STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, July 15, 2014

'Shujaa' waa Ujerumani haamini kama wametwaa ndoo

KIkosi cha Ujerumani na kocha wao wakishangilia ubingwa
Mario Gotze akiwa na famnilia yake akishangilia ubingwa
 MUUAJI aliyeizamisha Argentina na kuipata timu yake ya Ujerumani ubingwa wa Kombe la Dunia Mario Gotze amesema ilikuwa ni ndoto iliyokua kweli baada ya kuisaidia Ujerumani kutwaa Kombe la Dunia kwa kufunga goli pekee la mechi ya fainali dhidi ya Argentina kwenye Uwanja wa Maracana juzi.
Kiungo huyo wa Bayern Munich alianzia benchi katika mechi hiyo hiyo, lakini aliingizwa mwishoni mwa kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Miroslav Klose.
Gotze hakumuangusha kocha Joachim Low na akafunga goli katika dakika ya 113 kufuatia krosi ya Andre Schurrle na kuwapa Ujerumani ubingwa wa nne wa Kombe la Dunia.
"Ni hisia za aina yake, sijui nizielezee vipi. Nilipiga shuti tu na sikujua nini kitatokea. Ni ngumu kuamini," alisema nyota huyo mwenye umri wa miaka 21.
"Kwetu sisi,ndoto imekua kweli. Najivunia timu na nina furaha ya kupindukia kwa kila kilichotokea Brazil.
"Kila mchezaji katika timu yetu anastahili kutajwa hapa na tunajivunia kutwaa kombe hili."
Gotze amecheza mechi sita za Kombe la Dunia 2014 na amefunga magoli mawili.

MAYWEATHER KURUDIANA NA MAIDANA SEPTEMBA.

BINGWA wa masumbwi wa uzito wa welter ambaye hajapigwa mpaka sasa, Floyd Mayweather anatarajiwa kucheza pambano la marudiano na Marcos Maidana wa Argentina. 
Mayweather mwenye umri wa miaka 37 raia wa Marekani anatarajiwa kutetea mikanda yake ya ubingwa inayotambuliwa na Baraza la Ngumi Duniani-WBC na Chama cha Ngumi Duniani-WBA dhidi ya maidana aliyemdunda katika pambano lililofanyika Mei 3 mwaka huu. 
Wawili hao wanatarajiwa kupambana tena jijini Las Vegas, Septemba mwaka huu. 
Akihojiwa Mayweather ametamba kuwa ana uhakika wa kushinda pambano hilo pamoja na kukiri kuwa utakuwa mpambano na mgumu. 
Katika pambano lililofanyika Mei, jaji wa kwanza alitoa alama 114-114, wakati majaji wawili waliobakia walitoa alama 116-112 na 117-111 ambapo alama zote za juu zilikwenda kwa Mayweather. 
Mayweather anakaribia kufikisha rekodi ya kucheza mapambano 49 bila kupigwa iliyowekwa na bingwa wa zamani wa uzito wa juu Rocky Marciano, ambapo mpaka sasa ameshashinda mapambano 46 bila kupigwa.

Mnigeria, Wema, Sir Nature kupamba Usiku wa Matumaini

Wema Sepetu
TAMASHA la Usiku wa Matumaini la mwaka 2014 linatarajiwa kufanyika  Agosti 8 na litapambwa na wasanii mbalimbali nyota nchini pamoja na mwanadada mkali toka Nigeria Yemi Alade anayetamba na wimbo wa 'Johnny'
Kawaida ya tamasha hilo hufanyika Julai 7, lakini kutokana na mwaka huu tarehe hiyo kuangukia kwenye mfungo wa mwezi wa Ramadhani, waandaaji wake wameamua kupeleka hadi Nanenane kwa heshima ya waumini wa Kiislam.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo, Abdallah Mrisho alisema kuwa 'Usiku wa Matumaini' safari hii umeboreshwa kwa upande wa burudani ambapo Mnigeria Yami Alade anatarajia kutua kutumbuiza.
Mrisho alisema kwa upande wa wasanii wa nyumbani 'ujazo'umeongezwa kwa kuwakusanya wakali watupu kuanzia waigizaji, wasanii wa muziki wa kizazi kipya hadi wanamiochezo.
Wasanii wanaoatarajiwa kupanda jukwaani siku hiyo ni pamoja na Ali Kiba, Roma Mkatoliki, Madee, Juma Nature na wengineo kibao akiwamo Wema Sepetu atakayeimba na kucheza nyimbo za 'baby' wake, Diamond Platnumz.
"Upande wa masumbwi kutakuwa na pambano kati ya Mada Maugo na Thiomas Mashali, huku Khaleed Chokoraa aliyehamia kwenye ngumi atazipiga siku hiyo na Saim Memba, " alisema Mrisho kutoka kampuni ya Global Publishers ambao ndiyo waandaaji wa tamasha hilo la kila mwaka.
Aliongeza kuwa, Naibu Waziri wa Fedha na Mbunge, Mwingulu Nchemba atapanda ulingoni kuzipiga na Dk Hamis Kigwangala, huku wana Bongo Movie JB atazipiga na Cloud 112 na Irene Uwoya atappetana na Jackyline Wiolper.
"Pia kutakuwa na pambano la soka la Bongo Movie dhidi ya wapinzani wao Bongofleva na mechi ya wabunge wa Simba na Yanga ambao safari hii watakuwa na nyota wapya, Yanga wana Ridhiwani Kikwete na Simba wanaye Godfrey Mgimwa," alisema Mrisho.
Mwaka jana pambano la wabunge lilianzishwa na Rais Jakaya Kikwete kabla ya kupokewa na mwamuzi wa zamani wa kimataifa nchini, Othman Kazi 'Collina'.


KAJALA ampa UJUMBE mzito MWANAE akisherehekea miaka 12 ya kuzaliwa kwake

Paula
Kajala na mwanae Kajala
SIKU kama ya leo miaka 12 iliyopitaq  mwanadada Kajala Masanja alifanikiwa kujifungua mtoto wake aliyezaa na P Funk Majani aitwaye Paula.
Katika kuikumbuka siku hiyo muhimu kwa mwanae, Kajala kupitia ukursa wake wa INSTAGRAM ameandika ujumbe maalu kwa mtoto wake kueleza magumu yao yote waliopitia tangu siku ya kwanza Paula alipokuja duniani kwa kuzaliwa mpaka sasa...Kiukweli Kajala amefunguka mengi sana.....

Fainali za Usomaji wa Qur'an Julai 25

FAINALI za kumtafuta bingwa wa kuhifadhi Q'uran kwa njia ya kughani (Tajuweed) mwaka huu zitafanyika kwenye Msikiti wa Manyema jijini Dar es Salaam, Ijumaa ya mwisho ya mfungo mtukufu wa Ramadhani Julai 25 mwezi huu.
Aidha, siku hiyo itakuwa ni sawa na funga ya 27 ya mwezi huu mtukufu wa Ramadhani, hivyo waumini wa dini ya Kiislamu watakuwa ndani ya maombi maalum maarufu kama “Lailatul Qadir” ambayo huyatumia kuomba msamaha na kufutiwa madhambi maradufu na Mwenyezi Mungu.
Hayo yalisemwa na Katibu wa Taasisi ya Kuhifadhi na Usomaji wa Kuran ya Sheikh Yahya Hussein (Sheikh Yahya Hussein Tahfidh Q’uran and Tajweed Foundation), Maalim Hassan Yahya katika taarifa aliyotuma kwenye vyombo vya habari mwishoni mwa wiki.
 Maalim alisema  fainali hizo zitawakutanisha washindi wote wa michuano ya kusoma Koran watakaokuwa wameshinda kwenye michuano ya taasisi mbalimbali inayoendelea hivi sasa Afrika Mashariki na Kati.
“Tutakuwa na washindanaji walioshinda kutoka nchi zote za Afrika Mashariki na Kati ambazo ni Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, Congo DRC, Sudan Kusini na Tanzania,”alisema Maalim
Aidha alisema kuwa kutakuwa na majaji kutoka nchi hizo na wengine kutoka Saudi Arabia na Iran.
Alisema kuwa ni  washindi watatu wa mwanzo watapata nafasi ya kwenda Hijjah kwa gharama za taasisi yake pia watazawadiwa vyeti na fedha taslimu.

Brazili yamtimua 'Big Phil' ni baada ya aibu aliyowapa nyumbani


Scolari katika picha tofauti kabla ya kutimuliwa kocha wa Brazil
BRAZIL imemtimua kocha Luiz Felipe Scolari saa chache tu baada ya kumalizika kwa fainali za Kombe la Dunia ambalo walikumbana na vipigo vyao viwili vibaya zaidi katika historia yao ya michuano hiyo, moja ya magazeti yanayoongoza Brazil liliripoti jana.
Kikosi cha kocha Scolari cha Brazil kilikuwa kikipewa nafasi ya kutwaa ubingwa wa michuano hiyo lakini kilikumbana na kipigo cha aibu cha magoli 7-1 katika nusu fainali dhidi ya waliokuja kuwa mabingwa Ujerumani. Katika kukamilisha mwisho wao mbaya, walikumbana na kipigo kingine cha 3-0 dhidi ya Uholanzi katika mechi ya kusaka mshindi wa tatu.
Scolari, ambaye aliiongoza Brazil kutwaa taji lao la tano na la mwisho la Kombe la Dunia 2002, alisema baada ya mechi hiyo kwamba atawasilisha ripoti kwa mabosi wake katika Shirikisho la Soka la Brazil (CBF) na ni wakati huo tu hatima yake itaamuliwa.
Lakini gazeti la O Globo liliripoti jana kwamba Scolari alitimuliwa Jumapili usiku. Gazeti hilo lilisema taarifa rasmi ingetoka baadaye jana.
Hapakuwa na uthibitisho kutoka CBF, wala mshauri wa habari wa Scolari.
Scolari aliichukua timu hiyo Novemba 2012 na amepoteza mechi tano tu kati ya 29 alizokuwa madarakani. Aliiongoza Brazil kutwaa Kombe la Mabingwa wa Mabara mwaka jana kwa ushindi wa kukumbukwa wa 3-0 dhidi ya mabingwa wa dunia wa wakati huo Hispania katika mechi ya fainali.
Alikuwa ni mtu anayependwa sana Brazil kwa ucheshi wake na pia kwa wachezaji ambao humchukulia kama baba yao.
Alikuwa na sapoti ya taifa kuelekea kwenye Kombe la Dunia na kulikuwa na upinzani mdogo kwa kikosi alichoteua, jambo ambalo ni nadra sana nchini Brazil, kunakofahamika kama "taifa la makocha milioni 200."
Kama kuondoka kwake kutathibitishwa, makocha wanaopewa nafasi ya mapema kama warithi wake watakuwa ni Tite, kocha ambaye aliiongoza Corinthians kutwaa Kombe la Ligi ya Klabu Bingwa Amerika Kusini (Copa Libertadores) na Kombe la Dunia la Klabu 2012, na Muricy Ramalho, ambaye ni kocha wa sasa wa klabu ya Sao Paulo.

Monday, July 14, 2014

'Bethidei' mtoto wa Kajala ya kipekee

MUIGIZAJI nyota nchini Kajala Masanja anatarajiwa kumsindikiza mtoto wake Paula kusherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa kula bata na watoto wenye ulemavu wa akili wanaolelewa katika eneo la Sinza.
Kwa mujibu wa muongozaji na 'meneja' wa Kajala katika uzalishaji filamu, Leah Richard 'Lamata' Paula atasherehekea siklu yake ya kuzaliwa keshokutwa na Kajala ameamua kuiandalia sherehe hiyo kuwafariji watoto hao walemavu.
"Mtoto wa Kajala anatarajiwa kufanyiwa sherehe ya kuzaliwa kwake na mama yake yaani Kajala na shughuli nzima itafanyika katiia kituo cha kulelea watoto wenye Ulemavu wa akili Sinza, mtoto huyo atatumia siku hiyo kula na kucheza na watoto hao," alisema Lamata.
Lamata alisema Kajala ameamua kufanya hivyo kama njia ya kuwafariji watoto hao sambamba na kumpa darasa mwanae juu ya kutambua umuhimu wa kuwaheshimu na kuwajali watu wenye hali tofauti za kimaumbile na sherehe hiyo itahudhuriwa na watu mbalimbali wakiwamo nyota wa filamu nchini.

SUMAYE chupuchupu kufa ajali ya ndege

WAZIRI Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye (pichani), amenusurika kifo hivi karibuni baada ya ndege ya shirika la Precision Air, iliyokuwa ikitoka Mwanza kwenda Dar es Salaam kupata hitilafu ya injini.

Ndege hiyo, ambayo iliondoka Mwanza saa 2:30 usiku, ilipata hitilafu ya injini moja muda mfupi tu  baada ya kuruka, hali iliyomlazimu rubani wa ndege hiyo kubadili mwelekeo na kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
 
Akizungumza na Mtanzania jana, Sumaye, ambaye alikuwa mmoja wa abiria waliokuwemo kwenye ndege hiyo, alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
 
Sumaye alisema kitendo cha injini kupata hitilafu, ilimlazimu rubani wa ndege hiyo kuruka na injini moja mpaka KIA, ambako walitafutiwa ndege nyingine ili kuendelea na safari.
 
Alisema kutokana na tatizo hilo, abiria walilazimika kuondoka KIA kwa kugawanywa kwenye ndege tofauti zilizokuwa zikielekea Dar es Salaam ambapo Sumaye aliondoka saa 7 kasoro usiku.
 
Msemaji wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Bestina Magutu, alipotafutwa ili kujua kilichotokea kwenye ndege hiyo, alisema kuwa hakuwa na taarifa zozote za hitilafu ya ndege hiyo.
 
“Hebu ongea nao wenyewe, sijapata taarifa zozote mpaka sasa, nimetoka ofisini jana sikuwa na taarifa,” alisema Magutu.
 
Naye Mratibu wa Masoko wa Precision Air, Hilaly Mremi, alipozungumza na Mtanzania alikiri kutokea kwa hitilafu hiyo ya ndege.
 
“Kwa kifupi hakuna ajali iliyotokea, hitilafu zinazotokea kwenye ndege ni za kawaida kama ambavyo gari inaweza kuharibika na kupakiwa pembeni,” alisema Mremi.
 
Alisema safari za shirika hilo zinaendelea kama kawaida na kutaja namba ya ndege hiyo kuwa ni TW 415.
 
Ndani ya wiki hii, ndege mbili za shirika hilo zimenusurika ajali baada ya kupata hitilafu wakati zikiwa angani.
 
Mbali na ndege hiyo aliyokuwemo Sumaye, ndege nyingine ya shirika hilo yenye namba ya safari Pw 77 na ya usajili TWC, iliyokuwa ikitoka Mwanza kwenda Kilimanjaro ilinusurika kupata ajali juzi jioni na hivyo kulazimika kurudi na kutua kwa dharura uwanjani hapo baada ya kupata hitilafu ikiwa angani.
 
Mbali na Sumaye, Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, naye aliwahi pia kupata ajali mwaka jana akiwa kwenye ndege za shirika hilo.
 
Lowassa alikuwa miongoni mwa abiria 37 waliokuwa wamesafiri na ndege hiyo ambayo ilipasuka magurudumu manne ilipokuwa ikitua katika Uwanja wa Ndege wa Arusha.
 
Katika ndege hiyo pia kulikuwa na maofisa mbalimbali wa Serikali na Jeshi la Wananchi, ambao walikwenda kuhudhuria sherehe ya kutolewa kamisheni kwa maofisa wa jeshi katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli (TMA).
MTANZANIA

Riyama aiogopa kesho ya Isike Samuel

Riyama Ally
Isike Samuel
KIMWANA anayetesa kwenye kiwanda cha filamu nchini, Riyama Ally ameendelea kuongeza idadi ya filamu alizocheza baada ya kushirikishwa katika kazi mpya iitwayo 'Naiogopa Kesho' inayotarajiwa kuachiwa hivi karibuni.
Riyama aliyewahi kutamba kwenye makundi mbalimbali na kisha kwenye michezo ya kwenye runinga kabla ya kuibukia kwenye filamu, akitajwa miongoni mwa waigizaji wa kike walioshirikishwa katika filamu nyingi nchini, 'atauza sura' katika filamu hiyo mali ya Isike Samuel.
Akizungumza na MICHARAZO, Isike alisema filamu hiyo ya 11 kuiandaa kupitia kampuni yake ya Classic Vision pamoja na Riyama pia imewashirikisha wakali kama Hemed Suleiman 'PHD', Frank Kusenha, Steve wa Maisha Plus na yeye mwenyewe (Isike).
"Najiandaa kuachia filamu yangu ya 11 iitwayo 'Naiogopa Kesho' ambayo nimeiigiza mimi na kuwashirikisha kina Riyama Ally, Hemed, Frank Kusenha na wengine. Ni bonge la filamu ambayo mtu hapaswi kuikosa kwa mafunzo yake," alisema.
Isike aliyejitosa kuigiza na kuzalisha filamu tangu akiwa kidato cha pili akiwa na umri wa miaka 16 tu, alisema anaamini kazi hiyo itafunika sokoni kama ilivyokuwa kwa filamu zake nyingine za nyuma ambazo ni; 'Ivan Tears', 'Eyes on Me', 'Identity Card', 'Lonely', 'Tulizana', 'Rudi Kaburini', 'Sad Moment', 'Mr Masumbuko', 'Two Sisters' na 'Family Apart'.

Messi apozwa Brazil, 'James Bond' anyakua kiatu cha Dhahabu

James Rodriguez wa Colombia aliyetwaa kiatu cha dhahabu

Lionel Messi wa Argentina aliyeteuliwa kuwa MCHEZAJI BORA
NYOTA wa Argentina, Lionel Messi ambaye ameshindwa kutimiza ndoto za kunyakua Kombe la Dunia baada ya kunyakua kila aina ya tuzo katika maisha yake ya soka, amepozwa kwa kutangazwa kuwa MCHEZAJI BORA wa michuano ya Kombe la Dunia 2014. Messi aliyermaliza michuano hiyo akiwa na mabao manne sawa na Robin van Persie wa Uholanzi alinyakua tuzo hiyo akishuhudia timu yake ikishindwa kuizuia Ujerumani kunyakua taji la nne la michuano hiyo ikiwa kwenye ardhi ya Bara la Amerika ikiwa ni mara ya kwanza kwa timu kutoka barani Ulaya. Naye James Rodriguez 'James Bond' licha ya timu yake kutolewa hatua ya Roboi Fainali na Brazili amefanikiwa kunyakua kiatu cha Dhahabu kutokana na kuwa MFUNGAJI BORA wa michuano hiyo akiwa ametupia mabao sita akimzidi Thomas Muiller wa Ujerumani aliyemaliza wa pili na mabao matano. Kipa shujaa wa Ujerumani, Manuel Nieuer licha ya kuisaidia timu ya Ujerumani kutwaa taji katika mchezo wa fainali dhidi ya Argentina, pia alinyakua tuzo ya KIPA BORA katika michuano hiyo ambayo itakumbukwa kwa msisimko mkubwa iliyokuwa nayo.
Naye winga matata wa Ufaransa, Paul Pogba alinyakua tuzo ya Mwanasoka Bora Chipukizi. Mkali huyo anakipiga Juventus na amaekuwa akihusishwa na mipango ya kutaka kujiunga na Chelsea.


NI UJERUMANI 2014, WANAUME WAWEKA REKODI BRAZIL

Ujerumani wakishangilia taji lao baada ya kuilaza Argentina na kutwaa Kombe la Dunia 2014

Raha Tupu kwa Wanaumeeeeee!
Vita ilikuwa naona hii pichani




UJERUMANI imeweka rekodi ya kutwaa taji la Kombe la Dunia katika Bara la Amerika ikiwa ni mara ya kwanza kwa timu za Ulaya baada ya kuinyuka katika muda wa nyongeza Argentina waliokuwa waliopoiteza nafasi nyingi kuweza kumaliza kazi na kulibakisha taji hilo baranai humo.
Bao la dakika ya 113 kupitia kwa mtokea benchi  Mario Gotze lilitiosha kuwapa Ujerumani taji la nne la michuano hiyo huku wakiweka rekodi nyingine ya kucheza mechi zao saba bila kupoteza hata mchezo mmoja na ikiongoza kwa idadi kubwa ya mabao ya kufunga 18 na kufungwa manne tu.
Pambano hilo lililokuwa na kosakosa nyingi, Argentina ikipoteza nafasi nyingi za kufunga, lilishuhudia dakika 90 zikimalizika kwa sare ya 0-0 na kuongezwa dakika 30 za nyongeza.
Katika dakika hizo pambano liliwaweka roho juu mashabiki wa timu zote na Messi alikaribia kufunga bao la kusawazisha na pengine kuupelekea mchezo huo kwenye matuta, lakini Mchezaji Bora huyo wa michuano hiyo ya Brazili alipaisha kimaajabu mbele a Kipa Bora wa mashindano hayo ya 2014, Manuel Nieuer.
Mario Gotze aliyeingia uwanjani badala ya Miloslav Klose dakika mbili kabla ya muda wa kawaida kumalizika alipata pande safi ya Andre Schuerrle na kutuliza gambani kabla ya kumtungua kipa wa Argentina, Sergio Romelo.
Hii ni mara ya kwanza kwa Ujerumani kunyakua taji hilo kama nchi kamili ya Muungano wa Ujerumani Mbili ambazo zilikuwa zimetengena kwani mataji yake matatu ya awali ya mwaka 1954, 1974 na 1990 ilinyakua kama Ujerumani Magharibi 
 

Saturday, July 5, 2014

Je una msongo wa mawazo, dawa hii hapa sasa!!!



Waziri Mkuu afutwa kazi Senegal, kisa...!

 
WAZIRI mkuu nchini Senegal Aminata 'The Iron Lady' Toure ameachishwa kazi baada ya chama tawala kushindwa katika uchaguzi mkuu.
Maafisa wanasema kuwa Rais Macky Sall alimtaka Mwanamama huyo kujiuzulu baada ya kuhudumu chini ya kipindi cha mwaka mmoja.
Waandishi wanasema kuwa kutorodhika kwa wanachi kuhusu sera za uchumi za serikali hiyo ndio sababu kuu ya chama hicho kushindwa katika uchaguzi huo.
Waziri Mkuu huyo alikuwa mwanamke wa pili kushika wadhifa huo nchini humo tangu Mame Madior Boye kuweka rekodi alipochaguliwa mwaka 2001 na kudumu kwa kipindi kifupi chini ya utawala wa Abdoulaye Wade.
BBC