo alishaelezwa kuzikosa mechi mbili zijazo.
Chumba cha majeruhi cha Arsenal tayari kimeanza kupokea wagonjwa baada ya Yaya Sanogo na Kieran Gibbs kuwa majeruhi na kuikosa mechi dhidi ya Besiktas ambayo walitoka sare tasa huko Istanbul.
Haitakuwa rahisi kwa Arsenal katika mechi hiyo ya marudiano dhidi ya Besiktas, na zaidi kutokana na kuwakosa Aaron Ramsey na Mikel Arteta, lakini haijawahi kutolewa katika mechi hizo za mchujo za Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Hata hivyo, Mesut Ozil, Per Mertesacker na Lukas Poldolski watakuwamo kwenye kikosi cha Arsenal jambo ambalo linamshawishi kiungo Jack Wilshere kwamba wataonesha tofauti kubwa.
Mshale wa Kifo wa Aisha Bui kutua sokoni Jumatatu
![]() |
Kava la filamu mpya ya Aisha Bui iitwayo Mshale wa Kifo |
![]() |
Aisha Bui katika pozi |
Akizungumza na MICHARAZO, Aisha Bui alisema filamu hiyo aliyoigiza na wakali kama Mzee Chilo, Gabo wa Zagamba na wengine itaingia sokoni Agosti 25, huku kampuni yake ya bad Girl ikijipanga kuandaa kazi nyingine kali zaidi na hiyo.
Aisha Bui, alisema japo filamu hiyo ni kazi yake ya kwanza kuiandaa, lakini kwa jinsi ilivyoandaliwa kwa umakini mkubwa ni wazi mashabiki watajua ujio wake mpya siyo wa kubahatisha.
"Naiachia filamu yangu Jumatatu, nawaomba mashabiki waniunge mkono kwa kununua nakala halisi, ili kuiwezesha kampuni ya Bad Girl kuendelea kuwapa uhondo zaidi, kuna makubwa yapo njiani kutoka kwangu," alitamba Aisha Bui.
Nyota huyo aliyecheza filamu mbalimbali ikiwamo ya Saturday Morning, Better Days, Not Without My Son, Continous Love, Revenge of Love, Mirathi, Pain of Love, Crazy Love na The Second Wife, alisema ndani ya filamu hiyo mpya inasimulia kisa cha mfanyabiashara wa dawa za kulevya ambaye anamlazimisha askari Polisi kumsaidia kupitisha mzigo wake.
Hata hivyo kazi haiwi rahisi na kuibua kashkash kwa binti wa askari huyo Myrine nafasi iliyochezwa na Aisha kufanywa kama chambo.
"Ni simulizi linalosisimua na kutia simanzi na bahati nzuri walioiigiza kuanzia mimi mwenyewe, Gabo, Mzee Chilo na wengine tumeitendea haki," alisema Aisha.
Liverpool yarudi kumwania 'mtukutu' Mario Balotelli
![]() |
Balotelli enzi akiwa Manchester City |
Mwezi uliopita, Brendan Rodgers alisema Liverpool haiwezi kumsajili Balotelli, lakini amebadili moyo wake.
Mapema leo Balotelli aliwaambia Sky Italia: “Leo itakuwa siku yangu ya mwisho Milanello.”
Nyota huyo kurudi England kutateka hisia za mashabiki wengi wa soka wakikumbuka vituko vyake akiwa Manchester City kabla ya kuondoka mwaka 2013.
Balotelli amejihusisha na matukio mengi ya utovu wa nidhamu hususani wakati akicheza ligi kuu England
Ndani ya uwanja, alioneshwa kadi nyekundu wakati Man City ilipochuana na Asernal mwaka 2012 na kufungwa.
Nje ya uwanja, alikuwa na matukio ya mengi ya ukutuku.
Moja ya tukio la kukumbukwa pia ni kitendo chake cha kuonesha fulana iliyoandikwa ‘Why Always Me?’ alipofunga goli kwenye mechi ya mahasimu wa Manchester ndani ya dimba la Old Trafford mwaka 2011.
Pia aliingia katika mgogoro na kocha wa City wakati ule, Roberto Mancini ndani ya uwanja wa mazoezi na kukunjana.
Zaidi alimchapa kibao Jerome Boateng.
Tangu aliporudi nchini Italia amefunga mabao 30 katika mechi 54, idadi sawa na aliyofunga akiwa na City katika mechi 80.
Si rahisi kusahau kuwa nyota huyu tayari ameshinda makombe manne katika mataifa mawili, ubingwa ligi na kombe la FA na Coppa Italia akiwa na umri wa miaka 24.
Di Maria aomba kuondoka Real Madrid

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina amepoteza namba katika kikosi cha kwanza Madrid kufuatia kutua kwa James Rodriguez na Toni Kroos katika kipindi hiki cha usajili na amedhamiria kutafuta namba kwingineko.
Di Maria amekuwa akihusishwa sana na PSG na Manchester United katika miezi kadhaa iliyopita, lakini mabingwa hao wa Ligue 1 walisema hivi karibuni kuwa hawana mpango wa kumsajili winga huyo kutokana na sababu za kiuchumi, na hivyo kuiachia Man U nafasi kubwa ya kumpata.
"Ameniomba kuondoka katika kipindi hiki cha usajili. Amekataa ofa ya klabu ya kubaki Madrid, hivyo tunatafuta suluhisho," Ancelotti alisema kwenye mkutano na waandishi wa habari.
"Tutapata suluhisho kwa Di Maria kabla ya dirisha kufungwa, lakini kwa sasa anabaki kuwa mchezaji wa Madrid. tuko katika hali ambayo mchezaji anatakiwa kujitafutia klabu mwenyewe.
"Kama Di Maria atashindwa kupata suluhisho mwenyewe, atabaki hapa. Tunamkaribisha na anaweza kuendelea kufanya kazi hapa. hakuna shida."
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 26, aliyejiunga na Madrid akitokea Benfica katika kipindi hiki cha uhamisho cha 2010, ana mkataba na Madrid hadi 2018, lakini anaweza kuuzwa kwa euro milioni 60.
Extra Bongo, Omar Tego kuwasindikiza Masai Safari Band
Uzinduzi wa albamu hiyo iitwayo 'Hakuna Kama Baba' utafanyika kwenye ukumbi wa Lunch Time na kwa mujibu wa Rais wa Masai Safari, Francis Mwaisela, Extra Bongo ni kati ya watakaowasindikiza siku hiyo.
Mwaisela alisema makundi mengine yatakayokuwapo ukumbini kuwapia tafu siku hiyo ni Coast Modern linaloongozwa na waimbaji ndugu, Omar na Maua Tego.
"Extra Bongo, Omar Tego na dada yake Maua Tego na wasanii wengine wa muziki wa kizazi kipya ndiyo watakaotusindikiza siku ya uzinduzi wa albamu yetu utakaofanyika Agosti 30," alisema Mwaisela.
Rais huyo wa Masai Band alizitaja nyimbo zilizopo katika albamu hiyo ni 'Hakuna Kama Baba', 'NJia Panda', 'Mikoni ni Kazi', 'Ndoa ni Mipango ya Mungu', 'Usiwasikilize Wambea,' na Kilio Changu'.
"Kwa sasa tupo kenye mazoezi makali kwa ajili ya uzinduzi huo ambao tumepania kuweka rekodi nchini," alisema Mwaisela
Queen Darlin ageukia filamu, kuuza sura kwa Chekibudi
DADA wa nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, Diamond Platnumz, Mwajuma Abdul 'Queen Darling' anatarajiwa kuibuka kwenye anga za uigizaji baada ya kushirikishwa katika filamu iitwayo 'Kisebusebu'.
Filamu hiyo na muigizaji nyota nchini Nurdin Mohammed maarufu kama 'Chekibudi' imekamilishwa kurekodiwa hivi karibuni na inafanyiwa mchakato wa kuachiwa mwezi ujao.
Chekibudi aliiambia MICHARAZO kuwa, Queen Darling anayetamba na nyimbo kama 'Wajua Nakupenda', 'Maneno' na 'Wanatetemeka' pamoja na remix ya 'Nakomaa na Jiji', ameitendea haki filamu hiyo.
"Huwezi kuamini kama Queen Darling ni msanii wa muziki wa kizazi kipya kwa jinsi alivyotenda haki mbele ya kamera," alisema Chekibudi na kuongeza mbali na msanii huyio filamu hiyo pia ameiigiza yeye (Chekibudi), Tiko Hassan na wakali wengine.
Wasanii kadhaa wa bongofleva wamekuwa pia wakitamba katika Bongo Movie kama Snura, Shilole a.k.a Shishi Baby na Hemed Suleiman a.k.a PHD.
Babu Tale acharuka tuhuma za Diamond na Dawa za Kulevya
![]() |
Diamond (kulia) akiwa na Meneja wake, Babu Tale na Aunty Ezekiel |
"Tunalipwa milioni 20 show moja, tunalipwa dola elfu 25,000 show moja, hii ni zaidi ya madawa ya kulevya. “We get more money from music, sio kwenye madawa ya kulevya, hatufanyi hizo biashara na kama wanahisi sisi tunafanya tunawaruhusu watufanyie investigation hata kwa muda wa miaka kumi ina maana tunavyopita pale airport hawana vifaa vya kutuchunguza? Ipo wazi hata Global walishindwa kufanya kazi na sisi kwa sababu sisi ni wakubwa.
Sasa leo hii tunauza madawa ya kulevya kwa sababu tunakomaa kwenye bei zetu. “September tunafanya show kubwa ya Unplugged na msanii wa kwanza hapa kufanya ile show ni Diamond na ile show hawalipi hela ya kis**e.
Wataendelea kuona watu wanauza madawa ya kulevya, hakuna msanii wa Tanzania anayefanya show kwa walau dola elfu 10,000 ni Diamond peke yake wengine ni dola 2000, 2500 elfu 3,000 mwisho.
Tuna show Marekani show kumi na tano (15), show kumi na tano dola elfu ngapi? Na kwa hapa Tanzania hatufanyi show chini ya dola elfu 15,000.”
Subscribe to:
Posts (Atom)