STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, November 7, 2014

Spurs, Everton yapeta Ligi Ndogo Ulaya, 2 zikifuzu mtoano

Benjamin Stambouli (left) and Asteras' Pablo Mazza battle for the ball at the Theodoros Kolokotronis Stadium
Kizaazaa katika pambano la Spurs wakati ikishinda 2-1
Andros Townsend opened the scoring for the English side converting a penalty he won after being fouled in the box
Andors Townsend akifunga bao la kwanza la Spurs
Phil Jagielka akishangilia bao la pili la Everton
Osmond akishangilia bao la kuongoza la Everton nyumbani jana dhidi ya Lille
32min: Mind you, Osman is looking handy now as his cross results in Lukaku glancing a header just off target.
Naismith akifunga bao la tatu la Everton jana
Lukaku akimiliki mpira mbele ya mchezaji wa Lille
TIMU za soka za Tottenham Hotspur na Everton za England zimeendelea kutamba kwenye michuano ya Ligi Ndogo ya Ulaya (UEFA Europe League) baada ya kupata ushindi katika mechi za zilizochezwa viwanja tofauti.
Everton ikiwa nyumbani Goodson Park, walipata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Lille ya Ufaransa katika mechi ya kundi H na kuwafanya wasaliwe pointi chache kabla ya kufuzu hatua ya mtoano.
Mabao ya washindi yaliwekwa kimiani na leon Osman katika dakika ya 27, Phil Jagielka Dk 42 na la kipindi cha la Steven Naismith.
Everton imefikisha pointi nane sawa na Wolfsburg wanaoshika nafasi ya pili nyuma yao.
Nayo Spurs ikiwa ugenini  nchini Ugiriki ilipata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Asteras Tripolis na kuongoza kundi C.
Andors Townsand alifunga bao la kuongoza dakika ya 36 kwa mkwaju wa penati kabla ya Harry Keane kufunga bao lake la nane katika mechi nane za Spurs dakika ya 42.
Wenyeji walipata bao la kufutia machozi katika dakika ya 90 huku Spurs ikimpoteza Feredico Fazio kwa mchezo mbaya.
Katika michezo mingine Dinamo Moscow ilipata ushindi wa bao 1-0 na kujihakikishia tiketi ya kucheza hatua inayofuata kwa kuilaza Estoril, huku Qarabağ ikikubali kipigo nyumbani cha mabao 2-1 dhidi ya Dnipro Dniprop.
Zürich ilishinda nyumbani mabao 3-2 dhidi ya Villarreal, Apollon ililala 2-0 nyumbani mbele ya Borussia M'gla.
HJK  nayo ilitakata kwao kwa kuilaza Torino kwa mabao 2-1, huku    København ilifumuliwa kwao kwa mabao 4-0 na Club Brugge wakati
Beşiktas ilishinda nyumbani 2-1 dhidi ya Partizan.
Mechi nyingine zilishuhudia Astra na Celtic zikitoshana nguvu kw akufungana bao 1-1,         Dinamo Zagreb ikilala kwao kwa mabao 5-1 mbele ya Salzburg na     Panathinaikos ikafungwa mabao 3-2 na PSV.
Timu ya Saint-Étienne na Inter Milan zilifungana bao 1-1, huku Feyenoord ikiitambia wageni wao Rijeka kwa mabao 2-0, Sevilla ikiwa nyumbani ikailaza Standard Liège mabao 3-1 na
Wolfsburg ikaicharaza Krasnodar kwa mabao 5-1 na Sparta Prague ikaicharaza Slovan Bratislava kwa mabao 4-0.
Napoli ya Italia ikiwa nyumbani iliitambia Young Boys kwa mabao 3-0 na  Dynamo Kiev     ikashinda nyumbani kwa mabao 2-0 dhidi ya AaB, nayo Rio Ave na Steaua Bucharest zilitoka sare ya 2-2, Guingamp ikashinda 2-0 dhidi ya Dinamo Minsk, huku Fiorentina na PAOK zikifungana bao 1-1 kama ilivyokuwa kwa timu za Lokeren na Trabzonspor, huku Legia Warszawa     iliifunga mabao 2-1 Metalist.

Sikia Uzushi Huu Eti, Mwisho wa Dunia 2032

http://straphaelcc.org/pictures/Curious%20Catholic/the-end-of-the-world-2012.jpg
Picha za Propaganda za kutaka kuwaaminisha watu kwamba Wanasayansi wamebaini Dunia imefika mwishoni kinyume na mafundisho ya dini kwamba anayeijua siku hiyo na Mungu pekee
 http://i.telegraph.co.uk/multimedia/archive/02433/_end-of-the-world_2433119b.jpgWAKATI mafundisho wa dini za Kiislam na Ukristo ukiweka bayana kwamba HAKUNA AIJUAYE Siku wala Saa, kwani ANAYEFAHAMU Siri ya MWISHO WA DUNIA ni MUNGU MUUMBA (ALLAH SW), Wanasayansi wameibuka na kudai kuwa Mwisho wa dunia unatarajiwa kuwa mwaka 2032.
Tarifa hiyo inakuja wakati binadamu wakiendelea na mipango yao ya kuifanya dunia kuwa sehemu salama ya kuishi kimazingira, kiulinzi na usalama.
Utabiri mpya wa kutisha unaonesha kuwa mwaka 2032 ndiyo mwisho wa sayari hii ya tatu katika mfumo wa jua. Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali katika mitandao ya internet, Sayari iitwayo Nibiru, ambayo kisayansi inafahamika kama Planet X ipo njiani kuigonga dunia na hivyo kusababisha majanga mbalimbali kutokea.
ITAONEKANA ANGANI KAMA MWEZI
Kwa mujibu wa mitandao hiyo ya kisayansi, sayari hiyo ambayo inaisogelea dunia kwa kasi kubwa, itaonekana kubwa na angavu wakati wa usiku angani na kuwa katika umbo la mwezi na hivyo kufanya miezi ionekane miwili.
DALILI KWAMBA IPO JIRANI
Taarifa zaidi za kisayansi zinasema kuwa, kadiri sayari hiyo inavyozidi kusogea, dunia itaanza kutikisika na kusababisha matetemeko ya ardhi kuongezeka sehemu mbalimbali. Mbali na dunia kutikisika na matetemeko, milipuko ya volcano nayo itatokea huku idadi kubwa ya milipuko hiyo mipya ikiongezeka, vimbunga vikubwa kama Tsunami vitaibuka na mwishowe dunia itapigwa na bomu la miamba midogo na vimondo kutokea angani.
DUNIA ITAKUMBWA NA GIZA NENE
Wakati volcano zote duniani zitakapoanza kulipuka na zingine mpya kujitokeza, dunia itafunikwa na giza nene  na matope kwa wakati wote wa usiku na mchana huku watu wakitakiwa kusoma maandiko na mafundisho ya Mitume walioyafunua kwenye vitabu vikieleza wasifu huo.
NI TUKIO LA AINA YAKE KARNE YA 21
Nibiru inatajwa kama kitu kinachoisogelea dunia kinachoaminiwa kusababisha madhara makubwa ambapo kama hakitaigonga dunia, kitasababisha mtikisiko usio wa kawaida kitakapopishana nayo. Baadhi ya wanasayansi wanaamini kuwa kitendo hicho kitatokea mapema katika karne ya 21 (tuliyonayo sasa). WANASAYANSI WAPINGANA
Baadhi ya wanasayansi wanapinga kwa maelezo kwamba hakuna ushahidi wowote wa kitafiti unaoonesha wazi kwa mabingwa wa anga za juu waliobobea wa masuala ya nyota.
MWANAMKE ALIWAHI KUOTA NDOTO
Kwa mara ya kwanza jambo hilo lilitokea mwaka 1995, wakati mwanamama Nancy Lieder muasisi wa mtandao wa ZetaTalk, aliwahi kudai kuoteshwa ndoto kwamba, Mei 2003 kuna kitu kitaingilia mfumo wa jua (solar system) na kusababisha dunia kutoboka tundu litakalosambaratisha sehemu kubwa ya kizazi cha binadamu. Lieder aliifafanua kuwa, kitu hicho kitakuwa na ukubwa wa mara nne ya dunia.
BAADA YA NDOTO
Baada ya mwanamama Lieder, mtu wa kwanza kuizungumzia Nibiru alikuwa Mark Hazlewood, mwanachama wa zamani wa mtandao wa ZetaTalk ambaye mwaka 2001 alichapisha kitabu kilichoitwa Blindsided na kusema kuwa mwisho wa dunia ungekuwa mwaka 2003 baada ya kuwasili kwa sayari ya kumi (Nibiru). Katika mfumo wa sasa, baadhi ya wanasayansi wanasema sayari ziko 12, wakizitaja kwa namba 1. Jua 2. Mercury 3. Venus 4. Dunia 5. Luna (mwezi) 6. Mars 7. Jupiter 8. Saturn 9. Uranus 10. Neptune 11. Pluto 12. Nibiru.
IMANI NYINGINE ZASEMAJE
Hata hivyo, utabiri mpya uliotolewa na watu wa jamii ya Vikings jijini New York, Marekani uliwahi kusema kuwa mwisho wa dunia ungekuwa Februari 22, mwaka huu baada ya ule wa Oktoba 21 mwaka juzi kushindwa kutokea huku aliyeendesha kampeni hizo akiwahi kufa kabla ya kuona huo mwisho wa dunia.. Mitandao mbalimbali pamoja na gazeti maarufu la Daily Mail la Uingereza lilielezea utabiri huo uliofanywa na jamii hiyo ukidai kuwa mwisho wa dunia utatokana na Mungu Odin kupigana na kuuawa na shetani Wolf Fenrir, hivyo kuiachia dunia anayoishikilia. Wamesema baada ya kuiachia dunia itafurika maji ambayo yatakuwa na sumu, hivyo viumbe wote watateketea.
WATUMISHI WA MUNGU TANZANIA
Baadhi ya watumishi wa Mungu nchini wamekuwa wakisimamia andiko la kwenye Biblia linalosema kuwa, hakuna mwanadamu anayeijua siku wala tarehe ya mwisho wa dunia na ni siri ya Muumba. Makanisa mengi nchini Tanzania yana sera tofauti lakini yanaongozwa na Biblia moja. Makanisa hayo ni Romani Katoliki, Lutheran (KKKT), Anglikana na makanisa ya kiroho kama Full Gospel& Bible Fellowship la Zakaria Kakobe. Kadhalika viongozi wa Kiislam ambao mara nyingi hawapendi kujikita kuzungumzia suala hilo za kuhubiri mafundisho wa Quran na Sunnah za Mtume Muhammad SAW kuwa dalili za awali za kutokea Kiama zimeshaonekana ikiwamo WANAWAKE kukosa haya, Wazazi kukosa huruma kwa watoto na Watoto kutowaheshimu wazazi wao, kujengwa miji na barabara mpya na dunia kuwa kijiji kimoja na ukatili kupindukia, njaa na magonjwa ya ajabu ajabu na kwamba bado badili 10 ambazo zitathibitishwa kuja kwa Masih Jadal (nabii wa uongo) atakayekuwa na jicho moja ambaye hata hivyo atakuja kuhamamizwa miaka 40 baadaye na Nabii Issa AS.

FREEMASON WABARIKI
Jamii ya Freemason tayari imebariki mwisho wa dunia kwamba umefika na dunia inatarajie tukio kubwa la pamoja. Mitandao ya jamii hiyo inataja kama hizi ni nyakati za mavuno kwa maana kwamba, upande wa Mungu na shetani kushindania watu huku waendao upotevuni  wakiwa wengi.
MFUMO WA DUNIA TANGU KUUMBWA
Kwa mujibu wa kitabu kinachoitwa Panorama ya Biblia, ulimwengu tangu kuumbwa kwake umekuwa na matukio makubwa kila baada ya miaka 2000 (inaweza isitimie au ikapita kidogo). Tangu kuumbwa kwa Adamu na Eva mpaka gharika inadaiwa ni miaka 2000. Gharika hadi dunia kubadili mfumo wa mawasiliano (Mnara wa Babeli) ni miaka 2000. Kuzaliwa kwa Yesu hadi saa ni miaka 2000 ambapo katika karne hii, dunia huenda ikaingia katika tukio kubwa sana ambalo halijawahi kutokea.

Polisi yathibitisha 37 kujeruhiwa, wa4 hoi ajali ya Happy Nation

ABIRIA wanne kati ya 37 waliojeruhiwa katika ajali ya basi iliyotokea mapema leo hii wilaya ya Mbalali, Mbeya baada ya tairi la basi hilo kupasuka wakati dereva akijaribu kumkwepa mwendesha baiskeli na kupinduka.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi amethibitisha muda mfupi uliopita kuwa watu 37 wamejeruhiwa vibaya, wanne wakiwa katika hali mbaya zaidi na walikuwa wakifanya mpango ya kuwahamisha kutoka Kituo cha Afya walipokimbizwa kwa matibabu ya awali ili kupelekwa Hospitali ya Rugaa ya Mbeya.
Kamanda Msani alisema kwa mujibu wa mashuhuda mwendo kasi ni tatizo lililosababisha ajali hiyo ambayo mmoja wa wajeruhi ni mtoto mdogo.
"Nipo eneo la tukio kwa sasa na tunafanya mpango wa kuwahamisha majeruhi walioo katika hali mbaya, kwani jumla ya abiria 37 akiwamo mtoto mmoja wanawake 16 wamejeruhiwa," alisema Kamanda huyo akihojiwa na Redio One Stereo.
Dereva wa ajali hiyo kwa mujibu wa Kamanda Msangi alipata upenyo na kutoroka baada ya ajali hiyo na kwamba vijana wake wameanza msako wa kumsaka popote alipo.

Simba wamcharukia Malinzi, waapa kufa na Dk Ndumbaro

https://hivisasa.co.tz/wp-content/uploads/2014/05/kiki.jpg
Rais wa Simba Evance Aveva (kulia)
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgL1LPgdchJFD1adg4pCb0Bka71FkdEYaLCebHqzuZj394iyl0gPdzuaSuhfdPDPCUfr3xHmouPBJf8kQ4CDaLpwoDGdnPe79JH20dEGBRlv9KMIySyX5wRElLkomaWlOOLC7-12vaN8eg/s1600/3.jpg
Dk Ndumbaro (kulia)
UONGOZI wa Klabu ya Simba umelivaa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuhusu kauli yao ya kuzitaka klabu kutojihusisha na wakili wa kujitegemea Damas Ndumbaro kupitia kampuni yake ya Maleta & Ndumbaro Advocate.
Rais wa Simba, Evans Aveva, amefunguka kuwa kwa upande wao bado wanaendelea kumsapoti Ndumbaro kwa asilimia 100 kwa sababu wao ndiyo waliomtuma na kudai kuwa watashirikiana naye kama kawaida katika masuala ya soka.
“Kamati iliyoshughulikia suala hilo ni huru na kwa upande wetu Simba tupo mstari wa mbele kuhusu suala hilo na tunamsapoti.
“Tutaendelea kumtumia Ndumbaro kama kawaida kwani tunatetea haki yetu na tunapinga vikali makato ya asilimia tano ya mapato.
“Hakuna waraka wowote tuliopewa klabu kuhusu jambo hilo,” alisema Aveva.
TFF ilitangaza kumfungia Ndumbaro kujihusisha na soka kwa miaka saba kutokana na kile kilichoelezwa kukiuka kanuni kadhaa za shirikisho hilo.

SALEH JEMBE

Aibu! Huu ndiyo waraka ulionaswa na UKAWA, Serikali yajitetea


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhQVSm8E31wk1Jp_U2mmpWrcXbH6mgu_fwkTutJQyIq563kVgdwvSVBmIjI4rpufX0TN47VUQ15FkEJLKiy63fbXZ-jXPKBrJ2cUtaFT36e4Xh62GuQ4Wqe69UpStKY1LLCavYlWUgS9xE/s1600/10697324_10152511503926156_3540962510431235374_o.jpg










HUU ni Waraka ambao ulinaswa na Umoja wa Katiba wa Wananchi (UKAWA) ambao umedaiwa kutolewa na serikali kwa ajili ya kuelekeza vyombo vya habari kuhakikisha wanasaidia KURA za NDIYO dhidi ya Katiba Pendekezwa wakati zoezi la upigaji kura kuipitisha kuwa Katiba Kamili kuibeba KATIBA hiyo inayopingwa na baadhi wananchi kutokana na ukweli imepuuza baadhi ya MAONI ya Wananchi na KUWEKWA MAONI ynayodaiwa kuwa masilahi kwa vigogo wa Chama Tawala kinachoiongoza nchi kwa sasa. Mapema leo asubuhi Msemaji wa Ikulu, Salva Rweyemamu alinukuliwa na BBC akikiri kuwepo kwa waraka huo akidai ni wa KAWAIDA na HAKUNA haja ya WATU  kupotoshwa kuwa ni MBINU za serikali KULAZIMISHA KATIBA hiyo hata kama ni kweli wapo wanayoipinga. Kwa hali hii ni kweli upo UHURU wa MAWAZO kwa WANANCHI?! IKULU inahusiana vipi na Kampeni Hii wakati suala hili?! Hii uthibitisho wa madai na vilio vya watu wengi kuwa KATIBA iliyopendekezwa siyo ya WANANCHI bali ni ya WATAWALA. MICHARAZO MITUPU yetu MACHO!

.

Newz Alert! Basi la Happy Nation lapinduka Mbeya


Picha kwa Hisani ya Joseph Mwaisango
TAARIFA ambazo zimepatikana kutoka mjini Mbeya zinasema kuwa  Basi la Happy Nation limepata ajali muda huu baada ya dereva wa basi ilo kufanya juhudi za kutaka kumkwepa mwendesha baiskeli kushindikana na kupelekea kutokea kwa ajali hiyo. Ajali hii imetokea eneo la  Igurusi na pia basi hilo lilitokea Mbeya kuelekea Dar es Salaam kwa basi hilo kupinduka kama livayoonekana pichani, Inaelezwa kuwa hakuna maafa isipokuwa watu kadhaa wamejeruhiwa katika ajali hiyo.

Thursday, November 6, 2014

Hatari! Njemba yanaswa na Dawa za Kulevya,


unnamed
Mtuhumiwa Hamis Mohamed (47) Mkazi wa Kondoa aliyekamatwa eneo la Mianzini jijini Arusha akiwa na madawa ya kulevya aina ya mirungi iliyokuwa inasafirishwa toka nchi jirani ya Kenya kuelekea Kondoa mkoani Dodoma (Picha:Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)
Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha
MTU mmoja aitwaye Hamis Mohamed (47) Mkazi wa Kondoa mkoa wa Dodoma, amekamatwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha baada ya kukutwa na madawa ya kulevya aina ya mirungi aliyekuwa anaisafirisha kwa mtindo wa aina yake.
Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Liberatus Sabas alisema kwamba tukio hilo lilitokea tarehe 05.11.2014 muda wa saa 11:00 jioni eneo la Mianzini ambapo mtuhumiwa huyo alikuwa anasafirisha madawa hayo kwenye gari aina ya Fusso basi lenye namba za usajili T. 577 BFM ambapo aliihifadhi kwenye magunia mawili huku juu na pembeni ya magunia hayo akiweka viatu.
‘’Katika magunia yale alikuwa ameweka viatu na katikati aliweka viroba 36 vya madawa hayo aina ya mirungi ambayo alikuwa anasafirisha toka nchini Kenya kupeleka Kondoa mkoani Dodoma hivyo ukiangalia unaweza kusema ni viatu pekee’’. Alifafanua Kamanda Sabas.
Alisema tukio hilo lilifanikiwa kutokana na mahusiano mema yaliyopo kati ya Jeshi hilo na raia wema ambao walitoa taarifa iliyofanyiwa kazi haraka na asakari wa Jeshi hilo.
Baada ya askari hao kupata taarifa hiyo walianza kulifuatilia gari hilo na lilipofika maeneo ya Mianzini jijini hapa kwenye maegesho ya basi hilo ndipo walipoanza kufanya upekuzi na kufanikiwa kukamata magunia hayo yaliyokuwa na viatu vilivyochanganywa na madawa hayo.
Kamanda Sabas alisema kwamba mtuhumiwa huyo bado anaendelea kuhojiwa na atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.

Newz Alert! Rais JK aenda USA kucheki afya yake

  
Rais Profesa Jakaya Mrisho Kikwete akisindikizwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe said Meck Sadik na Meneja wa Huduma za Shirika la ndege la Emirates katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Julius Nyerere Bw.  Aboubakar Juma leo Novemba 6, 2014 wakati akielekea kupanda ndege kuelekea Marekani kwa ajili ya uchunguzi wa afya yake
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameondoka nchini jioni ya leo, Alhamisi Novemba 6, 2014, kwenda Marekani kwa ajili ya uchunguzi wa afya yake.
Rais Kikwete atakuwa Marekeni kwa muda wa siku kumi.

Mwisho.

Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
06 Novemba,2014

Watatu kati ya waliokufa ajalini Ifakara watambuliwa!

http://api.ning.com/files/st-pA-4csCGQ4-t4jx12MikAxzFvyvUW-zC35WxKpbGhYiXhPqU4H5di0w8j4TwMDjoHYFJKlkEAnto0riRQW1TncFQ-7kLz/5ajali5.jpg
Mabaki ya basi la Al Jabir (Picha zote na Global Publishers)
 

Basi la Super Aljabir baada ya ajali.
Basi hilo likiwa limepinduka.
Baadhi ya miili katika ajali hiyo ikiwa eneo la tukio.
MIILI ya watu watatu kati ya 12 waliofariki katika ajali mbaya ya gari dhidi ya treni huko Ifaraka mchana wa leo imetambuliwa.
Watu hao walifariki dunia papo hapo na wengine 45 kujeruhiwa baada ya basi walililokuwa wakisafiria la Kampuni ya Al Jabir kugonga treni eneo la Kiberege Ifakara Wilaya ya Kilombero.
 Kamanda wa polisi mkoani Morogoro Leonard Paul alisema basi hilo lilokuwa likitokea Morogoro- Ifakara kugonga Treni ya Tazara iliyokuwa ikitokea Mbeya – jijini Dar es Salaam.
 Kamanda huyo  aliwataja marehemu watatu waliotambulika katika ajali hiyo kuwa ni Frugensia Lusangila (60), Albeta Lusangila (62) wakazi wa Ichonde Mangula na Joseph Kazwila (34) mkazi wa jijini Dar es Salaam.
 Kamanda Paulo alisema chanzo cha ajali hiyo ni  dereva wa basi hilo lenye namba za usajili T725 ATD Scania, alivuka barabara yenye makutano na reli bila ya kuchukua tahadhani na hivyo kuigonga treni.
Alisema kuwa majeruhi wa ajali hiyo wamepelekwa katika hospitali ya mtakatifu Fransis Ifakara na kituo cha afya Kibaoni kwa ajili ya matibabu.
Kamanda Paulo alisema miili ya marehemu nayo imehifadhiwa katika hospitali ya mtakatifu Francis Ifakara.
Alisema dereva wa basi hilo alikimbia mara baada ya ajali hiyo kutokea na polisi wanamtafuta wakati uchunguzi ukiwa bado unaendelea.

Ndege ya Rais wa China yadaiwa kutorosha nyara za Tanzania


Rais Xi JinPing wa Uchina alipozuru Tanzania mwaka uliopitaINADAIWA kuwa, Ndege ya Rais wa China, aliyekuwa ziarani nchini Tanzania mwaka uliopita ilihusija kutorosha nyara za taifa zikiwamo Pembe za Ndovu.
Inaelezwa kuwa wanunuzi, raia wa Uchina walinunua maelfu ya kilo za Pembe za Ndovu Tanzania kisha kuzitorosha kutoka nchini humo katika ndege ya kibinafsi ya raia wa Uchina Xi Jinping, wakati alipozuru bara Afrika. 
Kulingana na shirika la ujasusi la mazingira lililo na makao yake mjini London. 
Pembe hizo zilinunuliwa wiki moja tu kabla ya ziara ya rais huyo wa Uchina nchini Tanzania mwaka uliopita ambapo zilifichwa katika mifuko ya wanadiplomasia ili kutokamatwa. 
Uuzaji wa Pembe za ndovu ulipigwa marufuku mwaka 1989 ili kuwazuia wawindaji haramu kuwaua ndovu. 
Shirika hilo pia linadai kwamba wajumbe waliokuwa wakiandamana na Rais Xi walinunua viwango vikubwa vya pembe hizo.
Hata hivyo serikali imekanusha taarifa hizo za kuwepo kwa biashara ya Pembe za Ndovu nchini.
Msemaji wa serikali Assah Mwambene amemwambia mwandishi wa BBC Aboubakar famau kwamba ripoti kama hiyo zinatatiza jitihada za serikali kukabiliana na uuzaji haramu wa pembe za ndovu.

Mwambene amesema serikali ya Tanzania imeshtushwa na ripoti inayoelezea biashara haramu ya meno ya tembo kati ya baadhi ya viongozi wa nchi hiyo na China.
Serikali imesema imesikitishwa na ripoti iliyotolewa na taasisi ya uchunguzi ya mazingira inayodai kwamba majangili wa kichina wakishirikiana na baadhi ya viongozi wa serikali ya Tanzania ndio wanaoangamiza idadi ya tembo kutokana na biashara haramu ya meno ya tembo.
BBC  

TANGAZO KWA WANABLOGU WOTE TANZANIA

RAIS JK APANGUA WAKUU WA MIKOA, KANALI MASSAWE NJE!

http://api.ning.com/files/Hu6bOG3IkcRAJl9pt5BZONEg5d6srRLFuULjOo7Y1CbfmS7EUBSjP7yla0ZaLravxPaTvFQrk**5S7QDlPeW7XvoWqo9qwB9/RaisKikwete.jpg
Rais Jakaya Kikwete
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amefanya uteuzi wa wakuu wapya wanne wa Mikoa, amewahamisha wengine sita na ameamua kuwa wengine watatu watapangiwa kazi nyingine.

Taarifa iliyotolewa mjini Dodoma jioni ya leo, Jumatano, Novemba 5, 2014 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue inasema kuwa, Wakuu wapya wa Mikoa ni Bi. Halima Omari Dendego ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Dkt. Ibrahim Hamisi Msengi ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Bi. Amina Juma Masenza ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa na Bwana John Vianney Mongella ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera.

Taarifa inasema kuwa kabla ya uteuzi wake Bi. Dendego alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Dkt. Msengi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Bi. Masenza alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilemela na
Bwana Mongella alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha.

Taarifa hiyo inasema kuwa Wakuu hao wapya wa Mikoa wataapishwa kesho, Alhamisi, Novemba 6, 2014 saa saba mchana, Ikulu, Dar es Salaam.

Aidha, taarifa hiyo imesema kuwa Wakuu wa Mikoa ambao watapangiwa kazi nyingine ni Kanali (Mst) Fabian Massawe wa Kagera, Dkt. Christine Ishengoma wa Iringa na Kanali Joseph Simbakalia wa Mtwara.

Wakuu wa Mikoa ambao wamehamishwa vituo vya kazi ni Bwana Magesa S. Mulongo ambaye anakwenda Mkoa wa Mwanza kutoka Arusha, Dkt. Rehema Nchimbi ambaye anakwenda Mkoa wa Njombe kutoka Dodoma, Bwana Ludovick John Mwananzila anakwenda Tabora kutoka Lindi, Kepteni (Mst) Anseri Msangi anayekwenda Mkoa wa Mara kutoka Njombe na Mhandisi Everist Ndikilo ambaye anakwenda Arusha kutoka Mwanza.

Wengine waliohamishwa ni Luteni (Mst) Chiku A.S. Galawa ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kutoka Tanga, Dkt. Rajab Rutengwe ambaye anakwenda Mkoa wa Tanga kutoka Katavi, Bi Fatma Mwasa ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita kutoka Tabora na Bwana Magalula S. Magalula ambaye anahamishiwa Lindi kutoka Geita.

Taarifa hiyo imesema kuwa Wakuu wa Mikoa ya Dar es Salaam, Kigoma, Kilimanjaro, Manyara, Mbeya,Morogoro, Pwani, Rukwa, Shinyanga, Ruvuma, Singida na Simiyu watabakia kwenye vituo vyao vya sasa.

Aidha, Rais Kikwete amefanya uteuzi wa Wakuu wapya wa Wilaya, kuhamisha baadhi yao na kutengua uteuzi wa baadhi. Taarifa kamili itatolewa na Waziri Mkuu baada ya kuwa wamepangiwa vituo vya kazi.

Mwisho.


Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.

Simanzi! Ajali yachinja watu 12 Ifakara

http://rantsofasassystew.com/wp-content/uploads/2011/10/Breaking_News.jpg
HABARI zilizotufiki hivi punde zinasema kuwa kumetokea ajali mbaya iliyohusisha basi la Al Jabir ambalo lililigonga Treni na kusababisha vifo vya watu 12 papo hapo wakiwamo watoto wawili.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Morogoro ni kwamba ajali hiyo ilitokea majira ya saa 9 katika eneo la Kiberege, Ifaraka wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro.
Taarifa hizo zinasema kuwa basi hilo lenye namba za usajili T 725 ATD liliigonga Treni ya TAZARA na kusababisha roho za wanaume sita, wanawake wanne na watoto wawili waliokuwa kwenye basi hilo kupotea huku abiria wengine kuachwa na majeraha ya kutisha.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Leonard Paul amethibitisha taarifa hiyo na uchunguzi dhidi ya ajali hiyo unaendelea kujua chanzo chake.

FifPro yatishia kugomea Fainali za Kombe la Dunia za Qatar

http://s1.reutersmedia.net/resources/r/?m=02&d=20110914&t=2&i=500889270&w=580&fh=&fw=&ll=&pl=&r=img-2011-09-14T173158Z_01_NOOTR_RTRMDNC_0_India-593363-1
UMOJA wa Wachezaji wa Kulipwa FIFPro, umetishia kuigomea michuano ya Kombe la Dunia ya mwaka 2022 nchini Qatar.
Kiongozi wa umoja huo, Theo van Seggelen amesema kuwa wachezaji wanaweza kugomea kushiriki michuano hiyo iwapo itaendelea kushinikizwa kuchezwa katika majira ya kiangazi.
Joto katika nchi hiyo ya barani Asia hufikia hadi nyuzi joto 40 katika kipindi cha kati ya mwezi Mei na Septemba, ingawa muda haswa wa kufanyika michuano hiyo bado haujapangwa na Shirikisho la Soka la Dunia-FIFA.
Van Seggelen amesema Fifpro haitawaruhusu wachezaji kuhatarisha afya zao kwa kushiriki fainali hizo ambazo zimeleta mzozo tangu zilipotangazwa na shirikisho la sokla duniani, FIFA miakla michache iliyopita.
Aliongeza kwa kudai kuwa kama ikibidi anaweza kulipeleka suala hilo mahakamani ili kupata haki ya msingi.
Kiongozi huo amesema ana uhakika FIFA haitaweza kupingana na washauri wao wenyewe wa masuala ya afya kwa kuruhusu michuano hiyo kuchezwa majira ya kiangazi.
Van Seggelen pia aliponda ombi la vilabu vya Ulaya kutaka michuano hiyo kufanyika katika kipindi cha Aprili na Mei akidai kuwa halina mashiko kwani bado kipindi hicho kinaweza kuhatarisha afya za wachezaji.

Polisi wanasa Konyagi Feki Dar, wahusika watiwa mbaroni


BAADHI ya vibarua waliokodiwa kwa ajili ya kupakia Konyagi ili wapeleke kituo cha polisi Buguruni wakifanya kazi ya kujaza katika marobota ili waweke katika gari baada ya konyagi hiyo feki kukamatwa Dar es salaam jana kwenye moja ya Godown maeneo ya vingunguti karibu na kituo cha mchicha watuhumiwa walikamatwa na kupelekwa polisi
Baadhi ya watuhumiwa wa Konyagi feki wakifanya kazi ya  kupakia kwenye mabox konyagi hizo ambapo walikamatwa na jeshi la polisi na kufikishwa kituo cha polisi buguruni kwa uchunguzi zaidi

Baadhi ya watuhumiwa wakiwa chini ya ulinzi ambapo jana waliswekwa lumande na kulala ndani ya kituo cha polisi buguruni baada ya kukamatwa wakipakia Konyagi feki maeneo ya vingunguti Dar es salaam jana
MMOJA YA WATUHUMIWA AMBAYE ALIJITAMBULISHA KUWA YEYE NI MMILIKI WA KONYAGI FEKI AKIWA CHINI YA ULINZI BAADA YA KUKAMATWA JANA

Baadhi ya watumiwa waliokutwa katika godown lenye konyagi feki wakiendelea na kazi ya kupakia katika mabox watumiwa hawo walikamatwa na kulala lumande katika kituo cha polisi Buguruni Dar es salaam jana kwa uchunguzi zaidi
Baadhi ya maofisa usalama wakiangalia mzigo uliokamatwa ukipandishwa katika gari kwa ajili ya kuelekea kituo cha polisi buguruni


Baadhi ya vibarua waliokodiwa kwa ajili ya kupakia Konyagi ili wapeleke kituo cha polisi Buguruni wakifanya kazi ya kujaza katikaq marobota ili waweke katika gari baada ya konyagi hiyo feki kukamatwa Dar es salaam jana kwenye moja ya Godown maeneo ya vingunguti karibu na kituo cha mchicha watuhumiwa walikamatwa na kupelekwa polisi

Man City Majanga, Chelsea yabanwa Ulaya, Bayern haoooo!

Eden Hazard missed the chance to win the match for Chelsea against Maribor late on when his penalty was saved
Hazard akipiga penati iliyookolewa wakati Chelsea wakitoka sare ya 1-1
Seydou Doumbia heads CSKA Moscow into an early lead as he takes advantage of a static Manchester City defence
Man City wakiadhibiwa na Doumbia
Toure jumps for joy as he celebrates levelling the score in what was a crunch match for City in the Champions League
Yaya Toure akishangilia bao lake jana
City's miserable night, and their campaign, was summed up by Toure's red card as he followed Fernandinho to the dressing room
Kisha akaja akalimwa kadi nyekundu ya kwamba maisha yake Etihad
Gotze is mobbed by his Bayern team-mates after doubling the Germans' lead late in the second half
Wachezaji wa Bayern Munich wakishangilia mabao yao yaliyowapeleka kwenye 16 Bora ya Ulaya
Ribery celebrates opening the scoring after Bayern had dominated possession in the first half
Fracky Ribery akishangilia bao la kwanza la Bavarians
WAKATI mabingwa watetezi wa England Manchester City wakigaragazwa nyumbani na kujiweka katika nafasi finyu ya kufuzu hatua ya 16 Bora ya Ligi ya mabingwa, Chelsea wameponea chupuchupu baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 ugenini dhidi ya Maribor walioitandika vibaya wiki iliyopita.
Cheslea katika mechi ya Kungi G ilishtukizwa kwa bao lililofungwa dakika chache baada ya kipindi cha pili kuanza baada ya Agim Ibraimi kuifungia Maribor, kabla ya Nemanja Matic kusawazisha katika dakika ya 73.
Wakiwa na nafasi ya kuendeleza rekodi ya kipigo cha Maribor, Chelsea walipoteza penati baada ya mshambuliaji Eden Hazard kushindwa kukwamisha mpira wavuni.
Hata hivyo matokoe hayo bado yameiacha Chelsea kileleni mwa msimamo wa kundi hilo wakiwa na pointi nane wakifuatiwa na Schalke 04 iliyolala ugenini kwa mabao 4-2 mbele ya Sporting yenye pointi tano.
Katika mechi nyingine za michuano hiyo, Manchester City walijikuta wakijiweka pabaya kwa kukubali kipigo cha mabao 2-1 nyumbani dhidi ya CSKA Moscow, huku ikiwapoteza nyota wake wawili, akiwamo Yaya Toure aliyefunga bao pekee la timu hiyo.
Yaya alilimwa kadi ya pili ya njano na kusindikizwa na nyekundu na kuwa kadi yake ya kwanza tangu aanze kuichezea timu hiyo na tayari amewaomba radhi mashabiki wa klabu hioyo ya Etihad.
CSKA Moscow waliwashtukiza wenyeji kwa bao la mapema la dakika ya pili kupitia Seydou Doumbia akimalizia kati ya Natcho kabla ya Yaya Toure kusawazisha dakika sita baadaye ma Doumbia akamaliza udhia dakika ya 34 kwa kufunga bao la pili na katika kipindi cha pili wenyeji kuwapoteza Yaya na Fernandinho.
Kipigo hicho kimeiacha City wakiwa wanaburuza mkia wakiwa na pointi mbili wakitakiwa kupata ushindi mfululizo dhidi ya  Bayern Munich waliofuzu baada ya kuilaza Roma kwa mabao 2-0 na ile dhidi ya Roma wenyewe ambao wanashika nafasi ya pili wakilingana pointi na CSKA.
Katika mechi nyingine Porto ya Ureno ikiwa ugenini nchini Hispania ilipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Athletico Bilbao, huku Shakhtar Donetsk ya Uturuki wakiichakaza BATE kwa mabao 5-0 katika mechi za kundi H.

Messi achana naye, aitungua Ajax 2-0 na kumfikia Raul


Lionel Messi celebrates scoring his first goal against Ajax on Wednesday night
Messi akishangilia moja ya mabao yake yaliyomfanya amfikie raul
Messi heads into the Ajax goal for his 70th Champions League goal... he later scored his 71st
Messi akifunga  bao dhidi ya Ajax
NYOTA wa klabu ya Barcelona, Lionel Messi usiku wa jana ameweka relodi ya kumfikia kinara wa mabao wa muda wote wa Ligi ya Mabingwa, Rau baada ya kufunga mabao mawili wakati barcelona wakiilipua Ajax kwa mabao 2-0.
Messi amefikisha jumla ya mabao 71 na kulingana na Raul aliyewahi kutamba Real Madrid.
Mwanasoka Bora huyo wa mara nne wa zamani wa dunia alifunga mabo la kwanza kwa kichwa kabla ya kuongeza jingine na kufikia rekodi hiyo iliyowekwa miaka 10 iliyopita na Raul.
Ushindi huo umeifanya Barcelona kukamata nafasi ya pili ikiwa na pointi 9, moja ya vinara wa kundi F PSG ambayo ilishinda nyumbani 1-0 dhidi ya APOEL Nicosia na kulifanya kundi hilo kuzidi kuwa gumu bila kujua itakayofuzu hatua ya 16 Bora hadi michezo ijayo.

Ronaldo atamba yeye ni mkali bwanaa!

http://www.footballlive.ng/football/wp-content/uploads/2014/10/cr7goldenshoe.jpg
Ronaldo
CRISTIANO Ronaldo, Mwanasoka Bora Duniani, anaamini atajumuishwa kama mmoja kati ya wachezaji bora kabisa kuwahi kucheza mchezo huo wakati utakapofikia wakati wake wa kustaafu.
Nyota huyo wa Real Madrid na raia wa Ureno, 29 alipokea tuzo yake ya Kiatu cha Dhahabu cha Mfungaji Bora Barani Ulaya ikiwa ni mara ya tatu kwake jana huku pia akipewa nafasi ya kunyakuwa tuzo ya Ballon d’Or kwa mara ya tatu Januari mwaka huu.
Wakati akisisitiza kuwa bado ana miaka mingi ya kucheza soka katika kiwango cha juu, nyota alisema ana uhakika nafasi yake kama mmoja wa manguli wa soka katika historia tayari ameshajihakikishia.
Akihojiwa mara baada ya kukabidhiwa tuzo yake hiyo Ronaldo amesema siku zote anataka kuwa bora ndio maana anafanya jitihada kila kukicha.
Msimu huu Ronaldo bado ameendeleza rekodi yake nzuri ya kufunga akiwa tayari ameshafunga mabao 22 katika mechi 16 za mashindano yote na kuiwezesha Madrid kukwea kileleni mwa msimamo wa La Liga sambamba na kutinga hatua ya timu 16 bora.
Ronaldo alifungana mabao na Luis Suarez ambaye tyayari alishakabidhiwa tuzo yake hivi karibuni. kila mmoja alifunga mabao 31 katika ligi maarufu Suarez akiwa Liverpool japo kwa sasa amehamia Barcelona.
Make money by copying the best: http://bit.ly/cop
MCHEZAJI bora wa mwaka wa dunia, Cristiano Ronaldo anaamini atajumuishwa kama mmoja kati ya wachezaji bora kabisa kuwahi kucheza mchezo huo wakati utakapofikia wakati wake wa kustaafu. Ronaldo mwenye umri wa miaka 29 alipokea tuzo yake ya kiatu cha dhahabu ikiwa ni mara ya tatu kwa kuwa mfungaji bora wa michuano ya Klabu Bingwa barani Ulaya jana huku pia akipewa nafasi ya kunyakuwa tuzo ya Ballon d’Or kwa mara ya tatu Januari mwaka huu. Wakati akisisitiza kuwa bado ana miaka mingi ya kucheza soka katika kiwango cha juu, nyota huyo wa kimataifa wa Ureno ana uhakika nafasi yake kama mmoja wa manguli wa soka katika historia tayari ameshajihakikishia. Akihojiwa mara baada ya kukabidhiwa tuzo yake hiyo Ronaldo amesema siku zote anataka kuwa bora ndio maana anafanya jitihada kila kukicha. Msimu huu Ronaldo bado ameendeleza rekodi yake nzuri ya kufunga akiwa tayari ameshafunga mabao 22 katika mechi 16 za mashindano yote na kuiwezesha Madrid kukwea kileleni mwa msimamo wa La Liga sambamba na kutinga hatua ya timu 16 bora.

Make money by copying the best: http://bit.ly/copy_win