STRIKA
USILIKOSE
Friday, May 27, 2016
Kijana anusurika kufa kwa kujirusha kutoka mnara wa simu
Kijana Mmoja (picha) Jijini Mwanza amenusurika kifo baada ya
kujirusha kutoka katikati ya mnara wa simu.
Tukio hilo
limetokea hii leo na kuvuta watu wengi waliofika kumshuhudia kijana huo
ambae amepanda katika mnara huo tangu majira ya asubuhi na kukatalia
mnarani hadi majira ya saa sita mchana.
Mashuhuda wa tukio
hilo ambao pia ni marafiki wa karibu na kijana huyo, wamesema huenda
kijana huyo amefikia maamuzi hayo kutokana na ugumu wa maisha ambao
amekuwa akiulalamikia huku wengine wakisema ni kutokana na kuathiriwa na
matumizi ya dawa za kulevya ikiwemo gundi ambayo amekuwa akiyatumia.
Akizungumza kwa
niaba ya Kamanda wa jeshi la uokoaji na zima moto mkoani Mwanza, mmoja
wa maafisa wa uokoaji Mussa Kaboni, amsetoa rai kwa makampuni yenye
minara ya simu kuimarisha ulinzi katika minara hiyo ili kuondoa hatari
inayoweza kujitokeza kutoka kwa raia wasio wema.
Baadhi ya
mashuhuda wa tukio hilo walionekana kuchukizwa na kitendo cha kijana
huyo na kusikika wakifoka kwa hasira na makelele ya hali ya juu "rukaa,
ruka sasa, jirushe kama wewe ni mwanaume" hali ambayo ilikuwa
ikimuongezea morari kijana huyo na hivyo kujirusha kweli kutoka katikati
ya mnara huo.
Baada ya kijana
huyo kujirusha kutoka katikati ya mnara hadi chini, alipoteza fahamu na
kukimbizwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mwanza, Sekour Toure kwa
ajili ya huduma ya kwanza.
Credit:Mwanaharakati Mzalendo
Fomu za Uchaguzi Yanga zadoda Karume
| Manji (kati)n akitetea na Cannavaro na Chuji misimu kadhaa ya nyuma ya Ligi Kuu Bara |
Kamati ya Uchaguzi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ilitangaza leo Ijumaa ndio siku ya kufunguliwa kwa zoezi hilo, lakini mpaka jioni hii hakuna aliyejitokeza, huku kukiwa na taarifa kwamba Yanga wameugomea uchaguzi huo.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Alloyce Komba amedokeza kuwa, hakuna aliyejitokeza kuchukua fomu, lakini akiamini muda bado kwani wana siku 5 za zoezi hilo kufikia tamati.
Hata hivyo MICHARAZO imenasa taarifa kuwa, uchaguzi huo umesuswa na wana Yanga baada ya kutaka usifanyike kipindi hiki ambacho klabu yao itakuwa kwenye pilikapilika za kuelekea kwenye mechi zao za kimataifa ya Kombe la Shirikisho.
Yanga imepangwa Kundi A na timu za MO Bejaia ya Algeria, TP Mazembe ya DR Congo na Medeama ya Ghana na itaanza mechi zao siku mbili kabla ya kuvaana na Bejaia mjini Algiers, Algeria.
Uchaguzi wa Yanga umepangwa kufanyika Juni 15, lakini uongozi wa klabu hiyo ukitaka ufanyike tarehe moja na uchaguzi wao mdogo uliofanyika Julai 15, 2012 na kumuingiza Mwenyekiti na tajiri wao, Yusuf Manji.
Ronaldo kwa vijembe hajambo, awakejeli Barcelona kimtindo
HEBU msikieni CR7. Straika nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amesema kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya itakuwa na thamani kubwa zaidi kuliko mataji mawili yaliyonyakuliwa na wapinzani wao, Barcelona msimu huu.Ronaldo aliye na umri wa miaka 31 aliyekuwa majeruhi katika wiki za karibuni na kumfanya akose mechi ya nusu fainali ya mkondo wa kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Manchester City ni kama amewapiga kijembe wapinzani wao hao.
Hata hivyo juzi aliwaondoa hofu mashabiki wa timu hiyo akidai kuwa atakuwa fiti kwa asilimia 100 kwa ajili ya fainali hiyo dhidi ya Atletico Madrid.
Akihojiwa Ronaldo amesema kama wakishinda taji hillo la Ligi ya Mabingwa itakuwa ni thamani kubwa zaidi kwao kuliko mataji mawili ya Barcelona waliyoshinda hivi karibuni, kwani taji la michuano hiyo ya Ulaya liko katika ndoto za kila mchezaji. Klabu hasimu za jiji la Madrid, Real Madrid na Atletico Madrid zitakutana kesho Jumamosi katika fainali ya tatu zilizozikutanisha timu za Hispania na mechi ya fainali ya pili baina yao baada ya mwaka juzi 2014 kukutana na Real kushinda 4-1.
Kaka akumbukwa Brazil, aitwa kuziba pengo la Costa
![]() |
| Kaka akiwajibika kwa klabu yake ya Orlando |
Costa mwenye umri wa miaka 25, amepata majeraha ya misuli ambayo yatamfanya akose michuano hiyo maalumu ya kuadhimisha miaka 100 toka kuanzishwa kwake. Kaka mwenye umri wa miaka 34 ameichezea Brazil mechi 91 na kufunga mabao 29 katika kikosi hicho.
Costa alikuwa sehemu ya kikosi cha Bayern Munich ambacho kimeshinda taji la Bundesliga na Kombe la Ujerumani katika msimu wa mwisho wa Pep Guardiola na timu hiyo.
Brazil imepangwa kufungua pazia la Copa America kwa kucheza na Ecuador katika Uwanja wa Rose Bowl huko Pasadena, California Juni 4 mwaka huu, huku mechi zao nyingine mbili za kundi B zitakuwa dhidi ya Haiti na Peru.
Yanga yaibania Simba kucheza kimataifa
| Yanga |
| Simba |
Simba ilikuwa ikijipa matumaini ya kuwemo kwenye michuano ya Kombe la Kagame iliyopangwa kufanyika kuanzia mwezi ujao nchini, lakini michuano hiyo sasa haitafanyika tena Tanzania baada ya TFF kuchomoa kuiandaa.
Shirikisho hilo la Soka Tanzana, limetangaza kutoandaa michuano hiyo inayohusisha timu za nchi wanachama wa Shirikisho la Soka la Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), maarufu kama Kombe la Kagame kwa mwaka 2016 kama ilivyopendekezwa.
Sababu za TFF ya kutoandaa fainali hizo ni kwa kubanwa na ratiba ya michuano ya kitaifa na kimataifa.
Awali mkutano mkuu wa CECAFA, uliamua Zanzibar iwe mwenyeji wa michuano ya Kagame.
Baadaye kwa sababu zilizo nje ya uwezo wa ilionekana Zanzibar hawataweza kufanya.
Baada ya hapo TFF ilianza kuangalia uwezekano wa mashindano haya kwa kumshirikisha mabingwa wa 2015/16 ambao ni Yanga.
Kutokana na ratiba ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika (CAFCC) iliyotolewa na Shirikisho la Soka la Afrika (CAF), kipindi ch Juni hadi Agosti, 2016 Yanga watakuwa na kwenye michuano ya CAF hatua ya makundi hivyo ushiriki wao CECAFA utakuwa mgumu ilihali michuano ya CECAFA imepangwa kufanyika Juni na Julai, mwaka huu.
Watetezi wa taji hilo ni Azam na tayari Yanga ilikuwa ikisita kushiriki na kutoa nafasi kubwa kwa Simba kubeba jukumu, lakini kwa hali ilivyo watabidi wasubiri sana.
Dani Alves ainyima ubingwa Real Madrid Ulaya
![]() |
| Dani Alves |
| Atletico Madrid |
Atletico na Madrid zitavaana kesho, katika mechi ya kisasi kwea kocha Diego Simeone ambaye alifungwa kwenye fainali ya mwaka juzi na mabingwa hao wa kihistoria wa michuano hiyo ya Ulaya kwa mabao 4-1.
Atletico walio chini Diego Simeone ndio waliowang’oa mabingwa watetezi Barcelona katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo kabla ya kuitoa tena Bayern Munich kwenye hatua ya nusu fainali.
Madrid ndio timu pekee iliyopo mbele ya Atletico kwasasa ikiwa ni kama marudiano baada ya ile fainali ya mwaka 2014 ambapo Madrid waliibuka kidedea kwa kushinda mabao 4-1 katika muda wa nyongeza.
Hata hivyo, Alves ana mawazo tofauti katika fainali hiyo itakayofanyika katika Uwanja wa San Siro jijini Milan nchini Italia kwani anadhani Atletico wanastahili zaidi taji hilo kuliko Madrid. Alves amesema Atletico ni timu ambayo imepambana sana mpaka kufikia hapo walipo hivyo anadhani wanastahili taji hilo
Juventus kumng'oa Mascherano Nou Camp
MABINGWA wa Italia, Juventus imepanga kumng'oa Kiungo mahiri wa Barcelona, Javier Mascherano.Inadaiwa kuwa Muargentina huyo amekubali dili la kujiunga na mabingwa wa Serie A.
Duru za kimichezo zinasema kuwa, nyota huyo wa kimataifa wa Argentina amefanya mazungumzo na Juventus na anajiandaa kuhamia jijini Turin kiangazi hiki.
Mpaka sasa inadaiwa kuwa hakuna makubaliano yoyote kati ya Barcelona na Juventus na mabingwa hao wa Hispania wanahisiwa kutokuwa na mpango wowote wa kumuachia kiungo huyo mwenye umri wa miaka 31.
Mascherano alijiunga na Barcelona mwaka 2010 akitokea Liverpool na kufanikiwa kushinda mataji manne ya La Liga na mawili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa Camp Nou.
Ufaransa yaapa fainali za Euro 2016
UTAWALA wa nchi ya Ufaransa umesema kuwa inatarajia kuweka polisi zaidi ya 60,000 ili kulinda usalama katika michuano ya Euro 2016 itakayopanza Juni 10 wakiapa kuwa watafanya kila wawezalo kuhakikisha wanazuia shambulio lolote la kigaidi katika kipindi chote cha mashindano hayo.Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi hiyo, Bernard Cazeneuve ndiye aliyetoa kauli hiyo baada ya Uwanja wa Ufaransa uliopo jijini Paris ambao ndio utatumika kwa ajili ya mechi ya ufunguzi na fainali, kuleta rabsha Jumamosi iliyopita kabla ya fainali ya Kombe la Taifa.
Moshi mkubwa uliohisiwa kuwa bomu ulilipuka ndani ya uwanja na kusababisha mashabiki kuchanganyikiwa na kukimbia hovyo kuelekea milango ya kutoka nje ya uwanja.
Akihojiwa Waziri huyo amesema tukio la Jumamosi iliyopita halihusiani na maandalizi yao kwani waandaaji walikuwa tofauti.
Waziri huyo aliongeza kuwa katika michuano ya Euro 2016 inayotarajiwa usalama utakuwa ni kipaumbele chao cha kwanza ili kuhakikisha hakuna tukio lolote hatarishi ya kigaidi litakaloweza kutokea.
Jose Mourinho atambulishwa rasmi Man United
![]() |
| Jose Mourinho akitua rasmi Man United |
Mourinho, mwenye miaka 53 ametangazwa na klabuni na kuchapishwa picha akiwa na jezi za klabu yake mpya ambayo ilikuwa ikimsaka tangu alipotemwa Chelsea katikati ya msimu uliomalizika wa EPL.
Kocha huyo alisaini mkataba huo jana jioni baada ya mazungumzo ya siku tatu kabla ya kutambulishwa akiwa kavalia suti kali nyeusi jambo linaloashiria kuwa, Special One sasa ni mali ya Mashetani Wekundu na wapinzani wao wajipange kwa mikakati anayokuja nayo kocha huyo mjuzi.
Moja ya mikakati inayotajwa kuwa mikononi mwa Mourinho ni kumnyakua Willian anayekipiga Chelsea ambaye alinunuliwa na kocha huyo wakati akiinoa klabu hiyo ya The Blues.
Sunday, May 22, 2016
HIVI NDIVYO LIGI KUU BARA 2015-2016 ILIVYOISHA RASMI
| Mabingwa Yanga |
| Simba washindi wa tatu |
| Majimaji iliyoigomea Yanga mjini Songea |
Sports maarufu kama Wana Kimanumanu walilala mabao 2-0 mbele ya Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Manungu Complex, Turiani Morogoro, wakati Wagosi wa Kaya Coastal ikilala tena mabao 2-0 Mkwakwani Tanga mbele ya Prisons-Mbeya licha ya kwamba ilishashuka mapema katika ligi hiyo.
Mgambo JKT ilishindwa kukomaa kujiokoa kama misimu mitatu iliyopita ilivyopambana baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na Azam na kujikuta pointi zake kutotosha kuiokoa isirudi Ligi Daraja la Kwanza baada ya kucheza mfululizo tangu ilipopanda mwanzoni mwa miaka ya 2010.
Simba ikiwa Uwanja wa Taifa ilishindwa kuhimili vishindo vya JKT Ruvu na kulala mabao 2-1 ikiiacha Azam ikitwaa zawadi ya mshindi wa pili nyuma ya Yanga ikiwa msimu wa tano mfululizo kwa Wanalambalamba kutotoka kwenye Mbili Bora ya ligi hiyo tangu mwaka 2011-2012.
Mjini Songea Majimaji ikiwa Uwanja wake wa Majimaji, ililazimishwa sare ya mabao 2-2 na Mabingwa Yanga, huku ikishuhudiwa Ally Mustafa Barthez akifunga bao lake la kwanza katika Ligi Kuu, huku Paul Nonga akiifungia Yanga bao lake la kwanza katika Ligi Kuu tangu aliposajiliwa katika dirisha dogo mwishoni mwa mwaka jana.
Toto Africans imenusurika kushuka daraja licha ya kufungwa bao 1-0 na Stand United Uwanja wa CCM Kirumba, kama ambavyo Kagera Sugar ilivyoponea kwa Wana Shinyanga wengine Mwadui FC waliowazabua mabao 2-0.
Mbeya City ikiwa nyumbani ilishindwa kulipa kisasi cha kufungwa mabao 4-1 na Ndanda katika mchezo wao wa kwanza mjini Mtwara kwa kutoka suluhu kwenye Uwanja wa wa Sokoine, Mbeya.
Kwa namna msimamo ulivyo, Yanga iliyotwaa ubingwa mbali na kunyakua Kombe na Medali, pia imevuta mkwanja upatao Sh. 81,345,723/= kama washindi wa kwanza, wakati Azam ikizoa Sh. 40,672,861/= za ushindi wa pili.
Simba yenyewe imevuta donge la Sh. 29,052,044/= kwa kushika nafasi ya tatu wakati Prisons iliyokuwa ya nne ikiipiku Mtibwa Sugar imeweka kibindoni Sh. 23,241,635/=
Kadhalika kumalizika kwa ligi hiyo kumempa nafasi Amissi Tambwe wa Yanga kuibuka kinara wa mabao msimu huu akifunga jumla ya 21 na kujihakikishia zawadi ya Sh. 5,742,940/= mbele ya Hamis Kiiza wa Simba aliyekuwa akiongoza kwa muda mrefu kabla ya kupoteza makali yake.
Matokeo kamili na msimamo wa mwisho wa Ligi hiyo ni kama ifuatavyo;
Msimamo wa Ligi Kuu Bara:
P W
D L F
A Pts
1. Yanga
30 22 7 1 70 20 73
2. Azam
30 18 10 2
47 24 64
3. Simba
30 19 5 6 45 17
62
4. Prisons
30 13 12
5 29 22 51
5. Mtibwa
30 14 8
8 33 21 50
6. Mwadui FC 30 11 8 11 29 29 41
7. Stand Utd
30 12 4 14 28 29 40
8. Mbeya City
30 9 8 13 32 34 35
9. Ndanda
30
7 14 9 28 31 35
10.Majimaji 30
9 8 13 22 40 35
11.JKT Ruvu
30 8 8
14 31 43 32
12.Toto Africans
30 7 9 14
26 40 30
13.Kagera Sugar 30 8 7
15 23 34 31
14.Mgambo
30 6 10 14
24 36 28
15.African Sports 30
7 5 18 13 34 26
16.Coastal Union 30 5
7 18 15 41 22
Wafungaji:
21-Amissi Tambwe (Yanga)
19-Hamis Kiiza (Simba)
17-Donald Ngoma (Yanga)16-Jeremiah Juma (Prisons)
15-Elias Maguli (Stand)
12- Kipre Tchetche (Azam)
10-John Bocco (Azam)
Atupele Green (Ndanda)
9- Ibrahim Ajib (Simba)
Shiva Kichuya (Mtibwa)
Simon Msuva (Yanga)
8- Shomary Kapombe (Azam)
Fully Maganga (Mgambo)
7- Mbaraka Yusuf (Kagera)
Mussa Kiumbu (JKT Ruvu)
Waziri Junior (Toto)
Saady Kipanga (JKT Ruvu)
6- Danny Mrwanda (Majimaji)
AbdulRahman Mussa (JKT Ruvu)
6- Danny Mrwanda (Majimaji)
AbdulRahman Mussa (JKT Ruvu)
5-Said Bahanuzi (Mtibwa)
Samuel Kamuntu (JKT Ruvu)
Miraji Athuman (Toto)
Jerry Tegete (Mwadui)
Thabani Kamusoko (Yanga)
Mohammed Mkopi (Prisons)
Raphael Alpha (Mbeya)
Didier Kavumbagu (Azam)
Paul Nonga (Yanga)
4- Aziz Gillah (Mgambo)
Juma Abdul (Yanga)
Edward Christopher (Toto)
3- Michael Aidan (JKT Ruvu)
Haruna Moshi (Mbeya)
Pastory Athanas (Stand)
Adam Miraj (Coastal)
Kiggy Makassy (Ndanda)
Omar Mponda (Ndanda)
Peter Mapunda (Majimaji)
Danny Lyanga ( Simba)
Babu Ally (Kagera)
Mzamiru Yasin (Mtibwa)
Bryson Raphael (Ndanda)
Joseph Mahundi (Mbeya)
Deus Kaseke (Yanga)
Mudathir Yahya (Azam)
Kelvin Sabato (Mwadui)
Samuel Kamuntu (JKT Ruvu)
Miraji Athuman (Toto)
Jerry Tegete (Mwadui)
Thabani Kamusoko (Yanga)
Mohammed Mkopi (Prisons)
Raphael Alpha (Mbeya)
Didier Kavumbagu (Azam)
Paul Nonga (Yanga)
4- Aziz Gillah (Mgambo)
Juma Abdul (Yanga)
Edward Christopher (Toto)
3- Michael Aidan (JKT Ruvu)
Haruna Moshi (Mbeya)
Pastory Athanas (Stand)
Adam Miraj (Coastal)
Kiggy Makassy (Ndanda)
Omar Mponda (Ndanda)
Peter Mapunda (Majimaji)
Danny Lyanga ( Simba)
Babu Ally (Kagera)
Mzamiru Yasin (Mtibwa)
Bryson Raphael (Ndanda)
Joseph Mahundi (Mbeya)
Deus Kaseke (Yanga)
Mudathir Yahya (Azam)
Kelvin Sabato (Mwadui)
Alex Kondo (Ndanda)
2-Malimi Busungu (Yanga)
Ally Myovela (Prisons)
Mohamed Ibrahim (Mtibwa)
Ally Shomary (Mtibwa)
Fabian Gwanse (Mwadui)
Jabir Aziz (Mwadui)
Nassor Kapama (Coastal)
Thabit Khamis (JKT Ruvu)
Frank Domayo (Azam)
Abslim Chidiebele (Coastal)
Hamad Mbumba (Sports)
Ditram Nchimbi (Mbeya City)
Kassim Selembe (Stand)
Nizar Khalfan (Mwadui)
Juma Mahadhi (Coastal)
Paul Ngway (Kagera)
Farid Mussa (Azam)
Japhet Mkala (Toto)
Chande Magoya (Mgambo)
Ally Ramadhani (Sports)
Salum Kabunda (Mwadui)
Kelvin Yondani (Yanga)
Salim Mbonde (Mtibwa)
Abdallah Juma (Mbeya)
Stamili Mbonde (Majimaji)
Omar Issa (Sports)
Jumanne Alfadhil (Prisons)
Hassan Materema (Sports)
Frank William (Prisons)
Bolly Ajali Shaibu (Mgambo)
Jaffar Ramadhani (Toto)
2-Malimi Busungu (Yanga)
Ally Myovela (Prisons)
Mohamed Ibrahim (Mtibwa)
Ally Shomary (Mtibwa)
Fabian Gwanse (Mwadui)
Jabir Aziz (Mwadui)
Nassor Kapama (Coastal)
Thabit Khamis (JKT Ruvu)
Frank Domayo (Azam)
Abslim Chidiebele (Coastal)
Hamad Mbumba (Sports)
Ditram Nchimbi (Mbeya City)
Kassim Selembe (Stand)
Nizar Khalfan (Mwadui)
Juma Mahadhi (Coastal)
Paul Ngway (Kagera)
Farid Mussa (Azam)
Japhet Mkala (Toto)
Chande Magoya (Mgambo)
Ally Ramadhani (Sports)
Salum Kabunda (Mwadui)
Kelvin Yondani (Yanga)
Salim Mbonde (Mtibwa)
Abdallah Juma (Mbeya)
Stamili Mbonde (Majimaji)
Omar Issa (Sports)
Jumanne Alfadhil (Prisons)
Hassan Materema (Sports)
Frank William (Prisons)
Bolly Ajali Shaibu (Mgambo)
Jaffar Ramadhani (Toto)
Tanga ndio basi tena Ligi Kuu msimu ujao
| Mgambo JKT |
| Africans Sports |
| Coastal Union |
Sports imelala mabao 2-0 mbele ya Mtibwa Sugar, wakati Mgambo imeambulia sare ya bao 1-1 ambayo imeshindwa kuwabeba mbele ya Azam, na Coastal iliyoshuka mapema ikikubali tena kipigo cha bao 1-0 mbele ya Prisons uwanja wa Mkwakwani Tanga.
Matokeo ya mwisho ya mechi za kufungia msimu tutawaletea hivi punde, lakini ni kwamba Simba imelala mabao 2-1 mbele ya JKT Ruvu na kushindwa kunyakua nafasi ya pili iliyoenda kwa Azam kwa msimu wa tano mfululizo sasa.
Mgambo yachomoa, Mtibwa yazidi kuzamisha jahazi la Sports
| Mgambo JKT inapambana kuepukam kushuka daraja |
Mgosi afunga bao la kwanza la VPL, Stand ng'aring'ari
JIJINI Mwanza, Toto imetanguliwa bao 1-0 na Stand, huku Taifa Hassan Mussa Mgosi anafunga bao lake la kwanza katika Ligi Kuu msimu huu kwa kuipatia Simba bao la kufutia machozi Game ipo dakika ya 74.
Simba bado, Azam yapata bao, Kagera safii
| Azam inayoongoza dhidi ya Mgambo |
Van Gaal aaga Man Utd kumpisha Mourinho
![]() |
| Picha haihusiani na taarifa hii. KOcha Louis Van Gaal |
LVG ametoa kauli hiyo mchana huu akizungumza katika mkutano wake na wanahabari hotelini kwa kusema kuwa imetosha, ikiwa ni kama kuweka wazi kuwa anaondoka OT.
Kocha huyo amekuwa na wakati mgumu katika klabu hiyo, mashabiki wakitaka asepe zake kwa kushindwa kuirejesha klabu yao katika heshima kama ilivyokuwa chini ya Sir Alex Ferguson aliyestaafu miaka michache iliyopita.
Jose Mourinho amekuwa akitajwa kumrithi Mholanzi huyo, huku taarifa za jana zilikuwa zikidai kuwa, huenda LVG akawa Mkurugenzi wa Ufundi wa Man United, lakini kwa kaul;i aliyotoa mchana huu ni wazi, ndio basi tena.
Simba tayari ishagongwa 2-0 na maafande
MPAKA muda huu wakati mechi za mwisho za Ligi Kuu Bara zikiendelea kuchezwa, Simba tayari imeshafungwa mabao 2-0 na JKT Ruvu katika pambano lao linalochezwa Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam. Mabao ya maafande wanapigana kuepuka kushuka daraja yamefungwa na Abdulrahaman Mussa na Saady Kipanga likiwa bao lake la saba msimu huu.
Yanga iliyopo Songea, kuumana na Majimaji wapo nguvu sawa na wenyeji wao wa kufungana bao 1-1, wakati Mtibwa ikiwa Manungu, Turiani inaongoza bao 1-0.
Viwanja vingine bado ni vigumu wakati mechi zikiwa mapumzikoni kwa sasa. MICHARAZO itakufahamisha kila linaloendelea katika mechi hizo za mwisho wa msimu wa 2015-2016.
Yanga iliyopo Songea, kuumana na Majimaji wapo nguvu sawa na wenyeji wao wa kufungana bao 1-1, wakati Mtibwa ikiwa Manungu, Turiani inaongoza bao 1-0.
Viwanja vingine bado ni vigumu wakati mechi zikiwa mapumzikoni kwa sasa. MICHARAZO itakufahamisha kila linaloendelea katika mechi hizo za mwisho wa msimu wa 2015-2016.
Wazee Yanga wamng'ang'ania Manji Jangwani
| Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji |
Manjia amekaa madarakani kwa miaka miwili nje ya utaratibu wa Katiba ya klabu hiyo ya Jangwani.
Akizungumza na Wanahabari leo Jumapili jijini Dar es Salaam, akiweka bayana msimamo wa Wazee wa Yanga akiwa kwa pamoja na Mwenyeviti wa matawi wa mkoa wa Dar es salaam, Katibu wa Baraza hilo Ibrahim Akilimali, alisema kuwa, wanamuunga mkono Manji kwa asilimia zote kwani ameweza kuisaidia timu hiyo toka akiwa mdhamini mpaka kufikia kuwa Mwenyekiti wa klabu hiyo.
"Kwa upande wa Baraza la Wazee tunamuunga mkono Manji kwani toka Yanga imekuwa chini yake kumekuwa na mafanikio makubwa sana ikiwemo kuweza kuingia hatua ya makundi Kombe la Shirikisho na kama kuna masuala mengine ikiwemo ya uwanja uongozi mpya utakapoingia tutakaa nao kuweza kujua tunafikia wapi malengo yetu ya kujenga kwani tumeshafikia kwenye hatua bado kibali tu," alisema Akilimali.
Akilimali alisema, watu wasitake kuangalia suala la Uwanja kwa Manji tu, bali wakumbuke kuwa kuna viongozi wengine wamepita na hawajajenga cha msingi ni kuangalia wapi tunaelekea na nini kinachotakiwa kufanyika kwa maendeleo ya klabu yao.
Wazee hao walisema kwa pamoja kuwa mbali na hilo pia wanawapongeza wachezaji na benchi la ufundi kwa hatua nzuri waliyofikia ya kuchukua ubingwa kwa mara ya 26 pamoja na kuingia kwenye hatua ya makundi ya Kombe la Shirishiko ikiwa ni moja mafanikio wanayojivunia chini ya Manji.
Juma Abdul noma, ambwaga Ngoma tuzo ya VPL
![]() |
| Juma Abdul |
![]() |
| Juma Abdul (12) akiwajibika kimataifa |
Beki huyo anayeichezea pia Taifa Stars ameteuliwa kuwa Mchezaji Bora wa Ligi Kuu Bara kwa mwezi Aprili akimbwaga straika wake,Ngoma na kiungo wa JKT Ruvu, Hassan Dilunga.
Katika rekodi za Bodi ya Ligi Tanzania Bara (TPLB) iliyoketi Jumamosi iliyopita, imeonesha kwamba Abdul alicheza mechi zote tano za Ligi Kuu kwa mwezi Aprili ambapo pia aliifungia timu yake bao katika harakati za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu msimu wa 2015/16.
Rekodi hizo pia zinaonyesha kwamba beki huyo hakuonyeshwa kadi hata moja katika michezo hiyo mitano sambamba na kutoa mchango mkubwa katika michezo aliyoshiriki kwa mwezi Aprili, 2016.
Beki huyo atazawadiwa fedha Sh. Milioni 1= na wadhamini wa Ligi hiyo, Kampuni ya mtandao wa simu za mkononi ya Vodacom.
Uwezo aliouonyesha Abdul ulisababisha Kocha wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa ‘Master’ kumjumuisha katika kikosi chake kwa ajili ya mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Harambee Stars ya Kenya kadhalika Mafarao wa Misri katika mechi ya kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika utakaofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Juni 4, mwaka huu.
Wachezaji bora wa miezi minne iliyopita ni kiungo Thabani Kamusoko wa Young Africans (Desemba 2015), beki Shomari Kapombe wa Azam (Januari 2016), Mshambuliaji Mohammed Mkopi wa Prisons (Februari 2016) na Shiza Kichuya wa Mtibwa Sugar (Machi 2016).
Subscribe to:
Posts (Atom)





