STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, June 20, 2013

Waraka namba 2 wa Zola D kwa Watanzania

Zola D katika pozi
BARUA MAALUM KUTOKA KWA DAVID MICHAEL MLOPE,aka ZOLA D KWENDA KWA WATANZANIA WOTE WALIOSHIRIKI KATIKA MSIBA WA MANGWEAR.pamoJa na LANGA KILEO.

DAVID MICHAEL MLOPE BOX 70098 DAR ES LAAM TANZANIA.
PHONE +255715296889.
barua no 2.

naendelea pale nilipoishia kwenye barua ya mwanzo namba 1 ...... habari zenu ndugu zangu watanzania hope wote ni wazima na mnaendelea na mishe za maisha mimi mzima siJambo Japo nina stress nyingi sana mpaka nimepungua kg 3,kutokana na mawazo na kuto kulala tokea msiba wa arbert mangwear pia tumepata pigo Jingine la mdogo wetu langa kileo,siJui niseme nini kwa Jinsi inavyo niuma ila nina mwachia Mungu maana ndio kazi yake pia pole sana wazazi wa langa kileo baba na mama pamoJa na familia yote kwa uJumla pia asante sana watanzania wote walioJitokeza kwenye safari ya kumsindikiza ndugu yetu msanii mwenzetu langa kileo leo nataka kugusia sana upande wa maisha yetu na dini kama binadamu tunaopita tu kwenye hii dunia maana kila mtu atakufa vitabu vya dini vimeandika.Ndugu zangu wapendwa watanzania dunia imekwisha ndugu zangu tuanze kufanya ibada na kutenda yaliyo mema coz free masons wanawatumia ndugu zetu kwenye big brother na seemu mbali mbali kuwaonyesha wakiwa watupu uchi na kuwadanganya kwa pesa,na sasa wameingia africa mashariki kwa kishindo sana hawa free masons Juzi tu nimepigiwa simu na watu kampuni Jina siri yangu wanataka nikacheze video ya ngono na mwanamke kwa kitita cha milion 70 nikawaeleza siwezi kufanya uchafu kama huo,na leo tena wamenipigia wakisema watanipa milion 100 bado nimekataa Je unaelewa kwa nini nimekataa? free masons wanataka viJana shupavu na wenye akili na vipaJi ili waweze kuwatumia kuitangaza dini yao na wanaweza kukupa maisha ya Juu kwa gharama yoyote ile, Mungu atuepushe nao na Mungu atulindie watoto wetu inshallah wasiingie kwenye dini ya kishetani,wahi kuwapeleka madrasa watoto mapema waitambue dini mapema na kuwapeleka kwenye mafunzo ya dini kwenye makanisa tuliyoyazoea tokea kitambo na tuachane na makanisa mapya yanayoanzishwa kila kukicha na wachungaJi wao wanaJiita miungu watu,ndugu zangu naelewa watu wanaweza kuniona kama nilie changanyikiwa hapana ila nimeamua kupoteza muda wangu kukaa chini na kuandika machache ninayoyaona kwa upeo wangu na vipaJi alivyonipa Mungu kuelimisha na kuburudisha,siwezi kukaa kimya pale ninapo tizama taifa langu lina teketea kwa maovu,na tunapelekeshwa kishetani na dini feki na makampuni ya kigeni katika nchi yetu tuna acha utamaduni wetu na tunaingia kwenye utamaduni wa watu wa kishetani kwa upeo wetu mdogo na umasikini tumetekwa na pesa na starehe kiasi kama sisi wasanii ukitizama storia ya msanii mwanzo kabla aJawa super star alikuwa ni mtu wa kufanya ibada ila sasa amekuwa super star awezi tena kufanya ibada wala kutoa dhaka au kuwasaidia wazazi wake kisa yeye ni star na yupo bussy Je swali huyu star msanii ni kioo cha Jamii au amegeuka kuwa moto wa Jamii? kila kukicha kwenye magazeti utaskia story za sifa mbaya na picha chafu za wasanii sehemu flani wakifanya ngono na mambo mengine ya kumchafua Mungu wetu,ndugu zangu wasanii naomba tubadilike na tuwe mfano ili tuweze kuliongoza taifa letu salama na tuwafundishe wadogo zetu waige mfano mzuri wa tabia zetu nJema na sio uchafu wetu,ndugu zangu watanzania mimi sitaki kuwachosha maana nina MAMBO MENGI SANA YA KUANDIKA ILA NAONA KWA LEO NISHIE HAPA,NACHUKUA NAFASI HII KUAMBIA NAWAPENDA SANA WATANZANIA WENZANGU PIA NAWAPENDA VIONGOZI WANGU WA TANZANIA PIA NAIPENDA NCHI YANGU YA TANZANIA NIPO TAYARI KUFA KUITETEA NCHI YANGU NA WANACHI WANGU NAWATAKIA MAISHA MEMA NA FAMILIA ZENU NI MIMI MTIIFU WENU KATIKA UjENZI WA TAIFA LETU TUKUFU, DAVID MICHAEL MLOPE AKA ZOLA D.ITAENDELEA!!!!!

Zola D awashukuru Watz msiba wa Ngwair, Langa, lakini...!


Mwili wa Ngwair ukiingizwa kaburini, ambapo Zola D (mwenye miwani) naye alikuwa mmoja wa walioshiriki mazishi hayo mjini Morogoro.

BARUA MAALUM KUTOKA KWA DAVID MICHAEL MLOPE,ZOLA D KWENDA KWA WATANZANIA WOTE WALIOSHIRIKI KATIKA MSIBA WA MANGWEAR...

DAVID MICHAEL MLOPE BOX 70098 DAR ES LAAM TANZANIA.
PHONE +255715296889.

habari za leo watanzania wote ,nachukua nafasi hii kwa niaba ya wasanii wa kundi la chemba sqward east zoo,kuwashukuru watanzania wote walioshiriki katika msiba wa ndugu yetu mpendwa mangwear hakika nimeona upendo wenu kwa kumzika ndugu yetu Arbert k mangwear kwa upendo wenu mkubwa sana,mimi binafsi sina cha kuwalipa ila nina imani kubwa sana Mungu atawalipa,na sio kwa mangwear tu naomba mzidi kushilikiana na sisi wasanii wenu hata siku nikifa mimi au msanii mwingine naomba mtuzike KWA UPENDO msituache maana sie sote ni binadamu tunapita tu hapa kwenye hii dunia kila mtu atakufa muhimu ni kupendana na kushirikiana kwa upendo,pia kama tunagombana hapa duniani ni bora tupatane kabla ya kifo kutukumba siku yetu ya kufa hakuna anaetambua itakuwa lini, maana Mungu alisema ukisamehe na yeye atakusamehe siku yako ya kihama,kuna mambo mengi nimejifunza kwenye hii dunia,kwamba tujitahidi kufanya yaliyo mema kutengeneza njia bora siku tukifa,napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru sana wana kamati wote waliojitolea tokea mwanzo kuandaa safari kutoka south africa mpaka tanzania asante sana BRO P FUNK MAjANI , BONGO RECORDS kwa upendo wako na mchango wako kwetu sie wadogo zako Mungu ATAKULIPA ZAIDI NA ZAIDI ,ASANTE SANA RADIO CLOUDS FM KWA KUSHIRIKI KWA UPENDO WENU MKUBWA ,na wafanyakazi wake wote walioshiriki kwa upendo katika kukamilisha safari ya mpendwa wetu MANGWEAR,asante sana BRO ADAMU jUMA VISUAL LAB NIMEONA KAZI KUBWA ULIYOIFANYA MUNGU AKUBARIKI SANA ENDELEA KUWA NA MOYO HUO HUO , ASANTE SANA, BRO MIRAD AYO,BRO MAjIZO,BRO TC TIMOTH CHERULA,ADAMU MCHOMVU,RADIO TIMES FM,RADIO EAST AFRICA NA EAST AFRICA TV,ITV,CHANEL TEN BRO RIZ 1 KIKWETE,BRO SUGU,SIST j DEE,Dj CHOKA, PUSH NA WENGINE WENGI,AMBAO NIMEWASAHAU MAjINA YENU ASANTENI SANA SANA WOTE WALIOTOA MAGARI YAO KWENDA MOROGORO KUZIKA,PIA ASANTE SANA WANAKAMATI WA MOROGORO,ASANTE SANA VIONGOZI WA POLICE DAR ES SALAAM NA VIONGOZI WA POLICE MOROGORO KWA KUIMALISHA ULINZI KATIKA MSAFARA WA MANGWEAR KUANZIA DAR MPAKA MOROGORO NINA MAMBO MENGI SANA YA KUANDIKA ILA NAONA KWA LEO NISHIE HAPA,NACHUKUA NAFASI HII KUAMBIA NAWAPENDA SANA WATANZANIA WENZANGU PIA NAWAPENDA VIONGOZI WANGU WA TANZANIA PIA NAIPENDA NCHI YANGU YA TANZANIA NIPO TAYARI KUFA KUITETEA NCHI YANGU NA WANACHI WANGU NAWATAKIA MAISHA MEMA NA FAMILIA ZENU NI MIMI MTIIFU WENU KATIKA UjENZI WA TAIFA LETU TUKUFU, DAVID MICHAEL MLOPE AKA ZOLA D.ITAENDELEA!!!!!

Barabara ya Kimara King'ongo yafungwa mwezi mzima kisa....!




HIVI ndivyo wakazi wa Kimara King'ongo Kata ya Kimara na Samanga wanavyohenyeka majira ya asubuhi kwa kutembea kwa miguu kupandisha kilima sumbufu cha Peter's School ambacho kinatengenezwa kwa kuwekewa zege ili kuruhusu magari kupita bila usumbufu .
Matengenezo ya barabara hiyo yanayoendelea kwa sasa yamefanya njia hiyo ifungwe kwa mwezi mzima tangu Juni 1-30, ili ikiachiwa wakazi wa eneo hilo wafurahie huduma ya usafiri baada ya sasa kila siku asubuhi magari ushusha abiria darajani badala ya kuzunguka njia ya kutokea Stop Over au Kimara Temboni.

Hatimaye mhanga wa bomu la Arusha azikwa

HATIMAYE aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA (BAWACHA) Kata ya Sokoni I, Judith William Moshi, aliyefariki kwa mlipuko wa bomu kwenye viwanja vya Soweto jijini Arusha siku ya Jumamosi (Juni 15, 2013) wakati wa ufungwaji wa kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani umezikwa leo jijini humo.
Chini baadhi ya picha za msafara wa mazishi wa mwanadada huyo ambaye alikuwa miongoni mwa watu watatu waliokufa katika mlipuko huo ambao al manusura ungewakumba viongozi wa kuu wa chama hicho akiwamo Mwenyekiti wao, Freeman Mbowe (Mbunge).

Hapa ni Sugu akiwa na Peter Msigwa wakiongoza msafara.
Viongozi  wa chadema watua Arusha kwa ajili ya kutoa heshima zao za mwisho kwa wale waliofariki katika mkutano wa Chadema wakati wa mripuko wa bomu. Huku wakishirikiana na wananchi wa Arusha, John Mnyika ataongoza shughuli hizo.
Hili ndilo jeneza lililolobeba mwili wa marehemu ukipelekwa sokon 1


 

Mbowe, Lema wajisalimisha Polisi

Mwenyekiti wa CHADEMA  Fremaan Mbowe pamoja na mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema leo wamejisalimisha Polisi  baada ya jeshi hilo kutangaza linawasaka baada ya vurugu ziliztokea jana mjini Arusha.
Akiongea na waandishi wa habari,  Fremaan Mbowe alisema kuwa wao wamejisalimisha kama polisi walivyosema wanawatafuta na walipofika waliandika maelezo ambapo alisema kuwa polisi waliwaita kwa mambo mawili, moja likiwa ni kwa kuwahoji kwanini walifanya mkutano usio wa halali ambapo alisema kuwa;
"Jambo la kufanya mkutano pasipo kuwa halali sio kweli kwani polisi walituruhusu tukafanye mkutano katika sehemu hile lakini kinachotushangaza tumefanya wamekuja kutupiga mabomu na kusema sio wa halali na kuhusiana na ushahidi msimamo wangu upo pale pale tunao ushahidi wa kutosha na tunamjua aliyerusha bomu Jumamosi, lakini hatutautaoa hadi  Rais atakapounda Tume Huru ya majaji ili wafuatilie suala hili. Hao ndiyo tutawaonyesha ushahidi huo, lakini siyo Polisi hatuwezi kuwapa," alisema Mbowe.
Afande Chagonja akiongea na waandishi wa habari
Kwa upande wa Polisi kupitia Kamishna wa Mafunzo na Operesheni za Kijeshi,  Paul Chagonja akiongea na wanahabari alisema waliwahoji wabunge hao na kuwaomba ushahidi waliokuwa nao kama wanavyodai, lakini waheshimiwa hao hawakutoa ushirikiano.
"Mbowe alisema kuwa ana ushahidi na hata katika vyombo vya habari ametangaza lakini nashangaa tulivyomuuliza hapa amesema kuwa hana ushahidi wowote na wala hajawahi kutamka hivyo sasa sisi kwa kuwa kasema hivyo nitakaa na makachero wangu na tutaangalia jinsi ya kufanya"alisema Chagonja
Aidha alisema kuwa alimuliza mbunge wa Arusha mjini kwanini awali alikuja kuwasifia Polisi baadae akawageuka ilihali alishasema katu hawezi kusema uongo na kuwajibu kuwa, yeye anafuata mwenyekiti wake anachosema.

Polisi waua raia kwa risasi Mbeya, RPC afafanua kilichotokea




 Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya  Diwani Athuman
---

MAUAJI YA MTU MMOJA KUFUATIA VURUGU YA WANANCHI WA KIJIJI CHA LUMBILA WILAYA YA MBOZI KUWASHAMBULIA ASKARI WALIOKUWA WANAFANYA OPERESHENI.
--
MNAMO TAREHE 19.06.2013 MAJIRA YA SAA 13:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA LUMBILA KATA YA RUANDA WILAYA YA MBOZI MKOA WA MBEYA. RAJABU S/O WILSON MWASHITETE, MIAKA 25, MNYIHA, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA LUMBILA ALIUAWA KWA KUPIGWA RISASI NA ASKARI POLISI WALIOKUWA KATIKA MSAKO DHIDI YA WAHALIFU/WAPORAJI KATIKA ENEO LA MLIMA SENJELE.

CHANZO NI BAADA YA ASKARI POLISI WAKIWA KATIKA OPERESHENI ENEO HILO KUZINGIRWA NA KUNDI LA WANANCHI ZAIDI YA 150 WA KIJIJI HICHO WAKIWA NA SILAHA ZA JADI MAPANGA, MARUNGU, SHOKA NA MAWE WAKIWAZUIA ASKARI HAO KUKAMATA WAHALIFU NA KUANZA KUFANYA VURUGU BAADA YA KUWA WAMEKAMATA MALI INAYODHANIWA KUWA YA WIZI AMBAYO NI MAFUTA  AINA YA DIESEL MADUMU ZAIDI YA 100.

HATA HIVYO KUFUATANA NA VURUGU ZILIZOJITOKEZA WALIFANIKIWA KUCHUKUA MADUMU MACHACHE AMBAYO NI MADUMU MATATU YENYE UJAZO WA LITA 60, MADUMU MAWILI YENYE UJAZO WA LITA 20 NA 
MADUMU NANE LITA 30 HIVYO UVAMIZI HUO WA WANANCHI NDIO ULIOWAFANYA ASKARI POLISI WASHINDWE KUCHUKUA VIELELEZO VYOTE.


MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA MBOZI.  AIDHA KATIKA TUKIO HILI CHARLES  S/O JOSE  MWAWALO,MIAKA 27,MNYIHA,MKULIMA MKAZI WA KIJIJI CHA LUMBILA ALIJERUHIWA KWA KUPATA MICHUBUKO TUMBONI AMBAPO UCHUNGUZI UNAFANYWA KUBAINI NI KITU GANI KILICHOMJERUHI.

PIA WANANCHI WALIFUNGA BARABARA KUU YA MBEYA/TUNDUMA KWA KUWEKA MAWE NA MAGOGO NA KUSABABISHA MSONGAMANO MKUBWA WA MAGARI BARABARANI. 

HALI ILIKUWA SHWARI BAADA YA KAMANDA WA POLISI KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI KUFIKA ENEO LA TUKIO NA KUZUNGUMZA NA WANANCHI PAMOJA NA VIONGOZI WA ENEO HILO KISHA KUFUNGUA BARABARA .

ASKARI POLISI WANNE WALIJERUHIWA KATIKA TUKIO HILO KATI YAO WATATU WALIPATIWA MATIBABU NA KURUHUSIWA NA ASKARI MMOJA  AMELAZWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA KWA MATIBABU ZAIDI . 

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA BADALA YAKE KUWA NA UTAMADUNI WA KUTATUA KERO/MALALAMIKO YAO KWA NJIA YA MAZUNGUMZO KWA KUYAWASILISHA KATIKA MAMLAKA HUSIKA. AIDHA ANAWATAARIFU WALE WOTE WALIOWAHI KUIBIWA/KUPORWA MALI MBALIMBALI YAKIWEMO MAFUTA WAJITOKEZE POLISI KWA AJILI YA HATUA ZINAZOSTAHILI.


Signed By,
                          
[DIWANI ATHUMANI  

[DIWANI ATHUMANI   - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

NMB, Wabunge walivyoonyeshana kazi Dodoma

KATIKA kuendeleza na kuimarisha uhusiano mzuri baina ya Benki ya NMB na Watunga Sheria wa Bunge la Jamhuri, mwishoni mwa wiki timu hizo zilionyeshana kazi kwa kuumana katiuka pambano lililoandaliwa na Benki hiyo ambao uilihudhuriwa na mashabiki lukuki wa timu hizo wea mjini Dodoma.
 Hiki ndicho kikosi kamili cha timu ya benki ya NMB kilichong’ara katika mechi na timu ya Wabunge kwenye Uwanja wa Jamhuri.
 Kikosi kamili cha timu ya Wabunge.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mh. George Mkuchika ambae alikua ndiye mgeni rasmi akikagua kikosi cha timu ya NMB  kabla ya mpambano huo.
 Naibu waziri wa habari Vijana,Utamaduni na Michezo Mh.Amos Makalla (Jezi ya njano na Bluu) akipigwa chenga na  Afisa mkuu wa fedha NMB  Waziri  Waziri katika mtanange huo uliokuwa wa kukata na shoka.
 Mbunge wa Kinondoni Mh. Iddi Azan ambae ndiye mlinda mlango wa timu ya wabunge  (Jezi ya rangi ya chungwa) akiongoza wachezaji wenzake kufurahia goli moja walilolipata na kuwapa ushindi dhidi ya timu ya NMB
Mashabiki wa timu zote mbili wakifuatilia mtanange huo ambao uliisha kwa Wabunge kuibuka kidedea dhidi ya NMB.

Prof Lipumba mgeni rasmi miaka `13 ya Kikosi cha Mizinga

http://sphotos-a.ak.fbcdn.net/hphotos-ak-ash3/p480x480/712_467874856634160_1616825647_n.jpg
Kiongozi wa Kikosi cha Mizinga, Karama Masoud 'Kalapina'
 MWENYEKITI wa Chama cha CUF, Prof Ibrahim Lipumba anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika onyesho la maadhimisho la miaka 13 ya Kikosi cha Mizinga zinazotarajiwa kufanyika kesho kwenye ukumbi wa Msasani Club, jijini Dar es Salaam.
Kiongozi wa Kikosi, Karama Masoud 'Kalapina' aliiambia MICHARAZO kwamba, Prof Lipumba ndiye atakayekuwa mgeni rasmi baada ya mipango ya awali kumualika Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Idd Azan kushindikana kumpaka kwa kuwaomba udhuru.
Kalapina alisema maandalizi ya onyesho hilo ambalo mashabiki watalazimika kulipa Buku 5 tu mlangoni, yamekamilika ikiwemo kuongezeka kwa idadi ya wasanii na makundi yatakayowasindikiza katika onyesho hilo ambalo litaambatana na maonyesho mbalimbali yenye asili ya utamaduni wa Hip hop.
"Maandalizi ya onyesho la Kikosi cha Mizinga yamekamilika ikiwemo kutarajiwa Mwenyekiti wa Kitaifa wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba kuwa mgeni rasmi baada ya kumkosa Mhe. Idd Azan, pia burudani zimeongeza zaidi katika kunogesha miaka hiyo 13," alisema Kalapina. 
Mkali huyo ambaye pia ni mwanaharakati na mwanasiasa alisema baadhi ya wasanii watakaoshiriki kupigwa mizinga 21 ya Kikosi kesho ni Afande Sele, Young Killer, Manzese Crew, Stereo, Kala Jeremiah, LWP, Mansu-Lee, Gangwe Mob  wakiwa na Inspekta Harun na wengine wakiwamo Kikosi cha Mizinga chenyewe.
Shughuli nyingine zitakazoambatana na onyesho hilo ni maonyesho ya uchoraji na kupaka rangi, mitindi ya nguo na mavazi, kucheza break dance na utoaji wa tuzo kwa watu na asasi zilizosaidia Kikosi cha Mizinga kufika hapo ilipo ikiwa inatimiza miaka hiyo 13 tangu kuzaliwa kwake.

Wednesday, June 19, 2013

Mabondia Juma Fundi , Nassib Ramadhani kuzipiga Idd Pili


Bondia Juma Fundi kushoto akitunishiana misuri na Nasibu Ramadhani wakati wa utambulisho wa mpambano wao utakaofanyika sikukuu ya Idi pili wengine kushoto ni mratibu Duni Lianjara Promota wa Mpambano huo Side Mkigoma na kocha wa Nasibu Christpher Mzazi.
PROMOTA WA MPAMBANO WA MASUMBWI SIDE MKIGOMA KATIKATI AKIWAINUA MIKONO JUU MABONDIA JUMA FUNDI KUSHOTO NA NASSIBU RAMADHANI
Mabondia wakisaini mkataba

Ticha la twisheni lanaswa kwa kumbaka denti wa miaka 10

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwani Athmani amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba lilitokea juzi hivi karibuni katika kijiji cha Itunge wilaya ya Kyela mkoa wa Mbeya.


JESHI la Polisi Mkoani Mbeya linamshikilia Mwalimu wa Masomo ya Ziada akituhumiwa kumbaka Mwanafunzi wa darasa la nne mwenye umri wa miaka 10.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwani Athumani amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba lilitokea hivi karibuni katika kijiji cha Itunge wilaya ya Kyela mkoa wa Mbeya.
Alimtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Ipyana Gidion (30) mkulima na mwalimu wa masomo ya ziada (tuition) katika kituo cha Itunge Moravian   mtaa wa Mbugani Wilayani Kyela Mkoani hapa.
Alisema Mtuhumiwa huyo alimbaka mtoto mwenye umri wa  miaka 10, kyusa,mwanafunzi  darasa  la  nne  katika Shule ya msingi Mbugani mkazi wa Itunge “a” na kumsababishia maumivu makali mwilini.
Kamanda Diwani alisema  mbinu iliyotumika ni kuwaruhusu wanafunzi aliokuwa akiwafundisha  kuondoka na kubaki na mhanga kisha kumbaka katika chumba anachotumia kufundishia (darasani).
Aliongeza kuwa  mtuhumiwa  aliwahi kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 gerezani kwa kosa la kubaka na kutoka kwa rufaa na kwamba mhanga amepatiwa matibabu na kuruhusiwa ambapo taratibu zinafanywa ili mtuhumiwa afikishwe mahakamani
MBEYA YETU

Mbunge Nassari haamishiwa Muhimbili kwa matibabu zaidi


MBUNGE wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari amehamishiwa hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu zaidi kutokana na majeraha aliyoyapata kutokana na kushambuliwa na watu wasojulikana katika vurugu zilizotekea wakati wa uchaguzi wa udiwani mjini Arusha hivi karibuni.
Awali Mbunge huyo alilazwa hospitali ya Seriani kisha kuhamishiwa KCMC Moshi kwa matibabu kutokana na kushambuliwa na watu wanaodaiwa wafuasi wa CCM kwenye uchaguzi wa udiwani wilayanmi Monduli.

  DIAMOND PLATINUMZ ASAMBAZA VIDEO YAKE YA UKIMWONA



Na Elizabeth John

MKALI wa muziki wa kizazi kipya nchini, Naseeb Abdul ‘Diamond Platinum’ ameisambaza video ya ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Ukimwona’ ambayo inafanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio.

Akizungumza na Habari Mseto jijini Dar es Salaam, Diamond alisema kazi hiyo ameisambaza juzi katika vituo mbalimbali vya televisheni na kwamba anaamini itafanya vizuri kutokana na ubora wa mazingira aliyotumia kushuti video hiyo.

 “Najua mashabiki wangu wananijua vizuri sijaja kuuza sura mjini, naomba mashabiki wangu wakae mkao wa kula kwajili ya kuzipokea kazi zangu zingine zinazofuata kwani nina mashairi mengi yanasubiri muda tu wa kuingia mtaani,” alisema.

Diamond ni kati ya wasanii ambao wanafanya vizuri katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya huku akitamba na baadhi ya ngoma zake kama Kesho, Mapenzi basi, Ritha na nyinginezo.

EPIQ BSS 2013 YAZINDULIWA DAR

Mkurugenzi Mtendaji wa Benchmark Production Rita Paulsen akisisitiza jambo wakati akiongea na wandishi wabari wakati wa uzinduzi wa shindano la kuimba la Epiq Bongo Star Seach uzinduzi huo uliofanywa na kampuni ya simu za mkononi ya Zantel (katikati)  ni Afisa Biashara mkuu wa Zantel Sajid Khan na kushoto ni Mshindi wa Bss Walter Chilambo wa BSS

Tuesday, June 18, 2013

Hali ya hewa Arusha yarejea kwenye utulivu

MOTO UNAWAKA BAADA YA KUCHOMWA MATAIRI


HALI ya utulivu imeanza kurejea jijini Arusha baada ya hali kuchafuka kwa Jeshi la Polisi kufyatua mabomu ya machozi dhidi ya wafuasi na viongozi wa CHADEMA baada ya kukusanyika kwenye viwanja vya Soweto ili kujua namna watakavyoshiriki mazishi ya watu waliouwawa kwa Bomu siku ya Jumamosi.
Kwa mujibu wa taarifa toka Arusha zinasema kuwa hali imerejea kuwa tulivu baada ya mshikemshike wa Polisi kuwatimua wananchi hao na kuleta kizaazaa cha kutunishiana misuli na kurejea hali ya taharuki jijini humo baada ya hivi karibuni kukumbwa na matukio yaliyosababisha vifo vya watu wasio na hatia.

Msajili wa vyama alaani mlipuko wa bomu Arusha, avinyooshea kidole vyama vya CCM na CHADEMA

Msajili wa Vyama vya Siasa Tanzania, John Tendwa
Na Suleiman Msuya
MSAJILI  wa Vyama vya Siasa nchini John Tendwa amesema ili kuhakikisha kuwa amani inaendelea kudumu ni muhimu kuwepo kwa uvumilivu na kuheshimiana  kati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)  na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Kauli hiyo ameitoa leo Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam ikiwa ni siku chache baada ya kutokea kwa mlifuko wa bomu kwenye mkutano wa kampeni ya udiwani uliokuwa unaendeshwa na CHADEMA katika viwanja vya Soweto mjini Arusha.
Tendwa alisema kwa muda sasa kumekuwepo kwa msuguano mkubwa baina ya vyama hivyo viwili jambo ambalo linaonyesha dalili za kuhatarisha amani ya nchi na wananchi kwa ujumla.
Msajili huyo alisema vyama hivyo vinaonyesha kukosa  uvumilivu na kuheshimiana kwani kwa kipindi hiki kifupi cha kampeni za udiwani viomekuwa na fujo ambazo kila mmoja anamshutumu mwenzake jambo ambalo sio nzuri katika nchi.
Alisema kutokana na tukio hilo viongozi wao wameibuka na kushutumiana ambapo  Katibu Uenezi wa CCM Nape Mnauye alisikika akiwashutumu CHADEMA kuhusikana wakati Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe akisema CCM na Jeshi la Polisi wanahusika.
“Inasikitisha sana kuona watu wanakufa alafu watu wanajitokeza na kuanza kushutumiana kuwa huyu ndiye anahusika mimi nomba wapeleke ushahidi Jeshi la Polisi ili kuweza kusaidia upelelezi,” alisema.
Tendwa alisema katika kuhakikisha kuwa vyama hivyo vinaendelea kuheshimiana na kuvumiliana anatarajia kuita kikao ambacho kitashirkisha ofisi yake, jeshi la polisi na vyama hivyo kwani wanapoelekea ni pabaya.
Alisema iwapo uchaguzi wa Udiwani hali inakuwa hivyo je itakuwakuaje katika uchaguzi wa Serikali za Mitaaa na uchaguzi mkuu watu watarajie nini kwani ni ishara mbaya kwa Taifa ambalo linasifika kwa amani.
Aidha Msajili huyo alipotakiwa kuelezea juu ya ofisi yake kuvifuta vyama hivyo viwili vya CCM na CHADEMA alisema ofisi yake ina mamlaka hayo ila hiyo ni hatua ya mwisho kuchukuliwa iwapo itabidi.
Tendwa alisema uamuzi wa kuvifuta vyama hivyo unaweza kuwa na athari kubwa kwani utahitaji gharama kubwa za kufanyika uchaguzi jambo ambalo sio la kukimbilia.
Alisema ofisi yake inahitaji kukutana na vyama hivyo  kwani ndio njia sahihi ya kufikia muafaka kwa maslahi ya vyama hivyo na wananchi kwa ujumla.
“Ni lazima jamii itakatumbua kuwa maamuzi haya yanahusi CCM ambayo ipo madarakani ambapo matokeo yake ni kuvunja Serikali na kwa CHADEMA ni kuwaondoa wabunge wake hivyo uchaguzi kufanyika tena,”  alisema.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa nchini Peter Mziray amevitaka vyama hivyo kutambua kuwa nchi hii iwapo itaingia vitani wao ndio wahusika wakubwa.
Alisema Baraza hilo linatajia kukutana kwa pamoja likishirikisha vyama vyote vya siasa ambapo watatoka na azimio juu ya hali ilivyo hivi sasa kwani inaonyesha dalili za kupotea kwa amani.
Mziray ambaye ni Rais Mtendaji wa Chama cha African Progressive Party Tanzania (APPT Maendeleo alisema hali inayotoke kwa sasa jeshi la Polisi na vyombo vyote vya usalama vinapaswa kushutumiwa kwani vionyesha kutofanya kazi vizuri.
Mwenyekiti huyo alisema hali hiyo inasikitisha sana kutokana na ukweli kuwa watu wasio na hatia kupoteza maisha jambo ambalo halikubaliki.
“Kwa kweli vyama hivi viwili vimekuwa na matukio mbalimbali ambayo kwa muono wangu nadhani vinahitajika kubadilika kwani hali sio shwari ila vyombo vya usalama pia vina mapungufu yao,” alisema

Klabu Thailand yaja kusaka wachezaji wa kulipwa

Nembo ya klabu ya Thai Port FC
Na Boniface Wambura
KLABU ya Thai Port Football ya Thailand inatafuta wachezaji nchini Tanzania kwa ajili ya kucheza mpira wa miguu nchini humo na katika nchi nyingine barani Ulaya.

Kupitia kwa wakala wake, klabu hiyo imetuma taarifa kupitia Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ikitaka wachezaji wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 28 kwa ajili ya kuwafanyia majaribio ambapo watakaofuzu watacheza nchini humo na katika klabu nyingine za Ulaya ambazo wana ushirikiano nazo.

Wachezaji wenye nia ya kufanya majaribio wanatakiwa kutuma taarifa za wasifu wao (CV) kwa klabu hiyo kwa njia ya emaili, wawe na pasi ya kusafiria pamoja na pasi ya mchezaji (player passport).

Wakala atapitia vitu hivyo, na kwa wachezaji atakaowahitaji atawatumia tiketi za ndege na viza kwa ajili ya kwenda kufanya majaribio nchini humo, na watakaofanikiwa kabla ya kusaini nao mikataba watawasiliana na klabu zao nchini (kwa wale wenye klabu).

Polisi wafafanua sababu ya kulipua mabomu ya machozi leo Arusha


JESHI la Polisi limekipiga marufuku chama cha demokrasia na maendelo(CHADEMA)kufanya shughuli zozote za kuaga miili ya marehemu kwenye viwanja vya Soweto kwani zoezi la uchunguzi bado linaendelea kwenye viwanja hivyo .


Akizungumza ofisini kwake kamanda wa polisi mkoani Arusha, Liberatus Sabas amesema kutokana na uchunguzi unaoendelea wa tukio la bomu kwenye viwanja hivyo imeonelea kuwa si busara kuweka mkusanyiko wa watu kwani kutaharibu upelelezi.


Kamanda Sabas amedai  kuwa  jeshi la polisi  liliwataka viongozi wa chama hicho kuwaeleza wafuasi wao mahali sahihi watakapoweza kufanyia shughuli hiyo lakini si kwenye viwanja hivyo.

Hali kwenye viwanja hivyo imekuwa ya pilika pilika tangu juzi kwa wafuasi wa chama hicho kujikusanya tokea asubuhi hadi jioni kwa madai ya kuomboleza ..

Hata hivyo viongozi wa chama cha demokrasia na maendeleo walikaidi agizo hilo na  kuanza  kujikusanya uwanjani hapo pamoja na wafuasi wa CHADEMA, hali iliyoleta  mvutano kati ya viongozi  wa jeshi la polisi na  wafuasi hao.
Wakati mabishano hayo yakiendelea, Askari Polisi mmoja  alijichanganya na kuingia katikati ya wafuasi wa Chadema pembeni mwa uwanja huo ambao walikua wanasubiri kujua utaratibu wa kuaga miili ya Marehemu waliolipuliwa na bomu June 15 2013.

Baada ya hapo, wafuasi hao hawakupenda kitendo cha Polisi kujichanganya nao hivyo ikazuka ugomvi huku wakitaka atoke, baada ya dakika kadhaa  mabumu yalianza kusikika.

Baadhi ya viongozi wa juu wa chama hicho waliokuwepo uwanjani haponi mbunge wa jimbo la ubungo John Mnyika,Ezekia Wenje,Tundu lissu, Halima Mdee.

TFF yapongeza mashabiki kuiunga mkono Stars

Stars wakishangilia moja ya mabao yao dhidi ya Ivory Coast

Na Boniface Wambura

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linawashukuru washabiki kwa kujitokeza kwa wingi kwenye mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kati ya Taifa Stars na Ivory Coast (The Elephants) iliyochezwa juzi (Jumapili) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mwitikio wa washabiki katika mechi hiyo ilikuwa ni moja ya chachu ya kiwango kilichoonyeshwa na Taifa Stars, kwani walishangilia mwanzo hadi mwisho licha ya kupoteza kwa mabao 4-2.

Ni matarajio utakuwepo mwitikio kama huo huo katika mechi ijayo ya Taifa Stars ya michuano ya Afrika kwa Wachezaji wa Ligi za Nyumbani (CHAN) dhidi ya Uganda (The Cranes) itakayochezwa Dar es Salaam kati ya Julai 12-14 mwaka huu. Stars itaingia tena kambini Julai 4 mwaka huu kujiandaa kwa mechi hiyo.

Mbongo kukipiga Yemen, TFF yatoa ITC yake


Na Boniface Wambura
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa mchezaji Mtanzania Gossage Mtumwa ili aweze kucheza mpira nchini Yemen.

Mtumwa ambaye anatoka katika kituo cha kukuza na kuendeleza vipaji cha Rollingstone cha Arusha aliombewa hati hiyo na Chama cha Mpira wa Miguu cha Yemen (YFA) kwa ajili ya kucheza nchini humo.

TFF inamtakia kila la kheri Mtumwa katika safari yake ya Yemen, na ni matarajio yetu kuwa atakuwa balozi mzuri wa Tanzania nchini humo ili wachezaji wengine wa Tanzania nao wapate fursa ya kucheza mpira wa miguu nchini Yemen.


Kamishna Alferd Rwiza kuhudhuria Semina CAF

Na Boniface Wambura
KAMISHNA Alfred Kishongole Rwiza ameteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kuhudhuria semina ya makamishna itakayofanyika kuanzia Julai 6-7 mwaka huu katika makao makuu ya shirikisho hilo jijini Cairo, Misri.

Semina hiyo inashirikisha baadhi ya makamishna wa CAF walioko kwenye orodha ya makamishna ya shirikisho hilo kwa mwaka 2012-2014.

Rwiza ni mmoja wa makamishna wa CAF kutoka Tanzania, na mechi ya mwisho kusimamia ilikuwa ya Kombe la Shirikisho iliyochezwa Mei mwaka huu nchini  Msumbiji.

CAF tayari imeshamtumia tiketi Rwiza, na anatarajia kuondoka nchini Julai 4 mwaka huu kwenda Cairo kwa ndege ya EgyptAir.

Mbunge CHADEMA, Mr Sugu atapata ajali akielekea Arusha

Mbuinge wa Mbeya Mjini-CHADEMA, Mhe. Joseph Mbilinyi 'Sugu'
Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi amepata ajali hivi punde katika eneo la kasheki wilayani Hanan'g akielekea Arusha mjini.

Joseph Mbilinyi maarufu Sugu alikuwa akielekea Arusha mjini kuungana na wabunge wengine ktk shughuli ya kuaga marehemu
waliolipukiwa na bomu kwenye mkutano wa Chadema, mwishoni mwa wiki iliyopita.
Katika ajali hiyo hakuna mtu yoyote amejeruhiwa, Mbunge huyo yuko salama, gari la Sugu limeharibiwa vibaya baada ya kugongana na basi la abiria.

Kichanga chatafunwa na mbwa baada ya kutupwa kichakani

mbwa kama huyu amemtafuna kitoto kichanga
MTOTO mchanga ameliwa na mbwa na  kubakishwa mguu, baada ya mtu asiyejulikana kukitelekeza kichakani katika eneo la Magole, mtaa wa Kivule, Manispaa ya Ilala, jijini Dar es Salaam.Tukio hilo la kusikitisha limebainika baada ya mbwa huyo kukibeba kiungo hicho kutoka kilipokuwa na kukifikisha nyumbani anakofugwa majira ya sita mchana juzi.
Mwenye mbwa huyo aliyejitambulisha kwa jina la Maria John, aliiambia NIPASHE kuwa, kabla ya kupelekwa mguu huo, jana yake mbwa huyo alikwenda na utumbo ambao hata hivyo hakuna aliyekuwa  na hofu nao, kwani walidhani ni wa kuku.
 
“Niliona ni kitu cha kawaida tu, mbwa hutembelea maeneo mbalimbali labda ameokota mzoga wa kuku, lakini leo (juzi) nilipoona mguu nilistaajabu na kufahamu kuwa ni kiungo cha binadamu nilitoa taarifa kwa majirani na kupata msaada,” alisema.
 
Alisema lengo la kutoa taarifa kwa majirani zake ni ili waweze kujadiliana na  kutamfuta aliyefanya kitendo hicho cha kikatili kisha baadaye kutoa taarifa kwa mjumbe wa mtaa huo.
 
Mmoja wa majirani waliokusanyika kushuhudia tukio hilo ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini, alisema hajawahi kushuhudia tukio kama hilo.
 
“Ni tukio la kushangaza na kusikitisha sana kwa mtu kukatisha maisha ya kiumbe kisicho na hatia,kwani huwezi kujua mungu alimpangia nini duniani, hivyo kwa kweli kama mama najisikia uchungu sana,” alisema.
 
Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa eneo hilo, Grace Martin, alisema alipigiwa simu na mdogo wake kuwa, mbwa ameokota kiungo cha mtoto na  kutakiwa kurudi mtaani hapo haraka.
 
“Nilipofika nilihakikisha kuwa kweli ni mguu wa mtoto, niliamua kumpigia simu Mwenyekiti wa Mtaa kwa ajili ya msaada,”alisema.
 
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kivule,Joseph Gassaya alisema yeye alipojulishwa alitoa taarifa kwa Jeshi la Polisi kituo cha Stakishari Ukonga nao baada ya muda mfupi walifika eneo la tukio.
 
Alisema askari walitoa amri ya kukizika kiungo hicho katika eneo hilo, huku Jeshi la Polisi likiendelea na upelelezi wa kumsaka mama aliyefanya ukatili huo ili afikishwe kwenye vyombo vya sheria.
 
Chanzo:Nipashe

Monday, June 17, 2013

KONYAGI YAWAPIGA MSASA WABUNGE KUHUSU BIASHARA VIROBA


 Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distilleries Limited (TDL), David Mgwassa, akionesha kinywaji cha Afrika Kusini kilichofungwa kwenye viroba kama ambavyo Konyagi inafanya hapa nchini.Vinywaji kama hivyo vipo karibu nchi nyingi Ulimwenguni.

 Meneja wa Masoko wa Konyagi, Joseph Chibehe akielezea jinsi vinywaji vyao vinavyochangia mapato ta serikali
 Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kilimo,Maji na Mifugo, Said Nkumba akichangia mada hiyo kwa kuviasa baadhi ya vyombo vya habari kuacha kuandika habari za kudidimiza viwanda vya haba nchini. Kulia ni Idd Azzan Mbunge wa Kinondoni na Dunstan Kitandula ambaye ni Makamu Mwenyekiti was  Kamati ya Bunge ya Uchumi, Viwanda na Biashara.
                               Bidhaa mbalimbali zikiwa zimfungwa kwenye viroba
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distilleries Limited (TDL), David Mgwassa () akifafanua jambo katika semina ya wajumbe wa Kamati mbili za Bunge za Uchumi,Viwanda na Biashara  pamoja na Kilimo,Maji na Mifugo kuhusu baadhi ya vyombo vya habari vyenye uhusiano na nchi jirani vinavyotumika kupiga vita viwanda vya ndani kikiwemo cha Konyagi. Semina hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.
 Naibu Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Amos Makala, akichangia mada katika semina hiyo. Kushoto ni Naibu Waziri wa TAMISEMI, Kassim Majaliwa na Said Nkumba.
 Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uchumi, Viwanda na Biashara, Dunstan Kitandula akichangia mada hiyo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distilleries Limited (TDL), David Mgwassa (kushoto) akimkabidhi jezi Idd Azzan kwa ajili ya timu ya Bunge iliyocheza na timu ya Konyagi kwenye Uwanja wa Jamhuri, mjini Dodoma Jumamosi
 Mgwassa akikabidhi jezi ya timu ya Konyagi kwa Idd Azzan tayari kwa mtanange na timu ya Bunge
 Meneja Masoko wa Konyagi, Joseph Chibehe (kushoto) akimkabidhi W. Zuberi  msaada wa vyerehani, ambavyo alivipokea kwa niaba ya BNaibu Spika wa Bunge, Job Ndugai
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utawala Bora, George Mkuchika, akisalimiana na timu ya Bunge muda mfupi kabla ya pambano lao na timu ya Konyagi, kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

 George Mkuchika akisalimiana na wachezaji wa timu ya Konyagi
 Wachezaji wa timu ya Bunge wakisalimiana na wachezaji wa Konyagi
 Kikosi cha timu ya Bunge kilichochuana na Konyagi
Kikosi cha timu ya Konyagi kilichomenyana na Timu ya Bunge