KLABU ya Chelsea imezidi kujiimarisha baada ya kukamilisha uhamisho wa Loic Remy kwa dau la Pauni Milioni 8 kutokaq QPR, huku Mjapan Shinji Kagawa wa Manchester United akirejea klabu yake ya zamani ya Borrusia Dortmund.
Remy
aliyekuwa anatakiwa pia na Arsenal, anakwenda kuziba nafasi ya Fernando
Torres aliyehamia AC Milan kwa mkopo wa muda mrefu.
Uhamisho
huu ni faraja kwa Remy ambaye sasa anakwenda kujiunga na klabu
inayocheza Ligi ya Mabingwa Ulaya. Kocha Mreno, Jose Mourinho alihitaji
mshambuliaji baada ya kumtoa kwa mkopo Torres.Katika kuelekea mwisho wa kufungwa kwa dirisha la usajili barani Ulaya, Shinji Kagawa ambaye hakuwa akipewa nafasi kubwa ndani ya Mashetani WEkundu amerejea Ujerumani kuichezea Dortmund.
Kiungo huyo amerejea Dortmund kwa dau la Pauni Milioni 6.3, miaka miwili tu tangu aondoke klabu hiyo ya Ujerumani.
Kagawa atasaini Mkataba wa miaka minne na Dortmund, ambayo ilimuuza Mjapani huyo United mwaka 2012 kwa Pauni Milioni 12.
![]() |
| Shinji Kagawa akikabidhiwa uzi wake mpya wa Dortmund baada ya kuondoka Manchester Utd |
![]() |
| Remy akisaini mkataba wa kujiunga na Chelsea |
![]() |
| Akionyesha uzi mpya wa klabu yake ya Chelsea |





ARSENAL imeendelea kugawa pointi bada ya kulazimishwa sare ya pili mfululizo katika Ligi Kuu ya Engaland dhidi ya timu ya Leicester City uwanja wa ugenini.
MSHAMBULIAJI Ramadel Falcao amekanusha taarifa kwamba anaitamani Real Madrid na kudai taarifa iliyoandikwa kwenye akaunti ya Twitter haikuandikwa na yeye ndiyo maana ilikuwa hewani kabla ya kufutwa.






MSHAMBULIAJI nyota wa
klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo, amemtabiria mafanikio mchezaji
mwenzake wa zamani Angel Di Maria katika klabu yake mpya ya Manchester
United. 




SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeliandikia Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kutaka kipengele cha kutaka kwanza nchi iandae Fainali za Afrika kwa Vijana ndiyo iwe na sifa ya kuandaa Fainali za Afrika (AFCON) kiondolewe.
TIMU za Mgambo Shooting na African Sports za Tanga zitapambana Jumapili (Agosti 31 mwaka huu) katika mechi ya majaribio ya matumizi ya tiketi za elektroniki itakayochezwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga kwa kiingilio cha sh. 1,000 tu.






