STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, August 21, 2014

Snake Boy Jr, Nassib kurudiana Dar

Bondia Mohamed Matumla kushoto na Nassibu Ramadhani wakitunishiana misuli 
Na Mwandishi Wetu
 MABONDIA Nassibu Ramadhani pamoja na Mohamed Matumla 'Snake Boy Jr' wameingia makubaliano ya kuzipiga kwa mara ya pili siku ya septemba 27 katika ukumbi wa Friends Corner, Manzese Dar es salaam.

Akizungumzia mpambano huo mratibu wake Yassin Abdallah 'Ustadhi' amesema mabondia hao wamekubaliana na kusaini mkataba wa kuzipiga siku hiyo, ambapo ni marudiano baina yao kwani walishakutana mapema mwaka huu na Matumla kumshinda mpinzani wake kwa pointi.

Ustaadh alisema siku ya pambano hilo ambalo ameshindwa kutabiri kama ni Nassib atalipa kisasi au Matumla kuendeleza ubabe kutakuwa na michezo kadhaa ya utangulizi.

Baadhi ya michezo hiyo ni pamoja na lile pambano la

  Issa Omardhidi ya Juma Fundi katika uzani wa kg 53 raundi nane, Sadiq Momba vs Tasha Mjuaji kg 59 raundi nane, huku Juma Mustafa atamkabili Bakari Dunda kg 61 raundi sita.

Pia siku hiyo wanadada Lulu  Kayage atapambana na Fatma Yazidu kg 51 raundi nne.

siku hiyo pia kutakuwa na huuzwaji wa  DVD ambazo zinatoa mwanga kwa mchezaji kujua mchezo na kufahamu zaidi mbinu mpya zitumiwazo na mataifa mbali mbali Duniani.

Wakiwemo mabondia bingwa wa dunia kama Manny Paquaio,Floyd Maywether,Amir Khani, Mohamed Ali ,Mike Tayson na wengine wengi wanaotamba na waliotamba katika mchezo huo wa masumbwi Duniani
kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' ametoa wito kwa makampuni mbalimbali kujitokeza kutoa sapoti ya mchezo wa masumbwi kwani ndio mchezo pekee unaoweza kututoa kimasomaso watanzania tukafurahi

Azam yakwama Sudan, yang'oka Kagame kwa matuta

http://shaffihdauda.com/wp-content/uploads/2014/08/AZAM-FC-KIKOSI-1-546x291.jpg
WAWAKILISHI pekee wa Tanzania katika michuano ya Klabu Bingwa AfrikaMashariki na Kati, Kombe la Kagame,  Azam FC ya Chamanzi jijini Dar es Salaam imetupwa nje ya michuano hiyo mikubwa kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati baada ya kucharazwa mikwaju 4-3 dhidi ya El Marreikh ya Sudani katika mchezo wa pili wa robo fainali.Wachezaji ambao walielezwa awali kuwa wanasumbuliwa na vyama za paja lakini wakashuka katika dimba la Nyamirambo mjini Kigali Rwanda ndio walioigharimu Azam FC licha ya mlinda mlango  Mwadin Ally kufanya kazi nzuri ya kupangua penati ya wapinzani wao. 

Wachezaji walioipa tiketi ya kurejea nyumbani Azam FC kujiandaa na mchezo wao wa Ngao ya Hisani dhidi ya Yanga SC ni beki Shomary Kapombe na mshambuliajiLionel Saint- Preux kutoka Haiti.
Aidha kocha wa mabingwa hao wapya wa soka la Tanzania, Mcameroon JosephMarious Omog ameonekana amekuwa akiandaa Azam FC kitaalamu mnokuelekea mchezo huo, ambapo mbali na mambo mengine aliwaelekeza mifumona aina tofauti ya uchezajiikiwa ni pamoja na kutumia mipira mirefu na mifupi.
Omong aliwaandaa wachezaji wake pia kwa kupiga penaltilakini hakuna kilichofua dafu kutokana na upigaji wa kimakosa uliofanywa na Kapombe aliyepaisha penati yake juu na gonga mwamba na Preux aliyepiga mpira mwepesi na kumwezesha mlinda mlango wa Merreikh kuificha bila shaka.

Simba, Yanga kuonyeshana kazi Okt.12

Kikosi cha wakali wa Msimbazi
Vijana wa Jangwani
WATANI wa jadi Simba na Yanga watakutana mapema katika raundi ya nne ya ligi Oktoba 12 mwaka huu, kwa mujibu wa ratiba ya msimu mpya wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara 2014-15 iliyotolewa jana na shirikisho la soka nchini (TFF).
Miamba hao wa soka nchini watarudiana katika raundi ya 17 ya ligi hiyo Februari 8, 2015, ratiba hiyo imeonyesha.
Mabingwa Azam FC wataanza kampeni ya kutetea taji lao la kwanza kwa kuwakaribisha Polisi Morogoro kwenye Uwanja wa Azam Complex katika siku ya kwanza ya ufunguzi wa msimu Septemba 20, siku ambayo viwanja sita 'vitawaka moto'.
Yanga waliomaliza katika nafasi ya pili msimu uliopita wataanza msimu mpya chini ya kocha mpya Mbrazil Marcio Maximo kwa kucheza ugenini dhidi ya timu inayozinyima usingizi timu kubwa ya Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Jamhuri wakati Mbeya City waliomaliza katika nafasi ya tatu watawakaribisha JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya. Simba waliomaliza wa nne msimu uliopita wataingia katika mtihani wa kwanza chini ya kocha mpya Mzambia Patrick Phiri kwa kuwakaribisha Coastal Union kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katika siku hiyo ya ufunguzi wa msimu.
Mechi nyingine za siku ya ufunguzi zitakuwa ni wageni wa ligi hiyo Stand United watakaowakaribisha wageni wenzao Ndanda FC kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga huku Mgambo JKT ikiwa mwenyeji wa Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga wakati Ruvu Shooting itawakaribisha Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Mabatini, mkoani Pwani.
Yanga watakuwa na mechi mbili ngumu zilizofuatana katika raundi ya nane na ya tisa ya ligi pale watakapowakabili mabingwa Azam Novemba 9 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa na kisha kusafiri hadi ugenini Mbeya kuwavaa Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine siku sita baadaye.
Simba watawakaribisha Mbeya City katika raundi ya 10 ya ligi kwenye Uwanja wa Taifa Desemba 20 mwaka huu kabla ya kuwavaa Azam katika raundi ya 12 siku ya Mwaka Mpya Januari 1, 2015 kwenye Uwanja wa Taifa. Ligi hiyo itafikia tamati Aprili 18, 2015.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura, ratiba hiyo imezingatia michuano ya Chalenji itakayochezwa Novemba, usajili wa dirisha dogo Nov 15- Des 15, ushiriki wa klabu za Azam na Yanga kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa (CL) na Kombe la Shirikisho (CC).
Wambura alisema mechi za ligi hiyo zitachezwa wikiendi ili kuongeza msisimko/kuwapa fursa washabiki wengi zaidi kuhudhuria na kwamba katikati ya wiki imeachwa wazi kwa ajili ya mechi za Kombe la FA (Federation Cup).
"Vilevile kutakuwa na mechi Boxing Day na siku ya Mwaka Mpya," alisema Wambura.

Omar Katanga amfuata Kutenge EFM

Aliyekuwa mtangazaji wa Redio One katika kipindi cha “Spot Leo” Omary Katanga (pichani kushoto) naye pia ameamua kufuata nyayo za pacha wake Maulid wa Kitenge aliyejiunga na  kituo cha redio (93.7) E FM  mapema wiki hii.
Katanga, aliyeweka wazi na kuripoti katika kituo hicho, ameamua kumfuata pacha wake Maulid Kitenge, ikiwa ni siku ya tatu tu tangu Kitenge alipojitangaza kwenye ukurasa wake wa Facebook na mitandao mingine kuwa ameamua kujiuzulu kazi na saa chache kutangazwa kujiunga na kituo hicho.
Watangazaji haowaliokuwa wakipiga kazi pamoja kwenye kipindi cha michezo katika kituo cha Redio One, wanatarajiwa kuanza kusikika hewani E FM 93.7 kuanzia kesho katika kipindi cha michezo cha E Sports, ambacho kitakuwa kikiruka kila siku saa 7:00 – 7:30 jioni.
Watangazaji hao wanajiunga na watangazaji wengine maarufu kama Dennis Ssebo, Dickson Ponnela (Dizzo 1), DJ Majay, na Kanky.

Serikali kujenga kiwanda cha kuzalisha viua mbu

Frank Mvungi-Maelezo
Serikali kutumia Euro Milioni 16 katika ujenzi wa Kiwanda cha kuzalisha viuadudu vinavyoua viluwiluwi vya mbu wanaoambukiza malaria ulioko chini ya shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) unaotarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu.
Hayo yamesemwa na Meneja Uhusiano wa Shirika hilo Bw. Abel Ngapemba wakati wa mkutano nawaandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
“Hivi sasa majengo yote yamekwisha kamilika katika eneo la Maili moja Kibaha Mkoani Pwani na mitambo yote imeshawasili na wataalamu wanaifunga ambapo kabla ya mwisho wa mwaka   uzalishaji  wa majaribio utaanza” Alisema Ngapemba.
Akifafanua zaidi Ngapemba alisema kiwanda hicho kitasaidia kuzalisha ajira  za moja kwa moja zipatazo 172 kwa watanzania.

Pia Ngapemba alibainisha kuwa kiwanda hicho kitakuwa na uwezo wa kuzalisha lita milioni sita za viadudu kwa mwaka ambapo asilimia 80 ya dawa hizo zitatumika nchini na asilimia 20 zitauzwa nchi za nje ambazo tayari zimeonyesha nia ya kuzitaka dawa hizo.
Viadudu hivyo vinatengenezwa kutokana na vimelea ambao wanakuzwa kwa kutumia viinilishe mbalimbali na kunyinyiziwa katika maeneo yenye mazalia ya mbu ambapo viluwiluwi wa mbu wanapovila wanakufa
Kulingana na ripoti ya upembuzi yakinifu wa mradi huu uliofanywa na NDC kwa kushirikiana na kampuni ya Labiofam ya Cuba mwaka 2010, mbali na malaria kusababisha vifo vya Watanzania wapatao 80,000 kwa mwaka,ambapo watu milioni 18 huugua ugonjwa huo kila mwaka ambapo Serikali imekuwa ikitumia kiasi cha dola za marekani zipatazo milioni 240 kwa mwaka katika kupambana na ugonjwa huu.
Ujenzi wa Kiwanda hicho ulianza miaka miwili iliyopita na kuwekwa jiwe la msingi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.Jakaya Mrisho Kikwete October mwaka 2013 lengo likiwa kupambana na hatimaye kutokomeza mbu wanaoeneza malaria na magonjwa mengine yaenezwayo na mbu.

Taarifa za wabunge, wagombea watarajiwa Uchaguzi Mkuu kisasa zaidi

Uchaguzi Mkuu wa Wabunge na Rais unataraji kufanyika hapo mwakani, Wabunge na wanaotaka kuwania Ubunge katika majimbo mbalimbali nchini hata urais mnakaribishwa kuandaa TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA ILANI YA VYAMA VYENU. Kitabu kama hicho kitakuwezesha wewe Mgombea kuto tumia nguvu kuubwa ya kujinadi badala yake utavigawa kwa wananchi mbalimbali jimboni kwako nawe kuelewa nini umewafanyia katika kipindi ambacho ulikuwa madarakani. 

Pia wagombea wapya pia wanaweza andaa vitabu kama hivi kuonesha yale ambayo wameshiriki kuyafanya na wanataraji kuyafanya chini ya ilani za vyama vyao husika. 

Mawasiliano zaidi kwa wenye uhitaji: Mroki Mroki (pichani juu) 
+255 717 002303/0755 373999/0788207274 
au barua pepe: mrokim@gmail.com

Wednesday, August 20, 2014

Uhondo Tamasha la Home Gym waongezeka maradufu

UHONDO zaidi umezidi kuongezwa kwenye maandalizi ya Tamasha la Miaka 16 ya Kituo cha Mazoezi cha Home Gym baada ya waratibu wake kuongeza vikundi vya Ngoma Asilia.
Vikundi mbalimbali vya ngoma asilia toka Mbagala jijini Dar es Salaam na burudani ya muziki wa kizazi kipya vinatarajiwa kutumbuiza kwenye tamasha hilo litakalofanyika Sept. 6.
Tamasha hilo litafanyika kwenye uwanja wa Mwenge likijumuisha michezo mbalimbali ikiwamo ya soka kwa timu za maveterani, Jogging na watunisha misuli.
Akizungumza na Blogu hii, mratibu wa tamasha hilo, Andrew Mangomango alisema vikundi hivyo vya ngoma asilia vinatokea Mbagala na vitatumbuiza kabla ya wakati wa michezo ya tamasha lao la kuadhimisha miaka 16 ya Home Gym.
Mangomango alisema mpaka sasa wamefanikiwa kusajili klabu 12 za maveterani, klabu zaidi ya 20 za Jogging na wanamichezo mbalimbali wa kutunisha misuli, kunyanyua vitu vizito, mieleka na mabondia kwa ajili ya shoo la tamasha hilo.
Alisema kuwa tayari wadhamini mbalimbali wameanza kujitokeza kuwapiga tafu ikiwamo kampuni ya General Shami Investment Co. Ltd na wengine.
Mangomango alisema mbali na burudani na muziki na shoo za wanamichezo pia, siku hiyo wanamichezo mbalimbali watachuana katika kuvuta kamba, kukimbiza kuku na kukimbia kwenye magunia na washindi watapewa zawadi mbalimbali.

Sunday, August 17, 2014

MARIA SHILA NDIYE REDDS MISS KINONDONI 2014

Redd's Miss Kinondoni 2014, Maria Shila (katikati) akipunga mkono baada ya kutangazwa kuwa ndiye mshindi wa taji hilo na kuwaongoza warembo wengine 15 waliokuwa wakiwania taji hilo. 
Wengine mshindi wa pili Camila Cindy John (kulia) na mshindi wa tatu Queenlatifa Hasim. Shindano hilo lilifanyika Dar es Salaam usiku wa kuamia jana. (Picha: FK Blog).

Maafa! Jiwe laporomoka na kuua wanne Mwanza

http://radio-tanzania.de/wp-content/uploads/Bismarck-Rock.jpg
WATU wanne wa familia mbili tofauti wa  barabara ya Nyerere ‘A’ katika eneo la Mabatini wilayani  Nyamagana jijini Mwanza, wamefariki baada ya kuporomokewa na  jiwe kubwa lililoviringika kutoka mlimani kutokana na mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia juzi.
Kwa mujibu wa taarifa za kipolisi waliofariki ni pamoja na Sayi Otieno na mkewe Quenter Kweko walifariki papo hapo baada ya kukandamizwa na jiwe kubwa lilivunja nyumba waliyokuwa wakiishi eneo hilo, huku mtoto wao mwenye miaka 4 akinusurika kifo.
Baada ya jiwe hilo kuleta madhara katika nyumba hiyo, pia likalisukuma jiwe jingine ambalo liliporomoka na kuipiga nyumba ya Joseph William na kuwaua watoto wake wawili papo hapo waliotajwa Keflin Masalu (14) na Emaueli William (12) anayesoma darasa la tano huku Jophrey Joseph (14) wa darasa la saba wa Shule ya Msingi Mbugani akinusurika.

Polisi na uongozi wa serikali ya Mwanza imewataka wakazi waliojenga kwenye milima ya mawe na kuhatarisha maisha yao kuhama katika maeneo hayo kipindi hiki ambacho mvua zimeanza kunyesha ili kuepuka maafa zaidi.

Stoke City wamnyakua Victor Moses wa Chelsea

http://images.dailystar-uk.co.uk/dynamic/58/photos/178000/620x/6178.jpgWINGA wa Chelsea, Victor Moses amejiunga na Stoke City kwa mkopo wa muda mrefu kocha Jose Mourinho akijaribu kupounguza kikosi chake kuelekea msimu mpya.
Moses anaachana na kocha huyo Mreno na kwenda kujiunga na timu ya Mark Hughes Uwanja wa Britannia.
Mnigeria huyo alicheza kwa mkopo msimu uliopita Liverpool, lakini akawa anasotea namba kwenye kikosi cha kikosi cha Brendan Rodgers.

Tanzania wenyeji wa Wushu, nchi 8 kuja kuchuana




Mkurugenzi wa Mipango na Ufundi wa TWA, Karama Masoud 'Kalapina'
NCHI nane zikiwamo za China, Kenya, Iran na wenyeji Tanzania inatarajiwa kuchuana katika michuano ya kimataifa ya mchezo wa Wushu itakayofanyika kati ya Agosti 30-31 jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Chama cha Wushu Tanzania (TWA), Sempai Golla Kapipi aliliambia MICHARAZO kuwa, michuano hiyo itafanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja na Tanzania kuanzia saa 4 asubuhi.
Sempai Kapipi alisema wenyeji Tanzania itawakilishwa na klabu 23 na wachezaji wengine mmoja mmoja dhidi ya wawakilishi wa nchi za Kenya, Uganda, Iran, China, Libya, Nigeria na Zimbabwe.
"Nchi zilizothibitisha mpaka sasa kushiriki michuano hiyo ni majirani zetu wa Kenya na Uganda, Iran, China, Zimbabwe, Nigeria na Libya na wenyeji Tanzania itakayowakilishwa na klabu 23," alisema.
Katibu huyo alifafanua kuwa katika michuano hiyo kutakuwa na mitindo miwili itakayoonyeshwa kupitia mchezo huo maarufu kama Kungfu ya Sanda na Tai-ru itakayohusisha mapigano ya mapanga.
Sempai Kapipi alisema kuwa wapo katika mipango ya kuwaalika wanamichezo wa judo, karate na ngumi ili kuonyesha manjonjo yao.
Hii ni mara ya pili kwa chama hicho kuandaa michuano mikubwa ya mchezo huo baada ya awali kuandaa michuano ya taifa iliyohusisha klabu pekee za Tanzania iliyofanyika Ufukwe wa Coco mwaka 2011.
Naye Mkurugenzi wa mashindano wa chama hicho, Karama Masoud 'Karapina' alisema maandalizi yanaendelea vyema na wawakilishi wa nje ya nchi na klabu za mikoa mbalimbali wataanza kuwasili wiki ijayo.
"Kila kitu kimekaa vema na tutaanza kupokea wageni ndani ya wiki ijayo, hadi siku ya kuanza kwa michuano tunaamini wawakilishi wote watakuwa wameshawasili jijini Dar es Salaam," alisema Kalipina.

Arsenal yaanza vyema England, Spurs yatusua ugenini




ARSENAL imeianza vyema Ligi Kuu ya England baada ya kuitandika Crystal Palace ilitimtimua kocha wake, Tony Pulis kwa mabao 2-1.
Mchezo huo ambao ulikuwa wa mwisho kwa pazia la ufunguzi la ligi hiyo usiku wa jana ilishuhudiwa wageni wakitangulia kupata bao kupitia Hangeland dakika 35, kabla ya Koscienly kusawazisha dakika 45. Kipindi cha pili Arsenal walitengeneza nafasi nyingi lakini wakashindwa kuzitumia vizuri na mpaka dakika 90 bado ilikuwa 1-1, dakika 5 za nyongeza Aaron Ramsey akaifungia Gunners goli la ushindi.
Katika mechi nyingine za ligi hiyo Tottenham Hotspur ikiwa ugenini imepata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya West Ham licha ya kiucheza pungufu kwa muda mrefu baada ya beki wake mmoja kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 29.
Bao pekee liliwekwa kimiani na Eric Dier katika dakika za ziada katika mechi iliyopigwa kwenye uwanja wa Boleyn Ground.

Stoke City ikiwa nyumbani kwake nayo ilijikuta ikilala kwa Aston Villa kwa kufungwa 1-0, bao likiwekwa kimiani na Andreas Weimann dakika ya 50.
Leicester City ilikaribishwa tena kwenye Ligi Kuu kwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Everton, huku QPR ikilala nyumbani bao 1-0 dhidi ya Hull City, bao hilo likiwekwa kimiani na James Chester katika dakika ya 52.

Van Gaal aanza kwa kichapo nyumbani EPL


KOCHA mpya wa Manchester United , Mholanzi, Louis van Gaal amekaribishwa na kipigo cha mabao 2-1 katika mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu dhidi ya Swansea City ndani ya dimba la Old Trafford.
Hii ni mara ya kwanza kwa Man United kupoteza mechi ya ufunguzi wa msimu katika uwanja wake wa Old Trafford.
Swansea City walikuwa wa kwanza kuandika bao la kuongoza katika dakika ya 28 kupitia kwa Ki Sung-yueng.
Mshambuliaji na nahodha wa Man United, Wayne Mark Rooney aliisawazishia timu yake bao hilo katika dakika ya 53 baada ya kupiga tikitaka mpira wa kona uliochongwa na Juan Mata.
Gylfi Sigurdsson ndiye aliibuka shujaa wa kuifungia bao la ushindi Swansea katika dakika ya 72 na kukalia usukani wa ligi kuu kwa saa kadhaa.
Baada ya kumalizika kwa mechi hiyo pointi za muhimu alizozungumza Van Gaal ni:
-Sio kwamba safu ya ulinzi ndio inatakiwa kuboreshwa bali ni timu nzima.
-Amesema hatapaniki kwasababu ya Man United kupoteza.
-Atawapa nafasi zaidi wachezaji kumpatia ushindi.
Kikosi cha Manchester United: De Gea, Jones, Smalling, Blackett, Lingard (Januzaj), Fletcher, Herrera, Young, Mata, Rooney (c), Hernandez (Nani)
Wachezaji wa akiba: Amos, James, M Keane, Fellaini, Kagawa
Kikosi cha Swansea: Fabiański; Rangel, Williams, Amat, Taylor, Ki, Shelvey, Dyer, Sigurðsson, Routledge, Bony (Gomis)
Wachezaji wa akiba: Tremmel, Bartley, Richards, Tiendalli, Montero, Sheehan.

Azam watangulia Robo Fainali Kagame


MABINGWA wa soka nchini Azam wamefanikiwa kutinga hatua ya Robo fainali ya michuano ya Kagame baada ya kuibamiza Adama ya Ethiopia kwa mabao 4-1 katika mechi iliyocheza mjini Kigali, Rwanda.
Mechi hiyo iliyokuwa ya kukamilisha ratiba kwa Azam katika hatua ya makundi lilichezwa kwenye uwanja wa Nyamirambo na  maboa ya washindi yaliwekwa kimiani na nahodha, John Bocco 'Adebayor', Mcha Khamis 'Vialli', Didier Kavumbagu na Kipre Tchetche.
Ushindi huo umeifanya Azam kuongoza kundi lake kwa kuwa na pointi 8 baada ya sare mbili na ushindi wa mechi mbili na sasa itashuka dimbani Jumatano kuumana na El Merreikh ya Sudan.
Azam waliingia kwenye michuano hiyo kama zali baada ya waliokuwa wawakilishi wa Tanzania, Yanga kuenguliwa kwa kitendo cha kutaka kupelekea kikosi cha pili katika michuano hiyo mikubwa kwa ngazi za klabu kwa timu za Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
Hii ni mara ya pili kwa Azma kuicheza michuano hiyo, mwaka 2012 iliishiriki wakati Tanzania ikiwa wenyeji na ilifanikiwa kufika fainali na kufungwa mabao 2-0 na Yanga iliyokuwa imetwaa kwa mara ya pili mfululizo.

Friday, August 15, 2014

Hiki ndicvho kikosi kitakachowavaa magwiji wa Real Madrid

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi0PgyWbjR3xJl_pDRCaNGU3l8dtB2GOqTNf-JSpWlJu49gUt4n2uHIvOpPfV4Z9ddGl5h2g4yTsGK0Jhe_a8dPZrYOqWD9xeWlJLMBfnXfCK8BDTQtWuRA_uILS5LNfN6gPltqdA6sRYA/s1600/Simba+SC+2002.jpg
Baadhi ya nyota wa zamani wa Simba walioitwa katika timu ya Tanzania All Stars
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh1b2UD-fxCvuq6yPPbyH6hYAbnGbxw_AX1a_UUScixb7mZXk_whqMf7JuV-NzIgxAw6F42KBQ6yXvgJjwDP6uRwCsWw5tH5B9AeEgertpkEAM8sAl-lPITOVknWRfcUH4ihF5M3RkNjOE/s400/IMG_1860.jpg
Wengine wametoka katika kikosi hiki cha Yanga
MAKIPA wa zamani maarufu waliowahi kutamba na timu za Simba, Yanga na Taifa Stars, Mohammed Mwameja na Manyika Peter ni miongoni mwa wachezaji wa kikosi cha Tanzania All Stars kitakachovaana na magwiji wa Real Madrid ya Hispania, Agosti 23, mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana jana jijini Dar es Salaam zinasema kuwa kikosi hicho kitakuwa chini ya Kocha Charles Boniface akisaidiwa na Fred Felix 'Minziro' na Jamhuri Kihwelo ‘Julio’.
Mbali na Mwameja na Manyika wachezaji wengine wanaounda kikosi hicho ni mabeki; Nsajigwa Shadrack, Mecky Mexime, Boniface Pawasa, John Mwansasu, Abubakar Kombo, George Masatu na Habib Kondo,
Viungo Suleiman Matola, Shaaban Ramadhani, Salvatory Edward, Sabri Ramadhani ‘China’, Yussuf Macho, Abdul Mashine, Abdul Maneno, Mao Mkami, Steven Nyenge, Madaraka Suleiman, Akida Makunda na Mtwa Kihwelo.
Washambuliaji ni Monja Liseki, Iddi Moshi, Dua Said, Emmanuel Gabriel, Said Maulid, Thomas Kipese, Nasor Mwinyi ‘Bwanga’, Edibilly Lunyamila, Mohamed Hussein ‘Mmachinga’, Clement Kahabuka, Madaraka Suleiman na Akida Makunda.
Safu ya uongozi ya timu hiyo ya Tanzania ni pamoja na Mtemi Ramadhani, Hasannai Mnyenye, Omar Gumbo na Hamis Kisiwa na daktari wake ni Dk Mwanandi Mkwankemwa.
Wachezaji magwiji wa Real Madrid waliotamba kuanzia La Liga, wakacheza ligi nyingine za Ulaya, Kombe la Ulaya, Ligi ya Mabingwa na Kombe la Dunia waliowahi kuchezea Real Madrid watakuja nchini Agosti 22 kwa ziara maalum pamoja na kucheza mchezo wa kirafiki na kikosi maalum cha wachezaji nyota wa Tanzania Agosti 23, kabla ya kufanya ziara ya kitalii katika vivutio mbalimbali, ikiwemo kupanda mlima Kilimanjaro.
Real Madrid inakuja nchini kwa mwaliko wa kampuni ya Tanzania Sisi ni Nyumbani (TSN), chini ya Mkurugenzi wake Mkuu, Farough Baghozah.
Miongoni mwa nyota wanaotarajiwa kuja na Real nchini ni pamoja na Wanasoka Bora wa zamani wa Dunia, Mfaransa Zinadine Zidane, Mreno Luis Figo na Mbrazil, Ronaldo Lima.
Magwiji hao wa Real tayari wamekwishafanya matangazo ya ziara yao nchini wakisema wana hamu mno ya kukanyaga ardhi ya Tanzania.
Kampuni ya Vodacom Tanzania ni miongoni mwa makampuni yaliyojitokeza kudhamini ziara pamoja na Fastjet, Tropical, Pembe Flower, Lake Gas, EFM Radio na Ladger Plaza Bahari Beach.
Wito umetolewa kwa makampuni zaidi kujitokeza kudhamini ziara hiyo ya kihostoria nchini.

Serikali yawatoa hofu wananchi kuhusu Ebola

Screen Shot 2014-08-15 at 10.47.21 AM

SERIKALI imewatoa hofu wananchi wake baada ya kutoa ufafanuzi huu ya taarifa za kuingia kwa ugonjwa huo jijini Dar es Salaam na kuibua kizaazaa.
Ugonjwa wa Ebola ambao kwa sasa umeingia kwenye headlines za dunia kutokana na kuripotiwa kwenye nchi mbalimbali za Afrika sasa umeingia kugusa vichwa vya habari na kuihusisha Tanzania.
Waziri wa Afya wa Seif Rashid amesema wagonjwa waliohisiwa kupata maambukizo hayo kutokana na dalili za awali ni kutoka Benin na Mtanzania lakini baada ya vipimo wameonekana hawana maambukizo hayo.
Waziri Seif Rashid amesema kuwa tayari eneo maalumu limetengwa kwa ajili ya kufanyia uchunguzi wagonjwa wanaotiliwa shaka kuwa na ugonjwa huo ikiwa ni kauli iliyotoka baada ya kufanyiwa uchunguzi kwa wagonjwa wawili waliohisiwa.
Kupitia ukurasa wake wa facebook, Waziri Seif amesema vifaa maalumu vitakavyotumiwa na watoa huduma katika kuhudumia wagonjwa vimewekwa pia huku wizara ya afya ikiongeza uwezo wa kufanya uchunguzi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere ambao wasafiri wengi kutoka nje huutumia.

Tanzania yaporomoka FIFA, yashindwa hata na Sierra Leone

Kikosi cha Stars ambacho kiling'olewa michuanoni na Msumbiji na kuporomoka kwenye viwango vipya vya FIFA
TANZANIA imeporomoka kwa nafasi nne katika viwango vya soka vilivyotolewa na Shirikikisho la Soka duniani, Fifa.
Katika viwango hivyo ambavyo Ujerumani imeendelea kuongoza kwa ubora duniani ikifuatiwa na Argentina na Uholanzi, Tanzania imeshika nafasi ya 110 huku Msumbiji ambayo iliitoa kwenye kinyang'anyiro cha kuwania tiketi ya kucheza fainali za Mataifa ya Afrika mwakani nchini Morocco ikipanda kwa nafasi saba na kuwa ya 107.
Kwa upande wa Afrika Mashariki na Kati, Uganda imeendelea kuwa kinara ikipanda nafasi sita na kuwa ya 81 duniani ikifuatiwa na Rwanda ambayo ni ya 101 baada ya kupanda nafasi nane, Kenya inafuata ikiwa ni 104 licha ya kushuka nafasi tisa mwezi huu, huku Burundi ikiburuza mkia ikiwa ni ya 129 baada ya kushuka nafasi tatu.
Barani Afrika kwa ujumla, Algeria inaongoza huku kidunia ikishika nafasi ya 24 ikifuatiwa na Ivory Coast (25), Nigeria (33), Ghana (36) na Misri (38).
Chini ni 20 Bora ya Dunia safari hii ambayo inafungwa dimba na England;
1. Ujerumani,
2. Argentina
3. Uholanzi
4. Colombia
5. Ubelgiji
6. Uruguay 
7. Hispania
7. Brazil
9. Uswisi
10. Ufaransa
11. Ureno
12. Chile
13. Ugiriki
14. Italia
15. Costa Rica
16. Croatia
17. Mexico
18. Marekani
19. Bosnia and Herzegovina
20. England
AFRIKA 20 Ipo hivi:
    
1. Algeria
2. Ivory Coast
3. Nigeria
4. Ghana
5. Misri
6. Tunisia
7. Sierra Leone
8. Cameroon
9. Burkina Faso
10.Senegal
11.Mali
12.Libya
13.Guinea
14. Afrika Kusini
15.Cape Verde
16.Angola
17.Benin 
18. Kongo
19. Morocco
20. Uganda

Snura kukirudia Kigoda chake cha zamani!

Snura katika pozi
STAA wa nyimbo za 'Majanga', 'Umevurugwa' na 'Umeshaharibu', Snura Mushi, amesema yupo katika mipango ya kuurudia wimbo wake wa zamani uitwao 'Kigoda'.
Wimbo huo wa 'Kigoda', ulirekodiwa na Snura miaka zaidi ya 15 iliyopita wakati akianza kuibukia kwenye sanaa, lakini haukupata nafasi ya kumtambulisha kama kazi zake za sasa.
Akizungumza na MICHARAZO, Snura alisema ataurudia wimbo huo kwa kuuweka kwenye miondoko ya mduara akiamini utakubalika kwa vile ni wimbo uliokuwa na mistari iliyoshiba na yenye ujumbe mzuri.
Snura alisema kazi hiyo itafanywa mara baada ya kutengeneza video za nyimbo zake mbili zilizokamilika kwa sasa za 'Ime-expire' na 'Mtaka Basi' ambazo bado hazijaachiwa hewani.
"Nipo katika mpango wa kuurudia wimbo wangu kwa kwanza kabisa katika fani ya muziki uitwao 'Kigoda', ila kazi hiyo itafanywa baada ya kukamilisha video ya nyimbo zangu mpya za sasa," alisema Snura.
Msanii huyo ambaye pia  ni muigizaji wa filamu alisema kila uchao yeye huwaza namna ya kuwashushia mashabiki wake burudani kama njia ya kuwashukuru kwa kumpokea vyema katika fani hiyo.

Coast Modern kuwatoa watatu wapya

Omar Tego
KUNDI la muziki wa taarab la Coast Modern 'Watafiti wa Mipasho' limefanikiwa kuwapata wasanii watatu wapya chipukizi wanaiotarajia kuwatambulisha na kazi zao mpya wanazotarajia kuzirekodi hivi karibuni.
Chipukizi hao walionyakuliwa na kundi hilo linaliotamba kwa sasa na wimbo wa 'Katiba Mpya' ni Mwajuma Othman, Aisha Abdallah na Dualla Ally ambao wameanza mazoezi ya nyimbo zao kabla ya wiki mbili zijazo kuingia studio kuzirekodi.
Mkurugenzi wa kundi hilo, Omar Tego 'Special One' aliiambia MICHARAZO kuwa, wasanii hao wapya wana vipaji vikubwa vya kuimba na kuwatabiria kuja kufunika mbeleni mara baada ya kazi zao wanazoziandaa kurekodi kuanza kurushwa hewani.
Tego alisema tayari kila msanii ameshatungiwa wimbo wake na kuufanyia mazoezi kwa sasa na wataingia kuzirekodi kabla ya kuachiwa hewani wakati akijipanga kutengeneza video zake.
"Tuna vijana watatu wakali achaa...wawili wa kike na mmoja wa kiume na kwa sasa wapo katika mazoezi makali ya nyimbo zao kabla ya kuingia studio kuzirekodi," alisema Tego.
Kundi hilo limejipatia umaarufu mkubwa katika miondoko ya taarab kutokana na nyimbo kadhaa kama 'I'm Crazy for U', 'Kupenda Isiwe Tabu', Chongeni Fenicha', Mwanamke Kujiamini', 'Damu Nzito', 'Gubu la Mume' na nyingine.

Ribery hatimaye atundika daluga, kisa...!

http://www.soccerroomtoday.com/wp-content/uploads/2012/06/franck-ribery-p12.jpg
KIUNGO Mshambuliaji wa Ufaransa, Franck Ribery ametangaza rasmi kustaafu mechi za kimataifa.
Ribery (31), anayeitumikia Klabu ya Bayern Munich amekuwa mchezaji bora wa mwaka mara tatu nchini Ufaransa huku akiichezea timu ya taifa mechi 81 na kufunga mabao 16.
"Ninataka kujikita zaidi katika kuiangalia familia yangu na kuitumikia vema Bayern Munich na kutoa njia timu ya taifa kwa wachezaji wengi makinda," Ribery ambaye ameichezea Ufaransa katika fainali za Kombe la Dunia za 2006 na 2010 aliliambia Jarida la Ujerumani la Kicker.
Ribery ambaye alizikosa fainali za Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil kutokana na kuwa majeruhi, amekuwa mmoja wa nyota wenye vipaji tangu ametua Bayern kwa dau la paundi milioni 20 akitokea Marseille mwaka 2007, ametwaa ubingwa wa Bundesliga mara nne na mara moja Kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Kadhalika Ribery alishika namba tatu katika kinyang'anyiro cha tuzo ya Mchezaji Bora wa Dunia wa Mwaka 2013 (Fifa Ballon d'Or 2013), akimaliza nyuma ya Lionel Messi na mshindi Cristiano Ronaldo.
Uamuzi huo unamaana Ribery hatajumuishwa katika kikosi kitakachoshiriki michuano ya Euro 2016, ambayo itafanyika Ufaransa.

Ronaldo, Manuel Neuer kuwania tuzo Mchezaji Bora Ulaya

KWA muda wa miaka minne mfululizo Cristiano Ronaldo amekuwa katika orodha ya mwisho ya wachezaji bora wa UEFA ambao wamekuwa wakiwania tuzo ya Ulaya na mara hii pia yumo katika orodha hiyo akiwa pamoja na Arjen Robben na Manuel Neuer.

Mshambuliaji huyo wa Madrid Ronaldo atakuwa akitegemea kutwaa tuzo hiyo kwa mara ya kwanza baada ya kuingia katika kinyang'anyiro hicho tangu kuanza kuteuliwa mwaka 2011 lakini akishindwa kutwaa tuzo hiyo katika kila igizo.

Mshindi huyo wa Ballon D'Or alikuwa na msimu mzuri uliopita akishinda tuzo ya Copa del Rey pamoja na taji la 10 kwa Madrid la michuano ya European Cup - La Decima.

Cristiano Ronaldo akifunga goli la rekodi la 17 katika michuano ya vilabu bingwa Ulaya
Strike: Robben won the league and cup double for Bayern Munich and scored three World Cup goals for Holland
Robben alishinda mataji mawili ya ligi na kikapu kwa Bayern Munich na alifunga na aliifungia magoli matatu Uholanzi katika kombe la dunia
Glory: Manuel Neuer (centre) won the league and cup double with Bayern and the World Cup with Germany
Furaha: Manuel Neuer (katikati) alishinda Ligi na vikapu mara mbili akiwa na Bayern na kombe la dunia 
Saba waliokwama kutinga hatua ya mwisho




4) Thomas Muller (Germany, Bayern Munich) - 39 points 
5)Philipp Lahm (Germany, Bayern Munich) - 24 points
=) Lionel Messi (Argentina, Barcelona) - 24 points
7) James Rodriguez (Colombia, AS Monaco, now at Real Madrid) - 16 points 
8) Luis Suarez (Uruguay, Liverpool, now at Barcelona) - 13 points
9) Angel Di Maria (Argentina, Real Madrid) - 12 points
10) Diego Costa (Spain, Atletico Madrid, now at Chelsea) - 8 points

EBOLA YALETA KIZAAZAA CAF YAZUIA MECHI AFRIKA

http://tv360nigeria.com/wp-content/uploads/2014/03/Ebola-virus1.jpg.pagespeed.ic_.b7XBqLSN9I1.jpg 
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limezuia mechi zake kuchezwa Guinea, Liberia na Sierra Leone kutokana na kuripotiwa kuwepo kwa wagonjwa wengi wa Ebola katika nchi hizo.
Ikiwa ni njia mojawapo ya kuzuia kusambaa kwa virusi vya ugonjwa huo kupitia mkusanyiko wa watu, CAF imevitaka vyama vya mpira wa miguu vya nchi hizo kuchagua viwanja vingine huru kwa ajili ya timu zao zinazoshiriki michuano yake kwa kipindi hiki hadi katikati ya mwezi ujao.

CAF itafanya tathmini nyingine kuhusiana na ugonjwa huo kuanzia katikati ya Septemba ili kuona kama nchi hizo zinaweza kupokea timu ngeni kwa ajili ya mechi mbalimbali za michuano yake, na baadaye kufanya uamuzi wa kuruhusu au kuendelea kusimamisha.

Pia kutokana na mapendekezo ya Shirika la Afya Duniani (WHO), CAF imesema kwa nchi zenye virusi vya Ebola ni muhimu kwa vyama vyake vya mpira wa miguu kuufanyia vipimo vya afya msafara wa timu zao ili kuhakikisha wenye virusi vya ugonjwa huo hawasafiri.

DENI LAIPONZA TFF, MADALALI WALISHIKILIA BASI LA STARS

BASI la Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limekamatwa na madalali kwa amri ya mahakama kutokana na deni la sh milioni 140 ambalo tunadaiwa hadi litakapolipwa.

Amri hiyo imetokana na deni hilo la kampuni ya Punchline ya Kenya iliyokuwa ikichapa tiketi za kuingilia uwanjani kuanzia mwaka 2007. Hadi sasa tumeshalipa sh. milioni 70 katika deni hilo.

Jitihada zinafanyika ili kumaliza deni hilo. Pia tunachunguza mwenendo mzima uliosababisha kuwepo deni hilo.

YANGA YAIPIGA BAO SIMBA, YAMNASA BEKI WA JKT RUVU

Guu la kushoto; Yanga SC imeizidi kete Simba SC katika saini ya Edward Charles
YANGA SC imefanikiwa kumpata beki chipukizi wa JKT Ruvu, Edward Charles baada ya kukamilisha taratibu zote za usajili wake kutoka timu hiyo ya Jeshi la Kujenga Taifa na kumsainisha Mkataba wa miaka mitatu.
Yanga SC kwa miezi miwili sasa imekuwa ikisotea saini ya mchezaji huyo kwa kuanzia kufuata taratibu za kuvunja mkataba wake jeshini- hadi leo ilipokamilisha. Viongozi wa Yanga SC wakiongozwa na Francis Kifukwe leo walikuwa na kikao cha mwisho na uongozi wa JKT juu ya suala la uhamisho wa mchezaji huyo na mambo yamekwenda vizuri. Beki huyo alikuwa pia anawaniwa na mahasimu Simba SC, ambao jitihada zao ziligonga ukuta mapema, baada ya kuambiwa wapinzani wao Yanga SC, wamepiga hatua kubwa katika kufukuzuia huduma za chipukizi huyo. Edward sasa atajiunga na Yanga SC mara moja chini ya kocha Mbrazil, Marcio Maximo kuanza maandalizi ya msimu mpya. Ni Maximo aliyewasukuma viongozi wa Yanga SC kufukuzia haraka saini ya mchezaji huyo baada ya kutovutiwa na uchezaji wa beki wa sasa wa kushoto wa klabu hiyo, Oscar Joshua.  Edward Charles ni kati ya chipukizi waliopo timu ya taifa ya wakubwa kwa sasa, Taifa Stars chini ya kocha Mholanzi, Mart Nooij ambao wanainukia vizuri.   Ni mkabaji mzuri, ana nguvu, kasi- mbinu za anapokuwa na mpira na asipokuwa nao na pia hupanda vizuri kushambulia na kurudi kwa haraka. Anasifika kwa kupiga krosi nzuri pamoja na mpira iliyokufa.
BIN ZUBEIRY

Suarez apeta, apungiziwa adhabu na CAS

http://i.smimg.net/13/39/luis-suarez-liverpool.jpgHATIMAYE Mahakama ya Soka ya Kimataifa CAS, imekubali kupunguza adhabu ya kumfungia miezi minne Luis Suarez wa Barcelona baada ya kumuuma Giorgio Chiellini wa Italia wakati wa Kombe la Dunia.
CAS imetoa nafuu kwa Suarez na sasa Barcelona itamtambulisha rasmi Jumatatu na atapewa ruksa ya kufanya mazoezi na wenzake.
Mambo ambayo yamepunguzwa na yale yanayobaki kuwa adhabu ni kama yafuatayo.
Suarez ruhusa:
- Kufanya mazoezi na Barcelona.
- Kutambulishwa na Barcelona.
- Kucheza mechi za kirafiki, si zile za mashindano.
- Kucheza mechi za kirafiki za Uruguay dhidi ya Japan, Korea na Saudi Arabia katika miezi ya Septemba na Oktoba
- Kuhudhuria mechi uwanjani. 
- Kuhudhuria shughuli za matangazo zinazoihusisha Barcelona.
Suarez si ruhusa:
- Kucheza mechi yoyote ya mashindano akiwa na Barca hadi Oktoba 26.
- Kuichezea Uruguay mechi yoyote hadi zifikie mechi nane.