 |
Dk Ndumbaro |
KAMATI
ya Uchaguzi ya Simba imemuondoa kwa mara nyingine Michael Wambura
kutokana na kufanya kampeni kabla ya wakati huku akiwa ameonywa.
Pia
imesisitiza uchaguzi utafanyika Juni 29 kama ilivyopangwa kwa kuwa Rais
wa TFF, Jamal Malinzi aliyetangaza kuusimamisha, hana mamlaka hayo
kikatiba.
Mwenyekiti
wa kamati hiyo, mwanasheria na wakili maarufu nchini, Dokta Damas
Daniel Ndumbaro 'DDN' ndiye amefunga na kusema hayo.
Ndumbaro
amemwaga ripoti kamili ambayo inachambua mambo yote huku ikionyesha
kiasi gani Malinzi hana haki ya kusitisha uchaguzi huo kama
alivyotangaza jana.
IFUATAYO NDIYO RIPOTI KAMILI YA DAKTARI HUYO WA SHERIA NCHINI:
Kamati
ya Uchaguzi ya Simba Sports Club, ilifanya mkutano wake kawaida tarehe
15 Juni 2014 kujadili mambo mbalimbali ambayo yanayohusu uchaguzi mkuu
wa Simba Sports Club ambao umepangwa kufanyika tarehe tarehe 29 Juni
2014. Kamati ya Uchaguzi ya Simba sports Club inapenda kuujulisha umma,
hususan wapenzi wa Simba Sports Club mambo yafuatayo:
1. Kamati
ya Uchaguzi ya Simba Sports Club, kwa mujibu wa Ibara ya 10(6) ya
Kanuni za uchaguzi za TFF toleo la mwaka 2013, ndiyo chombo pekee chenye
mamlaka ya kutangaza, kubadilisha, kusimamisha au kufuta tarehe ya
Uchaguzi ya Simba Sports Club. Kwakuwa Kamati haijafanya hivyo, wala
hakuna mdau yoyote aliyeleta hoja ya kusimamisha uchaguzi, tunawajulisha
kuwa uchaguzi wa Simba Sports Club upo pale pale kama ambayo Kamati ya
Uchaguzi ya Simba Sports Club ilivyopanga. Maandalizi ya uchaguzi huo
yanaendelea vema na Uchaguzi utafanyika tarehe 29 Juni 2014 kama
ilivyopangwa hapo awali.
2. Kamati
imesikia kupitia vyombo vya habari kuwa TFF imesimamisha uchaguzi wa
Simba Sports Club mpaka hapo Kamati ya Utendaji ya Simba Sports Club
itakapoteua Kamati ya Maadili. Kamati ya Uchaguzi ya Simba Sports Club
inapenda kusema yafuatayo:
i. Mamlaka
ya kusimamisha uchaguzi ni kazi ya Kamati ya Uchaguzi ya Simba Sports
Club kwa mujibu wa ibara 10 (6) ya Kanuni za Uchaguzi, 2013
ii. Kamati
ya Uchaguzi ya Simba Sports Club ilipoanza mchakato wa uchaguzi ilitoa
tamko kuwa: “kwasababu Simba Sports Club haina kanuni za Uchaguzi,
Kamati ya Rufaa ya uchaguzi, wala Kamati za Maadili kwa mujibu wa ibara
za 16 (e) na (f) ya Katiba ya Simba Mwaka 2014, vyombo husika vya TFF
vitatumika”. Kulikuwa hakuna pingamizi toka kwa mtu yoyote juu ya kauli
hiyo, ikiwemo TFF.
iii. Tarehe
26 Mei 2013, Rais wa TFF aliialika Kamati ya Uchaguzi ya Simba Sports
Club katika chakula cha mchana. Katika mkutano huo, kauli ya aya (ii)
hapo juu ilirejewa na Kamati ya Uchaguzi ya Simba Sports Club ilikabidhi
rasmi mchakato mzima wa uchaguzi na kutoa ufafanuzi kuwa kamati husika
za TFF zitahusika, jambo ambalo halikupingwa na TFF.
iv. TFF
iliruhusu Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF kusikiliza Rufaa za
uchaguzi za Simba, hivyo basi haiwezi kuzuia Kamati zake nyingine
kusikiliza Masuala ya kimaadili. “Estopel” inawazuia TFF kufanya hivyo
sasa.
v. Wajumbe
wote wa Kamati ya Utendaji ya Simba Sports Club, isipokuwa watatu tu,
ni wagombea katika uchaguzi huu. Na hao watoto tayari wapo kwenye Kambi
za Kampeni za uchaguzi hii ambazo zipo bayana kabisa. Kuiagiza Kamati ya
Utendaji ya Simba iunde Kamati ya Maadili kusikiliza kesi za maadili
dhidi yao wenyewe ni kukiuka msingi wa haki ya asili (natural justice).
Ni dhahiri kuwa haki haiwezi kutendeka kwa wajumbe wa kamati ya utendaji
ya Simba Sports Sports Club, ambao ni watuhumiwa katika masuala ya
maadili, wachague majaji wa kuwahukumu. Hapo haki haitatendeka.
Ifahamike
kuwa, baada ya Kamati ya Utendaji ya Simba Sports Club kuteua Kamati ya
uchaguzi ya Simba Sports Club, Kamati hiyo haina mamlaka tena ya
kujadili, kuingilia au kuteua chombo kingine kufanya shughuli zinazohusu
uchaguzi ukizingatia kuwa wajumbe wake ni wagombea.
vi. Katika
Uchaguzi Mkuu wa TFF wa Mwaka 2013, ambao ulimuingiza Jamal Malinzi
Madarakani, FIFA walikuja, wakongea na pande zote na hatimaye, walisema
kuwa; “tunapendekeza kuwa uchaguzi mkuu usimame ili kuunda kamati
mbalimbali”. Mapendekezo hayo yalipokelewa na Kamati ya Uchaguzi ya TFF,
Bw. Deo Lyato, na hatimaye ni Kamati ya Uchaguzi ya TFF ndio
iliyotangaza kusimamisha Uchaguzi na sio Sepp Blatter.
vii. Kamati
ya Uchaguzi ya Simba Sports Club ni Kamati huru ambayo haipaswi
kuingiliwa na Chombo chochote kile. Ili kulinda uhuru huo, tunalazimika
kukanusha matamshi ya TFF kuhusu kusitisha Uchaguzi Mkuu wa Simba Sports
Club.
3. Malalamiko ya Kimaadili Kupelekwa FIFA.
Kwa
mujibu wa Ibara ya 11 (9) ya Kanuni za Uchaguzi za TFF, 2013, inatoa
mamlaka kwa Kamati ya Uchaguzi ya Simba Sports Club kupeleka masuala ya
maadili katika kamati ya maadili ya TFF. Tarehe 9 Juni 2014, Kamati ya
Uchaguzi ya Simba Sports Club ilipeleka Masuala ya Maadili katika Kamati
ya Maadili ya TFF. Kwakuwa TFF imekataa kusikiliza masuala ya maadili
ambayo yanakiuka Kanuni za maadili, Katiba za Simba, TFF na FIFA, Kamati
ya Uchaguzi ya Simba Sports Club, itapeleka Masuala ya Maadili FIFA ili
haki itendeke.
4. Kamati
ya Uchaguzi ya Simba Sports Club ilijadili kuhusu vitendo vya wagombea
kupiga kampeni kabla ya muda wa kampeni ulioruhusiwa. Kwa mujibu wa
Mchakato wa Uchaguzi ya Simba Sports Club, muda wa kampeni unaanza
tarehe 24 -28 Juni 2014. Hapo awali kamati ilibaini kuwa wagombea wawili
wa nafasi ya urais; Michael Richard Wambura na Evans Aveva walifanya
vitendo vya kampeni siku ya kuchukua na kurejesha fomu za kugombea.
Tarehe 25 Mei 2014, Kamati iliwapa ONYO KALI la maandishi wagombea hao
na kuwataarifu kuwa hatua kali zaidi zitachukuliwa dhidi yao, ikiwemo
kuondolewa katika kinyang’anyiro cha uchaguzi.
Baada
ya Kamati ya Uchaguzi ya Simba Sports Club kumuondoa Bw. Michael
Richard Wambura katika kinyang’anyiro cha uchaguzi Mkuu wa SImba Sports
Club, Bw. Wambura aliitisha Mkutano na waandishi wa habari, aliitukana
Kamati ya Uchaguzi ya Simba Sports Club, na kutoa matamshi ambayo ni
Kampeni.
Baadaya
ya Kamati ya Rufaa ya uchaguzi ya TFF kumrejesha Bw. Wambura katika
Kinyang’anyiro cha Uchaguzi Mkuu wa Simba, Bw. Wambura aliitisha tena
mkutano wa waandishi wa habari, aliisifu kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya
TFF, kwa mara kwanza aliisifu Kamati ya Uchaguzi ya Simba Sports Club na
kutoa matamshi ambayo ni wazi kuwa ni kampeni. Baadhi ya Matamshi
aliyoyatoa kupitia vyombo vya habari ni kama ifuatavyo:
i. “Simba Sports Club inahitaji zaidi wadhamini na sio wafadhili”
ii. “Wafadhili kazi yao in kutoa fedha mfuko wa kushoto na kuepeleka mfuko wa kulia”
iii. “Simba ilikuwa na viwanja vitatu lakini kimoja kimeuzwa na wajanja na vimebaki viwili tu”
Kamati
ya Uchaguzi ya Simba Sports Club ilitafakari matamshi hayo, na kubaini
kuwa hiyo ni kampeni ya waziwazi wakati muda wa kampeni bado haujaanza.
Kamati
ya Uchaguzi ya Simba Sports Club ililipa jambo ili uzito wa kipekee
kwasababu Mkosaji amekuwa na tabia ya kurudia kosa hilo hata baada ya
kupewe onyo la maandishi.
HIVYO
BASI: Kwa mujibu wa mamlaka ya kikanuni, hususan Ibara za: 6 (1) (a) –
(g); 6 (1) (L) na 14(3) za Kanuni za uchaguzi za TFF – 2013, Bw. Michael
Richard Wambura anaondolewa Katika Kinyang’anyiro cha Uchaguzi wa Simba
Sports Club, 2013, kwa kosa la kurudia kufanya kampeni kabla ya muda wa
kampeni ambao umepengwa."