RAIS wa CECAFA, Leodgar Tenga akiwa na Katibu wake, Nicolaus Musonye
Baraza
la vyama vya soka Afrika mashariki na kati (CECAFA) kwa sasa linaangalia
uwezekano wa kupata muandaaji mpya wa michuano ya mwaka huu 2014 ya
chalenji kufuatia Ethiopia kujitoa.
Katibu
mkuu wa Cecafa Nicholas Musonye amenukuliwa toka Nairobi, Kenya kuwa Ethiopia imejitoa kuandaa michuano hiyo.
“Ethiopia
imetuandikia na kusema hawako katika nafasi ya kuandaa michuano hiyo,”
Musonye amesema na kuongeza kuwa CECAFA imekubali kujitoa kwao
“Hatuna la kufanya zaidi ya kukubali ombi la lakini tayari tumeanza kazi ya kusaka mwenyeji mpya.”
Musonye
amethibtisha hilo licha ya shirikisho la soka la Ethiopia EFF
kuwaandikia wakiwa wamechelewa, lakini amesema kuwa michuano hiyo
itafanyika kwa tarehe iliyotajwa kati ya Novemba na Desemba na kwamba
mwenyeji mpya atatangazwa wiki iyayo.
"Sudan yuko tayari akingojea hivyo michuano inaweza kuelekea Khartoum, lakini tutatangaza baadaye wiki ijayo"
Mwaka uliopita 2013 michuano
hiyo ilifanyika nchini Kenya ambapo wenyeji walitwaa taji hilo baada ya
kuifunga Sudan katika mchezo wa fainali uliopigwa katika dimba la Nyayo
jijini Nairobi.
Maafisa
wa polisi nchini Afrika kusini wakipiga saluti jeneza la marehemu Senzo
Meyiwa wakati umati wa wananchi wa Afrika kusini wakifuatilia.
Maafisa wa pilisi wakiwa wamebeba jeneza lililofunikwa kwa bendera ya taifa ya Afrika kusini katikati ya uwanja.
Pichani
anaonekana mjane wa Meyiwa Mandisa Meyiwa (kulia), baba yake Sam
(wapili kutoka kushoto) na mama yake Ntombifuthi (watatu kutoka kushoto)
Meyiwa,
akiwa katika picha wakati akiitumikia timu ya taifa dhidi ya Congo
Oktoba 15. Mlinda mlango huyo ameagwa na wachezaji wenzake na mshabiki
Picha
iliyochukuliwa January 2013 ikionyesha Rais wa Afrika kusininPresident
Jacob Zuma (kushoto) akipiga picha na Senzo Meyiwa wakati alipotembelea
timu ya taifa mjini Soweto
Mjane wa Meyiwa
MAELFU ya waombolezaji waliofurika kwenye mazishi ya aliyekuwa Nahodha na Kipa tegemeo wa timu za Orlando Pirates na ile ya taifa, Bafana Bafana walionekana wakibubujikwa na machozi huku macho yao
yakiwa na rangi nyekundu wakiwa wamevalia jezi nyeusi na wengine
nyekundu wakisema buriani Senzo Meyiwa katika mji wa Durban.
Huzuni
ilitawala watu wakilia kwa uchungu wakimlilia mlinda mlango huyo aliye
uwawa akiwa na umri wa miaka 27 ambapo jeneza lake lilizungushwa
uwanjani huku watu wakipuliza vuvuzela na kuimba nyimbo za kisoka.
Wengi
waliohudhuria mazishi hayo waliungana kwa pamoja ndani ya uwanja wa
Moses Mabhida akiwemo mjane wa Meyiwa, wanasiasa,wachezaji wa mpira wa
miguu, watu mashuhuri na maarufu na kutoa salamu zao za mwisho kwa
mpendwa wao.
Meyiwa, alipigwa risasi Jumapili iliyopita, baada ya majambazi kuingia nyumbani
mwa mpenzi wake karibu na Johannesburg.
Mtuhumiwa wa mauaji ya Meyiwa
alifikishwa mahakamani Ijumaa na alishitakiwa kwa mauaji dhidi ya mlinda
mlango huyo maarufu nchini Afrika Kusini.
Kifo cha Meyiwa
kilisababisha mshituko mkubwa nchini Afrika Kusini na yameonyesha
kiwango cha juu cha uahlifu wa kutumia nguvu nchini humo.
Mazishi yanafanyika katika uwanja wa mpira wa miguu wa Moses Mabhida Stadium katika mji wa Durban nyumbani kwa Meyiwa.
Senzo Meyiwa alionekana kama kivutio katika mchezo wa mpira miongoni mwa wananchi wa Afrika Kusini.
Wengi wa waombolezaji wamevaa fulana zenye picha ya Meyiwa, mtu ambaye alikuwa kivutio kikubwa kimichezo.
Mazishi
ya mwanamichezo mwingine shujaa wa Afrika Kusini, bingwa wa zamani wa
dunia wa mbio za mita 800 Mbulaeni Mulaudzi, pia yatafanyika Jumamosi.
Mulaudzi aliuawa katika ajali ya gari kabla ya kifo cha Meyiwa.
Rais Zuma ameamuru bendera ya taifa ipepee nusu mlingoti siku ya Jumamosi ili kumuenzi mlinda mlango huyo wa timu ya taifa.
Mechi kati ya timu za Orlando Pirates na Kaiser Chiefs katika ligi ya Afrika Kusini imeahirishwa baada ya kifo cha Meyiwa.
Senzo Meyiwa alikuwa nahodha na mlinda mlango wa timu ya Afrika Kusini, Bafana Bafana.
Mamlaka
ya soka nchini humo wametangaza mchezo wa timu ya taifa ya Afrika
Kusini wa kufuzu fainali za kombe la mataifa ya Afrika dhidi ya Sudan
ifanyike Durban.
Polisi wamesema Ijumaa kuwa mtuhumiwa wa mauaji ya Meyiwa alitambuliwa katika gwaride la utambuzi.
Mtuhumiwa
huyo, Zanokuhle Mbatha, mwenye umri wa miaka 25, anakabiliwa na
mashitaka ya mauaji na ujambazi wa kutumia silaha na anatarajiwa
kufikishwa tena mbele ya mahakama Novemba 11.Polisi wametangaza zawadi
kwa mtu atakayewezesha kupatikana kwa taarifa zaidi kuhusu shambulio
hilo ili kuwanasa watuhumiwa wengine.
Meyiwa alipigwa risasi akiwa nyumbani kwa mchumba wake huko kusini mashariki ya jiji la Johannesburg Jumapili iliyopita
Mwanamke akibubujikwa na machozi wakati wa sherehe ya kuuaga mwili wa mpendwa wao Meyiwa.
Wasuichana kama hawa watanufaika na mradi huo wa Hakuna Wasichoweza unaofanywa baina ya T-MARC, USAID na VODACOM FOPUNDATION
Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa T-MARC, Maurice Chirimi akizungumza na wanahabari katika shughuli zake ndani ya T MARC hivi karibuni.
JUMLA ya wasichana 6,000 mkoani Mtwara walio umri wa Balehe wapo katika nafasi nzuri ya kujikinga na mimba za umri mdogo zinazowasababishia kuacha shule pamoja na kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.
Akizungumza na MICHARAZO jijini Dar es Salaam jana, Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa T-Marc Tanzania, Maurice Chirimi alisema mafanikio hayo yametokana na mradi unaojulikiana kama ‘Hakuna Wasichoweza’ unaotekelezwa na T-Marc kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID) na Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom.
Chirimi alisema kuwa, mradi huo ulianza mwaka 2013 ambapo USAID kwa kushirikiana na Vodacom kupitia mfuko wake wa kusaidia jamii (Vodacom Foundation waliwapa nguvu ili kufanikisha mradi huo.
Alifafanua kuwa, kupitia mradi huo, T-MARC imefanikisha kutoa mafunzo kwa wasichana walio mashuleni na wasi mashuleni ikiwa na lenga la kuwapatia elimu pamoja na kuwapatia pedi wasichana wanatoka katika familia maskini kwa ajili ya kujihifadhi wakati wakiwa hedhi.
Aliongeza mafunzo pamoja na pedi za bure zimewafikia wasichana 5,232 waliopo katika shule 24 za msingi na wengine 552 wasiokuwepo mashuleni katika kata 17 mkoani Mtwara.
“Mafunzo ya namna na kujihifadhi wakati wakiwa hedhi pamoja na afya ya uzazi yanafanyika chini ya uwezeshaji wa walimu waliopewa mafunzo na wauguzi wa jadi. Kitini cha kufundishia juu ya masuala haya kimeweza kuandaliwa na T-Marc kwa kushirikiana Taasisi ya Elimu Tanzania kupitia mradi huu wa ‘Hakuna Wasichoweza’,” alifafanua
Alisema kupitia mafanikio yaliyopatikana kwenye awamu ya kwanza ya mradi, T-MARC kwa msaada wa dola za Kimarekani 166,000 itaupanua mradi na kuwafikia wasichana wengine 4,200 katika shule mpya 10 na kuongeza shirika lake litawapatia mafunzo walimu wengine 20 kwa ajili ya kuwafundisha na kuwaelekeza wasichana
Kwa upande wake, Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Rosalynn Mworia alisema Vodacom Foundation ikitambua mchango wa mwanamke katika jamii inayomzunguka kwani ukimwelimisha mwanamke ni sawasawa na kuelimisha jamii.
Alisema mara nyingi ukosefu wa elimu sahihi juu ya afya ya uzazi umekuwa ukiwafanya wasichana kuanza kuacha kuhudhuria vipindi vyao mashuleni yote hayo pia ni kwa kukosa nguo za kujihifadhi wakiwa katika siku za hedhi na kuwafanya watoto kuanza ngono wakiwa katika umri mdogo bila kujua madhara yake jambo ambalo huwasababishia mimba na kuwafanya washindwe kutimiza ndoto zao za kielimu.
Wachezaji wa Celta Vigo wakishangilia bao pekee dhidi ya Barca
Neymar licha ya kukukuruka kutaka kuendeleza rekodi ya mabao Barca alikwama jana kwa Celta Vigo
Messi akisikitika baada ya kukosa bao
BAO pekee lililofungwa dakika ya 55 na JoaquĆn Larrivey wa Celta Virgo lilitosha kuizamisha Barceona ikiwa nyumbani kwao katika pambano la La Liga lililochezwa uwanja wa Camp Nou.
Barcelona ikiwa na kikosi chake kamili walishindwa kuhimili vishindo vya wageni wao na kulala huku nyota wake Luis Suarez, Lionel Messi na Neymar wakikosa mabao mengi ya wazi wakiwa lango la wpainzani wao ambao ushindi huo nui wa kwanza kwao kenye uwanja wa Camp Nou.
Kocha Luis Enrique amekuwa akitumia mfumo wa kuwachezesha kwa pamoja washambuliaji hao watatu kwa imani ya kuifanya timu yake itishe, lakini bado mfumo huo haujazaa matunda kwani wiki iliyopita walikumbana na kipigo cha mabao 3-1 kwa Real madrid katika pambano la El Classico mjini Madrid.
Kwa kipigo hicho imeifanya Barcelona kuporomoka hadi nafasi ya tatu ikiachia usukani wa ligi mikononi mwa wapinzani wao Real Madrid yenye pointi 24 na mabingwa watetezi Atletico Madrid waliopo wa pili na pointi 23, moja zaidi ya ilizonazo wakali hao wa 'Cataluna',
Barca wana hatihati ya kuporomoka zaidi iwapo Sevilla itakayokuwa ugenini leo itashinda mechi yake dhidi ya Athletic Bilbao kwani zinalinda pointi 22, ila wenzao wana mchezo mmoja mkononi ambao unachezwa leo ambapo kama itashinda itakwea hadi kileleni ikiiengua Real Madrid.
Celta Vigo scored with one of only four attempts on target to win the match
Brazil striker Neymar could not add to his record of 11 goals in all competitions for Barcelona this season
Barcelona's Lionel Messi remains on 250 La Liga goals, one behind Telmo Zarra's all-time record
CHRISTIANO Ronaldo ameendeleza rekodi yake ya mabao baada ya usiku huu kuifungia timu yake ya Real Madrid bao moja wakati wakipata ushindi wa mabao 4-0 ugenini dhidi ya Granada.
Ronaldo alifunga bao lake la 17 katika mechi 10 na kutimiza mabao 23 katika mechi 12 za michuano yote ya msimu huu mpaka sasa 9 katika dakika ya pili ya mchezo kabla ya James Rodriguez kufunga mengine mawili na Karim Benzema kumaliza udhia na kuipa madrid ushindi huo mnono.
Majirani na wapinzani wa jadi wa Real, Atletico Madrid wakiwa nyumbani walipata ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Cordoba.
Mabao ya washindi yalifungwa na Delgado Pacheco aliyejifunga dakika ya 43 kabla ya wageni kusawazisha kupitia kwa Ghilas dakika ya 53 na Griezmann kuongezea wenyeji bao dakika tano baadaye na Mario Mandzukic kufunga bao la tatu na Raul Garcia kuhitimisha bao la nne kabla ya Ghilas kufunga bao la pili la Cordoba.
Hivi Barcelona wapo uwanja wa nyumbani kuumana na Celta Virgo na matokeo bao 0-0.
JKT Ruvu walioshindwa kulicheza gwaride la Polisi Moro
WAKATI klabu ya Simba ikiendeleza wimbo lake la sare, watani zao Yanga wamezamishwa kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba kwa kulazwa bao 1-0 na Kagera Sugar, huku maafande wa JKT Ruvu wakilala uwanja wa Chamazi ikiwa ni wiki moja tangu wavunje rekodi ya kuwa timu ya kwanza kuifunga Azam.
Simba ikiwa kwenye uwanja wa Jamhuri ililazimishwa sare ya 1-1 na Mtibwa Sugar na kuendeleza rekodi yao ya kutoshinda katika michezo 12.
Simba walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Joseph Owino, Nahodha wa vijana wa Msimbazi, kabla ya wenyeji kuchomoa bao kupitia kwa Mussa Hassan Mgosi, huku beki wa zamani wa Yanga, David Luhende akikosa penati ambayo ingeweza kuisaidia Mtibwa kuibuka na ushindi.
Mjini Bukoba, Yanga ikiwa na furaha ya kushinda 3-0 dhidi yha Stand United, ilijikuta ikichezea kichapo cha bao 1-0 mbele ya Kagera Sugar huku nahodha wake, Nadir Haroub Cannavaro akilimwa kadi nyekundu kwa mchezo mbaya dhidi ya mfungaji wa bao pekee la wenyeji, Paul Ngwai.
Kipigo hicho kimepokewa kwa masikitiko na kocha Marcio Maximo aliyelallamikia wachezaji wa Kagera kujaingusha na mwamuzi kutokuwa makini katika mchezo huo mbali na kulalamikia ubovu wa uwanja wa Kaitaba ambao umekuwa ukiisumbua Yanga kila mara kwa kuchezea kichapo.
Katika pambano jingine lililochezwa uwanja wa Chamazi, JKT Ruvu ilizimwa na maafande wenzao wa Polisi baada ya kulala mabao 2-1.
Mabao ya washindi yaliwekwa kimiani na nyota wa zamani wa Simba na Taifa Stars, Danny Mrwanda aliyefunga yote mawili na lile la wenyeji waliokuwa wametoka kushinda mechi mbili mfululizo likiweka wavuni na Jaffar Kisoki kabla ya Polisi kusawazisha na kuata la ushindi.
Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea kesho kwa pambano moja tu kati ya Mgambo JKT itakayokuwa wenyeji wa Mbeya City.
Sanchez akishangilia moja ya mabao yake mawili leo
Oscar akiifungia Chelsea bao la kwanza
Wanyama akiwa na wachezaji wenzake wakishangilia bao lake pekee la mapema lililotokana na shuti kali la umbali kama mita 40 na kuipa Soputhampton ushindi wa bao1-0 ugenini
VINARA wa Ligi Kuu ya England imezidi kujiimarisha kileleni mwa ligi hiyo baada ya kuizamisha QPR kwa mabao 2-1 na Arsenal kuifanyia mauaji Burnley kwa kuinyuka mabao 3-0.
Chelsea ikiwa uwanja wa nyumbani wa Stanford Bridge ilipata mabao yake kupitia kwa Oscar dakika ya 32 na mkwaju wa penati ya dakika ya 75 kupitia Eden Hazard na bao la wageni lilifungwa na Carlie Austin. Ushindi huo umeifanya Chelsea kufikisha mechi ya 10 ila kupoteza katika ligi hiyo.
Katika mechi nyingine Arsenal ilipata ushindi nyumbani wa mabao 3-0 dhidi ya Burnley kupitia mabao mawili ya Alexis Sanchez na jingine la Alex Oxlade-Chamberlain.
Nayo timu ya Southampton imeendeleza wimbi lake la ushindi na kuifukuza Chelsea ikiwa nafasi ya pili baada ya kupata ushindi ugenini dhidi ya Hully City bao pekee likifungwa na Vincent Wanyama.
Everton ikiwa nyumbani iling'ang'aniwa na Swansea City na kutoka suluhu bila ya kufungana, huku West Brom wakipata ushindi mwembemba ugenini wa bao 1-0 dhidi ya Leicester City, huku West Ham United ikiwa ugenini ililazlmisha sare ya 2-2 dhidi ya Stoke City.
BAO pekee lililofungwa na mchezaji wa zamani wa Toto Africans na African Lyon, Jacob Massawe lilitosha kuipa ushindi wa kwanza Ndanda ikiwa uwanja wake wa nyumbani kwa kuilaza mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Azam kwa bao 1-0. Kipigo hicho ni cha pili mfululizo kwa Azam baada ya mechi iliyopita mabingwa hao kufungwa bao 1-0 na JKT Ruvu na kuwaacha 'Matajiri' hao kusalia na pointi zao 10 baada ya kucheza mechi 7. Ushindi huo umeipa faraja wenyeji Ndanda ambao walikuwa hawajapa ushindi wowote kwenye uwanja wa nyumbani baada ya kufungfwa mechi mbili mfululizo na Ruvu Shooting na Mgambo Fc. Katika mechi nyingine Prisons-Mbeya ikiwa ugenini mjini Shinyanga ililazimisha sare ya bao 1-1 dhidi ya Stand United. Prisons walianza kuandika bao mapema kupitia kwa Ibrahim Mamba kabla ya wenyeji kusawazisha kupitia kwa Heri Mohammed. Nayo timu ya Ruvu Shooting wamejikuta wakizimwa wimbi lake la ushindi baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Coastal Union. Bao pekee la Wagosi wa Kaya liliwekwa kimiani na Itubu Imbem dakika ya 54,
Stand Utd-Heri Mohammed
Prisons-Ibrajim Mamba
Mario Balotelli akichezwa vibaya na mchezaji wa Newcastle Un ited leo
BAO pekee lililowekwa kimiani na Ayonze Perez limeifanya Newcastle United kuendeleza maajabu baada ya jioni ya leo kuilaza Liverpool bao 1-0.
Perez alifunga bao hilo dakika ya 73 na kuifanya timu hiyo ya Newcastle imepata ushindi wa tatu mfululizo baada ya kuinyuka Spurs na kisha kuivua taji la Capital One League, Manchester City.
Kipigo hicho kimezidi kuiweka pabaya Liverpool ambayo imeshindwa kuonyesha makali yake kama ilivyokuwa msimu uliopita ilipoonekana kama ingetwaa taji la Ligi ya England kabla ya kuzidiwa na Man City.
“OKTOBA
31 mwaka huu kupitia vyombo vya habari Wakili Damas Ndumbaro alitoa
shutuma mbalimbali dhidi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Tunapenda kuuleza umma wa Watanzania yafuatayo;
1.Hukumu
dhidi ya Wakili Ndumbaro ilitolewa na chombo halali kwa mujibu wa
Katiba ya TFF. Hivyo, TFF inatoa tahadhari kwa wanafamilia wa mpira wa
miguu kutomhusisha Wakili Ndumbaro katika masuala ya mpira wa miguu
katika kipindi hiki anachotumikia adhabu.
2.Hadi
sasa TFF haijapokea rufani yoyote kutoka kwa Wakili Ndumbaro. Hii ni
kwa kuwa kupitia barua yake kwa TFF aliagiza asikabidhiwe nyaraka yoyote
kutoka TFF hadi Oktoba 30 mwaka huu, hivyo hukumu ya Kamati ya Nidhamu
dhidi yake alikabidhiwa Oktoba 30 mwaka huu. Alichokifanya Wakili
Ndumbaro ni kuleta TFF barua ya kusudio la kukata rufani.
3.Tuhuma
za ubadhirifu wa TFF zilizotolewa na Wakili Ndumbaro si za kweli. TFF
inatafakari hatua za kisheria na kikanuni za kuchukua dhidi ya tuhuma
hizi.
4.Mkataba wa TFF na TBL:
TFF
inapenda kuwahakikishia wadau wa mpira wa miguu kuwa hakuna ubadhirifu
wa aina yoyote katika matumizi ya fedha za mkataba wa TFF/TBL. TFF
ingependa itoe kwa umma ufafanuzi wa vipengele vya mkataba huo na jinsi
unavyoendeshwa lakini masharti ya mkataba huo (confidentiality clause)
yanatuzuia kufanya hivyo.
Rais
wa TFF, Jamal Malinzi alikutana na klabu za Ligi Kuu na kuzielekeza
zikae na kujadili kanuni za Ligi, kisha zipendekeze maboresho ili
yajadiliwe katika kikao kijacho cha Kamati ya Utendaji.
TFF
inapenda kuchukue fursa hii kusisitiza umuhimu wa kufuata mifumo
tuliyojiwekea katika kutatua matatizo/kero zetu mbalimbali, utulivu ni
muhimu katika kuendeleza mpira wa miguu,”.
(IMETOLEWA NA MKURUGENZI WA MASHINDANO WA TFF, BONIFACE WAMBURA MGOYO)
IMETHIBITISHWA kuwa nahodha wa
Man United, Wayne Rooney ataanza mechi ya kesho Jumapili dhidi ya Man City katika pambano la watani wa jadi wa jiji la Manchester.
Rooney amemaliza adhabu ya
kadi nyekundu na imethibitika kuwa yupo fiti kwa pambano hilo, ingawa mkali mwingine Radamel
Falcao hatacheza kwa sasa bado yu majeruhi.
Man Utd ikimkosa Falcon wenzao Man City watakaokuwa nyumbani uwanja wa Etihad watawakosa David Silva, Frank Lampard na Yaya Toure walio majeruhi, lakini samir Nasir atakuwapo dimbani.
Timu hizo zinakutana kesho katika pambano la Ligi Kuu ya England sambamba na mechi nyingine ya Aston Villa dhidi ya Spurs huku matokeo baina yao yakisomeka hivi:
2013-14 - Utd 0-3 City, City 4-1
Utd
2012-13 - Utd 1-2 City, City 2-3
Utd
2011-12 - City 1-0 Utd, City 2-3
Utd (FA Cup), Utd 1-6 City
2010-11 - City 1-0 Utd (FA Cup),
Utd 2-1 City, City 0-0 Utd,
2009-10 - City 0-1 Utd, Utd
3-1 City (FA Cup), City 2-1 Utd (League Cup), Utd 4-3 City
Kiemba akichuana na Coutinho wakatia wa pambano la Simba na Yanga hivi karibuni
Haruna Chanongo (kushoto)
Shabaan Kisiga
WACHEZAJI Amri Kiemba na Haroun Chanongo wameshindwa kutokea kwenye kikao cha Kamati ya Nidhamu ya Simba SC kilichokua kifanyike jana ili kujitetea kutokana na kupewa adhabu ya kusimamishwa kusikojulikana huku wakiwa hawataoa udhuru wowote kama Shaaban Kisiga waliyesimamiwa naye. Rais wa Simba SC, Evans Elieza Aveva alisema kuwa Kiemba na Chanongo hawakutokea licha ya kutakiwa kufanya hivyo na wala hawajatoa taarifa yoyote, huku Kisiga akitoa udhuru. “Tuliwaagiza wafike makao makuu ya klabu Saa 4:00 asubuhi (jana), lakini hadi saa 6:00 mchana walikuwa hawajafika na hawakutoa taarifa yoyote, kwa hivyo ikabidi Wajumbe wa Kamati ya Nidhamu watawanyike,”alisema. Hata hivyo, Aveva alisema baadaye Kisiga alipiga simu kujieleza kwamba amekwama kwenye foleni na waakamuambia hana sababu ya kufika tena, kwa sababu kikao kimeahirishwa. Alipoulizwa ni hatua gani watachukuliwa wachezaji hao, Aveva alisema; “Kwanza Kamati ya Nidhamu ilete ripoti ya maandishi kwa Kamati ya Utendaji juu ya kikao chao, baada ya hapo Kamati ya Utendaji itatoa uamuzi,”alisema. Watatu hao, Shaaban Kisiga ‘Malone’, Amri Kiemba na Haroun Chanongo waliondolewa kwenye kambi ya Simba SC mapema wiki hii kwa sababu mbalimbali. Kisiga alirejeshwa Dar es Salaam kutoka Mbeya kwa tuhuma za kutoa majibu ya kifedhuli kwa uongozi kabla ya mchezo na Prisons Jumamosi, wakati Kiemba na Chanongo wanatuhumiwa kucheza kwa kiwango cha chini.