STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, May 11, 2015

Mbeya City yawatunuku nyota wake, kocha Mwambusi

IMG-20150510-WA0010KLABU ya Mbeya City imewapa tuzo wachezaji wake pamoja na Kocha Juma Mwambusi kwa kuiwezesha timu hiyo kukamata nafasi ya nne katika Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2014-2015.
Tuzio hizo zilitolewa mara baada ya mchezo wao wa mwisho wa Ligi Kuu kati yao ya Polisi Moro ambapo Mbeya iliibuka washindi wa bao 1-0.
Kwenye tuzo hizo Kocha mkuu Juma Mwambusi alipata tuzo kama kocha mwenye mafanikio makubwa ndani ya kikosi cha city na ligi kwa ujumla Paul Nonga, Deus Kaseke, Themi Felix walipata tuzo ya heshima kwa kufanya vizuri misimu miwili  Rafael Alfa na Kenny Ally walipata tuzo ya  wachezaji chipukizi waliofanikiwa Haningtony Kalyusubula alipata tuzo ya  mlinda lango bora  na Juma Nyosso, Hassan Mwasapili na Peter Mwalyanzi walipata tuzo ya uchezaji bora
IMG-20150510-WA0009
Halikadhalika wachezaji wengine 18 nao walipata zawadi  ikumbukwe kuwa zawadi na tuzo hizo walizopata wachezaji wa City zimeambatana na bahasha iliyonona vizuri kutoka uongozi na mashabiki wa Mccfc.

IMG-20150510-WA0004
Hanington Kalyesubula akipokea tuzo

Carlo Ancelotti ajipa matumaini kwa Juventus

http://i.telegraph.co.uk/multimedia/archive/02921/ancelotti_2921770b.jpgMENEJA wa klabu ya Real Madrid, Carlo Ancelotti anaamini kikosi chake kinaweza kugeuza matokeo ya mabao 2-1 waliyochapwa na Juventus na kutinga hatua fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Pamoja na kutoka sare ya mabao 2-2 katika mchezo wa La Liga dhidi ya Valencia juzi. Mabingwa hao wa Ulaya sasa wako nyuma ya vinara Barcelona kwa alama nne huku kukiwa kumebaki michezo miwili katika ligi. 
Akihojiwa kocha Ancelotti amesema wanahitaji kuwa mawazo chanya na kuthamini jinsi walivyocheza vyema katika mchezo huo. 
Kocha huyo aliendelea kudai kuwa makosa madogo madogo ndio yaliyowagharimu, lakini wanahitaji kutulia na kujiandaa kwa ajili ya mchezo wao wa keshokutwa (Jumatano) dhidi ya Juventus.
Katika mfululizo wa michuano hiyo kesho Jumanne, Bayern Munich watakuwa nyumbani Alliaz Arena ikli kubadilisha matokeo ya mabao 3-0 iliyonyukwa katika mechi ya wiki iliyopita nchini Hispania.

Moyes anogewa La Liga, azipotezea klabu za EPL

http://img.thesun.co.uk/aidemitlum/archive/01727/moyes_1727193a.jpgAMENOGEWA! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya Meneja wa klabu ya Real Sociedad, David Moyes amezipasha klabu za Ligi Kuu zinazomuwinda kuwa hana mpango wa kwenda popote kufuatia tetesi kuwa atarejea nchini Uingereza. 
Kocha huyo raia wa Scotland alitimuliwa na Manchester United baada ya kuinoa katika kipindi cha miezi 10, Novemba mwaka jana kutokana na klabu hiyo kutofurahishwa na matokeo. 
Moyes alirejea tena uwanjani akiwa kocha wa klabu hiyo katika  mazingira ambayo alikuwa hana mazoea nayo katika Ligi Kuu ya Hispania. 
Wiki za karibuni kumezuka tetesi kuwa klabu za West Ham United na Newcastle United zimekuwa zikitaka saini yake, lakini mwenyewe amedai hana mpango wa kuondoka Hispania kwa sasa. 
Akihojiwa Moyes amesema kwa sasa anataka kuimarisha kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao, jambo ambalo amefikia hatua nzuri hivyo hawezi kuacha mpaka azma yake itimie.

Maskini Dk Ndumbaro, TFF yakomaa naye!

http://static.goal.com/401800/401857_heroa.jpgNa Rahim Junior
TUMAINI la Mjumbe wa Bodi ya Ligi na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa klabu ya Simba, Dk Damas Ndumbaro kutoka kifungoni, limefifia baada ya Kamati ya Rufaa ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutupilia mbali rufaa yake.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Mwenyekiti wa Kamati ya Rufaa ya Nidhamu ya TFF, Revocatus Kuuli, inasema kwa maamuzi hayo yaliyofikiwa kwa turufu ya kura, ambapo wajumbe watatu waliafiki kupiga chini hoja za mrufani na mmoja kukubaliana naye ni kwamba, Ndumbaro ataendelea kutumikia adhabu yake kutojihusha na michezo kwa muda wa miaka saba.
Dk Ndumbaro alikata rufaa katika kamati hiyo kupinga maamuzi ya Kamati ya nidhamu iliyomkuta na hatia kwa kitendo chake cha kupinga maamuzi ya TFF ya kutaka klabu za Ligi Kuu kukatwa asimilia tano za fedha za wadhamini na kumtia kifungoni Oktoba mwaka jana.
Hata hivyo kwa mujibu wa taarifa hizo za TFF ni kwamba baada ya mahojiano kati ya mrufani Dk Damas Ndumbaro na Wakili wa TFF, Emmanuel Muga, pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Rufaa ya Nidhamu iliamuriwa kutupiliwa mbali kwa hoja za mrufani kwa maamuzi ya kura 3-1.
"Kwa uamuzi huu kamati inadhibitisha uamuzi wa Kamati ya Nidhamu iliyosomwa Oktoba 13, 2014 uamuzi huu umefikiwa baada ya wajumbe kupiga kura na uamuzi kupitishwa kwa wingi wa kura za wajumbe watatu, dhidi ya mjumbe mmoja wa kamati hii kwa hoja ya 2,3 na 4 na wajumbe wote 4 walikubaliana kutupiliwa mbali hoja ya kwanza.
"Kwa hiyo Dk Damas Ndumbaro ataendelea kutumikia adhabu yake kwa kutojihusisha na shughuli yoyote ya Mpira wa Miguu (Soka) kwa kipindi cha miaka saba.
"Hata hivyo mrufani Dr Damas Ndumbaro anayohaki ndani ya siku 10 kuanzia leo Mei 10,2015 ya kuomba marejeo ya uamuzi huu mbele ya kamati ya Rufaa ya Nidhamu ya TFF chini ya Ibara 142 ya kanuni za nidhamu za TFF ya mwaka. " sehemu ya taraifa hiyo inasomeka hivyo.
Ebu isome taarifa hiyo ya Kamati ya Rufaa ya Nidhamu:


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAREHE 11 MEI 2015
 

  MAAMUZI YA KAMATI YA RUFAA YA NIDHAMU
BAADA ya mahojiano kati ya mrufani Dr Damas Ndumbaro na Wakili wa TFF     Nd Emmanuel Muga, pamoja na Wajumbe wa Kamati ya rufaa ya nidhamu kuwahoji wote, Mrufani na Wakili wa TFF, Kamati ya rufaa ya nidhamu ilichukua uamuzi ufuatao:-
Hoja ya kwanza cha rufaa, kwamba kamati ya nidhamu haikuwa na nguvu za kisheria kusikiliza shauri lake, Kamati ya rufaa ya nidhamu baada kusikiliza hoja za pande zote mbili, kwa uamuzi wa Wajumbe wote kwa maana ya kuwa zote nne za Wajjumbe wa kamati ya rufaa ya nidhamu, ilitupilia mbali hoja hiyo na kuona kwamba kamati ilikuwa na mamlaka ya kusikiliza shauri hilo kwa kuwa mkata rufaa ni afisa wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF kwa mujibu wa Katiba ya TFF ya 2013. Uamuzi katika hoja hii uliamuliwa kwa kura 3 dhidi ya moja.
Hoja ya pili inayosema kwamba kamati ilikosea kisheria kwa kutompa muda wa kuleta utetezi wake wala vielelezo vyovyote vile kwenye shauri lake.
Kamati ya rufaa ya Nidhamu kwenye Shauri hili, baada ya kufanya maamuzi kwa kupiga kura, kura za Wajumbe watatu zilitupiliwa mbali hoja yake na kura moja kati ya kura nne ilikubaliana na hoja yake kwa uamuzi huo, kamati ya rufani ya nidhamu ilitupilia mbali hoja hiyo kwa uamuzi wa wingi wa kura kwa maana ya kuwa tatu dhidi ya kura moja.
Sababu za kutupilia mbali hoja hizo ni kwamba mrufani alipata wito wa kwenda kwenye shauri, na akawakilishwa na wakili wake ( Nestory Peter Wandiba ) kwenye Shauri hilo. Shauri liliposikilizwa kwa mara ya kwanza tarehe 10/10.2014 shauri lilipangwa kusikilizwa tarehe 11/10/2014 Lakini siku hiyo ya pili si wakili wala Dr Ndumbaro alifika kwenye shauri hilo kwa maana hiyo basi shauri lililazimika kusilikizwa upande mmoja kwa mujibu wa kanuni za nidhamu za TFF ibara ya 94 (3).
    3. Hoja ya tatu linalosema kwamba kamati ilikosea kusiliza shauri upande mmoja bila ya mtuhumiwa kuwepo, ni kukiuka haki yake ya msingi ya  kusikilizwa.
    Kamati baada ya kusikiliza utetezi kutoka pande zote mbili kamati ilifanya uamuzi kwa kupiga kura, na kura tatu (wajumbe watatu) walitupilia mbali hoja hiyo, dhidi ya kura moja (mjumbe mmoja) aliyeikubali hoja hiyo. Sababu za kutupilia mbali hoja hiyo ni kutokana na ukweli kwamba mrufani alipata wito wa kuhudhuria shauri hili na akamtuma wakili wake, lakini mrufani alishindwa kuonyesha vielelezo vya kuonyesha kwamba angesafiri kwenda nje ya nchi ili kamati ya nidhamu iweze kuahirisha shauri mpaka wakati ambao angekuwa amerejea lakini hakufanya hivyo.
   Hata hivyo kwa mujibu wa Ibara 144(2) (3) za kanuni ya nidhamu za TFF, mrufani  angeweza pia kuomba kamati ya nidhamu ibatilishe uamuzi iliyoutoa dhidi yake ili aweze kusikilizwa utetezi wake pia hakufanya hivyo na aliamua kukata rufaa.
    4. Hoja ya nne inayosema kwamba kamati ilikosea kisheria katika uchambuzi wa ushahidi wa mlalamikaji na hatimaye kutoa uamuzi uliomtia hatiani.
    Kamati ya rufani ya nidhamu ilisikiliza kwa umakini hoja za pande zote mbili na kujiridhisha kwamba mrufani alifanya makosa kwa kutoa taarifa isiyosahihi na kupotosha maamuzi ya TFF kinyume na kanuni ya 41 (6) ya kanuni za ligi kuu ya Tanzania toleo la 2014 (4) na pia kushawishi, kupotosha au kuzuia maamuzi/utekelezaji wa maamuzi ya TFF kinyume na kanuni ya 41(16) ya kanuni za ligi kuu za Tanzania ya (2014).
    Wakati wa kufanya maamuzi, wajumbe watatu(3) kwa maana ya kura tatu zilitupilia mbali hoja hiyo, na kura moja, kwa maana ya mjumbe mmoja alikubaliana na hoja hiyo. Kwa maana hiyo, kamati ya rufaa ya nidhamu ya TFF imetupilia mbali hoja hiyo.
    Kwa uamuzi huu kamati inadhibitisha uamuzi wa kamati ya nidhamu iliyosomwa tarehe 13/10/2014, uamuzi huu umefikiwa baada ya wajumbe kupiga kura na uamuzi kupitishwa kwa wingi wa kura za wajumbe watatu, dhidi ya mjumbe mmoja wa kamati hii kwa hoja ya 2,3 na 4 na wajumbe wote 4 walikubaliana kutupiliwa mbali hoja ya kwanza.
    Kwa hiyo Dr Damas Ndumbaro ataendelea kutumikia adhabu yake kwa kutojihusisha na shughuli yoyote ya Mpira wa Miguu (Soka) kwa kipindi cha miaka saba.
    Hata hivyo mrufani Dr Damas Ndumbaro anayohaki ndani ya siku 10 kuanzia leo tarehe 10/05/2015 ya kuomba marejeo ya uamuzi huu mbele ya kamati ya Rufaa ya Nidhamu ya TFF chini ya Ibara 142 ya kanuni za nidhamu za TFF ya mwaka.
    Kila upande utabeba gharama zake Hukumu inasomwa leo tarehe 10/05/2015/
Revocatus L. K. Kuuli.
MAKAMU MWENYEKITI.
IMETOLEWA NA TFF

Sunday, May 10, 2015

Rasmi Kagame Cup kupigwa Dar kuanzia Julai 11-Agosti 02

http://www.bongo5.com/wp-content/uploads/2012/07/kagame-cup-2012.jpeg 
HATIMAYE imefahamika kuwa, michuano ya Kombe la Kagame kusaka Bingwa wa Afrika Mashariki na Kati kwa ngazi za klabu itapigwa Tanzania.
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limekubali kuwa wenyeji wa michuano ya Kombe la Kagame baada ya kutafakari kwa kina.
Baraza la Vyama vya Soka kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) waliiteua Tanzania kuandaa michuano hiyo, lakini uongozi wa TFF, ulisema ungekutana kujadili kabla ya kutoa tamko.
Hata hivyo kwa mujibu wa taarifa ya shirikisho hilo ilitolewa jana kwa vyombo vya habari TFF imethibitisha kuwa wamekubali kuandaa michuano hiyo na kutangaza kwamba itaanza kutimua vumbi lake kuanzia Julai 11 na kufikia tamati Agosti 2, mwaka huu.
TFF imeweka bayana kwamba Cecafa ndiyo itakayotangaza timu shiriki pamoja na ratiba nzima ya michuano hiyo ambayo mara ya mwisho kufanyika Tanzania ilikuwa mwaka 2012 ambapo Yanga ilitwaa taji kwa mara ya pili mfululizo kwa kuilaza Azam katika fainali iliyopigwa Uwanja wa Taifa. Mwaka mmoja nyuma yaani 2011 Yanga ilitwaa tena taji michuano ilipochezwa jijini Dar es Salaam kwa kuilaza Simba bao 1-0.
Bingwa mtetezi wa michuano hiyo kwa sasa ni wababe wa Azam, El Merreikh ya Sudan ambao walitwaa taji katika fainali zilizochezwa mwaka jana mjiji Kigali, Rwanda baada ya kuilaza APR bao 1-0.

Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika haya hapa

http://45minites.com/wp-content/uploads/2015/02/ES-Setif.png
Watetezi wamewekwa kundi B

http://www.nationalswitchng.com/wp-content/uploads/2015/01/caf-CHAMPIONS-LEAGUE_1.jpg
Kundi A: Smouha (Misri), Moghreb Tetouan (Morocco), TP Mazembe Englebert (DR Kongo) na Al Hilal (Sudan).

Kundi B: Entente Setif (Algeria, mabingwa watetezi), USM Alger (Algeria), Al Merreikh (Sudan), MC Eulma (Algeria)

Mwanariadha Afa kwa Sumu India, wengine taaban

http://i.ndtvimg.com/i/2015-05/kerala-suicide_650x400_61431019961.jpgNEW DELHI, India
POLISI wa nchini India wanachunguza kifo cha mwanariadha wa kike mwenye umri wa miaka 15 na wengine watatu wakinusurika kifo baada ya kula kile kinachodaiwa matunda yaliyowekwa sumu, alisema waziri.

Ilielezwa kuwa wanariadha 10 walikula `othalanga’ matunda pori, ambayo yaliwekwa katika vifungashio vyenye sumu katika kituo hicho cha michezo huko Alappuzha kusini ya jimbo la Kerala kinachoendeshwa na Mamlaka ya Michezo India (SAI).

Wanariadha hao walikutwa wakiwa wamepoteza fahamu katika hosteli yaol Jumatano jioni na walikimbishwa hospitalini ambako mmoja wao alifariki dunia huku wengine watatu wakiwa katika hali mbaya.

Wote wanne inaaminika kuwa walisaini taarifa ya kifo, walisema viongozi hao, lakini hakuna taarifa zaidi zilizotolewa kuhusu barua hiyo.

Walisema ni mapema mno kuhisi kuhusu kifo cha wanariadha hao chipukizi waliokuwa wakifanya mazoezi lakini ndugu wa waathirika hao walisema kuwa wasichana hao walikuwa wameathirika kiakili kutokana na kusumbuliwa na wanariadha wakubwa na makocha katika kituo hicho.

Waziri wa Vijana na Michezo Sarbananda Sonowal alisema polisi wanachunguza na Mkurugenzi Mkuu wa SAI alikuwa akiongoza taasisi hiyo pia.

"Sheria itachukua mkondo wake, lakini nakuhakikishia kuwa kama kuna mtu yoyote kutoka katika mamlaka ya michezo nchini India atapatikana na hatia kuhusiana na suala hili, atachukuliwa hatua za kisheria mara moja," alisema Sonowal katika taarifa yake.

Mkurugenzi Mkuu wa SAI Injeti Srinivas aliwaambia waandishi wa habari kuwa "ni tukio la kushtua sana ".

"Wasichana wanne walijaribu kujiua. Sasa tunataka kuwapatia vifaa vya bora vya afya, " alisema.

Rais TFF awapo pole wahanga wa mafuriko

http://shaffihdauda.co.tz/wp-content/uploads/2015/04/malinzi11.jpg
Rais wa TFF, Jamal Malinzi
Na Rahma White
RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ametuma salamu za pole kwa wakazi wa Dar es salaam na hasa wale walioathirika na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es salaam kwa siku ya tatu mfululizo sasa.
Katika salamu zake kupitia kwa Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Mecky Sadik, Malinzi amesema familia zimepoteza makazi, miundombinu ya usafiri na michezo imeharibika na hata kuwa katika hali ya kutotumika, wanawake watoto, familia, shughuli za kiuchumi na kimichezo zimeathirika na mvua hizi.
TFF inaunga mkono juhudi za Mkuu wa Mkoa Dar es salaam, Serikali na wadau wote wanaoshugulika  kupunguza makali ya janga hili.

Polisi Moro, Masau Bwire warudi Ligi Daraja la Kwanza

Mbeya City wamemaliza kwa ushindi nyumbani dhidi ya Polisi

Polisi wameenda na maji

Yanga walioendelea kutoa takrima kwa timu pinzani
 
Azam walimaliza kwa kishindo nyumbani

JKT Ruvu licha ya kichaapo cha Simba wamenusuurika kushuka draja

Ndanda wamepona baada ya kuilaza Yanga
Simba waliomaliza ligi kwa kishindo kwa kuiparua JKT Ruvu

Prisons wameponea chupuchupu
Mtibwa wamemaliza kwa kichapo nyumbani mbele ya Coastal Union
PAZIA la Ligi Kuu ya Tanzania Bara limehitimishwa kwa michezo saba na kushuhudiwa timu za Polisi Moro na Ruvu Shooting ya Msemaji mwenye tambo nyingi, Masau Bwire wakishuka daraja kwenda FDL.

Ruvu inayonolewa na kocha Mkenya Tom Olaba ilikuwa ugenini Uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga na kujikuta ikipokea kipigo cha bao 1-0 na wenyeji wao Stand United ambayo ushindi huo umeifanya kufikisha pointi 31 katika nafasi ya 10.

Polisi Moro iliyopanda kucheza Ligi Kuu msimu huu, ilikubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Mbeya City na kujikuta ikirudi ilipotoka na hiyo inatokana na mwenendo wa kusuasua tangu kuanza kwa msimu huu ikiwemo uongozi kubadilisha makocha mara kwa mara.

Polisi Moro ndiyo timu pekee msimu huu ambayo imefundishwa na makocha watatu, ilianza na Adolf Rishard 'Adolf' kisha ikamfukuza na kumchukua Amri Said, ambaye naye aliamua kujiondoa na nafasi yake kuchukuliwa na John Tamba, lakini hadi siku jana walijikuta wakiburuza mkia wakiwa na pointi zao 25 katika mechi 26 walizocheza.
Katika uwanja wa Nang'wanda Sijaona mkoani Mtwara, Mabingwa wapya wa msimu huu Yanga waliendelea kuonja shubiri baada ya kupoteza mchezo huo kwa kufungwa bao 1-0 na wenyeji Ndanda FC, Wakati kwenye Uwanja wa Azam Complex wenyeji Azam walitoka sare ya bila kufungana na Mgambo JKT ya Tanga.
Kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kocha, Mbwana Makatta, alifanikiwa kuiokoa timu ya Tanzania Prisons isishuke daraja msimu huu baada ya kuilazimisha sare ya bila kufungana na Kagera Sugar aliyomaliza nafasi ya sita ikiwa na pointi 32, huku sare hiyo ikiwasaidia maafande hao kufikisha pointi 29 na kuepuka janga la kurudi kushuka daraja la kwanza msimu ujao.
Katika uwanja wa Manungu Turiani, Mtibwa Sugar ililala nyumbani kwa kufungwa mabao 2-1 na Coastal Union ya Tanga na matokeo hayo kuifanya timu hiyo iliyokuwa na kipindi kigumu licha ya kunza msimu huu vizuri kumaliza nafasi ya saba msimu huu ikiwa na pointi 31 huku Wagosi wa Kaya wakimaliza nafasi ya tano wakiwa na pointi 34.
Msimamo wa mwisho wa Ligi Kuu ya Bara:
                      P    W    D    L    F     A    Pts

1. Yanga         26  17    4    5    52   18   55
2. Azam         26   13   10   3    36   18   49

3. Simba        26   13    8    5    38   19   47
4.  Mbeya City26    8    10   8    22    22  34
5.  Coastal     26    8    10   8    21    25   34
6.Kagera        26    8     8   10   22    26   32
7. Mtibwa       26    7    10   9    25    25   31
8. JKT Ruvu    26    8    7    11   20    25   31
9. Ndanda      26    8    7    11    21   29   31
10.Stand        26    8    7    11    23   34   31
11. Prisons     26    5   14    7    18    22   29
12. Mgambo   26    8    5    13   18    28   29
13. Ruvu        26    7    8    11   16    29   29
14. Polisi Moro26    5   10   11   16    27   25

Matokeo:
JKT Ruvu       v  Simba            (1-2)
Mtibwa Sugar v  Coastal Union (1-2)
Stand Utd      v  Ruvu Shooting(1-0)
Mbeya City     v  Polisi Moro     (1-0)
Kagera Sugar v  Prisons          (0-0)
Ndanda          v  Yanga           (1-0)
Azam             v  Mgambo JKT  (0-0)

WAFUNGAJI:
17- Simon Msuva                                (Yanga)
14- Amissi Tambwe                             (Yanga)
11- Abaslim Chiidiebele               (Stand Utd)
10-Didier Kavumbagu                         (Azam)
     Rashid Mandawa              (Kagera Sugar)
     Emmanuel Okwi                             (Simba)
9- Malimi Busungu                         (Mgambo)
8- Samuel Kamuntu                      (JKT Ruvu)
    Ibrahim Ajibu                                  (Simba)
    Ame Ali                                         (Mtibwa)  
 7-Rama Salim                                   (Coastal)
6- Kipre Tchetche                                (Azam)
    Danny Mrwanda                             (Yanga)
    Heri Mohammed                             (Stand)
5- Jacob Massawe                           (Ndanda)
    Yahya Tumbo                                    (Ruvu)
    Atupele Green                               (Kagera)
    Mussa Mgosi                                (Mtibwa)
    Nassor Kapama                            (Ndanda)
4- Ally Shomari                                 (Mtibwa)
    Themi Felix                             (Mbeya City)
    Said Bahanuzi                        (Polisi Moro)
    Frank Domayo                                 (Azam)
    Mrisho Ngassa                                (Yanga)
    Kpah Sherman                                (Yanga)
    Gaudence Mwaikimba                   (Azam)
    Andrey Coutinho                           (Yanga)
    Ramadhani Singano                      (Simba)
3- Dan Sserunkuma                            (Simba)
    Elias Maguli                                     (Simba)
    Ally Nassor                                 (Mgambo)
    Raphael Alpha                       (Mbeya City)
    Aggrey Morris                                  (Azam)
    Paul Nonga                             (Mbeya City) 

NB:WAKILISHI WA NCHI, ZILIZOSHUKA DARAJA

Chelsea kupeleka taji laao la ubingwa Thailand

http://soccerblitz.net/wp-content/uploads/2015/03/chelseaWinCapitalOneCup15_large.jpg
Chelsea walipotwaa taji lao la Kombe la Ligi (Capital One)

WAKATI leo wakiwa nyumbani kukabiliana na Liverpool, Mabingwa wapya wa England, Chelsea inatarajiwa kwenda kulitambulisha taji lao nchini Thailand.
Chelsea wamejumuisha katika ratiba yao kuwa Mei 30 wataenda jijini Bangkok, Thailand na kucheza na nyota wa soka wa Thailand. 
Chelsea ambao wamewahi kwenda kucheza mechi za kirafiki nchini Thailand mwaka 2011 na 2013, wanatarajiwa kucheza mchezo huo katika Uwanja wa Rajamangala kabla ya kupaa kuelekea Australia kuchukuana na Sydney FC Juni 2 mwaka huu. Chelsea pia watacheza michuano ya Kombe la Kimataifa nchini Marekani dhidi ya timu za New York Red Bulls, Paris Saint-Germain na Barcelona Julai. Waratibu wa mchezo huo huko Bangkok wamedai kuwa utakuwa mahsusi kuadhimisha miaka 88 ya kuzaliwa mfalme wa Thailand. Chelsea leo watakuwa kwenye uwanja wao wa Stamford Bridge kuwakaribisha vijogoo vya Anfield katika mfululizo wa Ligi Kuu ya England. Mechi hiyo ni muhimu zaidi kwa Liverpool wanaowania nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya mwakani, fursa hiyo imekuja baada ya Soothampton na Tottenham Hotspur kuchemsha katika mechi zao za wikiendi hii kwa kupokea vipigo.

Kibaka amliza Benni McCarthy, ampora kila kitu akiwa saluni

http://3.bp.blogspot.com/-YGgvai_tplY/Tv8nwIMi6YI/AAAAAAAAMrk/8yk4O-snDNU/s1600/32832.jpg

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Afrika Kusini, Benni McCarthy ameporwa na mtu mwenye silaha wakati akiwa saluni ya kunyoa nywele jijini Johannesburg, Afrika Kusini. 
Wakala wa McCarthy, Percy Adams amesema mteja wake huyo alikumbwa na kadhia hiyo akiwa saluni hapo na kuporwa vitu vyake kadhaa vya thamani ikiwemo saa, hereni na pete yake ya ndoa. 
Adams aliendelea kudai kuwa katika tukio hilo hakuna aliyejeruhiwa na wateja wengine waliokuwemo hawakuguswa zaidi ya McCarthy peke yake. 
McCarthy mwenye umri wa miaka 37, amewahi kushinda taji la michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na klabu ya FC Porto ya Ureno huku akishikilia rekodi ya kufunga mabao mengi katika timu yake ya taifa ya Bafana Bafana akiwa na mabao 32. 
Matukio ya uporaji wa kutumia sialaha yanaonekana kuwa ya kawaida nchini humo baada ya golikipa na nahodha wa Bafana Bafana kuuawa mwaka jana katika tukio kama hilo la uporaji akiwa nyumbani.

Yathibitika Yaya Toure kutimka Manchester City

http://www.standard.co.uk/incoming/article9842399.ece/binary/original/Yaya%20Toure.jpg
Yaya Toure anayesemekana anatarajiwa kuikacha Man City kwenda Inter Milan
WAKALA wa kiungo Yaya Toure amedai kuwa ana uhakika wa asilimia 90i kuwa mteja wake huyo ataondoka katika majira ya kiangazi. 
Aprili, Toure ambaye amebakisha mkataba wa miaka miwili ambao unamuingizia kitita cha Euro 265,000 kwa wiki, alikuwa akitaka kufanya mazungumzo na maofisa wa City kuhusiana uhamisho katika majira ya kiangazi. 
Meneja wa Inter Milan, Roberto Mancini ameonyesha nia ya wazi ya kutaka kumsajili kiungo huyo ambaye anatimiza miaka 32 Mei 13, na wakala wake Dimitri Seluk amekiri kuna uwezekano mkubwa wa kuondoka City. 
Seluk amesema ingawa hakuna kilichoamuliwa mpaka sasa lakini ana uhakika wa asilimia 90 kuwa mteja wake anaweza kuondoka katika timu hiyo majira ya kiangazi. 
Toure alijiunga na City akitokea Barcelona mwaka 2010 na amefanikiwa kushinda mataji mawili ya Ligi Kuu na moja la Kombe la FA, pia taji la Mataifa ya Afrika akiwa na timu yake ya taifa ya Iviry Coast mapema mwaka huu.

Ngumi kupigwa mjini Bagamoyo, Super D kugawa vifaa kwa wakali

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiQeWrEKx0_mnCSl1J8PJPUA6_zw9p_yAOeZomH3PlujJqmd-14VYhlB3pKSf7PHU9eX1DZtKUMI9cS9-QGU2VjQhu79Pbzw72lNYISSHPE4Pp4xjpa8cUno_Tb72KVlAzOr64GIftMRVk/s1600/10702151_751229401589872_1190688698899816254_n.jpg
Super D akionyesha baadhi ya DVD anazosambaza kwa ajili ya kutoa mafunzo ya ngumi,
Na Rahim Kimwaga
NDONGA zinatarajiwa kupigwa mjini Bagamoyo wakati mabondia Idd Pialali wa Kiwangwa atakapopanda ulingoni kuzipiga na Adam Ngange wa Chanika katika pambano liotakalochezwa Mei 16.
Mpambano huo utapigwa kwenye ukumbi wa Che kwa Che, uliopo mjini humo na tyari kila bondia ameanza tambo akijigamba kuibuka na ushindi siku hiyo.
Mbali na pambano hilo lililoandaliwa na kampuni ya Sharrif Promotion, pia siku hiyo kutakuwa na mapambano mengine kadhaa ya utangulizi yatakayowahusisha mabondia machachari.
Kwa mujibu wa mratibu huyo mabondia watakaowasindikiza Pialali na Ngange ni pamoja na lile litakalowakutanisha Rashidi Haruna dhidi ya Kaminja Ramadhani.
Michezo mingine ni kati ya Halid Hongo atakayebiliana na Kishoki Mbish, huku Abdallah Samata atazidunda na Maono Alli 
Mgeni rasmi katika pambano hilo ambalo viiongilio vyake vinaanzia Sh. 5000 kwa viti vya kawaida na Sh. 8000 kwa V.I.P atakuwa ni bodnia Cosmas Cheka, mdogo wa bingwa wa zamani wa dunia wa WBF, Francis Cheka 'SMG'.
Pia katika mipambano hilo, kutakuwa na upatikanaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Floyd Mayweathar vs Manny Paquaio 2015 , Saul 'canelo' Alverez, Mike 'Iron' Tyson, Muhammad Ali, Felix Trinidad, Miguel Cotto na wengine wengi, huku vifaa vya mchezo vitagawiwa na kocha  Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine vitauzwa kwa gharama nafuu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha mchezo wa masumbwi nchini.

Kampuni ya Bima ya UAP yatoa elimu kwa wakulima Kanda ya Ziwa

Picha tofauti zinaoonyesha  Pamba zilizokuwa zimehifadhiwa katika ghla na kuungua na chini ni maafisa wa kampuni ya Bima UAP wakiwa na Meneja wa Kiwanda cha JIELONG Holdings Tanzania LTD Kiki Huwa Xu (kushoto).

Na Renatha Msungu
WANANCHI wa mkoa wa Shinyanga wamenufaika na elimu ya kutunza maghala ya chakula na pamba iliotolewa na kampuni ya bima ya UAP kwa ajili ya
kuzuia wasipatwe na majanga ya moto.
Elimu hiyo imetolewa kwa wakazi wa mkoa huo, baada ya mmiliki wa ghala la Jielong Holdings, Kiki Jielong kuunguliwa na ghala lake la pamba
lililopo nje kidogo ya mji wa Shinyanga, kwenye hafla ya kukabidhi hundi kwa ajii ya fidia hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Shinyanga jana, Meneja Maendeleo wa biashara wa UAP Raymond Komanga, alisema hii ni moja ya
faida ya kujiunga na bima ya nyumba ambayo inasaidia kutoa fidia ya hasara inayopatikana kwenye maghala kama hilo la Jielong.
Komanga alisema kutokana na hilo wameamua kutoa elimu kwa wafanya biashara na wamiliki wa maghala mkoani humo ili waweze kujikinga na athari ambazo  zinaweza kutokea wakati wowote.
Alisema wamekuwa wakipata kesi nyingi za aina hiyo na kuzitatua tu kwa wale ambao wamejiunga na bima kwa ajili ya kujikinga na majanga yanayotokea katika sehemu zao za kazi.
Alisema wameanza mkoani Shinyanga na wataendelea katika mikoa mingine ili kutoa elimu ya kujikinga na majanga mbalimbali ya moto na mengine yanayowatokea kila kukicha.
Alisema wananchi wengi hawajakata bima jambo ambalo linawapa shida mara baada ya kupata matatizo ya kuunguliwa na nyumba na kushindwa
kuzirejesha kwa wakati.
Kwa upande wake mmiliki wa ghala hilo na ambaye ni meneja Utawala wa kampuni ya Jielong, alisema wanaishkuru UAP kutokana na kuwarejeshea
fedha hizo haraka baada ya kupata ajali hiyo ya moto katika ghala lao.
Alisema wao ni wanachama wa muda mfupi lakini walipotoa taarifa mara moja watu wa bima walijitokeza na kuwasaidia kufidia gharama
zilizoungua katika ghala hilo la kuhifadhia pamba.
Akielezea chanzo cha moto ndani ya ghala hilo alisema umetokana na joto la ndani ya ghala baada ya bidhaa zilizopo ndani kubanana na kukosa hewa na kusababisha pamba kuwaka moto.
Alisema moto huo ulisambaa kwa kasi kubwa kutokana na kwamba pamba inashika moto kwa haraka kuliko kitu kingine.
Alisema anawashauri wafanya biashara ambao hawajakata bima wajitokeze kwenda kukata bima hiyo kwa kuwa ina manufaa makubwa sana, hasa wakati wa matatizo.
Meneja madai wa UAP Emmanuel Michael aliwataka wafanya biashara kuwa makini na bidhaa zao ili kuepusha majanga ya moto yasiwatokee.
Alisema wafanya biashara wengi wamekuwa wazembe kujifunza elimu ya kujikinga na majanga ya moto ambayo huwapatia hasara kubwa katika
biashara zao za kila siku.

Wednesday, April 8, 2015

YANGA NJIA NYEUPEE, YAMZIBA MDOMO JULIO KWA 8-0

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEinj8FsP_aDKXr8JLCGkYb7oGiMFKfaPcj8820SGepcKAM55k0Uq2GxQrLCnguU3GwSrYripfOY8Ta3XUFVzdVLqv_dEEqHfLLmZvc13ggQClezx2G2o24dgIxNCG46MD36j1TlFROkrZ4/s1600/DSC_7835.JPGNJIA nyeupe kwa Yanga kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu baada ya jioni hii kugawa dozi ya maana kwa Coastal Union, huku watetezi Azam wakilazimishwa na Mbeya City.
Yanga ikiwa kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam imemfunga mdomo kocha anayechinga sana, Jamhuri Kihwelu 'Julio' baada ya kupata ushindi wa mabao 8-0, huku Amissi Tambwe akifunga mabao manne na kurejea rekodi aliyoiweka msimu uliopita wakati akiwa Simba. Kipigo hicho kimekuja katika Ligi Kuu tangu Yanga ilipoifanyia Kagera Sugar mwaka 1998 ambapo Edibily Lunyamila alifunga pekee yake mabao matano.


Mabao mengi ya Yanga katika mchezo huo yalifungwa na Simon Msuva aliyefunga mawili, Salum Telela na Kpah Sherman aliyefunga bao lake la kwanza akiwa na Yanga tangu ajiunge nayo miezi minne iliyopita.
Kwa ushindi huo Yanga imefikisha jumla ya pointi 43 na mabao 36 ya kufunga na kuwaacha Azam kwa pointi sita baada ya watetezi hao kulazimishwa sare ya 1-1 na Mbeya City kwenye uwanja wa Chamazi.
Kwa kufunga mabao manne, Tambwe amefikisha mabao 9 msimu huu katika Ligi Kuu wakati Msuva amezidi kumuacha mbali Didier Kavumbagu wa Azam kwa kufikisha mabao 13 dhidi ya 10 ya mpinzani wake huyo ambaye leo hakushuka dimbani katika pambano la Mbeya City.

Liverpool yamnyatia Alexandre Lecazette

http://cdn.sports.fr/images/media/football/ligue-1/scans/lyon-domine-lille-grace-a-un-triple-de-lacazette/alexandre-lacazette/12966789-1-fre-FR/Alexandre-Lacazette.jpgKLABU ya Liverpool iko tayari kuungana na vilabu vingine vya Ligi Kuu kumfukuzia nyota wa Lyon ya Ufaransa Alexandre Lacazette katika kipindi cha majira ya kiangazi. 
Wakongwe wa Ujerumani Burussia Dortmund pia wamekuwa wakifuatilia mwenendo wake wakati Manchester City nao wamekuwa wakimkodolea macho nyota huyo mwenye umri wa miaka 23 toka Novemba mwaka jana. Klabu za Chelsea, Arsenal na Tottenham Hotspurs nazo pia zimeshatuma maskauti wao kuangalia mwenendo wa mchezaji huo huku Newcastle wakiendelea kumfuatilia pamoja na kushindwa kumsajili hapo nyuma. 
Safari hii Liverpool wamejipanga kuimarisha safu yao ya ushambuliaji mapema yasije kuwakuta kama walivyomuuza Luis Suarez kwenda Barcelona na kulazimika kumnunua Mario Balotelli ambaye hata hivyo amekuwa hana msaada sana msimu huu. Baada ya Balotelli kushindwa kung’aa na Daniel Sturridge akiendelea kusumbuliwa na majeruhi huku kukiwa hakuna uhakika wa kuendelea kuwa na Raheem Sterling msimu ujao, Brendan Rodgers anahitaji kupata chaguo zaidi katika kikosi chake.

AFCON 2017 KAZI KWELI, STARS WAPEWA MISRI, NIGERIA

http://www.fullshangweblog.com/wp-content/uploads/2014/07/TAIFA1.jpg
Taifa Stars
Kombe la AFCON
SAFARI ya Taifa Stars ya Tanzania katika mchakato wa kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) zitakazofanyika nchini Gabon mwaka 2017, inaonekana kuwa ngumu. Hii ni baada ya  Shirikisho la Soka Afrika (Caf) kuipanga kundi moja la G pamoja na vigogo.
Kwa mujibu wa droo iliyofanyika jana jijini Cairo, Misri, Tanzania imepangwa kundi moja na mabingwa wa kihistoria wa michuano hiyo, Misri, pia wakipewa mabingwa wa mwaka jana, Nigeria na Chad. Huku Morocco, Tunisia zilizokuwa zimefungiwa na CAF nazo zikijumuishwa katika droo hiyo.
Timu 16 zitakazopenya katika hatua hiyo ya makundi ndiyo watakaoenda Gabon kusaka ubingwa ambao kwa sasa unashikiliwa na Ivory Coast waliotwaa mapema mwaka huu kwa kuilaza Ghana.
Tanzania kwa mara ya kwanza na mwisho kufuzu fainali hizo ilikuwa mwaka 1980 wakati michuano hiyo ilipofanyika nchini Nigeria na kwa miaka zaidi ya 30 imekuwa ikisota kusaka nafasi ya kushiriki tena bila mafanikio.
Makundi ya michuano hiyo ambayo awali ilikuwa iandaliwe na Libya kabla ya hali ya machafuko ya kisiasa kuifanya ijitoe ni kama yafuatavyo;
Kundi A: Tunisia, Togo, Liberia, Djibouti
Kundi B: Madagascar, DRC, Angola, CAR
Kundi C: Mali, Equatorial Guinea, Benin, South Sudan
Kundi D: Burkina Faso, Uganda, Botswana, Comoros
Kundi E: Zambia, Congo, Kenya, Guinea Bissau
Kundi F: Cape Verde, Morocco, Libya, Sao Tome
Kundi G: Nigeria, Egypt, Tanzania, Chad
Kundi H: Ghana, Mozambique, Rwanda, Mauritius
Kundi I: Cote d'Ivoire, Sudan, Sierra Leone, Gabon
Kundi J: Algeria, Ethiopia, Lesotho, Seychelles
Kundi K: Senegal, Niger, Nambia, Burundi
Kundi L: Guinea, Malawi, Zimbabwe, Swaziland
Kundi M: Cameroon, South Africa, Gambia, Mauritania

Ally Choki, Super Nyamwela warudi Twanga Pepeta

Luiza Mbutu akiwatambulisha Ally Choki na Super Nyamwela leo jijini juu ya kurudi kwao Twanga pepeta
MUIMBAJI nyota wa muziki wa dansi nchini, Ally Choki ametangazwa kurudi African Stars 'Twanga Pepeta' ikiwa ni miezi michache tangu bendi yake ya Extra Bongo kusambaratika.
Kiongozi wa bendi hiyo, Luiza Mbutu alimtangaza Choki na Super Nyamwela kurudi tena Twanga leo mbele ya wanahabari ikiwa ni miaka michache tangu alipoihama bendi hiyo kwenda kuanzisha bend iliyokufa ya Extra Bongo.
"Tumeamua kuiboresha bendi yetu ya mama ya Twanga Pepeta na huu ni uamuzi wangu binafsi sikushurutishwa na mtu yeyote ieleweke hivyo," alisema Choki katika utambulisho huo uliofanyika Kinondoni jijini Dar es Salaam.
“Twanga ni bendi yangu, hakuna ubishi ni bendi ambayo nimeitumikia kwa miaka mingi sana hivyo kwa kuanzia nitatoka na kibao kiitwacho ‘Kichwa Chini’ ambacho nitaimba na Luiza ukitoa somo kwa wanaume,” alisema Choki .
Aliongeza tayari kuna nyimbo mbili zilizo tayari kufyatuliwa na kuzitaja kuwa ni ‘Usiyaogope  Maisha’ na ‘No Discuss’.
Choki alidokeza pia kuwa hana mpango wa kuasisi tena bendi kwa sababu hataki ‘stress’ kwani kumiliki bendi ni pasua kichwa.
Naye Nyamwela alisema amerudi nyumbani na yupo tayari kwa ajili ya kuchapa kazi na Kiongozi wa Twanga Pepeta, Luiza Mbutu alisema wanatarajia kuandaa onyesho maalum la utambulisho wa wakali hao Aprili 18, jijini Dar es Salaam

TFF yampongeza Tenga, kuziona Twiga, Shepolopolo buku 2

http://shaffihdauda.co.tz/wp-content/uploads/2015/04/malinzi1.jpg
Rais wa TFF, Jamal Malinzi
RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF Jamal Malinzi, amempongeza Bw Leodgar Tenga kwa kuchaguliwa kuendelea kuwa mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika (CAF).
Aidha Rais Malinzi ametuma salamu za pongezi kwa wajumbe  waliochaguliwa kuwa wajumbe wapya wa Shirikisho la Mpira wa Miguu baranai Afrika (CAF) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani FIFA.
Katika salamu hizo na nakala zake kutumwa kwa Rais wa CAF Bw. Issa Haytou na Rais wa FIFA Bw. Blatter, Malinzi amewatakia kila la kheri katika majukumu hayo mapya,na  kwa ajili ya maendeleo ya mpira wa miguu duniani.
Tenga amechaguliwa nafasi hiyo baada ya kuwa mgombea pekee kutoka kanda ya Afrika Mashariki aliyejitokeza kuwania nafasi hiyo na kuungwa mkono na nchi zote wanachama wa CECAFA.

Wakati huo huo kiingilio cha kuziona timu za Twiga Stars dhidi ya Wazambia ni Sh 2000 katika pambano la marudiano ya kuwania Fainali za Soka za Wanawake Afrika. Mechi inatarajiwa kuchezwa wikiendi hii.

Monday, April 6, 2015

YANGA KWELI WANAUMEEEEEEE!

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjPVvCUhWRWhNyy8Wg2dj2opEk2yN6YVnLZqmUVO5-Ut6u4sEUMdoKRdNE0NCaZSdwQ5lDuOp_BFLU_wpVN9ckZ7CIJAVZRNBT5IP_XAZKAKZxsTmKW3QBpRi0f11WMh3T5Y1gnjkD8-L8E/s1600/DSC_0067.JPGYANGA kweli wanaume! Ndiyo wawakilishi pekee wa Tanzania waliosalia kwenye michuano ya kimataifa kwa mwaka huu baada ya Azam, KMKM na Polisi Zanzibar kung'olewa mapema. Pia ndiyo timu pekee ya Afrika Mashariki iliyosalia kwenye michuano ya kimataifa, kadhalika ni moja ya klabu tatu pekee za ukanda wa CECAFA zilizopenya katika raundi ya pili ya michuano ya Afrika 2015.
Kwa mujibu wa matokeo ya mwishoni mwa wiki kwa mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho, Yanga ni timu pekee ya Afrika Mashariki na Kati kusalia katika Kombe la Shirikisho, lakini ikiungana na klabu za Al Merreikh na Al Hilal za Sudan zilizopenya raundi hiyo kupitia Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu.
Yanga ilipata nafasi hiyo ya kuvuka hatua hiyo na kukabiliwa na kibarua kigumu mbele ya Watunisia wa Etoile du Sahel baada ya kuing'oa FC Platinum ya Zimbabwe kwa jumla ya mabao 5-2. Mwishoni mwa wiki walitandikwa bao 1-0, lakini ushindi mnono wa mabao 5-1 katika mechi ya awali umewabeba.
Kwa mujibu wa 16 Bora iliyotolewa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF), timu zilizopenya raundi ya pili katika Kombe la Shirikisho ni; Onze Créateurs ya Mali, ASEC Mimosas ya Ivory Coast, Djoliba ya Mali,  Hearts of Oak ya Ghana, ASO Chief ya Algeria, Club Africain ya Tunisia, Warri Wolves ya Nigeria MK Etancheite wa DR Congo, Zamalek ya Misri na FUS Rabat ya Morocco.
Nyingine ni CF Mounana ya Gabon, Orlando Pirates ya Afrika Kusini, Yanga ya Tanzania, Etoile du Sahel ya Tunia, Royal Leopards ya Swaziland na AS Vita ya DR Congo.
Kwa upande wa Ligi ya Mabingwa Afrika, zipo timu za USM Alger ya Algeria, AS Kaloum ya Guinea,
SM Sanga Balende ya DR Congo,  Al-Hilal ya Sudan, Al-Merreikh ya Sudan, Espérance de Tunis ya Tunisia, MC El Eulma ya Algeria, CS Sfaxien ya Tunisia, AC Léopards ya Congo na Smouha ya Misri.
Klabu nyingine ni Moghreb Tétouan ya Morocco, Al-Ahly ya Misri, Raja Casablanca ya Morocco, watetezi ES Sétif ya Algeria, Stade Malien ya Mali na TP Mazembe ya DR Congo.
Mechi za awali ya hatua hizo zitachezwa kati ya Aprili 17-19 na marudiano kufanyika Mei 1-3 na timu ambazo zitapenya katika Kombe la Shirikisho zitaumana na zile zitakazoangushwa katika Ligi ya Mabingwa kwa ajili ya kuwania kutinga hatua ya makundi kuanza safari ya kusaka mamilioni ya CAF.

Simba wanacheka, walipa kisasi kwa Kagera, Mtibwa hoi

http://shaffihdauda.co.tz/wp-content/uploads/2015/02/HMB_8444.jpg
Simba katika moja ya mechi zao za Ligi Kuu msimu huu
http://kabumbu.co.tz/wp-content/uploads/2015/01/KIKOSI-SIMBA-SC.jpg
WANAUMEEEE!
SIMBA wanachekaaaa! Baada ya jioni hii kupata ushindi wa mabao 2-1 mbele ya timu ngumu ya
Kagera Sugar katika mechi ya kiporo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
Simba ambayo inaendelea kuomboleza vifo vya wanachama wake wa tawi la Maendeleo maarufu
kama Simba Ukawa waliofariki kwa ajali ya gari mjini Morogoro wakati wakielekea Shinyanga
kuwahi pambano hilo pamoja na kifo cha baba wa nahodha wao msaidizi, Jonas Mkude imepumua.
Ushindi huo wa mjini Shinyanga licha ya kusaidia kulipa kisasi kwa wapinzani wao, lakini pia
imewafanya wapunguze pengo la pointi dhidi ya mabingwa watetezi Azam wanashika nafasi ya
pili.
Simba imefikisha pointi 35, moja pungufu na ilizonazo Azam ambao keshokutwa watashuka dimba
la Taifa kuvaana na Wagonga Nyundo wa Mbeya City katika mfululizo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Mabao ya washindi katika pambano hilo lililoahirishwa toka Jumamosi kutokana na uwanja wa
Kambarage kujaa maji ya mvua, yaliwekwa kimiani na Ramadhani Singano 'Messi' katika dakika ya
49 kwa shuti kali la mbali na panalti ya Ibrahim Ajibu katika dakika ya 65.
Penalti hiyo ilikuja baada ya mabeki wa Kagera kunawa mpira langoni mwao katika harakati za
kuokoa goli na Ajibu kufunga kiufundi. Kabla ya hapo Rashid Mandawa alifunga bao lake la 10
msimu huu na kumkamata Didier Kavumbagu pale aliposawazisha bao la Messi dakika ya 60.
Katika mechi ya kiporo kingine mapema leo asubuhi Mtibwa Sugar walishindwa kuhimili vishindo vya Stand United na kukubali kichapo cha bao 1-0, kikiwa ni kipigo cha pili kwao mjini Shinyanga.
Awali wiki iliyopita walicharazwa mabao 2-1 na Kagera Sugar na kwa kichapo hicho wameifanya timu hiyo waliokuwa wakiongoza Ligi kwa muda mrefu kuporomoka hadi nafasi ya 12. Nafasi moja juu ya mstari wa timu mbili za kushuka daraja msimu huu kwenda Ligi Daraja la Kwanza (FDL).
 

Msimamo baada ya matokeo ya  leo ni kama ufuatavyo;

                        P   W   D     L     F      A    Pts
1. Yanga          19   12   4    3    28    11    40
2. Azam FC      18   10   6    2    25    12    36
3. Simba         21    9    8    4    27    15    35
4. Kagera        21    7    7    7    19    20    28
5. Mgambo      20    8    3    9    17    19    27
6. Ruvu           19    6    8    5    13    16    26
7.Coastal         21    5    9    7    14    15    24
8. Mbeya City   20    5    9    6    15    17    24
9. JKT Ruvu     21    6    6    9    16    20    24
10. Ndanda      21    6    6    9    18    24    24
11. Stand         20    6    6    8    15    23    24
12. Mtibwa       21    5    8    7    19    20    23
13. Polisi Moro  21    4    9    8    13    21    21
14. Prisons       19    3    11   5    14    20    20

Mechi zijazo:
KESHO JUMATANO
Azam vs Mbeya City



Sunday, April 5, 2015

NI YANGA NA WATUNISIA, TP MAZEMBE YAPENYA


YAMETIMIA! Wawakilishi pekee wa Tanzania Yanga imefahamika sasa kukutana na Etoile du Sahel ya Tunisia baada ya waarabu hao kulazimisha sare ya 1-1 ugenini dhidi ya Benfica de Luanda ya Angola katika mechi yao ya marudiano ya Kombe la Shirikisho.
Etoile imesonga mbele kwa jumla ya mabao 2-1 baada ya mchezo wa kwanza nyumbani kushinda bao 1-0 na sasa watavaana na Yanga waliosonga mbele dhidi ya FC Platinum ya Zimbabwe ambao jana waliwacharaza bao 1-0.
Kipigo hicho cha ugenini hakikuizuia Yanga kusonga mbele kwani ilikuwa na hazina ya ushindi wa mabao 5-1 yaliyopatikana katika mechi ya kwanza jijini Dar es Salaam.
Mechi ya mkondo wa kwanza ya Yanga na Etoile itachezwa kati ya April 17-19 jijini Dar es salaam kabla ya kurudiana mjini Tunisia wiki mbili baadaye ambapo mshindi atasubiri kucheza mchujo wa mwisho dhidi ya timu zitakazoangukia pua kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika baadaye Juni tayari kwa ajili ya kutinga hatua ya makundi kuvuna mamilioni ya CAF.
Aidha TP Mazembe ya DRC imesonga mbele kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuitoa Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini kwa jumla ya mabao 3-2 baada ya leo kushinda nyumbani 3-1 na kulipa kisasi cha kufungwa bao 1-0 ugenini.

Friday, April 3, 2015

Yanga yaenda Zimbabwe matumaini kibao, TFF yaitilia ubani

http://taarifa.co.tz/wp-content/uploads/2015/01/yanga1.jpg
Yanga Kila la Heri katika mechi yenu ya kesho dhidi ya FC Platinum
WAKATI Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu wa nchini TFF, Jamal Malinzi ikiwatakia kila la kheri wawakilishi pekee wa Tanzania kwenye kombe la Shirikisho Afrika, Yanga, kikosi cha timu hiyo kimeondoka leo nchini kuelekea Zimbabwe.
Yanga wameondoka leo majira ya asubuhi kuwahi pambano lao la kesho dhidi ya FC Platinum litakalochezwa kwenye Uwanja Mandava uliopo Gweru Bulawayo.

Rais wa TFF, Jamal Malinzi amesema Young Africans hawapaswi kubweteka na ushindi walioupata awali wa mabao 5-1, kikubwa wanapaswa kwenda kupambana kusaka ushindi ugenini ili kuweza kufuzu kwa hatua inayofuata ya timu 16.
Endapo Young Africans itafanikiwa kuwatoa FC Platinum itaingia katika hatua ya 16 bora na itakutana na mshindi kati ya timu za Benifica de Luanda ya Angola au Etoile du Saleh ya Tunisia.
Yanga wakiwa na ari kubwa wameondoka leo nchini na kuahidi kuendelea kuwapa raha watanzania kwa kupata ushindi ugenini mbele ya wachimba madini hao wa Bulawayo.
Yanga inahitaji sare ya aina yoyote na hata kama itapoteza mechi hiyo ya marudiano chini ya mabao manne inaweza kusonga mbele kwa ajili ya raundi ya pili.
Kikosi cha wachezaji 18 na viongozi saba wameondoka wakisema wanaenda kupambana kuhakikisha Tanzania inaendelea kuwepo miongoni mwa wawakilishi wa michuano ya kimataifa baada ya Azam, KMKM na Polisi kung'oka mapema.

Wenger, Giroud wang'ara England, watwaa tuzo

LONDON, England
KOCHA wa Arsenal Arsene Wenger ametangazwa kuwa kocha wa mwezi wa Ligi Kuu ya England na mshambuliaji Olivier Giroud akiwa mchezaji wa mwezi.Gi

Arsenal ilishinda mecwon four successive Premier League ghi nne mfululizo za Ligi Kuu mwezi Machi, ikifunga mabao tisa na kufungwa mawili tu.

Mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa Giroud alifunga mara tano, wakati Newcastle ilipocheza dhidi ya Everton, QPR na  West Ham.

Hii ni mara ya 14 Wenger, mwenye umri wa miaka 65, kutwaa tuzo ya kocha bora wa mwezi katika miaka yake 19 ya kuifundisha Arsenal.

Arsenal kwa sasa iko katika nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu ya England wakati zikiwa zimebaki mechi nane kabla ya ligi hiyo haijafikia mwisho.

Timu hiyo iko pointi saba nyuma ya vinara Chelsea, ambao wana mchezo mmoja mkononi.

The Gunners itawakaribisha Liverpool iliyopo katika nafasi ya tano kwenye uwanja wa Jumamosi.

Mechi zilizobaki za Arsenal za nyumbani ni pamoja na ile dhidi ya Chelsea itakayofanyika Aprili 26 na safari ya Manchester United iliyopo katika nafasi ya nne Mei 17.