STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, June 29, 2013

LINA ALLAN NDIYE MISS REDD'S KANDA NYANDA ZA JUU KUSINI.

 MSHINDI WA MISS REDD'S TANZANIA KANDA ZA NYANDA ZA JUU KUSINI LINA ALLAN AKIWA ANAFURAHIA BAADA YA KUWA MSHINDI WA KWANZA
  MSHINDI WA MISS REDD'S TANZANIA KANDA ZA NYANDA ZA JUU KUSINI LINA ALLAN AKIWA NA WASHINDI WENGINE AMBAO WALISHINDA TANO BORA
 MSHINDI WA MISS REDD'S TANZANIA KANDA ZA NYANDA ZA JUU KUSINI LINA ALLAN AKIVISHWA TAJI LA USHINDI NA MSHINDI AMBAYE ALIKUWA ANASHIKILIA TAJI HILO NAOMI JONES

 
 WASHIRIKI WA MISS REDD'S TANZANIA KANDA ZA NYANDA ZA JUU KUSINI WAKIWA WANAONESHA VIPAJI
 BWANA HIDAN ERICCO AKITANGAZA WASHINDI WALIOINGIA KATIKA TANO BORA
 WASHINDI WALIOFANIKIWA KUINGIA KATIKA TANO BORA 

PICHA NA MBEYA YETU

Friday, June 28, 2013

MWANADADA ANASWA NA 'UNGA' WA SH. MIL. 170/

Mwanadada Saada akiwa katika pozi
Saada siku ya mahafali yake ya kuhitimu masomo ya Chuo Kikuu mwaka jana
MWANADADA Mfanyabiashara anayefahamika kwa jina la Saada Kilongo (26), amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi akishtakiwa kwa kosa ya kukamatwa na na dawa za kulevya zenye thamani ya Sh Milioni 170.
Mwanadada huyo alifikishwa katika mahakama hiyo kusomeshwa mashtaka yake jana, ambapo kesi yake ilitajwa mbele ya Hakimu Mfawidhi  Nyigulila Mwasebo na hakuweza kujibu lolote na kisha  kurudishwa rumande mpaka Julai 10 wakati kesi yake itakapotajwa tena.
Kwa mujibu wa watu wanaomfahamu Saada wanadokeza kuwa ni mwaka jana tu alitoka kuhitimu masomo yake ya Chuo Kikuu.
SOURCE -ZEDDYLICIOUS

AMANA SHOOTING MABINGWA AIRTEL RISING STARS

Nahodha wa Amana Shooting, Abdul Mussa akipokea kombe la ubingwa wa irtel Rising Stars mkoa wa Ilala kutoka kwa mwenyekiti wa chama cha soka Ilala, Emmanuel Kazimoto huku ofisa wa IDYOSSA, Hugo Seseme (katikati) akishuhudia kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam jana.
 
Mshambuliaji  wa Amana Shooting Juma Kizairo akiwania mpira wa juu dhidi ya mchezaji wa  Buguruni Youth Center, Edward Jonas wakati wa mashindano ya soka ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars mkoa wa Ilala kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam jana. Amana Shooting ilishinda 1-0.


Mshambuliaji wa Amana Shooting, Juma Kizairo akichanja mbuga kuelekea golini wakati wa mashindano ya soka ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars mkoa wa Ilala kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam jana. Amana Shooting ilishinda 1-0.

Timu ya Amana Shooting imetwaa taji la ubingwa wa mkoa wa Ilala katika mashindano ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 ya Airtel Rising Stars baada ya kuifunga Buguruni Youth Centre 1-0 katika mchezo wa mwisho uliofanyika katika uwanja wa kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam, Alhamisi Juni 27.

Gori la pekee la Amana Shooting liliwekwa wavuni na mshambuliaji hatari Issaka Majaliwa dakika ya 32 baada ya ya kuwalamba chenga mabeki wa Buguruni Youth Center na kufunga kirahisi na kumuacha kipa Omari Hamisi akiduwaa. Hamisi Majaliwa alionyesha kipaji cha aina yake baada kuifungia timu yake magoli yote matatu iliyofunga katika mashindano hayo ngazi ya mkoa.

“Tumekiona kipaji cha huyu kijana na naamini atakuja kuwa mchezaji mzuri akiendelea kucheza kwa juhudi,” alisema katibu mkuu wa chama cha mpira wa miguu Ilala, Kanuti Daudi wakati akiongea na waandishi wa habari baada ya mchezo huo kumalizika.

Daudi alitamba kwamba kwa vipaji walivyonavyo mwaka huu timu ya Ilala kombaini ina nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa Airtel Rising Stars ngazi ya taifa

Katika jiji la Mwanza, timu ya Alliance Schools Academy aliweka hai matumaini yake ya kutwaa kombe la ubingwa wa Airtel Rising Stars ngazi ya mkoa baada ya kuibugiza timu ya Nyamagana United 4-0 katika uwanja wa Nyamagana. 

Katika mchezo huo mshambuliaji hodari Athanas Adam ndiye aliyeng’ara vilivyo akifunga ‘hat trick’ kabla ya Kelvin Falu hajahitimisha karamu hiyo ya magoli dakika chache kabla ya mchezo kumalizika.  

Mashindano ya Airtel Rising Stars ngazi ya taifa yatashirikisha timu za wasichana na wavulana kutoka mikoa tisa – Kinondoni, Ilala, na Temeke itakayoleta timu za wasichana na wavulana wakati Tanga, Kigoma na Ruvuma zitashirikisha wasichana pekee huku mikoa ya Morogoro, Mwanza na  Mbeya ikiwa na timu za wavulana tu.

Maandalizi kwa ajili ya mtanange huo wa taifa yamekamilika na timu kutoka mikoani zinatarajiwa kuanza kuwasili jijini Dar es Salaam wikiendi hii tayari kwa mashindano hayo yatakayofanyika kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Karume kuanzia Julai 2 hadi 7.

Fainali za ARS Taifa vile vile zilifanyika katika uwanja huo ambapo Temeke waliibuka washindi.

Rais Jakaya Kikwete afanya uteuzi

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu, Dk Jakaya Kikwete amefanya uteuzi wa Naibu Kamishna Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokozi kwa kumteua Luteni Kanali Lidwino Simon Mgumba kushika nafasi hiyo. Taarifa rasmi ya uteuzi huo inasomeka hapo chini;
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiOxJxLYgFuxn-RwAXKouftWopq0s59oACZeLnIxhuGYZO7b4rk5PKcF-xexbeR5LNjB4NKtYUjc5DLWRPnKMBEftQHyApfFCvnLUWk5JhTjm4IsfqDL4HYvjMQc5RAN2zTLG0oJm7mMF0/s640/JL.jpg
Add caption

NAIBU MKURUGENZI WA CUF ATEKWA MTWARA

 
NAIBU Mkurugenzi wa Oganaizesheni Uchaguzi na Bunge wa Chama Cha Wananchi CUF - Shaweji Mketo ametekwa na wanausalama na wanajeshi waliopiga kambi Mtwara MJINI.

Mketo alienda Mtwara MJINI jana na Leo asubuhi alihudhuria mahakamani ambapo kesi ya Mwenyekiti wa vijana CUF taifa (JUVICUF) Katani Ahmed Katani iliahirishwa.

Baada ya ahirisho hilo, Mketo alikutana na wanachama wa CUF walioko Mtwara MJINI na kufanya nao kikao cha ndani. Katika kikao hicho alielezwa namna wananchi wanavyoteswa kikatili na askari jeshi. Moja ya jambo aliloelezwa ilikuwa ni juu ya mama mmoja aliyebakwa na askari na kisha mamlaka zote zimekataa kumsaidia kuujulisha umma unyama aliofanyiwa.

Mkurugenzi wetu Mketo alipojulishwa jambo hilo aliomba akutane na mama huyo. Baada ya kikao, Mketo na viongozi waandamizi wa wilaya akiwamo mhe. Kulaga ambaye ni katibu wetu wa wilaya walianza safari ya 
kuelekea Msimbati ambako mama huyo amejisitiri baada ya kubakwa na kunyimwa msaada na vyombo vilivyopaswa kumsaidia.

Mketo alifika Msimbati na kukutana na mama huyo na akachukua ushahidi mbalimbali. Wakati wanarudi Mtwara MJINI ndipo walipotekwa na Askari jeshi. Hivi sasa ukipiga simu za Mketo 0782 095 434 na ile ya Kulaga 0789 604968 zote zinapokelewa na askari jeshi na wanajibu kwa matusi ya nguoni na kebehi za Hali ya juu.

Tumefanya juhudi za kuwasiliana na viongozi mbalimbali wa ngazi za juu wa polisi na serikali bila mafanikio. Nimempata hewani RPC wa Mtwara ambaye anakiri kuwa hajawashikilia viongozi wetu. Nimemjulisha kama wako mikononi mwa wanajeshi na wanausalama anasema hana mamlaka yoyote juu yao. HII ina maana kuwa mkuu wa Jeshi la polisi wa mkoa Leo hana dhamana ya raia wanaokamatwa na kuteswa katija eneo lake la kazi. Kama Leo Mtwara iko chini ya Jeshi la wananchi na wanatesa watakavyo, Mbona rais hajatangaza Hali ya hatari Mtwara??

Kwa taarifa zenye ushahidi, hadi sasa askari jeshi hao wameshawakamata na kuwapeleka makambini zaidi ya wananchi 100 ambapo wote hao wameteswa kinyama kwa kuvuliwa nguo zote, kumwagiwa maji mwili mzima, kupakwa chumvi mwilini na kuanza kutandikwa viboko vya miti maalum na kisha wakimaliza kuteswa huachiwa na kurudishwa uraiani kuuguza vidonda vinavyotokana na vipigo. Hakuna utawala wa sheria Mtwara, ni ubabe, ukatili na dhuluma. Hakuna mahakama wala JAJI, kila anayedhaniwa kuwa anapaswa kukamatwa lazima atakamatwa na kamwe hapelekwi mahakamani, anateswa kikatili na kuachiwa.

Kwa namna askari waliowashikilia wanavyojibu kikatili, unaweza kupata picha Mketo, Kulaga, dereva Kashinde na yeyote mwingine walivyo chini ya mateso makali ya wanyama hawa.

Tunaposema kuwa nchi hii kuna siku kila mtu atachoka tusilaumiwe. Siku hiyo itakapofika hatutasita kuamuru raia wapambane na askari kila watakapowaona, tutakapofika hapo nchi itabakia vipandevipande. Haiwezekani Leo kusini mwa Tanzania kumegeuka sehemu ya mateso, ukatili na unyama.

Tunaendelea kupambana kwa nguvu kuhakikisha kuwa serikali inawajibika, jeshi linawajibika. Hatutakubali kuona uhuru na utu wa wananchi wa nchi hii unapotezwa kwa faida za watu wachache.

Vyombo vya HABARI hivi sasa haviripoti chochote kuhusu mateso ya wananchi Mtwara. Ripoti za mateso ni Arusha, DSM na Mwanza. Nani atasimamisha ukatili huu wa watu wasio na hatia kama siyo mimi na wewe?

Mawakili wetu pamoja na mimi binafsi tunaelekea Mtwara kesho, lazima haki itendeke na tutaitafuta haki kokote na kwa njia yoyote.

J. Mtatiro,
Naibu Katibu Mkuu,
Chama Cha Wananchi CUF,
Tanzania Bara.
+255717536759.

Golden Bush, Chuo Veterani kumaliza ubishi kesho Mlimani

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjv1SWGpAVVh3AeFAONPcqAEhha3BStjvn0YNGauB0GUtXNqJi_5DzbDbFPasom9XhppZgtV61Wt3Tx5XDUuOYbqCg2Y_fAaCiqjp8Kgx8gkWVdVA2RrALkRqpPNAZ5t_EpMpEJpL_xt04/s1600/Golden.JPG
Kikosi cha Golden Bush Veterani ambacho kesho asubuhi kinatarajiwa kuvaana na Chuo Kikuu Veterani
BAADA ya tambo za muda mrefu kutoka kwa wachezaji wa timu mbili zenye upinzani za Golden Bush Veterani na Chuo Kikuu Veterani, mzizi wa fitina unatarajiwa kukatwa rasmi kesho wakati zitakaposhuka dimbani viwanja vya Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM) kupambana.
Timu hizo zimekuwa zikitupiana vijembe vya hapa na pale kwamba ni lazima mmoja kesho alie, huku Golden Bush ambayo mlezi wake aliyewahi kung'aa na timu ya Chuo Kikuu Veterani akiwachimba mkwara wapinzani wake kwamba kesho wakisalimika basi kipigo kitakuwa kama walichopewa Tahiti mbeleya Hispania katika michuano ya Kombe la Mabara inayoendelea nchini Brazili.
Mlezi na msemaji huyo, Onesmo Waziri 'Ticotico' anayetarajiwa kuongoza safu ya ushambuliaji ya timu yake asubuhi ya kesho, alisema kikosi chao kipo imara na kimejiandaa vyema kwa pambano hilo baada ya wikiendi iliyopita kutamba kwenye Bonanza maalum Jimbo la Ukonga kwa kutwaa taji.
"Tunapenda kuwafahamisha wapenzi wa soka kwamba siku ya jumamosi tarehe 29 June viwanja vya Chuo kikuu cha Dar ES salaam kutakuwa na patashika ambapo wapinzani wa jadi Golden Bush na Chuo veterans wataumana kuanzia saa moja na nusu asubuhi," alisema Ticotico na kuongeza;
"Ni mechi ambayo mpenzi wa soka hutakiwi kukosa kwasababu timu zote zitachezesha vikosi vya kwanza kabisa. Maandalizi yamekamilika kwa asilimia 100 na timu zote ziko tayari kwa mpambano huo," alisema.
Mshambuliaji huyo matata, alisema makocha wao, Madaraka Seleman 'Mzee wa Kiminyio' na Herry Morris 'Ng'onyi' tayari wamekiweka hadharani kikosi chao kitakachoshuka dimbani kuwaadhibu Chuo ambapo alisema golini atakaa nyota wa zamani wa Yanga, Steven Marash, shavu la kulia atasimama Salum Swedi 'Kussi', kushoto Faraj Salum 'Kipara' huku halfback four atasimama John Mwansasu na mkoba Wisdom Ndhlovu.
"Namba sita atacheza Godfrey Bonny 'Ndanje' na winga wa kulia atacheza yeye 'Ticotico', na namba nane atasimama Salum Athuman 'Mbududu', mkali wa zamani wa Jangwani, na mshambuliaji wa kati atacheza Kudura Omar, huku Inside 10 Omary Mgonja na winga wa kushoto itamilikiwa na Abuu Ntiro.
Ticotco alisema wachezaji wa akiba watakaowapokea wenzao ni wakali zaidi kuliko hata watakaolianza pambano hilo na kuhimiza mashabiki wajitokeze kwa wingi kuona wanavyowatoa nishai wapinzani wao ambao nao wamejitutumua na kutamba kwamba hawana maneno zadi watafanya kazi moja tu ya kuzima ndoto za Golden Bush Veterani.

NMB BUSINESS CLUB, SASA ZAMU YA KARATU


Mkuu wa kitengo cha wajasiliamali wadogo wadogo na wakati wa NMB ,Filbert  Mponzi akimkabidhi mwenyekiti wa  NMB Business Club Paulith Jack  mara tu baada ya kuibuka kidedea kwenye mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa NMB Business Club Karatu .


BENKI ya NMB imeendelea kuwa kinara katika kubuni na kuboresha huduma mbali mbali za kibenki, ili kuwawezesha wateja wake kupata unafuu na urahisi wa upatikanaji wa huduma za kibenki nchini Tanzania.

Katika kulizingatia hili, NMB imezidi kuzindua klabu maalum za wafanyabiashara maarufu kama NMB Business Club. Hadi sasa zaidi ya NMB Business Club 29 zimekwisha zinduliwa nchi nzima.

Kupitia NMB Business Club wajasiliamali wanaowezeshwa na benki ya NMB wamekua wakipata nafasi ya kujifunza jinsi ya  kuandika michanganuo ya biashara zao na pia kuendelea kua vinara wa biashara.
Mhandisi mkuu wa Wilaya ya  Karatu, Tulinumpoki Mwakalukwa akitoa shukrani zake  kwa NMB mara baada ya kuzindua rasmi  NMB Business Club  wilaya ya Karatu. Kushoto ni Meneja wa NMB tawi la Karatu , Evarist Mtaro na mkuu wa kitengo cha wajasiliamali wadogo wadogo na wakati  wa NMB Filbert  Mponzi.
Sehemu ya wanachama wa NMB Business Club wilaya ya Karatu wakifurahia uzinduzi wa NMB Business Club.

Yosso wawili Bongo waula Umangani

http://multivu.prnewswire.com/mnr/prne/aspire/40779/images/40779-football-dreams-logo.gif
Na Boniface Wambura
WACHEZAJI wawili kutoka Tanzania wamechaguliwa miongoni mwa 50 waliofanyiwa majaribio nchini Uganda kwa ajili ya kuingia katika kituo cha kuendeleza vipaji (centre of excellence) kilichoko Doha nchini Qatar kupitia mpango wa kukuza vipaji wa Aspire Football Dream.
Abdulrasul Tahir Bitebo (15) ambaye ni mshambuliaji kutoka Kituo cha Uwanja wa Karume, na Martin Omela Tangazi (14) ambaye ni beki kutoka Kituo cha Ukonga ndiyo waliochaguliwa kutoka Tanzania kuingia katika kituo ambapo watakaa kwa mwezi mmoja kabla ya kusaini mkataba rasmi wa kuendelezwa.
Wachezaji wengine walikuwa wakitoka katika nchi za Uganda na Kenya. Mchezaji mwingine aliyefuzu katika nafasi tatu zilizokuwepo ni kutoka nchini Kenya.
Mpango wa Aspire Football Dream unafadhiliwa na Mtoto wa Mfalme wa Qatar katika nchi 16 duniani, na kwa hapa nchini uko chini ya Idara ya Ufundi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
TFF ina jumla ya vituo 14 vya kuendeleza vipaji kupitia mpango huo wa Aspire Football Dream. Vituo hivyo ni Karume, Kigamboni, Tandika, Kawe, Ukonga, Kitunda, Mbagala, Magomeni, Makongo, na Tabata vilivyo katika Mkoa wa Dar es Salaam. Vingine ni Bagamoyo kilichopo mkoani Pwani, Morogoro, Arusha na Moshi mkoani Kilimanjaro.
Kituo kingine cha kuendeleza vipaji (centre of excellence) cha Aspire kipo Dakar nchini Senegal.

Marudiano ya Nusu Fainali za RCL kuchezwa wikiendi hii

Na Boniface Wambura
Mechi za marudiano za hatua ya nne ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) zitachezwa Jumapili (Juni 30 mwaka huu) kwenye viwanja vya Sokoine jijini Mbeya, na Kambarage mjini Shinyanga.
Friends Rangers ya Dar es Salaam ambayo katika mechi ya kwanza ilifungwa nyumbani mabao 3-0 itakuwa mgeni wa Stand United FC mjini Shinyanga wakati Kimondo SC itaikaribisha Polisi Jamii ya Mara jijini Mbeya. Katika mechi ya kwanza timu hizo zilitoka sare ya mabao 2-2.
Hatua ya mwisho ya RCL itachezwa Julai 3 mwaka huu kwa mechi za kwanza wakati zile za marudiano zitafanyika Julai 7 mwaka huu. Timu tatu za kwanza zitapanda daraja kucheza Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu ujao.

TFF kuendesha kozi sita tofauti


Na Boniface Wambura
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) litaendesha kozi sita tofauti za mpira wa miguu kati ya Julai na Septemba mwaka huu.
Kozi hizo ni FIFA 11 For Health itakayofanyika Hombolo mkoani Dodoma kuanzia Julai 8 hadi 19 mwaka huu. Julai 6 hadi 15 mwaka huu kutakuwa na kozi ya mpira wa miguu wa ufukweni (Beach Soccer) itakayofanyika jijini Dar es Salaam.
Waamuzi wa FIFA nao watakuwa na kozi itakayofanyika kati ya Agosti 22 hadi 26 mwaka huu jijini Dar es Salaam wakati kozi ya ukocha kwa ajili ya Copa Coca-Cola itafanyika jijini Dar es Salaam kati ya Agosti 12 na 17 mwaka huu.
Vilevile kutakuwa na kozi ya mpango wa grassroots unaolenga wachezaji mpira wa miguu (wasichana na wavulana) wenye umri kuanzia miaka 6-12 itafanyika kuanzia Septemba 9 hadi 13 mwaka huu jijini Dar es Salaam wakati tamasha (festival) la grassroots litafanyika Uwanja wa Karume, Septemba 14 mwaka huu.

Michuano ya Kilwa Cup yafikia patamu


MICHUANO ya soka iliyoandaliwa na Mbumbe wa Kilwa Kusini, imefikia patamu baada ya timu nne kupenya hatua ya Nusu Fainali.
Timu hizo zilizopenya hatua hiyo inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi mwanzoni mwa wiki ijayo ni pamoja na Kisiwani Fc, Fresh Nigger, Transporter Fc na Masoko Veterani.
Kwa mujibu wa Kamati ya mashindano hayo yaliyodhaminiwa na Mbunge wa Jimbo hilo, Seleman Said Bungura 'Bwege' nusu fainali ya kwanza itafanyika Jumatatu Julai Mosi kwa pambano kati ya Kisiwani dhidi ya  Masoko Veterani ambayo ilipenya hatua hiyo baada ya kuinyuka Mpara Fc katika hatua ya robo fainali kwa mabao 2-0 yaliyofungwa na Shaaban Kassali na Salum Tery
Nusu Fainali ya pili itachezwa Jumanne Julai 2 kwa pambano la kukata na shoka kati ya Transporter na Fresh Nigger.
Kocha wa Masoko Veterani, Abdallah Ahmad, ametamba timu yake kuibuka na ushindi katika pambano lao dhidi ya Kisiwani licha ya kwamba wapinzani wao ni timu ya nnyumbani kwao Kilwa Kisiwani.
Ahmad alisema amewaandaa vyema vijana wao kuendelea kutoa dozi kama ilivyofanya kwa Mpara ili kutimiza ndoto zao za kuwa mabingwa wa michuano hiyo.

Redd's Miss Vyuo Vikuu Tanzania 2013 kupatikana Julai 5

Mratibu wa shindano la Redd's Miss Vyuo Vikuu Tanzania, Agnes Mathew
http://www.bongo5.com/wp-content/uploads/2012/09/Msanii-Ney-wa-Mitego-naye-akipagawisha-kwa-hisia-kali.jpg
Ney wa Mitego atakayenogesha shindano hilo Ijumaa ijayo
http://gushit.com/files/bookmark_photos/61d62d0476L.jpg
Rich Mavoko naye atakuwepo siku hiyo
JUMLA ya warembo 16 wanatarajiwa kuchuana kuwania taji la urembo la Redds Miss Vyuo Vikuu Tanzania 2013 linalotarajiwa kufanyika Ijumaa ijayo (Julai 5) kwenye ukumbi wa San Cirro, Sinza jijini Dar es Salaam.
Warembo hao wanatarajiwa kusindikizwa na burudani kabambe kutoka kwa wasanii nyota nchini Ney wa Mitego, Rich Mavoko, Mori P, Rocka na madansa wengine.
Mratibu wa shindano hilo, Agnes Mathew wa kampuni ya Aggy Classic Entertainment alisema kuwa wasanii hao wawili ni baadhi ya watakaowasindikiza warembo 16 watakaochuana kwenye kinyang'anyiro hicho.
"Shindano la Redd's Miss Vyuo Vikuu Tanzania 2013, litakalofanyika Julai 5 litasindikizwa na burudani toka kwa wakali kama Ney wa Mitego, Rich Mavoko, Rocka, Mori P na wengine," alisema.
Agnes alisema maandalizi ya shindano yao yanaendelea vyema na kuwataja baadhi ya warembo watakaochuana siku hiyo ambao kwa sasa wanaendelea kujifua mazoezini katika ukumbi wa Grand Villa, chini ya mkufunzi wao, Bless Ngowi kuwa ni Sia Mtui, Feube Urio na Rosemary Alloyce.
"Warembo wengine ni pamoja na Nyangeta Kiboja, Eveline Mathew, Juliet Msaki, Severine Minga," alisema Agnes.
Mratibu huyo aliongeza kwa kuwataja wadhamini  mbalimbali waliojitokeza kulipiga tafu shindano lake kuwa ni pamoja na Ngorongoro Coservetion, Redds, Lake gas, Cocacola, Cloud's Fm, Times Fm, Grand Villa Hotel, Sibuka Tv &Radio, EATV/Radio na Magic FM.
Agnes  alisema warembo watakaoshinda mchuano hiyo mbali na kujinyakulia zawadi mbalimbali zikiwemo fedha taslim pia watapata nafasi ya kushiriki fainali za Redd's Miss Tanzania 2013 litakalofanyika baadaye mwaka huu na kutoa wito kwa mashabiki wa burudani kujitokeza kwa wingi katika shindano hilo ambalo litakuwa na burudani nyingine mbali na muziki wa kizazi kipya kama njia ya kulinogesha zaidi.

Mwisho

Thursday, June 27, 2013

Hali ya Mzee Mandela bado tete

Mzee Mandela
BINTI wa Nelson Mandela anasema kiongozi huyo wa zamani wa Afrika kusini yupo katika hali mahututi.
Makaziwe Mandela alizungumza kwenye radio ya taifa Alhamis wakati wanafamilia walipokusanyika kwenye hospitali ya Pretoria Mediclinic Heart  ambapo Bwana Mandela amelazwa kwa siku ya 19 sasa.
Rais Jacob Zuma aliahirisha safari yake kuelekea Msumbiji Jumatano baada ya kumtembelea Mandela hospitali.
Wakati huo huo Rais wa Marekani Barack Obama yupo nchini Senegal kwenye kituo chake cha kwanza katika ziara yake barani Afrika ya kuhamasisha biashara, uwekezaji na usalama wa chakula.
Ajenda zake alhamis zinajumuisha mikutano na dhifa rasmi ya chakula cha jioni na Rais wa Senegal Macky Sall pamoja na mazungumzo ya utawala wa sheria na viongozi wa mahakama katika eneo.
Bwana Obama na mke wake Michelle pia watatembelea kisiwa cha Goree, eneo la UNESCO World Heritage ambalo kutoka karne ya 15 hadi 19 lilikuwa kituo kikubwa cha biashara ya utumwa kwenye pwani ya Afrika.
Kutoka nchini Senegal, bwana Obama anapanga kuelekea Afrika kusini na kutembelea kisiwa cha Robben, gereza ambalo rais wa zamani wa Afrika kusini Nelson Mandela alifungwa kwa takribani miongo miwili. Pia atasimama nchini Tanzania kabla ya kurejea nyumbani nchini Marekani. 
 
VOA

Mwanamke matatani kwa kumuua mumewe kisa debe la Karanga


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwani Athumani

Na Esther Macha, Mbeya
MWANAMKE mmoja mkazi wa kijiji cha Iganduka wilayani Mbozi Mkoani Mbeya makrina Simbowe (42) anashikiliwa na jeshi la polisi Mkoani hapa kwa kosa la kumuua mumewe aitwaye Rodrick Mwaipasi (55)baada ya mwanamke huyo kuuza karanga debe mbili bila idhini ya mume wake.
Tukio la kifo cha mwanaume huyo linatokana na marehemu kuhoji kwa mke wake juu ya kuuza karanga debe mbili bila idhini yake na hivyo mwanamke huyo kumsukuma mume wake ambaye aliangukia kisogo na kufariki papo hapo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake Kamanda wa polisi Mkoani Mbeya Bw.Diwani Athuman alisema tukio hilo limetokea juni 24 mwaka huu majira ya saa 2.00 usiku katika kijiji cha Iganduka wilayani hapa
Baada ya marehemu kusukumwa alidondoka na kupelekwa katika hospitali mbozi mission ambapo hata hivyo alikuwa ameshafariki kutokana na kuangukia kisogo.

Aidha Diwani alisema chanzo cha mzozo huo ugomvi wa kifamilia uliotokea kati yao kisha marehemu kusukumwa na mke wake na kufariki dunia.

Hata hivyo Kamanda Athuman alisema kuwa mtuhumiwa amekamatwa na taratibu zinafanywa ili afikishwe mahakamani ,na kutoa wito kwa jamii kutatua matatizo/migogoro yao kwa njia ya mazungumzo badala ya kujichukulia sheria mkononi kwa kutumia hasira na nguvu.

Safisha Jiji yaendelea kuwaliza wafanyabiashara Dar


ASKARI WA MANISPAA YA  YA KINONDONI WAKISHIRIKIANA ASKARI JESHI LA POLISI LA KUZUIA GHASIA FFU WALIFANYA OPERESHENI SAFISHA JIJI KATIKA ENEO LA STANDI YA MABASI YA DALADA MWENGE LEO









Opresheni safisha jiji inayoendelea jijini Dar imeendelea kuwaacha wamachinga na wafanyabiashara wengine wakitimuliwa katika maeneo waliyozoea kujipatia riziki kaa inavyoonekana pichani hali ilivyokuwa Mwenge baada ya majuzi kufanywa hivyo eneo la Manzese siku chache operesheni hiyo ilipofanyika Posta.

Njemba yaua mtu kwa kisu, kisa...!

Na Esther Macha, Mbeya
JESHI la polisi Mkoani Mbeya linamshikilia Mkazi wa kijiji cha Saman’ombe wilayani Momba Mkoani hapa livingstone mulyatete (42) kwa kosa la kumuua kwa kumchoma kisu Patrick Yohana (30)baada ya marehemu kumtania mtuhumiwa kuwa amenunua piki piki mbovu.
Akizungumza na waandishi wa habari  Kaimu Kamanda wa polisi Mkoani hapa Bw. Barakael Masaki alisema kuwa tukio hilo limetokea juni 26 mwaka huu majira ya saa 12.30 mchana katika kijiji cha Samang’ombe .
Bw. Barakael alisema kuwa chanzo cha ugomvi huo kati ya marehemu na mtuhumiwa ni ugomvi uliotokea kati yao baada ya marehemu kumtania mtuhumiwa kuwa piki piki yake ni mbovu ndipo alipochukua kisu na kumchoma katika ubavu wa kulia na kusababisha kifo chake papo hapo.
Alisema kuwa taratibu zinafanywa ili mtuhumiwa aweze kufikishwa mahakamani mara moja na kujibu tuhuma hizo dhidi yake.
Aidha Kamanda Masaki ametoa wito kwa jamii kudhibiti hasira zao ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza.

Basi la Sabena lapaja ajali na kuua kichanga Mbeya


Mtambo wa Wachina ukinyenyua gari la Kampuni ya Sabena baada ya kupata ajali eneo la maji mazuri Kawetere barabara ya Chunya likiwa linaelekea Tabora leo Asubuhi.






Baadhi  ya abiria walionusurika  wakihamisha mizigo yao kutoka katika gari lililopata ajali ya Kampuni ya Sabena baada ya kupata ajali eneo la maji mazuri Kawetere barabara ya Chunya likiwa linaelekea Tabora leo Asubuhi.

Wachina wanaojenga barabara ya Chunya wakishangaa gari la Kampuni ya Sabena baada ya kupata ajali eneo la maji mazuri Kawetere barabara ya Chunya likiwa linaelekea Tabora leo Asubuhi.
Majeruhi wa ajali hiyo Ramadhani Kipese (45) akiwa na majeraha kichwani.

Kondakta wa gari la Kampuni ya Sabena Seif Salum (34) akisaidia kuokoa mizigo ya abiria baada ya kupata ajali eneo la maji mazuri Kawetere barabara ya Chunya likiwa linaelekea Tabora leo Asubuhi.

Gari la Polisi likiwa eneo la tukio kuokoa mizigo ya majeruhi walolazwa katika Hospital ya Rufaa ya Mbeya.
                             ********************************************
KICHANGA cha Miezi 6 kimefariki dunia papo hapo na wengine zaidi ya 60 wamenusurika kufa  katika ajali mbaya iliyohusisha Basi kampuni ya Sabena baada ya kuacha njia na kutumbukia katika Mtaro  pembezoni mwa Barabara eneo la Maji mazuri Kawetere nje kidogo ya Jiji la Mbeya.
  Kwa mujibu wa Wahanga wa ajali hiyo iliyotokea jana wamesema imetokana na mwendokasi ambapo Dereva alishindwa kulimudu basi hilo lililokuwa likitokea Mbeya kuelekea Mwanza.
Wamesema ajali hiyo imetokea majira ya Saa moja asubuhi  ambapo katika ajali hiyo watu kadhaa walijeruhiwa na kukimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya huku wengine wakipatiwa huduma ya kwanza kisha kuendelea na safari baada ya kubadilishiwa gari.
Gari hilo lenye namba za usajili T 887 AYG liliharibika vibaya na kushindwa kuendelea na safari ndipo lilipoletwa basi lingine kampuni hiyo hiyo ya Sabena kwa ajili ya kuendelea na Safari.
Kondakta wa Basi hilo Seif Salum(34) amesema chanzo cha ajali hiyo ni ubovu wa gari uliosababisha kupasuka kwa mpira wa Breki hivyo gari kushindwa kusimama na kutumbukia mtaroni.
Amemtaja Dereva wa basi hilo kuwa ni Suddy Hussein ambaye inasadikika kuwa alikimbia baada ya ajali hiyo ingawa kondakta alitoa taarifa kuwa kafuata matibabu Hospitalini.
 Picha na Mbeya yetu.

Tevez atangulia Juve, Kolarov njiani kumfuata

Aleksandar Kolarov and Carlos Tevez - Manchester City v Aston Villa - Capital One Cup Third Round
Kolarov, Tevez wakiwa na Balotelli walipokuwa wote Manchester City
MSHAMBULIAJI nyota wa timu ya Manchester City, Carlos Tevez ametua kwa mabingwa wa Italia, Juventus, huku 'kibibi' hicho cha Turin kikiamini kuwa kitafanikiwa kumchukua Aleksandae Kolarov ili kuichezea klabu yao.
Tevez aliyekuwa akiwindwa na klabu mbalimbali ikiwemo Ac Milan, ametua Juventus na kukabidhiwa jezi namba 10 baada ya kufaulu vipimo vya afya.
Juventus inaamini baada ya kumnyakua Muargentina huyo, mchezaji mwingine atakayetua Turin ni Mserbia Kolarov, 27 aliyesajiliwa na City kwa thamani ya pauni Mil 16 miaka mitatu iliyopita akitokea Lazio ya Italia.
City haijaweka wazi mipango ya kumuachia beki huyo, lakini hiyo tgayari kocha mpya wa timu hiyo  amefua wazi kutokuwa na mpamngo na beki huyo na kutoa nafasi ya kumfuata Tevez Juventus kirahisi.Tevez alinukuliwa akifurahia kutua kwake Juve ambayo msimu huu iling'olewa kwenye hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich.
Mshambuliaji huyo atakuwa mchezaji wa kwanza kuvaa jezi namba 10 tangu ilivyovuliwa na Alessandro del Piero.

Kisura wa Miss Utalii ang'ara Kosovo, Bodi yampongeza


Mrembo Mwanakombo Kessy akipata kiburudisho baada ya kazi nzuri nchini Kosovo
Mwanakombo Kessy akiwa na warembo wenzake baada ya shindano la Miss Freedom of the World na kutwaa taji la Best Model


MSHINDI namba tano wa shindano la Miss Utalii Tanzania, Mwanakombo Kessy amefanikiwa kunyakua tuzo ya 'Mwanamitindo Bora' katika mashindano ya Miss Freedom of the World 2013 lililofanyika mwishoni mwa wiki nchini Kosovo na Bodi ya Miss Utalii Tanzania imepongeza.
Mrembo huyo alishinda taji hilo Juni 24  na kuwa taji la sita la kimataifa kwa Tanzania kunyakua kupitia shindano la Miss Utalii.
Kwa ushindi huo kisura huyo amevuna mkataba mnono wenye thamani ya Sh Mil 64 na kampuni ya kimataifa ya Johns Jonson ya Massimo Buttiglieriom.
Kutokana na mafanikio hayo Bodi ya Miss Utalii imemmiminia pongezi kisura huyo na kufurahia kazi kubwa aliyoenda kuifanya Kosovo na kudai ni muendelezo wa rekodi nzuri la shindano lao anga za kimataifa.
Rais wa Miss Utalii Tanzania, Gideon Chipungahelo 'Chipps', alisema wamefurahi mno kwa tuzo aliyopewa Mwanakombo na wanampongeza kwa kazi kubwa aliyofanya ya kuipeperusha vyema bendera ya tanzania na kuonyesha shindano lao sivyo linavyochukuliwa hapa nchini.
"Ushindi huu ni kwa Taifa zima la Tanzania, watanzania wote hata wale wabaya wetu, wapika majungu wetu, wazushi wetu na wazee wa fitina. Tunatambua ushindi huu wa taji la 6 la kidunia, na mafanikio yetu kila mwaka katika mashindano ya Dunia, " alisema Chipps.
Chipps alisema wanampongeza mrembo wao na wanamsubiri kwa hamu atakaporejea nchini kwa ajili ya kumpa mapongezi ya heshima kwa alichokifanya ikiwa ni siku chache baada ya kushika nafasi ya tano katika shindano lililofanyika jijini Tanga.

Rais Obama apeperusha Tamasha ya wasanii Mkuranga

Rais wa Marekani, Barrack Obama anayetarajiwa kutua nchini wiki ijayo
 TAMASHA la Mastaa Chipukizi lililokuwa lifanyike Jumamosi Juni 29 kijiji cha wasanii Mwanzega Mkuranga limeahirishwa ili kutoa nafasi kwa  wasanii na viongozi mbalimbali kushiriki kikamilifu katika maandalizi na mapokezi ya  Rais wa Marekani, Baraka Obama.
 
Mwenyekiti wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA), Caaasim Taalib alisema jana kuwa wanachama wengi waliokuwa washiriki tamasha hilo watakuwa katika maandalizi ya ujio wa Rais Obama hivyo litafanyika mwezi Agosti baada ya sikukuu ya Idd el Fitri.
 
Taalib alisema anawaomba radhi wananchi wa Mkuranga, viongozi mbalimbali na wasanii washiriki wa tamasha hilo waliokuwa wamejiandaa kuonesha vipaji vyao katika tamasha hilo .
 
‘Tumeamua kutoa nafasi hii kwa wanachama wa SHIWATA ili washiriki kikamilifu kudumisha amani katika wakati huu ambao tunatembelewa na Rais Obama na wasanii washiriki kikamilifu, tunaomba tutoe taarifa katika vyombo vya dola mara tunapoona kuna unjifu wa amani’ alisema Taalib.
 
 
Mwenyekiti huyo alisema mgeni rasmi aliyekuwa ameandaliwa, Naibu Waziri wa Kilimo, Adam Malima amepelekewa ujumbe huo pamoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida na wabunge wa Dar es Salaam nao wamearifiwa kuhusu kusogezwa mbele tamasha hilo .
 
Alisema sambamba na tamasha hilo, SHIWATA ilikuwa ikabidhi nyumba kwa mchezaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Jellah Mtagwa na wasanii wengine 14 ambao wamekamilisha michango ya ujenzi  wa nyumba zao katika kijiji chao cha Mwanzega Kimbili, Mkuranga.
 
Wengine watakaokabidhiwa nyumba zao ni msanii maarufu nchini, Lumole Matovola ‘Big’ wa Bongo movie ambaye ni wanachama wa SHIWATA wangine ni Mwandishi wa Habari, Josephine Moshi, Farida Ndimbo wa Jeshi la Magereza, Flora Kafwembe wa JKT Mgulani na Nyanza Kisadugwa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).  
 
 Mpaka sasa SHIWATA imejenga nyumba 24 kwa ajili ya wasanii katika eneo la hekari 300 na wanajiandaa kulima shamba la hekari 500 walizonazo ili kujikwamua kimaisha.