STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, January 13, 2017

Sasa ni mapumziko Azam 1, Simba 0

Kotei akithibitiwa na mabeki wa Azam wakiongozwa na Gadiel Michael (2)
Mashabiki wa Azam
DAKIKA 45 za kwanza za fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi, ni mapumziko wakati Azam ikiwa mbele kwa bao 1-0 dhidi ya Simba. Kwa wastani pambano lilikuwa fifte fifte, licha ya Azam kukosa bao la pili baada ya kichwa cha Bocco kushindwa kuingia kimiani dakika moja kabla ya mapumziko.

Kazimoto katoka, Mavugo achukua nafasi yake

DAKIKA tatu kabla ya mapumziko, Simba inamtoa Mwinyi Kazimoto na kumuingiza Laudit Mavugo. Kazimoto kajitonesha enka yake ya mguu na benchi la Msimbazi limeamua kumtoa.
Azam wakikosa bao muda mfupi uliopita. Sure Boy akishirikiana na John Bocco. Azam 1 Simba 0.

Dak 33, Azam bado ipo mbele kwa bao 1-0

SIMBA wanafanya kosa kosa nyingi langoni mwa Azam, ikiwa dakika ya 33 sasa matokeo yakiwa bado 1-0 Azam ikiongoza.

Dakika 21, Azam 1 Simba O

PAMBANO bado kali kwelikweli kila timu ikishambulia, ikiwa dakika ya 21 sasa mabao bado 1-0. Azam ikiongoza.

Himid Mao anaiandikia Azam bao tamu la

HIMID Mao 'Ninja' anaiandikia Azam bao dakika ya 13 kwa shuti kali la Dar mpaka Moro, lililomuacha Kipa Agyei ashindwe kuokoa.
Azam 1 Simba 0

Pambano la Simba na Azam limeanza

PAMBANO la fainali za Kombe la Mapinduzi kati ya Simba na Azam limeanza kama dakika 10 zilizopita na Wekundu wa Msimbazi wanafanya mashambulizi makali langoni mwa Azam.
Kichuya ameonekana msumbufu kwa mabeki wa Azam, lakini bado Simba wamekosa plan ya kupata bao mapema.
Azam wameonekana kuimarika na wamejaribu kama mara mbili kumpima Daniel Agyei, lakini milango imekuwa migumu. Micharazo itaendelea kukuwaletea dondoo za mchezo huu.

Azam yaivaa Simba kuitemi, Himid Mao ndani, Domayo anasubiri

Kikosi cha Azam, hapo Domayo tu ndio yupo nje kumpisha Himis Mao 'Ninja'
Na Rahma White
MABINGWA wa Kombe la Kagame, Azam imemjumuisha kikosi Himid Mao 'Ninja', wakati wakijiandaa kuvaana na Simba muda mchache kwenye pambano la fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi 2017 litakalochezwa Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Sehemu kubwa ya kikosi hicho ni kile kile kilichoizamisha Yanga na Taifa Jang'ombe kwenye nusu fainali kwani golini atasimama Aishi Manula, akisaidiwa na Shomari Kapombe na Gadiel Michael, huku kati wakiwamo Aggrey Morris na Yakubu Mohammed, wakati kati kuna majembe kama Himid Mao na Shephan Kingue, huku pemeni wakicheza Salum Abubakar 'Sure Boy' na Joseph Mahundi wakati safu ya ushambuliaji itaongozwa na Nahodha, John Bocco 'Adebayopr' akisaidiana na Yahya Mohammed.

Akiba: Mwadini Ali, David Mwantika, Frank Domayo, Mudathir Yahya, Enock Atta-Agyei, Samuel Afful na Shaaban Idd.

Majembe ya Simba yatakayoivaa Azam usiku huu, Kazimoto ndani

Na Rahma Junior
KOCHA wa Simba amekitoa hadharani kikosi chake kitakachoivaa Azam muda mchache kwenye pambano la fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi 2017 litakalochezwa Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Sehemu kubwa ya kikosi hicho ni kile kile kilichoizamisha Yanga kwenye nusu fainali kwani golini yupo, Mghana Daniel Agyei kama kawa akilindwa na mabeki wa pembeni Janvier Bokungu na Mohammed Hussein 'Tshabalala' huku kati wakiwamo Abdi Banda na Method Mwanjali.
Jonas Mkude, Muzamir Yassin na James Kotei wakisimama kati, huku mshambuliaji akiwa Juma Liuzio 'Ndanda' na mawinga wakiwa ni Shiza Kichuya na Mkongwe, Mwinyi Kazimoto.


Akiba: Manyika Peter, Hamad Juma, Novaty Lufunga, Said Ndemla, Jamal MNyate, Pastory Athanas na Laudit Mavugo.

Kocha Lyon anamtaka Depay hata leo hii

Depay
KOCHA wa klabu ya Olympique Lyon, Bruno Genesio amefichua kuwa straika wa Man United, Memphis Depay ni moja ya vipaumbele vyake katika usajili wa Januari.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi inaelezwa kuwa, huenda akaondoka klabu hapo mwezi juu kwenda katika klabu hiyo ya Ligi Kuu ya Ufaransa, ingawa inadaiwa kikwazo ni dau la Pauni 13 milioni lililotajwa kutaka kulipwa na Lyon.
Mabosi wa Mashetani Wekundu wanataka kumuuza mchezaji huyo kwa Pauni milioni 15.
Hata hivyo, Kocha Genesio amefichua juu ya kumhitaji mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 kwa kusema; "Depay ni kipaumbele changu."
"Ni mchezaji aliyekamilika kwa kila kitu na atatufaa kuziba nafasui ya (Rachid) Ghezzal, iwapo mchezaji huyo ataamua kuondoka Lyon," aliongeza Genesio.
Depay amekuwa hana nafasi ndani ya kikosi cha Kocha Jose Mourinho, huku ikielezwa 'ubishoo' ndio unaomponza, hivyo njia pekee ya kuokoa kipaji chake ni lazima apate timu ya kuichezea na Lyon inasisitiza inamtaka.

Nani kubeba taji la Mapinduzi Cup 2017?

Na Rahma White
LIMEBAKI kama saa moja na ushei tu kabla ya Simba na Azam kumaliza ubishi kwenye pambano la fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi 2017 litakalopigwa kwenye Uwanja wa Amaan, visiwani Zanzibar.
Simba inacheza fainali yake ya sita katika msimu huu wa 11 wa michuano hiyo, ilihali Azam itakuwa ni ya tatu, lakini ikiwa na rekodi ya kusisimua ya kuingia fainali chache lakini haijawahi kuacha taji.
Iliingia mwaka 2012 na 2013 na mara zote likabeba taji mbele ya Jamhuri ya Pemba na KCCA, wakati Simba katika fainali zake tano za awali imetwaa mara tatu ikiwa klabu yenye historia ya kutwaa mara nyingi taji hilo.
Licha ya rekodi hizo za kusisimua kwa wababe hao wa Ligi Kuu Bara, bado timu yoyote itakayocheza vema na kutumia kwa ufanisi dakika 90 inaweza kubeba taji na kuhitimisha siku 15 za michuano hiyo iliyoanza Desemba 30, 2016.
Makocha na wachezaji wa timu zote wamekuwa wakitambiana tangu walipofahamu watakutana kwenye mchezo huo utakaoanza majira ya Saa 2:15, lakini ukweli ni kwamba lolote linaweza kutokea usiku huu visiwani humo.
Simba inayotarajiwa kupanga kikosi karibu chote kilichoitoa nishai Yanga kwa kuifunga kwenye nusu fainali, inaivaa Azam ikiwa haijkapoteza mechi yoyote ila imeruhusu bao moja wavuni wake, tofauti na Azam ambayo haijafungwa kabisa.
Mbali na mashabiki usiku kutaka kushuhudia timu ipi itakuwa bingwa mpya wa michuano ya mwaka huu, pia fainali hizo zitakuwa na utamu mwingine wa kujua wachezaji gani watakaonyakua tuzo za Ufungaji Bora, Kipa Bora, Mchezaji Bora Chjipukizi na Mchezaji Bora wa michuano.
Mpaka sasa tuzo ya Mfungaji Bora ni kama inarudi tena kwa Simon Msuva aliyetwaa mwaka 2014 akiwa na mabao manne sawa na aliyonayo msimu huu, licha ya timu yake ya Yanga kutolewa.
Wachezaji waliokuwa wakimfukuzia winga huyo mchachari, Bokota Labama wa URA Uganda ma Abdulsamad Kassim wa Jang'ombe Boys timu zao zimeaga michuano, japo Laudi Mavugo mwenye mabao mawili anaweza kumvurugia.
Kipa Bora nafasi ipo wazi kwa Aishi Manula wa Azam ambayo mpaka timu yake ikiivaa Simba, hajaruhusu bao lolote na akiwa ameonyesha kiwango cha hali ya juu, huku Daniel Agyei wa Simba naye aliyeibuka shujaa katika mechi ya nusu fainali dhidi ya Yanga kwa kuokoa penalti mbili za Deo Munishi 'Dida' na ile ya Haji Mwinyi anaweza kujikuta akibeba, iwapo Simba itafanya yake usiku huu.
Kwenye tuzo ya Mchezaji Bora Chipukizi ni vigumu kufahamu kwa sasa kwa sababu kuna vijana wengi walioonyesha makali akiwamo Enock Atta-Agyei wa Azam ambaye ndio kwanza anamiaka 18, lakini amepiga soka la nguvu Zanzibar.
Bila shaka ni suala la kusubiri kujua mambo yatakuwaje na MICHARAZO MITUPU litakuletea hatua kwa hatua ya pambano hilo mpaka mwisho wa fainali hiyo, usiache kuperuzi blog yako makini upate uhondo.

Kijeba cha Congo chazingua, CAF chapigwa mkwara

Na Alfred Lucas, TFF
BADO hakijaeleweka. Lile sakata la kijeba cha timu ya taifa ya vijana ya Congo, Langa Lesse Bercy, halijatafutiwa ufumbuzi mpaka sasa, ila safari hii Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), limetoa nafasi ya mwisho kwa Shirikisho la Soka la Jamhuri ya Congo (FECOFOOT) kumpeleka mchezaji huyo  jijini Libreville, Gabon ili apimwe kipimo kipya cha MRI ili kutambua umri wake.
CAF limetaka FECOFOOT kumpeleka mchezaji huyo huko Libreville, Gabon ndani ya siku 10 zijazo kuanzia jana Januari 12, 2017.
CAF limepata kumwita mchezaji huyo mara mbili mwaka jana, na FECOFOOT imeshindwa kumpeleka kwa sababu mbalimbali wanazozijua FECOFOOT.
Kwa mujibu wa kanuni za mashindano ya kimataifa ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17, vijana waliohitajika kucheza ni wale wenye umri wa chini ya miaka 17.
Langa Lesse Bercy, amelalamikiwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwamba amezidi umri hivyo kuhitajika kumpeleka kwani hakustahili kucheza hatua ya kufuzu kwa michuano hiyo ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana.
Fainali za vijana zinatarajiwa kufanyika katika nchi nyingine itakayotangazwa hapo baadaye baada ya Madagascar kuondolewa kuandaa fainali hizo baada ya kubainika kutokamilisha baadhi ya taratibu.
Hii inatokana na ripoti ambayo CAF wameipata kutoka kwa wakaguzi wa maandalizi ya fainali hizo. CAF imefungua kandarasi ya kwa nchi wanachama wengine kuandaa fainali hizo. Mwisho wa kupokea maombi ni Januari 30, mwaka huu.
Kadhalika Kamati ya Utendaji ya CAF, imemteua Rais wa zamani wa TFF, Leodegar Chilla Tenga kuwania nafasi ya uwakilishi katika Shirikisho la Kimataifa la Soka (FIFA).
Katika nafasi hiyo kutoka nchi za Afrika zinazozungumza Kiingereza, Tenga atachuana na Rais wa zamani wa Shirikisho la Soka la Zambia, Kalusha Bwalya na Kwesi Nyantakyi wa Ghana.
Wengine waliopitishwa kuwania nafasi ya uwakilishi katika Kamati ya Utendaji ya FIFA kutoka nchi za Afrika ni Tarek Bouchamaoui wa Tunisia ambaye anaingia kwenye kundi la nchi zinazozungumza lugha za Kiarabu, Kireno na Kihispaniola.
Kwa nchi zinazozungumza lugha ya Kifaransa wamo Constant Omari Selemani wa DR Congo na Augustin Sidy Diallo wa Cote d’Ivoire wakati nafasi nyingine za wazi ihuhusisha mwanamke mmoja, wamo Almamy Kabele Camara (Guinea), Chabur Goc (South Sudan), Danny Jordaan (Afrika Kusini), Hani Abo Rida (Misri)  na Lydia Sekera (Burundi).

Maafande wa Ruvu washindwa kutambiana Mabatini

JKT Ruvu
Ruvu Shooting
Na Rahim Junior
MAAFANDE wa JKT Ruvu na Ruvu Shooting zimeshindwa kutambiana jioni ya leo baada ya kutoka sare ya bao 1-1 katika muendelezo wa Ligi Kuu Bara iliyoanza tena baada ya kusimama kwa wiki mbili.
Timu hizo zimevaana kwenye Uwanja wa Mabatini, Mlandizi na JKT imeshindwa kulipa kisasi cha kipigo cha bao 1-0 ilichopewa na ndugu zao hao kwenye mchezo wa duru la kwanza.
JKT ndio waliojkuwa wa kwanza kuandika bao la kuongoza lililopatikana mapema dakika ya tatu tu, kupitia Renatus Morris, lakini Ruvu Shooting ilichomoa dakika sita baadaye kupitia mfumania nyavu wao mahiri, Abdulrahman Mussa.
Bao la Mussa limemfanya kufikisha jumla ya mabao nane na kubakisha moja tu kuwanasa vinara wa magoli, Shiza Kichuya wa Simba, Amissi Tambwe na Simon Msuva wa Yanga wenye mabao tisa kila mmoja.
Sare hiyo haijabadilisha lolote katika nafasi kwa timu hizo, kwani Ruvu imeongeza pointi na kufikisha 24, lakini imesalia nafasi iliyokuwapo sawa na JKT ambayo inasalia mkiani ikiwa na pointi 15 tu,  ikiwa imecheza mechi 19.
Ligi hiyo itaendelea tena kesho Jumamosi kwa mechi mbili ambapo mjinio Shinyanga, Chama la Wana, Stand United itavaana na Mwadui kwenye Uwanja wa Kambarage, huku Ndanda itakaribishwa na Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba mkoani Kagera.
Msimamo wa Ligi Kuu Bara
                               P  W   D  L   F   A  Pts

1. Simba                 18 14  2   2  30  6  44
2. Yanga                 18  12  4   2  39  9  40
3. Azam                  18  8   6   4  23  15 30
4. Mtibwa Sugar      18  8    6   4  22  19 30
5. Kagera Sugar      18  8   4   6   19  18 28
6. Mbeya City          18  6   6   6   16  16 24
7. Ruvu                   19  5   9   5   18  20  24
8. Stand Utd            18  5   7   6   16  16  22
9. Prisons                18  5   7   6   10  13  22
10.Mwadui               18  6   4   8   16  22 22
11.African Lyon        18  4   8   6   11   16  20
12.Mbao                  18  5   4   9   17  24  19
13.Ndanda               18  5   4   9   15  24  19
14.Majimaji              18  5   2  11  13  26  17
15.Toto Africans        18  4   4  10  11  20  16
16.JKT Ruvu            19   3   9   7    7  17   15

Wafungaji:   

9- Shiza Kichuya                           (Simba)
     Simon Msuva                            (Yanga)   
     Amissi Tambwe                         (Yanga)
8- Abdulrahman Mussa      (Ruvu Shooting)
7- Rashid Mandawa             (Mtibwa Sugar)
    Donald Ngoma                           (Yanga)
    John Bocco                                 (Azam)
6- Mzamiru Yasin                           (Simba)
    Haruna Chanongo            (Mtibwa Sugar)
5- Omar Mponda                          (Ndanda)
    Obrey Chirwa                             (Yanga)
    Riffat Khamis                           (Ndanda)
    Victor Hangaya                         (Prisons)
    Mbaraka Yusuf                 (Kagera Sugar)
    Rafael Daud                        (Mbeya City)
    Venance Joseph                 (African Lyon)
4-Peter Mapunda                         (Majimaji)
    Kelvin Sabato                   (Stand United) 
    Laudit Mavugo                           (Simba)
    Marcel Boniventure                 (Majimaji)
    Boniface Maganga                       (Mbao)
    Deus Kaseke                              (Yanga)
    Shaaban Kisiga              (Ruvu Shooting)
    Mohammed Ibrahim 'MO'            (Simba)   
    Tito Okello                          (Mbeya City)
3- Hood Mayanja                   (African Lyon)
    Ibrahim Ajib                              (Simba)
    Abdalla Mfuko                         (Mwadui)
    Subianka Lambert                    (Prisons)
    Ditram Nchimbi                  (Mbeya City)
    Wazir Junior                      (Toto African)
    Issa Kanduru                 (Ruvu Shooting)
    Ally Nassor 'Ufudu'          (Kagera Sugar)
    Kelvin Friday                   (Mtibwa Sugar)
    Mfanyeje                                (Majimaji)
    Francisco Zukumbawira                (Azam)
    Shaaban Idd                               (Azam)
    Jamal Mnyate                             (Simba)
    Jamal Soud                       (Toto Africans)
2- Adam Kingwande              (Stand United)
    Samuel Kamuntu                    (JKT Ruvu)
    Vincent Philipo                             (Mbao)
    Mcha Khamis                               (Azam)
    Danny Mrwanda                (Kagera Sugar)
    Pastory Athanas                 (Stand United)
    Paul Nonga                                (Mwadui)
    Adeyum Saleh                    (Stand United)
    Jacob Massawe                   (Stand United)
    Fully Maganga                  (Ruvu Shooting)        
    Themi Felix                       (Kagera Sugar)
    Mudathir Yahya                             (Azam)
    Atupele Green                         (JKT Ruvu)
    Jerry Tegete                              (Mwadui)
    Jamal  Mwambeleko                      (Mbao)
    Vincent Barnabas              (Mtibwa Sugar)
    Adam Salamba                  (Stand United)
    Jaffar Salum                     (Mtibwa Sugar)

Diamond akikinukisha Gabon, Vita ya Afcon 2017 imeiva

Zimbabwe
Guinea Bissau

Senegal

Watetezi Ivory Coast
Taji linalowaniwa
Ghana
Uganda

LIBREVILLE, GABON
KUMEKUCHA. Kesho Jumamosi pazia la michuano ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon 2017), kusaka bingwa wa bara la Afrikalitafunguliwa.
Wenyeji wa michuano hiyo Gabon, itakata utepe kwa kuvaana na Guinea Bissau kabla kabla ya wababe Cameroon kukwaruzana na Burkina Faso katika pambano jingine tamu linalosubiriwa kwa hapo kwenye ufunguzi wa michauno hiyo.
Tanzania ambayo ina miaka karibu 37 inajifariji kwa kuwakilishwa na mwimbaji wa muziki wa kizazi kipya, Naseeb Abdul 'Diamond Platinumz' atakayepamba sherehe za ufunguzi sambamba na wakali wa Nigeria akiwamo Mr Flavor.
Tanzania ilishiriki mara ya kwanza na mwisho mwaka 1980 ilipofanyikia Nigeria, lakini pamoja na kukosekana kwao bado mashabiki wa soka watazitumia runinga zao kufuatilia michuano hiyo itakayofikia tamati Februari 5 wakati Bingwa atakapofahamika.
MICHARAZO MITUPU inakuletea orodha ya vikosi vitakavyochuana kwenye michuano hiyo pamoja na ratiba nzima ya Afcon 2017.

ALGERIA
Makipa: Malik Asselah (JS Kabylie), Rais M’Bolhi (Antalyaspor/TUR), Chemseddine Rahmani (Mouloudia Bejaia)
Mabeki: Mohamed Benyahia, Mohamed Meftah (both USM Alger), Hichem Belkaroui (Esperance/TUN), Mokhtar Belkhiter (Club Africain/TUN), Ramy Bensebaini (Rennes/FRA), Liassine Cadamuro (Servette/SUI), Faouzi Ghoulam (Napoli/ITA), Aissa Mandi (Real Betis/ESP), Djamel Mesbah (Crotone/ITA)
Viungo: Mehdi Abeid (Dijon/FRA), Nabil Bentaleb (Schalke/GER), Yacine Brahimi (Porto/POR), Rachid Ghezzal (Lyon/FRA), Adlene Guedioura (Watford/ENG), Riyad Mahrez (Leicester City/ENG), Saphir Taider (Bologna/ITA)
Mastraika: Baghdad Bounedjah (Al Sadd/QAT), Sofiane Hanni (Anderlecht/BEL), Islam Slimani (Leicester/ENG), El Arabi Hillel Soudani (Dinamo Zagreb/CRO)
Kocha: George Leekens (Ubelgiji)

BURKINA FASO
Makipa: Herve Koffi (ASEC/CIV), Moussa Germain Sanou (Beauvais/FRA), Aboubacar Sawadogo (Kadiogo)
Mabeki: Yacouba Coulibaly (Bobo), Issoufou Dayo (Berkane/MAR), Bakary Kone (Malaga/ESP), Souleymane Kouanda (ASEC/CIV), Patrick Malo (Smouha/EGY), Issouf Paro (Santos/RSA), Steeve Yago (Toulouse/FRA)
Viungo: Prejuce Nacoulma, Alain Traore (both Kayserispor/TUR),Cyrille Bayala (Sheriff Tiraspol/MDA), Adama Guira (Lens/FRA), Charles Kabore (Krasnodar/RUS, capt), Bakary Sare (Moreirense/POR), Blati Toure (Omonia Nicosia/CYP), Abdoul Razack Traore (Karabuspor/TUR), Bertrand Traore (Ajax Amsterdam/NED), Jonathan Zongo (Almeria/ESP)
Mastraika: Aristide Bance (ASEC/CIV), Banou Diawara (Smouha/EGY), Jonathan Pitroipa (Al Nasr/UAE)
Kocha: Paulo Duarte (Ureno)

CAMEROON
Makipa: Jules Goda (Ajaccio/FRA), Georges Mbokwe (Coton Sport), Fabrice Ondoa (Sevilla/ESP)
Mabeki: Fai Collins (Standard Liege/BEL), Mohamed Djeitei (Nastic Tarragone/ESP), Ernest Mabouka (Zilina/SVK), Michael Ngadeu Ngadjui (Slavia Prague/CZE), Jonathan Ngwem (Progresso Sambizanga/ANG), Nicolas Nkoulou (Lyon/FRA), Ambroise Oyongo (Impact Montreal/CAN), Adolphe Teikeu (Sochaux/FRA)
Viungo: Franck Boya (Apejes Academy), Arnaud Djoum (Hearts/SCO), Georges Mandjeck (Metz/FRA), Edgar Salli (Saint-Gallen/SUI), Sebastien Siani (Ostend/BEL)
Mastraika: Vincent Aboubakar (Besiktas/TUR), Christian Bassogog (Aalborg/DEN), Benjamin Moukandjo (Lorient/FRA), Clinton Njie (Marseille/FRA), Robert Ndip Tambe (Spartak Trnava/SVK), Karl Toko-Ekambi (Angers/FRA), Jacques Zoua (Kaiserslautern/GER)
Kocha: Hugo Broos (Ubelgiji)
 
DR CONGO
Makipa: Joel Kiassumbua (Wohlen/SUI), Nicaise Kudimbana (Antwerp/BEL), Ley Matampi (TP Mazembe)
Mabeki: Jordan Ikoko (Guingamp/FRA), Joyce Lomalisa (V Club), Chancel Mbemba (Newcastle/ENG), Issama Mpeko (Mazembe), Fabrice N'Sakala (Alanyaspor/TUR), Marcel Tisserand (Ingolstadt/GER), Gabriel Zakuani (Northampton/ENG, capt)
Viungo: Merveille Bope (Mazembe), Herve Kage (Kortrijk/BEL), Neeskens Kebano (Fulham/ENG), Jacques Maghoma(Birmingham/ENG), Paul-Jose M'Poku (Panathinaikos/GRE), Remy Mulumba (Ajaccio/FRA), Youssouf Mulumbu (Norwich/ENG)
Mastraika: Cedric Bakambu (Villarreal/ESP), Jeremy Bokila (Al Kharitiyat/QAT), Jonathan Bolingi (Mazembe), Jordan Botaka (Charlton/ENG), Dieumerci Mbokani (Hull City/ENG), Firmin Ndombe Mubele (Al Ahly/QAT)
Kocha: Florent Ibenge
EGYPT
Makipa: Sherif Ekramy (Al Ahly), Essam El Hadary (Wadi Degla, capt), Ahmed El Shennawy (Zamalek)
Mabeki: Ahmed Fathy, Ahmed Hegazy, Saad Samir (all Ahly), Ahmed Dwidar, Ali Gabr (both Zamalek), Ahmed Elmohamady (Hull City/ENG), Omar Gaber (Basel/SUI), Karim Hafez (Lens/FRA), Mohamed Abdel-Shafi (Ahly Jeddah/KSA)
Viungo: Tarek Hamed, Ibrahim Salah (both Zamalek), Abdallah El Said (Ahly), Mahmoud Hassan (Mouscron/BEL), Mohamed Elneny (Arsenal/ENG), Amr Warda (Panetolikos/GRE)
Mastraika: Ahmed Hassan (Braga/POR), Marwan Mohsen (Ahly), Mahmoud Abdel-Moneim (Ahly Jeddah/KSA), Mohamed Salah (Roma/ITA), Ramadan Sobhy (Stoke City/ENG)
Kocha: Hector Cuper (Argentina)

GABON
Makipa: Anthony Mfa Mezui (clubless), Yves Stephane Bitseki Moto (Mounana), Didier Ovono (Ostend/BEL)
Mabeki: Aaron Appindangoye (Laval/FRA), Bruno Ecuele Manga (Cardiff City/WAL), Franck Perrin Obambou (Stade Mandji), Johann Serge Obiang (Troyes/FRA), Benjamin Ze Ondo (Mosta/MAL), Lloyd Palun (Red Star/FRA), Andre Biyogho Poko (Karabukspor/TUR), Yoann Wachter (Sedan/FRA)
Viungo: Guelor Kanga Kaku (Red Star/SRB), Mario Lemina (Juventus/ITA), Levy Clement Madinda (Nastic Tarragona/ESP), Didier Ndong (Sunderland/ENG), Junior Serge Martinsson Ngouali (Brommapojkarna/SWE), Merlin Tandjigora (Meixian Hakka/CHN), Samson Mbingui (Raja Casablanca/MAR)
Mastraika: Serge Kevyn Aboue Angoue (Uniao Leiria/POR), Pierre-Emerick Aubameyang (Borussia Dortmund/GER, capt), Cedric Ondo Biyoghe (Mounana), Denis Athanase Bouanga (Tours/FRA), Malick Evouna (Tianjin Teda/CHN)
Kocha: Jose Antonio Camacho (Hispania)

GHANA
Makipa: Razak Braimah (Cordoba/ESP), Adam Kwarasey (Rosenborg/NOR), Richard Ofori (Wa All Stars)
Mabeki: Harrison Afful, Jonathan Mensah (both Columbus Crew/USA), Frank Acheampong (Anderlecht/BEL), Daniel Amartey Leicester City/ENG), John Boye (Sivasspor/TUR), Edwin Gyimah Orlando Pirates/RSA), Baba Rahman (Schalke/GER), Andy Yiadom Barnsley/ENG)
Viungo: Afriyie Acquah (Torino/ITA), Emmanuel Agyemang-Badu (Udinese/ITA), Christian Atsu (Newcastle/ENG), Ebenezer Ofori (AIK Stockholm/SWE), Thomas Partey (Atletico Madrid/ESP), Samuel Tetteh (Leifering/AUT), Mubarak Wakaso (Panathinaikos/GRE)
Mastraika: Ebenezer Assifuah (Sion/SUI), Andre Ayew (West Ham/ENG), Jordan Ayew (Aston Villa/ENG), Asamoah Gyan (Al Ahly/UAE, capt), Bernard Tekpetey (Schalke/GER)
Kocha: Avram Grant (Israeli)

GUINEA-BISSAU
Makipa: Rui Dabo (Cova Piedade/POR), Papa Mbaye (Aguadulce/ESP), Jonas Mendes (Salgueiros/POR)
Mabeki: Mamadu Cande (Tondela/POR), Eridson (Freamunde/POR), Emmanuel Mendy (Ceahlaul Piatra Neamt/ROU), Rudinilson Silva (Lechia Gdansk/POL), Agostinho Soares (Sporting Covilha/POR), Juary Soares (Mafra/POR)
Viungo: Tony Silva Brito, Toni Silva, Zezinho (all Levadiakos/GRE), Bocundji Ca (Paris FC/FRA, capt), Idrissa Camara (Avellino/ITA), Francisco Junior (Stromsgodset/NOR), Jean-Paul Mendy (Quevilly-Rouen/FRA), Piqueti (Sporting Braga/POR), Sana (Academico Viseu/POR), Naní Soares (Falgueiros/POR)
Mastraika: Amido Balde (Maritimo/POR), Abel Camara(Belenenses/POR), Joao Mario (Chaves/POR), Frederic Mendy (Ulsan Hyundai/KOR)
Kocha: Baciro Cande

IVORY COAST
Makipa: Sylvain Gbohouo (TP Mazembe/COD), Ali Badra Sangare (Tanda), Mande Sayouba (Stabaek/NOR)
Mabeki: Serge Aurier (PSG/FRA), Mamadou Bagayoko (Saint-Trond/BEL), Eric Bailly (Manchester Utd/ENG), Simon Deli (Slavia Prague/CZE), Wilfried Kanon (ADO Hague/NED), Lamine Kone (Sunderland/ENG), Adama Traore (Basel/SUI)
Viungo: Victorien Angban (Granada/ESP), Geoffrey Serey Die (Basel/SUI, capt), Cheick Doukoure (Metz/FRA), Franck Kessie (Atalanta Bergamo/ITA), Yao Serge N'Guessan (Nancy/FRA), Jean-Michaël Seri (Nice/FRA)
Mastraika: Wilfried Bony (Stoke City/ENG), Max-Alain Gradel (Bournemouth/ENG), Salomon Kalou (Hertha Berlin/GER), Jonathan Kodjia (Aston Villa/ENG), Nicolas Pepe (Angers/FRA), Giovanni Sio (Rennes/FRA), Wilfried Zaha (Crystal Palace/ENG)
Kocha: Michel Dussuyer (Ufaransa)

MALI
Makipa: Soumaila Diakite, Djigui Diarra (both Stade Malien), Oumar Sissoko (Orleans/FRA)
Mabeki: Mahamadou N'Diaye, Charles Traore (both Troyes/FRA), Ousmane Coulibaly (Panathinaikos/GRE), Salif Coulibaly (TP Mazembe/COD), Mohamed Konate (Berkane/MAR), Youssouf Kone Lille/FRA), Hamari Traore (Reims/FRA), Molla Wague Udinese/ITA)
Viungo: Yves Bissouma (Lille/FRA), Lassana Coulibaly (Bastia/FRA), Moussa Doumbia (Rostov/RUS), Mamoutou N'Diaye (Royal Antwerp/BEL), Samba Sow (Kayserispor/TUR), Yacouba Sylla (Montpellier/FRA, capt), Adama Traore (Monaco/FRA), Sambou Yatabare (Werder Bremen/GER)
Mastraika: Kalifa Coulibaly (Gent/BEL), Moussa Marega (Guimaraes/POR), Bakary Sako (Crystal Palace/ENG), Moustapha Yatabare (Karabukspor/TUR)
Kocha: Alain Giresse (Ufaransa)

MOROCCO
Makipa: Yassine Bounou (Girona/ESP), Yassine El Kharroubi (Lokomotiv Plovdiv/BUL), Munir Mohamedi (Numancia/ESP)
Mabeki: Amine Attouchi (Wydad Casablanca), Mehdi Benatia (Juventus/ITA, capt), Fouad Chafik (Dijon/FRA), Manuel Da Costa (Olympiacos/GRE), Nabil Dirar (Monaco/FRA), Hamza Mendyl (Lille/FRA)
Viungo: Karim El Ahmadi (Feyenoord/NED), Youssef Ait Bennasser (Nancy/FRA), Aziz Bouhaddouz (Saint-Pauli/GER), M’bark Boussoufa (Al Jazira/UAE), Mehdi Carcela (Granada/ESP), Fayçal Fajr (Deportivo Coruna/ESP), Omar El Kaddouri (Napoli/ITA), Mounir Obbadi (Lille/FRA), Romain Saiss (Wolves/ENG)
Mastraika: Rachid Alioui (Nimes/FRA), Youssef El Arabi (Lekhwiya/QAT), Khalid Boutaib (Strasbourg/FRA), Youssef Ennesyri (Malaga/ESP)
Kocha: Herve Renard (Ufaransa)

SENEGAL
Makipa: Abdoulaye Diallo (Caykur Rizespor/TUR), Khadim N'Diaye (Horoya/GUI), Pape Seydou N'Diaye (Niarry Tally)
Mabeki: Saliou Ciss (Valenciennes/FRA), Lamine Gassama (Alanyaspor/TUR), Kalidou Koulibaly (Napoli/ITA), Cheikh M'Bengue (Saint-Etienne/FRA), Kara Mbodj (Anderlecht/BEL), Zargo Toure (Lorient/FRA)
Viungo: Mohamed Diame (Newcastle/ENG), Papakouli Diop (Espanyol/ESP), Idrissa Gueye (Everton/ENG), Cheikhou Kouyate (West Ham/ENG, capt), Papa Alioune Ndiaye (Osmanlispor/TUR), Cheikh N'Doye (Angers/FRA), Henri Saivet (Saint-Etienne/FRA)
Mastraika: Keita Balde (Lazio/ITA), Famara Diedhiou (Angers/FRA), Mame Biram Diouf (Stoke/ENG), Moussa Konate (Sion/SUI), Sadio Mane (Liverpool/ENG), Ismaila Sarr (Metz/FRA), Moussa Sow (Fenerbahce/TUR)
Kocha: Aliou Cisse

TOGO
Makipa: Kossi Agassa (clubless), Cedric Mensah (Le Mans/FRA), Baba Tchagouni (Marmande/FRA)
Mabeki: Serge Akakpo (Trabzonspor/TUR), Vincent Bossou (Young Africans/TAN), Djene Dakonam (Saint-Trond/BEL), Maklibe Kouloun (Dyto), Gafar Mamah (Dacia/MDA), Sadate Ouro-Akoriko (Al Khaleej/KSA), Hakim Ouro-Sama (Port)
Viungo: Lalawele Atakora (Helsingborgs/SWE), Franco Atchou (Dyto), Floyd Ayite (Fulham/ENG), Ihlas Bebou (Fortuna Dusseldorf/GER), Matthieu Dossevi (Standard Liege/BEL), Henritse Eninful (Doxa/GER), Serge Gakpe (Genoa/ITA), Alaixys Romao (Olympiacos/GRE), Prince Segbefia (Goztepe/TUR)
Mastraika: Emmanuel Adebayor (clubless, capt), Komlan Agbeniadan (WAFA/GHA), Razak Boukari (Chateauroux/FRA), Kodjo Fo-Doh Laba(Berkane/MAR)
Kocha: Claude le Roy (Ufaransa)

TUNISIA
Makipa: Moez Ben Chrifia (Esperance), Rami Jeridi (Sfaxien), Aymen Mathlouthi (Etoile Sahel, capt)
Mabeki: Zied Boughattas, Hamdi Nagguez (both Etoile Sahel), Aymen Abdennour (Valencia/ESP), Chamseddine Dhaouadi (Esperance), Slimen Kchok (CA Bizertin), Ali Maaloul (Al-Ahly/EGY), Hamza Mathlouthi (Sfaxien), Mohamed Ali Yaakoubi (Caykur Rizespor/TUR), Syam Ben Youssef (Caen/FRA)
Viungo: Mohamed Amine Ben Amor, Hamza Lahmar (both Etoile Sahel), Larry Azouni (Nimes/FRA), Ahmed Khalil (Club Africain), Wahbi Khazri (Sunderland/ENG), Youssef Msakni (Lekhwiya/QAT), Ferjani Sassi (Esperance), Naim Sliti (Lille/FRA)
Mastraika: Ahmed Akaichi (Ittihad Jeddah/KSA), Saber Khalifa (Club Africain), Taha Yassine Khenissi (Esperance)
Kocha: Henryk Kasperczak (Poland)

UGANDA
Makipa: Salim Jamal (Al Merrikh/SUD), Robert Odongkara (Saint George/ETH), Denis Onyango (Mamelodi Sundowns/RSA)
Mabeki: Timothy Awany, Joseph Ochaya (both KCCA), Shafiq Batambuze (Tusker/KEN), Denis Iguma (Al Ahed/LIB), Isaac Isinde (clubless), Murushid Juuko (Simba/TAN), Nicholas Wadada (Vipers)
Viungo: Khalid Aucho (Baroka/RSA), Mike Azira (Colorado Rapids/USA), Geoffrey Kizito (Than Quang Ninh/VIE), William Kizito (Rio Ave/POR), Tony Mawejje (Throttur/ISL), Hassan Wasswa (Nijmeh/LIB),Moses Oloya (Hanoi T and T/VIE), Godfrey Walusimbi (Gor Mahia/KEN)
Mastraika: Geoffrey Massa (Baroka/RSA, capt), Farouk Miya (Standard Liege/BEL), Yunus Sentamu (Ilves/FIN), Geofrey Sserunkuma (KCCA), Muhammad Shaban (Onduparaka)
Kocha: Milutin Sredojevic (Serbia)

ZIMBABWE
Makipa: Donovan Bernard (How Mine), Takabva Mawaya (ZPC Kariba), Tatenda Mkuruva (Dynamos)
Mabeki: Teenage Hadebe, Lawrence Mhlanga (both Chicken Inn), Onismor Bhasera (SuperSport Utd/RSA), Bruce Kangwa (Azam/TAN), Oscar Machapa (V Club/COD), Elisha Muroiwa (Dynamos), Costa Nhamoinesu (Sparta Prague/CZE), Hardlife Zvirekwi (CAPS Utd)
Viungo: Kudakwashe Mahachi, Danny Phiri (both Golden Arrows/RSA), Khama Billiat (Mamelodi Sundowns/RSA), Willard Katsande (Kaizer Chiefs/RSA, capt), Marvelous Nakamba (Vitesse Arnhem/NED)
Mastraika: Tinotenda Kadewere (Djurgardens/SWE), Cuthbert Malajila (Wits/RSA), Nyasha Mushekwi (Dalian Yifang/CHN), Knowledge Musona (Ostend/BEL), Tendai Ndoro (Orlando Pirates/RSA), Evans Rusike (Maritzburg/RSA), Mathew Rusike (CS Sfaxien/TUN)
Kocha: Kallisto Pasuwa

Makundi yapo hivi:



Ratiba ipo hivi:
Jumamosi 14 Januari 2017


   
Gabon v Guinea-Bissau Stade d'Angondje 18:00
Burkina Faso v Cameroon Stade d'Angondje 21:00
Jumapili 15 Januari 2017
       
Algeria v Zimbabwe Stade de Franceville 18:00
Tunisia v Senegal Stade de Franceville 21:00
Jumatatu  16 Januari 2017
       
Cote d'Ivoire v Togo Stade d'Oyem 18:00
DR Congo v Morocco Stade de Franceville 21:00
Jumanne  17 Januari 2017
       
Ghana v Uganda Stade de Port Gentil 18:00
Mali v Egypt Stade de Port Gentil 21:00
Jumatano 18 Januari 2017
       
Gabon v Burkina Faso Stade d'Angondje 18:00
Cameroon v Guinea-Bissau Stade d'Angondje 21:00
Alhamis  19 Januari 2017
       
Algeria v Tunisia Stade de Franceville 18:00
Senegal v Zimbabwe Stade de Franceville 21:00
Ijumaa  20 Januari 2017
       
Cote d'Ivoire v DR Congo Stade d'Oyem 18:00
Morocco v Togo Stade d'Oyem 21:00
Jumamosi 21 Januari 2017
       
Ghana v Mali Stade de Port Gentil 18:00
Egypt v Uganda Stade de Port Gentil 21:00
Jumapili 22 Januari 2017
       
Guinea-Bissau v Burkina Faso Stade de Franceville 21:00
Cameroon v Gabon Stade d'Angondje 21:00
Jumatatu  23 Januari 2017
       
Senegal v Algeria Stade de Franceville 21:00
Zimbabwe v Tunisia Stade d'Angondje 21:00
Jumanne  24 Januari 2017
       
Togo v DR Congo Stade de Port Gentil 21:00
Morocco v Cote d'Ivoire Stade d'Oyem 21:00
Jumatano 25 Januari 2017
       
Egypt v Ghana Stade de Port Gentil 21:00
Uganda v Mali Stade d'Oyem 21:00





































































Barcelona, Real Madrid zatenganishwa

BAADA ya mechi za marudiano ya Kombe la Mfalme (Copa del Rey), droo ya Nane Bora ya michuano hiyo ya nchini Hispania imetoka, huku vigogo Barcelona na Real Madrid zikitenganishwa kwenye hatua hiyo.
Katika droo hiyo Real Sociedad itavaana na Barcelona, wakati Real Madrid wakipewa Celta Vigo wakianzia nyumbani, huku Alcorcon itamalizna na Alaves na Atletico Madrid itakwaruzana na Eibar.
Mechi hizo kwa mujibu wa ratiba zitaanza kuchezwa Januari 18-19 na marudiani zitachezwa kati ya Januari 25/26 kwa ajili ya kupata timu za kutinga nusu fainali.
Katika hatua hiyo ya Nane Bora ni klabu moja tu ya Ligi Daraja la Pili ya Alcorcon iliyopenya na zilizosalia zipo La Liga.

Ratiba kamili ipo hivi:

Real Sociedad   v Barcelona
Alcorcon           v Alaves
Atletico Madrid  v Eibar
Real Madrid      v Celta Vigo

Taifa Stars, Uganda The Cranes hapatoshi Afcon 2019

Kikosi chja Tanzania
Droo ya kuwania fainali za Afcon 2019
DROO ya kuwania fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa mwaka 2019 zitakazofanyika nchini Cameroon imefanyika jana usiku na Tanzania kuwekwa kundi moja pamoja na Uganda, Cape Verde na Lesotho.
Tanzania ambayo haijashiriki fainali hizo tangu mwaka 1980 kama itakomaa katika maandalizi mazuri inaweza kusonga mbele kwani safari hii kundi lao sio tishio kama ilivyokuwa katika mbio za  kwenda Afcon 2017.
Katika mbio Tanzania ilipangwa na vigogo Misri, Nigeria na Chad kabla nchi hii haijajitoa kundini.
Katika droo hiyo Kenya pia itaanzia hatua ya makundi, ikiwa imepangwa Kundi F pamoja na Ghana, Ethiopia na Sierra Leone, wakati Rwanda ipo Kundi H pamoja na Ivory Coast, Guinea na Afrika ya Kati (CAR).
Mshindi wa kila kundi atafuzu moja kwa moja AFCON ya 2019, wakati timu nyingine tatu zitakazomaliza nafasi ya pili na wastani mzuri zaidi ya nyingine zitafuzu kama washindi wa pili bora.
Michuano hiyo itaanzia kwa hatua ya mchujo, Raundi ya Awali itakayohusisha timu za Comoro, Djibout, Madagascar, Mauritius, Sao Tome E Principe na Sudan Kusini.
Timu zitakazofuzu hapo zitaingia moja kwa moja kwenye makundi A, B na C kukamilisha idadi ya timu nne nne. Kundi Ab lina timu za Senegal, Equatorial Guinea na Sudan, B kuna wenyeji Cameroon, Morocco na Malawi na C kuna Mali, Gabon n Burundi.
Cameroon ikiongoza Kundi, mshindi wa pili atafuzu moja kwa moja na kama itashika nafasi ya tatu au ya nne, mshindi wa kwanza atafuzu moja kwa moja na mshindi wa pili atawania nafasi tatu za ziada za kufuzu kama mmoja wa washindi wa pili bora.
Hatua ya mchujo itachezwa kati ya Machi 20 na 28 wakati mechi za kwanza za makundi zitaanza Juni 5 na 13, za pili Machi 19 na 27 2018, za tatu Septemba 3 na 11, 2018 za nne Oktoba 8 na 16, 2018 na za tano Novemba 5 na 13, 2018.
Mbali za Afcon 2019 Tanzania pia itakuwa na kibarua cha kuwania fainali za Chan 2018 zitakazofanyika nchi ya Kenya.

Thursday, January 12, 2017

SIMBA, AZAM NI ZAIDI YA VITA KOMBE LA MAPINDUZI 2017

Kikosi cha Simba
Wababe wa Chamazi, Azam FC
Na Rahma White
HABARI ndio hiyo. Leo Alhamisi ndio kilele cha sherehe za Mapinduzi, ukiwa ni mwaka wa 53, lakini kazi bwana ipo kesho kwenye Uwanja wa Amaan.
Unajua nini? Wekundu wa Msimbazi, Simba kesho itavaana na Matajiri wa Azam kwenye pambano la fainali za michuano ya Kombe la Mapinduzi 2017.
Sasa kama ulikuwa haujui ni kwamba Simba ndio klabu iliyotwaa Kombe la Mapinduzi mara nyingi, ikifanya hivyo mara tatu tangu lianze kuchezwa kwa mfumo wa sasa. Pia Simba ndio klabu iliyotinga mara nyingi kwenye fainali  ambapo pambano lao la kesho dhidi ya Azam litakuwa ni la sita sita ikiiacha Mtibwa Sugar waliokuwa wakilingana nao ambayo msimu haikualikwa.
Vinara hao wa Ligi Kuu Bara kesho itavaana na Azam klabu inayofuata kwa kulibeba taji hilo mara nyingi nyuma ya Simba, ikilitwaa mara mbili tena ikiwa klabu pekee kuwahi kulitetea ikifanya hivyo mwaka 2012 na 2013.
Simba imefika hatua hiyo ya fainali za mwaka huu kwa kuitambia Yanga kwa mikwaju ya penalti 4-2 baada ya kumaliza dakika 90 la pambano lao bila milango ya timu hiyo kuguswa, huku Azam ikifika hatua hiyo kwa kuing'oa Taifa Jang'ombe kwa bao 1-0.
Azam ndio klabu ambayo mpaka inafika fainali wavu wake haujaguswa ikiweka rekodi, huku Simba ikifuata ikiruhusu bao moja tu.
Kwa mnasaba huo fainali ya kesho itakuwa tamu ile mbaya kwani, licha ya kila timu kusaka heshima ya kulibeba taji hilo, lakini pia zinataka kuonyesha nani mkali zaidi katika suala zima la kulinda lango lao.
Mchezo huo wa kesho una uhondo zaidi kwenye eneo la kiungo ambako klabu zote zinatambia mafundi walionao ambao wamezifanya kuwa kali katika kuzuia na kushambulia.
Makocha wa pande zote wamekuwa wakijinasibu timu zao kuibuka na ushindi, lakini kwa kulinganisha na rekodi zilizopo ni lazima Simba iwe makini mbele ya Azam ambao waliistaajabisha Yanga kwa kuipiga mabao 4-0.
Ingawa mpaka sasa kwenye michuano hiyo ya Mapinduzi, Azam imekuwa wanyonge wa Simba, lakini kwa namna walivyoizima Yanga ni wazi Simba isiende kichwa kichwa Uwanja wa Amaan kama wanataka kurejesha taji lao hilo walilolipoteza mwaka jana na kuliacha likibebwa na URA ya Uganda.
Kocha Msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja amekiri pambano litakuwa gumu, lakini kubwa wanachotaka ni kurudi jijini Dar es Salaam na taji hilo, huku Idd Nassor 'Cheche' akiamini hakuna cha kuwazuia kubeba Kombe la mwaka huu.
Vikosi vya timu hizo vinatarajiwa kuwa hivi;
AZAM: Aishi Manula, Shomari Kapombe, Gadiel Michael, Yakub Mohammed, Aggrey Morris, Stephan Kingue, Salum Abubakar, Frank Domayo, John Bocco, Yahya Mohammed na Joseph Mahundi.
SIMBA:
Daniel Agyei, Janvier Bokungu, Mohammed Hussein, Abdi Banda, Method Mwanjali, Jonas Mkude, Shiza Kichuya, Mzamiru Yasin, Juma Liuzio, Mohammed Ibrahim na James Kotei.

Mabingwa wa Mapinduzi

2007-Yanga
2008-Simba
2009-Miembeni
2010-Mtibwa Sugar
2011-Simba
2012-Azam
2013-Azam
2014-KCCA
2015-Simba
2016-URA
2017-  ''

Utamu wa Ligi Kuu Bara umerudi tena

JKT Ruvu
Toto Africans
Ruvu Shooting
Na Rahim, Junior
ACHANA na pambano la kesho la fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi,
itakayozikutanisha Simba na Azam kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar, unaambiwa utamu wa Ligi Kuu Bara nao unarudi rasmi wikiendi hii.
Ligi hiyo iliyokuwa mapumziko ya wiki kama mbili hivi, inarudi kwa michezo itakayochezwa mfululizo kuanzia leo mpaka Jumatano.
Wapinzani wa jadi, maafande wa JKT Ruvu na Ruvu Shooting zinatarajiwa kumaliza ubishi katika pambano linalosubiriwa kwa hamu kwenye Uwanja wa Mabatini, ulioko Mlandizi mkoani Pwani.
Pambano hilo la kisasi linafanyika huku kila timu ikiwa katika hali tofauti, JKT Ruvu wakiwa hoi mkiani, huku wapinzani wao angalau wakipumua maeneo ya juu na wanatambia ushindi wa bao 1-0 iliyopata katika mechi yao ya kwanza.
Kwa mujibu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ligi hiyo itaendelea Jumamosi kwa pambano jingine la 'derby' ya Mkoa wa Shinyanga kati ya Stand United na Mwadui  zitakazovaana kwenye Uwanja wa Kambarage mjini humo, huku kukiwa hakuna mbabe wa mechi ya awali.
Jumamosi pia kutakuwa na mtanange mwingine mkali wa Kagera Sugar itakayokuwa mwenyeji wa Ndanda ya Mtwara kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Utamu utaendelea tena Jumapili kwa mchezo mmoja tu ambapo Mbao itaialika African Lyon ya Dar kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Kivumbi cha ligi hiyo inayoingoa raundi ya nne ya duru la pili, itaendelea tena Jumatatu kwa mchezo mmoja tu kati ya Prisons Mbeya itakayokuwa mgeni wa Toto Africans kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Michezo mitatu ambayo ilikuwa haijapangiwa tarehe hapo awali kwa alama ya TBA ikiwa na maana ya kutajwa baadaye (To Be Announced), tayari Bodi ya Ligi, chombo cha TFF, kinachosimamia na kuendesha ligi, imepanga tarehe.
Jumanne ya Januari 17, 2017, Yanga itakuwa ugenini mjini Songea kuvaana na Majimaji kwenye Uwanja wa Majimaji na siku inayofuata yaani Jumatano, Mtibwa Sugar itakayocheza na Simba kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro wakati Azam itakuwa mwenyeji wa Mbeya City Uwanja wa Azam Complex.
Mchezo huu wa Azam na Mbeya City umepangwa kuanza saa 1.00 usiku wakati michezo yote tajwa hapo juu itaanza saa 10.00 jioni lengo likiwa ni kutoa nafasi kwa mashabiki kushuhudia mechi nyingi kupitia Kituo cha runinga cha Azam.

Ratiba ya VPL imekaa hivi;
 
Jan 13, 2017   
JKT Ruvu v Ruvu Shooting

Jan 14, 2017Stand United v Mwadui
Kagera Sugar v Ndanda

Jan 15, 2017Mbao v African Lyon

Jan 16, 2017
Toto Africans v Prisons

Jan 17, 2017Majimaji v Yanga

Jan 18, 2017Mtibwa Sugar v Simba
Azam v Mbeya City
 

Zaha aanza mambo Ivory Coast ikiilipua Uganda x3

Straika Serge Aurier akishangilia bao la tatu la Tembo ya Afrika dhidi ya Uganda The Cranes
STRAIKA Wilfried Zaha akiichezea Ivory Coast kwa mara ya pili tangu alipoikana England, ameanza kuonyesha cheche zake baada ya kufunga bao lake la kwanza kwa Tembo hao wa Afrika wakiichapa Uganda kwa mabao 3-0.
Pambano hilo lilikuwa la kirafiki la kimataifa kujiandaa na michuano ya Afcon 2017 inayoanza wikiendi hii na lilichezwa nchini Ivory Coast na kushuhudia mpaka mapumziko hakuna timu iliyoona lango la mwenzake.
Zaha anayeichezea Crystal Palace wa England,  alifunga hilo katika dakika ya 58, ikiwa ni la pili kwa timu yake kwani dakika saba nyuma yake Jonathan Kodjia kuifungia Ivory Coast bao la kwanza.
Bao jingine la Serge Aurier katika dakika ya 72 na kuwazamisha wawakilishi wa ukanda wa Cecafa, Uganda ambayo inaends Gabon ikiwa ni mara ya kwanza tangu miaka 38 iliyopita waliposhiriki fainali hizo za Afrika.
Katika mechi nyingine ya kimataifa za kirafiki kwa maandalizi ya Afcon 2017 itakayochezwa Gabon kuanzia wikiendi hii, Senegal iliitambia Congo kwa mabao 2-0.

Liverpool majanga, yapigwa kidude na Southampton

Nathan Redmond akishangilia bao lake alililowatungua Liverpool usiku wa jana kwenyer Uwanja wa St Mary's katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Ligi (EFL)
LIVERPOOL imekwama aisee, baada ya usiku wa kuamkia leo kuchapwa bao 1-0 na Southampton katika mechi ya Nusu Fainali ya kwazna Kombe la Ligi.
Kwa ushindi huo, Southampton imejiweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele kama itafanya kweli kwenye mechi ya marudiano ugenini Januari 25.
Bao lililowazamisha vijana wa Jurgen Klopp liliekwa kimiani na Nathan Redmond katika dakika ya 20 katika mchezo huo mkali uliopigwa kwenye Uwanja wa St. Mary's mjini Southampton.
Kipigo hicho cha Liverpool kimekuja siku chache tangu walipong;anganiwa na timu ya daraja la chini ya Plymouth katika mechi tya raundi ya tatu ya Kombe la FA ambao watarudiana nao Januari 18.
Wikiendi hii Liverpool itakuwa na kibarua kigumu mbele ya Man United ambayo juzi iklipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Hull City katika mechi ya kwanza ya nusu fainali ya Kombe la Ligi na kujiweka pazuri kutinga fainali.
Vijana wa Klopp watakuwa na wiki ngumu kwa kutakiwa kucheza mfululizo mara baada ya kuumana na Man United Jumapili hii.