STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, May 13, 2014

Shinji Kagawa aitwa kikosi cha Japan WC2014

WACHEZAJI nyota Keisuke Honda na Shinji Kagawa ni miongoni mwa wachezaji 23 walioteuliwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Japan kitakachoshiriki michuano ya Kombe la Dunia mwezi ujao. Kocha Alberto Zaccheroni ambaye amekuwa kocha wa Japan toka mwaka 2010 amechagua wachezaji 12 wanaocheza soka barani Ulaya na 11 wanaocheza katika Ligi Kuu ya nchi hiyo maarufu kama J League. Honda anayecheza klabu ya AC Milan na Kagawa anayecheza Manchester United wanategemewa kwa kiasi kikubwa na nchi yao katika kuhakikisha wanavuka hatua ya makundi katika kundi C ambapo wamepangwa sambamba na Ivory Coast, Ugiriki na Colombia. Japan kwa kipindi kirefu imeshindwa kuwa na washambuliaji wa kutegemewa na Zaccheroni anatarajia kuwategemea Honda na Kagawa katika kutengeneza nafasi na kufunga mabao mengoi ya timu hiyo katika michuano hiyo.

Kikosi Kamili cha Japan:
Makipa: Shuichi Gonda (Tokyo), Eiji Kawashima (Standard Liege), Shusaku Nishikawa (Urawa Reds)

Mabeki: Masahiko Inoha (Jubilo Iwata), Yasuyuki Konno (Gamba Osaka), Masato Morishige (Tokyo), Yuto Nagatomo (Inter), Gotoku Sakai (Stuttgart), Hiroki Sakai (Hannover), Atsuto Uchida (Schalke), Maya Yoshida (Southampton)

Viungo: Toshihiro Aoyama (Sanfrecce Hiroshima), Yasuhito Endo (Gamba Osaka), Makoto Hasebe (Nuremberg), Keisuke Honda (Milan), Shinji Kagawa (Manchester United), Yoichiro Kakitani (Cerezo Osaka), Hiroshi Kiyotake (Nuremberg), Manabu Saito (Yokohama F Marinos), Hotaru Yamaguchi (Cerezo Osaka)

Washambuliaji: Shinji Okazaki (Mainz), Yoshito Okubo (Kawasaki Frontale), Yuya Osako (1860 Munich)

Zahoro Pazi hajui lolote Simba

WINGA machachari wa klabu ya Simba, Zahoro Pazi, amesema hana taarifa zozote za kuwa miongoni mwa wachezaji wanaotakiwa kuachwa ndani ya timu hiyo kwa msimu ujao.
Aidha mchezaji huyo ambaye ni mtoto wa mmoja wa makocha wa timu hiyo, Idd Pazi 'Father' amesema yeye bado ana mkataba na klabu hiyo na kama itakuwa kweli hatakiwi Msimbazi hana neno.
Akizungumza na MICHARAZO, Pazi alisema amekuwa akisoma na kusikia taarifa dhidi yake zikitolewa au kunukuliwa kutoka kwa kocha wake, Zdrakov Logarusic, lakini hajafahamishwa rasmi na viongozi.
"Sina taarifa yoyote rasmi ya kutaka kutemwa Simba, kwa vile nina mkataba na klabu yangu naendelea kujitambua kama mchezaji wa Simba nikiendelea kujipanga kwa msimu ujao," alisema.
Nyota huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar, Azam na JKT Ruvu alisema hata kama Simba itaamua kuuvunja mkataba wao, hatakuwa na neno zaidi ya kutuliza akili yake ili kujipanga upya kuendeleza kipaji chake.
Pazi aliyesajiliwa na Simba msimu ulioisha hivi karibuni alikuwa akipata wakati mgumu mbele ya Logarusic, japo katika mechi za lala salama za ligi hiyo alikuwa akipewa nafasi na kufunga mabao.
Hivi karibuni iliripotiwa kuwa Pazi na baadhi ya wachezaji zaidi ya 10 wapo kwenye mipango ya kutemwa ndani ya Simba kutokana na pendekezo la kocha Logarusic lililopo katika ripoti yake kwa viongozi.

Kikosi cha England hiki hapa, wapo Jack Wilshere, Cole atemwa

KOCHA wa timu ya taifa ya Uingereza, Roy Hodgson ametua kikosi cha wachezaji 23 atakaowatumia kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia akiwajumuisha nyota wawili wa Arsenal Jack Wilshere na Alex Oxlade-Chamberlain pamoja na kuwa majeruhi. 
Wilshere alirejea uwanjani katika mchezo wa mwisho dhidi ya Norwich jana baada ya kukaa nje toka Machi baada ya kuumia kifundi cha mguu wa kulia wakati akiwa katika majukumu ya kimataifa. 
Oxlade Chamberlain yeye alikosa nusu ya kwanza ya msimu kwa kuuguza goti na bado kuna hati hati Arsenal wakamkosa katika mchezo fainali ya Kombe la FA kutokana na majeraha kigimbi. 
Pamoja na hayo meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amesema Hodgson hapaswi kujali sana afya za wachezaji hao kwani bado kuna mwezi mmoja kabla ya Kombe la Dunia hivyo wana muda wa kutosha wa kupona kabisa. 
Kwa upande mwingine chipukizi kama Luke Shaw, Ross Barkley na Raheem Sterling wote wamepata nafasi ya kuwepo katika kikosi cha Hodgson.

Kikosi kamili cha Uingereza ni:
Makipa: Joe Hart (Manchester City), Fraser Forster (Celtic), Ben Foster (West Brom)

Mabeki: Glen Johnson (Liverpool), Phil Jones (Manchster United), Phil Jagielka (Everton), Gary Cahill (Chelsea), Chris Smalling (Manchester United), Luke Shaw (Southampton), Leighton Baines (Everton)

Viungo: Steven Gerrard (Liverpool), Frank Lampard (Chelsea), Jordan Henderson (Liverpool), Ross Barkley (Everton), Jack Wilshere (Arsenal), Alex Oxlade-Chamberlain (Arsenal), Raheem Sterling (Liverpool), Adam Lallana (Southampton), James Milner (Manchester City)

Washambuliaji: Daniel Sturridge (Liverpool), Wayne Rooney (Manchester United), Danny Welbeck (Manchester United), Rickie Lambert (Southampton)

Wachezaji za ziada :
John Ruddy (Norwich City), John Stones (Everton), Jon Flanagan (Liverpool), Tom Cleverley (Manchester United), Michael Carrick (Manchester United), Jermain Defoe (Toronto), Andy Carroll (West Ham)

Yanga yataka mzizi wa fitina kwa Mbuyu Twite wamsainisha upya

Mbuyu Twite akiwa na Bin Kleb (picha na maktaba)



Mlinzi kiraka wa timu ya Young Africans Mbuyu Junior Twite leo ameongeza mkataba mpya wa mwaka mmoja kuendelea kuitumikia klabu ya Yanga baada ya kufikia makubaliano na uongozi na kupata majibu ya Shirikisho la Soka nchini TFF juu ya idadi ya wachezaji wa kimataifa kwa msimu ujao 2014/2015.
Usajili wa Twite umefanyika leo makao makuu ya klabu ya Yanga chini ya Katibu Mkuu Bw Beno Njovu ambapo mchezaji amesema ataendelea kujitolea kwa uwezo wake kuisaidia timu yake ya Yanga.
Katibu Mkuu wa Young Africans Beno Njovu amesema wameingia mkataba wa mwaka mmoja na Twite baada ya pande zote kukubaliana, hivyo kuanzia sasa Twite ataendelea kuwa mchezaji wetu kwa msimu ujao wa 2014/2015 na kusisitiza kuwa usajili ndio umeanza sasa.
Akiongea mara baada ya kuweka sahihi kwenye mkataba wake mpya Twite amesema anajisikia furaha kuendelea kuwa mchezaji wa Yanga, kwani anafurahia maisha ya Jangwani, wapenzi, washabiki, viongozi na wachezaji ni marafiki/ndugu ndani na nje ya Uwanja.
Aidha Twite amesema Yanga ni miongoni mwa timu kubwa barani Afrika, zenye washabiki na waachama wengi hivyo wangu ni fahari kuendelea kuitumika timu hii ambayo tangu kujiunga nayo nimekua nikijtoa kwa moyo wangu wote kusaka mafanikio. 
Mbuyu Twite amekua ni mchezaji wa Young Africans kwa kipindi cha miaka miwili tangu Julai 2012 alposajiliwa huku katika kipindi hicho chote akiwa ni mchezaji wa kikosi cha kwanza ambapo msimu uliopita aliweza kuisadia timu yake kutwaa Ubingwa wa Lig Kuu ya Vodacom na msimu huu kushika nafasi ya pili.
YOUNG AFRICANS

Friday, May 9, 2014

HAWA NDIYO WAIGIZAJI WAREMBO ZAIDI BONGO MOVIE


Irene Uwoya
Kiwanda cha filamu Tanzania kimezalisha waigizaji wengi wenye majina makubwa sasa. ifatayo ni orodha ya waigizaji 10 wakike wenye mvuto na kuvutia zaidi kati ya wengi waliopo.

Filamu alizocheza
Question Mark, Apple ,Safari, Zawadi Yangu, Innocent Case, Nyota Yangu, Last Card, Doa la Ndoa, Ngumi ya Maria, Chupa Nyeusi, Kiapo, Eagle Eyes, Diversion of Love, Fair Decision, Pretty Girl, Damu Moja, Shakira, Yolanda, Tanzanite

Elizabeth Lulu Michael
Filamu alizocheza
Oxygen, Elizabeth Michael,House Boy, Ripple of Tears, Confusion,Ritazo, Family Disaster, Woman with Principal, Foolish Age nk

Wema Sepetu
Filamu alizocheza
House Boy, Crazy Tenant, Basilisa, The Diary, Lerato, Tafrani, White Maria, Sakata, Family Tears, Madame

Skyner Ally
Filamu alizocheza
What is It, Why I Did Love, I Hate My Birthday’, Kizungumkuti’, Unpredictable, Shahada

 
Yobnesh Yusuph aka Batuli
Filamu alizocheza
Kazi Yangu, Waves of Sorrow, Fungate,Get Out, The Glory of Ramadhan, My Fiance,Ripple of Tears, Machozi

Jacky Wolper
Filamu alizocheza
After Death, Impossible,My Princess,Tikisa, Mahaba Niue, Pain for Pain P.F.P, Think Before,

Identity Card, Babylon, Before Wedding,I am Not Your Brother,Curse of Marriage, Ulimi, Mr.Nobody, Pusi na Paku, Lupepo Village, Hukumu ya Mande, Mtekaji, Chocolate, End of Evil, The Diplomat, My Intention, Time After Time, Chaguo Langu, Siri ya Moyo Wangu, God is Great, Saa4, Swadakta, Gaitan, The Impact,Mens Day Out, Dunia Nyingine, Determination, Aching Heart, Shoga Yangu, Mafisadi wa Mapenzi,All About Love, Eagle Eyes, Wrong Decision, Mtegoni, Fake Love, Life 2 Life, Mtumwa, Secretary, Last Minutes, Jozani.

 
 Nargis Mohamed
Filamu alizocheza
Magic House, Yellow Banana, Woman with Principal nk


Irene Paul
Filamu alizocheza
Love & Power, Kibajaji, Kalunde, Fikra Zangu, Penzi la Giza, Love Me or Love Me Not, I Hate My Birthday, The Shell, Handsome wa Kijiji


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgwsHv5OD53NQrNgvCQl2mGbOg0fGdrFS9K1i994pRdbT5bVCWdcMaCc57PrTxHTpk9hSgCFOYToo6JzW9Lu1PcS2tIEzsZHz89cWPj71R0AuDmIGuDk3nf_4ua9a0TIwjc08EBqrTgqbQ/s1600/P1010017.JPG               Shamsa Ford
Filamu alizocheza
Zawadi Yangu, Babylon, Get Out, Dont Try, I Think I hate My Wife, Loreen, Zawadi ya Birthday, Red Mzula, Mafisadi wa Mapenzi, Crazy Love, Saturday Morning



Salma Jabu aka Nisha
Movie alizocheza
Tikisa, Subiri Mama, Matilda, I am Lost, Pusi na Paku, Mchana wa Kiza,Kashfa Macho Yangu,Red Cross
 http://api.ning.com/files/xLH1QA7JYqCMGrVhlG4X5OjJKgpgXl04KJV1Rwlg38jbHQjHvCNi5OaaFW2tVeu2fRyYekZwet8tmh3e5T3GCo7z60VDBbje/AuntEzekiel2.jpg
                               Aunt Ezekiel
Filamu alizocheza
Pumba, Jungu la Urithi, Eyes on Me, Radio Presenter,Machozi Yangu, The Beauty Fools, Kijogoo,Siku za Maajabu, Best Losers, Alice & Janel, I Hate My Birthday, Lost Souls,Mens Day Out, Shoga Yangu, Lonely Heart, The Mask, Green Light, Sound of Death,Black Sunday,Taste of Love, Endless Love, Same Girl, The Village Pastor, Wicked Love, The Cold Wind

http://www.eatv.tv/media/picture/large/shilole.jpg Shilole
Filamu alizocheza
Chungu ya Nafsi, Barmaid, Macho Yangu, Kisasi cha Jessica, Mafisadi wa Mapenzi, Talaka Yangu


http://www.bongocelebrity.com/wp-content/uploads/2013/07/tatu.jpg                         Kajala Masanja
Filamu alizocheza
House Girl & Boy, Dhuluma, Shortcut, Basilisa, Devil Kingdom nk


http://api.ning.com/files/4jXfPWfoQHT2w6JX*yjkRMYviPQtx53F88QBQi7wErChIiWht9NQ86Za3dBhRKar08hNqT4OmMT0ZUkGGRZDHRlfuiMolUt4/RoseNdauka2.jpg Rose Ndauka
Filamu alizocheza
Waiting Soul, One Night, Fall in Love, Waves of Sorrow,Malaika,The Same Script, The Specialist, Real Promise, Swahiba,Kwa Heshima Ya Penzi, Love Me or Love Me Not,Jessica,Because of You, Ruben and Angel, The Diary, Solemba,Bad Girl, Cut Off, Sound of Death, Why Did I Love, Mahabuba

 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiXNOtf3uwUqr1vdmB-od-pIOAWQeVgpgxeWb8ldJx2POgrOYstvrIVNvR5-CfHFochNQelG9GjeUClNd4_-rF0d1XMlNwJ_QZplKKVjIOE-bmmRmjSa2LVvUjXNRP1mYfY4KSehN1l7Tvq/s1600/warda4.jpg

Warda Walid
Filamu alizocheza
Triple L, Nipende Monalisa, The Lost Adam



Monalisa

Thursday, May 8, 2014

Mtanzania mwingine adakwa na 'Unga' Kenya

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiR-x2JlYi-ME1lAl7jUW45J716UnmxnN8WsOfegN9uP6qvMV4KtGzI7jM1XI2MSs7NO-TZu6netj0h9WyxrA0gGDLL8gOBxxjoXB7-IKGAVWAxgYcak7eG3R2X_9MqLqw0zOwxdthyphenhyphenN8T8/s640/Drugs(3).jpgMWANAMME mmoja Mtanzania amekamwata katika uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta Nairobi Kenya akiwa amebeba dawa za kulevya akiwa njiani kuelekea Antananarivo ambapo mzigo huo ulitokea Tanga kisha ukapita Mombasa na baadae kwa ndege mpaka Nairobi.
Mzigo wenyewe ni wa cocaine na Heroin ambazo zote zina thamani ya zaidi ya shilingi milioni 24 za Kitanzania na dawa hizo alikua  ameziingiza katika njia ya haja kubwa.
Mkuu wa kitengo cha CID katika uwanja huo Joseph Ngisa amesema mshukiwa alikamatwa JKIA na akawekwa kwenye chumba cha uchunguzi na baadae akatoa tembe za cocain na tembe za Heroin na tayari ameshapelekwa Mahakamani.

Mwezi March mwaka huu watanzania wanne walikamatwa katika uwanja huohuo walipopatikana na heroin yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 75 za Kitanzania na wote walifikishwa mahakamani na kukiri kosa.
Wanawake watatu na mwanaume mmoja kila mmoja akishtakiwa kando kwa kosa la kusafirisha dawa za kulevya na walikua wameingia Kenya kupitia Namanga na walikamtwa wakiwa njiani kuelekea Hong Kong.
Kuanzia March 2014 mpaka leo hii May ni jumla ya Watanzania watano wamekamatwa kwenye kiwanja cha ndege Nairobi wakiwa kwenye pilika za kusafirisha dawa za kulevya kwenda kwenye mataifa mengine.

Real Madrid bado watesa kwa Utajiri Duniani

http://i.dailymail.co.uk/i/pix/2013/02/11/article-2277207-17848A69000005DC-464_964x505.jpgKLABU ya Real Madrid bado imeendelea kung'ang'ania kileleni katika orodha ya vilabu vyenye thamani zaidi duniani(Most Valuable Football Clubs) kwa mujibu wa jarida la Forbes.
Katika orodha hiyo klabu ya Manchester United imeendelea kuwa juu ya vilabu vya England licha ya kufanya vibaya msimu huu.
Manchester United imeshuka thamani kwa 11% tangu ilipomuajiri David Moyes kama kocha wake mkuu.

Chini ya Moyes Manchester United imepata hasara ya £181.5m, huku majirani zao Manchester City wao wamepanda thamani kwa 25%
Orodha kamili ya Klabu hizo Tajiri Duniani ni;

Yanga waitana kuijadili katiba yao



UONGOZI wa klabu ya Young Africans Sports Club umeitisha mkutano mkuu wa wanachama wa mabadiliko ya Katiba ili wanachama waweze kutoa maamuzi kwenye baadhi ya vipengele vilivyoongezwa kabla ya kuelekea kwenye mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa viongozi.
Akiongea na waandishi wa habari makao makuu mitaa ya Twiga/Jangwani, Katibu Mkuu wa Young Africans Bw Beno Njovu amesema wamefikia kuitisha mkutano huo wa mabadiliko ya Katiba ili wanachama wapate fursa ya kupitisha baadhi ya vipengele kabla ya kuelekea kwenye uchaguzi mkuu.
“Tumekua na mawasiliano na TFF juu ya kuongezwa baadhi ya vipengele kwenye Katiba yetu kabla ya kufanya uchaguzi mkuu wa viongozi, baada ya hapo ni nafasi kwa wanachama wa Yanga sasa kukutana na kuweza kupitisha hivyo vipengele vitakavyoongezwa kwenye Katiba Mpya” alsiema Beno.
Aidha Beno amesema wanachama wakishapitisha/kukubaliana juu ya hivyo vipengele ndipo uoungozi utawasilisha mapendekezo hayo kwa TFF ambayo ikishayabariki, yatapelekewa kwa Msajili nae akiyapitisha ndipo itakua tayari ni Katiba halali ambayo itatumika kwwenye uchaguzi mkuu.
“Nawaomba wanachama wa Yanga wajitokeze kwa wingi kwenye mkutano wa mabadiliko juni mosi 2014  ili waweze kupitisha hivyo vipengele ambavyo vitapelekea kuwa na Katiba Mpya itakayotumika kwa  shughuli za kila siku za klabu ya Yanga SC” aliongea Beno. 
Eneo na Ukumbi utakapofanyika mkutano huo Juni Mosi 2014 utatangazwa hivi karibuni mara baada ya taratibu zote kukamilika.
CHANZO: TOVUTI YA YANGA

Yanga, TPB wapo kisasa zaidi kidigitali

Makamu Mwenyekiti wa kalbu ya Yanga SC Bw Clement Sanga (katikati) akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya Benki ya Posta, kulia ni mkurugenzi masoko wa Benki ya Posta Bw. Deo Kwiyukwa
Klabu ya Young Africans imeeingia makubaliano na Benki ya Posta nchini juu ya mabadiliko ya utengenezaji wa kadi za wanachama kutoka kwenye mfumo wa zamani (analogy) kwenda kwenye mfumo mpya wa kisasa (digital) ambapo sasa wanachama wake watakua wakitumia kadi zenye mfumo wa ATM.
Mkurugenzi Masoko wa Benki ya Posta  nchini Bw. Deo Kwiyukwa amesema wamefikia makubaliano hayo baada ya kukaa na viongozi na kuona njia hiyo itaisaidia klabu kuongeza mapatao kwani wigo wake wa kuandikisha wanachama utakua ni mkubwa kwa nchi nzima na kwa muda mfupi.
“Badala ya wanachama kuja Dar es salaam makao makuu kujaza fomu za uanachama watakua wanaweza kufanya hivyo popote walipo kwa kwenda ofisi za Benki ya Posta na kujaza fomu hizo na baadae kupewa kadi ya uanachama” alisema Deo. 
Gharama za kujiunga na uanchama zitabakia zile zile Tshs 15,000/=, na ada ya mwaka elfu Tshs 12,000/= ambapo mwanachama wa Yanga atapata kadi ya TPB yenye logo ya timu yake ambayo pia ataitumia kwenye shughuli za kibenkI kwa huduma ya kuweka na kutoa fedha.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga Clement Sanga amesema anaishukuru Benki ya Posta kwa kuweza kufikia makubalianao hayo, kwa kutumia mfumo huu wa kisasa tutaweza kujua idadi ya wachama wetu walio hai kwa wepesi zaidi na taarifa zetu zitaweza  kuwafikia wanachama kwa uharaka zaidi.
Uzinduzi rasmi wa kadi mpaya za uanachama utafanyika tarehe 16.05.2014 kwenye hoteli ya Hyatt Kempsinki eneo la Posta (zamani Kilimanjaro Hotel) na mara baada ya uzinduzi moja kwa moja zoezi la kuhamisha wanachama kutoka kwenye mfumo wa analogy kwenda digital utaanza.
CHANZO: TOVUTI YA YANGA

Kumekucha uchaguzi Simba

http://ptblog.pesatimes.com/wp-content/uploads/2014/05/ndumbaro-300x2531.jpg
WANACHAMA wa klabu ya soka ya Simba wataanza kuchukua fomu za kuwania uongozi wa klabu hiyo katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Juni 29.
Kwa mujibu wa mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa klabu hiyo Damas Ndumbaro fomu zitatolewa kuanza kesho kuelekea kwenye kinyang'anyiro hicho cha uchaguzi unaokuja baada ya uongozi wa akina Ismail Aden Rage kumaliza muda wao kesho.

FIFA yaanika orodha mpya ya viwango duniani

http://www.dailyvedas.com/wp-content/uploads/2014/04/Team.jpgWAKATI Brazil ikipanda kwa nafasi mbili katika orodha ya viwango vya soka duniani hadi kuingia kwenye Top 4, Tanzania yenyewe imeendelea kung'ang'ania katika nafasi ya 122 duniani.
 Brazil wenyeji wa michuano ya Fainali za Kombe la Dunia za mwaka huu, imezipiku nchi za Colombia na Uruguay waliokuwa wamewatangulia katika mwezi uliopita ikiwa nyuma ya Hispania inayooendelea kuongoza orodha ya FIFA iliyotangazwa leo.
Mbali na Hispania, nchi nyingine zilizoitangulia Brazil ni Ujerumani wanaoshika nafasi ya pili kama orodha ya Aprili na Ureno kadhalika wakiwa nafasi ya tatu.
Katika orodha ya 20 Bora, nyuma ya Brazil kuna Colombia, Uruguay, Argentina, Uswiss, Italiaa, Ugiriki, England, Ubelgiji, Chile, Marekani, Uholoanzi, Ufaransa, Ukraine, Russia, Mexico na Croatia iliyofunga ndimba.
Kwa orodha ya Afrika Ivory Coast imeendelea kuongoza orodha ikiwa katika nafasi ya 21 duniani ikifuatiwa na Misri wanaokamata nafasi ya 24, Algeria (25), Ghana (38), Cape Verde (42), Nigeria (44), Tunisia (49), Cameroon (50), Guinea (51) na Mali (59) waliofunga 10 Bora ya Afrika.
Ukanda wa CECAFA kama kawaida Uganda wameendelea kutisha wakishinda nafasi ya 18 Afrika na 86 Duniani, ikifuatiwa na  Ethiopia wanaokamata nafasi ya 101 Duniani na 27 Afrika.
Nyingine zinazozifuata timu hizo ndani ya CECAFA ni Kenya, Sudan, Tanzania, Burundi, Rwanda, Eritrea, Sudan Kusini, Somalia na Djibout inayoburuza mkia.

Hiki ndicho kikosi cha timu ya Ujerumani

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEibSP_Yg7CYyjdkHBV1ejPgbs7Bwfb81J1wLzQfBJrScwYqEj7mtWCc6wRXIWut4Ls_dd3I2MJM49ksFvcyOJZ-bQ18cGvhgJEf7NbxuRm8xDt7Fod8xS0VJKkv7m7IOZHJGV1JoIMiD6sf/s400/Germany+National+Football+Team+Fifa+World+Cup+2014+6.png
SIKU moja baada ya Brazil kutangaza kikosi chao cha ushiriki wa Fainali za Kombe la Dunia, Ujerumani nao wametengaza leo kikosi chake, huku klabu ya Arsenal ikifanikiwa kuwatoa wachezaji watatu akiwamo Kiungo Mesut Ozil.
Wengine walioteuliwa katika kikosi hicho kwa ajili ya Fainali za Dunia zitakazofanyika mwezi ujao nchini Mshambuliaji wa Chelsea, Andre Schurrle pia ameteuliwa katika kikosi hicho kilichotangazwa na kocha wa timu hiyo Joachim Low.
Kikosi kamili cha Ujerumani ni;
 Makipa: Manuel Neuer (Bayern Munich), Roman Weidenfeller (Borussia Dortmund) na Ron-Robert Zieler (Hannover)

Mabeki: Erik Durm (Borussia Dortmund), Jerome Boateng (Bayern Munich), Kevin Grosskreutz (Borussia Dortmund), Benedikt Howedes (Schalke), Mats Hummels (Borussia Dortmund), Marcell Jansen (Hamburg), Philipp Lahm (Bayern Munich), Per Mertesacker (Arsenal), Shkodran Mustafi (Sampdoria) na Marcel Schmelzer (Borussia Dortmund).
 
Viungo: Lars Bender (Bayer Leverkusen), Julian Draxler (Schalke), Matthias Ginter (Freiburg), Leon Goretzka (Schalke), Mario Gotze (Bayern Munich), Andre Hahn (Augsburg), Sami Khedira (Real Madrid), Toni Kroos (Bayern Munich), Max Meyer (Schalke), Thomas Müller (Bayern Munich), Mesut Ozil (Arsenal) na Marco Reus (Borussia Dortmund)

Washambuliaji: Lukas Podolski (Arsenal), Andre Schurrle (Chelsea), Miroslav Klose (Lazio) na Kevin Volland (Hoffenheim).

Kocha Mkuu Yanga asitisha mkataba, apata ulaji Saudia

Kocha wa Yanga, Hans aliyesitisha mkataba na klabu hiyo
TAARIFA ambazo inatolewa muda huu na Uongozi wa Yanga ni juu ya kuacha kazi kocha wa timu hiyo Hans Van Der Plujim ambaye aliungana na timu hiyo January 2014,sababu za kocha huyo kuacha kazi ni kile kilichoelezwa kuwa amepata dili nchi nyingine na mkataba wake na Yanga ulikua unamalizika July mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Yanga inasema kuwa, Hans Van Der Pluijm kocha mkuu wa timu ya Young Africans leo amewaaga rasmi wachezaji wake, viongozi, wapenzi  na wanachama baada ya kumalizaa wake wa miezi sita na sasa anakwenda kujiunga na timu Al Shoalah FC iliyopo Ligi Kuu nchini Saudi Arabia. 
Kocha huyo mdachi ambaye ameiongoza Young Africans kwa kipindi cha miezi mitano amesema anashukuru kwa sapoti aliyokua akiipata kutoka kwa wachezaji, viongozi, wapenzi na wanachama wa timu hii kwa kipindi chote alipokuwa nchini Tanzania.
"Najua wengi itawashangaza kuona naondoka lakini ukweli ni kwamba niikua na hiyo deal hata hata kabla ya kuja Yanga, nilikua na makubaliano na timu ya Al Shoalah FCmakubaliano ambayo yanaanza mwezi ujao hivyo nilikubaliana na viongozi wa Yanga kuja kufanya kazi kwa kipindi cha miezi sita tu, nashukuru tumefanya kazi salama na baada ya mkataba huo kuisha nipo tayari kurudi kuja kufanya kazi Tanzania" alisema Hans
Naipenda Yanga SC, nimejaza fomu kuomba uanachama hivyo mimi ni sehemu ya Yanga na katika usajili ujao nitawasaidia kuleta wachezaji wazuri ambao wataisaidia timu kwenye msimu ujao kwa Ligi ya Vodacom na mashindao ya Kimataifa.
Kocha Hans anaondoka leo nakwenda Ghana kisha baadae atakwenda nchini Saudu Arabia tayari kwa kujiandaa na maandalizi ya msimu ujao katika timu yangu hiyo ambayo nitaitumikia kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Kuhusu usajili kocha mkuu ameshakabidhi ripoti yake ya kiufundi jana, viongozi wanaifanyia kazi kisha baadae itawekwa wazi.

Michuano ya Beach Soccer yafikia patamu Dar

MICHUANO ya soka ya ufukweni (beach soccer) inayoendeshwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ikishirikisha vyuo mbalimbali vya Dar es Salaam imeingia hatua ya robo fainali.
Robo fainali hiyo inayoshirikisha timu nane itachezwa Jumamosi (Mei 10 mwaka huu) kwenye ufukwe wa Escape One uliopo Mikocheni kuanzia saa 5 asubuhi, huku Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) na Taasisi ya Ustawi wa Jamii (SWI) zikicheza robo fainali ya kwanza.
Chuo Kikuu cha Ardhi (AU) na Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere watcaheza robo fainali ya pili kuanzia saa 6 kamili. Saa 8 kamili itaanza robo fainali ya tatu itakayozikutanisha Taasisi ya Uhasibu (TIA) na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).
Robo fainali ya mwisho itakayoanza saa 9 kamili itakuwa kati ya Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) na Chuo cha Utumishi Magogoni. Washindi watacheza nusu fainali Jumapili (Mei 11 mwaka huu) kwenye ufukwe huo huo.
Mechi za kutafuta mshindi wa tatu, na ile ya fainali zitachezwa kwenye ufukwe huo huo wikiendi ya Mei 17 mwaka huu.