![]() |
| Hussein Javu |
Javu aliyesajiliwa na Yanga misimu miwili iliyopita akitokea Manungu, alisema kukutana kwake tena na Said Bahanuzi 'Spiderman' na wakali wengine ndani ya Mtibwa kumempa uhakika wa kurejesha heshima yake na ya klabu hiyo kwa mjumla katika ligi hiyo ya msimu huu.
Mtibwa iliyoanza kwa kasi katika ligi ya msimu uliopita kabla ya kutetereka, itaanzia mechi zake ugenini kabla ya kurudi Manungu kuzisubiri Ndanda na Majimaji kisha kuikaribisha Yanga katika pambano litakalochezwa Sept 30 kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
"Kwa mziki huu uliopo Manungu, sioni wa kuizuia Mtibwa kurejesha heshima yake msimu huu, ni kazi pevu lakini tumejiandaa kufanya makubwa, hasa kutokana na kurudi nyumbani chini ya kocha Mecky Maxime," alisema Javu.
Javu, Bahanuzi ni baadhi ya wachezaji wapya nane waliotua kwa Wakata Miwa hao kwa ajili ya kuunda kikosi cha msimu huu cha Mtibwa Sugar chenye wachezaji 28, wakiwamo 20 waliokuwa msimu uliopita.
Wengine nane wapya ni kipa Hussen Sharrif 'Casillas' na Issa Rashid 'Baba Ubaya' ambao nao wamerudisha majeshi nyumbani wakitokea Simba.











KLABU ya Southampton imekiri kuwa Manchester United wanamuwania winga wao wa kimataifa wa Senegal Sadio Mane, lakini ikatamka wazi kwamba mkali huyo hauzwi ng'o.
USHINDI una raha bhana we acha tu!, Meneja wa vinara wa Ligi Kuu ya England, Manchester City, Manuel Pellegrini ameanza kuchonga baada ya chama lake kupata ushindi katika mechi mbili mfululizo.
HII huenda ni taarifa isiyopendwa kusikika masikioni mwa mashabiki wa Chelsea, Vyombo vya Habari nchini Hispania vimetoa taarifa kuwa klabu ya Chelsea imefanikiwa kuizidi maarifa mahasimu wao Manchester United katika usajili wa mshambuliaji wa kimataifa wa Hispania Pedro Rodriguez kutoka Barcelona.