STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, August 3, 2015

Shule ya Joyland wahimiza amani Uchaguzi Mkuu 2015

Wahitimu wa masomo ya awali shule ya Kimataifa ya Joyland, wakiimba wimbo wa Shule wakati wa mahafali ya pili ya shule hiyo iliyopo Tuangoma Kigamboni jijini Dar es Salaam
Wanafunzi  shule Darasa la nne Shule ya Kimataifa ya Joyland, wakiimba wimbo wa Shule wakati wa mahafali ya pili ya shule hiyo iliyopo Tuangoma Kigamboni jijini Dar es Salaam

Wahitimu wa masomo ya awali shule ya Kimataifa ya Joyland, wakiimba wimbo wa Shule wakati wa mahafali ya pili ya shule hiyo iliyopo Tuangoma Kigamboni jijini Dar es Salaam

Wanafunzi  wa Darasa la awali  Shule ya Kimataifa ya Joyland, wakiimba wimbo  wakati wa mahafali ya pili ya shule hiyo iliyopo Tuangoma Kigamboni jijini Dar es Salaam
Capt 5
Wanafunzi waDarasa pili Shule ya Kimataifa ya Joyland, wakicheza ngoma ya utamaduni (Ndolela) wakati wa mahafali ya pili ya shule hiyo iliyopo Tuangoma Kigamboni jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Shule ya Kimataifa ya Joyland, Fedrick Otieno akiwasaidia watoto wa darasa la awali kupanda juu ya jukwaa kuimba wimbo maalum wakati wa mahafali ya pili ya shule hiyo iliyopo Tuangoma Kigamboni jijini Dar es Salaam

Skauti wa Shule ya Kimataifa ya Joyland, wakiruka sarakasi  wakati wa mahafali ya pili ya shule hiyo iliyopo Tuangoma Kigamboni jijini Dar es Salaam
Mhitimu wa masomo ya awali shule ya Kimataifa ya Joyland, Colin Christopher akisoma hotuba wakati wa mahafali ya pili ya shule hiyo iliyopo Tuangoma Kigamboni jijini Dar es Salaam

Mkaguzi Mkuu wa Elimu Kanda, Shani Kanungira akitoa hotupa ya awali kabla ya mgeni rasmi wakati wa mahafali ya pili ya shule hiyo iliyopo Tuangoma Kigamboni jijini Dar es Salaam

Mwakilishi wa Afisa Elimu ya Msingi Manispaa ya Temeke, Frank Makingi akizungumza Tuangoma Kigamboni Dar es Salaam wakati wa mahafali ya pili ya shule hiyo
Na Tariq Badru
UONGOZI wa Shule ya Kimataifa ya Joyland, umewaomba kuwa kuwakumbusha watanzania na hasa viongozi na wanasiasa kuhakikisha Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu unakuwa wa amani na utulivu.
Mkurugenzi wa shule hiyo, Fredrick Otieno alisema vurugu za aina yoyote kutokana na ushindani wa kisiasa unaweza kuiweka Tanzania pabaya na kuvuruga kila kitu na kuwapa wakati mgumu watoto na watu wengine wasiojiweka ambao wanahitaji utulivu na amani kufanya mambo yao.
Otieno aliyasema hayo wakati wa hotuba yake katika mafahari ya wanafunzi wa masomo ya awali wa shule hiyo ya Joyland yaliyonyika mwishoni mwa wiki Tuangoma Kigamboni, jijini Dar es Salaam.
"Leo wanafunzi na watoto wanafurahi na sisi wazazi na walezi tunajumuika pamoja shuleni kuwapongeza wahitimu wetu, kama kunakuwa na vurugu hili haliwezi kufanyika na watoto hawatapata haki yao ya kusoma au kufurahia maisha yao duniani," alisema Otieno.
Aliongeza ni vema wanasiasa, viongozi na wananchi kwa ujumla kushiriki uchaguzi uliopo mbele yetu kwa amani na utulivu kwa hizo ni neema ambazo kwa mataifa mengine wanatafuta kwa vile nchi zao zimevurugwa kwa sababu na mambo hayo na mengine yaliyokimiza amani na utulivu.
Aidha aliwakumbusha wazazi nchini kote kujenga utamaduni wa kuwalipa ada watoto wao na kufuatilia nyendo za watoto wao wanapokuwa likizo na hata shuleni ili kurahisisha kazi kwa walimu katika kuwapa elimu itakayojenga misingi imara ya maisha yao ya baadaye. Alisema kwa mfano shuleni kwake wazazi na walezi wamekuwa wazito wa kulipa ada kiasi kwamba shule inadai zaidi ya Sh milioni 100, lakini wanashindwa kuwafukuza watoto kwa vile wanaamini hawana makosa yoyote na ndiyo maana wanataka wazazi na walezi kutimiza wajibu wao katika suala la elimu za watoto wao.
Mkurugenzi huyo alisisitiza kuwa hakuna hazina bora kama mtoto kupewa elimu ambayo huja kumsaidia ukubwani kwa kuzingatia kuwa dunia ya sasa inaendeshwa kisasa na bila elimu bora na ya kutosha ni vigumu kijana kusimama na kukabiliana na changamoto hizo.
Naye Mkaguzi Mkuu wa Elimu Kanda, Shani Kanungira aliwasisitiza wazazi kutumia kujitolea na kutimiza wajibu wao kuwasomesha watoto badala ya kutumia fedha nyingi kwa mambo yasiyo na tija kwa watoto na familia zao kwa ujumla.
Shani alitoa nasaha yake kabla ya kumpisha Mwakilishi wa Afisa Elimu ya Msingi Manispaa ya Temeke, Frank Makingi aliyesisitiza umuhimu wa wazazi na walezi kujenga utamaduni wa ushirikiano dhidi ya walimu wa shule wanazosoma watoto wao.
Makingi alisema siyo kila jambo la wanafunzi kuachwa mikononi mwa walimu tu, kadhalika alikumbusha kuwasaidia watoto katika kuwalea katika maadili mema ili kulifanya taifa kuwa na raia wema na viongozi wazuri na waadilifu wa baadaye.

Monday, July 20, 2015

Michael Olunga aipeleka Gor Mahia robo fainali Kagame Cup

http://www.standardmedia.co.ke/images/saturday/stdrclwhqpq.jpg
Michael Olunga
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgKxRDIwrjKq6PNP8GUEXC5s6MqT9DpyWecXpY324qzrHOoXoIVRN1JTFo2JKNATy2Jsgaq2axLJ8TZAjWy9G7sdYv_QZSQK4XJBmlJA8gqO93Qfu2HMbmhFDE2Tvc2HSUBSkRfgJDIcrg/s1600/IMG_3285.JPG
Olunga (kulia) alipoikimbiza Yanga katika mechi yao ya kwanza ya Kombe la Kagame ambapo alifunga moja kuisaidia Gor Mahia kushinda 2-1
MSHAMBULIAJI nyota wa Gor Mahia, Michael Olunga ameendelea kuonyesha dhamira yake ya kunyakua kiatu cha dhahabu katika michuano ya Kombe la Kagame baada ya jioni hii kutupia mabao mawili kambani wakati timu yake ikiizamisha KMKM kwa mabao 3-1.
Olunga alifunga mabao hayo katika kipindi cha pili na kuiwezesha Gor Mahia kuwa timu ya kwanza kukata tiketi ya kucheza robo fainali ikitokea Kundi A kwa kukusanya pointi sita na mabao matano baada ya mechi yao ya awali kuitoa nishai Yanga kwa mabao 2-1.
Katika mechi huo wa kwanaa Olunga anayewindwa na Simba, ingawa ni ngumu kumpata kwani ana mkataba wa miaka miwili, alifunga bao moja.
Kwa kufunga mabao hayo mawili jana, imemfanya kuongoza orodha ya wafungaji wa michuano hiyo akiwa na magoli matatu akimzidi kete Sallah Bilal wa Al Khartoum ambaye alikuwa akiongoza kwa mabao mawili baada ya mchana wa leo kuingoza timu yake kuilaza Telecom kwa mabao 5-0.
Mara baada ya mechi yake ya Yanga, Olunga alinukuliwa akisema kuwa amekuja Tanzania akiwa na nia moja ya kuwa Mfungaji Bora wa michuano hiyo, kitu kinachoonyesha ni kweli baada ya kufanikiwa kufunga mabao hayo mawili.
Kabla ya Olonga kufunga mabao hayo, Meddie Kagere mkali mwingine wa Gor Mahia aliifungia timu hiyo bao la mapema akimalizia pande la Olunga kabla ya KMKM kusawazisha na kwenda mapumziki timu zikiwa sare ya 1-1 mpaka kwenye dakika ya 65 Olunga alipoanza kufanya yake na kuwazamisha Wazanzibar.

FIFA yatangaza tarehe ya uchaguzi wake mpya

http://shaffihdauda.co.tz/wp-content/uploads/2015/04/Sepp-Blatter.jpg
Rais wa Fifa, Sep Blatter aliyetangaza kujiuzulu mrithi wake atapatika February
SHIRIKISHO  la Soka Duniani, FIFA limetangaza kwamba uchaguzi mkuu wa Rais utafanyika Februari 26 mwakani.
Maamuzi haya yamefanyika leo katika kikao cha kamati ya utendaji ya Shirikisho hilo kilichofanyika mjini Zurich, Uswisi.
Sepp Blatter aliyejiuzulu siku nne baada ya kuchaguliwa amethibitisha kuwa ataendelea kukaa madarakani mpaka uchaguzi mkuu utapofanyika kupata mrithi wake.
Wakati huo, kundi la watu wanaoshinikiza  kufanyika kwa mageuzi wamekutana leo mjini humo wakimuomba katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan kuongoza mapinduzi hayo.
Kundi hilo limesema Annan ni mtu makini ambaye anapaswa kuongoza tume ya mageuzi wakati  huu Dunia ikielekea kupata mrithi wa Sepp Blatter aliyejiuzulu Urais kutokana na kashfa nzito ya rushwa iliyokumba FIFA.
Shirika la Ujasusi la Marekani, FBI liliwatia mbaroni Maafisa saba wa ngazi za juu wa FIFA kwa tuhuma za rushwa.

Stewart afungka mbinu walizoizamisha KCCA

Stewart Hall akiteta na Migi
KOCHA Stewart Hall ni mjanja sana, baada ya kufichua siri ya kuwaanzisha viungo wengi na kucheza soka la kujihami na kushambulia kwa kutumia mipira mirefu. Akizungumzia mbinu zake, Hall alisema alilazimika kutumia mbinu hiyo kwa sababu wachezaji wake wengi bado hawapo fiti. “Tupo katika kipindi cha maandalizi ya mwanzo wa msimu, wachezaji wangu Kipre Tchetche, Didier Kavumbagu na Ramadhani Singano bado hawajawa fiti kwa asilimia mia, lakini naamini tutafika fainali.” alisema Hall Hall aliongeza kuwa timu inayomtisha zaidi ni Gor Mahia kwa sababu wamekuja wakati ligi ya Kenya inaendelea hivyo wachezaji wao wapo fiti.

UTAMU WA KOMBE LA KAGAME WAZIDI KUNOGA DAR

https://thumbp22-ne1.mail.yahoo.com/tn?sid=2126005954&mid=AKh2imIAABZpVaY5ZwsQCBMD2%2BU&midoffset=2_0_0_1_4350124&partid=2&f=1214&fid=Inbox&m=ThumbnailService&w=3000&h=3000http://rushyashya.net/IMG/jpg/apr_fc_team_-_rwanda_-_kigalitoday-2-2.jpg
APR Rwanda
http://shaffihdauda.co.tz/wp-content/uploads/2015/07/Yanga-leo-14.jpg
Yanga na Gor Mahia
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgU-pwUoReK1Inoqwa-tv9F7B4FsQQHzQW9GaG7wzubvb9SCAbF6zgGuLW0T-HTTo2ede7ls9zqJuGTrYNNSoghMV8GO4-5kfnAbuNX1yjWmHghK_qRzBu2MQ1YkUVYSo-N7z6p23PgLzs/s640/426464_358635040821389_1508036080_n.jpg
Al Shend
http://kabumbu.co.tz/wp-content/uploads/2015/01/kikosi-azam-fc.jpg
Azam ya Tanznaia Bara
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiYr-ePKerYIvN49hCZ9IJI-ICEdPieA86ey85RJHvQ131iGA6GEbCXWWbDogjLkjX3y6u7CQrhi07Wnmkj3cDy2Drr-O8hj23no_e0NxN6qDxt_0KSgzSb0084QpabXSEI7dIMJoRXD4bc/s1600/1385637_526389100785782_1638137288_n.jpg
Telecom ya Djibout
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg3v7qvqTyHyaPiHb4iJPQ2UjF7MIw0nVpNbqWGraZLfn3zrJ6t9J4bGJ0Ok268cn_goKj9RqzWVvhzIbNvWOTsBfGmrrJGfaTXfZfAcFez2kVA97hfblC6PDlqUiHoUIKjm5SeoML2U9q_/s1600/IMG_9898.JPG
KMKM ya Zanzibar
http://entebbenews.com/wp-content/uploads/2014/09/KCCA-Mulindwa-9.jpg
KCCA ya Uganda
Kikosi cha Yanga

Kikosi cha Gor-Mahia

Mchezaji wa Yanga, Amis Tambwe akiwa chini huku wachezaji Collins Okoth (kulia) na Harun Shakava (kushoto) wa Gor Mahia ya Kenya wakiwania mpira wakati wa mchezo wa ufunguzi wa mashindano ya Kombe la Kagame uliochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo. Yanga imefungwa mabao 2-1.
Mashabiki wa Yanga

MICHUANO ya Kombe la Kagame imezidi kushika kasi ikiwa inaingia siku yake ya tatu leo tangu yalipofunguliwa rasmi siku ya Jumamosi, huku Al Khartoum ya Sudan ikitoa onyo kwa kuopata ushindi wa kishindi mchana huu dhidi ya Telecom ya Djibout.
Wawakilishi hao wa Sudan waliokuwa sambamba na Al Shandy kuchukua nafasi za mabingwa watetezi Al Merreikh na Al Hilal waliitandika bila huruma Telecom kwa mabao 5-0 na kukwea kileleni mwa Kundi A, ingawa kwa sasa Gor Mahia inayokamata nafasi ya pili na KMKM waliopo nafasi ya tatu wakiendelea kutifuana kwenye Uwanja wa Taifa.
KMKM ambayo ilichukuliwa poa katika kundi hilo, inaendelea kuonyesha kuwa haisindikizi mtu kwani ilitanguliwa kufungwa bao la kwanza na Gor Mahia iliyowazamisha Yanga kwa mabao 2-1 katika pambano la ufunguzi juzi, lakini ikakomaa na kulirejesha dakika tisa baadaye.
Wakenya walipata bao la mapema dakika ya tatu kupitia Meddie Kagere aliyemaliza pande tamu la Michael Olunga ambao ulimbabatiza beki mmoja wa KMKM na kumpoteza kipa wao, lakini Simon Mateo alifunga bao dakika ya 12 tu ya mchezo na muda huu wametoka kukosa bao la wazi.
Mpaka sasa wakati karibu timu zote zikiwa zimeshacheza mechi moja moja, Yanga na Telecom ndio wanaoburuza mkia katika kundi A zikiwa hazina pointi, ingawa Yanga wanakamata nafasi ya nne.
Katika Kundi B, APR ya Rwanda inaongoza msimamo baada ya kuishinda Al Shandy kwa bao 1-0 katioka mchezo wa kwanza, huku timu za Heggan ya Somalia na LLB AFC ya Burundi zinafuatia baada ya jana kutoka suluhu ya kutofungana.
Malakia ya Sudan Kusini inaongoza kundi C ikiwa na pointi tatu sawa na Azam iliyoitambia KCCA ya Uganda jana, lakini wanatofautiana kwa mabao ya kufunga na kufungwa. Malakia iliitambia Adama City ya Ethiopia kwa bao 2-1, wakati Azam yenyewe iliishinda KCCA bao 1-0.
Mpaka muda huu unaosoma blogu hii jumla ya mabao 18 yameshatinga wavuni kwa mechi 8 zilizokwisha kucheza mpaka sasa baada ya jioni hii Gor Mahia kuitambia KMKM kwa mabao 3-1.


Utamu wa michuano hiyo upo hivi kwa mwaka huu wa 2015
MAKUNDI:

KundiA: Yanga-Tanzania, Gor Mahia-Kenya, Khartoum-Sudan, Telecom-Djibout, KMKM-Zanzibar
Kundi B: APR-Rwanda, Al Shandy-Sudan, LLB-Burundi, Heegan-Somalia,
Kundi C: Azam-Tanzania, Malakia-Sudan Kusini,  KCCA- Uganda, Adama City- Ethiopia.

Viwanja:
Taifa- Temeke
Karume-Ilala


MATOKEO:

APR              1-0  Al Shandy
KMKM           1-0  Telecom
Yanga           1-2  Gor Mahia
Adama City   1-2  Al Malakia
LLB              0-0   Heegan
Azam           1-0   KCCA
Telecom        0-5  Al Khartoum
Gor Mahia     3-1  KMKM
 

MSIMAMO:
Kundi A:
                      P  W  D  L   F  A PtsGor Mahia       2   2   0  0   5  2  6Al Khartoum    1   1   0  0   5  0  3
KMKM             2   1   0  1   2  3  3
Yanga             1   0   0  1   1  2  0
Telecom          2   0   0  2   0  6  0

Kundi B:
                     P  W D  L  F  A Pts
APR               1   1  0  0  1  0  3
LLB AFC         1   0  1  0  0  0  1
Heegan          1   0  1  0  0  0  1
Al Shandy      1   0  0  1   0  1  0

Kundi C:

                     P  W D  L  F  A  Pts
Al Malakia       1  1 0  0  2  1   3
Azam              1  1 0  0  1  0   3
Adama City     1  0  0  1  1  2  0
KCCA              1  0  0  1  0  1  0

Wafungaji:

3-Michael Olunga         (Gor Mahia)

2- Salah Bilal               (Al Kahrtoum)
1- Ousmaila Baba         (Al Khartoum)
    Haruna Shakava       (Gor Mahia)
    Michael Olunga         (Gor Mahia)
    Kirkir Glay (og)         (Gor Mahia)
    John Bocco               (Azam)
    Bizimana Djihad        (APR)
    Takele Elemayehu     (Malakia)
    Samuel Ssekamatte  (Malakia)
    Jafar Delil                 (Adama City)
    Juma Mbwana           (KMKM)
    Wagdi Abdallah         (Al Khartoum)
    Murwan Abdallah      (Al Khartoum)
    Meddie Kagere          (Gor Mahia)
    Simon Mateo            (KMKM)
    Meddie Kagere          (Gor Mahia)
RATIBA
KESHO Jumanne

Saa 8 Mchana  Al Shandy vs LLB-Karume
Saa 10 Jioni     Heggan vs APR-Karume
Saa 10 Jioni     Malakia vs Azam-Taifa

Jumatano

Saa 10 Jioni     Khartoum vs KMKM-Karume
Saa 8 Mchana  KCCA vs Adama City-Taifa
Saa 10 Jioni     Telecom vs Yanga-Taifa

Julai 23

Saa 8 Mchana  Hegaan vs Al Shandy-Taifa
Saa 10 Jioni     APR vs LLB-Taifa

Julai 24

Saa 8 Mchana  Khartoum vs Gor Mahia-Taifa
Saa 10 Jioni     KMKM vs Yanga-Taifa

Julai 25

Saa 8 Mchana  KCCA vs Malakia-Taifa
Saa 10 Jioni     Adama City vs Azam-Taifa

Julai 26

Saa 8 Mchana  Gor mahia vs Telecom-Taifa
Saa 10 Jioni     Yanga vs Khartoum-Taifa

Julai 27 Mapumziko
Julai 28-Robo fainali
B1 vs A3
A1 vs Best Looser

Julai 29
B2 vs C2
Ca vs A2

Julai 30-Mapumziko

Julai 31-Nusu Fainali
Winner B2/C2 vs C1/A2
    ""      B1/A3 vs A1/Best Looser
Agosti 01-Mapumziko

Agosti 02-Fainali

Saturday, July 11, 2015

DK SLAA NDIYE MGOMBEA URAIS WA UKAWA

WAKATI CCM ikiendelea na mchakato wake wa kumteua mgombea mmoja wa Urais miongoni mwa wagombea watano waliopitishwa na Kamati Kuu ya chama hicho, Umoja wa Katiba ya Watanzania (UKAWA) wamemaliza udhia kwa kumteua Mgombea wao wa Urais kwa Uchaguzi wa 2015.
.

Baada ya jina la katibu Mkuu wa Chadema Dk Wibroad Slaa likiwa limeteuliwa na UKAWA kuwa mgombea wake wa nafasi ya Urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba.
Dakika chache zilizopita kwenye ukurasa  wa @twitter wa Dr Slaa kathibitisha kuteuliwa na UKAWA.
.

Nashukuru UKAWA kwa imani kubwa. Kazi ya mabadiliko iliyoanza 1992 kwa vyama vingi imebakiza miezi michache kushinda. Kura yako ni ukombozi –  @willibrordslaa
Nashukuru UKAWA kwa imani kubwa. Kazi ya mabadiliko iliyoanza 1992 kwa vyama vingi imebakiza miezi michache kushinda. Kura yako ni ukombozi.

Man United yamtambulisha rasmi Memphis Depay

Meneja wa Manchester United Louis van Gaal Leo huko Old Trafford Jijini Manchester alimtambulisha rasmi Mchezaji mpya Memphis Depay mbele ya Wanahabari katika Mkutano maalum na pia kuthibitisha Mchezaji wa Kimataifa wa Italy Matteo Darmian anaelekea England kukamilisha Uhamisho wake kutoka Torino.
Hata hivyo, Van Gaal alikataa kuzungumza lolote kuhusu habari za kuuzwa kwa Mholanzi mwenzake Robin van Persie kwa Klabu ya Uturuki Fenerbahce.
Akijibu swali kuhusu kuuzwa kwa Van Persie, Van Gaal alisema: "Tukihisi anapaswa kwenda, utasikia toka Manchester United. Kwa sasa bado."
Alipohojiwa kuhusu mipango yao ya Uhamisho na kama inakwenda kama walivyotarajia, Van Gaal alikataa kusema kwa undani na badala yake kueleza: "Huwezi kujibu hilo kwani kununua na kuuza ni kitu kinachoendelea na hatujafika mwisho wake. Mwisho ni Agosti 31. Hatuwezi kusema lolote kuhusu Uhamisho wetu, mikakati yetu kwani nyie mtaandika kila kitu."
Aliongeza: " Manchester United haiwezi kununua kwa sababu ya kununua tu. Ukinunua lazima iwe ni kitu bora kuliko ulichonacho."
Nae Memphis Depay, mwenye Miaka 21 na alienunuliwa Mwezi uliopita kutoka PSV Eindhoven ya Holland Klabu aliyoisaidia kuwa Mabingwa Msimu uliopita huku yeye akiwa ndie Mfungaji Bora wa Ligi, alisisitiza amejiunga na Manchester United ili kutwaa Vikombe vyote vinavyowezekana na yeye atajituma hadi mwisho.
Depay aliongea: "Hii ni Klabu kubwa Duniani na hivyo ni lazima nicheze kwa ajili ya Vikombe. Nimekuja kushinda Vikombe."
Alipoulizwa kuhusu kufanana na Cristiano Ronaldo aliejiunga Man United akiwa na Miaka 18, Depay alieleza: "Sitaki kujifananisha na Mtu kama yeye. Cristiano Ronaldo ni mmoja wa Wachezaji bora Duniani na sitaki kusema sana, nitaachia Miguu yangu iongee!"

Friday, July 10, 2015

Turan ajifunga miaka mitano Barcelona

http://static.sportskeeda.com/wp-content/uploads/2014/02/arda_turan-2116949.jpgKIUNGO wa kimataifa wa Uturuki, Arda Turan amekamilisha usajili wake katika klabu ya Barcelona baada ya kutia saini katika mkataba wa miaka mitano leo. 
Barcelona walikubali kutoa kitita cha Euro Milioni 41 kwa Atletico Madrid kw ajili ya nyota huyo wiki iliyopita. 
Hata hivyo, Turan amesisitiza hana shaka kuhusu uwezekano wa kurejea Atletico kwa muda mpaka Januari pindi Barcelona watakaporuhusiwa kumtumia. Kwa sasa Barcelona wanatumikia adhabu ya kutosajili kwa msimu miwili baada ya kukutwa na hatia ya kukiuka Sheria za Shirikisho la Soka Duniani-FIFA kwa kusajili wachezaji walio chini ya umri wa miaka 18 kinyume cha sheria, adhabu ambayo inaishia Januari mwakani. Mkali huyo ametua akitegemewa kuziba pengo lililoachwa na Xavi aliyekimbilia Umangani.

Man United yamtengea kitita Thomas Muller

http://leadership.ng/wp-content/uploads/2015/07/thomas-muller.jpgBAADA ya kuelekea kumpoteza mshambuliaji wake matata, Robin van Persie, klabu ya Manchester United imepanga kutoa kitika cha pauni Milioni 60 ili kumnasa mshambuliaji wa Kijerumani Thomas Muller.
Muller mwenye umri wa miaka 25 anaichezea klabu ya Bayern Munich na United itamsajili Mjerumani huyo kama mbadala wa RVP ambaye anatarajiwa kuuzwa klabu ya Fenerbahce ya Uturuki. Klabu hiyo ya Uturuki imekubaliana na Mashetani Wekundu kulipa dau la Pauni Milioni 4.7 kama ada ya uhamisho wa RVP ambaye atafanyiwa vipimo vya afya wikiendi hii na kusaini mkataba wa miaka minne ambao utamuwezesha kulipwa mshahara wa Pauni 200,000 kwa wiki. 
Nyota huyo alijiunga na United akitokea Arsenal kwa kitita cha Pauni Milioni 24 Agosti mwaka 2012 na alianza vyema msimu wake wa kwanza akimaliza kama Mfungaji Bora wa EPL wakati taji likienda Old Trafford. 
Lakini Van Persie sasa amepungua makali kutokana na kuwa chini ya kiwango kutokana na majeruhi yaliyomuandama chini ya kocha Louis van Gaal.

Azam yaenda Tanga kutambulisha nyota wake

https://thumbp22-ne1.mail.yahoo.com/tn?sid=2126005954&mid=AL92imIAABY%2FVZ%2BaswTxoL0v9NM&midoffset=2_0_0_1_4179536&partid=11&f=1214&fid=Inbox&m=ThumbnailService&w=3000&h=3000
Wachezaji wakijiandaa na safari kuelekea Tanga
https://thumbp22-ne1.mail.yahoo.com/tn?sid=2126005954&mid=AL92imIAABY%2FVZ%2BaswTxoL0v9NM&midoffset=2_0_0_1_4179536&partid=4&f=1214&fid=Inbox&m=ThumbnailService&w=3000&h=3000
Usiniangushe Migi
https://thumbp22-ne1.mail.yahoo.com/tn?sid=2126005954&mid=AL92imIAABY%2FVZ%2BaswTxoL0v9NM&midoffset=2_0_0_1_4179536&partid=5&f=1214&fid=Inbox&m=ThumbnailService&w=3000&h=3000
Muingereza mwenyewe huyu hapa
https://thumbp22-ne1.mail.yahoo.com/tn?sid=2126005954&mid=AL92imIAABY%2FVZ%2BaswTxoL0v9NM&midoffset=2_0_0_1_4179536&partid=7&f=1214&fid=Inbox&m=ThumbnailService&w=3000&h=3000
Migi akipasha na wenzake mapema leo

KLABU ya Azam ikiwa na nyota kadhaa wa kimataifa akiwamo Jean Baptiste Mugiraneza 'Migi'na Muingereza Ryan Burge imeondoka jijini kuelekea Tanga tayari kwa mechi mbili za kujipima nguvu kujiandaa na Kombe la Kagame litakaloanza wiki ijayo jijini Dar es Salaam.
Azam iliyofanya mazoezi mapema leo asubuhi itashuka dimba la Mkwakwani, Tanga kesho kuumana na Africans Sports kabla ya Jumapili kupepetana na Wagosi wa Kaya kwa mechi ya pili, kisha kurudi Dar kusubiri mechi zake za kundi C katika michuano hiyo ya Kagame itakayomaliza Agosti 2.
Mabingwa wa zamani wa Tanzania wanaenda kunoa makali kabla ya kuja kufanya kweli Dar katika Kagame ambayo inashirikisha timu 13 na Azam imepangwa kundi moja na KCCA ya Uganda, Al Malakia ya Sudan Kusini na Adama City ya Ethiopia.
Katika mechi hizo za wikiendi, Azam itatambulisha nyota wake wapya akiwamo Migi na Burge ambao wapo hatua ya mwisho kutua kwa Matajiri hao wa Tanzania.

Yohan Cabaye arejea England, aitosa PSG

http://e2.365dm.com/14/02/768x432/Yohan-Cabaye-Paris-St-Germain_3076500.jpg?20140201152736
Yohan Cabaye
KIUNGO fundi wa zamani wa Newcastle United, Yohan Cabaye amerejea Ligi Kuu ya England kutoka Ligue 1 ya Ufaransa.
Kiungo huyo amemwaga wino wa kukipiga klabu ya Crystal Palace akitokea PSG ya Ufaransa na kumfanya aungane tena na kocha wake, Alan Pardew. 
Klabu ya Crystal Palace imethibitisha kumsajili kiungo huyo wa kimataifa wa Ufaransa kwa mkataba wa miaka mitatu. 
Inaaminika kuwa Palace imelipa ada ya Pauni milioni 10 kwa ajili ya kumnasa kiungo huyo aliyefanya kazi na Pardew kwa miaka mitatu wakati kocha na yeye wakiwa katika klabu ya Newcastle United. Kipindi akiichezea timu hiyo, Cabaye alikuwa akihesabiwa kama mmoja wa viungo bora katika Ligi Kuu. Kiwango chake hicho ndio kilichangia kwa kiasi kikubwa kuwafanya PSG kutoa karibu pauni milioni 20 kumsajili mapema mwaka jana.

Jordan Henderson rasmi nahodha wa Liverpool, amrithi Gerrard

http://i1.liverpoolecho.co.uk/incoming/article8381445.ece/ALTERNATES/s1227b/Gerrard-Henderson.jpg
Nakukabidhi mikoba, usiniangushe!
WAKATI ikiendelea kumbembeleza nyota wake Raheem Sterling asalie klabuni, Liverpool, imethibitisha Jordan Henderson kuwa nahodha mpya wa timu hiyo akichukua nafasi ya Steven Gerrard aliyeondoka mwishoni mwa msimu uliopita. 
Henderson ambaye amesaini mkataba mpya Aprili mwaka huu, ndio aliyekuwa akipewa nafasi kubwa ya kupewa beji hiyo baada ya Gerrard kuhamia katika klabu ya Los Angeles Galaxy ya Marekani. 
Akihojiwa Henderson amesema siku zote amekuwa akitaka majukumu zaidi hususani katika kipindi hiki cha soka lake. 
Nyota huyo aliendelea kudai kuwa anajiona amekuwa kwasasa na yuko tayari kwa majukumu hayo kwani amejifunza mengi kutoka Gerrard katika kipindi chote ambacho chini yake.

Friday, June 26, 2015

YANGA KUANIKA SILAHA ZAKE MBELE YA WAZIRI PINDA



http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2015/02/Mizengo-Pinda1.jpgSTRAIKA Donald Ngoma wa FC Platinum ya Zimbabwe alitarajiwa kutua nchini jioni ya leo na ilitarajiwa jioni ya kesho angeishuhudia Yanga inayotaka kumsajili ikitambulisha nyota wake wapya katika pambano dhidi ya Sc Villa ya Uganda.
Hata hivyo mchezaji huyo imeshindikana kutua leo, lakini hakuna kilichoharibika kwani Yanga itatambulisha nyota wake wote mbele ya Waziri Mkuu na Mtangaza Nia ya Urais, Mhe. Mizengo Pinda. Waziri Pinda atakuwepo katika pambano hilo ili kubariki silaha hizo mpya za Jangwani wakati wa mchezo huo maalum wa kuchangisha fedha za Ujenzi wa Majengo ya Watoto Wanaoisha katika Mazingira Magumu.
MKurugenzi wa asasi wa Nyumbani Kwanza, Mossy Magere aliiambia MICHARAZO MITUPU kuwa, Yanga itavaana na SC Villa ambapo pia kutakuwa na burudani ya kutosha kwa watakaohudhuria.
Mossy alisema kuwa, Waziri Pinda ndiye mgeni rasmi katika pambano hilo ambalo Yanga watalitumia kutambulisha nyota wake wapya na kusindikizwa na burudani ya muziki toka kwa kundi la Yamoto Band.
"Maandalizi yamekamilika na kwamba wageni mbalimbali tumewaalika, ila Waziri Pinda ndiye atakayekuwa mgeni rasmi na atabariki kikosi hicho cha kocha Hans Pluijm," alisema Mosi.
Mosi alisema kuwa SC Villa walitua juzi jioni wakiwa na kikosi cha wachezaji 18 na viongozi watano na kwamba jana walipasha misuli kwenye Uwanja wa Taifa kabla ya leo kuivaa Yanga.
Yanga ambao imetoka kuichapa Friends Rangers kwa mabao 3-2 katika mechi ya mazoezi, inauchukuliwa kwa uzito mkubwa mchezo huo wa leo kwani ni sehemu ya maandalizi ya ushiriki wao wa michuano ya Kagame na kocha atataka kupima uwezo wa wachezaji wao mbele ya Villa.
Baadhi ya wachezaji wapya wa Yanga ambao watakuwa majaribuni ni Malimi Busungu, Geofrey Mwashiuya na kipa Benedict Tinocco kwani Mwinyi Haji Ngwali na Deus Kaseke wapo kambi ya Taifa Stars kujiandaa na pambano la marudiano la kuwania Chan dhidi ya Uganda The Cranes.
Katibu Mkuu wa Yanga, Dk Jonas Tiboroha alinukuliwa juzi kuwa, huenda akawashtukiza mashabiki wa klabu hiyo katika mchezo huo wa kesho, bila kufafanua lakini imebainika ni kwamba Donald Ngoma alipangwa kuwepo uwanjani kuwashuhudia wenzake kwani angetua nchini ili kumalizana na klabu hiyo.

Jennifer Mgendi kufanya tamasha kubwa Dar Jumapili

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj7CxGiIU1N594esKNg1xe0mepyXDXaYznz92rl6kyK9TGgAbFQXUuEIonXEf3N5HWzU5AqbhmndSU2qveH5Qc0NqREOL9nlP95F4KqStJZMwq-XxH4wfAbnkufcoKfvtHZZh7_jyqffWUi/s1600/MGENDI.JPG
Jennifer Mgendi
MUIMBAJI nyota wa muziki wa Injili ambaye pia ni muigizaji na mtayarishaji wa filamu nchini, Jennifer Mgendi anajiandaa kuifanya tamasha kubwa kwa ajili ya Kumshukuru Mungu kwa kuweza kudumu kwenye fani hizo kwa miaka 20 sasa.
Jennifer alidokeza kuwa Tamasha hilo lililopewa jina la 'Tamasha la Miaka 20 ya Shukrani litafanyika kwenye Kanisa la DCT lililopo Tabata Shule karibu na Kituo cha Polisi Tabata siku ya Jumapili Juni 28 na kusindikizwa na wasanii mbalimbali wa muziki wa Injili nchini.
"Natarajia kufanya tamasha la Shukran ya Miaka 2o, litakalofanyika Juni 28 ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Askofu Mkuu wa TIG, Dk Barnabas Mtokambali na waimbaji mbalimbali watanisindikiza akiwamo Bahati Bukuku, Bonny Mwaitege, Cosmas Chidumule, Ency Mwalukasa, Mchungaji Charles Jangalason na wengineo," alisema Jennifer.
Jennifer alisema ana haki ya kumshukuru Mungu kwa kumwezesha kumpa kipaji na kumwezesha kudumu katika huduma ya uimbaji kwa miaka hiyo yote 20.
Muimbaji huyo kwa sasa anatamba na albamu nane za muziki wa Injili tangu alipojitosa kwenye fani hiyo mwaka 1995 na katika tamasha hilo ataizundua video ya albamu yake inayotamba sasa ya 'WEMA NI AKIBA'.
Mbali na kwenye muziki, Jennifer pia anatamba kwenye filamu akiwa anakimbiza kwa sasa na kazi zake kadhaa ukiwamo 'Teke la Mama', 'Chai Moto', 'Pigo la Faraja', 'Mama Mkwe' na nyinginezo ambazo zimemfanya kuwa matawi ya juu licha ya kwamba hana makeke kama wasanii wengine.

Unyama! Watu 17 wauwawa hotelini

UNYAMA dhidi ya wanadamu umeendelea tena baa da ya Watu wenye silaha wameshambulia hoteli moja ya kitalii iliyoko kwenye pwani ya Tunisia na kuwauwa watu 27.
Maafisa wa serikali ya Tunisia wamesema kuwa mmoja wa washambuliaji hao aliuawa kwa kupigwa risasi na maafisa wa ulinzi na kuwa waliosalia bado wanasakwa na polisi.
Shambulio hilo lilitokea katika mji wa Sousse, ambao huwavutia maelfu ya watalii kutoka bara Ulaya na Afrika ya Kaskazini.
Hili lilikuwa shambulizi la pili dhidi ya hoteli ya watalii nchini Tunisia katika kipindi cha miezi michache iliyopita.
Inaaminika kuwa washambuliaji hao waliwavamia watalii ufukweni.
Mnamo mwezi Machi mwaka huu, wanamgambo wa Kiislamu waliokuwa wamejihami kwa bunduki waliwauawa zaidi ya watu 26 katika makavazi ya Bardo, iliyoko katika mji mkuu wa nchi hiyo Tunis.
Makavazi hayo ya Bardo hilo lilikuwa maarufu sana kwa watalii.
October mwaka wa 2013, mlipuaji wa kujitoa, alijilipua nje ya nyumba moja mjini Sousse, baada ya maafisa wa polisi kutibua jaribio lake la kutaka kuingia ndani na kuishambulia.
BBC

Simba waiwahi TFF kuhusu makocha wa makipa

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi-ErV4LDze29At9zLOJ5-K7zmESxzpny61EoTZ3Oj0BwcGnaHSSYJesvEuGbG8W3_LmcXp-5IKsJPPyMBUZZ6N0_rCe840K_0q4lFxI8OEaEgFOGs4iLDRaMuGeQX20S4EGDP4_CFZ-_A/s1600/Simba+logo+white.jpg
SIMBA wajanja sana, wakati Shirikisho la Mpira wa Mpira wa Miguu nchini (TFF) likitoa agizo na kuvioomba klabu zote zinavyoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom kuwasilisha jina la kocha wa magolikipa kufikia jumatatu ya tarehe 29 Juni, 2015 katika ofisi za TFF, tayari klabu hiyo imeshamleta kocha wake kutoka Kenya, Abdul Salim.
TFF imeandaa kozi ya magolikipa hivyo inahitaji kupata jina la kila kocha wa magolikipa ili kuweza kushiriki kwenye kozi hiyo itakayoanza tarehe 13 - 17 Julai, 2015 jijini Dar es Salaam kwa mpango huo Simba itakuwa imeikatia denge TFF mapema. Coastal Union nayo ilifanya yao mapema juzi baada ya kumsainisha kocha wa zamani wa KCC ya Uganda, Lumu Fred ili kuwanoa makipa wa timu hiyo itakayokuwa chini ya Kocha Mkuu, Jackson Mayanja pia wa Uganda aliyekuwa akiinoa Kagera Sugar katika msimu uliopita.

SITA ZAPANDA DARAJA, MADINI ARUSHA NAO WAMO!

KLABU za Abajalo FC ya Tabora, Alliance FC (Mwanza), Changanyikeni Rangers FC (Dar es Salaam), Coca-Cola Kwanza FC (Mbeya), Madini SC (Arusha), na Sabasaba United FC (Morogoro) ndizo timu zilizopanda kucheza Ligi Daraja la Pili (SDL) msimu wa 2015/2016.
Timu hizo zimepanda daraja baada ya kufanya vizuri kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) iliyomalizika hivi karibuni kwenye vituo vya Lindi, Manyara na Rukwa na kushirikisha jumla ya timu 27.

SDL inayoshirikisha timu 24 zilizogawanywa katika makundi manne inatarajia kuanza kutimua vumbi Oktoba 17 mwaka huu. Ligi hiyo itachezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini, na timu itakayoongoza kundi ndiyo itakayopanda daraja kucheza Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kwa msimu wa 2016/2017.

Kundi A lina timu za Abajalo FC (Tabora), Green Warriors (Dar es Salaam), Milambo FC (Tabora), Mvuvumwa FC (Kigoma), Singida United (Singida) na Transit Camp (Dar es Salaam).

Kundi B lina timu za AFC (Arusha), Alliance FC (Mwanza), Bulyanhulu FC (Shinyanga), JKT Rwamkoma FC (Mara), Madini SC (Arusha) na Pamba SC (Mwanza).

Wakati kundi C lina timu za Abajalo FC (Dar es Salaam), Changanyikeni Rangers FC (Dar es Salaam), Cosmopolitan (Dar es Salaam), Kariakoo FC (Lindi), Mshikamano FC (Dar es Salaam) na Villa Squad (Dar es Salaam).

African Wanderers ya Iringa, Coca-Cola Kwanza FC (Mbeya), Mkamba Rangers (Morogoro), Sabasaba United FC (Morogoro), Town Small Boys (Ruvuma) na Wenda FC ya Mbeya ndizo zinazounda kundi D.

Dirisha la usajili wa wachezaji limeshafunguliwa tangu Juni 15 mwaka huu, na litafungwa Agosti 6 mwaka huu.

TFF yavichimba mkwara vyama vya soka mikoani

KUFUATIA pendekezo la sekretariet ya TFF ambalo baadae lilipitishwa na Mkutano Mkuu wa TFF kila mkoa unatakiwa kuwa na kituo chake cha kulea na kukuza vipaji vya mpira wa vijana umri kuanzia miaka 8-17.

Kwa mikoa ambayo tayari ina kituo ambacho inakiendesha yenyewe TFF inaonba ipatiwe taarifa hiyo ikiwa ni pamoja na kufahamishwa jina la kituo, jina la mwalimu na sifa zake na utaratibu wa mafunzo.

Kwa mikoa ambayo haina kituo TFF inagiza mikoa hiyo kuingia ubia na kituo kimoja ambacho tayari kina program ya kukuza na kuendeleza vipaji ili kijulikane kuwa ni kituo maalum cha mkoa husika.

Katika hilo TFF inaagiza kamati ya utendaji ya mkoa husika iandae muhtasari wa kikao cha utendaji cha chama cha mkoa wa kupitisha maamuzi hayo, MoU (makubaliano rasmi) yasainiwe kati ya chama cha mkoa na kituo husika na hati hiyo nakala yake iletwe TFF.

MoU hiyo ionyeshe majukumu ya chama cha mpira cha mkoa kama kutoa vifaa, kutoa mwalimu, usimamizi nk na pia kuonyesha majukumu ya mwenye kituo kama kutoa uwanja,ulinzi nk. MoU itaonyesha pia nani atafaidika na vipaji vitakavyoibuliwa kati ya mzazi,kituo na chama cha mkoa.

TFF itaandaa MoU ya mfano kwa ajili ya vyama vyote vya mikoa na ingependa kufikia tarehe 31/Desemba/2015 kila mkoa uwe umetekeleza jambo hilo
.

Stars ya Kwanza yaanza kujifua jijini Dar

Kocha wa Stars, Boniface Mkwasa (kulia)
KIKOSI cha timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kinachodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager kimeanza mazoezi leo asubuhi katika uwanja wa Boko Veterani kujiandaa na mchezo wa marudaino kuwania kufuzu kwa CHAN dhidi ya uganda mwishoni mwa wiki ijayo.

Stars inayonolewa na makocha wazawa, Charles Mkwasa na msaidizi wake Hemded Morocco, itakua ikifanya mazoezi asubuhi na jioni katika uwanja huo wa Boko Veterani, huku timu ikiweka kambi yake katika hoteli ya Kiromo mjini Bagamoyo.

Wachezaji wote walioitwa wameripoti kambini tangu jana na leo wamefanya mazoezi asubuhi isipokua Aggrey Morris ambaye ni majeruhi nafasi yake imekuchukuliwa na Vicent Andrew (Mtibwa Sugar) na Jonas Mkude aliyekwenda kufanya majaribio Afrika Kusini nafasi yake ikizibwa na Mudathir Yahya (Azam FC).

TFF yafunga kozi ya Makocha wa Vijana

Viongozi wa TFF, Rais Jamal Malinzi na Katibu Mkuu, Celestine Mwesigwa
SHIRIKISHO la Soka Nchini (TFF) leo limefungua kozi ya makocha wa mpira wa miguu kwa watoto na vijana kwa nchi nzima kwa lengo la kuhakikisha vijana wengi wanapata nafasi ya kufundishwa mpira na kuucheza mpira kuanzia katika umri mdogo.

Akifungua kozi hiyo, Katibu Mkuu wa TFF Mwesigwa Selestine amesema ili nchi/Taifa lifanikiwe katika soka ni lazima kuwekeza katika mpira wa watoto na vijana ambao makocha hao ni sehemu ya uwekezaji huo.

“Tumekua na mashindano ya Taifa U-13, kikosi cha timu ya Taifa ya U-15 ambayo inashirikisha vijana wadogo, vijana hao wanapaswa kupata malezi na mafunzo yenu waalimu ili wafikiapo kuchezea timu za Taifa wawe wamekua kwenye msingi bora wa kuujua mpira wa miguu” alisema Mwesigwa.

Naye mkufunzi wa FIFA wa kozi hiyo ya makocha kutoka nchini Ujerumani, Eric Muller amesema hata ujerumani imefanikiwa baada ya kuwekeza katika soka la vijana, mwaka 2000 kwenye fainali za Euro nchi yao ilishika nafasi ya mwisho katika msimamo kundi lao kwa kupata poniti moja, lakini uwekezaji walioufanya kwenye soka la watoto na vijana umewapelekea kutwaa Ubingwa wa Dunia mwaka 2014.

Washiriki wa kozi hiyo ni makocha wa timu za vijana za mikoa yoye Tanzania, ambao watashirki na timu zao za mikoa katika michuano ya Copa Coca Cola mwaka huu.

Kozi hiyo ya makocha wa timu za watoto/vijana inayoendeshwa na wakufunzi wa FIFA, Ulric Mathews kutoka shelisheli na Eric Muller kutoka nchini Ujerumani itamalizika jumatatu tarehe 29 Juni, 2015
.

Kazi imeanza, makocha Simba watua

Alianza huyu wa Kenya kwanza
Mwishowe wakakutana wote kwa pamoja
KLABU ya Simba imeonyesha haina utani baada ya makocha wake wapya Dylan Kerr kutoka Uingereza na Abdul Salim kutoka Kenya atakayewanoa makipa kutua nchini mchana huu wakitokea makwao.
Makocha hao wamelamba shavu la kuinoa Simba baada ya aliyekuwa kocha wa klabu hiyo, Goran Kopunovic kushindwa kuelewana na uongozi wa Rais Evans Aveva.
Kocha wa kwanza kutua nchini alikuwa Mkenya aliyewahi kuzinoa timu mbalimbali ikiwamo Gor Mahia na AFC Leopard ambaye alitua majira ya saa nane mchana kabla ya Kerry kutua saa 10 kwa Ndege ya Shirika la Emirates.
Makocha hao wametua tayari kuanza yao katika klabu hiyo ambayo kwa miaka mitatu sasa haijaonja taji la Ligi Kuu, huku ikiwa imebadilisha makocha wasiopungua watano tangu walipotwaa taji la mwisho msimu wa 2011-2012 ikiwa chini ya Cirkovic Milovan aliyefurshwa baadaye.
Kikosi cha wachezaji wa Simba kwa sasa wanajifua kwenye Gym ya Chang'ombe kabla ya kuanza rasmi mazoezi yao Julai Mosi ambapo Rais Aveva alidokeza kuwa itakuwa visiwani Zanzibar kwa muda wa majuma sita.
Hata hivyo Simba itaanza kambi hiyo bila baadhi ya nyota wake kadhaa wakiwamo wale waliopo katika kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars inayojiandaa kuifuata Uganda the Cranes katika pambano la marudiano la kuwania fainali za CHAN-2016 zitakazofanyika Rwanda.
Wengine ambao hawatakuwapo ni Jonas Mkude aliyetimkia Afrika Kusini kwa ajili ya kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa katika klabu ya Afrika Kusini, huku Okwi akiwa kwao kwa ajili ya Fungate ya Arusi yao anayofunga kesho kwao Uganda na Raphael Kwireza akiwa amepewa mapumziko ya mwezi mmoja kusikilia majereha yake yanayomtibulia kukipiga Msimbazi licha ya kuwa na mkataba wa miaka miwili unaomalizika mwakani.