| Ronaldo na El Shaarawy wakichuana |
| Beki wa Madrid Nacho akimdhiobiti mchezaji wa AC Milan |
![]() |
| Karim Benzema akifunga bao la pili la Madrid kwa mkwaju wa penati |
El Shaarawy alifunga mabao mawili katika kipigo hicho kilichokuwa cha kwanza kwa vijana wa Carlo Ancelotti tangu Septemba na kuhitimisha 'ubabe' wa Madrid ambao walikuwa hawajapoteza mchezo wowote katika mechi 22 katika msimu huu.
Jeremy Menez wa Milan ndiye aliyeanza kufungua milango baada ya kufunga bao la kuongoza katika dakika ya 24 kabla ya El Shaarawy kuongeza goli la pili katika dakika 31 kwa shuti kali.
Dakika nne baadaye Madrid walifanikiwa kuchomoa bao moja kupitia kwa Mwanasoka Bora Duniani, Cristiano Ronaldo kufunga akiwa ndani ya 'boksi' akimtungua kipa Diego Lopez na kuzifanya timu ziende mapumziko Milan wakiwa mbele kwa mabao 2-1.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na kushuhudiwa Milan wakiongeza bao la tatu dakika ya 49 kupitia tena kwa El Shaarawy kabla ya watokea benchi Giampaolo Pazzini na M'Baye Niang kushirikiana vyema na na Pazzini kuukwamisha mpira kimiani katika dakika ya 73 kuaindikia Milan bao la nne.
Real Madrid ilijipatia bao la pili la kujifutia machozi kupitia mshambuliaji wake wa Kifaransa Karim Benzema, aliyefunga bao kwa mkwaju wa penalti katika dakika ya 84.
Kwa ushindi huo AC Milan walikabidhiwa kombe lililopokewa na nahodha wake, Riccardo Montolivo.

























PAMBANO la kukata na shoka baina ya Yanga na Azam limemalizika matokeo yakiwa ni yale yale ya mabao 2-2 na kuendelea kuwa nyuma ya Mtibwa Sugar wanaoongoza msimamo.
TIMU ya soka ya Mbao ya Mwanza imekamata uongozi wa Kundi B la michuano ya Ligi Daraja la Pili (SDL) baada ya jana (Desemba 27 mwaka huu) kuizamisha JKT Rwamkoma ya Mara mabao 2-1.
MSHAMBULIAJI wa klabu ya Barcelona, Pedro amedai kuwa mchezaji mwenzake Lionel Messi ndiyo mchezaji bora kuliko yeyote duniani na anastahili kushinda tuzo ya Ballon d’Or mbele ya Cristiano Ronaldo. Messi amewahi kushinda tuzo hiyo kwa mara nne mfululizo kabla ya Ronaldo kuingilia kati na kunyakua tuzo hiyo mwaka jana ikiwa ni mara ya pili kwa upande wake.





KOCHA wa timu ya taifa ya Cameroon, Volke Finke ametaja kikosi cha awali cha wachezaji 27 kwa ajili ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika itakayofanyika huko Guinea ya Ikweta.