STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, January 2, 2015

Bosi wa Wigan afungiwa kwa ubaguzi

http://cdn.images.express.co.uk/img/dynamic/67/590x/Dave-Whelan-538904.jpgMMILIKI wa klabu ya Wigan Athletic Dave Whelan amefungiwa kwa wiki sita kujishughulisha na masuala yeyote ya michezo na kutozwa faini ya paundi 50,000 kwa kutoa kauli ya kibaguzi kuwalenga watu wenye asili ya Uyahudi na Wachina. 
Tajiri huyo mwenye umri wa miaka 78 ambaye amepewa wiki moja kukata rufani kuhusiana na adhabu hiyo pia ametakiwa kuhudhuria darasa la ushauri litakalokuwa likiendeshwa na Chama cha Soka cha Uingereza. 
Mwezi uliopita Whelan alikubali tuhuma hizo lakini alikataa kauli alizotoa wakati akihojiwa na gazeti moja kuwa za kibaguzi. 
Novemba mwaka huu Whelan alidai kuwa atajiuzulu kama akikutwa na hatia ya kuwa mbaguzi.

Simba bado gonjwa, yapigwa na Mtibwa Mapinduzi Cup

KIKOSI cha Simba kikiwa tayari na vita dhidi ya Mtibwa kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi, ambapo Mnyama alikubali kipigo cha bao 1-0 lililowekwa kimiani na Nahodha wao wa zamani, Henry Joseph katika dakika ya 44. Kipigo hicho ni cha pili mfululizo kwa Simba baada ya wiki iliyopita kupigwa baoa 1-0 na 'ndugu' wa Mtibwa, Kagera Sugar kartika pambano la Ligi Kuu Tanzania Bara. (Picha kwa hisani ya ZanziNews
Wachezaji wa timu ya Mtibwa Sugar wakipasha moto misuli kabla ya kukaguliwa na Mgeni Rasmi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, wakati wa ufunguzi wa michuano hiyo iliyoanza jana Uwanja wa Amaan Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akisalimiana na Kamisaa wa Mchezo huo Muhsin Kamara, wakati wa uzinduzi wa michuano ya Kombe la Mapinduzi yaliozinduliwa leo na Balozi Seif, katika uwanja wa Amaan.    
Makamu wa Pili wa Rais wac Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Wachezaji wa timu ya Simba kabla ya kuanza kwa mchezo huo wa ufunguzi uliofanyika uwanja wa Amaan usiku jana.
Makamu wa Pili wa Rais wac Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Wachezaji wa timu ya Mtibwa Sigar,kabla ya kuaza kwa mchezo huo wa ufunguzi uliofanyika uwanja wa Amaan usiku wa jana
Wachezaji wa timu ya Simba wakisalimiana na Wachezaji wa timu ya Mtibwa Sugar kabla ya kuaza kwa mchezo wao wa ufunguzi uliofanyika uwanja wa Amaam. Timu ya Mtibwa imeshinda bao 1--0
Kikosi cha Simba kilichokubali kipigo cha bao 1-0 kwa mara ya pili mchezo wa mwanzo dhidi ya Mtibwa Sugar baada ya msimu uliopita kunyukwa mabao 4-2.
Kikosi cha  timu ya Mtibwa Sugar kilichotoka kifua mbele dhidi ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya timu ya Simba wakati wa mchezo wa ufunguzi wa Kombe la Mapinduzi uliofanyika usiku wa jana uwanja wa Amaan Zanzibar.
Makamu wa Rais wa Simba, Nyange Kaburu alikuwa akishuhudia kipigo kando ya kocha wa Mbeya City, Juma Mwambusi.
KOcha mpya wa Simba, Goran Kapunovic akiwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba wakifuatilia mchezo huo wa jana
Makocha wa Yanga, Hans van der Pluijm na Boniface Mkwasa walikuwapo uwanjani

Yanga yamtosa Kaseja Kombe la Shirikisho Afrika

Kipa Juma Kaseja
Yanga
Azam
KLABU ya Yanga imemtosa rasmi kipa wao waliye kwenye mgogoro naye, Juma Kaseja baada ya kutolituma jina lake kwenye kikosi cha timu hiyo kwa ushiriki wa michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Jina la Kaseja si miongoni mwa wachezaji 24 waliopo kwenye orodha iliyotumwa ofisi za CAF kwa usajili wa michuano hiyo ambayo itakayoanza katikati ya mwaka huu kwa Yanga kuumana na BDF IX ya Botswana.
Kaseja amekuwa na mgogoro na klabu hiyo ya Jangwani kutokana na kutochezewa kwenye mechi za Ligi Kuu hivyo kuomba kupitia wakili wake kuachwa na timu hiyo, huku Yanga wakitangaza kuendelea kumkomalia kwa kuwa wana mkataba naye.
Wakati Yanga ikituma majina 24, nao mabingwa wa Tanzania Azam watakaoshiriki Ligi ya Mabingwa Afrika wakianza kibarua chao kwa kuumana na El Merreikh imetuma pia idadi ya wachezaji kama hiyo kwa ajili ya ushiriki wa michuano hiyo watakayoicheza kwa mara ya kwanza mwaka huu.
Kikosi cha Yanga kilichowasilishwa CAF kwa mujibu wa taarifa ambazo MICHARAZO inayo ni Makipa: Ally Mustafa 'Barthez' na Deogratius Munishi 'Dida', Mbuyu Twite, Juma Abdul, Nadir Haroub 'Cannavaro', Edward Charles, Kelvin Yondani, Salum Telela, Rajab Zahir, Andrey Coutinho na Haruna Niyonzima.
Wengine ni Said Juma, Hassan Dilunga,  Sherman Kpah, Jerson Tegete, Pato Ngonyani, Nizar Khalfan, Mrisho Ngassa, Alphonce Matogo, Amissi Tambwe, Hussein Javu, Said Juma,  Danny Mrwanda na Simon Msuva.
Kikosi cha Azam kilichopelekwa CAF ni; Mwadini Ali, Gadiel Michael, Shomari Kapombe, Serge Wawa, Erasto Nyoni, Kelvin Friday, Salum Abubakar 'Sure Boy', Khalid Haji, Kipre Tchetche, Didier Kavumbagu, David Mwantika, Aggrey Morris na Amri Kiemba.
Wengine ni Said Morad, Frank Domayo, John Bocco, Yahya Mudathir, Brian Majwega, Khamis Mcha, Himid Mao, Gaudence Mwaikimba, Waziri Salum, Aishi Manula na Wilfred Michael Bolou.

Wednesday, December 31, 2014

AC Milan yaitoa nishai Real Madrid Umangani

Ronaldo na El Shaarawy wakichuana
Beki wa Madrid Nacho akimdhiobiti mchezaji wa AC Milan
Karim Benzema akifunga bao la pili la Madrid kwa mkwaju wa penati
MSHAMBULIAJI Stephan El Shaarawy aliiwezesha timu yake ya AC Milan ya Italia kupata ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Mabingwa wa Ulaya, Real Madrid ya Hispania katika pambano la kimataifa la kirafiki lililochezwa mjini Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu.
El Shaarawy alifunga mabao mawili katika kipigo hicho kilichokuwa cha kwanza kwa vijana wa Carlo Ancelotti tangu Septemba na kuhitimisha 'ubabe' wa Madrid ambao walikuwa hawajapoteza mchezo wowote katika mechi 22 katika msimu huu.
Jeremy Menez wa Milan ndiye aliyeanza kufungua milango baada ya kufunga bao la kuongoza katika dakika ya 24 kabla ya El Shaarawy kuongeza goli la pili katika dakika 31 kwa shuti kali.
Dakika nne baadaye Madrid walifanikiwa kuchomoa bao moja kupitia kwa Mwanasoka Bora Duniani, Cristiano Ronaldo kufunga akiwa ndani ya 'boksi' akimtungua kipa  Diego Lopez na kuzifanya timu ziende mapumziko Milan wakiwa mbele kwa mabao 2-1.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na kushuhudiwa Milan wakiongeza bao la tatu dakika ya 49 kupitia tena kwa El Shaarawy kabla ya watokea benchi Giampaolo Pazzini na M'Baye Niang kushirikiana vyema na na Pazzini kuukwamisha mpira kimiani katika dakika ya 73 kuaindikia Milan bao la nne.
Real Madrid ilijipatia bao la pili la kujifutia machozi kupitia mshambuliaji wake wa Kifaransa Karim Benzema, aliyefunga bao kwa mkwaju wa penalti katika dakika ya 84.
Kwa ushindi huo AC Milan walikabidhiwa kombe lililopokewa na nahodha wake, Riccardo Montolivo.

KIPUTE CHA MAPINDUZI KUANZA KESHO, RATIBA HII HAPA

Kikosi cha Simba kitakachoanza kibarua cha Mapinduzi Cup dhidi ya Mtibwa Sugar usiku wa kesho
Mtibwa Sugar watakaivaa Simba kesho usiku katika Mapinduzi Cup
Yanga X1
Yanga safari hii imekubali kushiriki kamili gado
MSIMU mpya wa Michuano ya Kombe la Mapinduzi unatarajiwa kuanza rasmi kesho kwa michezo mitatu 'Mnyama' Simba akitarajiwa kushuka dimbani Usiku kuvaana na Mtibwa Sugar, huku Azam wakitarajiwa kuvaama na KCCA ya Uganda Ijumaa.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa ni kwamba kesho mechi ya kwanza itawakutanisha JKU na Mafunzo majira ya saa 9 alasiri kabla ya Polisi-ZNZ kuvaana na Shaba jioni.
Yanga ambayo imekuwa 'ikisumbua' ushiriki wake katika michuano hiyo safari hii imekubali kikamilifu kushiriki na wenyewe wataanza kibarua Jumamosi kwa kuvaana na Sports Club Villa ya Uganda.
Jumla ya makundi matatu yamegawanywa yakiwa na timu nne kila moja nayo ni;
Kundi A:  SC VILLA,  YANGA, POLISI,  SHABA.
Kundi B: KCCA,  AZAM,  KMKM na MTENDE.
Kundi C: SIMBA, MTIBWA, JKU, na MAFUNZO.
RATIBA KAMILI YA MAPINDUZI CUP IKO HIVI:
Alhamisi 1 Januari 2015:
Saa 9:00  JKU vs MAFUNZO.
Saa.11:00.  POLISI VS SHABA.
Saa 2:15.    SIMBA VS MTIBWA.

Ijumaa 2 Jan 2015 
Jioni saa 10:00  KMKM VS MTENDE              KUNDI        B
Usiku Saa 2:00 KCC VS AZAM.                        KUNDI       B

Jumamosi 3Jan 2015.
Jioni Saa 10:00 JKU VS MTIBWA                  KUNDI       C
Usiku Saa 2:00 YANGA VS SC.VILLA             KUNDI      A

Jumapili  4 Jan 2015                           
Jioni saa 9:00 KCC VS MTENDE                        KUNDI    B
Jioni saa 11:00 KMK VS AZAM.                          KUNDI    B 
Usiku saa 2:15. MAFUNZO VS SIMBA                KUNDI    C 

Jumatatu 5 Jan 2015                     
Jioni saa 10;00 SC VILLA VS SHABA               KUNDI    A
Usiku saa 2:00 YANGA VS POLISI                     KUNDI    A

Jumanne 6 Jan 2015
Jioni saa 9:00 AZAM VS MTENDE                   KUNDI     B
Jioni saa 11: 00  MTIBWA VS MAFUNZO        KUNDI     C 
Usiku saa 2:15. SIMBA VS JKU                           KUNDI    C

Jumatano 7 Jan 2015
Jioni saa 9;00  POLISI VS SC VILLA                KUNDI      A 
Jioni saa 11:00  KCC VS KMKM                         KUNDI     B
Usiku saa 2:15. YANGA VS SHABA                  KUNDI      A

Alhamisin 8 Jan 2015.
Jioni saa 10:00  WINNER B VS RUNNERS  A.
Usiku saa 2:00 WINNER  A VS BEST LOOSER 1

Ijumaa 9 Jan 2015
Jioni saa 11:00 WINNER C VS BEST LOOSER 2
Usiku saa 2;00 RUNNERS  B VS RUNNERS C.

Jumapili 11 Jan 2015.
SEMIFINAL 1 
Jioni saa 10:00. WINNER 1 VS WINNER 2
SEMIFANAL 2
Usiku saa 2:00  WINNER  3 VS WINNER 4
 Tarehe 13/1/2015 itakuwa fainali ya michuano hiyo itakayofanyika usiku katika uwanja wa amaan Zanzibar. kuhitimisha michuano hiyo.

Newz Alert! Mtuhumiwa wa Dawa za Kulevya apigwa risasi akitoroka


MTUHUMIWA wa kesi ya Dawa za Kulevya, anayedaiwa kuwa ni  raia wa Sierra Leone amepigwa risasi na kufariki katika harakati zake za kutaka kutoroka katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Inadaiwa mtuhumiwa huyo Abdul Koroma alikuwa akitaka kuwaacha kwenye mataa askari Magereza kwa kuruka uzio kabla ya kuwahiwa kwa kupigwa risasi.
I





Bw' Misosi akifa hataki promo videoni

MSANII Joseph Rushahu 'Bwana Misosi' anajiandaa kurekodi video ya wimbo wake mpya uitwao 'Nikifa Sitaki Promo' ambao ameimba akishirikiana na waimbaji nyota wa muziki wa dansi Ramadhan Masanja 'Banzastone' na Athanas Montanabe wa  bendi ya Wana Extra.
Akizungumza kwa njia ya simu akiwa jijini Tanga alipoenda kwa mapumziko ya Sikukuu ya Mwaka Mpya, Misosi aliyetamba na nyimbo kama 'Nitoke Vipi', 'Mungu Yupo Bize' na 'Watoto wa Kitanga', alisema video ya wimbo huo alioutengenezwa katika studio za Plexity Records chini ya mtayarishaji aitwaye Zest inaanza kurekodiwa wiki ijayo akirejea jijini Dar es Salaam.
Misosi alisema alikwama kuitengeneza mapema video hiyo kutokana na pilikapilika za Krismasi na kuwepo nje ya jiji kwa waimbaji walioshirikiana kuutengeneza wimbo huo.
"Kwa sasa nipo Tanga na ninatarajiwa kurejea mwishoni mwa wiki ili kujipanga kuanza kutengeneza video ya wimbo wangu mpya," alisema.
Msanii huiyo alidokeza kuwa, mara baada ya kukamilika kurekodiwa kwa video hiyo ataiachia pamoja na 'audio' yake na alisema itakuwa ndani ya mwezi huu wa Januari.
"Haiwezi kuvuka mwezi huu kabla ya kazi hiyo mpya kutoka hadharani, nataka kuuanza mwaka nikiwa Misosi mpya," alisema.

Tuesday, December 30, 2014

Mwanasoka Bora Afrika kujulikana Januari 8 nchini Nigeria

http://www.football-marketing.com/wp-content/uploads/2012/01/PUMA-Yaya-Toure.jpg
Yaya Toure
SHIRIKISHO la Soka Afrika, CAF linatarajia kutoa tuzo kwa Wachezaji Bora kwa mwaka huu Januari 8 mjini Lagos Nigeria.
Kiungo wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, golikipa Vincent Enyeama wa Nigeria na kiungo Yaya Toure mmojawao ndiye atakayetwaa tuzo ya mwaka ya Mwanasoka Bora wa Afrika.

Mbali na hao pia wachezaji wengine watatu watachuana kwenye tuzo ya Mwanasoka Bora kwa wachezaji wa ndani ya Afrika
Wachezaji wanaowania tuzo hiyo ambayo ilikuwa ikishirikiliwa na Mohammed Aboutrika wa Misri ni;
Akram Djahnit (Algeria) El Hedi Belamieri( Algeria)Firmin Mubele Ndombe (DR Congo)
Kwa upande wa wanasoka wawanawake wanaowania tuzo hizo ni;
Annette Ngo Ndom (Cameroon) Asisat Oshoala (Nigeria) Desire Oparanozie (Nigeria)
Upande wa wanasoka chipukizi tuzo hiyo inawaniwa na Asisat Oshoala (Nigeria) Fabrice Ondoa (Cameroon),Uchechi Sunday (Nigeria)
Wanaowania tuzo ya kipaji kinachochipukia ni
Clinton N’jie (Cameroon) Vincent Aboubakar (Cameroon) Yacine Brahimi (Algeria)
Makocha wanaowania tuzo hizo za CAF ni;

Florent Ibenge (DR Congo) Kheireddine Madoui (ES Setif) Vahid Halilhodžić (kocha wa zamani wa Algeria)
Timu Bora ya Mwaka tuzo yake inawaniwa na; Algeria, Libya, Nigeria
Timu Bora ya Wanawake ya Mwaka ni;
Cameroon, Nigeria, Nigeria U-20
Klabu bora ya Mwaka
Al Ahly (Egypt) AS Vita (DR Congo) ES Setif (Algeria)
Huku Rais wa Tp Mazembe Moise Katumbi Chapwe akitarajiwa kupewa tuzo ya kiongozi bora wa michezo wa mwaka.

Real Madrid yasisitiza Gareth Bale HAUZWI kokote!

Bale celebrates winning the FIFA Club World Cup earlier in December 
Gareth Bale
RAIS wa klabu ya Real Madrid, Florentino Perez amesisitiza kuwa Gareth Bale hauzwi na kuzitaja taarifa kwamba amepokea ofa kutoka Manchester United ni upuuzi mtupu.
Bale, aliyejiunga na Real Madrid akitokea Tottenham kwa dau lililovunja rekodi ya uhamisho duniani ya karibu Pauni Mil. 85 Septemba 2013 amekuwa akidaiwa kuwa yu mbioni kurejea tena Ligi Kuu ya England.
United imedaiwa kuwa tayari kutoa Pauni 120 ili kumnyakua nyota huyo wa kimataifa wa Wales, lakini Perez amepuuza taarifa hizo na kudai Bale, 25 hawezi kuondoka Santiago Bernabeu.
Perez aliliambia gazeti la michezo la Marca: "Hatujapokea ofa yoyote kuhusu Gareth Bale, siyo klabu ya Manchester United wala klabu nyingine yoyote.,"
"Kadhalika hatutakuwa tayari kusikilizia ofa yoyote juu ya Bale kwani ni mchezaji muhimu mno kwetu," alisema Perez.
Bale amekuwa na wakati mzuri tangu ajiunge na kigogo hicho cha Hispania akiunda safu kali ya ushambuliaji akishirikiana na  Cristiano Ronaldo na Karim Benzema.
Nyota huyo wa zamani wa Southampton aliisaidia Real Madrid kunyakua taji la 10 la Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuwafumua wapinzani wao wa Madrid, Atletico Madrid kwa mabao 4-1 katika fainali iliyozikutanisha timu hasimu za jiji moja.

Crsitiano Ronaldo kidume 2014, atwaa tuzo nyingine


MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo amemaliza mwaka kwa staili ya aina yake kwa kubeba tuzo nyingine ya mchezaji bora wa mwaka au Globe Soccer Awards huko Dubai.
Mreno huyo amekuwa na mwaka mzuri huku akivunja rekodi kwa kuwa na mabao mengi katika msimu mmoja wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya wakati alipoiongoza Real Madrid kunyakuwa taji lake la 10 la michuano hiyo.
Ronaldo pia anapewa nafasi kubwa ya kushinda tuzo ya Ballon d’Or inayotolewa na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA kwa mara ya pili mfululizo Januari 12 mwakani licha ya kukabiliwa na upinzani kutoka kwa Lionel Messi na Manuel Neuer alioingia nao kwenye 3 Bora ya tuzo hiyo.
Mchezaji huyo ambaye alikuwepo mwenyewe kupokea tuzo hiyo katika sherehe zilizofanyika katika Hotel ya Atlantis Palm aliwashukuru mashabiki, wachezaji wenzake na viongozi wa Real Madrid kwa ushirikiano wanaompa na kufanya kupata mafanikio hayo.
Aidhsa kocha wa Madrid Carlo Ancelotti naye alitunukiwa tuzo hiyo kama kocha wa bora wa mwaka kutokana na mafanikio aliyoipa timu hiyo kwa mwaka huu

BABY MADAHA ANAKUJA NA SAINT & GHOST

http://api.ning.com/files/KtF8hZpsH-3lMXDW7ufVoIr4iNPkkwwMRNxku*jb0MDMU7Iz*sLL7Hfl9BdoYxrd9FpJEMbPW8DsGjHTHEQX05k1rl-IZhsZ/babymadaha.jpg
Baby Madaha
BAADA ya kutuymia muda mrefu akiwa amejichimbia Kenya kufanya shughuli zake za muziki, mwanadada Baby Madaha anajiandaa kuvunja ukimya kwenye soko la filamu kwa kuibuka na 'Saint & Ghost'  ambayo imesheheni nyota mbalimbali wa filamu nchini.
Akizungumza na MICHARAZO mapema leo, Baby Madaha alisema filamu hiyo inayotengenezwa kupitia kampuni yake, iitwayo Darkangel Film Production and Entertainment imewashirikisha wakali kama Kulwa Kikumba 'Dude', yeye (Baby Madaha), Hidaya Njaidi,  Grace Mapunda 'Mama Kawele', Ramadhani Ally 'Tafu', Ahmed Olotu 'Mzee Chillo' na wengine.
"Nimbo chimbo kwa sasa natengeneza filamu yangu iitwayo 'Saint and Ghost' ambayo naitengeneza kupitia kampuni yangu na inawashirikisha wasanii mbalimbali nyota nikiwamo mimi mwenyewe, Mzee Chillo, Mama Kawele, Mama Njaidi, Taffu, Dude na wengine na ni bonge la kazi la kuanzia mwaka 2015," alisema Baby Madaha.
Mwanadada huyo anayetamba na nyimbo kama 'Summer Holiday' akiwa na albamu mbili sokoni za Amore na Desperado' amejipatia umaarufu mkubwa katika uigizaji wa filamu baadhi ya kazi alizowahi kuzicheza ni 'Nani', 'Misukosuko3', 'Mpishi', House Na.44' na 'Ray of Hope' iliyoshinda tuzo ya kimataifa nchini Nigeria.

DECEMBER LIKIZO FESTIVAL KUFANYIKA KESHO MBEZI BEACH

TAMASHA la tatu la December Likizo Festival linatarajiwa kufanyika kesho jijini Dar es Salaam likihusisha na maonyesho ya muziki, mavazi na filamu sambamba na semina mbalimbali juu ya kuboresha ufanisi wa vipaji vya sanaa.
Mratibu wa tamasha hilo, Steven Sandhu 'Triple S',  alisema kwa wiki nzima kumekuwa na shughuli mbalimbali za tamasha hilo na leo ndiyo kilele chake.
Sandhu ambaye ni mwanamitindo na muigizaji filamu alisema kilele cha tamasha (le grand Finale) la mwaka huu litafanyika kwenye hoteli ya Landmark iliyopo Mbezi Beach.
"Tamasha la tatu la 'December Likizo Festival kwa mwaka wa 2014 litafikia kilele kesho kwenye Landmark Hotel kwa maonyesho mbalimbali na kwa wiki nzima kuelekea kilele cga tamasha hilo kulikuwa na shughuli mbalimbali," alisema.
Sandhu alisema anashukuru uitikiaji wa wito kwa wasanii na washiriki wengine wa tamasha hilo na kuongeza imani yake kama ilivyokuwa kwa matamasha mawili ya nyuma ya mwaka 2012 na 2013, hata la mwaka 2014 litafana zaidi," alisema.

KWA MASHABIKI WA WENGE MUSICA BCBG

Liverpool yaendelea 'maajabu' EPL, yaifumua Swansea City 4-1

The 26-year-old is mobbed by his Liverpool team-mates after helping his side towards a vital three points at Anfield
Liverpool wakishangilia mabao yao
Moreno now has two Premier League goals to his name since joining Liverpool from Sevilla in the summer
Moreno akishangilia bao la kuongoza la Livwerpool
Reds midfielder Lallana runs towards the Kop in celebration of his second half goal
Adam Lallana akishangilia moja ya mabao yake mawili
Three Swansea players look on as Lallana sends a left-footed finish past Fabianski to send Liverpool into a commanding lead
Lallana akiwatesa mabeki wa Swansea
MABAO mawili yaliyofungwa na Adam Lallana na moja la kujifunga la beki wa Swansea City imeiwezesha Liverpool kupata ushindi wake wa pili mfululizo katika Ligi Kuu ya England.
Ikiwa kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Anfield, Liverpool ilianza pambano hilo kwa mashambulizi langoni mwa wageni wao na kuandika bao la kwanza katika dakika ya 33 kupitia kwa Alberto Moreno aliyemalizia kazi ya Henderson.
Kipindi cha pili kilikuwa na mafanikio zaidi kwa vijana wa Branden Rodgers baada ya Lallana kuandika bao la pili dakika ya 51 kabla ya Swansea kuandikisha bao lao pekee dakika moja baadaye kupitia Gief Sigurdsson.
Adam Lallana alirudi tena kambani kwa kuandika bao la tatu la Liverpool dakika ya 61 na dakika tano baadaye beki wa Swansea City, Shelvey alijifunga katika harakati za kuokoa mpira na kuifanya Liverpool kupaata ushindi mnono wa mabao 4-1 na kuchupa hadi nafasi ya nane katika msimamo wa ligi hiyo.
Liverpool wamefikisha pointi 28 sawa na Swansea lakini imefanikiwa kuwashusha wapinzani wao kwa uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Ushindi huo wa Liverpool wa mabao manne ni wa kwanza tangu nyota wao, Lusi Suarez kutimkia Barcelona.

Kumekucha! Patrick Phiri atimuliwa Simba, Kopunonic amrithi

Patrick Phiri (kushoto) aliyetimuliwa Simba wiki kadhaa baada ya Yanga kumtimua Marcio Maximo
http://umwungeri.com/wp-content/uploads/2014/09/1331248128Goran-Kopunovic.jpg
Kocha mpya wa Simba, Goran Kopunovic
BAADA ya Yanga kumtimua kocha wao Marcio Maximo kutokana na kipigo cha mechi yao na mtani wao Simba kwenye mechi ya 'bonanza' ya Nani Mtani Jembe2, Simba nao wamefuata mkumbo huo baada ya kutangaza kumtimua kocha wao Mzambia, Patrick Phiri.
Simba imemfukuza kocha huyo kutokana na kutoridhishwa na matokeo iliyopata timu yao katika msimu huu ikiwamo kipigo cha bao 1-0 ilichopewa na Kagera Sugar mwishoni mwa wiki.
Kocha huyo aliyemrithi Zdravkov Logarusic aliyetimuliwa mapema amekuwa hana matokeo mazuri tangu ajiunge na timu hiyo August mwaka huu.
Hii ni mara ya tatu kwa Phiri kuifundisha Simba tangu ajiunge na timu hiyo August mwaka huu ameiongoza katika michezo 22 na kushinda nane, kati ya hizo ni moja tu ya Ligi Kuu na moja ya Nani Mtani Jembe.
Aidha taarifa zinasema kuwa Mserbia Goran Kopunovic kutoka Polisi Rwanda ndiye atakayeinoa Simba na kocha huyo atawasili kesho Jumatano.
Kocha huyo mpya aliyewahi kuzinoa timu za APR atakuja na msaidizi wake Mnyarwanda Jean Marie Ntagawabila na kumaanisha kuwa hata kocha msaidizi wa Simba aliyekuwa na Phiri, Suleiman Matola naye ameenda na maji katika maamuzi yaliyofikiwa na uongozi wa juu wa Simba.
Simba na Yanga kwa muda mrefu sasa zimekuwa na utamaduni wa kutimua na kuajiri makocha wapya kila mara bila kujali vipindi wanavyokuwa na timu zao, jambo ambalo linadaiwa limekuwa likiwachanganya wachezaji kwa kushindwa kunasa mafunzo ya makocha wanaoletwa na kabla ya kuzoeana nao hutimuliwa.
Bahati mbaya ni kwamba klabu hizo zimekuwa zikitimua makocha hata wakati timu zao zikiwa katika nafasi nzuri tofauti na inavyoshuhudiwa Ulaya klabu zikiwatimua makocha kutokana na timu kufanya vibaya.